Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

NHIF YATOA MIFUKO 245 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

$
0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF)umekabidhi mifuko 245 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza inayojengwa eneo la Lusanga ambayo itaondoa changamoto ambazo walikuwa wakikumbana nazo wananchi.

Makabidhiano hayo yalifanyika juzi wilayani Muheza na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally Mwakababu kwa Mkuu wa wilaya hiyo Mhandisi Mwanasha Tumbo ambapo mifuko hiyo itasaidia ujenzi huo

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo wa saruji,Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha aliushukuru mfuko huo kwa kuona umuhimu kusaidia juhudi walizoanzishwa za ujenzi wa hospitali hiyo ili kuwapunguzia adha wananchi ikiwemo kuunga mkono jitihada za harambee iliyoendshwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu.

Alisema msaada huo umefika wakati muafaka wakiwa kwenye harakati za kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo ambao ni muhimu kwa ustawi wa wakazi wa wilaya hiyo katika kuhakikisha wanakuwa nayo ili iweze
kuwahudumia.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ujenzi wa hospitali hiyo ambao utagharimu bilioni 11 mpaka itakapo kamilika lakini hatua iliyopo kwa harambee walioifanya Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu waliweze kupata bilioni 1.7.
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimkabidhi mifuko ya saruji 245 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza ambayo ilitolewa na mfuko huu kuunga mkono juhudi hizo kushoto ni Mhasibu wa NHIF Tanga Hellena Manyanda na katikati aliyevaa kilemba ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi mifuko ya saruji 245 Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Julius Mgeni kushoto wanaoshuhudia ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu katikati kushoto ni Mhasibu wa NHIF Tanga Hellena Manyanga na kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Sophia Kaku.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiteta jambo na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga Ally Mwakababu katikati .


WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI

$
0
0

VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo amewataka waratibu wa elimu kata kuachana kabisa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na uzembe na badala yake watimize majukumu yao ipasasavyo bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi pikipiki 17 kwa waratibu wa elimu kata katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuweza kuwawezesha vizuri usafiri kwa ajili ya kuweza kusimamia na kuboresha sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali hususn vijijini.

Pia Jafo amewaagiza maafisa elimu wote kuhakikisha wanaweka mipango endelevu ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi, ambapo pia ametoa onyo kali kwa waratibu hao ambao watazitumia pikipiki hizo kwa kufanyia shughuli nyingine kwa maslahi yao binasfi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe Hamisi Dikupatile amemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuamua kutoa pikipiki hizo 17 ambazo zitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa waratibu wa elimu kata ambao hapo awali walikuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kusafiri umbari mrefu kwenda katika vituo vyao vya kazi.

Naye Afisa elimu wa Wilaya ya Kisarawe Shomari Bane aliahidi kulisimamia kwa hali na mali suala la usimamizi kwa waratbu wote wa kata kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na sekondari na kuondokana na changamoto ya kushuka kwa elimu.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikibabiliwa na changamoto kubwa ya kufanya vibaya katika sekta ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kupekekea kuzindua kampeni maalumu kwa ajili kuweza kutokomeza divisheni ziro.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo akiwasha moja ya pikipiki kati ya 17 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia waratibu elimu wa kata katika halmashauri ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo akiendesha moja ya pikipiki kati ya 17 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia waratibu elimu wa kata katika halmashauri ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu.
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo akimkabidhi funguo mmoja wa waratibu wa elimu kata wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, ambao wamepatiwa pikipiki 17 kwa ajili ya kusimamia sekta ya elimu.(NA VICTOR MASANGU)

TAZAMA LIVE MAPOKEZI YA UJIO WA NDEGE MPYA BOEING 787-8 DREAMLINER,DAR

Vodacom Tanzania yaandaa hafla ya 'Bring Your Kid to Work,' .

$
0
0
 Watoto wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, wakicheza muziki wakati wa hafla ya Bring your kid to work iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
 Watoto wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakishindana kucheza mchezo wa Fusball wakati wa hafla ya Bring your kid to work iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania plc, wakishindana kurusha kamba wakati wa hafla ya Bring your kid to work iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WATAALAM WA DAWASA, DAWASCO KUTOA MAJIBU YA UPOTEVU WA MAJI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

SERIKALI imewaagiza wataalamu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) na Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) kutoa majibu kuhusu upotevu wa maji unaosababisha hasara kubwa kwa Serikali.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Process Makame Mbarawa ameagiza hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya maji iliyopo chini ya Dawasa ya Ruvu Juu na Ruvu chini.

Profesa Mbarawa ameeleza  licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya kumaliza tatizo la maji, Dar es Salaam na Pwani, asilimia 44 ya maji kati ya lita milioni 504 zinazozalishwa kila siku katika vyanzo mbali mbali hupotea kabla ya kufika kwa mtumiaji wa mwisho.

 Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, takribani bilioni nne hupotea kila mwezi kutokana na upotevu wa maji hayo, upotevu ambao ni mkubwa wakati wananchi wakiwa hawana maji. 

"Serikali inapoteza fedha nyingi kutokana na upotevu wa maji njiani kabla ua kufika kwa mtumiaji wa mwisho, ni wakati umefika sasa kwa wataalumu wetu kumaliza tatizo na kutoa majibu yanayoeleweka, lazima Tuingie kwa undani tuangalie maji haya yanapotelea wapi" amesema Profesa Mbarawa

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akikagua mtambo wa Ruvu Chini, wakati wa ziara yake ya kikazi, Ruvu, mkoani Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu mtambo wa mpya wa Ruvu Juu wa kudhalisha maji, mkoani Pwani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kukagua kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Dk. Suphian Masasi, kuhusu kituo cha kusukuma maji ghafi katika mtambo wa Ruvu Juu, Mkoa wa Pwani.
Mkazi wa Kiluvya wilayani Ubungo akitoa malalamiko yake kuhusu mfumo wa kulipia maji unaotumiwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), unavyowasumbua wananchi kupata huduma ya majisafi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea tabia ya kutowajibika miongoni mwa watumishi kwa kisingizio cha mgawanyo wa madaraka.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

Amesema kuna maafisa ushirika ambao hawataki kuwajibika kwa sababu wameajiriwa TAMISEMI na wengine wako chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

"Afisa Ushirika wa Wilaya yuko mkoani ambako ni chini ya TAMISEMI, Mrajis Msaidizi wa Mkoa yuko Wizarani. Serikali ni moja, kwa hiyo wote bado mnawajibika kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa," alisema.

Aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) wasiwapangie kazi nyingine zilizo nje na taaluma yao maafisa ushirika wa wilaya na wahakikishe wanatoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri zao.

"Msimpe kazi ya kufundisha Afisa Ushirika kwa sababu hakuna mtu mwingine. Afisa Ushirika aachwe afanye kazi ya ushirika na atoe taarifa kwenye vikao vyenu. Madiwani mnapokutana kwenye Baraza, mpeni nafasi Afisa Ushirika aeleze maendeleo ya ushirika yakoje katika wilaya yenu."

Alisema changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya ushirika ni wizi na ubadhirifu miongoni mwa watendaji wa vyama vya ushirika waliopewa dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha vyama hivyo.

WAZIRI KIGWANGALLA AWASIMAMISHA KAZI MAOFISA NA ASKARI WOTE 27 WA TAWA KATIKA PORI LA AKIBA UWANDA

$
0
0
Na Hamza Temba, Rukwa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewasimamisha kazi Maofisa na Askari Wanyamapori wote 27 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA katika Pori la Akiba Uwanda akiwemo Kaimu Meneja, Lackson Mwamezi kwa kushindwa kusimamia vizuri pori hilo na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku tatu tangu amsimamishe kazi meneja wa Pori hilo, Mark Chuwa kwa tuhuma kama hizo pamoja na tuhuma nyingine ikiwemo kushindwa kuondoa ngo'mbe zaidi ya 12,000 ambao wamedaiwa kuwepo ndani ya pori hilo.

Pori la Akiba Uwanda lipo katika bonde la ziwa Rukwa katika wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na linasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Dk. Kigwangalla amefanya uamuzi huo jana alipotembelea pori hilo sambamba na kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kilyamatundu ambapo alipokea taarifa ya malalamiko kuhusu askari hao kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye uwezo na kuwaruhusu kuchunga hifadhini huku wakiwanyanyasa masikini kwa kukamata mifugo yao.

Alifafanua tuhuma hizo kuwa ni pamoja na kudaiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki Ziwa Rukwa kwa kuwatozwa kila mmoja Sh. 100,000/- kwa mwezi na kuruhusu mifugo kuchungwa hifadhini kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo kila mfugaji hutozwa kati ya Shilingi milioni sita hadi saba.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Kilyamatundu, Shija Imeli (kulia) alipokuwa akiwasilisha malalamiko yake kuhusu tuhumu za kuwapa rushwa ya shilingi milioni 5.8 Askari watano wa Wanyamapori wa Pori la Akiaba Uwanda (pichani) ili alishe mifugo yake kwa kipindi cha miezi mitano ndani ya pori hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa, wakikagua mazingira ya Pori la Akiba Uwanda baada kuwasimamisha kazi maafisa na askari wote 27 wa pori hilo kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Watumishi hao wananalalamikiwa kupewa rushwa ili kuruhusu wananchi wachunge mifug hifadhini na kwa wale ambao hawatoi rushwa huishia kukamtwa mifugo yao. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa mkoa wa Rukwa, wakikagua mazingira ya Pori la Akiba Uwanda baada kuwasimamisha kazi maafisa na askari wote 27 wa pori hilo kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Watumishi hao wananalalamikiwa kupewa rushwa ili kuruhusu wananchi wachunge mifug hifadhini na kwa wale ambao hawatoi rushwa huishia kukamtwa mifugo yao.

Rais Magufuli aongoza mapokezi ya ndege Boeing 787-8 Dreamliner

$
0
0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitia sahihi pamoja na Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho kwa ajili ya makubaliano ambayo Serikali imeikodisha Ndege yake mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner kwa Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya kufanyia biashara ya usafiri wa anga.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TIMU NANE ZATINGA ROBO FAINALI SPRITE BBALL KINGS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MICHEZO minne ya hatua ya 16 bora ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 imefanyika katika viwili tofauti na timu nane kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali.

Mechi hizo zimepigwa Jumamosi na Jumapili huku michezo minne ya awali ikipigwa katika Viwanja vya Airwing huku mingine ikipigwa Viwanja vya Bandari Kurasini Jijini Dar ed Salaam.

Katika mchezo wa kwanza, timu ya DMI ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 113 dhidi ya 64 vya Fast Heat na Mechi ya pili ilikua ni kati ya Flying Dribbellrs dhidi ya Ukonga Hitmen ambapo Flying Dribbllers walifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapun 87 dhidi ya 63.

Mchezo wa tatu ulikua baina ya Airwing na St Joseph ambapo Ushindi wa vikapu 98 vya St Joseph dhidi ya 78 vya Airwing uliwapeleka hatua ya robo fainali.Mchezo wa nne ulikua ni baina ya Portland wakichuana na Mbezi Beach KKKT, na Portland kuondoka na ushindi mkubwa wa Vikapu 126 dhidi ya 54.

Mechi zingine nne zimechezwa kwenye Viwanja vya Bandari Kurasini jana zikiwakutanisha Mchenga BBall Stars dhidi ya Oysterbay, Mchenga kufanikiwa kuingia robo kwa vikapu 117 dhidi ya vikapu 56. Mchezo wa pili kati ya Stylers alikua anapambana na Temeke Heroes, na Temeke kufanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 76 dhidi ya vikapu 58 vya stylers.
Mchezaji wa Portlands Dennis Babu (jezi nyeupe) akipambana na mchezaji wa Mbezi Beacj KKKT wakati wa mchezo wao wa hatua ya 16 bora uliomalizika kwa Portland kuondoka na ushindi wa Vikapu 126 dhidi ya 54 ya Michuano ya Sprite BBall Kings.
Mchezaji wa Ukonga Warriors Richo Rover akijaribu kumkwepa Baraka Mopere wa Flying Dribbllers wakati wa mchezo wao wa hatua ya 16 ya Michuano ya Sprite BBall Kings baina yao uliomalizika kwa Flying Dribbllers kuondoka na ushindi wa Vikapu 87 kwa 63.

RPC ARUSHA:MADEREVA AMBAO HAWATAZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARNI KUCHUKULIWA HATUA

$
0
0
Na Vero Ignatus Arusha.

Ukaguzi wa magari ya abiria na mizigo umefanyika leo mkoani Arusha ukiongozwa na Kamanda wa polisi Ramadhani Ngazi ,ambapo yamebainika makosa mbalimbali yakiwemo baadhi ya madereva hawana leseni ,magari mabovu,mifumo ya breki na mifumo ya usukani ni mibovu.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo RPC amesema lengo kuu la ukaguzi huo ni kuhakikisha abiria wanaposafiri wanakuwa salama pamoja na chombo husika .Aidha amewataka madereva kufahamu kuwa lazima wazingatie kanuni za sheria za usalama barabarani kwani atakaekiuka sheria itafuata mkondo wake.

Akisisitiza umuhimu wa kufunga mikanda Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amesema kuwa utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40%ya kufunga mkanda unaokoa maisha pale ajali inapotokea.

"Watafiti wanasema kuwa asilimia 40%ya kufunga mkanda hivyo ni vizuri elimu hii mkaitoa hata kwenye familia zenu umuhimu wa kufunga mkanda uwapo ndani ya chombo cha usafiri" alisema Bukombe.Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Joseph Bukombe amewaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri kutengeneza na kurekebisha mifumo ya ndani ya magari yao,badala ya kuweka urembo wa kupaka rangi

Baadhi ya madereva wamepongeza jitihada hizo za jeshi la polisi ,Kwa upande wao madereva,akiwemo Salum Said ambao wamewashauri wenzao waache tabia za kutumia vilevi.Pia wamelipongeza jeshi la polisi kwanjitihada wanazozifanya zanihakikikisha kila dereva anapata elimu ya kutosha ili kuhakikisha wanajitahidinkuzuia ajali zinazosababishwa na kizembe.


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi akizungumza na waandishi juu ya zoezi la ukaguzi wa magari katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoaninna nchi jirani aliyepo kushoto kwake ni RTO mkoani hapo Joseph Bukombe.Picha na Vero Ignatus
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'aziakikagua matairi kwenye moja ya gari .Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi akiendelea na ukaguzi wamagari kama inavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus.

DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17

$
0
0
Na Mathias Canal, Sengerema-Mwanza

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wametatua mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17.

Mgogoro huo umemalizika kwa maelewano ya pande zote mbili kuwa na kauli moja ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho amekubali kuketi meza moja na Uongozi wa chama hicho cha ushirika ili kukubaliana namna bora ya kuchochea Maendeleo katika kijiji na Taifa kwa ujumla badala ya kuendeleza mgogoro usiokuwa na maslahi kwa pande zote.

Alisisitiza umuhimu wa ushirika nchini ambapo aliwaeleza wananchi hao kutoendeleza vita ya kutokuwa na maelewano kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma shughuli za Maendeleo ya kijiji na Taifa kwa ujumla wake.

Pia, Dkt Tizeba ametangaza Kiama kwa maafisa ugani wanaokaa maofisini badala ya kuwasaidia wakulima kwenye hatua muhimu za uandaaji wa shamba na hatimaye wakati wa Kilimo.Katika mkutano huo Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angelina Mabula aliwataka wananchi hao kuwa na utamaduni wa kuketi pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzitatua kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Naibu waziri wa ardhi, nyumba na  maendeleo ya makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Nyamatongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 Julai 2018.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza jambo wakati wa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baada ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 Julai 2018.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha ushirika Nyamatongo Ndg Willium Elikana mara baada ya kuridhia mgogoro kumalizika.

MAKONDA ASEMA ATAWAJIBU WOTE WATAKAOBEZA UJIO WA DREAMLINER

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa yupo tayari kuwajibu watu wote ambao wataonekana kubeza ujio wa ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner.

Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati anatoa utambulisho kwa Rais Dk.John Magufuli kuhusu baadhi ya wageni waliofika kushuhudia tukio la ujio wa ndege hiyo.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa Rais Magufuli kutowajibu wote ambao watabeza ujio wa ndege hiyo katika mitandao ya kijamii na kwamba kazi ya kuwajibu ataifanya yeye na kuungwa mkono na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Naomba nitoe ombi kwako Rais umekuwa ukitufanyia mambo makubwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.Hata hivyo nikuombe usiwajibu watu ambao watabeza ,kazi hiyo nitaifanya mimi tena kwa kuwafuata huko huko mitandaoni.“Rais ukiwa pale Ikulu endelea tu na mipango yako ya kuwafanyia maendeleo Watanzania wote, hili la kuwajibu wanaobeza mambo makubwa ambayo unayafanya tutafanya sisi,”amesema Makonda.

Amemsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo ambayo Watanzania wanayoana na wale ambao hawataki kuyaona basi watege masikio yao vizuri.“Ndege hii najua leo itakuwa kwangu na baadae itakwenda Mwanza, Arusha na Mbeya.Hata hivyo ndege hii itakwenda zaidi ya Bara la Afrika.

“Yoyote ambaye anapinga kinachofanyika maana yake anapingana na ukweli.Kuna mafanikio makubwa yanaonekana na ambaye haoni basi atege masikio yake vizuri asikie,”amesema Makonda.

MICHUZI TV: ALICHOKISEKA RAIS MAGUFULI WAKATI WA UJIO WA NDEGE MPYA YA AIR TANZANIA

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 9, 2018

RAIS MAGUFULI: WASIOPENDA UJIO WA NDEGE MPYA WATAPA TAABU SANA

$
0
0
*Asema anaamini Watanzania wengi wanatambua umuhimu wa ndege hiyo
*Asisitiza ujio wa ndege hizo zimenunuliwa kutokakana na kuziba mianya ya rushwa.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema ujio wa ndege mpya unafurahiwa na kila Mtanzania na kwamba yule ambaye haifurahii ajue atapa taabu sana huku akiwashukuru Watanzania wote kwa kufanikisha ujio wa ndege hizo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati anazungumza kabla ya ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ambapo amefafanua kuwa ujio wa ndege hizo unatokana na kutekeleza ahadi ya kufufua shirika la ndege nchini. Amesema katika juhudi hizo Serikali imeamua kununua ndege saba kwa fedha za Serikali na kwamba tayari ndege tatu zilishawasili nchini na leo ni ndege ya nne kuwasili nchini. 
“Mafanikio haya ni makubwa sana na niseme hajajileta yenyewe bali ni ya Watanzania wote.Nitumie nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote na kubwa zaidi anawashukuru kwa kulipa kodi kwani ndio imesababisha kununuliwa kwa ndege hizo saba. “Hivyo niwashukuru wote ambao wameshiriki katika ujio wa ndege hizi.Ukweli Watanzania tukiamua tunaweza na niishukuru Kamati ya Miundombinu kwa kukubali kununuliwa kwa ndege hizi na kuunga mkono juhudi zinazoendelea,”amesema Rais Magufuli.

Ameongeza Serikali ya CCM iliamua kufufua shirika la ndege kuna sababu tatu , mowapo ni kurudhisha heshima ya Taifa kwani ilikuwa ni aibu kuwa nchi ambayo ina kila kitu halafu hakuna hata ndege ilikuwa ni aibu. “Tuliona tuanze kuitoa aibu hii ambayo tulikuwa tunaipata Watanzania.Kuna nchi ndogo lakini zina ndege lakini sisi hatukuwa nazo.Hivyo tuliona lazima tuiondoe aibu huu kwa kuwa na ndege.

“Watanzania wanahitaji usafiri wa ndege kwani mchango wake ni mkubwa na unahihitajika sana.Zipo sababu za watu kutopanda ndege ikiwamo ya kutokuwepo na miundombinu. “Sababu nyingine ya waanchi wengi kutopanda ndege ilikuwa ni gharama.Kwa watu wa Kagera wanafahamu kwenda Bukoba na kurudi ilikuwa ni Sh.milioni moja lakini sasa kupitia ndege za ATCL ni Sh.400,000,”amefafanua Rais.

Pia amesema sababu ya kufufua ATCL ni kukuza utalii kwani Tanzania inashika nafasi ya pili duniani huku akifafanua pamoja na kuwa na vivutio vya utalii idadi ya watalii ni ndogo. Amesema hiyo inatokana na kukosekana kwa ndege kwani kote ambako wanapokea idadi kubwa ya watalii inatokana na uwepo na ndege za uhakika katika nchi zao. Mnapokuwa na ndege watalii wengi wanakwenda kuangalia utalii wanatumia ndege , hivyo hata uamuzi wa ndege hii ni kutaka kubeba watalii wengi.

“Na ninaamini ndege hii itakapoanza kufanya kazi na ile nyingine itakapokuja itaongeza watalii,”amesema Rais Magufuli. Amesema amesikiliza maoni ya wananchi mbalimbali kutokana na ujio wa ndege hiyo ambapo wengi wameizungumzia vema na hivyo anwashukuru kwa ushirikiano wao. Pamoja na kuimarisha shirika la ndege ,Rais Magufuli amesema pia Serikali ya CCM inaendelea kuboresha usafiri wa majini , ujenzi wa miundombinu ya barabara yakiwamo madaraja na kwamba daraja linalojengwa Tazara litaitwa Mfugale. ia Rais Magufuli amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya nishati ya umeme, miundombinu ya afya na elimu na kufafanua anaamini ifikapo mwaka 2025 Watanzania watakuwa katika uchumi wa kati.

Rais Magufuli amesema maendeleo yanayopatikana sasa yanatokana na kuzima mianya ya rushwa na upotevu wa fedha kwani hivi sasa amebana upotevu wa fedha na matokeo yake fedha zinatumika katika kufanya maendeleo ya nchi.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

NAIBU KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA-ZANZIBAR AKABIDHI SH.MILIONI 1.5 KWA UONGOZI WA CHUO CHA KILIMO NA MIFUGO CHA KAOLE BAGAMOYO

$
0
0
NA ELISA SHUNDA,BAGAMOYO 

UMOJA wa wazazi Taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM, umeahidi kuendelea kusaidia kuboresha chuo cha Kilimo na ufugaji cha Kaole ili kiendane na hadhi ya kuwa chuo bora kitakachotambulika kitaifa na kimataifa, pamoja na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya Tano kwa kuelekea kwenye manufaa ya uchumi wa viwada nchini.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Taifa kutoka Zanzibar, Najma Murtaza Giga alipokuwa mgeni rasmi katika mahafari ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika Chuoni kaole-Bagamoyo mkoani Pwani.

Giga ambaye pia ni Mbunge na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge kwenye bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amewapongeza walimu na watumishi mbalimbali waosimamia chuo hicho kwa kufanya kazi kwenye werefi mkubwa wa kuongeza idadi ya wahitimu katika chuo hicho kwa mwaka huu kufikia 108 tofauti na mwaka jana ambao wahitimu walipungua kufikia 72.

‘’ki ukweli chuo chetu kinachosimamiwa na umoja wa wazazi Taifa wa chama cha mapinduzi CCM, kinapaswa kijitangaze na kipewe sapoti kubwa hasa kwa wazaz, walezi, wadau na serikali kwa ujumla ili kiwe na hadhi kama vyuo vingine na kiiendane na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli” alisema Giga.

Akizungumzia kuhusiana na suala la ajira katika serikali ya awamu ya tano, Giga aliwataka wanafunzi wanaosoma chuoni hapo na wale waliohitimu kwamba wasiwe na wasiwasi kuhusiana na suala hilo kwani najira kwao itapatikana pia hakusita kuwatakawanafunzi hao kwamba wasikimbilie kuajiriwa peke yao bali wahakikishe wanakuwa na m binu mbadala wa kujiajiri na kutoa elimu hiyo kwa vijana wengine waliopo mitaani.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (katikati) akimkabidhi cheti cha Stashahada cha Kuhitimu Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji,Rais wa Chuo cha chuo cha Kilimo na ufugaji cha Kaole,Glorious Kalabamu (kushoto) katika Mahafali ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi la CCM Mkoa wa Pwani,Dk.Zainab Gama na Mkuu wa Chuo hicho,Sinami Simba. Picha zote na Elisa Shunda
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (katikati) akimkabidhi cheti cha Stashahada cha Kuhitimu Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji,Rais wa Chuo cha chuo cha Kilimo na ufugaji cha Kaole,Asnat Kasukuru (kushoto) katika Mahafali ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi la CCM Mkoa wa Pwani,Dk.Zainab Gama na Mkuu wa Chuo hicho,Sinami Simba (mwenye shati la bluu).
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka Zanzibar,Najma Murtaza Giga (katikati) akiwaongoza wahitimu kuingia katika viunga vya chuo kuanza sherehe za mahafali hiyo.

STOP!! KUHUSISHA WATOTO NA VIGODORO NA NGOMA ZA USIKU MKOANI PWANI

$
0
0
Katibu tawala mkoani Pwani, Zuberi Samataba akitembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho ya kielimu yaliyoandaliwa na baadhi ya wanafunzi Chalinze Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya Juma la elimu kimkoa yaliyofanyika Chalinze mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali Chalinze Mkoani Pwani wakionyesha mabango katika maadhimisho ya Juma la elimu kimkoa yaliyofanyika Chalinze.

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE

SERIKALI Mkoani Pwani, imekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wazazi ya kuwahusisha watoto wao kwenda katika vigodoro,  kudhurula nyakati za usiku na badala yake wawasimamie katika suala la elimu ili kuinua taaluma zao. Aidha imewaonya wazazi wanaowakataza watoto wao kwenda shule na wengine kuwashawishi watoto hao kufanya vibaya kwenye mitihani yao ya kumaliza darasa la saba na kidato cha nne.

Akitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani, Katibu tawala wa mkoa huo, Zuberi Samataba alisema, wapo wazazi na walezi ambao ndio chanzo cha kudidimiza suala la elimu. Alieleza, endapo watambaini mzazi ama mlezi akimwachia mtoto kuzurula na kumhusisha kwenye vigidoro na ngoma za usiku atakiona.

"Serikali haiwezi kukubali mzazi akaachia mtoto kiholela, watoto ni wa serikali, mzazi atakaebainika kufanya hayo hatutamvumilia, hii inasababisha kudumaza elimu mkoani kwetu"

Alizielekeza halmashauri kuwachukulia hatua wazazi wanaowaachia huru watoto wao kwani wanahatarisha maisha ya watoto hao hasa kusababisha mimba za utotoni. Samataba alikemea mimba za utotoni, na amesisitiza kuchukuliwa hatua kali kwa wanaosababisha mimba hizo.
Alisema, zipo taarifa zilizokuwa zikidai wapo wazazi wanaojua watoto wao wanafanya vizuri darasani ambapo wanawakataza kufanya vizuri kwenye taaluma zao.

Nae kaimu afisa elimu mkoa ,Hedegald Makundi alieleza uandikishaji katika elimu ya awali  bado upo  chini  tofauti na wanaoandikishwa darasa la  kwanza.

"Elimu ya awali lengo lilikuwa ni kuandikisha  wanafunzi 35,418 walioandikishwa ni 26,997 sawa na asilimia 76 ambapo uandikishaji darasa la kwanza lengo ilikuwa 47,686 walioandikishwa ni 52,551 sawa na asilimia 110" alieleza Hedegald.

Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani, Ramadhani Maneno alisema ili kuhakikisha elimu inaboreshwa ni  lazima kushirikiana wadau, wazazi na walimu kutatua changamoto za kielimu bila kuiachia serikali pekee.

MPINA AAMURU KUUNDWA KWA IDARA YA ULINZI WA MIFUGO NA MAZAO YAKE

$
0
0
Na John Mapepele,Dodoma

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru kuundwa Kitengo kipya cha Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali za Mifugo katika Idara ya Uzalishaji na Masoko cha wizara hiyo ili kutoa ulinzi wa kutosha wa mifugo na mazao yake baada ya kubainika kuwepo mianya mikubwa ya utoroshaji rasilimali hizo nje ya nchi na uingizaji holela wa mazao hayo nchini.

Pia ameagiza kuandaliwa mkakati wa kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato yatokanayo na sekta ya mifugo baada ya kubainika kuwepo kwa mianya mingi na mbinu haramu zinazotumiwa kukwepa kulipa mapato ya Serikali hatua inayosababisha sekta ya mifugo kutoa mchango mdogo katika Pato la Taifa.

Sambamba na hilo pia Waziri Mpina ameagiza kupitiwa upya kwa mfumo wa uagizaji, ununuzi na usambazaji wa dawa za mifugo ambapo wafugaji wengi wamelalamikia mfumo wa sasa hasa katika upatikanaji wa dawa, bei kubwa, kuuziwa dawa zilizokwisha muda wa matumizi na dawa nyingi kutokuwa na viwango vya ubora unaotakiwa.

Akizungumza jijini Dodoma jana wakati wa tathmini ya operesheni ‘Nzagamba’, iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu katika mikoa yote ya Tanzania Bara, Waziri Mpina alisema makusanyo ya maduhuli kutokana na operesheni hiyo jumla ya Tsh bilioni 7.1 zilikusanywa kutokana na tozo, kodi na faini mbalimbali ambapo kumepelekea makusanyo ya maduhuli ya wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18 kufikia sh bilioni 19.5 ikilinganishwa na Tsh bilioni 12 zilizokusanywa katika mwaka wa fedha 2016/17.

Waziri Mpina alisisitiza kuwa awali Serikali ilikuwa inakusanya mapato yatokanayo na sekta ya mifugo yaliyokuwa kati ya Bilioni 10 hadi 12 kwa mwaka licha ya idadi kubwa ya mifugo iliyoko nchini hatua ambayo iliisukuma wizara hiyo kufanya operesheni ‘Nzagamba’ ili kubaini mianya ya upotevu wa mapato yatokanayo na sekta hiyo.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya serikali katika kikao hicho kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Abdallah Ulega 
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Mh Mahamoud Mgimwa na wajumbe wa kamati hiyo akisikiliza mawasilisho ya Taarifa za Operesheni Nzagamba kutoka kwa wawasilishaji leo 
 WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiwa kwenye picha ya pamoja na kikosi kazi alichokiunda cha Operesheni Nzagamba 2018 na viongozi wakuu wa wizara na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Mh Mahmoud Mgimwa .


RAIS MAGUFULI ALIVYOWAONGOZA WATANZANIA KUPOKEA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER

JUMUIYA YA ISTIKAMA ZANZIBAR YAKABIDHI MSAADA WA FEDHA KWA WANANCHI WALIOPATWA NA MAAFA YA UPEPO KISIWA CHA TUMBATU

$
0
0

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

Jumuiya ya Istiqama Zanzibar kwa kushirikiana na Radio Adhana imekabidhi msaada wa shilingi 13,600,000/ kwa wananchi wa Shehia tatu za Tumbatu waliopata maafa ya upepo uliotokea tarehe 30 mwezi uliopita. 

Mwenyekiti wa Kitengo cha Maafa Jumuiya ya Istika Zanzibar Said Hemed Al shaybar alikabidhi msaada huo katika hafla iliyofanyika Shehia yaTumbatu Uvivini na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatib Makame.A 

Al shaybar alisema Jumuiya ya Istiqama imepokea kwa masikitiko makubwa athari zilizosababishwa na upepo huo ambapo watu sita walijeruhiwa kwa kuangukiwa na bati na matufali na kuharibu nyumba 136 za wananchi na nyumba za Ibada na vyuo vya Qur ani. Mwenyekiti huyo alitoa mkono wa pole kwa wananchi wote wa Tumbatu Maafa ya upepo huo na kuwaomba wawe wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu kwani hiyo ni Rehma za Mwenye-ez-Mungu. 

Aliahidi kuwa Jumuiya ya Istiqama itaendelea kushirikiana na wananchi wote wa Zanzibar watakaofikwa na Maafa ya aina hiyo kwa kuwapatia msaada wa hali na mali utakaoweza kuwasaidia kuwapunguzia matatizo. 

Hata hivyo aliwataka wananchi waliopata msaada huo kuutumia katika malengo yaliyokusudiwa ya kununua vifaa vya ujenzi ili waweze kurejea katika hali ya maisha ya kawaida. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Kukabaliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame alisema uwamuzi wa Jumuiya ya Istikama ya kutoa msaada huo ni kusaidia juhudi za Serikali za kuwafariji wananchi wanaopatwa na maafa ya aina hiyo. 

Alisema Serikali kwa upande wake ilianza kutoa msaada kwa wananchi waliopata maafa hayo katika shehia tatu za uvivini, Bomani na Mtakuja mara tu baada ya kutokea na hatua ya Jumuiya Istikama ni muendelezo wa kuwasaidia wananchi hao. Aliwashauri wananchi wa Zanzibar kuendelea kuungana na kushirikiana hasa panapotokezea matatizo ya kiminaadamu bila kujali tofauti zao kwani kufanya hivyo ni kuendeleza umoja na udugu uliopo.
MWENYEKITI wa kitengo cha Maafa Jumuiya ya Istikama Zanzibar Said Hemed Alshaybar akimkabidhi Msaada wa Fedha Bi. Dawa Jabiri Haji mkaazi wa Tumbatu Uvivini ambae Nyumba yake iliharibiwa na upepo. 
MKURUGENZI Mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame akimkabidhi Msaada wa fedha Makame Mdungi Makame mkaazi wa Shehiya ya Bomani.
MWENYEKITI wa Kitengo cha Maafa katika Jumuiya ya Istikama Zanzibar Said Hemed Alshaybar akizungumza na Wananchi wa Tumbatu baada ya kukabidhi Msaada wa fedha kwa waliopatwa na Maafa ya upepo. 
SHEHA wa Shehiya ya Uvivini Hassan Muhidini akitoa shukurani kwa niaba ya Masheha wa Shehiya wenzake wa shehia tatu za Tumbatu, kwa Jumuiya ya Istikama, baada ya kukabidhiwa msaada wa fedha kwaajili ya kununulia vifaa vya ujenzi. Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar. 
WAFANYAKAZI wa Jumuiya ya Istikama Zanzibar wakiwa kwenye Boti wakielekea katika Kisiwa cha Tumbatu kwaajili ya kukabidhi Msaada wa fedha kwa Wananchi waliopatwa na Maafa ya Upepo hivi karibuni. 
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images