Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

Wizara ya Ardhi Yaahidi Ushirikiano Kwa Naibu Katibu Mkuu Mpya

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) na kumuaga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(kulia) ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo leo Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu  ofisini Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu (aliyekaa mbele kushoto) na kumkabidhi vitendea kazi leo Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya kukaribishwa kwake katika ofisi za Wizara hiyo leo Jijini Dodoma.Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali  alikuwa Naibu wa Wizara hiyo, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika(katikati) na Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) wakifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi zawadi ya ua kwa ajili ya pongezi na kumuaga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusilukaambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo leo Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika(katikati) akimkabidhi zawadi na Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) katika hafla fupi ya mapokezi yake na kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka (kulia) leo Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NUSU FAINALI YA KWANZA YA WORLD CUP NI KESHO

$
0
0

Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
Nusu fainali ya kwanza ya Fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi inatarajiwa kuchezwa kesho kwa kuzikutanisha timi za Ubelgiji na Ufaransa.

Mchezo huo wa kwanza utakuwa  ni muhimu kwa makocha wote wa timu mbili , Roberto Martinez wa Ubelgiji na Didier Deschamps wa Ufaransa.

Kwa upande wa Kocha wa Ufaransa Deschamps ameweka wazi mkakati wake wa kutaka kuweka rekodi ya kushinda taji hili akiwa meneja baada ya kuiongoza Ufaransa kushinda taji hilo mwaka 1998 akiwa nahodha wa kikosi cha dhahabu.

Deschamps atapambana na mchezaji mwenzie aliyekua katika kikosi hicho cha dhababu mwaka 1998 wakichukua ubingwa wa dunia Thiery Henry ambaye yupo kwenye benchi la ufundi la Timu ya Ubelgiji kwa sasa

Martinez kwa upande wake anaongoza kikosi chake ambacho kinatajwa kuwa na wachezaji wengi nyota katika historia ya soka la Ubelgiji.

Ebelgiji iliwaondoa Brazil katika hatua ya robo faainali kwa mabao 2-1 wakati Ufaransa iliinyuka Uruguay kwa mabao 2-0.

VIGOGO WATANO WA KNCU LTD,TCCCO WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi

VIONGOZI watano wa Chama cha Ushirika mkoa wa Kilimanjaro(KNCU LTD) na Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Tanganyika (TCCCO) leo wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa Mashtaka tofauti yakiwemo ya uhujumu Uchumi.

Waliofikishwa Mahakamani na kupandishwa Kizimbani ni pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Kikuu cha Ushirika ,Kilimanjaro (KNCU) Aloisi Kitau (70) Makamu Mwenyekiti mstaafu wa KNCU,Hatibu Mwanga(70) na Meneeja Mkuu wa KNCU ,Honest Temba (38).

Wengine waliofikishwa mahamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi ,Pamela Mazengo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Kukoboa Kahawa (TCCC0) Maynard Swai (57) na aliyekuwa Meneja Mkuu wa TCCCo ,Andrew Kleruu wanaotajwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mtambo wa kukoboa Kahawa.

Wakili wa serikali Jaqueline Nyantori aliieleza mahakamani kuwa Washitakiwa ,Maynard Swai na Andrew Kleruu wanakabiliwa na makosa mawili huku akiyataja kuwa ni Matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia serikali hasara .

Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mandamizi ,Shadrack Martin,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdalah Chavula na Wakili wa serijali Jacqueline Nyantori huku Wakili Julius Semali akimtetea Mshtakiwa Honest Temba na Wakili Captain Sawayaeli Shoo akimtetea Mshtakiwa Hatibu Mwanga.



Watuhumiwa hao wakishushwa Mahakamani mapema leo chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi,kusomewa mashtaka yao

WANAFUNZI WAISHANGAA BASI ILIYOTEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR

$
0
0
 Wanafunzi wa shule ya mshingi Bunju 'A' wakiwa wakiangalia mabaki ya basi la Dar Express lililoteketea kwa moto jana usiku katika eneo la Bunju, jijini Dar es salaam wakati likiwa njiani kutokea Jijini Arusha. katika tukio hilo kakukuwa na mtu aliyepoteza maisha wala majeruhi bali ni mali za baadhi ya abiria ndio ziliteketea. Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni moja ya tairi ambayo ilipasuka lakini haikubadilishwa hili iliweza kushika moto.
 Wanafunzi hao wakiendelea kuiatazama basi hiyo baada ya kuteketea kwa moto.

MICHUZI TV: TRA MBEYA YAJA NA MBINU MPYA KWA WAFANYABIASHARA

IFIKAPO 2019 VIJIJI 35 VITAPATA UMEME WA REA NGORONGORO-OLENASHA

$
0
0

Na.Vero Ignatus ,Ngorongoro.

Naibu Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mbunge wa Ngorongoro Mhe. Wiliam Olenasha amesema hadi kufikia mwaka 2019 vijiji 35 vitakuwa vimepata umeme wa REA awamu ya tatu na baadae wataendelea na maeneo mengine.

Ameyasema hayo tar 8 August 2018 katika kijiji cha Sakala alipofanya mkutano wa hadhara wa wananchi na kusema kuwa kila nyumba lazima itawaka umeme kinachotakiwa ni wananchi kuwa tayari kuupokea umeme huo.

Olenasha amesema tayari nguzo za umeme zinaendelea kupita katika maeneo mbalimbali lengo ni kuhakikisha ngorongoro inabadilika kuanzia miundombinu iliyopo mpaka mazingira yenyewe ya maisha ya watu na kuwa ngorongoro mpya.“Wote ni mashahidi hili hatuzungumzi tena siyo hadithi nguzo tayari zinasambaa katika vijiji tunategemea ifikapo mwaka 2019 vijiji 35 vitakua vinawaka umeme”Alisema Olenasha

Wakati wanaendelea kusubiria kupata wa umeme Olenasha amewataka wananchi kuendelea kujenga nyumba zenye ubora zaidi ili mazingira yabadilike kwa kuwa Ngorongoro iliyokuwa inajulikana mwanzo kwa migogoro sasa inajulikana kwa maendeleo chanya.Wakitoa maoni yao baadhi ya wananchi wamesema kuwa kuwepo kwa umeme utawarahisishia wao kufanyashughuli za maendeleo ikiwemo kukuza kipato kwa wafanyabiashara ambao wanategemea umeme tofauti na ilivyo hivi sasa wanapata changamoto ya huduma ya matumizi ya vitu vinavyohitaji umeme.

Katika ziara Mbunge huyo ya kuwatembelea wananchi , wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wamempongeza kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi kipindi alipoomba kura ya kuchaguliwa kuliongoza jimbo hilo.Jimbo la Ngorongoro lina kata 28 Olenasha amezitembelea zote na kuzungumza na wananchi hii ikiwa ni mara yake ya nne kufanya hivyo .


Naibu waziri wa Elimu ambaye pia ni mbunge wa Ngorongoro akizungumza na wananchi.



MAMA SALMA KIKWETE AWANYOOSHEA KIDOLE WAZAZI, WALEZI WANAOWAFUNGIA NDANI WATOTO WENYE ULEMAVU, ATAKA WAPEWE HAKI ZAO

$
0
0


Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZAZI na Walezi nchini wameshauriwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile na badala yake wahakikishe wanaacha watoke nje na kubwa zaidi wapatiwe haki zao za msingi ikiwamo ya elimu.

Amesema watoto wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kufanya mambo makubwa yakiwamo ya kutimiza ndoto zao, hivyo kuwafungia ndani ni kuwanyima haki zao za msingi, hivyo jamii yenye tabia hiyo ni vema wakaiacha.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mchanganyiko Kariakoo jijini Dar es salaam.

Mama Salma alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi msaada wa vifaa vya kufundisha zikiwamo Laptop maalum kwa wanafunzi wenye ulemavu waliopo shuleni hapo. Msaada huo umetolewa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem.Hivyo Mama Salma ametumia nafasi hiyo kuwashauri wazazi na walezi ambao wana watoto wenye ulemavu wa aina yoyote ile kutowafungia ndani.

“Kitendo cha kumfungia mtoto ndani kwasababu ya ulemavu alionao si jambo nzuri na wala halimpendezi Mwenyezi Mungu kwani mtoto hakuomba kuwa alivyo.Pia kumfungia mtoto ndani unamfanya ashindwe kukua kutokana na kukosa miale ya jua na hasa ya nyakati za asubuhi.

“Nitoe rai watoto wenye ulemavu waachwe wawe huru na wapewe haki zao za msingi ikiwamo elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo yake ambayo yatamfanya atimize ndoto yake.Tuwaendeleze watoto wenye ulemavu kufikia malengo yao,”amesema Mama Salma.
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al- Najem, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa  mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi  walemavu  shule katika shule ya  Msingi Uhuru Mchanganyiko, vyenye thamani ya shilingi milioni 80.picha na Emmanuel Massaka (Globu ya jamii).
 Balozi wa Kuwait nchini,  Jasem Al- Najem na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mama Salma Kikwete,wadau mbalimbali wa elimu wakikagua vifaa hivyo walivyo vikabidhi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko vitakavyo wasaidia walemavu katika masomo yao,jana jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akizungumza  katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SIKU MAALUM YA ASALI, WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU WATOA NENO...


TUMEANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA VITENDO-RC MASENZA

$
0
0
Na Francis Godwin Michuzi Blog, Iringa 

MKUU wa mkoa (RC) wa Iringa Amina Masenza amesema kuwa mkoa wake umeanza utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa la kutaka wanaume kupimwa virusi vya UKIMWI ili kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU nchini.

Akizungumza leo katika ukumbi wa siasa ni kilimo mara baada ya kuwaongoza wadau wa maendeleo mkoani Iringa walioshiriki kikao cha mikakati ya utekelezaji wa agizo la waziri mkuu kupima VVU ,Masenza alisema kuwa zoezi la upimaji wa VVU kwa wanaume mkoani Iringa litasaidia kuwatambua wale ambao wameambukizwa na kuanzishiwa dawa za ARVs huku wale ambao hawajaathirika kujikinga na VVU.

Alisema kuwa michango ya wajumbe wa kikao hicho iliyotolewa ya kutaka wanaume kuhamasishwa kupima VVU kwa hiari majumbani kwao ni michango ambayo itasaidia kufikia malengo ya mapambano dhidi ya UKIMWI iwapo wanaume wote mkoani hapa wataonyesha ushirikiano katika zoezi hilo pindi litakapo anza .

Alisema kuwa taarifa za mganga mkuu wa mkoa wa Iringa zinaonyesha tatizo la UKIMWI bado kubwa ndani ya mkoa na kuwa pamoja na ukubwa wa tatizo ila bado kuna wadau wengi wa mapambano ya UKIMWI .

Kuwa kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU na utoaji wa dawa za kupumbaza VVU iliyozinduliwa na Juni 19 mjini Dodoma na waziri mkuu imekwenda sanjari inajumuisha na usemi usemao Furaha yangu pima jitambue hivyo kampeni hiyo itanaza kwa wanaume na baadae makundi mengine katika jamii .

Kuwa makundi hayo ni pamoja na mabinti wa miaka kuanzia 15 hadi 21 ,wanawake wajawazito na wengine wote na kuwa njia pekee ya kufanikisha kampeni hiyo ni wananchi wote kujitokeza kupima VVU .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiongoza kupima VVU katika kikao cha mikakatiya kuanzakampeni za kupima UKIMWI kwa wanaume 
Viongozi wa mkoa wa Iringa wakiwemo wakuu wa wilaya ya Mufindi na kilolo wakionyesha karatasi baada ya kupima VVU 
Washiriki wa kikao cha kuweka mikakati ya zoezi la upimaji UKIMWI wanaume wakiwa katika kikao hicho.

SIRI NZITO "TUNA MISITU MIZITO AMBAYO HUJAWAI KUIONA TANGU KUZALIWA"

SERIKALI YATOA MILL 400/- KWA AJILI YA UJENZI KWA KITUO CHA AFYA KATA YA NKENDE

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime

SERIKALI imetoa Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha Afya katika kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kwa lengo la kusogeza huduma ya afya karibu na Wananchi.

Huku wananchi hao wakichangia kununua eneo lenye thamani ya Sh.milioni 8 kwa lengo la upanuzi wa eneo hilo ili kuweza kufanikisha mchakato huo. 

Akizungumzia ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime Elias Ntiruhungwa amesema kuwa tayari Serikali imeshapelekal kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Nkende.

“Mpaka nazungumza kwa sasa hivi tayari fedha zipo kwenye akaunti na hivyo nataka kuona wiki hii kila kitu kimekamilika na ujenzi kuanza mara moja leo nimeambatana na wataalamu wote ili kumaliza mapema shughuli hii,” amesema Elias.Pia Elias amewapongeza wananchi kujitoa kununua eneo kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa kituo cha Afya na kuahidi kuendelea kushirikiana nao vyema ili kumaliza mapema ujenzi huop.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote amesema kuwa wananchi wamewiwa ujio wa ujenzi wa kituo cha afya na ndo maana wamejitoa kwa nguvu zao ili maeneo ya kutosha yapatikane huku akishukuru Serikali kutoa Fedha hizo.

“Nimeweza kushawishi wananchi wangu kuchangia na mimi nikiwa wakwanza kuchangia ili tununue eneo la kutosha ata kama halitatosha bado kunaeneo lingine takribani heka tisa bado tutapendekeza eneo hilo ili kujenga Kituo cha afya kwa lengo la kunusuru Wananchi ambao ulazimika kwenda katika hospitali ya Wilaya ya Tarime,” amesema Komote.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na Wakazi wa kata ya Nkende katika mtaa wa Magena ambapo wanatarajia kujenga kituo cha Afya baada ya Serikali kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 400.
Zahanati ya Mtaa wa Magena ambayo inahudumia wakazi wa kata ya Nkende Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote akiongea na Wananchi katika eneo la mtaa wa Magena ambapo wanatarajia kujenga kituo cha Afya.
Jengo linalomilikiwa na Ccm tawi la Magena ambalo wametoa eneo hilo lenye thamini ya Millioni 10 ili kujenga Kituo cha Afya

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

In Loving Memory of Our Beloved Mama The Late Monica Haule Mwasalyanda - 1st Death Anniversary

$
0
0
C:\Users\user\Downloads\IMG_3916.JPG
Dear Mama,
You have been a blessing to us from God. Your memories will always live on and as days pass by you will always be remembered and your spirit lives on. We thank God for you as a wonderful gift to our lives and even though we loved you more. We know you are in a better place.
Eternal rest grand to her, O Lord and let perpetual light shine upon her, May her rest in peace. Amen
May your soul rest in eternal peace our Beloved Mom until we meet again.
Deeply missed by your Children, Inlaws, Grandchildren, Brothers, Sisters, Family, Friends and Neighbours.

DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA MAPOROMOKO YA KALAMBO, AMBAYO NI YA PILI KWA UREFU AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakifurahia kufika karibu na kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo yapo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, maporomoko haya ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa wakinawa mikono kwenye mto kalambo ambao unatengeneza Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa muda mfupi baada ya kutembelea Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika. Eneo hilo la kivutio linaendelea kuboreshwa kwa kujengewa ngazi maalum zinazowawezesha watalii kufika hadi kwenye kina cha maporomoko hayo.
Muonekano mwanana wa Maporomoko ya Mto Kalambo.

ZIARA YA IGP SIRRO YAENDELEA WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea zawadi ya Mbuzi iliyotolewa na Askari wa kike wa Wilaya ya Serengeti baada ya kuzungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Wilaya hiyo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Juma Ndaki .
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifurahia ngoma na kikundi cha utamaduni cha Kijiji cha Rubanda Wilayani Serengeti wakati alipofika kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Rubanda Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi) 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima wakati alipofika ofisini kwake na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Nurdin Babu wakati alipofika ofisini kwake na kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo wakati wa Ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kihalifu na kuzipatia ufumbuzi.

TANGAZO LA MUHADHARA DMV Jumamosi Julai 14, 2018

$
0
0

Salaam Aleikum warahmatullah,
Kutakuwa na Muhadhara wa mawaidha ya Dini kutoka kwa Mashekhe wetu wa kutoka nyumbani, tunaombwa tuhudhurie na kuwajulisha wenzetu tupate kunufaika sote kutoka kwa Wahadhiri wetu:-
▪Sheikh Nurdin Kishki (Tanzania)
▪Sheikh Yusuf Abdi (Kenya)
▪Sheikh Ashraf Ndayisenga (Rwanda)
Address :-
Muslim Community Center (MCC) 
15200 New Hampshire Ave, 
Silver Spring, MD 20905

Kuanzia Saa Kumi Jioni hadi saa Nne usiku (4pm mpaka 10pm)
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:-
Ali Mohamed 301 500 9762
Shamis 202 509 1355

DC KINONDONI AKABIDHIWA MWENGE WA UHURU, KUZINDUA MIRADI YA SH BILL 13 9 WILAYANI HUMO

Introducing: Bado (Remix) - Mwasiti Featuring MwanaFa , Chege & Marioo

Watumishi Wilayani Ileje mkoani Songwe waonywa dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao

$
0
0
Na Daniel Mwambene, Afisa Habari Ileje 
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wameonywa dhidi ya matumizi 
onyo hilo,lilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Haji Mnasi alipokuwa akizungumza na watumishi wake katika ukumbi wa Sekondari ya Ileje wakati wa kikao kazi alichokuwa ameitisha kwa Kata za Isongole na Itumba. mabaya ya mitandao ya kijamii ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuwakumba. 
Mnasi alisema watumishi hawana budi kujiunga katika makundi mbalimbali ya kimitandao ikiwa ni haki yao ya msingi katika kutoa na kupata taarifa mbalimbali katika kidjitali lakini pia waangalie sheria za kimtandao ili kujiweka salama siku zote. 
“Kuna watu wamekuwa wakipokea na kusambaza taarifa bila kutafakari,zikiwemo taarifa ambazo hazistahili kusambazwa kisheria hii ni hatari kwa ajira zenu mkizingatia kuwa wote tu watekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala (CCM)” alisisitiza kiongozi huyo. 
Aliongeza kuwa ndani ya Halmashauri yake kuna makundi kadhaa ya ‘Whatsapp’ ambayo yameundwa ili kuwezesha watumishi kupashana habari za kimaendeleo na si kukebehi serikali iliyopo madarakani akisema kuwa atakayefanya hivyo atabeba mzigo wake mwenyewe. 
Onyo hilo linakuja wakati Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini (TCRA) ikiendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mtandao ambapo sheria mpya zilishapitishwa ikiwa ni hatua mojawapo ya kuimarisha utaifa uliojengwa kwa muda mrefu unaoweza kuhatarishwa kupitia matumizi mabaya ya vyombo vya mawasiliano kama redio zilivyotumika vibaya wakati wa mauaji ya halaiki kule Rwanda na Burundi 
Kwa upande wao watumishi hao waliiomba serikali kutuma taarifa kwa walengwa kwa wakati ili kuharakisha utekelezaji. 
Bw. Herman Shola ambaye ni mwalimu wa Sekondari ya Itumba alisema kuwa kuchelewa kwa taarifa kufika kwa wakati hunachangia hata uchelewevu kwenye vikao. 
Pamoja na mambo mengine watumishi hao toka kada mbalimbali ngazi ya wilaya hadi kijiji walikumbushwa wajibu wao utakampatia mwananchi huduma bora na kwa wakati. Aidha watumishi hao walimweleza mwajiri wao juu ya kero mbalimbali zinazopunguza ari ya kufanya kazi yakiwemo malipo ya likizo na kuchelewa kupanda kwa madaraja kwa mujibu wa sheri za Utumishi wa Umma. Vikao hivi ni mwendelezo wa vikao vinavyoendelea wilayani humo ikiwemo mikutano ya hadhara inayolenga kupunguza kero za wananchi na watumishi ili waweze kufurahia kuishi ndani ya wilaya hii.
DED wa Ileje Ndg.Haji Mnasi(aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Kata za Itumba na Isongole kwenye ukumbi wa Sekondari ya Ileje wakati wa kikao kazi alichoitisha

 Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wiya ya Ileje toka Ofisi ya DED NA Kata za Itumba na Isongole wakimsikiliza Mkurugenzi wao Ndugu Haji Mnasi
Mwalimu Zayumba Gabriel wa Sekondari ya Itumba (aliyesimama)akitoa kero yake kuhusu malipo ya likizo.

DC SAME AONGOZA MSARAGAMBO NA WANANCHI WAKE

$
0
0
Katika msaragambo uliofanyika kata ya Stesheni eneo la mighareni - Wilayani Same, iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Rosemary Senyamule, Ilikuwa ni kusafisha, kuchimba,  kufukia na kujaza udongo mashimo katika barabara inayoelekea eneo la shule ya sekondari mighareni.

Kwa kuitikia wito wa uongozi wa Wilaya hiyo wa kila Jumatatu ya wiki kufanya kazi za kijamii, wananchi zaidi ya 500 walijitokeza kushiriki kazi hiyo ambapo baada ya hapo kulikuwa na mkutano wa kusikiliza kero. 

Kero iliyotajwa zaidi ni maji na kutokuwepo kwa barabara za mitaa kwenye maeneo mengi ya vitongoji, hivyo TARURA, SAUWASA waahidi kutatua kero hizo. 

Baada ya kushiriki kazi hiyo na kusikiliza kero, DC Senyamule apongeza kwa kuanza na kichaka na kumaliza na barabara inayopitika. 

Aliwaagiza viongozi wa kata kufuatilia michango na kuhakikisha shule inakamilika na kupokea wanafunzi 2019. Awataka kusoma mapato na matumizi na kutoa takwimu za uhakika za waliochanga. 

Mwanaume aliyebeba ndoo kichwani ni Mkt. wa mamlaka wa mji mdogo wa Same. 
" Tukiendelea na ushirikiano huu viongozi Same itakimbia" Kwani wananchi wanapata moyo wa kufanya kazi. Alisema DC huyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (mwenye kilemba) akishikiana na wananchi wake kuondoa udongo wakati wa zoezi la kuchonga barabara ya inayoelekea eneo la shule ya sekondari mighareni.
 Wananchi wa Wilaya wa Same wakishirikiana kwa pamoja kufanikisha zoezi hilo.
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images