Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

GAVANA WA BENKI KUU AIPONGEZA TRA KWA KUKUSANYA KODI YA MAJENGO KIELEKTRONIKI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Prof. Florens Luoga ameipongeza TRA kwa kukusanya kodi ya majengo kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Prof. Luoga amesema kuwa, mfumo huo umesaidia kupunguza adha kwa wananchi ambao sasa wengi wao wanatumia simu za mkononi kulipia Kodi ya Majengo badala ya kwenda kupanga foleni benki.

"Nimefurahishwa sana na uboreshaji wa mifumo ya malipo hususani katika kulipia Kodi ya Majengo ambapo watu wengi wanatumia simu zao za mkononi kulipia kodi hiyo badala ya kwenda benki kukaa kwenye foleni. Hii ni moja ya maboresho makubwa yaliyofanywa na TRA hivyo nawapongeza sana," alisema Gavana.

Gavana Luoga ameongeza kuwa, mifumo ya malipo inapoboreshwa husaidia walipakodi kulipa kodi zao kwa urahisi na kwa wakati na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla.Aidha, Prof. Luoga ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwa sababu maendeleo yaliyopo nchini yanatokana na kodi mbalimbali zinazolipwa na wananchi hao.

"Wito wangu kwa walipakodi na wananchi wote ni kuwasihi kuendelea kulipa kodi kwa wakati kwani faida zote wanazozipata kutokana na mfumo wa utawala waelewe kwamba umetokana na kodi mbalimbali wanazozilipa. Wanachi wanatakiwa kuelewa kwamba, upatikanaji wa elimu, maji, barabara, umeme na mambo mengine kama hayo yote yametokana na kodi," alieleza Prof. Luoga.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inashiriki maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo inatoa huduma mbalimbali kama vile kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.

Huduma nyingine ni pamoja na kuelezea haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Mashine za Kielektroniki za kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (katikati) akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea Banda la TRA katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (kulia) akimsikiliza Afisa Mwandamizi Mchambuzi Mifumo ya Biashara wa TRA, Bw. Mathias Chanila wakati akielezea shughuli zinazofanywa na Kitengo cha Utafiti na Sera mara alipotembelea Banda la TRA katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (kulia) akiwaeleza jambo Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu ambao pia ni Wanachama wa Klabu ya Kodi (TRA Tax Club) ya TRA mara alipotembelea Banda la TRA katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Prof. Florens Luoga (kulia) akiagana na Msimamizi wa banda la TRA Bw. Julius Caesar mara baada ya kumaliza kutembelea banda hilo katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)

MAAFISA WA BUNGE WAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

Afisa Habari wa Ofisi ya Bunge Ndg. Deonisius Simba akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Naibu Mpambe wa Bunge (DSA) Ndg Peter Magati akitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam 

Afisa Utumishi wa Ofisi ya Bunge Ndg. Twaha Said pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge Ndg. Athuman Hussein wakitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam
Mshauri wa mambo ya Sheria kutoka Ofisi ya Bunge Ndg. Mariam Mbaruku pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari Ofisi ya Bunge Ndg. Zuhura Mtatifikolo wakitoa Elimu kwa Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Bunge la Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam 

Washiriki wa Urembo Zingatieni Maadili na Utamaduni wa Kitanzania- Shonza

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha. 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa washiriki wa mashindano ya urembo nchini kuzingatia maadili na tamaduni za kitanzania kwa kuwa kielelezo bora kwa jamii .

Hayo ameyasema jana Jijini Arusha wakati wa shindano la kumtafuta mrembwende wa Jiji hilo , yaliyoandaliwa na The Function House chini ya uongozi wa Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga yaliyoshirikisha warembo 19.

“ Ninyi ni kioo cha jamii, mnaangaliwa na jamii nzima hivyo msibweteke mnapopata umaarufu bali muwe kielelezo bora cha utamaduni na maadili ya Kitanzania ” amesema Mhe. Juliana Shonza . Anazidi kufafanua kuwa sanaa ya urembo ni ajira kama zilivyo ajira nyingine,na kuwaomba wazazi na jamii kutoa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha mabinti wanatimiza ndoto zao katika sanaa hiyo.




Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa Jiji la Arusha, shughuli iliyoandaliwa na The Fuction House chini ya Mkurugenzi Bw. Tilly Chizenga jana Jijini hapo. 
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (Katikati) akifuatilia matukio mabalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na washiriki wa urembo waliokuwa wanawania taji la Miss Arusha, jana katika ukumbi wa Lake Nyasa AICC, kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Bw. Kalisti Lazaro na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa The Fuction House Mrs. Chizenga. 
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (mwenye gauni la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa taji la Miss Arusha baada ya kumalizika kwa mashindano hayo jana Jijini hapo . Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha .


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YA NIGERIA YATUMA UJUMBE NCHINI KUJIFUNZA NAMNA WATANZANIA WANAVYOWEZA KUISHI KWA AMANI NA MBINU ZA MAFANIKIO YA RAIS DKT MAGUFUL

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa umma na Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika akizungumza na ujumbe wa maafisa wa serikali kutoka Nigeria waliofika nchini kujifunza mbinu za mafanikio ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na namna uchumi wa Tanzania unavyokuwa kwa haraka, kujua namna Watanzania wanavyoweza kuishi kwa pamoja bila migogoro ingawa kuna makabila mengi nchini na pia kufahamu utamaduni na historia ya Tanzania na Utawala bora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kuzungumza na ujumbe wa maafisa wa serikali kutoka Nigeria waliofika nchini kujifunza mbinu za mafanikio ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na namna uchumi wa Tanzania unavyokuwa kwa haraka, kujua namna Watanzania wanavyoweza kuishi kwa pamoja bila migogoro ingawa kuna makabila mengi nchini na pia kufahamu utamaduni na historia ya Tanzania na Utawala bora.

RC MAKONDA APOKEA MWENGE WA UHURU, WAANZA KUZINDUA MIRADI WILAYA YA ILALA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Julai 07,2018 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili asubuhi ya leo uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere,  ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo.

Makonda ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru utakuwa Jijini Dar es salaam kwa Muda wa siku tano ambapo utazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 38 yenye thamani ya Shillingi Billion 33.4.

Aidha Makonda amesema katika miradi itakayozinduliwa kupitia mbio za mwenge, miradi 16 itazinduliwa, Miradi 14 itawekewa mawe ya msingi na Miradi 8 itatembelewa.Mwenge wa Uhuru umeanza kwa kukimbizwa Wilaya ya Ilala na baada ya hapo utaenda Wilaya za Kigamboni, Kinondoni, Ubungo na kumalizia na Wilaya ya Temeke.

Akikabidhi mwenge huo kwa kwa mkuu wa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Seleman Abdallah ameshukuru uongozi wa Mkoa kwa kuwa nao pamoja katika shughuli nzima ya mapokezi ya mwenge na amewatakia kila la heri kati mbio hizo.Naye msimamizi na mkimbiza mwenge taifa Charles Fransis Kabeho amewashukuru wakazi waliojitokeza na amehaidi kufikisha ujumbe wa mwenge katika jiji la Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,(kulia)akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba,Hemed Suleiman Abdallah leo katika uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa ajili ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeo katika wilaya hiyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,Ndugu Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Kivule (picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

Semu ya viongozi mbalimbali wakiwa katika uwaja wa ndege Mwalimu Nyerere kuupokea mwenge wa Uhuru ulikua ukitoka Pemba Zanzibar.

WANANCHI WA KALAMBO WAZUIA KWA MUDA MSAFARA WA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

$
0
0
Na Hamza Temba, Kalambo, Rukwa

Msafara wa Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla umelazimika kusimama kwa muda baada ya kusimamishwa na kundi kubwa la wananchi wa kijiji cha Kisumba kilichopo wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wakiwa na mabango yanayoeleza kero zao mbalimbali.

Miongoni mwa kero hizo ni pamoja na wanyamapori jamii ya Tembo kuvamia mashamba yao na hivyo kukosa chakula na kukosekana kwa huduma muhimu ya maji iliyotokana na kuchakachuliwa kwa mradi wa maji wa jumla ya shilingi milioni 663 kijijini hapo.

Mkazi wa kijiji hicho, Leonard Kiombe, alisema mara nyingi wamekuwa wakiwasimamisha viongozi kwa sababu ya kero ya maji, "tulipata mradi wa milioni 663 wakasema zaidi ya vijiji 6 vitapata maji lakini kijii cha kisumba mpaka sasa hatuna maji, mradi umechakachuliwa na maji hayatoki" alisema.

Akijibu kero hizo, Waziri Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha Taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kutengeneza vikundi vya wananchi wa vijiji vyote vinavyopakana na Hifadhi ya Msitu wa Kalambo na Pori la Akiba Lwafi ili wawezeshwe fedha za mikopo ama mizinga ya kufugia nyuki ambayo wataipanga pembezoni mwa mashamba yao ili kuzuia tembo wasiingie kwenye mashamba. 

Alisema teknolojia hiyo imethibitika kusaidia kudhibiti tembo wasilete madhara kwenye makazi ya watu kwa kuwa nyuki hufukuza tembo na endapo tembo nao wakinusa harufu ya nyuki huwa sio rahisi kusogelea maeneo hayo, hivyo ameagiza mradi huo utekelezwe ndani ya kipindi cha miezi miwili kabla mvua za masika kuanza.

Waziri Kigwangalla pia ametoa wito kwa wananchi hao kuacha kufanya shughuli zao kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo maeneo ya mapito ya wanyamapori kwakuwa kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha na ustawi wao.Akizungumzia kero ya maji, Dk Kigwangalla aliwaahidi wananchi hao kuiwasilisha kwa waziri husika ili iweze kuapatiwa ufumbuzi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisumba katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akiondoka kuendelea na ziara yake baada kujibu kero mbalimbali za wananchiwaliosimamisha msafara wake katika kijiji cha Kisumba katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Rukwa, Albinus Mugonya ambaye amebeba mabango yenye kero za wananchi hao. 
Sehemu ya wananchi hao wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisumba katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao jana.

DKT MWIGULU NCHEMBA AREJEA JIMBONI KWAKE APOKELEWA KWA SHANGWE,AMSHUKURU RAIS MAGUFULI

OLENASHA:KINACHOTAKIWA KWA WANANCHI NI MAENDELEO NA SIYO SIASA CHAFU

$
0
0

Na.Vero Ignatus Ngorongoro

Mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa elimu sayansi na Teknolojia William Olenasha ameanza ziara ya kutembelea wananchi wa jimbo lake kwa ajili ya kueleza kazi aliyofanya kwa muda wa miaka mitatu tangu achaguliwe na wananchi wake ikiwemo mradi wa barabara ya Lami kutoka Loliondo mpaka Mto wa Mbu.

Imekuwa ni desturi ya mara kwa mara kwa mbunge huyo kutembelea wananchi wake kila kata ambapo kila kata amepita mara nne tangu achaguliwe kuwa muwakilishi wa wananchi Bungeni.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Ngaresero pamoja na kata ya Pinyinyi zilizopo katika wilaya hiyo Olenasha amesema kuwa yeye ni mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi wanyonge ambao wana changamoto hivyo lazima azitatue kwa kuwa ndiyo jambo alilotumwa na wananchi kuwawakilisha.Amesema kwasasa serikali inayoongozwa na Raisi John Magufuli imejitofautisha sana na kipindi cha nyuma kwakuwa hata maeneo ambayo yalisahaulika kwa muda mrefu kwa sasa yameshaanza kupatiwa vipau mbele ikiwemo pia miradi mikubwa ambayo imepelekwa katika jimbo hilo la Ngorongoro.

Olenasha amesema kuwa tayari kupitia yeye kama mbunge wananchi wameshaanza kuletewa mradi mkubwa wa barabara ya lami ambao ni wa kihistoria kutoka Loliondo mpaka mto wa Mmbu kilomita 213 mradi ambao wengi walizani ni ndoto tayari umeshaanza kujengwa.“Napenda kuwataarifu wananchi kuwa ujenzi wa barabara ya lami umeshaanza na shilingi Bilioni 87 zimeshatolewa tayari jambo ambalo wengi walidhani ni ndoto lakini imewezekana na mradi umeanza kwa ksi kubwa”Alisema Olenasha

Hata hivyo Olenasha amemshukuru Raisi Dokta Magufuli kwa kuwapa kipau mbele katika kuletea wananchi wake maendeleo ambapo nje na mradi huo wa Barabara upo mradi wa Umeme,Afya,maji na Elimu ambapo miradi hiyo imeshaidhinishiwa fedha kwa ajili ya kuanza mara moja.Kwa upande wa wananchi ambao wameshiriki mkutano huo wa Mbunge wamesema kuwa tangu kuanza kwa historia ya Uhuru hawajawahi kupata mawasiliano hata ya Simu wala kuona kituo cha afya lakini kupitia mbunge wao wameona mafanikio hayo.

Pamoja na hayo wamesema kuwa mbunge wao amekuwa mstari wa mbele katika suala la maendeleo kwasababu kila mara anatembea jimboni kwake licha ya kuwa na changamoto zilizopo lakini wanampa ushirikiano mzuri ili afanikishe kile ambacho ameshakianza kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Olenasha,ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ngorongoro William Olenasha akizungumza na wananchi wa jimbo hilo.
Wananchi wa kijiji cha Ngarasero wakimsikiliza mbunge wao Wiliam Olenasha katika ziara yake ya kutembelea wananchi

RAIS NA AMIRI JESHI MKUU DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku  Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la  Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) aliowatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akipatiwa muhtasali na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Luteni jenerali Paul Massao wakati wa hafla ya  hafla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mafunzo wakati wa hafla ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018
 Sehemu ya  Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) waliotunukiwa kamisheni na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018.

Kikosi cha gwaride la kimya kimya kikitumbuiza wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine katika picha ya pamoja na watunukiwa baada ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akiondoka eneo la gwaride baada ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 123 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  leo Jumamosi Julai 7, 2018

TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA

$
0
0



Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kupeleka timu ya wataalam wa fani mbalimbali 167 katika nchi tano tofauti kwa lengo la kujifunza namna ya kusimamia uendeshaji wa treni ya kisasa itakayotumia umeme.

Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ikiendelea na ujenzi wa reli ya kisasa maarufu Standard Gauge Rail(SGR) ambapo treni yake itasafiri kwa kasi ya umbali wa kilometa 160 kwa saa.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Masanja Kadogosa amesema timu ya wataalamu hao itaondoka wakati wowote kuanzia sasa.

Amefafanua watalaam hao watatoka katika kada mbalimbali zikiwamo za watalaam wa mawasiliano, umeme, madaraja, usafirishaji, mafundi na madereva.Ametaja nchi ambazo wameingia nazo makubaliano ya kuwafundisha wataalam hao ni Korea Kusini, Uturuki, Ethiopia, China na India." Tumeamua hivyo kutokana na kwamba tunahitaji kuwajengea uwezo watalaam wetu kutoka kwa nchi ambazo zenyewe zina uzoefu wa uendeshaji wa reli ya aina hii. Watalaam hao wataondoka muda wowote kutoka sasa,amesema.

Amefafanua kwa wanaokwenda nchini Uturuki waliamua kusubiri kidogo kutokana na mchakato wa uchaguzi wa nchi hiyo.Akizungumza ujenzi wa reli hiyo amesema utaambana na ujenzi wa karakana za kisasa ambazo zitaenda sambamba na matumizi na teknolojia mpya inayotumia umeme tofauti na karakana zilizopo.Ameongeza ujenzi wa reli hiyo utamalizika kwa wakati kama ilivyopangwa kwani unaendelea kwa kasi na ufanisi mkubwa na tayari mkandarasi ameahidi kuongeza vifaa na watalaam.

Amesema ujenzi wa nguzo katika eneo la kutoka Stesheni ya Dar es Slaam mpaka Stesheni ya Ilala unaendelea vizuri ambao ni asilimia 30 ya ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Stesheni ya Pugu.Akizungumzia mikakati ya TRC amesema licha ya ujenzi wa reli ya kisasa pia wanaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya reli katika maeneo mbalimbali.

Amesema lengo ni kuongeza uwezo wa shirika katika kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TRC Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari katika banda la shirika hilo kwenye viwanja vya maonesho vya Sabasaba leo wakati akizungumzia maen deleo ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya SGR kutoka Dar-Moro- Dodoma na ukarabati wa Reli ya Kati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Bw. Masanja Kadogosa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wageni kutoka mataifa kadhaa ya nje waliofika kwenye banda la TRC wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TRC.

Waziri Mahiga atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)

$
0
0
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alipotembelea banda la Wizara. 
Mhe. Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa 
Mhe. Mahiga akiwa kwenye banda la kituo cha kumbi za mikutano cha kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba. Mbele yake ni baadhi ya watumishi wa kituo hicho. 
Mhe. Mahiga akikabidhiwa zawadi ya mchoro na Bibi Hoyce Temu kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa (UN). Waziri Mahiga alitembelea banda la UN kwenye maonesho ya sabasaba na kupata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini. 

WARATIBU ELIMU WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Waratibu elimu Kata wameishukuru serikali kwa kuwapatia pikipiki ambazo zitawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa. 

Pikipiki hizo walizopatiwa waratibu hao ni miongoni mwa pikipiki zilizotolewa na serikali kwa waratibu elimu wa Kata zote hapa nchini zenye lengo la kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa waratibu hao.

Waratibu hao wametoa pongezi zao mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akikabidhi pikipiki 17 kwa waratibu elimu wote wa wilaya hiyo ya kisarawe. Waratibu hao wamemuahidi waziri huyo kwamba watafanya makubwa katika elimu kwa kuwa pikipiki hizo zitawasaidia zoezi la uratibu wa elimu katika kata zao. 

Kwa upande wake, Waziri Jafo amewaasa waratibu hao kuzitumia pikipiki hizo kwa lengo la kupandisha taaluma katika maeneo yao. "Ikumbukwe kwamba serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa posho ya madaraka kwa waratibu elimu kata pamoja na wakuu wa shule za msingi na serikali hapa nchini,"amesema.Amebainisha kuwa kupatikana kwa pikipiki hizo kutawezesha kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hapa nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akizungumza na waratibu wa elimu kata ya Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akikabidhi pikipiki kwa waratibu kata ya Kisarawe.
Baadhi ya pikipiki za waratibu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akikabidhi pikipiki kwa waratibu wa elimu.

CUF WATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO KATIKA KATA 79,MAJIMBO MAWILI

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakitashiriki Uchaguzi mdogo wa marudio katika Kata 79 na majimbo mawili ambao umetengazwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.

Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa habari, Uenezi na Uhusiano na Umma Mbarala Maharagande ametoa taarifa ya kutoshiriki kwenye uchaguzi kwa vyombo vya habari na kufafanua uamuzi huo umetokana na Kamati ya Utendaji baada ya kufanya uchambuzi na tathimini ya kina kuhusu tangazo la kufanyika uchaguzi huo.

Maragande ambaye yeye anatoka CUF ya upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Ahmad amesema sababu za msingi za kutoshiriki katika uchaguzi huo ni nyingi moja wapo ikiwa ni mgawanyiko wa uongozi Katika uchaguzi huo uliojitokeza kutokana na mgogoro aliodai umepandakizwa na Profesa Ibrahim Lipumba na Washiriki wake

Hivyo amesema CUF unaona ni ishara kwa sasa kuelekeza nguvu na rasilimali zake chache zilizopo katika kushughulika na kupata ufumbuzi wa mgogoro uliopo. Ameongeza kuwa CUF inatoa mwito kwa vyama rafiki vyote katika UKAWA kukaa pamoja kufikia muafaka na maridhiano na kusimamisha wagombea bora, imara, na madhubuti kugombea nafasi hizo zote.

"CUF inatoa mwito kwa viongozi na wanachama wake wote katika maeneo yote ya marejeo ya uchaguzi kwa Tanzania Bara kushirikiana bega kwa bega na kuunganisha nguvu za pamoja na vyama rafiki vya UKAWA katika uchaguzi huu ili kuishinda CCM,"amesema.

Maharagande amesema katikankata 79 zilizotangazwa, CUF imepoteza Kata 4 ilizokuwa inaziongoza kwa madiwani wake ambao waliamua kwenda CCM. Kata mbili zipo manispaa ya Jiji la Tanga Mjini na Kata moja Mtwara Vijijini na Diwani mmoja Kufariki (Wilaya ya Kwimba).

Kutokana na vigezo vya kitaalamu na kitakwimu na ramani ya maeneo utakapofanyika uchaguzi huo wa marudio CUF ingeweza kushiriki kikamilifu katika Kata za mkakati 11 pekee.

Wilaya ya Siha yapiga hatua kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

$
0
0
 Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Hope Rusibamayila akishirikiana na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro kutoa maelekezo kwa wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund namna ya Kibuyu Chirizi kikifanya kazi ya kuosha mikono kwa sabuni baada yakutoka Chooni.

 Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund wakiendelea na ziara yao yakukagua baadhi ya miundombinu waliyoisaidia katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro. 
 Picha ya Pamoja ya Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kilari wakionesha kalamu zao juu kuonesha furaha zao baada ya kupokea kutoka katika Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund

 Mwanafunzi Kutoka Shule ya Msingi ya Kilari Vaileth Wilfred akimkabidhi ujumbe Afisa Elimu Wilaya ya Siha Rose Sandi baada ya kumaliza Shairi lao, kulia kwake ni  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Endrew Method na wa mwisho ni Afisa Mipango wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Bw. Oscar Kaitaba. 
 Picha yapamoja ya Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund baada ya kumaliza shughuli ya kutembelea na kukagua miundombinu katika Shule ya Msingi Kilari wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro.

KAMPUNI YA KUFANYA MATENGENEZO YA UMEME BILA KUUKATA YATUA DODOMA

$
0
0
NA Said Mwishehe Blogu ya Jamii

UAMUZI wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya utawala madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli umesababisha Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrique Live Power Line Maintenance T&D Ltd Donald Mwakamele kuamua kuirudisha kampuni yake iliyokuwa nchini Botswana na kuihamishia makao makuu ya nchini Dodoma.

Mwakamele ni mtaalam wa kimataifa wa kufanya matengenezo ya umeme bila kuuzima kupitia teknolojia hiyo imemfanya awe maarufu katika nchini mbalimbali barani Afrika lakini sasa anasema uongozi wa Rais Dk.Magufuli umemfanya arudi nchini na lengo lake kubwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuelekea uchumi wa kati na ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na Michuzi Blog Mwakemele amesema kilichosababisha arudishe mitambo yake ya kufanya matengenezo ya kuunganisha umeme bila kuuzima umetokana na namna ambavyo Rais Magufuli ameonesha dhamira ya dhati ya kuwainua Watanzania kiuchumi.

Amesema Rais Magufuli ameonesha namna ambavyo anataka kuona nchi yetu inapiga hatua na hivyo ameamua kuja na kauli mbiu ya viwanda , hivyo kwa kutumia taaluma yake ameamua kurudi nchini ili kuhakikisha wawekezaji hawapati nafasi ya kushuhudia umeme ukikatika kwani anao utaalam ambao ukitumika hakuna siku ambayo umeme utakatika.

“Nimekuwa nchini Botswana kwa miaka sita sasa na nikiwa huko nilikuwa nafanya kazi na Shirika la Umeme la nchi hiyo ambalo linafahamika kama BPC.

“Kazi yangu kubwa ilikuwa kufanya matengenezo ya umeme bila kuukata.Pia nilipewa jukumu la kuwasomesha wataalam wao kutumia teknolojia hii ambayo inafahamika kama Live Power Maintenance,”amesema.Amesema akiwa nchini huko amepata nafasi ya kusikiliza hotuba za Rais Magufuli na kuibaini dhamira njema aliyonayo katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.Hivyo ameamua kuirejesha mitambo na kampuni yake nchini ili ashiriki kikamilifu kuunga mkono jitihada za Rais.
 Mataifa Mengi yaliyoendelea katika masuala ya viwanda yanaitumia sana teknolojia hiyo kama wanavyoonekana katika picha hii.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrique Live Power Line Maintenance T&D Ltd Donald Mwakamele kulia akiwapa maelezo  wataalam kutoka nchini Kenya ambao walijifunza teknolojia hiyo kwake Morogoro  na sasa wanaitumia nchini mwao.
 Gari Maalum la Mitambo ya kurekebisha umeme bila kuzima ambalo limewasili mkoani Dodoma tayari kwa kazi hiyo.
Gari hili pia ina eneo maalum linalotumika kama darasa kwa wananfunzi lilikwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia kazi hiyo.


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 8, 2018

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete atembelea banda la Nssf maonesho ya saba saba

$
0
0


Rais wa awamu ya nne Mh Dkt Jakaya Kikwete akipata maelezo kuhusiana na huduma mbali mbali zinazofanywa na Shirika la Taifa ya Hifadhi ya jamii NSSF kutoka kwa Kaimu Meneja uhusiano na masoko Bwana Salim Khalfan ,pembeni yake ni Mkurugenzi wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania Tan Trade, Edwin Rutegaruka mara baada ya kutembelea katika banda la NSSF kwenye maonesho ya 42 Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya sabasaba,jijini Dar

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji atoa wito kwa taasisi za umma kuunganishwa kwenye mfumo wa ununuzi wa umma

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewahamasisha wanyabiashara na wazabuni kutembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma – PPRA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Sabsaba ili kuelimishwa kuhusu Mfumo mpya wa ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (Tanzania National e-Procurement System – TANePS) pamoja na kujisajili kwenye mfumo huo. 

Dkt. Kijaji alitoa wito wakati alipotembelea banda la PPRA na kupatiwa maelezo kuhusu mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na namna mfumo huo unavyofanya kazi. Amesema dhamira ya Serikali ni kuondoa malalamiko kwenye manunuzi ya Umma kwa upande wa wazabuni na Umma kwa ujumla kwa kuhakikisha michakato yake inafanyika kwa uwazi na ushindani ili mwisho wa siku ipate thamani halisi ya fedha inayotumika kwenye manunuzi. 

Pia ametoa wito kwa PPRA kuhakikisha taasisi zote za Umma zinaunganishwa kwenye mfumo huo mapema iwezekanavyo.Kwa upande wake Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa PPRA Bi. Giftness David alisema, kwa kuanza, mfumo wa TANePS umeanza kutumiwa na taasisi za Umma mia moja kwa ajili ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba, bidhaa na huduma mtambuka. Ameongeza kwamba, kwa wakati huu, PPRA imetoa kipao mbele katika kutoa mafunzo kwa watoa huduma (wazabuni) na taasisi nunuzi kuhusu matumizi ya mfumo huo. 

TANePS ni mfumo ulioandaliwa na PPRA ili kukidhi matakwa ya sheria ya ununuzi wa Umma, na unawezesha mchakato mzima wa ununuzi wa bidhaa, vifaa, huduma na kazi za ujenzi kufanyika kwa njia ya mtandao (kielektroniki).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la PPRA
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipata maelezo kuhusu shughuli zinazotekelezwa na PPRA kutoka kwa Mtaalam wa Mifumo ya Habari wa Mamlaka hiyo Bi. Giftnes David
Mmoja wa wafanyabiashara walojitokeza kusajiliwa kwenye mfumo wa TANePS akielekezwa namna ya kujisajili na Mtaalam wa Mifumo wa PPRA Bi. Giftnes David 
Baadhi ya watumishi wa PPRA wakifurahia matunda ya kazi wanazofanya kwenye banda la Mamlaka hiyo katika viwanja vya Sabasaba

WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea tabia ya kutowajibika miongoni mwa watumishi kwa kisingizio cha mgawanyo wa madaraka.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.


Amesema kuna maafisa ushirika ambao hawataki kuwajibika kwa sababu wameajiriwa TAMISEMI na wengine wako chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika."Afisa Ushirika wa Wilaya yuko mkoani ambako ni chini ya TAMISEMI, Mrajis Msaidizi wa Mkoa yuko Wizarani. Serikali ni moja, kwa hiyo wote bado mnawajibika kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa," alisema.

Aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) wasiwapangie kazi nyingine zilizo nje na taaluma yao maafisa ushirika wa wilaya na wahakikishe wanatoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri zao.

"Msimpe kazi ya kufundisha Afisa Ushirika kwa sababu hakuna mtu mwingine. Afisa Ushirika aachwe afanye kazi ya ushirika na atoe taarifa kwenye vikao vyenu. Madiwani mnapokutana kwenye Baraza, mpeni nafasi Afisa Ushirika aeleze maendeleo ya ushirika yakoje katika wilaya yenu."

Alisema changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya ushirika ni wizi na ubadhirifu miongoni mwa watendaji wa vyama vya ushirika waliopewa dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha vyama hivyo.Alisema changamoto nyingine ni ukosefu wa elimu ya kutosha ya ushirika miongoni mwa wanachama, viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika; kuporomoka kwa imani ya ushirika miongoni mwa jamii na kwa baadhi ya wanachama kutokana na vyama vya ushirika kushindwa kukidhi mahitaji ya wanachama wake.

TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018 lafunguliwa mjini Zanzibar

$
0
0
TAMASHA la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018, limefunguliwa juzi usiku huku Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikijipiga kifua kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoikabili tasnia ya filamu nchini. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa tamasha hilo la 21 katika ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi, alikiri kuwa pamoja na mafanikio yake, kuna maeneo ambayo halijafanya vizuri.

Alisema miongoni mwa upungufu huo, ni kutokufikiwa ufanisi wa asilimia 100 katika ulinzi wa haki za wabunifu na watengenezaji filamu, akisema iko haja ya kuuangalia upande huo kwa jicho la tatu ili wasanii hao wafaidi matunda ya jasho lao.

Aliiambia hadhira iliyofurika ukumbini hapo wakiwemo watalii kutoka nchi mbalimbali, kuwa Serikali ya Zanzibar ilianzisha kwa nia njema Ofisi ya Msimamizi wa Haki za Ubunifu (COSOZA), mfumo unaoendeshwa kimataifa ili kulinda haki za wasanii.

Alifahamisha kuwa tasnia ya filamu ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kusaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kijamii hasa uhaba wa ajira, kama ilivyo katika mataifa mengine yaliyopiga hatua kubwa kifilamu na matamasha yanayotambulika kimataifa.

“Kwa upande wa serikali, naamini taasisi na vyombo husika vitaendelea kusimamia upatikanaji wa haki kwa waliopoteza jasho lao katika tasnia hii ili nao wanufaike kwa malengo waliyojiwekea,” alisema.Waziri huyo alisema kuanzishwa kwa COSOZA ni sehemu ya msukumo wa serikali katika kutoa mchango ili kuwainua kimaisha wananchi waliojikita katika tasnia ya filamu.


 Baadhi ya vikundi mbalimbali pichani juu na chini vikiwasili kwenye uzinduzi wa tamasha hilo la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) mwaka 2018.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>