Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Introducing "Bado" Remix by Mwasiti Featuring MwanaFA , Chege & Marioo


IJUE DREAMLINER

$
0
0
​Na Geofrey Chambua 
kutoka vyanzo mbalimbali 

 Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ni ya ukubwa wa wastani, yenye injini mbili inayotengenezwa na kampuni ya Boeing ya Marekani. 
Kwa mara ya kwanza ndege hii ilirushwa mnamo mwaka 2009 na ilikua ipewe jina la 7E7 (E Ikimaanisha Efficiency-Ufanisi) lakini ikabadilishwa na kuitwa 787 Ili kuendana na mazoea ya ;majina ya ndege a aina hiyo. 

Hata hivyo namba 8 inahusishwa na bahati (kwa kichina na ndio wanaoongoza kwa kununua ndege nyingi za aina hii. Kutegemea na Muundo na Toleo, Bei yake ni kati ya dola 146 hadi $200 milioni Uzito wake ikiwa bila abiria ni 117,617 kilograms, sawa na Tembo 29!!!!!!!na urefu wa BAWA ni sawa na Mita 60 (yaani utembee hadi nusu ya uwanja wa mpira uongeze mita 10) 
Matumizi yake ya mafuta ni wa asilimia 20 chini cha ndege ya ukubwa sawa na huo na ndiyo ndege ya Boeing inayotumia kiwango cha chini zaidi cha mafuta. 

 Injini zake zimejengwa kwa njia maalumu ili kupunguza sauti ndani na pia nje ya ndege kwa hadi asilimia 60. Madirisha yake ni makubwa kuliko ya ndege zingine za ukubwa kama huo kwa asilimia 65 (47 by 28 centimeters) 


Kinyume na mfumo unaotumiwa kawaida wa kufungua kuongeza au kupunguza mwangaza wa dirisha kwenye ndege, kwa ndege hii ni kibonyezo ambacho hutumika kwa kutumia teknolojia ya kabadilisha rangi ya kioo kukiwezesha kudhibiti mwangaza unaoingia.
Ina uwezo wa kubeba hadi abiria 262 ikiwa pia na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 13,621 bila kusimama. Boeing 787-8 ilijengwa kuchukua mahala pa ndege aina za 67-200ER na 300ER.

MICHUZI TV: TRA MBEYA YAJA NA MBINU MPYA KWA WAFANYABIASHARA

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 10, 2018

BREKING NYUZZZZ....: HAKIMU AKATAA KUJITOA KESI YA VIONGOZI TISA WA CHADEMA

$
0
0
Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, Wilbard Mashauri amesema hawezi kujitoa kusikikiza kesi ya uchochezi dhidi ya washtakiwa tisa ambao ni viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe lililomtaka ajitoe kwenye kesi hiyo, sababu ombi hilo halina mashiko na analikataa.

MMAREKANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KILO MBILI ZA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Raia wa Marekani mkazi wa jimbo la Michigan, Lione Lionel Rayford, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kukutwa na zaidi ya kilo mbili dawa za kulevya.

Mmarekani huyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha sheria Namba 15 (1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya sheria Namba 15 ya mwaka 2017. Inayosomeka pamoja na paragrafu 23 ya Jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200 marejeo ya 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 3 ya 2016.

 Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Constantine Kakula amedai kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Julai 4, 2018 huko katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Wanjah Hamza inedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa alikutwa akisafirisha Madawa ya kulevya aina ya Heroine yenye uzito wa kilogramu 2.188.

Hata Hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Madawa ya kulevya hadi mahakama Kuu au mpaka wapate kibali kutoka kwa DPP.

Kufuatia hayo, mahakama imeamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi Julai 19, 2018. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

WAZIRI ISACK KAMWELWE AZUNGUMZA NA BALOZI WA SERIKALI YA JAMHURI YA KOREA KUSINI

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akisalimiana na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania, Bw. Song Geum-young wakati alipokutana nae katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akifafanua jambo kwa ujumbe kutoka Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania na wawakilishi kutoka Wizarani kwake wakati alipokutana nao katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam leo.
 Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania, Bw. Song Geum-young akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati alipokutana nae katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akiagana na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania, Bw. Song Geum-young baada ya mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam leo.

NEC yafanya mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa Nchini

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage akifafanua jambo kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage (hayupo pichani) kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
  Baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage (hayupo pichani) kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Athumani Kihamia akifafanua jambo kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini na watendaji wa Tume hiyo kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage (mwenye tai nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa tume hiyo pamoja na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa mara baada ya kueleza taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu. Picha na MAELEZO

Yanga FB Fans FC yapiga mtu ‘mkono wa nyani’ wakati wa majaribio ya App ya Spocha

$
0
0
 Timu ya mashabiki na wanachama wa Yanga inayofahamika kama Yanga Fb Fans imeichapa mabao 6-4 timu ya wadau wa kandanda, Kandanda Fc, katika mchezo ambao mkali ulioombwa na Yanga kupitia app ya Spocha. Mchezo huu ulifanyika katika kiwanja Posta Kijitonyama siku ya Jumapili.

Spocha ni App ambayo ipo katika majaribio ya awali, ambayo kwa sasa inalenga kuzikutanisha timu mbalimbali za soka. Timu ambazo zimesajili katika App ya Spocha, zitaweza kupanga ratiba za mechi zao na kujaza matokeo,huku timu hizo pia zikiwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu za mechi walizocheza.
 Timu ambayo itakuwa imejisajili katika Spocha, itakutanishwa na timu zilizojiunga katika mkoa husika na kutokana na aina ya timu, mathalani timu za Maveterani zitaweza kuwasiliana vizuri na kupanga mechi zao.

 Kitu kingine kizuri kupitia Spocha ni kuwa matokeo yote yaliyojazwa katika App hii yataonyesha kila kinara wa mkoa au aina ya kundi ambalo timu ipo,mathalani Makampuni ya Simu, Benki au sekta ya Usafirishaji.

 Spocha imebuniwa na kutengenezwa na kampuni ya GALACHA na inapatikana kwa watumiaji wa simu zinazotumia Android tu kwa sasa, katika Google Play. Baada ya majaribio kukamilika Spocha itazinduliwa rasmi.

 Timu zote zilizoshiriki mechi hii, Yanga FB Fans na ya wadau wa Kandanda Fc zinapatikana katika Spocha kuanzia sasa, na kama kuna timu inahitaji mechi itatakiwa kupakua na kujisajili katika Spocha na zitatakiwa maombi ya mechi kupitia Spocha tu.

CARTOONIST HANGOUT

MICHUZI TV: BARIDI NDONDO CUP TUKUYU SIO YA MCHEZO MCHEZO

VIONGOZI MBALIMBALI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA TRA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akimwelezea haki na wajibu wa mlipakodi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Nduguru akimtambulisha Afisa wa TRA kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally (wa pili kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Afisa Mwandamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Julius Caesar wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kefa Mwambene akimkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.

(Picha zote na Benedict Liwenga)

TAMASHA LA NGOMA DANCE LA TULIA TRUST KUSHIRIKISHA MIKOA YOTE TANZANIA BARA, VISIWANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TULIA Trust waandaaji wa mashindano ya ngoma za jadi nchini wenye kauli mbiu ya "Tuuenzi Utamaduni Wetu" wanataraji kuanza mchakato wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 wakihusisha mikoa yote nchini na visiwani Zanzibar.

Akizungumza na vyombo vya habari Mratibu wa mashindano hayo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameeleza kuwa wako tayari kwa ajili ya mchakato huo  utakaofanyika kuanzia Septemba 20 mpaka 22 mwaka huu huko Rungwe- Tukuyu mkoani Mbeya.

Ameeleza  lengo la mashindano hayo ni kuuenzi utamaduni wetu na kuonesha dunia wana utamamaduni wao na wameanza katika ngoma za jadi ila wataenda mbali zaidi katika  nyanja nyinginezo kama vile lugha, chakula na mavazi.

Aidha ameeleza kuwa wanashirikiana na Serikali katika kupunguza umaskini, hivyo walengwa waone ngoma ni  kazi ambayo itawaongezea kipato, ameeleza kuwa kwa mwaka huu wamelenga kuwa na vikundi 108 vitakavyokutanisha washiriki takribani 2200 ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo vikundi 63 vilihusishwa na 2017 kulikuwa na vikundi 89 na washindi walipewa zawadi mbalimbali kama vile fedha taslimu, pikipiki na ile ya kuendelezwa kimasomo katika chuo cha Sanaa Bagamoyo katika ngazi mbalimbali na hadi kufikia sasa takribani washiriki 30 wamepata fursa hiyo.

Kuhusu mafanikio  Dk.Tulia ameeleza kuwa washiriki watapata zawadi mbalimbali na kuwezeshwa zaidi, na amesema kuwa hadi sasa wana mkataba na hoteli za kitalii ambazo ngoma za jadi hutumbuiza na mafanikio yaliyotia moyo zaidi ni yale ya kikundi cha Bujora dance kutoka jijini Mwanza kuwakilisha taifa nchini India katika miji 3 na kurudi na ngao ya  ushindi nchini.

Kuhusu utaratibu wa kuwapata washiriki hao Dkt Tulia ameeleza kuwa watashirikiana  na maafisa utamaduni kote nchini katika mchakato wa kupata washindi hao aidha ametoa wito kwa makampuni ya simu kuwasaidia wananchi hao kupitia nyimbo zao ili waweze kupata kipato.
Mratibu wa Tamasha la Tulia Trust Dance Festival Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo litakalofanyika Septemba 20 hadi 22 Rungwe Tukuyu Mbeya Mwaka huu.

UONGOZI YANGA WATAMBULISHA MOHAMED BANKA

$
0
0
UONGOZI wa Yanga umemtambulisha kiungo mahiri Mohamed Banka aliyekuwa anakipiga katika kikosi cha Mtibwa Sugar.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga Hussein Nyika amesema kuwa Banka amesaini kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kutumikia kikosi cha wana jangwani hao.

Amesema kuwa, wamemsajili Banka kwa mapendekezo ya kocha kwani aliweza kumfuatilia kipindi cha ligi kuu.

Kwa upande wa Banka mwenyewe amesema kuwa amekuja Yanga kucheza mpira na kuirjesha Yanga katika viwango vyake.

Banka amesema anajua kuwa kuna ushindani wa namba hasa kwa timu kubwa kama Yanga ila kikubwa ni mazoezi tu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga Hussein Nyika akiwa pamoja na Kiungo Mohamed Banka baada ya kutambulishwa pembeni ni Meneja wa timu Hafidh Saleh.

TDB KUIKOPESHA TANZANIA SHILINGI BILIONI 900 KUJENGA RELI YA KATI YA KISASA NA MRADI WA UMEME KILWA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (Trade and Development Bank-TDB), itaikopesha Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 400, sawa na takriban shilingi bilioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) na Mradi wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kilwa.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Rais wa Benki hiyo yenye Makao yake Makuu Jijini Nairobi Nchini Kenya, Bw. Admassu Tadesse, alipokutana na kufanya mazungunzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.

Bw. Tadesse amesema kuwa Benki yake imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati ya kisasa pamoja na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kilwa mkoani Lindi.

"Tanzania ni mdau mkubwa wa Benki hii ikiwa inashika nafasi ya 7 kati ya nchi na taasisi 37 zinazomiliki hisa zake ambapo inamiliki hisa asilimia 6.4" alisema Bw. Tadesse.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akijadiliana na ugeni wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika - TDB (hawamo pichani) kuhusu uboreshaji wa sekta ya nishati ya umeme ili kujenga uchumi wa viwanda.  Kulia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo.
 Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB, Bw. Admassu Tadesse (katikati) akitoa ufafanuzi wa mkopo wenye masharti nafuu utakaosaidia ujenzi wa Reli ya Kati ya Kiwango cha Kimataifa(SGR) na nishati ya umeme pamoja na miradi mingine midogomidogo. Kulia ni Mkuu wa Wakala wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB Bi. Neema Siwingwa na kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Kisheria wa Benki hiyo Bw. David Bamlango.
 Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (kulia) ukijadiliani na ujumbe wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB (kushoto) namna ya kufadhili ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa -(SGR) na Mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya Gesi wa Kilwa.
  Ujumbe wa Serikali ya Tanzania (kulia) ukijadiliani na ujumbe wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika –TDB kwenye picha ya pamoja mara baada ya majadiliano ya namna Benki hiyo itakavyoikopesha Serikali kiasi cha dola milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa pamoja na Ujenzi wa mradi wa Umeme wa Gesi wa Kilwa utakaozalisha megawati 318 za umeme.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO WAANZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA UTALII

$
0
0
Na Ripota Wetu, Arusha 
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kutekeleza mkakati wa kushirikishana na wawekezaji waliopo sekta ya utalii ili kubaini maeneo mapya yanayofaa kwa uwekezaji kwenye hifadhi hiyo.

Wajumbe wa Menejimenti ya NCAA wamefanya ziara ya kutembelea maeneo hayo yanayofaa kuwa uwekezaji katika huduma tofauti ikiwamo hoteli, kambi, utalii wa magari ya waya maeneo ya bonde la Ngorongoro na Embakai.

Chini ya uratibu wa Mpango wa matumizi bora (GMP), imeelezwa kwamba maeneo haya yataongeza makusanyo ya mapato kutokana na shughuli za utalii kwenye mamlaka ya hifadhi hiyo.

Akizungumza kwenye ziara hiyo Naibu Mhifadhi wa mamlaka hiyo Asangye Bangu alisema, ziara hiyo imelenga kuangalia maeneo yanayofaa kwa uwekezaji  kama hoteli,kambi za muda za kulala wageni ,utalii wa baluni na biashara nyingine ndani ya hifadhi ikiwamo kuhakikisha wanakuwa na mpango endelevu wa uhifadhi,utalii na jamii inanufaika
 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro Asangye Bangu akizungumza na wafanyabiahara wawekezaji waliofanya ziara ya kujionea maeneo mapya ya uwekezaji kwenye hifadhi hiyo. 
 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) Asangye Bangu kulia, akizungumza na wafanyabiahara wawekezaji waliofanya ziara ya kujionea maeneo mapya ya uwekezaji kwenye hifadhi hiyo.  
 Wawekezaji na baadhi ya wafanyakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro wakijadiliana baadhi ya masuala ya utalii pembeni mwa kivutio cha mwamba wa Nasera Rock kinavyopatikani hifadhin humo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii nchini (TATO), Wilbard Chambulo akiwaonyesha wawekezaji wenzake pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro baadhi ya maeneo yanayozunguka kivutio cha Nasera Rock.
 Baadhi ya wawekezaji waliotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Mhifadhji Asangye Bangu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANAYANGA WALIA NA ABBASI TARIMBA

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii

WANAYANGA wamechukizwa na kitendo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Yanga Abbasi Tarimba kuzungumza habari za klabu hiyo zisizokuwa na uhakika kwenye kituo cha redio.

Ambapo wamedai kuwa Mwenyekiti  huyo ameongozana mpinga maendeleo wa Yanga Mohammedi Msumi kwenda redioni,ikiwa walichotegemea  kutoka kwake ni kuelezea ameifanyia nini klabu hiyo toka alivyochaguliwa Juni 10 mpaka leo Julai 10 mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es  Salaam  Mwenyekiti wa  matawi ya klabu ya yanga Tanzania Bakili  Makele amesema  kuwa fedha za Sportpesa  zinatoka kwa mujibu wa mikataba na si kwa matakwa ya Tarimba kama anavyojinasibu kuwa amelipa wachezaji,ikiwa hakuna fedha yake yoyote  iliyopokelewa klabuni.

Makele amekanusha kuwa hakukuwa na taarifa ya kuvunjwa  kwa kamati hiyo ya Tarimba katika mkutano wao uliofanyika,ingawa  wanachama hao walileta hoja hiyo mezani

Makele amesema katika hoja hiyo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga alikataa na kwa kuwa hakuwa na majukumu ya  kuvunja mamlaka ya mkutano mkuu.

"Tunasikitika kwa hesmima ya Tarimba  hapaswi kukurupuka kama anavyopokea taarifa kwa akina msumi na kuzifanyia maamuzi,sasa tunaamini adui mwingine wa maendeleo ya klabu ya yanga ni yeye,amesema Makele.

WAZIRI LUGOLA AKABIDHIWA RASMI OFISI NA MWIGULU, ASEMA KIJITI ALICHOKABHIWA HATAANGALIA NYUMA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kijiti cha kuiongoza Wizara yake alichokabidhiwa na aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, atakikimbiza kwa kasi kwa kuwa yeye aliwahi kuwa mwanariadha. 
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano yaliyofanyika ofisini kwake, jijini Dodoma leo, Lugola alisema amekabidhiwa kijiti cha majukumu hayo mapya atahakikisha anasonga mbele kwa kutekeleza majukumu aliyopewa na Rais John Magufuli. 
“Leo nimekabidhiwa ofisi, nimekabidhiwa dhana alizokua anatumia Daktari wa Falsafa Mwigulu, pamoja na shughuli alizokua anazifanya mpaka hapa alipofikia, pia mimi niliwahi kuwa mwanariadha, na nilikua nashiriki mbio za kupokezana kijiti, na  unapokabidhiwa kijiti, hautazami nyuma, ni kuendelea na safari,” alisema Lugola. 
Pia Waziri Lugola alisema anapenda kuwaaambia Watanzania kuwa, atafanya kazi kwa kujiamini na yale mambo ambayo alielekezwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kuyafanyia kazi, anaahidi atayashughulikia pamoja na majukumu mengine ya kiutendaji. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo. Hata hivyo, Waziri Lugola alisema aliwahi kuwa mwanariadha, hivyo atahakikisha anasonga mbele kuendelea na safari, hata angalia nyuma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipongeza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba mara baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Waziri Nelson Kaminyoge, alipokua anataka kumkabidhi taarifa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba ilia aweze kukabidhiwa taarifa hizo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi ya Waziri huyo, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuaga aliyekua Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Mwigulu Nchemba, mara baada ya kukabidhiwa taarifa kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAKAMA WILAYA YA MBOZI YAHAIRISHA KUTOA HUKUMU KESI YA MBUNGE HAONGA WA CHADEMA

$
0
0
Na Emanuel Madafa,Mbeya 

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya imehairisha kutoa hukumu ya kesi ya jinai iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Chadema, Jimbo la Mbozi, Pascal Haonga na wenzake wawili.

Akihairisha kutoa hukumu hiyo leo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Nemesi Chami, amesema hukumu hiyo imehairishwa mpaka  Agost, 10 mwaka huu, kutokana na majukumu mengi ya kimahakama pamoja na uzito wa kesi yenyewe. 

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili wa Serikali Joseph Pande akisaidiwa na Baraka Mgaya

Aidha, kesi hiyo ya jinai namba 117/2017 inawahusisha washitakiwa watatu ambao ni Mbunge Pascal Haonga, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Karasha Mashaka Mwampashi na katibu wa Mbunge, Williferd Mwalusanya.

Imeelezwa kuwa Agosti 28 mwaka  2017, washitakiwa hao, wakiwa katika ukumbi wa ofisi za mamlaka ya Mji wa Mlowo, Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, majira ya saa nane mchana, waliwazuia askari polisi kutekeleza majukumu yao, kufanya vurugu na kukataa kutoka nje ya ukumbi.

Washitakiwa wote watatu wapo nje kwa dhamana na kwamba wanatetewa na Wakili Boniphace Mwabukusi, ambaye aliunga mkono uamuzi wa mahakama hiyo kwa kuamini itatenda haki kwa pande zote mbili.

Baadhi ya wabunge wa Chadema, walijitokeza kusikiliza kesi hiyo akiwemo Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda na Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Franky Mwakajoka.
Mbunge wa Jimbo la Mbozi (Katikati ) akiwa na watuhumiwa wengine pamoja na wafuasi wa Chadema , katika kesi inayomkabili Mahakama ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe .

PROF SILAYO AZUNGUMZIA UMUHIMU WA NYUKI, AELEZEA MIPANGO YA TFS KUHUSU ASALI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa asilimia 85 ya mazao yanachavishwa na nyuki hivyo wakiondolewa wanaweza kusababisha ukosefu wa chakula duniani.

Profesa Silayo amesema hayo jijini Dar es Salaam wakatiakizungumza katika Siku Maalum ya Asali ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza hatua mbalimbali zinazchukuliwa na TFS katika sekta ya Asali. 

Akifafanua zaidi amesema uchavishwaji wa mazao unafanywa na nyuki kwa asilimia kubwa, hivyo wakiondolewa duniani hakutakuwa na chakula."Kwahiyo watumiaji mnayo fursa ya kuuza nyuki...kuna makundi takribani milioni 10 ya nyuki ambao wamekuwa wakizagaa hovyo, hivyo kupitia fursa hii itatusaidia kuzalisha makundi ya nyuki ambayo yatauzwa sehemu mbalimbali," amesema.

Amesema uuzaji wa asali na nta umeongezeka ambapo mwaka 2012 ziliuzwa tani 137 na kuingiza pato la Sh. Bilioni 1.05 na kwa mwaka 2016 iliuza tani 241 sawa na Sh. Bilioni 2.
Amesema ongezeko hilo limechangiwa na maboresho mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika na hivyo katika kuelekea uchumi wa viwanda, sekta ya nyuki ni miongoni kwa sekta inayokuwa kwa kasi sana.

Profesa Silayo amesema mbali na mafaniko hayo kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo kutokufikiwa kwa wadau mbalimbali ambao wako pembezoni kwa nchi pamoja na ubora wa asali na mazao kutokufikia kiwango cha kimataifa.Akifafanua zaidi kuhusu asali, Profesa Silayo amesema amepata nafasi ya kuzungumza na wadau wa asali nchini na kwamba kwa sehemu kubwa wanahitaji kuendelea kuelimishwa zaidi kuhusu masoko.
Amesema TFS imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha mazingira na kuhamasisha bidhaa ya asali ambapo asali ya Tanzania ina soko kubwa na inapendwa. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(Tantrade), Edwin Rutageruka, Emmanuel Miselya amesema mazao ya asali yamekuwa yakiongezeka nchini ambapo tani 138 zinazalishwa.Amesema wameamua kuweka siku hiyo maalum yenye kauli mbiu ya 'Mazao ya Nyuki kwa Maendeleo ya Viwanda' lengo likiwa kuwapa fursa wadau mbalimbali ili kukutana na kubadilishana mawazo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki.Wakati huohuo wafanyabiashara wa asali nchini wamemetoa ombi la kupata soko la uhakika.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS )  Profesa Dos Santos Silayo akipewa maeezo kuhusiana na bidhaa ya Asali inavyopatikana na changamoto zake katika suala zima la biashara.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>