Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110176 articles
Browse latest View live

UN YATUNUKU UBUNIFU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
LATIFA Mohammed Ngea kutoka Zanzibar ameibuka kidedea katika tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu na kupata hundi ya shilingi milioni 3.

Latifa ni miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.Latifa alipata tuzo hiyo kwa kubuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo.

Mfumo huo unaojiendesha wa umwagiliaji maji unaweza kutumia king’amuzi ili kubaini wapi pana unyevu na wapi pakavu ili maji yaweze kupelekwa.Tangu kuanza kwa maonesho hayo takribani wiki sasa, wageni mbalimbali wamepata nafasi ya kuona ubunifu wa vijana hao katika roboti, sanaa na kilimo.Aidha walionesha ubunifu wao unavyofanyakazi sanjari na kauli mbiu ya sabasaba mwaka huu inayosema “Kukuza biashara kwa maendeleo ya viwanda”.

Baada ya wananchi kuwasikiliza wabunifu wote watatu, wageni walipata fursa ya kupiga kura nani waliamini alionyesha ubunifu bora zaidi, ndipo Latifa alipoibuka mshindi.Mbunifu mwingine alikuwa ni Gracious Fanuel anayetoka mkoani Kilimanjaro alipata ushindi wa pili. 

Huyu yeye alitengeneza roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana majumbani.Roboti aliyotengeneza ni mfano wa Mkono ambao unaweza kuendeshwa kwa simu ya mkononi na anatarajia kukuza ubunifu wake ili ufikie hatua ya kuwa na mkanda wa uzalishaji bidhaa na pia kusaidia watu wenye ulemavu.

Mbunifu mwingine ni Amos Mtambala, kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali yeye alishika nafasi ya tatu. Amos alipata mafunzo kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) na tangu hapo amekuwa akipanua mtandao wake na kuwachukua zaidi ya vijana 100 ambao hutengeneza kazi za sanaa na kuuza nchini na pia kimataifa.

Zaidi ya watu 500 katika Viwanja vya Sabasaba na kupitia mitandao ya kijamii walipiga kura kwa kijana yule wanayeamini aliandaa ubunifu bora zaidi.Mshindi wa kwanza alipata shilingi milioni 3 huku mshindi wa pili akipata shilingi milioni 2 na wa tatu shilingi milioni 1.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu kwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
Mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar aliyebuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (katikati), mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) huku wakiwa wameshikilia hundi zao.



NSSF KUTOA MAFAO SITA KWA WOTE SEKTA ISIYO RASMI

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limedhamiria kutoa mafao yote sita yatolewayo ili kuisaidia sekta isiyo rasmi kujikinga na majanga mbalimbali na kujikwamua Kiuchumi

Akizungumza katika semina hiyo kwa viongozi wa vikundi vya ujasiriamali mkoani pwani, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng.Evaristi Ndikilo.

Alisema sekta isiyo rasmi ina kundi kubwa sana ambalo halijafikiwa na Hifadhi ya jamii hivyo ni fursa na muhimu kwa wale wote walio katika sekta hiyo wakiwemo mamalishe, bodaboda, wakulima, wavuvi, walio katika vikundi kama SACCOS na Vikoba kujiunga na NSSF ili waweze kujikinga na majanga mbalimbali.

Pia Mkuu wa mkoa ameongezea kuhimiza wajasiriamali wote wa Mkoa wa Pwani kujiunga na Mfuko wa hifadhi ya Jamii ili koungeza pato la Mkoa wa pwani na pia aliwahimiza viongozi mbalimbali wa serikali kuunga mkono mpango huu kwani utaisaidia serikali ya awamu ya tano katika mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii.




Pia mkuu huyo wa mkoa amesema wajasiriamali wengi wanavilio vikubwa kwa kukosa mikopo na pia riba kubwa pindi warejeshapo mikopo hiyo..,Lakini amelipongeza sana shirika la Taifa la hifadhi ya jamii kuliona hilo na kukaa chini pamoja na Benki ya Azania kutoa mikopo kwa wajasiriamali wote na kwa riba nafuu kupitia vikundi vyao.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evaristi Ndikilo akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya uzalishaji mali wakati wa semina iliyoandaliwa na NSSF inayohusu Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi.
Viongozi wa Vikundi vya uzalishaji mali wakiwa katika semina iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya kuratibisha Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi.

Breaking Newzzzzzzzzzzz:VIGOGO WATANO WA KNCU WAFIKISHWA MAHAKAMANI.

$
0
0
  
Vigogo watano wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU) wakiwemo mwenyekiti wa sasa wa KNCU Aloyce Kitau na Mwenyekiti mstaafu wa KNCU ,Maynald Swai wamefikishwa muda huu katika viunga vya mahakama ya Hakimu mkazi,Moshi.

Wamo pia aliyekuwa Meneja wa TCCCo Andrew Kleruu, Meneja wa KNCU ,Honest Temba na Makamu mwenyekiti wa KNCU,Khatibu Mwanga.

HABARI ZAIDI TUTAWALETEA.

WAZIRI LUGOLA, JENISTA MHAGAMA WAFANYA KIKAO KUJADILI MFUMO WA PAMOJA WA KUTOA VIBALI VYA KAZI NA UKAAZI, JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kuhusu utaratibu wa kuunganisha mifumo ya vibali vya kazi na ukaazi. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Vibali vya Ukaazi, Idara ya Uhamiaji, Mary Palmer, kushoto ni Afisa wa Kitengo cha Vibali vya Ukaazi, Isaac Fota, pamoja na Afisa Mahafudhi Nassoro. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo, kabla ya kikao chake na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.  

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu), akimsikiliza Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alipokua akifafanua jambo kuhusiana na mfumo unaoziunganisha Wizara hizo mbili, wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini Dodoma leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika kikao cha kujadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi. Kulia meza kuu ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama. Mfumo huo unaoziunganisha wizara hizo mbili. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini Dodoma leo.  

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwa ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kuwasili jijini humo leo. Waziri Lugola alifanya kikao na Maafisa Uhamiaji kutoka Kitengo cha Vibali vya Ukaazi, na baadaye alifanya kikao na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama jijini humo, wakijadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi ambao unaziunganisha Wizara hizo mbili.  

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akikaribishwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, ofisini kwake jijini Dodoma, kabla ya Mawaziri hao kuanza kikao cha kujadili mfumo wa pamoja wa utoaji wa vibali vya kazi na ukaazi ambao unaunganisha wizara hizo mbili. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, jijini humo leo. 

KATIBU MKUU WA CCM DKT BASHIRU ATEMBELEA BANDA LA NSSF SABASABA

$
0
0
Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM ,Dk Ally Bashiru akimsikiliza Afisa  Matekelezo wa NSSF  Kassim Mfunda aliyekuwa akitoa maelezo na taratibu namna ya wanachama wanavyoweza kujiunga na shirika hilo na kujipatia huduma mbalimbali zikiwemo za Mafao.
Afisa huduma kwa wateja  Riziki Kibwasali akimpatia zawadi Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ally Bashiru ,pembeni yake ni Afisa Uhusiano wa NSSF Angella Msangi.Kushoto ni Mkurugenzi  wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) ,Edwin Rutegaruka akishuhudia tukio hilo
Afisa Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Angella Msangi akitoa maelezo ya huduma mbali mbali zinazofanywa na shirika hilo kwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk Ally Bashiru alipotembelea kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea  jijini Dar es salam,pembeni ni Afisa mkuu  matekelezo kitengo cha Hiari,Abas Cothema

NEWZ ALERT: KIONGOZI MBIO ZA MWENGE AGOMA KUZINDUA JENGO LA ZAHANATI MSASANI

$
0
0
 

Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Francis amegomea kuzindua jengo la Zahanati ya Mkoroshini (pichani) ilioyopo Msasani jijini Dar es Salaam kutokana na kutokidhi viwango vya ujenzi vya jengo hilo.

Vilevile limekuwa na gharama za juu kwenye ujenzi wa jengo hilo ambapo amewataka TAKUKURU kufuatilia suala hilo kwa undani ili kubaini yaliyomo ndani ya ujenzi huo na gharama kwa ujumla.

ZANZIBAR 24 WATOA MSAADA WA CHAKULA KWA SOBA HOUSE YA DESTROIT YA MCHINA MWANZO

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Waathirika wa dawa za kulevya wanaoishi katika nyumba ya kurekebisha tabia (Soba House) ya Detroit iliyoko Kwamchina mwanzo wameiomba Serikali kuendeleza mapambano ya kupiga vita uingizaji na utumiaji wa dawa hizo nchini.

Vijana hao walitoa ombi hilo baada ya kupokea msaada wa chakula uliotolewa na Mtandao wa Kijamii Zanzibar 24 ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya kutimia miaka mitatu tokea kuanzishwa mtandao huo.

Kijana Alawi Abdalla anaeishi nyumba hiyo alisema ikiwa Serikali haitaongeza nguvu za kuwatafuta na kuwakamata waingizaji wakubwa wa dawa za kulevya vijana wengi wataendelea kuathirika.

Aliwashauri vijana ambao bado hawajaanza kutumia dawa za kulevya wasijaribu kuzionja  kwani sio kitu cha kuonja na nihatari kwa usalama wa afya zao.

Alawi aliishauri Serikali kuwatafutia msaada wa nyenzo za kufanyia kazi vijana waliopita Soba House na kufanikiwa kurekebisha tabia zao ili watakapo rejea katika jamii waweze kujitegemea.
 Mtendaji Mkuu wa Zanzibar 24 Suleiman Juma Is-haka akimkabidhi Mkuu wa Soba House ya Detroit Rashid Kassim msaada wa chakula katika hafla iliyofanyika katika nyumba hiyo iliyopo Kwamchina mwanzo.
 Baadhi ya vijana wanaoishi nyumba ya kurekebisha tabia ya Detroit iliopo kwa Mchina mwanzo wakifuatilia kukabidhiwa msaada wa chakula uliotolewa na Mtandao wa Kijamii wa Zanzibar 24.
 Mkuu wa Soba House ya Detroit  Rashid Kassim akitoa shukrani zake mbele ya waandishi wa habari wa Zanzibar 24 baada ya kupokea msaada wa chakula katika hafla iliyofanyika kwenye nyumba hiyo Kwamchina mwanzao.
Mmoja wa vijana wanaoishi nyumba ya kurekebisha tabia ya Detroit Alawi Abdalla akizungumza na waandishi wa habari  wa Zanzibar 24 Amina Omar (kulia) na Fat-hiya Shehe katika hafla iliyofanyika Kwamchina mwanzao. Picha na Ramadhani Ali  Maelezo Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mkulima Mkoani Dodoma kizimbani kwa kukutwa na vipande tisa vya meno ya tembo

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

Mkulima Hassan Sangali (22) mkazi wa Pingalama wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kukamatwa akiwa na vipande Tisa vya meno ya tembo.


Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Juni 9, 2018 eneo la Kimara Wilaya ya Ubungo mshtakiwa huyo alikamatwa na vipande hivyo Tisa chenye thamani ya dola za marekani 30,000 ambapo ni sawa na Sh 66,720,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.


Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.


Kesi imeahirishwa hadi Julai 23,2018 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamepeekwa rumande wote.


MBUNGE WA MANONGA AZINDUA MADARASA NA MABWENI KIDATO CHA TANONA SITA MKOANI TABORA

$
0
0
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali amezindua rasmi madarasa 2 na mabweni 3 yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

Gulamali ameeleza kuwa huo ni moja kati ya miradi ya kimaendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika jimbo hilo na amefurahi kuzindua mradi huo ambao utawasaidia wanafunzi wengi kutimiza ndoto zao kielimu.

Aidha ameeleza kuwa miradi ya kimaendeleo katika sekta ya afya, Umeme, elimu na miundombinu ni muhimu kwa wananchi katika kuleta maendeleo hivyo kama serikali hawana budi kuipa kipaumbele. Katika mwaka huu wa fedha, vijiji vyote katika jimbo la Manonga vitapata umeme na tayari  Mbunge huyo ameshatekeleza ahadi yake kwa kukabidhi gari jipya la wagonjwa jimboni humo.

Uzinduzi wa madarasa na mabweni hayo utawasaidia wanafunzi kujiunga na elimu ya kidato cha tano Mkoani humo na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekondari ya juu kutokana na uhaba wa shule. 

Katika uzinduzi huo Gulamali aliambatana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka WCB wakiongozwa na Lavalava pamoja na Maromboso walioambatana na jopo la timu yao.
Mradi wa madarasa 2 na mabweni 3 yaliyozinduliwa na mbunge wa Manonga yenye thamani ya shilingi Milioni 265 yatakayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika sekondari ya Ziba Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Afisi Kuu CCM Zanzibar.
Kikao hicho kilichobeba ajenda kuu mbili, ambazo ni Mapendekezo ya Kupiga Kura za maoni katika uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe na Mapendekezo ya Wanachama wa CCM wanao omba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uwakilishi jimbo la Jang’ombe.
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Dkt. Ali Mohammed Shein yupo safarini nje ya nchi hivyo wajumbe walimchagua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa muda na kuongoza kikao hicho.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kwenye ukumbi wa Afisi Kuu Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Idd na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Sadalla. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kwenye ukumbi wa Afisi Kuu CCM Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Idd
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Sadalla akisoma ajenda zitakazojadiliwa kwenye Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar. 
 Wajumbe waliohudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Lipuli yasajiri wachezaji wanne

$
0
0
Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
TIMU ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa jana imekamilisha  usajili wa wachezaji wake wapya wanne kutoka timu tofauti ili kuongeza nguvu kwenye msimu wa 2018/19.

 Lipuli wameweza kuwapata  nyota wawili waliowahi kukipiga klabu ya Simba pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga , Paul John Nonga kutoka Mwadui FC ya Shinyanga aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Usajili umewahusisha beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, William Lucian ‘Gallas’ kutoka Ndanda FC ya Mtwara na mshambuliaji Miraj Madenge ‘Shevchenko’ kutoka Mwadui FC ambao wote kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja pamoja na Issa Ally Rashid, mchezaji huru ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili. 

Gallas na Miraji waliwahi kukipiga katika klabu ya Simba kuanzia timu ya Vijana  kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na baadaye kuchwa mwaka 2014.

Lipuli iliyoanza vizuri msimu wake wa kwanza ndani ya ligi kuu vodacom wakiwa chini ya kocha Selemani Matola  imedhamiria kufanya vizuri msimu kwa kufanya usajili utakaokuwa na tija na kuleta ushindani ndani ya ligi.
Beki William Lucian 'Gallas' akipokea kandarasi yake ya mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Lipuli Fc ya Iringa.

JESHI LA POLISI PWANI LAFANYA UKAGUZI WA LESENI 1,710 ZA MADEREVA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

JESHI la polisi mkoani Pwani ,linaendelea na ukaguzi kwa madereva na magari ambapo leseni za madereva 1,710 zimekaguliwa huku leseni ya mmoja ikionesha akiwa amezaliwa mwaka 1951 huku akionyesha kuwa na umri mdogo.

Aidha madereva watano walikamatwa kwa kosa la kutokuwa na leseni ,madereva saba walikamatwa kwa kutokuwa na sifa daraja la D/L,PSV.

Akielezea kuhusiana na ukaguzi huo, kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani, Blasius Chatanda ,alisema dereva mwingine mmoja leseni yake ilionyesha amezaliwa mwaka 1951 wakati anaonyesha yeye akiwa na miaka 27 huku akiendesha gari la abiria.Alisema ukaguzi huo ni endelevu na atakaebainika kwenda kinyume na sheria za usalama barabarani atatozwa faini ama kufikishwa mahakamani.

Chatanda aliwaasa madereva ,kubadilika kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka kugharimu maisha ya watu na wengine kubakia na ulemavu wa viungo.Pamoja na hayo ,alikemea baadhi ya madereva wanaoendesha kwa mwendo kasi na wale wanaotumia vileo .

Akielezea mikakati wanayoendelea nayo kudhibiti ajali za barabarani ,alisema ifikie wakati madereva wakatumia taaluma zao kwa kuendesha wakiwa makini bila kukiuka sheria jambo linalosababisha ajali ambazo nyingine ni za uzembe wa madereva.

Chatanda alieleza wamejipanga kufanya misako ya usiku na mchana, mara kwa mara kwa magari makubwa na madogo hadi watakapohakikisha ajali zinapungua kabisa."Tuna askari wetu wa usalama barabarani waliotanda kama utitiri kwenye barabara zetu za mkoa ,tuna vipima vileo ,ambapo tunahakikisha dereva atakaekutwa na kosa lolote la kukiuka sheria zinazostahiki atakiona" alisisitiza Chatanda.

Pia kunafanyika operesheni za mara kwa mara ili kuwakamata wale madereva bodaboda watakaokuwa hawataki kutii sheria bila shuruti kwa kuwachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani ili kupunguza ajali na vifo kwa waendesha pikipiki.

Heads of State Owned Enterprises meet on Industrialisation Agenda

$
0
0
The Minister of Finance and Planning, Hon. Dr. Philip Mpango will officiate a National Roundtable Dialogue on “The Role of State Owned Enterprises (SOEs) in Implementing the Industrialisation Agenda” today. 

This one-day event is organised by UONGOZI Institute in collaboration with the Office of the Treasury Registrar in the Ministry of Finance and Planning. 

According to a statement released by UONGOZI Institute, the meeting aims to bring heads of State Owned Enterprises together to examine the role of SOEs and their contribution in the implementation of the industrialisation agenda. 

A keynote presentation by Dr. John Page, Senior Fellow in the Global Economy and Development Program at the Brookings Institution in Washington, D.C will be delivered at the event, with subsequent presentations and discussions focusing on lessons from other countries, how SOEs can take advantage of the opportunities emerging during the process of industrialization, and how SOEs can meet the challenges arising from the process of industrialization. 

Over 60 Board Chairpersons and Chief Executives of State Owned Enterprises are expected to participate in the dialogue.

POLISI JAMII WAWILI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

Polisi Jamii wawili na dereva mmoja wakazi wa Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za uhujumu uchumi kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 239.5.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Faraja Nguka  aliwataja washtakiwa hao kuwa ni dereva mkazi wa Mbezi Luis, Kefas Mlenzi (30), Polisi Jamii, Juma Mtali (35) na  Polisi Jamii, Greyson Muhapa maarufu kama Masu (32) wote wakati wa Mbezi Luis.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Ally Salum, wakili Nguka amedai Juni 28/ 2018 huko Mbezi katika Wilaya ya Ubungo washtakiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa na vipande 30 vya meno ya tembo vyenye thamani USD 105,000 sawa na Sh 239,505,000 bila ya kuwa na Kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi za uhujumu uchumi, isipokuwa mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP

Kesi imeahirishwa hadi Julai 23, 2018 kwa mijibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mchezaji wa Stand United atimkia Klabu ya KMC Fc

$
0
0
UONGOZI wa Klabu ya KMC Fc imefanikiwa kupata saini ya aliyekuwa mchezaji wa Stand United, Ally Ally na kuitumikia klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Ally Ally amejiunga na KMC FC ya Kinondoni, iliyopanda ligi kuu msimu wa 2018/19 baada ya kumalizana na waajiriwa wake wa zamani.

Beki huyo aliyekuwa mwiba mkali katika mechi za ligi kuu msimu uliopita akiitumikia Stand United amejiunga na KMC baada ya mambo kutoenda sawa katika klabu yake ya zamani kutokana na kutolipwa fedha za mshahara wake.

Ally ambaye ni beki huyo wa kati hivi karibuni aliibuka na kusema Stand kuwa anaidai mshahara wa miezi takribani mitatu na akaadhidi hataweza kuendelea kuichezea klabu hiyo.

KMC ambayo imepanda kushiriki Ligi Kuu Kuu Bara msimu ujao imezidi kukifanyia maboresho kikosi chake ambapo imenyaka saini za wachezaji wenye uzoefu katika ligi ikiwemo kipa Juma Kaseja aliyewahi kung'ara Simba.
 Meneja wa timu ya KMC Fc Walter Harrison(kushoto) akikabidhiana mkataba na beki wa kati Ally Ally baada ya kutia saini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo.
Beki wa kati Ally Ally akitia saini kandarasi ya kuitumikia klabu ya KMC Fc akishuhudiwa na Meneja wa timu hiyo Walter Harrison.

Michuzi TV UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE) WAENDELEA VIZURI - KADOGOSA

MHANDISI ATASHASTA NDITIYE AZINDUA MKUTANO WA 16 WA SAPOA, HUDUMA YA POSTA MLANGONI KUFIKA KOTE NCHINI

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri wa  uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amezindua mkutano wa 16 wa SAPOA ambao ni muunganiko wa mashirika ya Posta kwa nchi za SADC.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Nditiye ameeleza kuwa mkutano huo ni kwa lengo la kupeana mawazo namna ya kuendesha shirika hilo katika ukanda wa SADC kanda ya Afrika na duniani kwa ujumla.

" Tanzania ni mwanachama pia katika muunganiko wa SADC  na duniani kwa ujumla na kama shirika linafanya shughuli ambazo zinafahamika  na licha ya kusuasua kwa sasa liko hai na imara na litapeleka gawio kwa serikali,"amesema. Aidha ameeleza kuwa shirika hilo lipo vizuri na katika usafirishaji wa vifurushi na mizigo kwa wakati na salama zaidi.

Kuhusu na maendeleo ya sayansi na teknolojia hasa katika matumizi ya mitandao kuzorotesha huduma zao Nditiye amesema kuwa wana ukurasa wao ujulikanao kama Www.posta.co.tz ambao unafanya vizuri ambao unawasaidia watanzania kusafirisha na kuuza bidhaa popote alipo na malipo yatamfikia alipo.

Nditiye ametoa mwito kwa wananchi kupitia TAMISEMI kutaja majina ya mitaa nchini kote ili shirika kuweza kutoa huduma kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya posta mlangoni.Kwa upande wa Posta Masta Mkuu Hassan Mwang'ombe amesema kuwa hiyo ni fursa kwao katika kujifunza kutoka kwa wadau wa mataifa mbalimbali ili kuongeza mbinu na maarifa katika kuhudumia wateja wao.

Amefafanua kuwa mkutano huo utawasaidia katika kuboresha huduma hasa ya teknolojia sambamba na utekelezwaji wake.Mkutano huo umehudhuriwa na nchi 13 kama vile Malawi, Burundi, Afrika ya Kusini na Tanzania ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo.
Naibu Waziri ya uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 16 wa SAPOA ulioshirikisha nchi 13 jijini Dar leo.

BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA TAWI LAKE JIPYA LA MBAGALA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya KCB Tanzania imefanya uzinduzi wa tawi lake la 14 lililopo Mbagala jijini Dar es salaam. Tawi hilo limezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt Ashatu Kijaji akiwa ameambatana na Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu.

Dkt Ashatu  amesema kuwa amefurahishwa na utendaji kazi wa benki ya DCB ndani ya miaka mitano ikiwemo ulipaji wa kodi na jumla ya Bilioni 40 imelipwa kama kama cooperate Tax na kodi nyinginezo.

Amesema kuwa KCB imeshirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa barabara na majengo mbalimbali, udhamini waligi kuu ya soka Tanzania ikiwa ni lengo la kuinua sekta ya michezo.

Katika uzinduzi huu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Zuhura Muro aliweza kusena baadhi ya mafanikio machache ambayo KCB imeweza kufanya kwa jamii.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akizindua tawi la Benki ya KCB Mbagala akiwa pamojpana Mkurugenzi Mtendaji Cosmas Kimaro na Mwenyekiti wa Bodi Zuhura Muro leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akikata utepe baada ya kuzindua tawi la Benki ya KCB Mbagala leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi waliojitokeza pamoja na viongozi wa Benki ya KCB wakati wa uzinduzi wa tawi la Mbagala Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki KCB Zuhura Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Benki hiyo Mbagala leo Jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wachimbaji Wadogo Kunufaika na Vituo Vya Umahiri

$
0
0
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika chuo cha Madini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof Simon Msanjila  na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi. 
Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Madini Prof Simon Msanjila(kushoto)  na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi wakibadilishana mkataba wa ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo  na vitakavyojengwa  katika  chuo cha Madini Dodoma. 
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki na Naibu Waziri wake Mhe. Stanslaus Nyongo wakishuhudia utiaji saini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo vitakavyojengwa  katika chuo cha Madini Dodoma.Wanaotia saini ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof Simon Msanjila  na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi. Picha zote na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA. 

MATUKIO MBALIMBALI NDANI YA MAONESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Picha mabalimbali za wananchi waliofika kununua bidhaa mbalimbali katika maonesho ya 42 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba  yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Blog)




Viewing all 110176 articles
Browse latest View live




Latest Images