Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa sh. bilioni 43 zikiwa ni madeni kwa watumishi wa umma na kati ya hizo sh. bilioni 16.25 zimelipwa kwa walimu.

“Hadi kufikia mwisho wa mwezi uliopita, jumla ya sh. bilioni 43 zimelipwa kwa watumishi 27,389 ambao kati yao watumishi 15,919 ni wa sekta ya elimu tu na madeni yao yanafikia sh. bilioni 16.25,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Julai 13, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga akiwa aktika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

“Mapema mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa sh. bilioni 200 za kulipa madeni ya watumishi na hadi sasa madeni ambayo yameshahakikiwa ni sh. bilioni 127 na mengine ni ya wazabuni,” amesema. 

Amesema hivi sasa Serikali inadhibiti uzalishaji wa madeni ya watumishi kwa kuzuia uhamisho kama hakuna fedha, kuzuia rufaa zisizokuwa za lazima na ambazo hazina ufuatiliaji wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya, na kuhimiza matumizi ya Bima ya Afya kwa watumishi wa umma.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Julai 13, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack . 
 Baadhi ya Watumishi na Viongozi wa vyama vya Siasa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Julai 13, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Julai 13, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI,  Joseph Kakunda na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA NDUGAI AMJULIA HALI MBUNGE WA CHAANI NYUMBANI KWAKE MJINI UNGUJA

$
0
0
   Spika wa  Bunge Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Chaani Khamis Yahya Machano (kulia) alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Unguja Mjini, Zanzibar mapema leo.
Spika wa  BungeJob Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Chaani Mheshimiwa Khamis Yahya Machano (kulia) alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Unguja Mjini, Zanzibar mapema leo. Wa kwanza kushoto  ni Machano Othman Said (Mb). PICHA NA BUNGE

UWT TEMEKE WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA NDEGE YA NNE BOEING 787-8 DREAMLINER

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
JUMUIYA ya Umoja  wa Wanawake  Tanzania (UWT) Wilaya ya Temeke wamempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufulu kwa kuweza kutekeleza ahadi ya kununua ndege ya nne kati ya saba alizoziahidi.

UWT Temeke wamesema kuwa hiyo ni moja ya ahadi zilizoanishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi na wamemuomba aweze kutimiza ahadi zote ili kuhakikisha upinzani wanakosa la kusema.

Akizungumza na wajumbe wa UWT Wilaya ya Temeke, Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi  amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Chama cha Mapinduzi imedhamiria kutimiza ahadi zote zilizoanishwa wakati wa kampeni  na tayari zinafanyiwa kazi ikiwemo kununua ndege ya nne kati ya saba na zile zitakazoanza kutekelezwa kwenye bajeti ya 2018/19.

"Rais wetu Dkt Magufuli aliahidi kununua ndege saba zitakazokuwa mali yetu na mpaka sasa ameshanunua ndege  ikiwemo Boeing  787-8 Dreamliner  na kutimiza idadi ya ndege nne kati ya saba alizotoa ahadi kwenye kampeni zake mwaka 2015,"amesema Mb Mariam.
Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi  akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Wilaya ya Temeke wakati wa hafka yao ya kumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Temeke, Rukia Kamal akizungumza na wajumbe wa UWT Temeke wakati wa hafla ya kumpongeza  Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.

Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Temeke Kimenta Mavala akielezea jambo mbele ya wajumbe na Mgeni rasmi wa hafla yakumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.
 Wajumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT)  Wilaya ya Temeke wakiwa katika hafla ya kumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.
 Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe  wa UWT Wilaya ya Temeke wakati wa hafla ya kumpongeza  Mwenyekiti wa Chama na Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kununua ndege ya nne Boeing 787-7 Dreamliner kati ya saba alizozitoa katika ahadi yake wakati wa kampeni za uchaguzi 2015.


JWTZ YAMTAKA ALIYELALAMIKIA HUDUMA HOSPITALI YA LUGALO AJITOKEZE KUBAINI UKWELI VINGINEVYO WATAMSAKA

$
0
0
Na Luteni  Selemani Semunyu
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limekanusha taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko juu matibabu  ya mtoto anayedaiwa kuvunjika na kupatiwa  huduma  katika Hospitali kuu ya jeshi ya Lugalo.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo  Jijini  Dar es Salaam msemaji mkuu wa Jeshi Kanali Ramadhani Dogoli alimtaka aliyejinasibisha kama mlalamikaji kuwasilisha malalamiko yake kama yana ukweli ili hatua zichukuliwe kwa wahusika.

“ Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linamtaka malalamikaji alete taarifa kwenye uongozi ili kama matukio hayo yametokea tuweze kuchukua hatua kwa wahusika” Alisema kanali Dogoli.

 Aliongeza kuwa iwapo aliyedai kulalamika atashindwa kufanya hivyo jeshi litaaamini kuwa mlalamikaji alikusudia kuichafua hospitali yetu kwa maslahi binafsi  na kwa sababu hiyo tutamtafuta haraka na kumchukulia hatua zinazomstahili.

Msemaji huyo wa JWTZ Mnamo Julai 10 mwaka huu ilisambaa habari ikilalamika huduma zisizoridhisha  katika kitengo cha mifupa katika hospitali ya lugalo  baada ya kudai  mtoto wake mkono umeunga vibaya na kutakiwa kupatiwa matibabu tena.

Hata hivyo alisema baada ya kupata taarifa walifanya uchunguzi ambapo yalipitiwa majina ya watoto wote waliotibiwa tangu April hadi 30 Juni mwaka huu hakuna mtoto aliyefika mara mbili kwa waliopata mivunjiko.

“ Watoto wawili tu ndio walitibiwa na wazazi wao walithibitisha kuwa maendeleo yao ni mazuri majibu yalipelekea kubaini kuwa labda muhusika alikusudia kuichafua Hospitali yetu” Alisema kanali Dogoli.

Kwa upande wake Mkuu wa tiba wa JWTZ Meja Jenerali Dk Denis Janga alisema amesikitishwa na taarifa hiyo ambayo pia imewagusa wataalam wa hospitali hiyo ambayo imekuwa ikitoa huduma kwa wananchi tofauti na majeshi mengine ambapo hospitali za jeshi zinahudumia wanajeshi na Familia zao pekee.

Alisema wataalam wa hospitali hiyo ni wataalam kama watalaaam wengine waliopata mafunzo ndani na n je ya nchi kama ilivyo wataalam wengine na kamwe hawatokatishwa tamaa na maneno ya kuichafua hospitali hiyo.

Mkuu huyo wa Tiba jeshini alisema wameapa kuilinda na kuitetea katiba na wamejitolea kuwahudumia watanzania hivyo hawatosita kufanya hivyo kwa moyo wao wote.

“ Kamwe hatutasita kuwahudumia Watanzania  kwa maneno ya uongo na kuwataka watanzania kuwapuuza watu wenye mtazamo wa kuwagombanisha na wananchi na sasa ni wakati wa kutiana moyo kwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali” Alisema Meja Jenerali Janga .

Hospitali za Jeshi nchini ikiwemo  Hospitali kuu ya jeshi Lugalo  zimekuwa zikishiriki katika utoaji wa huduma kwa Wananchi kwa Zaidi ya ya asilimia 70 ukilinganisha na idadi ya Askari na wategemezi wao wanaopata huduma katika hospitali hizo.
 Msemaji Mkuu wa Jeshi Kanali Ramadhani Dogoli ( Wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu malalamiko ya uzushi dhidi ya Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo wapili kulia ni Mkuu wa Tiba Jeshini Meja Jenerali Denis Janga na wakwanza kulia ni Mkuu wa Hospitali ya Lugalo Brigedia Gabriel Muhdize leo  Jijini Dar es Salaam (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Moja ya majengo ya Hospitali Kuu ya jeshi ya Lugalo ambayo imekuwa ikitoa huduma kwa wananchi raia kwa Asilimia 70 ukilinganisha na Wanajeshi  na Familia Zao wanaofika kutibiwa katika Hospitali hiyo( (Picha na Luteni Selemani Semunyu)  

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA UPANUZI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA NA KUSHUHUDIA UUZAJI WA PAMBA WILAYANI KISHAPU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Old Shinyanga hadi Kishapu, Mwadui na Kolandoto Julai 13, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia kwake)  baada ya kuzindua Mradi wa Upanuzi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Old Shinya hadi Kishapu, Mwadui na Kilandoto Julai 13, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi, Kezia Ndegeleke wa kijiji cha Isoso ambaye alikuwa na malalamiko ya kutolipwa fidia ya ardhi. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya wilaya ya Kishapu Julai 13, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishuhudia uuzaji wa pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwangongo wilayani Kishapu Julai 13, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwangongo, Pius Kushoka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama pamba wakati alipotembelea ghala la Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwangongo wilayani Kishapu Julai 13, 2018.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na wanne kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mwangongo,  Pius Kushoka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM

$
0
0
Na Khadija Seif , Globu ya jamii.

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Leticia Ghati Mosore  pamoja na wajumbe wenzie wanne wamerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta chachu ya maendeleo.  

Leticia  amebainisha sababu mbalimbali zilizowafanya kuhama chama cha hicho na kupongeza utawala wa awamu ya tano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuona mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo na kiutendaji.

Mwenyekiti huyo amesema "utendaji wa serikali ya Sasa unatendeka Kwa uwazi, ukusanyaji wa mapato ni mzuri ,na hadi Sasa hivi imenunua ndege Kwa Kodi za watanzania na imejenga barabara za juu "fly overs" pamoja na kujenga reli ya kisasa ".  

Amefafanua zaidi na kusema serikali iliyopo madarakani imeweza kuwajali wananchi wake kwa kupeleka dawa hospitali zote nchini, imesambaza umeme vijijini kwa mradi wa umeme wa Vijijini ( REA) hayo yote yanatokana na ukusanyaji wa mapato kuwa mzuri .

Ameeleza kuwa upande wa vyama vya upinzani hawazioni juhudi hizo na zaidi wamekaa na kuponda jitihada za serikali huku wakipinga  bajeti isipitishwe huku maendeleo yakiwa yanaonekana Kwa macho.

Leticia amefafanua kuwa wameamua kuhama chama cha NCCR Mageuzi   Kwa ridhaa yao wenyewe na kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Magufuli.

Waliohama chama hicho ni pamoja na Katibu wa chama hicho Kata ya Segerea Lilian Kichunga,Katibu wa Chama cha Wanawake Mossy Kichau, Mwenyekiti wa Jimbo la Segerea Yunes Zacharia pamoja na Mjumbe Vidaline Nicholaus.

KAMISHNA MKUU WA TRA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA KIKODI ZINAZOIKABILI SEKTA YA UZALISHAJI WA MVINYO

$
0
0
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsikiliza Mtaalam wa kutengeneza mvinyo wa Kiwanda cha Kutengeneza Mvinyo (CETAWICO) cha Jijini Dodoma, Bw. Erick Shulz namna mvinyo unavyochambuliwa kwa kutumia mtambo maalum kiwandani hapo wakati alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kutambua changamoto zinazowakabili Wawekezaji.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kutengeneza Mvinyo (CETAWICO), Bw. Fiorenzo Chesini (kulia) akimuonyesha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (katikati) kifaa maalum kutumikacho kupimia kiasi cha ukali wa mvinyo wakati alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kutambua changamoto zinazowakabili Wawekezaji.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kutengeneza Mvinyo (CETAWICO), Bw. Fiorenzo Chesini akimueelezea namna ya baadhi ya mashine za kiwandani hapo zinavyofanya kazi mpaka kuhakikisha kuwa mvinyo mzuri unapatikana, wakati alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kutambua changamoto zinazowakabili Wawekezaji.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)

Na. Rachel Mkundai
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Charles Kichere ameahidi kushughulikia changamoto za kikodi zinazoikabili sekta ya uzalishaji mvinyo nchini ili kuwawezesha wawekezaji na Wakulima wa zao la zabibu kuweza kunufaika.

Kauli hiyo ameitoa Jijini Dodoma alipotembelea kiwanda kinachozalisha mvinyo cha Central Tanzania Wine Company CETAWICO ambapo alipata fursa ya kuzungumza na mwekezaji wa kiwanda pamoja na wakulima wa zabibu ambao ndiyo wazalishaji wa malighafi kiwandani hapo.

“Nimezumgumza na mwekezaji wa kiwanda hiki na changamoto ninazoziona ni za kisera, na hivyo nitaziwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango ili ziweze kufanyiwa kazi”, amesema Kamishna Kichere.

Aidha, Kamishna Kichere amemtaka mwekezaji wa kiwanda hicho kuwasilisha changamoto hizo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili zipatiwe ufumbuzi kwa upande wa masuala ya kibiashara.

“Ni vema changamoto hizi pia uziwasilishe katika wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili ziweze kushughulikiwa sambamba na masuala ya sera za kodi  ambayo yatashughulikwa na Wizara ya Fedha na Milanzi”, amesisitiza Kichere.

Kwa upande wake mwekezaji wa kiwanda hicho, Bw. Fiorenzo Chesini amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA kwa kumtembelea kiwandani hapo na kusema kuwa, kwa kushirikiana na Serikali changamoto za kikodi na nyinginezo zinazoikabili sekta ya uzalishaji mvinyo zinaweza kutatuliwa.

“Kwa kutembelewa na Kamishna Mkuu wa TRA, nina uhakika  changamoto zetu sasa zitatatuliwa na sisi tutaendelea kufanya uwekezaji Tanzania na kununua zabibu nyingi kutoka kwa wakulima”, amesema Bw Chesini.

Kwa upande wao baadhi ya Wakulima wa zao la zabibu katika kijiji cha Hombolo Mkoani Dodoma wameiomba Serikali pamoja na mwekezaji wa kiwanda hicho kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili mwekezaji aweze kununua zabibu zao katika msimu ujao.

“Msimu wa mavuno unakaribia sana kufika hapo mwezi Agosti na kama unavyoona zabibu zimeshakomaa ila hatuna uhakika kama mwekezaji atanunua zabibu zetu, tunaomba serikali itusaidie kumaliza changamoto ili tuweze kuuza zabibu zetu msimu ujao”, alisema mkulima Fred Mwaluko.

Hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko juu ya uwepo wa kodi kubwa kwenye pombe kali zinazozalishwa nchini kulinganisha na pombe kali zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ambapo kiwanda cha CETAWICO ndicho kinachotengeneza sehemu kubwa ya malighafi inayotumika kutengeneza baadhi ya pombe kali za hapa nchini ambapo malighafi hiyo pia inatokana na zao la zabibu.

MWENYEKITI WA CCM RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BARAZA JIPYA LA WADHAMINI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza jipya la wadhamini wa Chama cha Mapinduzi CCM Ikulu jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia mstari wa kwanza ni Dkt. Haruni Kondo, Anna Abdallah(Mwenyekiti wa Baraza) na Jaji Mstaafu Mark Bomani wa kwanza kushoto. Wengine mstari wa nyuma kuanzia kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally, Christopher Gachuma, John Chiligati, Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay, Pandu Kificho pamoja na Hassan Mzee wa mwisho (kushoto) mstari wa nyuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na baadhi ya Wajumbe wa Baraza jipya la wadhamini wa Chama cha Mapinduzi CCM Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mmoja wa wajumbe wa Baraza jipya la wadhamini wa Chama cha Mapinduzi CCM Hassan Mzee ambaye ni mmoja kati ya watu waliochanganya udongo wakati Tanganyika ilipoungana na Zanzibar na kuunda nchi moja ya Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye kikao pamoja na Wajumbe wa Baraza jipya la wadhamini wa Chama cha Mapinduzi CCM Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAKIMBIZI WAPEWA SIKU SABA KURUDI MAKAMBINI

MAKAMISHNA WASAIDIZI WAANDAMIZI WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku(kulia)  akiwa kwenye gari maalum pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga(kushoto) wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.

 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakitoa salaam ya heshima kwa Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.
 Makamishna Wasaidizi Waandamizi wastaafu wa Magereza wakipita wakiwapungia mikono maafisa, askari na wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.
  Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo..
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku  akisalimiana na Kamishna wa Magereza, Gedion Nkana mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga wastaafu hao katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga(katikati) paoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku( wa pili kulia)  walioketi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza waliosimama mstari wa nyuma mara baada ya hafla ya kuwaaga wastaafu hao. Wengine walioketi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Magereza, Augustine Mboje, wa pili toka kushoto ni Kamishna wa Magereza, Hamis Ngarama na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Magereza, Gedion Nkana
Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Makao Makuu ya Magereza.

ZURIEL SPEAKS IN PRETORIA during Mandela Centenary and BRICS Summit Preparations

$
0
0
With many events leading to the BRICS Summit, the arrival of Barack Obama, and the Nelson Mandela Centenary celebrations, the Government of South Africa has invited Girl Education advocate and Film Maker - Zuriel Oduwole as a thought leader, to share her insights on various issues revolving around the many events unfolding in the Rainbow nation. 
 She was welcomed to the Department of International Relations and Corporations [DIRCO] by the Senior Director for US Region; Arnorld Lyle. 
Zuriel spoke about the powerful Legacy of Nelson Mandela, its global impact as regards true leadership, and the role a relevant and practical curriculum can play in educating the next generation of African leaders. 
 She shared more of her story and mission on ARISE News UK's Abuja Studio last week, on her sway to South Africa

Two weeks ago in Accra - Ghana, Zuriel, met her 28th world leader H.E. President Nana Akufo-Addo,and shared her idea with him of how to make Ghana a premier location shoot for big budget films from the US, following the shoot of aspects of the film "ALI" there years ago. She shared more of her story and mission on ARISE News UK's Abuja Studio last week, on her way to South Africa 

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI WAKABIDHIWA ZAWADI YA USHINDI WA PILI

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (mwenye tai nyekundu) akimuangalia Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias, baada ya kumkabidhi cheti cha ushindi wa pili katika kipengele cha Wizara, Mamlaka na Wakala za Serikali zilizofanya vizuri katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yaliyofungwa Jumamosi Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (mwenye tai nyekundu) akiwa pamoja na washindi wa nafasi ya pili na tatu ya Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa aliowakabidhi wakati wa kufunga maonesho hayo. Wengine ni Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Stella Manyanya (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe. Hamis Hafidh Hassan (mwenye tai ya blue) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara, Bw. Edwin Rutageruka (mwenye suti ya blue).
 Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason (katikati) akiwapongeza washiriki wa Maonesho kwa ushindi wa pili mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka leo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,        Bw. David Elias, akiwa ameshikilia zawadi ya cheti cha ushindi wa pili mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla ya kufunga maonesho ya Saba Saba leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Bw. Christopher Anyango.

Wakurugenzi wakiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa maonesho ya 42 ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) kwa mwaka 2018 mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi wa pili kwenye hafla ya kufunga maonesho hayo Jumamosi Julai 13, 2018 kwenye viwanja vya Maonesho, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

VOA SWAHILI: Duniani Leo Julai 13, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO SAUDI ARABIA

$
0
0

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo katika kozi mbalimbali kutoka Serikali ya Saudi Arabia.
Mafunzo hayo yatatolewa katika Chuo Kikuu cha Imam Abdulrahman bin Faisal kilichopo Saudi Arabia. Taarifa kamili kuhusu ufadhili, kozi na taratibu zote za namna ya kuomba zinapatikana kupitia tovuti ya Chuo hicho www.iau.edu.sa 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
12 Julai, 2018

WAKULIMA DAKAWA WANUFAIKA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

$
0
0
Na Mwandishi Maalum - DAKAWA
Wakulima wa kilimo cha Mpunga katika skimu ya kilimo cha Umwagiliji ya Dakawa wamenufaika na kilimo hicho baada ya serikali kukarabati mindombinu ya umwagilijai ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ofisi, ukarabati wa pump na  mifereji ya upili.
Hayo yameelezwa Mjini Dakawa na  Mhandisi wa Kanda ya Morogoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Senzie Meeda, alipozungumza na waandishi wa habari  walipotembelea skimu ya umwagiliaji ya Dakawa.
Mhandisi Meeda, ameeleza kuwa Serikali kupitia shirika la kimaitaifa la misaada la Marekani USAID lmetumia takribani kiasi cha shilingi Bilioni 20, katika ujenzi wa skimu hiyo,  na mpaka sasa asilimia themanini (80%) ya kazi hiyo inaendelea vizuri na inategemea kukamilika mwezi December mwaka huu.
“Njia zote za kwenda mashambani zinapitika, maeneo ya pembezoni ambayo yalikuwa hayafikiki mwanzoni sasa yanafikika, Pump Mpya za kisasa zinazotumia umeme mdogo zimefungwa hivyo uzalishaji umeongezeka ambapo mkulima anaweza kuvuna hadi tani sita (6) kwa hekta hili limesaidia sana kuongeza kipato na kutengeneza ajira.” Alisema Mhandisi Meeda.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha wakulima wadogo wa umwagiliaji Dakawa Bi.  Bertha Chilosa, ametoa shukrani kwa serikali kwa niaba ya wakulima wa dakawa na kusema kuwa kilimo kimekuwa na uchumi mkubwa katika eneo hilo na kubadilisha maisha yao na kuiomba serikali kuwasaidia wakulima hao kutafuta masoko ya uhakika ili kuwe na bei ya uhakika.
“Naiomba serikali itusaidie katika jambo hili, maana kutokuwa na soko la uhakika kunasababisha madalali wanakuja hapa kununua mpunga kwa bei ya kulangua na kutasababishia sisi wakulima wadogo kupata hasara, Naiomba serikali ichukue jukumu hili, ili mkulima asinyanyasike, sambamba na hili, ninaiomba serikali iongee na Mabenki ili yaweze kutupunguzia riba katika mikopo tunayopewa.” Alisisitiza Bi. Bertha
Skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya dakawa ambayo ipo chini ya mradi wa Irrigation and Rural  Roads, katika program ya Feed the Future ina ukubwa wa hekta 3225 ambapo hekta 2000 zina miundombinu ya umwagiliaji, hekta 1000 bado hazijaendelezwa na hekta 225 ni za makazi na huduma za kijamii.
Shamba hilo la Dakawa lilijengwa na kumilikiwa na serikali kwa kupitia NAFCO tangu mwaka 1981 hadi mwaka 2003, na mwaka 2008 katika kubinafsisha mashirika ya umma  likakabidhiwa kwa ushirika wa wakulima wadogo Dakawa.
Na imeelezwa chama cha wakulima wadogo wa kilimo cha umwagiliaji dakawa, kina jumla ya wanachama 850 ambapo 500 ni wanaume na 350 ni wanawake.
  Mhandisi wa kanda ya Morogoro, kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Senzie Maeda, akiongea na waandishi wa habari katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji cha Dakawa, kilichopo katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
 Miundombinu inayopeleka maji katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Dakawa iliyojengwa na Shirika la Kimataifa la misaada la Marekani (USAID) kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliji.

 Mwenyekiti Msaidizi wa cha Chama cha wakulima wa umwagiliaji Dakawa Bi.Bertha Chilosa akiongelea  Mafanikio na baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima katika kilimo hicho.
 Moja ya shamba la mpunga lililopo katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji cha Dakawa mkoani, Morogoro.


Wakulima wakiweka katika magunia  mpunga uliyovunwa na kifaa maalum cha kuvunia zao hilo katika moja ya shamba lililopo katika skimu ya umwagiliaji ya Dakawa mkoani Morogoro.

WIZARA YA MADINI YAKABIDHI ENEO LA MRADI WA SMMRP KWA MKANDARASI WILAYANI MPANDA

WASIFU WA KAMISHNA JENERALI MTEULE WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI

$
0
0
KAMISHNA JENERALI MTEULE WA JESHI LA MAGEREZA, 
DCP PHAUSTINE  M. KASIKE,ndc

CGP Mteule DCP Phaustine M. Kasike, Alizaliwa mwaka 1965 na alipata Elimu ya Sekondari katika Shule ya Iyunga, Mbeya Mwaka 1984 na Elimu ya Kidato cha sita alihitimu katika Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro Mwaka 1987.
Alijiunga na Jeshi la Magereza katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya mwezi Mei, 1989 na kuhitimu Januari, 1990 ambapo alipata mafunzo ya awali ya uaskari Magereza.
Mwaka 1992 alipata mafunzo ya Uhusiano wa Kimataifa kwa ngazi ya Stashahada katika Chuo cha Diplomasia Tanzania, Dare s salaam.  Mwaka 1999 alitunukiwa shahada ya kwanza ya Mahusiano ya Kimataifa na Utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mwaka 2015 alitunukiwa shahada ya Uzamili katika masuala ya Usalama na Stratejia katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Tanzania (NDC) Aidha, amehudhuria pia kozi inayohusu Usimamizi wa Utekelezaji wa Sheria (Law Enforcement) nchini Ghana mwaka 2006.
Katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza amepandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Sajini wa Magereza(1990), Sajini taji wa Magereza(1993), Mkaguzi Msaidizi wa Magereza (1996), Mkaguzi wa Magereza (2001), Mrakibu Msaidizi wa Magereza (2005), Mrakibu wa Magereza (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (2010), Kamishna Msaidizi wa Magereza (2011), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (2017), Naibu Kamishna wa Magereza ( 2018).
Amewahi kufanya kazi katika nafasi ya Afisa Mafunzo Msaidizi Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu ya Magereza (1990- 1991 na 1993 – 1995), Afisa Msaidizi Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa Makao Makuu ya Magereza wakati huo huo Msaidizi Mkuu wa Jeshi la Magereza (1999 – 2007).

Aidha, Mwaka 2007 – 2012 alihudumu katika nafasi ya Afisa Msaidizi Kitengo cha Usalama Makao Makuu ya Magereza, Afisa Mwelekezi Mwandamizi Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Tanzania (2013  -  2017),  Mkuu wa Kitengo cha Parole (2017) na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (2018).  

 Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dar es salaam.
13 Julai, 2018.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF IDDI ATEMBELEA BANDA LA (NSSF) LEO

$
0
0


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Kaimu meneja Uhusiano na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Salim Khalfan wakati akimpa maelezo alipotembelea kwenye banda la shirika hilo katika maonesho ya Sabasaba yaliyomalizika na kufungwa leo kwenye viwanja vya (TanTrade) Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo katikati ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka na kulia ni Afsa Uhusiano na masoko Bi Angela Michael.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa (NSSF) mara baada ya kuwasili katika banda hilo leo kwa lengo la kulitembelea.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Afisa Uhusiano wa (NSSF) Bi Angela Michael wakati alipowasili katika banda hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Uhusiano na Masoko wa (NSSF) Bi. Angella Michael baada ya kutembelea katika banda hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa (NSSF) mara baada ya kutembelea banda hilo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 14, 2018

TFS NA WADAU WAANZA SAFARI YA KUTEMBELE A MSITU WA ASILI WA AMANI

$
0
0
Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),Mariam Kobelo  mapema leo asubuhi akigawa Vipeperushi kwa Wakazi wa Dar es Salaam ambao wanafanya safari ya kutembelea Msitu wa Asili wa Amani uliopo Muheza mkoani Tanga ,Safari hiyo ambayo imeratibiwa na TFS imewakutanisha wadau mbalimbali kwenda kujionea mazao ya Misitu
Baadhi ya Wadau waliopo katika safari hiyo wakipitia majarida yanayoelezea Msitu wa asili wa Amani na Vivutio vyake.
Baadhi ya Wanafunzi waliojumuika katika Safari hiyo wakisoma Makala mbalimbali zilizomo kwenye Jarida linalozungumzia Msitu wa asili wa Amani.
Baadhi ya Wadau waliopo katika safari hiyo wakipitia majarida yanayoelezea Msitu wa asili wa Amani na Vivutio vyake.
Wadau wakiw akatika basi tayari kwa ajili ya Safari kuelekea Tanga kutembelea msitu wa asili wa amani
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images