Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

MARUFUKU BUTURA NA BIASHARA YA MAGENDO KATIKA KAHAWA-DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Kagera

Biashara ya kuuza Kahawa nje ya nchi pasina kufuata utaratibu wa kisheria (magendo) imepigwa marufuku hivyo atakayebainika kuendelea na biashara hiyo atachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Agizo hilo limehusisha pia zuio la wananchi kuuza kahawa mbichi ingali bado shambani haijakomaa (Butula) kwani kufanya hivyo ni kudhoofisha na kuzorotesha juhudi za muda mrefu alizotumia mkulima wa kahawa na kumkosesha mapato stahiki.

Marufuku hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 10 Julai 2018 wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa.

Waziri Tizeba alisema kuwa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ambayo ndio mkataba wa wananchi na serikali yao inatoa maelekezo ya kuwezesha upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo kwa kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za Masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara.

Alisema serikali itajitahidi kutafuta bei nzuri ya zao la kahawa ndani na nje ya Afrika Mashariki ili wananchi wapate faida na tija ya Kilimo huku akieleza kuwa wakulima wa kahawa kote nchini hawawezi kuona mafanikio ya Kilimo hicho kwa kuendeleza biashara ya magendo sambamba na biashara ya kahawa mbichi ikiwa shambani (Butura).
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akieleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi wakati akizungumza na wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wadau wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini mkutano uliowakutanisha wadau wa zao hilo uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa zao la kahawa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isingiro Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018. Wengine pichani kulia ni waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Mhe Salum Kijuu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Tizeba wakikagua na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Msingi cha Karukwanzi Wilayani Kyerwa, Leo 10 Julai 2018.


DC TARIME AUNDA KIKOSI KAZI KUCHUNGUZA WALIOTAFUNA BIL 5/- ZA WANANCHI WA VIJIJI VITANO

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime 

MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Glorious Luoga ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza na kukamatwa kwa watu ambao wamehusika kutafuna fedha Sh.bilioni tano ambazo ni za wananchi wa vijiji vitano.

Amevitaja vijiji hivyo ni Kewanja, Genkuru, Kerende, Nyangoto na Nyamwaga. 

Akizungumzia fedha hizo Mkuu wa Wilaya amesema zilipaswa kuingia kwenye akaunti za vijiji kutokana na mikataba iliyokuwepo baina ya vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara.

Amesema lakini watu wachache wakafanya hujuma ya kujipatia fedha hizo kinyume cha sheria.Hivyo ametoa siku 14 kwa kikosi hicho kuhakikisha wote watakaotuhumiwa kutokana na sakata hilo kukamatwa mara moja huku mali zao zinazohamishika na zisizohamishika kukamatwa.

"Na wahusika wote kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu na fedha hizo lazima zirudishwe kwa ajili ya kufanya maendeleo ya wananchi."Hizi ni fedha nyingi ambazo zingeleta maendeleo ya wananchi.Nikipita wananitupia lawama kumbe fedha zipo zinaliwa na watu wachache.Siwezi kufumbia macho suala hili," Luoga.

Luoga amesema kampuni hiyo imeanza kujipatiwa fedha hizo baada ya kufoji mikataba na kusababisha kufuta mikataba ya Vijiji hivyo ya mwaka 1995 kufutwana kisha fedha hizo kuanza kulipwa na Mtu binafsi bila wananchi kunufaika .

Aidha ametoa mwito kwa jamii kuishi kwa kufuata sheria na kudaia kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika kuvuruga Serikali.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorios Luoga akiongea na Vyomba vya habari katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akionyesha baadhi ya Mikataba ilikuwa ikisainiwa na kampuni ya  Keng’anyi Enterprises Limited pamoja na Mikataba ya Vijiji Vitano ukiwemo Mkataba wa Mwaka 1995.
Baadhi ya Watumishi wa serikali wakiwemo watendaji wa kata wakiwa katika kikao hicho cha Mkuu wa wilaya ya Tarime

KAGERA SUGAR WAFANYA USAJILI WA WACHEZAJ SABA KWA WAKATI MMOJA

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TIMU ya Kagera Sugar 'Wana Nkurukumbi' wamefanya usajili wa wachezaji saba kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikoso chao msimu ujao wa 2018/19.

Katika usjaili huo Kagera wamemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa  Yanga na Majimaji FC msimu uliopita, Jerryson Tegete kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufikia makubaliano kwa ajili ya kuwatumikia Wanankurukumbi.

Katika usajili huo, Kagera wamefanikiwa pia kupata saini ya  aliyekuwa kipa namba moja wa Ndanda FC, Jeremiah Kisubi kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wakata miwa hao wa Kaitaba, Kagera pamoja na nahodha wake Khemedi Khoja anayepiga namba tatu tofauti uwanjani.

Wachezaji wengine ni kiungo mshambuliaji Majid Khamis kutoka Ndanda Fc kwa kuingia nae mkataba wa mwaka mmoja akiwa sambamba na mshambuliaji Omary Mponda naye kutoka Ndanda akiwa amekamilisha uhamisho wake kwa kusaini mwaka mmoja na Kagera pamoja na beki wa kati Amad Waziri kutoka Ndanda FC naye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga ndani ya Kaitaba na Kagera Sugar.

Beki wa kushoto aliyewahi kukipiga Yanga na Mwadui Fc David Luhende  amemwaga wino wa mwaka mmoja kuitumikia Kagera.Usajili huo unakua ni mkubwa kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu zote ikiwa ni kuimarisha kikosi chao.

MKUU WA WILAYA ARUSHA AIPONGEZA SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW KWA KUHAMASISHA ELIMU

$
0
0

Na Pamela Mollel,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro ameipongeza Taasisi ya Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha .

Aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa ambapo alisema shirika hilo limekuwa bega kwa bega katika kuhamasisha maswala mbalimbali ya Elimu na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo

“Foundation for Tomorrow wamekuwa mstari wa mbele sana katika maswala ya elimu mfano mzuri leo wameanda Tuzo maalumu kwa mwalimu bora ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa umahiri mkubwa”alisema Daqarro

Kwa upande wake Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Tuzo hiyo ni kutia hamasa miongoni mwa walimu waliobainika kufanya kazi zao kwa bidii na umahiri mkubwa

Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro aipongeza Taasisi ya Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha maswala ya elimu katika Mkoa wa Arusha awataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo' aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini hapa, ambapo Taasisi hiyo iliandaa Tuzo maalumu kwa mwalimu bora(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo ,iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Levolosi jijini hapa,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa wameaanda Tuzo hiyo kwa shule za msingi jiji la Arusha na Meru kwa walimu 20
Mkuu wa wilaya ya Arusha,,Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya sombetini,Caroline Kiyoja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilola kiserikali la Foundation For Tomorrow
Waalimu kutoka shule za msingi jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja Tuzo hiyo maalumu iliandaliwa na shirika la Foundation For Tomorrow kwaajili ya waalimu waliobainika kufanya kazi zao kwa umahiri mkubwa.

TAARIFA YA KIFO CHA JOYCE CRARA KIBAJA WA MAKONGO JUU JIJINI DAR

$
0
0

FAMILIA ya marehemu mzee Julius Vincent Kibaja wa Makongo Juu inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Joyce Crara Kibaja kilichotokea tarehe 5 /7/2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kitengo cha Mifupa Moi.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki kokote walipo.Taratibu zote za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Makongo Juu na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 14/7/2018 katika Kijiji cha Kwemhosi wilayani Muheza mkoani Tanga.

... Kwa maana mimi sasa namiminwa na wakati wa kufariki kwangu umefika ...Nimepiga vita vilivyovizuri mwendo nimemaliza imani nimeilinda ...2 Timotheo 4:6-7.

WAZIRI WA FEDHA AHIMIZA MAADILI TRA, AZUNGUMZIA UTOZAJI KODI KWA HAKI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya 

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Philipo Mpango ametoa onyo hatakuwa tayari kuona fedha ambazo zimepitishwa katika bajeti ya fedha ya mwaka 2018/2019 zikitumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa na atakaebainika atachukuliwa hatua kali. 

Mpango ametoa kauli hiyo jana alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ambapo alikutana na mkuu wa kitengo cha maadili na kutoa maagizo mbalimbali yakiwamo linalowataka watumishi wa kitengo hicho kufanya kazi kwa maadili.

Amefafanua kitengo hicho ni kitengo baba katika suala la maadili hivyo haitakiwi kuonekana mtumishi wake au wa idara nyingine akikiuka maadili ya kazi. Amewataka wasimamizi wa kitengo hicho wasicheze na nyoka na kwamba mtu anayekiuka maadili ya kazi hana tofauti na nyoka. 

"Mnatakiwa kuwa wakali ili fedha za umma zisipotee. Bajeti ya serikali imepita na leo(jana)imetimiza siku tisa tangu mwaka mpya wa fedha uanze. Hivyo kuweni makini."Katika kitengo cha maadili watu nane wamefukuzwa kati ya watumishi 23.Na kwangu nitakuwa tayari kufukuza hata wote iwapo nitabaini maadili hayazingatiwi. Hivyo hakikiesheni mnasimama katika maadili ya kazi,"amesema.

Wakati huo huo amesema asilimia 60 ya Watanzania ni vijana hivyo wanatakiwa kuelimishwa mapema ili wawe na utamaduni wa kulipa kodi.
Pia amewatakaTRA kuhakikisha wanawapenda walipa kodi na kuwatoza kwa haki kulingana na shughuli anayoifanya.Amesisitiza kodi za wananchi zikusanywe vizuri kama ilivyopangwa ambapo akiwa hapo amewaleza TRA kuwa tarakimu za fedha zilizopo zinafurahisha lakini inatakiwa zifike ili zisaidie jamii. 

Mpango amefafanua ni vema watumishi wa Idara hiyo kutambua kuwa kitengo hicho si sehemu ya kufanya mambo ya hovyo hovyo. "Najua ujumbe umetumwa na umefika,kuweni makini na fanyeni kazi kwa ajili ya taifa letu, "amesisitiza Mpango. 

MWENYEKITI WA CCM RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongoza Kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichofanyika katika Ofisi ndogo za chama  hicho Lumumba Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli  akipiga makofi  pamoja na wajumbe wengine wa Kamati Kuu (CC) ya CCM mara baada ya kuwasili  ukumbini kwa ajili ya kuongoza Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ndogo za chama  hicho Lumumba Jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

Kesi ya Mbunge wa Mbozi Pascal Haonga na wenzake yapigwa tarehe


Kenya-Swiss deal

Waziri Mwakyembe afanya ziara ya kukagua Miundombinu ya Viwanja vya Michezo Mkoani Manyara

$
0
0
.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye miwani) akimsikiliza Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Sekondari ya Singe (Mwenye koti la kijivu) Bw. Amos Sungi alipotembelea viwanja vya michezo vilivyopo katika shule hiyo leo Mkoani Manyara.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto) akikagua kiwanja cha mpira wa miguu kilichopo katika shule ya Sekondari ya Singe alipokuwa katika ziara ya kukagua viwanja vya michezo leo katika Mkoa wa Manyara.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Singe (hawapo katika picha) alipofanya ziara ya kuwatembelea miundo mbinu ya viwanja katika shule hiyo leo Mkoani Manyara.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akionyeshwa ramani ya kiwanja cha mpira na Mpima Ardhi wa Halmashauri wa Mji wa Manyara Bw. Iddi Lulamia  wakati wa ziara ya kukagua miundo mbinu ya michezo katika Mkoa wa Manyara.

 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waalimu wa Michezo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, leo Mkoani Manyara.

Serikali yaendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya Filamu Nchini

$
0
0
 Na Lorietha Laurence-WHUSM, Manyara. 
Serikali imendelea kuweka msukumo wa kukuza Sekta ya filamu nchini,kwa kuendeleza utafiti, ubunifu na teknolojia ikiwemo kujenga mazingira wezeshi kwa wadau wake ili kuleta matokea chanya katika tasnia hiyo . 
Hayo yamesemwa Mkoani Manyara na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu katika Mkoa huo yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini. 
 Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Mkoa wa Manyara una mazingira mazuri yenye fursa ya kuandaa filamu nzuri zenye ubora na uhalisia wa vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Mkoa huo. 
 “Watu wa Manyara tumieni fursa hii nzuri mliyoipata katika mafunzo haya ambayo yanatolewa bure kwa kutengeneza filamu nzuri, ukizingatia mazingira yenu yana uhalisia mzuri wa kuvutia” amesema Dkt, Mwakyembe. 
Aidha alizidi kufafanua kuwa kuna mambo mengi ya kuweka katika filamu, ikiwemo tamaduni zinazopatikana katika Mkoa wa Manyara, milima pamoja na uoto wa asili kitu kitakacholeta hali ya utofauti na wa kipekee . 
Naye Kaimu Katibu Tawala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Misaile Musa alizidi kuwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwa makini ili kuleta mabadiliko kwa kutengeneza filamu bora zenye viwango. 
 Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bibi. Joyce Fissoo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu nchini, ili kuwa na waandaji bora wa filamu.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na wadau wa filamu (hawapo katika picha) wakati wa kufungua mafunzo  ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu leo katika Mkoa wa Manyara.

 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Misaile Musa (kushoto) akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa  mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa Filamu wa Mkoa huo, ambayo yameandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kulia ni Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo akiwasilisha mada kuhusu wajibu na majukumu ya Bodi ya Filamu katika kukuza sekta ya filamu , leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta hiyo wa Mkoa wa Manyara.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Multi Choice nchini Bw. Johnstone Mshana akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu leo  Mkoani Manyara.
Wadau wa sekta ya filamu wa Mkoa wa Manyara wakifuatilia uwasilishwaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wadau hao leo Mkoani humo.  Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Susan Kiwanga, akichangia hoja katika taarifa hiyo, ya utendaji wa shirika hilo. 


Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, Charles Kitwanga (kulia), akichangia hoja katika taarifa hiyo, ya utendaji wa shirika hilo.  
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa maelezo zaidi kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, kuhusu utekelezaji wa taarifa hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Seleman Kakoso na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moshi Seleman Kakoso, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Posta wakati akihitimisha mkutano huo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu, wakiwa katika picha ya pamoja kionesha alama ya dole gumba ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kauli mbiu ya Shirika ya 'Lets Go' mara baada ya kumaliza ziara yao kwenye shirika hilo, Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

WAZIRI KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA MSITU WA NORTH EAST MPANDA, TONGWE NA MAPOROMOKO YA NKONDWE MKOANI KATAVI

$
0
0
.
Muonekano wa Maporomoko ya Nkondwe jana ambayo ni moja ya kivutio cha utalii, katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu Maporomoko ya Nkondwe na fursa za utalii zinazopatikana katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Salehe Mbwana Mhando.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wakifurahia maporomoko ya Nkondwe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya asili mkoani humo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia maumbo ya asili kwenye miamba iliyopo karibu na Maporomoko ya Nkondwe ambayo ni miongoni mwa kivutio cha utalii katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi jana.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Salehe Mhando.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya Tanganyika akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo, Selehe Mhando (kulia kwake) wakiwa wamepumzika kidogo baada ya kupanda mlima uliopo ndani ya Msitu wa Hifadhi wa North East Ugala baada ya kutembelea maporomo ya Nkondwe jana.

Bilioni 45 kupeleka umeme kwa Vijiji 150 Morogoro

$
0
0
Na Veronica Simba – Kilosa
Imeelezwa kwamba, jumla ya shilingi bilioni 45 za kitanzania, zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kupeleka umeme katika Vijiji 150 vya Mkoa wa Morogoro, kupitia Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA.)
Hayo yamebainishwa Jumatatu, Julai 9, 2018 na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Mandela, Kata ya Magole, wilayani Kilosa; ambapo pamoja na mambo mengine, alizindua rasmi uwashaji wa umeme wa REA IIIA, kwa Mkoa wa Morogoro.
Akifafanua zaidi, Naibu Waziri alisema kuwa, miradi hiyo kwa ujumla wake, katika Awamu ya Kwanza inajumuisha Vijiji 3559 ambavyo vitatumia takribani shilingi bilioni 900 za kitanzania.
“Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais wetu John Magufuli, imejielekeza katika kuhakikisha nishati inafika kwenye maeneo mengi nchini ili kwenda kusukuma uchumi wa viwanda ambao tunaujenga,” alisema.
Akielezea hatua itakayofuata baada ya uzinduzi huo, Naibu Waziri alisema kuwa, ni kuwaunganishia wateja umeme katika maeneo husika, ambapo alisema gharama yake ni shilingi 27,000 tu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akikata Utepe maalum, kuashiria uzinduzi rasmi wa uwashaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA), kwa Mkoa wa Morogoro. Tukio hilo lilifanyika Jumatatu, Julai 9, 2018 katika Kijiji cha Mandela, Kata ya Magole, wilayani Kilosa.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mfuru, Kata ya Kitete, Wilaya ya Kilosa, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme kwa Mkoa wa Morogoro, Jumatatu, Julai 9, 2018.
 Mwakilishi wa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme wilayani Kilosa, kupitia Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA), Wingod Siyao kutoka Kampuni ya State Grid Electrical & Technical Works Ltd; akitoa ahadi mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba chekundu), kukamilisha Mradi huo kwa wakati. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kijijini Mfuru, Kata ya Kitete, Wilaya ya Kilosa, Jumatatu, Julai 9, 2018.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mandela, Kata ya Magole, Wilaya ya Kilosa, wakitoa maoni yao kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), wakati wa hafla ya  kuzindua rasmi uwashaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA), kwa Mkoa wa Morogoro. Tukio hilo lilifanyika Jumatatu, Julai 9, 2018. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

JUMLA YA WAHAMIAJI HARAMU 1470 KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI WAKAMATWA MKOANI KAGERA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

JUMLA ya wahamiaji haramu 1470 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa Mkoani Kagera kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ofisa uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo alisema kuwa kwa kipindi cha January hadi June 30 mwaka jumla ya wahamiaji haramu walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya mipaka iliyopo Mkoani humo.

Towo alisema kuwa kati yao Warundi 994,Waganda 223,Warwanda 193,Wathiopia 19,wacongo 39 na wakenya 2 jumla yao ni 1470.

Alisema jumla ya raia 5,787 wa Burundi kutoka kambi za Mtendeli,Nduta na Nyarugusu zilizopo Mkoani Kigoma pia kambi ya rumasi Ngara wamerejea nchini kwao kwa hiyari.Alisema jumla ya raia 90 kutoka Mataifa mbalimbali wamemaliza vifungo vyao katika Magereza yaliyopo mkoani Kagera na wote wamerejeshwa makwao.

"Kwa mwaka huu toka january hadi June hakuna mkimbizi yoyote aliyeingia nchini kwasababu kule kwao kwasasa kumetulia"alisema.

Ofisa Uhamiaji u huyo alisema kuwa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya utaifa linaenda vizuri Mkoani Kagera na mpaka sasa jumla wananchi 491513 ili kupata vitambulisho vya utaifa lengo ni kuandikisha wananchi 1,200,000.

Alisema pia zoezi la uzinduzi wa hati za kusafiria za kielectronic kwa mkoa wa Kagera ulifanyika tarehe 8 mwezi wa 6 mwaka huu linaenda vizuri kwani mpaka sasa wameshapokea jumla ya maombi 72 na hati 64 zimeshatolewa na kukabidhiwa kwa wahusika.
 Ofisa wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu y utendaji kazi wa uhamiaji Mkoa wa Kagera
Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Ofisa wa uhamiaji Mkoa wa Kagera Abdallah Towo ofisini kwake

KICHWA CHA UMTITI CHAIPELEKA UFARANSA KUINGOJA UINGEREZA AMA CROATIA KWENYE FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA SOKA 2018

$
0
0
Ufaransa wanamsubiri aidha Uingereza ama Croatia baada ya goli la kichwa la kipindi cha pili la Samuel Umtiti kutosha kuwapeleka Wafaransa hao kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Soka mwaka huu. 
Kipindi cha kwanza kiliisha butu ingawa makipa Thibaut Coutous wa Ubelgiji na Hugo Llorisa walipofanya maajabu ya kuokoa na kufanya mchezo ulale 0-0 hadi mapumziko. 
Pigo la kichwa la Umtiti kutoka majalo ya mpira wa kona lilitosha kuwatia wehu mashabiki wa Ufaransa. Ubelgiji walijaribu, bila mafanikio, kutunza rekodi yao ya kutofungwa, lakini Ufaransa walisimama kidete na kuhakikisha wanatinga fainali kuwasubiri aidha Uingereza ama Croatia wanaocheza kwenye nusu fainali ingine kesho. 

BRITISH COUNCIL IELTS

Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania

$
0
0

BALOZI wa Korea Kusini, Mh. Geum-Young Song amesema kwamba  atasaidia haja ya uwekezaji wa uunganishaji magari nchini Tanzania pamoja na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha tehama kwa nchi za Kusini, Kati na Mashariki ya Afrika.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Balozi huyo wa Korea Kusini alisema kwamba atahakikisha anafanya kila kinachowezekana kushawishi makampuni ya magari ya Korea kusini kuanza kuunganisha magari hayo nchini Tanzania.
Dk. Mengi katika mazungumzo hayo alisisitiza haja ya kuanza mazungumzo ya kina ya ushirikiano katika kuunganisha magari kabla ya kuingia katika masuala ya simu zenye utendaji wa kisasa (Smart Phones) na tehama kwa ujumla.
Alisema pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Mengi kuhusu haja ya kuwa na kampuni ya kuunganisha magari nchini Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda taifa kutengeneza magari yake yenyewe, alisema kama taifa wana mpango wa kusaidia Tanzania kuwa taifa la viwanda likiongoza katika tehama.
Alisema kwa kuwa taarifa na mambo mengi ya habari ndio nguvu kwa vijana kuelekea katika ustawi wangelipenda kuwa na  eneo ambalo vijana watalitumia katika kupata maarifa na kuyatumia kuboresha hali zao na kukua kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo Dk. Mengi alisema kwamba kuwapo na viwanda vya magari nchini Tanzania ni ndoto yake na kwamba alikuwa amepanga kwenda Sri Lanka kushawishi ushirika katika uunganishaji magari kuelekea kuyatengeneza Tanzania.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi akizungumza na Balozi wa Korea Kusini nchini, Geum-Young Song wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Biashara na Uwekezaji wa Korea, Hong Kyun Lee. Balozi wa Korea, Dk Mengi wazungumzia uunganishaji magari ya Korea nchini Tanzania.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.07.2018

OPERESHENI ENDELEVU YA UKAGUZI WA MGARI USIKU NA MCHANA ARUSHA YAPAMBA MOTO

$
0
0
Na.Vero Ignatus,Arusha.

Ni operesheni endelevu ya kukagua magari na pikipiki yenye makosa mbalimbali ya usalama barabarani mkoani Arusha ,ambapo jumla ya magari 1719 yalikaguliwa pikipiki 182,madereva 189 walipimwa ulevi na dereva mmoja wa basi alikutwa na kilevi, anashikiliwa na jeshi la polisi.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Ramadhani Ng'anzi amesema jumla ya makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyokamatwa kuanzia tarehe 07.07 hadi 09.07.2018 ni 1901 na jumla ya tozo na notification zilizokusanywa kwa kipindi hicho ni shilingi milioni hamsini na saba na thelatini elfu.(57,030,000)

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amesema mabasi ya abiria 102 yalikaguliwa kati ya hayo 7 yalikutwa mabovu ambapo yalizuiliwa yasiendelee na safari sambamba na malori 129 kati ya hayo 16 yamng'olewa namba kwa ubovu ili wamiliki wa magari hayo wakayatengeneze.

Kwa sababu mtu anaweza kwenda shimoni huko akarudi jionihiyo siyo issue,kari ni zima?inakiwango?dereva anayeendesha anasifa ya kuendesha!ndiyo kitu amabacho tunakitaka"alisisitiza RTO.mesema wameamua kufanya oparesheni hiyo usiku na mchana kwani madereva hao wanapaki magari mchana usiku wanayaweka barabarani kuendekea na shughuli kama kawaida.

"Tumeamua kufanya oparesheni hii mchana hayaonekani wanapaki kwahiyo usiku ndiyo tunafanya ili tuwapate " alisema Bukombe.Jumla ya pikipiki 161 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani na kuandikiwa faini ,leseni 365 zilikaguliwa kati ya hizo 104 zimekwisha muda wake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kikuu cha polisi Arusha,aliyepo kulia kwake ni Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Joseph Bukombe.Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha Joseph Bukombe akionyesha moja ya makosa waliyoyabaini baada ya kufanya ukaguzi kwenye moja ya Lori la kubebea mizigo.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya pikipiki zilizokamatwa zikiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani Arusha.

Mkaguzi wa Magari kutoka kikosi cha usalama barabarani akionesha jinsi ambavyo gari kwa nje linaonekana jipya lakini kwa ndani lina ubovu,kama inavyoonekana katika picha chuma kikiwa kimevungwa na mfuko wa kiroba
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images