Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalalama barabarani kwa kushirikiana na RSA wafanya ukaguzi wa magari Stendi ya nanenane Dodoma

$
0
0
Na.Vero Ignatus .Dodoma. 

Taasisi ya RSA kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kimefanya ukaguzi wa magari yanayoingia na kutoka stendi kuu ya mabasi mkoani Dodoma nanenane.

Ukaguzi huo umeenda sambaba pamoja na kutoa elimu kwa abiria namna ya kufunga mikanda awapo ndani ya gari,kuzifahamu haki zao za msingi pamoja na kupaza sauti kutokaa kimya pale anapomuona dereva anakiuka sheria na taratibu za usalama barabarani

John Seka ni mwenyekiti wa RSA nchini amesema Imekuwa ni tabia ya Taasisi hiyo kufanya hivyo mara kwa mara ili kuwakumbusha madereva wajibu wao,kufuata taratibu na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa madereva wazembe .

"Tumejaribu kupenyeza elimu kuhusu maswala ya usalama barabarani na tumefanya hivyo kwasababu ajali zimekuwa zikiongezeka kila siku,hivyo tumeona na sisi kama RSA kuna umuhimu wa kupaza sauti kwaajili ya usalama barabarani"

Askari wa kikosi cha usalama barabarani wankituoncha mabasi mkoani Dodoma Koplo Athuman amewataka RSA kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi katika kutoa taarifa, pale wanapoona mwenendo mbaya wa madereva wawapo barabarani kwani itasaidia kupunguza ajali.Sisi askari hatupo mahali pote ila nyie RSA mkitupa taarifa tutazitendea kazi,endeleeni kutoa elimu kwa abiria na kwa madereva hii itasaidia kupunguza ajali.Alisema Athumani.

Katika ukaguzi huo uliofanyika katika stendi hiyo ya mabasi makosa mbalimbali yamegundulika likiwemo la baadhi ya mabasi kuwaongezea abiria nauli,magari kukosa mikanda,pamoja na baadhi ya magari kuktwa na ubovu mbalimbali.
Baadhi ya mabalozi wa Usalama barabarani wakiwa katika stendi kuu ya mabasi mkoani Dodoma.
Meneja wa TIRA Kanda ya Kati Stella Rutaguzaal akizungumza na mabalozi wa usalama barabarani leo Mkoani Dodoma
Mmoja wa askari wa kikosi cha usalama barabarani akimsaidia mmiliki wa mabasi ya Kamwana Nassoro Khlfani


CHUNYA WAKABIDHIWA UTEKELEZAJI MRADI WA SMMRP

Rais Magufuli awaapisha Balozi Sokoine na CGP Kasike Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike ( watatu kutoka kulia),Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Balozi Joseph Edward Sokoine(watatu kutoka kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wapili kutoka kulia, viongozi wengine wa Serikali pamoja na Maafisa mbalimbali kutoka Jeshi la Magereza nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike ( watatu kutoka kulia),Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Balozi Joseph Edward Sokoine(watatu kutoka kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wapili kutoka kulia, viongozi wengine wa Serikali pamoja na Maafisa mbalimbali kutoka Jeshi la Magereza nchini.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizugumza jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike pamoja na Kamishna Mstaafu wa Jeshi hilo la Magereza Dkt. Juma Ali Malewa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Phaustine Martin Kasike mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 15, 2018

BANDARI YA NYAMIREMBE MKOANI GEITA KUFUFULIWA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (MB), ametembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani Geita akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Deusdedith Kakoko, pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Mhandisi Harun Senkuku. 

Miradi aliyoitembelea ni pamoja na Bandari ya Nyamirembe iliyoko kijiji na Kata ya Nyamirembe Wilayani Chato ambayo ilikua ikitumika tangu enzi ya Mkoloni ambayo kwa sasa haifanyi kazi. Waziri amewaeleza wananchi wajiandae kufurahi kwani muda si mrefu bandari hiyo itafufuliwa na kuanza kazi; ni baada ya kujitokeza kumlaki kwa fuaraha baada ya kumuona akitembea kwenye bandari hiyo. 

Amesema “mwezi wa nane mwaka huu tunasaini mkataba, tunairudisha Bandari ya Nyamirembe. Na sasa tunajenga meli kubwa, itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria elfu moja mia mbili (1,200), mizigo tani mia nne (400) ambayo itapita hapa kwenda Bukoba ndiyo maana kituo hiki lazima tukijenge na mkandarasi anaingia hapa mwezi wa nane. 

Hivyo ni ushindwe mwenyewe mwananchi kwa sababu sasa meli itakuwepo, barabara ya lami ipo, kiwanja cha ndege kinaendelea kujengwa unataka nini tena?” alimaliza kwa kushangiliwa na wananchi. 

Kisha,  Waziri ametembelea na kujionea maendeleo ya hatua ya ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo yenye urefu wa kilomita sitini na saba (Km.67) inayojengwa kwa kiwango cha lami na kufurahishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kupewa taarifa kuwa, barabara hiyo imeshajengwa hadi kilomita hamsini na saba (Km.57) hivyo bado kilometa kumi (Km.10) ili iweze kukamilika. 
 kibao cha bandari ya nyamirembe
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (wa pili kushoto) na alioambatana nao wakitafakari jambo.
 Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (mweye kofia nyeusi-kulia) ,akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari,Mhandisi Deusdedith Kakoko, (kushoto) wakitembea wakati wa ukaguzi wa bandari hiyo.
Barabara ya bwanga-biharamulo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe (kulia) akipeana mkono wa kwaheri na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

KIONGOZI wa mbio za mwenge mwaka huu, Charles Kabeho ,amekataa kuzindua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.

Hali hiyo imezua sintofahamu mara baada ya kusomwa ripoti ya matumizi ya fedha ambazo hazijaeleweka zimetumikaje huku serikali ikiwa imechangia kiasi cha sh.milioni 400.

Aidha kwa mujibu wa taarifa ya wilaya imedaiwa wananchi wamechangia milioni tatu wakati taarifa ya mkoa inaonyesha ilichangia milioni moja.Akizungumza kwenye kituo hicho cha afya, Kabeho alishtushwa na kuhoji kutokea kwa hali hiyo.

Alimtaka mkuu wa wilaya atoe kauli yake na kukataa kuuzindua mradi mpaka watakapotoa taarifa ya uhakika.Kabeho aliasa halmashauri na wilaya mbalimbali ,kusimamia miradi ya maendeleo ili iendane na thamani halisi ya fedha .

Nae mkuu wa wilaya ya Rufiji,Juma Njwayo aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama hususani taasisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) kufuatilia suala hilo.Kati ya miradi tisa ambayo ilipaswa kukaguliwa,kuwekwa jiwe la msingi na kuzinduliwa wilayani Rufiji ,iliyogharimu bilioni 2.654.40 mradi huo mmoja ulikwama kuzinduliwa .

July 13 mwenge huo ulikuwa Rufiji na July 14 umetembelea miradi ya maendeleo katika wilaya ya Kibiti.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Charles Kabeho akiongea na mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ,wakati akikagua wodi ya watoto ikiwa ni sehemu ya majengo ya mradi wa kituo cha afya cha Ikwiriri ,Rufiji, mkoa wa Pwani.

WAZIRI WA UJENZI ATOA MAAGIZO MRADI WA BARABARA YA LAMI NYAKANAZI KABINGO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amemuagiza mkandarasi wa mradi wa barabara ya Nyakanazi Kabingo Nyanza road work  kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu kilometa 23 kati ya kilometa 50 za lami ziwe zimekamilika kwa kiwango cha lami.

Ametoa maagizo hayo jana wilayani Kakonko mkoani Kigoma wakati alipoanza ziara yake akitokea mkoani Geita ambapo alianza kwa kutembelea barabara hiyo inayounganisha mkoa wa Kigoma na mikoa mingine.

Mhandisi Kamwelwe amesema wananchi wa Mkoa wa Kigoma hawajawahi  kuona lami, hivyo wanashauku kubwa ya kuona barabara hiyo ya lami inakamilika na Rais amewaletea mradi huo lazima na wao wafaidi ndani ya utawala wa awamu ya tano na wao wapate barabara.

Amesema barabara hiyo imepitiliza muda kwani ilitakiwa iwe imekamilika na kwa sasa wataenda na mkandarasi huyo kwa kupeana muda wa kukamilisha kazi kidogo.Pia amewatala Kampuni ya Nyanza road work kumsimamia mtu waliomuajiri kufanya kazi usiku na mchana ilimradi ukamilike kwa wakati."Nimeanza kumkagua Nyanza road work sijaridhishwa na mradi  unavyoendelea.Mradi huu umeanza mwaka 2014  na ulitakiwa uwe umekamilika.

Aidha amesema tayari wametanganza zabuni ya mradi mwingine wa Kabingo hadi Nduta kilomita 89 baada ya mienzi miwili watasainiana mkataba na mkandarasi mwingine aanzie hapo.Amefafanua malengo ni  miaka miwili maeneo yote yaliyobaki mkoani Kigoma yatakuwa na wakandarasi  ili mkoa wa Kigoma ufunguke kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema wananchi wanataka barabara iwepo na lami wamechoka vumbi kila siku, na  kuwataka wakandarasi kasi walioionyesha leo baada ya kusikia Waziri anakuja waendeleze kasi hiyo.

Waziri huyo amewasili jana mkoani Kigoma ambapo atakuwa katika ziara ya siku nne,ambapo akiwa mkoani hapo atatembelea barabara ya Nyakanazi Kabingo na Kasulu Kidahwe zenye wakandarasi pamoja na kutembelea bandari ya Kigoma na Uwanja wa ndege.
Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano Muhandisi Isack Kamwelwe (pichani kati) akitoa malekezo kwa Meneja mradi wa barabara ya Nyakanazi-Kabingo kutoka kampuni ya Nyanza Road Work Massimo Cartula kuhusiana na ujenzi wa barabara hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala
 Ujenzi wa bara bara Nyakanazi-Kabingo ukiendelea kwa kusua sua,ambapo Waziri Ujenzi amutolea maagizo mazito kuhakikisha mradi huo
ifikapo Agosti 30 mwaka huu kilometa 23 kati ya kilometa 50 za lami ziwe zimekamilika kwa kiwango cha lami.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 2 MKURANGA

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii

MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani yenye zaidi ya Sh. bilioni 2.9.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filibeto Sanga wakati alipokuwa akisoma taarifa ya Wilaya hiyo ya miradi ya Maendeleo wakati wa Mwenge huo ukiwa wilayani hapo.

"Miradi itazinduliwa katika mwenge huu na imetekelezwa kwa nguvu za wananchi. Katika kuchangia nguvu zao,Serikali kuu kutuwezesha fedha ikiwamo na wadau wa maendeleo," amesema.Aliongeza kuwa miradi hiyo ya maendeleo itasimamiwa vizuri ili kuwawezesha wananchi kunufaika nayo.Pia amesema miradi yote ipo katika ubora na imesimamiwa kikamilifu kutokana na fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi hiyo.

Akizungumza kuhusu elimu amesema kuwa,Wilaya imejikita katika kusimamia suala la elimu ambapo idadi ya wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na chekechea inaongezeka kila mwaka.Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo amesema kuwa Mkoa huo una wilaya saba ambapo miradi ya maendeleo yenye zaidi ya thamani ya shilingi bilioni 162 itazinduliwa katika mbio hizo za mwenge.

Ndikilo aliyasema hayo wakati akikabidhiwa mwenge na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.Ndikilo alikabidhiwa Mwenge na Makonda,katika kijiji cha Kipara Mpakani kilichopo Mkuranga.Ndikilo amesema atahakikisha wakimbiza mwenge wote sita wanakaa kwa usalama katika Mkoa huo.
 Mku wa Mkoa wa Pwani Muhandisi,Everist Ndikilo  akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga.(picha na Emmanuel Massaka MMG)
 Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu  Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mkamba kilichopo kijiji cha Kizapala  Mkuranga  mkoa wa Pwani,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh.Abdallah Ulega .
 Kiongozi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu  Charles Kabeho akifungua vyumba sita vya vya madarasa ya shule ya msingi Kipara mpakani Mkuranga  mkoa wa Pwani.(picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi wa waliojotokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.


Rais Magufuli atengua uteuzi wa DC Kahama,Shinyanga na Amteua Anamringi Macha kuchukua nafasi hiyo

$
0
0
Mkuu wa Wilaya mteule wa Kahama mkoani Shinyanga,Ndugu Anamringi Macha


UTENDAJI, SIASA ZA JPM ZALETA MKUTANO WA CPC TANZANIA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii


NAOMBA kutumia nafasi hii kwanza kabisa kutoa salamu kwa Watanzania wote.

Pili naomba nitoe salamu zangu za unyenyekevu kwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk. John Magufuli.

Baada ya salamu hizo pia naomba nitumie nafasi hii kupongeza jitihada za Rais Magufuli katika kuwatumikia Watanzania wote na kubwa zaidi harakati zake za kuhakikisha tunapiga hatua.

Pia, ahsante Rais Magufuli kwa jitihada zako ambazo umekuwa ukizifanya katika kuhakikisha tunakuwa nchi ya kujitegemea kupitia rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu ametujaalia katika nchi yetu.

Ila Rais nikunong'oneze kuwa ujio wa Dreamliner umenikosha sana kama si kunifurahisha. Ni juzi tu macho ya Watanzania yameshuhudia ujio wa ndege hiyo kubwa na ya kisasa.Inahitaji uwe na akili za wendawazimu ili uweze kukosoa ujio wa ndege hiyo. Pia, inahitaji kujitoa ufahamu ili upate nafasi ya kuupotosha umma kuwa ujio wa Dreamliner haustahili.

Kwa mwenye akili timamu na anayejua nini maana ya maendeleo ataungana  na watanzania wote kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uamuzi wa kununua ndege kwa lengo la kuliboresha Shirika la Ndege la ATCL. Ahsante Rais.Baada ya utangulizi huo nielezee hivi leo hii nimeamua kujikita katika kuzungumzia urafiki kati ya nchi za Tanzania na China. 

Nazungumzia urafiki huo nikitambua kuwa Julai 17 mpaka Julai 18 mwaka huu Tanzania inapokea ugeni mkubwa ambao utahudhuria mkutano wa kidunia ambao unahusisha vyama vya kisiasa ambavyo vilikuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika.

Mkutano huo utafanyika jijini Dar es Saalam. Ni mkutano ambao umeandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Ni mkutano  mkubwa haswaa. Yaani mkubwa naomba unielewe. Kwa msisitizo niandike kwa herufi kubwa kwamba NI MKUTANO MKUBWA SANA.

Hivyo kabla ya kuzungumzia mkutano huo niombe nizungumzie alau kwa uchache urafiki wa miaka mingi kati ya Tanzania na China. Kwa kukumbusha tu uhusiano kati ya Tanzania na China umeleta faida kubwa za kimaendeleo.Kupitia urafiki huo kuna mambo mengi Watanzania tumenufaika nayo na wao China yapo mambo mengi ambayo wamenufaika nayo kutoka na urafiki wao na sisi.Uhusiano wa China na Tanzania umekuwa na mafanikio makubwa ya kuziunganisha nchi hizo katika kusaidiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Kila mmoja anaweza kuelezea namna anavyoona inafaa kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili lakini jambo la msingi na la kuzingatiwa Tanzania na China wamekuwa na urafiki wa muda mrefu uliofanikisha mambo mengi kufanyika.Kumbukumbu zinaonesha baada tu ya uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, wataalam wa kilimo, ujenzi na madini walifika kusaidia wenzao wa Tanzania katika fani zao.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake  walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam Machi 22, 2017 


Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong  walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam Machi 22, 2017.PICHA NA IKULU.

RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BARACK OBAMA ASIFIA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA BAADA YA KUMALIZA ZIARA BINAFSI YA SIKU NANE NCHINI

$
0
0

Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela
Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akipewa zawadi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela
Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira mara baada ya kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (pichani kushoto), alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela
Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP,Hamisi Issa mara baada ya kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (pichani kushoto), alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 yaNelson Mandela.PICHA NA IKULU

TAMUFO YAZIONYA KAMPUNI ZA KUUZA MUZIKI ZA NCHINI KENYA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umeyataka makampuni ya Kenya yanayouza nyimbo za wanamuziki wa Tanzania bila kufuata utaratibu kuacha kufanya hivyo mara moja.

Ombi hilo limetolewa na Rais wa TAMUFO Dk.Donald Kisanga mjini Arusha juzi wakati viongozi wa TAMUFO walipofanya mkutano na Vikundi mbalimbali vya Kwaya ili kuwajengea uelewa na kuhakikisha wanafaidika na kazi zao za muziki na kuwaunganisha na fursa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa gharama nafuu kupitia umoja huo.

"Natoa onyo kali kwa makampuni ya Kenya yanayouza nyimbo zilizoimbwa na watanzania na kurekodiwa na Tanzania kuuzwa kenya Kinyume cha Taratibu na kuwakosesha wanamuziki wa Tanzania Kufaidika na kazi zao na serikali kukosa mapato kupitia kodi" alisema Kisanga

Alisema katika mkutano huo Kampuni ya Kenya ya Africha ilikiri kosa na Kuahidi kuwalipa Wanamuziki Wa Tanzania Pesa zao bila masharti yoyote baada ya kiziuza bila ya kufuata taratibu na kuwa TAMUFO na kampuni hiyo watatiliana saini za makubaliano kwenye mkutano huo. 

Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel alivitaja Vikundi vilivyohudhuria mkutano huo kuwa ni Kwaya Kuu Habari Njema na Kwaya ya UinjilistI za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mjini kati Arusha, Kwaya kongwe za Ulyankulu Mapigano na Ulyankulu Barabara ya 13 zote za Tabora.
Wadau wa muziki kutoka Tanzania na Kenya wakiwa katika mkutano na viongozi wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), ulioshirikisha vikundi mbalimbali vya Kwaya ili kuwajengea uelewa na kuhakikisha wanafaidika na kazi zao za muziki unaoendelea jijini Arusha. Kushoto mbele mwenye tai ni Rais wa TAMUFO Dk. Donald Kisanga.
Majadiliano yakiendelea.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wamuaga Mkurugenzi Mtendaji Ian Ferrao

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania  Plc aliyemaliza muda wake, Ian Ferrao akiwapungia mikono wafanyakazi wa Kampuni hiyo  ikiwa ni ishara ya kuwaaga wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Plc aliyemaliza muda wake, Ian Ferrao akiwashukuru wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Plc, Ian Ferrao aliyemaliza muda wake  (kulia) akikabidhi zawadi na Meneja Ruzuku wa Vodacom  Vodacom Tanzania Foundation  Sandra Oswald  kwa niaba ya wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Affairs   wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania aliyemaliza muda wake, Ian Ferrao akivishwa shuka la kimasai  ikiwa ni sehemu ya zawadi na mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo,  wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Plc aliyemaliza muda wake, Ian Ferrao  akiwa na mke wake baada ya kukabidhiwa zawadi za mila za kimasai na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Plc aliyemaliza muda wake, Ian Ferrao akiangalia zawadi alipokuwa akikabidhiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo  wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MPINA ARUHUSU UINGIZAJI WA NYAVU ZA KUVULIA SAMAKI NA DAGAA KUTOKA NJE YA NCHI.

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameruhusu uingizaji wa vyavu za kuvulia samaki na dagaa kutoka nje ya nchi baada ya kubaini kuwa viwanda vya kuzalisha nyavu hizo vilivyopo nchini kushindwa kuhimili mahitaji ya soko la ndani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wavuvi.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya operesheni Sangara 2018 jijini Dodoma, Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu- Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatama kuhakikisha kuwa katika kipindi cha siku 14 awe amekamilisha kupitia maombi na kuruhusu uingizaji wa nyavu hizo kutoka nje ya nchi. Pia kuweka utaratibu ambao hautaathiri soko la viwanda vya ndani.

Mbali na hilo Waziri Mpina ameigiza wizara yake kuandaa mkakati wa kudhibiti upotevu wa mapato, usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini ili kuondoa mianya yote ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuweka ulinzi thabiti wa rasilimali za uvuvi.

Pia ametaka Wizara hiyo kufanya mapitio ya mkakati wa ufugaji wa samaki kwenye maji, kufufua vituo vya kuzalisha vifaranga na kufanya tathmini ya uwekezaji wa sekta binafsi na kuainisha mahitaji ya sasa ili kuongeza uzalishaji utakaochangia kupunguza nguvu ya uvuvi kwenye maziwa na hivyo kutokomeza uvuvi haramu, kuongeza ajira na upatikanaji wa malighafi za viwanda nchini.

Akizungumzia matokeo ya operesheni Sangara 2018, Waziri Mpina alisema jumla ya watuhumiwa 3,998 walikamatwa kwa makosa mbalimbali na kutozwa faini na wengine kufikishwa Mahakamani,

nyavu haramu 575,152, makokoro 11,144 na kamba za kokoro zenye urefu wa mita 859,304 zilikamatwa na kuteketezwa kwa moto.Pia ndoano 1,910, 135 zisizoruhusiwa kisheria ziliharibiwa.

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA MAENEO YA KILIMO

$
0
0
Wakulima katika eneo la Dakawa Wilayani Mvomero, wameiomba Serikali kuwaongezea eneo ambalo halitumiki kwa shughuli yoyote ile waweze kulitumia kwa kilimo cha mpunga.

Maombi hayo yametolewa baada ya kukamilika kwa ukarabati wa eneo lenye ukubwa wa hekta (2000), ambapo wananchi wamepata hamasa ya kulima baada ya kuona mafaniko ya tokanayo na kilimo cha umwagiliaji.

Akizunguma na waandishi wa habari katika skimu ya Dakawa, Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Senzia Maeda, amesema Serikali kupitia Tume hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani USAID pamoja na kampuni ya SDM Smith ambayo imesanifu ukarabati wa eneo la awali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa Hekta (500) katika hizo hekta (1000) na amesema kuwa makablasha ya zabuni yapo tayari.

“Hatua inayoendelea kwa sasa ni kwa Serikali kuu kupitia Tume kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuendeleza hilo eneo.” Alisisitiza Maeda. Na aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ilifikia uamuzi wa kuendeleza eneo la Dakawa baada ya kuridhishwa na ukulima wa kisasa

Awali, Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero, Bw. Florent Kyombo amesema pamoja na eneo hilo kuwa katika hatua nzuri ya uendelezwaji, Idara ya kilimo kupitia serikali ya wilaya na wataalam wa kilimo imeweza kuthibiti panya waharibifu wa mazao pamoja na ndege aina ya kwelea kwelea kwa kuharibu mazalio yao yote pamoja na suala zima la kuwasadia wakulima kupata mikopo katika baadhi ya mabenki nchini.

Bw. Arcado Ruhengiza ni mmoja wa wakilima katika skimu ya Dakawa ambapo yeye alisema kuwa endapo serikali itaongeza eneo kwa ajili ya kilimo cha mpunga, itawawezesha wakulima wengi zaidi kulima kisasa na kukuza sekta ya kilimo nchini kutokana na mafanikio waliyoyapata kupitia shamba hilo.

Mhandisi wa kanda ya Mororgoro kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Senzia Maeda, akiongea kuhusu upanuzi wa eneo lenye ukubwa wa Hekta (1000) kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Dakawa, wilayani Mvomero.
Ghala la kuhifadhia mazao lililojengwa na serikali katika skimu ya Dakawa wilayani Mvomero, ili kuweza kuwasaidia wakulima kuuza mazao yako kwa bei nzuri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake kuhusu mpango mzuri wa Serikali kwa wakulima wa kilimo cha mpunga kinachofanyika katika skimu ya Dakawa.
Katika Picha, Mkulima Bw. Arcado Ruhengisa akitoa Ombi la Upanuzi wa eneo lenye ukubwa wa Hekta (1000) kwa Serikali kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ili wakulima waweze kongeza pato la Taifa, ajira kwa vijana na chakula kupitia kilimo cha umwagiliaji.

WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA YA MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika silaha za jadi alizokabidhiwa na Wazee wa Mila wa Kisukuma katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Kituo cha Afya cha Tinde mkoani Shinyanga Julai 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wazee wa mila wa Kisukuma baada kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Tinde mkoani Shinyanga Julai 14, 2018.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Bw. Terence Little ambaye ni Asset Protection Manager wa Kamapuni ya uchimbaji madini ya Acacia na viongozi wengine wa Kampuni hiyo  wakati alipotembelea mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama Julai 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KANGI LUGOLA ATEMBELEA KITUO CHA UCHAPAJI NYARAKA ZA UHAMIAJI,KILICHOPO MTONI KIJICHI,JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kutoka kushoto), akimsikiliza Mchapaji wa nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na Idara ya Uhamiaji,Enos Lwinga, wakati alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kutoka kushoto), akimsikiliza Mchapaji wa nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na Idara ya Uhamiaji,Enos Lwinga, wakati alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akikagua  nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na Idara ya Uhamiaji,  alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam.Kulia  ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala, akifafanua jambo kwaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(kushoto), wakati waziri alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji ,Eva Kikoti  akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), wakati waziri alipotembela kiwanda cha uchapaji nyaraka hizo kilichopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam . Kulia  ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala.

“LAMBALAMBA MARUFUKU MKOANI SONGWE”-CHIKU GALLAWA

$
0
0
Waganga wote wa jadi wanaopiga ramli chonganishi maarufu kama Lambalamba wamepigwa marufuku kufanya shughuli hizo mkoani Songwe huku wenyeviti wa vijiji ambavyo lambalamba watabainika kuendelea na shughuli hizo, hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

Marufuku hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa katika kikao cha wadau wa Afya mkoani hapa ambapo ameeleza kuwa changamoto mojawapo ya sekta ya afya ni uwepo wa waganga wa jadi ambao huwapotosha wananchi kwa imani zisizo za kweli.

Gallawa amesema, “Hatutaki kuona wala kusikia hivi vikundi vya vya lambalamba, kazi yao kubwa ni ulaghai na kuwaibia fedha wananchi, na ninaagiza, mwenyekiti yeyote wa kijiji atakayebainika kuwaendekeza hawa watu tunaanza naye kumchukulia hatua kali za kisheria”.

Ameongeza kwa kuwaagiza wakuu wa wilaya zote mkoani hapa wasimamie kuhakikisha wananchi hawatapeliwi na lambalamba hususani wilaya za Mbozi na Ileje ambako lambalamba wameonekana mara kwa mara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi na Machifu Mkoa wa Songwe Mwenenzunda Mteleshwa amesema kuwa yeye hawatambui lambalamba hivyo serikali iwachukulie hatua za kisheria kwakuwa wanaenda kinyume na taratibu za utoaji wa huduma za jadi.
Mkuu wa Mkoa wa Chiku Gallawa akizungumza katika kikao cha wadua wa Afya kilichofanyika katika chuo cha Uuguzi Mwambani Mkwajuni-Songwe, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samwel Jeremia na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude.

MKURUGENZI TARIME MJI ATAGANZA MGOMBEA UDIWANI KATA YA TURWA KUWA MSHINDI, APITA BILA KUPINGWA.

$
0
0
Na Frankius cleophace Tarime.

Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa ameamua kumutangaza aliyekuwa Mgombea udiwani kata ya Turwa kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw Chacha Mwita Ghati kwa madai kuwa amepita bila kupingwa huku akieleza kuwa wagombea Wenzake kutoka vyama vya upinzani wamekosea kujaza fomu jambo ambalo lilisababisha msimamizi Msaidizi wa wa uchaguzi ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata kutowateua kuwa wagombea katika Uchaguzi huo mdogo.

Elias amesema kuwa Uteuzi umefanyika na Mgombea wa CCM akawa ameteuliwa pekee yake na baada wagombea wengine kutoka CHAHADEMA, ACT Wazalendo pamoja na NCCR Mageuzi kukosa sifa za kuteuliwa ili waweze kugombea ameweza kupitia mapingamizi yaliyoletwa na wagombea hao baada ya kijiridhisha akiwa na wataalamu wenzake akaamua kutangaza Mgombea huyo Mmoja kuwa amepitwa bila kupangwa.

“Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 45 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa No4 ya Mwaka 1979 sura ya 292 kinasema endapo mgombea aliyeteuliwa ni mmoja baada ya pingamizi kukamilishwa.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mimi anapaswa kutalifu mgombea kwa barua kuwa amepita bila kupingwa na pia nitafaamisha tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu suala hilo, hivyo mimi kama Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Tarime Mjii natangaza rasmi kuwa Mgombea wa CCM Chacha Mwita Ghati amepita bila kupingwa” alisema Elias.

Pia Mkurugenzi huyo amemutaka Chacha kusubiri mpaka pale atakapoapishwa na kukabidhiwa cheti kutokana na tarehe za uchaguzi zilizotangangazwa na Tume ya Taifa ya Uchgaguzi.“Pamoja na kwamba amepita bila kupingwa asianze kazi ya udiwani kwa sababu tarehe za Uchaguzi hazijafika mpaka Agosti 12 Mwaka huu na sisi ndo tutaapisha diwani huyo na kuanza kazi ya udiwani lakini kama kuna mtu upande wa pili hajakubaliana na maamuzi yangu sheria iko wazi atakata rufaa” alisema Ntiruhungwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime Mkoani Mara Elias Ntiruhungwa akitanganza rasmi mgombea Udiwani kata ya Turwa Chacha Mwita Ghati CCM baada ya kupita bila kupingwa.
Wananchi wakiwa katika ofisi ya Kata ya Turwa kwa ajili ya kusikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime akitangaza rasmi Mgombea udiwani kata ya Turwa.
Baadhi ya wanachama wa CCM Wakiwa na mgombea udiwani kata ya Turwa Chacha Mwita Ghati wa pili kutoka kushoto aliyevaa sare ya chama hicho.

JAFO AWAPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza wanafunzi na walimu wa Shule ya sekondari Kibaha kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kwenye matokeo ya kidato sita mwaka huu yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo katika shule hiyo ambayo ni miongoni mwa shule alizozitembelea Januari mwaka huu na kuweka mikakati ya kuhamasisha shule hizo zifanye vyema kwenye mitihani ya Kitaifa.

Waziri Jafo amesisitiza kwamba matokeo haya mazuri yanayoanza kujitokeza kwa shule za serikali yametokana na juhudi kubwa ya Rais John Magufuli katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ambapo shule kongwe zote zipo katika hatua mbalimbali ya ukarabati sambamba na maboresho mengine katika sekta ya elimu. 

Jafo amemshukuru Rais Magufuli kwa moyo wake wa kuipambania jamii ya watanzania hadi kufikia mafanikio hayo makubwa yanayoanza kujitokeza hapa nchini. 

Aidha Jafo ameanza mkakati wa kuzifanya shule za serikali hapa nchini kushika nafasi zaidi ya sita katika ya kumi bora kwa matokeo ya kidato cha sita mwakani. Katika kufanikisha mkakati huo, Waziri Jafo ameitisha kikao cha kazi kwa wakuu wa shule pamoja na walimu wa taaluma wa shule za sekondari za vipaji maalum na shule za serikali zilizoingia katika nafasi ya 30 bora katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu ambapo kikao hicho kinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma Agosti 2 mwaka huu.

Awali, kabla ya pongezi hizo,Walimu na wanafunzi wa Kibaha wamekiri wazi kwamba hamasa aliyotoa Waziri Jafo iliwafanya kuwa na uchungu na nguvu ya mapambano katika elimu hadi kufikia mafaniko hayo makubwa waliyoyapata.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kibaha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akikagua ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari Kibaha.
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live




Latest Images