Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUBORESHA MFUMO WA HUDUMA ZA VIBALI VYA AJIRA NA UKAAZI NCHINI

$
0
0

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Idara ya Uhamiaji) imekusudia kufanya mabadiliko ya kimfumo ambayo yatahusisha utoaji wa vibali ya ajira nchini pamoja na vibali vya ukaazi ili kuhama kutoka mfumo wa zamani na kuwa na mfumo wa kielektroniki.

Maboresho hayo yanakwenda sambamba na matumizi ya TEHAMA, ambapo kutakuwa na utaratibu wa kuwa na kadi moja (smart card), ambayo itakuwa na taarifa za muhusika kuhusu kibali cha ajira pamoja na hati ya ukaazi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alikukutana na waandishi wa habari hii jijini Dodoma.

Waziri Mhagama alieleza kuwa, kuanzishwa kwa mfumo huo utasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wageni nchini zenye uhakika na zitakazo patikana kwa wakati ili kudhibiti mianya yote rushwa kwa watendaji kwa kuwa taarifa zote zitapatikana katika kanzidata maalum.

“Uwepo na mfumo huu mpya utasaidia kuondokana na mianya yote ya rushwa kwa Watendaji wa Serikali pamoja na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wageni na malengo ya ujio wao hapa nchini kwani taarifa zote zitapatikana kwenye kanzidata maalum,”alisisitiza Mhagama

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba alieleza kuwa mfumo huu wa kadi moja utasaidia hutatua changamoto ya uchuleweshaji wa vibali ili kuondokana na usumbufu wa ufuatiliji wa vibali hivyo kwa wageni.

“Lengo kubwa la mabadiliko haya ni kuwa na kadi moja itakayomruhusu mgeni kufanya kazi kulingana na sheria na taratibu zilizopo na kuwaondolea usumbufu usio wa lazima na kuongeza ufanisi kwa watendaji wa Serikali,” alisisitiza Mwigulu

Aidha alitoa rai kwa Taasisi zote zinazotumia wageni kuhakikisha wanafanya uhakiki wa taarifa za wageni hao hususan uhalali wa kuwepo kwao pamoja na kazi wanazozifanya ili kuepuka udanganyifu unaoweza kujitokeza.

“Nitoe rai kwa Taasisi zote zinazotumia wageni katika ofisi zao kuhakiki na kujiridhisha taarifa za vibali vya ajira na ukaazi wa wageni hao ili kuepuka taarifa zisizo sahihi na kuhakikisha kila kila mgeni anakuwa na kibali halali kinachomruhusu kuwepo nchini,”alisisitiza Mwiguli
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao kuzungumzia azma ya Serikali ya kuboresha mfumo wa huduma za vibali vya ajira na ukaazi nchini Juni 28, 2018 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba akitoa ufafanuzi wa masuala ya vibali vya ajira na ukaazi kwa waandishi wa habari walipokutana mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) walipokutana Bungeni Dodoma Juni 28, 2018.

KAMPUNI ZA BIMA KURUHUSIWA KUSAJILI MAWAKALA KADRI YA UWEZO WAO, SERIKALI YAPUNGUZA MASHARTI

$
0
0
*Kamishna wa Bima nchini atoa ufafanuzi , aipongeza kampuni ya Sanlam kwa kutimiza miaka 100


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMISHNA wa Bima nchini Dk.Baghayo Saqware amesema kuanzia Agosti mwaka huu kampuni za bima nchini yataanza kusajili mawakala wa bima wao wenyewe kadri wanavyoweza huku mchakato wa ununuzi wa bima kwa njia ya kibenki ukiendelea.

Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kutimiza miaka ya 100 ya kampuni ya bima ya Sanlam tangu kuanzishwa kwake.Hivyo mbali ya kuipongeza Sanlam kwa kutimiza miaka 100 akatumia nafasi hiyo kutoa majibu ya changamoto ambazo ziliwasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sanlam Ibrahim Kduma.

Kaduma pamoja na kuzungumzia mafanikio ya kampuni hiyo kwenye masuala ya bima ametaja changamoto tatu ambazo zinakwamisha sekta ya bima nchini.Changamoto hizo ni masharti magumu ya kusajili wakala wa bima, kuchelewa kwa mchakato wa benki kutumika kununua bima pamoja na kodi kubwa.

Hivyo Dk.Saqware amewahakikisha watoa huduma za bima nchini kuwa tayari yameandaliwa mabadiliko ya sheria na hivyo kampuni ya bima itakuwa na uwezo wa kusajili mawakala wengi kadri ya uwezo wao.

Kuhusu benki kufanya shughuli za bima Dk.Saqware amefafanua changamoto hiyo nayo itapata ufumbuzi hivi karibuni kwani hivi sasa wanaandaa kanuni na Agosti mwaka huu watazipeleka kwa wadau ili wazipitie na kisha kuanza kutumika bada ya kupata baraza za Waziri.

"Kuhusu benki kufanya shughuli za bima hili lilichekelewa kwasababu Benki Kuu Tanzania(BoT) ilikuwa inataka kujiridhisha na sas imekubali , hivyo ni changamoto ambayo kimsingi imepata ufumbuzi wake na kilichobaki ni kuandaliwa kwa kanuni ili benki nazo zitumike kwenye masuala haya ya bima"amesema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wapili kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya kampuni hiyo.Hafla hiyo iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Ibrahim Kaduma (kulia) pamoja na viongozi wengine akigonganisha glasi pamoja na wateja wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya Sanlam tangu kuanzishwa kwake. Wa tatu kushoto ni Kamishna wa Bima Dk Baghoyo Sakwale ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo pia wadau mbalimbali wa masuala ya bima walihudhuria.

SERIKALI YAUTAKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KUONGEZA KASI YA KUBUNI MIKAKATI NA MABORESHO

$
0
0
SERIKALI imeutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuongeza kasi katika kubuni mikakati na maboresho ikiwemo taratibu za kujiunga ambazo zitawawezesha wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma zake.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa NHIF mjini Morogoro ambapo amesema kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha watu wote wanakuwa na bima ya afya.

"Serikali ya Awamu ya Tano imeweka nguvu kubwa katika utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi hivyo ninawaagiza muongeze kasi katika ubunifu na maboresho mbalimbali ambayo yatakwenda sambamba na matarajio ya Serikali yanayolenga wananchi wengi zaidi kuwa katika mfumo wa kupata huduma za matibabu kwa mfumo wa bima ya afya,” amesema Dk. Ndugulile.

Amewataka watumishi wa Mfuko hususan Mameneja wa Mikoa kutokaa maofisini mwao na badala yake watoke nje kwa ajili ya kuhamasisha wananchi, kuangalia huduma wanazopata katika vituo vya kutolea huduma pamoja na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali.

Akizungumzia utendaji kazi wa Baraza, amewataka wajumbe wa baraza hilo kutambua wajibu wao ndani ya baraza kwa kuwa ni chombo muhimu katika kubuni na kuweka mipango thabiti ya kuendesha taasisi ambayo ina dhamana kubwa ya kuangalia ama kushughulikia huduma za matibabu kwa wanachama.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizindua Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi nyaraka za kuongoza Baraza hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga.
Wajumbe wa Baraza la Pili la NHIF, wakionyesha ishara ya mshikamano baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Baraza hilo.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza wakionyesha ishara ya mshikamano.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 29, 2018

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO MGENI RASMI KONGAMANO LA MUHAS JULAI 2

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako anataraji kuwa mgeni rasmi katika kongamano la sita la kisayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) litakalofanyka Julia 2 hadi Julai 3 mwaka huu katika ukumbi wa LAPF Millenium Tower, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Andrea Pembe amesema jukumu mojawapo la MUHAS ni kutoa mafunzo ili kujenga rasilimali watu ya fazi za afya, kufanya tafiti na kushiriki kikamilifu utoaji huduma za afya kwa umma.

Amesema ili matokeo ya tafiti zinazofanywa yaweze kutumiwa na watekelezaji, wadau, wafanyakazi wa huduma za afya na wengine wanaofanya kazi katika maeneo husika ya kitaalamu, matokeo ya tafiti hizi hayana budi yasambazwe kwa ufanisi. “Hivyo basi, madhumuni ya kongamano hili la sita ni kushirikiana, kuelezana, kujifunza na kubadilishana ujuzi unaotokana na matokeo ya tafiti kati ya watafiti mbali mbali.

"Watoa huduma wa afya, watekelezaji wa mikakati na sera mbalimbali na wadau wengine wote ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kushirikisha jamii kwa ujumla kupitia vyombo mbalimbali vya habari,"amesema. Pia katika Kongamano hili, Chuo kitaeleza mafanikio ya tafiti na athari zake kwa upande wa kijamii na maendeleo ya uchumi wa nchi. Katika Kongamano la sita la kisayansi, Chuo kitaonesha matokeo ya tafiti za hivi karibuni ya kisayansi kutoka miradi mbali mbali ya tafiti zinazotoka ndani na nje ya nchi katika kipindi cha miaka ya nyuma.

" Kitu cha muhimu zaidi katika jamii ya wanataaluma wa MUHAS ni kuwa watapata fursa ya kushiriki matokeo yao na kubadilishana mawazo na wataalamu pamoja na wadau kutoka sehemu mbalimbali za nchi na duniani kote ikiwa lengo kuu ni kuboresha afya kupitia tafiti," amesema Prof. Pembe. Amesema kauli mbiu ya Kongamano hili ni “Uimarishaji wa Uchumi wa Viwanda kupitia Tafiti za Afya kwenye nchi zenye kipato cha chini”.

Kauli mbiu hiyo imechaguliwa mahususi kusisitiza umuhimu wa matumizi ya matokeo ya tafiti za kisayansi za afya katika kuchangia uimarishaji wa uchumi wa viwanda hapa Tanzania na chi nyingine zenye uchumi wa kipato cha chini. Amesema hiyo ni kutokana na ukweli kuwa ili kuimarisha uchumi wenye viwanda Taifa linatakiwa kuwa na majibu ya changamoto zinazokabili sekta ya afya na kuboresha ukuaji wa uchumi. Ametaja kuwa katika kongamano hilo makala za kisayansi 164 zitawasilishwa kwa njia ya maongezi (Oral Presentations).

Amesema makala zitakazowakilishwa zimeangukia katika mada ndogo ndogo zifuatazo: Tafiti za Afya ya Uzazi,Tafiti wa Magonjwa yasiyoambukiza, Tafiti wa Magonjwa yanayoambukiza,Utafiti wa Msingi katika Maswala ya Afya, Tafiti za Sera na Mifumo ya Afya, Tafiti za Teknolojia ya Habari mawasiliano pamoja na Afya, Tafiti za Afya ya Kinywa, Tafiti za Tiba Asili na Tiba Mbadala, Huduma za Dawa za Tiba,Tafiti za Maswala ya Jinsia na Afya.

Amesema jumla ya washiriki na wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchini na nje ya nchi kutoka nchi za Rwanda, Uingreza, Japan, Uturuki, Itali na Marekani. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrea Pembe akizungumza na Waandishi wa habarai kuhusu Kongamano lake la sita la Kisayansi tarehe 2 na 3 Julai 2018. Kongamano hili litafanyika katika ukumbi wa LAPF Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ofisa Uhusiano wa Muhas akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu Mkutano huo utakaoanza jumatatu.

Unesco wakabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali

$
0
0
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamekabidhi rasmi kijiji cha digitali cha Ololosokwan katika sherehe kubwa iliyofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Katika kukabidhiana huko Unesco imesema kwamba itaendelea kutoa msaada katika mtandao wa intaneti kwa miezi sita ijayo.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Dk. Abdul Rahman Lamin, Ofisa msimamizi wa ofisi ya Unesco, Ann Therese Ndong-Jatta alisema kwamba wakati wanakabidhi facility hizo wamefurahishwa na ushirikiano mkubwa waliopewa katika mradi huo.

Kijiji cha digitali cha Ololosokwan ni moja ya vijiji vinne ambavyo vimefadhiliwa huku vikitoa huduma muhimu za elimu, afya na biashara kuendeshwa kidigitali.Kijiji hicho cha digitali ambacho ni matokeo ya ushirikiano kati ya UNESCO na kampuni ya Samsung imelenga kutoa elimu kwa kutumia njia ya mtandao, kufaniklisha tiba mtandao na pia kutumia mtandao wa kompyuta katika kuwezesha biashara.

Ofisa huyo alisema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano uliopo ili mradi uweze kuendelea kuchangia maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Aidha aliitaka serikali kuhakikisha kwamba inaendeleza ushawishi kwa wananchi wa eneo hilo la Ngorongoro kutumia vyema teknolojia ya kisasa katika kufanikisha maisha endelevu ya zana zilizopo.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akizungumza na wananachi wa kijiji cha Ololosokwan pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Abudl Rahman Lamin (wa tatu kushoto) akimwakilisha Ann Therese Ndong’ Jatta, Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki akimkabidhi rasmi ripoti ya mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa tatu kulia) kwa ajili ya uendelezaji baada ya majaribio wakati wa hafla iliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. 

Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (waliosimama kwa nyuma), Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (wa pili kushoto), Diwani wa kata ya Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ololosokwan, John Pyando (kulia).
 Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA  HAPA

KATIBU MKUU WA CCM BASHIRU ALLY AMTAKA MFANYABIASHARA JIJINI DODOMA KUREJESHA ENEO LA CCM ANALODAIWA KULIHODHI KWA MIAKA MINGI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk. Bashiru Ally amemtaka mfanyabiasha aliyetajwa kwa jina moja la Deogratius wa jijini hapa, kurejesha kwa hiari yake eneo la CCM ambalo anadaiwa kulihodhi kwa miaka kadhaa sasa katika Kata  ya Makutupola wilaya ya Dodoma Mjini ambalo amekujenga ukumbi na fremu kadhaa za maduka.
Dk. Bashiru ametoa agizo hilo kwa mfanya biashara huyo jana alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika Kata ya Nakutupola jijini hapa.Amesema amefikia uamuzi huo kwa sababu mfanyabiashara huyo ameonekana kutokuwa na uaminifu wa kutosha kwa kuwa hivi karibuni alizungumza nae ofisini kwake na kuahidi kukutana ili kufanya makabidhiano ya eneo hilo kwa sherehe na nderemo kwenye kikao hicho.

"Cha kushangaza juzi akikuja mwenyewe ofisini kwangu tukaxungumza kwa muda wa saa mbili tukakubaliana leo aje kwenye kikao hiki kukabidhi eneo letu kwa sherehe na ndelemo lakini leo nimempigia hadi simu akasema eti ameenda Dar es Salaam kushughulika na masuala ya mwanae, sasa  endeleeni na mazungumzo  na utaratibu wa makabidhiano akabidhi kwa hiari eneo letu", alisema Dk Bashiru

Dk. Bashiru aliwataka wanachama na viongozi wa CCM kutofanya vurugu za aina yoyote kwa Mfanya biashara huyo na kusema Mchakato uliotumika kurejesha ukumbi ndio utakaotumika kurejesha eneo lote la  Chama na mali yote iliyopo kwenye eneo la hilo ni mali ya CCM.

Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally amewapokea Winston Edward Katibu Kata hiyo wa CUF na Baraka Tayara Katibu kata wa Chadema pamoja na wanachama 181 kutoka vyama hivyo. Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akipokelewa na Viongozi mbali mbali alipowasili kata ya Makutupola wilaya ya Dodoma mjini jana Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwapungia Mkono kikundi cha ngoma Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM na Jumuiya zake wa Kata ya Makutupola jana.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali inatarajia kuzindua muongozo wa Uendeshaji Viwanda nchini Julai 2

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

SERIKALI imesema katika kukuza biashara nchini imesema inatarajia kuzindua Muongozo wa Uendeshaji Viwanda nchini Julai 2, mwaka huu kupitia Serikali Mitaa ili kutekeleza lengo la ufufuaji na uendeshaji viwanda nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika VIwanja vya Maonyesho ya 42 Sabasaba, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante Ole Gabriel, amesema tayari Serikali imeridhia uanzishwaji wa mchakato huo.

Alisema tayari mikakati mbalimbali inaandaliwa kuhakikisha mkakati huo unakua endelevu.Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda na ili kufikia malengo tutazindua mpango huu,"alisema Gabriel.Profesa Ole Gabriel sema kauli mbiu ya Maonyesho ya Sabasaba mwaka huu ni ukuzaji Biashara kwa ajili ya maendeleo ya Viwanda.

Gabriel alisema, kauli mbiu hiyo imeteuliwa kwa lengo kukuza uchumi wa viwanda hapa nchini.Amesema unapoangalia uchumi wa viwanda ni lazima uangalie bidhaa zinazouzwa ndani ya nchi," alisema Gabriel.Alisema Serikali ya awamu ya Tano imejidhatiti kuweka uchumi wa viwanda hivyo ni wajibu kwa kila taasisi itengeneze bidhaa bora itakayoingia katika uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (Tantrade), Edwin Rutageruka, alisema wanakuza biashara ili kupata kodi, ajira na kukuza viwanda nchini.Amesema maonyesho ya mwaka huu, yatafunguliwa Julai 2, ambapo hadi hivi sasa tayari wageni 33 wametoka nje ya nchi na washiriki wa ndani ni 2,956 na taasisi za Serikali 127.

"Tunashukuru kwa mwaka huu washiriki wa nje wameongezeka kwa mwaka jana walikuwepo 30,"alisema Rutageruka 
katibu MkuuTIBU Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Olisante Ole Gabriel, akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Shirika Simu Tanzania (TTCL) Rachael Mremi kuhusu huduma ya 4G wakati alipotembelea banda la shirika hilo, katika Maonyesho ya 42 ya ya Kimataifa ya Biashara, viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, B, Dar es salaam.

JARIDA LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII - JAN-JUNE, 2018

TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limezindua treni ya mizigo kuelekea nchini Uganda ikiwa imebeba shehena ya mzigo wa tani 2,400 wa Shirika la Chakula Duniani (WFP).

Kubebwa kwa shehena hiyo ya mizigo kwenye treni kumenusuru takribani dola 96,000 sawa na Sh.211,200,000 za gharama ya usafirishaji.

Treni hiyo iliyoanza safari leo imezinduliwa na Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji Focus Makoye Sahani na kueleza utekelezaji huo ni maagizo ya Rais wa  Dkt John Magufuli kwa Wakurugenzi wa Shirika la Reli na mamlaka ya bandari kuhakikisha treni ya mizigo inafanya kazi akiwa katika ziara ya kikazi nchini Uganda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sahani amesema kuwa treni hii ya mizigo ilisimama toka Agosti mwaka 2009 wakiwa chini ya mwekezaji ila kwa juhudi zilizofanywa na mamlaka ya bandari na shirika la Reli limefanikisha kurejea kwa usafiri huo kuelekea nchini Uganda.

Sahani amesema kuwa, kwa mara ya hii ya kwanza wamepata ofa ya tani 2,400 toka kwa WFP utakuwa ni kwa treni tatu pia wanashukuru  kwani njia ya reli ni usafiri mzuri na wenye uhakika na wameweza kushirikiana na Shirika la Reli nchini Uganda na kufanikiwa kukarabati eneo la kilometa 9 kuelekea Kampala lililokuwa linasumbua.

"Tumeshirikiana na Shirika la Reli Uganda kufungua njia inayoelekea Kampala kwa kuwapatia vifaa vya kufungulia njia hiyo,"amesema Sahani.
Ameongeza  amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweza kupata vichwa vya treni vipya na vifaa vingine ambavyo vitaboresha huduma zao za usafirshaji kuanzia sasa.

Mkuu wa Usafirishaji wa WFP Muhamad Mabuyu amesema kuwa wameokoa dola 40 kwa kila tani ambapo thamani yake ni zaidi ya milioni 211 za kitanzania kama wangetumia usafiri wa njia ya barabara, na hiyo hela kwa sasa itatumika kununulia mahitaji mengine kwa ajili ya wahanga mbalimbali.
Mabuyu amesema, treni hiyo ya mizigo itatoka kuanzia katika hifadhi yao ya chakula bandarini Dar es Salaam na itafika moja kwa moja katika hifadhi yao ya nchini Uganda katika Jiji la Kampala.

"Tumeweza kutumia usafiri wa njia ya reli kwani ni rahisi na wenye uhakika kwakuwa mwaka 2017 tulisafirisha tani 16,000 kuelekea Mkoani Dodoma na haikupotea hata kiroba kimoja cha kilo 50,"amesema. 
Mabuyu amesema,mbali na tani hizo zinazoelekea Kampala, kuna tani zingine 15,000 zinaanza kuingia kesho ambazo pia tutatumia usafiri wa njia ya reli kuzisafirisha na iwapo wangetumia magari ya tani 30 wangeingia gharama kubwa sana ya magari 500 ila watatumia treni 19 kufikisha mzigo huo .

WFP wamesifia huduma za TRC na kueleza yeye kama mdau wa usafirishaji anaupongeza  uongozi wa TRC na Serikali kwa ujumla kwa kufanikisha huduma hiyo ya njia ya reli kurudi ikiwa ni baada ya miaka 10.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Focus Makoye Sahani akizindua treni ya mizigo na kuashiria kuanza kwa huduma hiyo baada ya kusimama kwa kipindi cha miaka 10.
Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Makoye Sahani akizungumza na waandishi wa habari kabla kuzindua treni ya mzigo kuelekea nchini Uganda ikiwa ni baada ya miaka 10 toka kusitishwa kwa huduma hiyo ya usafirishaji.
Mkuu wa Usafirishaji wa Shirika la Chakula Duniani Nchini Tanzania (WFP) Muhamad Mabuyu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea ubora na ufanisi mzuri wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika ufanisi wa usafishaji mizigo wakati wa uzinduzi wa treni ya mizigo kuelekea Nchini Uganda.

WAZIRI LUKUVI KUONGOZA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHELTER AFRIQUE - KENYA

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi amekutana na viongozi wakuu wa Kampuni ya kuwezesha upatikanaji wa nyumba za bei nafuu – Shelter Afrique jijini Dar es Salaam.

Waziri Lukuvi alikutana na viongozi hao kwa kikao maalum ofisini kwake – Dar es Salaam. Viongozi hao ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo; Bwn. Femi Adowele na Katibu wake; Francesca Kakooza.Aidha, Suala mahususi lililowakutanisha viongozi hao lilikuwa ni kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 37 wa Kampuni hiyo unaotegemewa kufanyika hivi karibuni nchini Kenya, ambapo Waziri Lukuvi ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi wanachama, ambazo ni kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Shelter Afrique imedhamiria kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya Nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maisha bora ya watu.

Mambo mbalimbali katika sekta ya Nyumba yanatarajiwa kuzungumziwa katika Mkutano huo wa 37, hususan katika jitihada za kupatikana kwa makazi bora na nafuu katika nchi wanachama, ambapo changamoto Kuu imekuwa ni Rasilimali fedha.Tanzania ni nchi mojawapo Mwanachama wa Shelter Afrique kati ya nchi 44 za barani Afrika .

Tanzania ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32 ambao ulifanyika N’djamena, Chad 2013, uliopitishwa na Azimio Namba GM/ 2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa Kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika. 

Mkutano wa mwaka huu wa 37, unategemewa kufanyika Nairobi, Julai 20, 2018.

Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Waogeleaji wa Bluefins kushiriki mashindano ya Kenya

$
0
0
Jumla ya waogeleaji 11 wa klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins watashiriki mashindano ya Mombasa yaliyopangwa kuanza leo.

Mashindano hayo ya kimataifa, yanashirikisha waogeleaji mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki na klabu hiyo ndiyo pekee inayoiwakilisha nchi.

Muasisi na kocha mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja wachezaji ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano hayo kuwa ni Aminaz Kachra, Lina Goyayi, Muskan Gaikwad na Aliyana Kachra ambao ni wanawake.

Waogeleaji wa kiume ni Delbert Ipilinga, Christian Fernandes, Parth Motichand, Isaac  Mukani, Sahal Harunani, Aaron Akwenda na Hassan Harunani.
Alisema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo pamoja na kushiriki kwa mara ya kwanza katika historia.

“Haya ni mashindano yetu ya kwanza ya nje ya nchi tokea klabu yetu ianzishwe, na tumeamua kufanya hivi baada ya kupata mafanikio makubwa sana katika michezo ya ndani kwa kushika nafasi ya pili na ya tatu, tumeona kuwa ni wakati sasa kwa waogeleaji wetu kuvuka mipaka ya nchi na kupima uwezo wao,” alisema Alidina.

Alifafanua kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo ili kuiletea sifa Tanzania.
“Napenda kuishukuru BMT na Kamati ya Muda ya chama cha kuogelea nchini kwa kutupa msaada mkubwa pamoja na vibali, tumefarijika sana na tunahidi kuleta ushindi katika mashindano hayo,” alisema Alidina.

CERA yafika Tanzania

$
0
0
Dar es Salaam: CERA Sanitaryware, chapa inayokua kwa kasi imezinduliwa kwenye hoteli ya Ramada Encore jijini Dar es salaam hivi karibuni. CERA inashirikiana na Imports International(T)Ltd (IIL), wadau wao nchini kwa ajili ya usambazaji, huduma kwa wateja na kujenga chapa ya CERA nchini Tanzania. Imports International (T) Ltd –IIL – imebobea na inajulikana kwa kuleta mafanikio makubwa katika kuwakilisha bidhaa za kifahari za kimataifa hapa nchini kupitia maadili mazuri ya ufanyaji biashara na huduma bora kwa wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa IIL Bw. Trushal Jethwa ni mtu mwenye maono mazuri na ana dhamira ya dhati ya kutoa mchango mkubwa kuboresha ufanisi katika sekta ya ujenzi kwa kuleta bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kimataifa, nchini Tanzania. Tokea mwaka 2004, IIL imejikita katika usambazaji wa bidhaa bora zinazofaamika kimatafika kutoka Makampuni mbalimbali duniani kama Saint Gobain, Gyproc, Weber, ISOVER, Insutech n.k.

Cera Sanitaryware Limited, kampuniya vifaa vya bafuni inayokua kwa kasi India, imekuwa mstari wa mbele katika ubunifu tangu uanzilishi wake manmo mwaka 1980. CERA imeweza kunyakua tunzo mbalimbali kwenye sekta ya ujenzi. Pia, imefanikiwa kushinda tunzo ya “Bidhaa Bora Ya Mwaka” kwa miaka 4 mfululizo katika maudhui ya ubunifu. Sio hivyo tu, CERA imetunukiwa “Chapa Inayoaminika na wateja” katika utafiti uliofanywa na gazeti la Reader’s Digest. Katika soko la Indiam wateja wameitunuku CERA na tunzo ya “Power Brand” .

Kampuni ya CERA inahesabika kati ya chapa kubwa za bara la Asia. CERA pia ipo kati ya chapa 100 zenye tuzo ya “Architecture & Design”. Pamoja na hayo, CERA pia inajulikana kwa teknolojia ya “green”, ambayo inajali mazingira, katika utengenezaji wa bidhaa zao zote. Ina mkusanyiko kubwa ya bidhaa zinatomia matumizi madogo ya maji. Kampuni ya CERA ina uwepo katika nchi 38, ndani ya mabara 4, na hakika hii huifanya kuwa kampuni ya kimataifa inayofikia kila kiwango kilichwekwa kwa ajili ya vifaa vya bafuni.

Bw. Dilip Thakkar, Meneja Mkuu (Export) wa Cera Sanitaryware Limited alikuwepo kwenye uzinduzi huo kukutana na wasanifu, washauri, wadau wa ujenzi. Alielieza kuhusu maono yake ya chapa ya CERA barani Africa – hasa nchini Tanzania. Aliongelea pia kuhusu kufungua showroom ya CERA katika jengo kuu la IIL iliyopo barabara ya Nelson Mandela karibu na Wiazara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo itakua suluhisho la wateja wote na kuongeza matarajio ya watanzania kujipatia mabafu yenye ubora zaidi.

Bidhaa zote za CERA, yaani vyoo na bafu, mabomba, vigae, mabeseni ya kunawia n.k. vitakuwepo kwenye showroom ambayo itafunguliwa saa 3 asubuhi hadi saa 11 na nusu jioni kutoka Jumatatu hadi Ijumaa and saa 3 na nusu asubuhi hadi saa 8 na nusu mchana kwa siku ya Jumamosi.
Kwenye tukio hili, Bw. Zaheer ambaye ni meneja wa CERA Tanzania na soko la Afrika, alishukuru wageni wote waliokuwepo na kuahidi kwamba yeye na timu yake watahakikisha wateja wote wataridhika kwa 100% na bidhaa zote za CERA.

BENKI YA CRDB YADHAMINI MKUTANO WA MAKANDARASI JIJINI DODOMA

$
0
0
Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulikia wateja wakubwa na taasisi, Jane Ikira, akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, alipotembelea banda la benki hiyo. Katikati ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo anayeshughulikia wateja wakubwa na taasisi, Shima Danford.
Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulikia wateja wakubwa na taasisi, Shima Danford (katikati), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika banda lao wakati wa mkutano wa mashauriano na wadau na maonyesho ya bidhaa na huduma za ujenzi yanayofanyika mkoani Dodoma.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la LAPF-Dodoma, Martha Ngwenya, akipeana mkono na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, alipotembelea banda la benki hiyo.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Nasibu Kalamba (kushoto), akielezea juu ya huduma na bidhaa zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kulia).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RC TABORA KUPAMBANA NA WACHOMAJI MOTO MISTU

$
0
0

WATENDAJI wa ngazi mbalimbali Mkoani Tabora wameagiza kuanza zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu ambao wamekuwa na tabia ya kuchoma moto ovyo wakati wa maandalizi ya mashamba na wengine kwa ajili ya kutaka nyasi ziote upya kwa ajili ya mifugo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey MwanriMwanri alitoa kauli hiyo jana Wilayani Uyui wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Kakola na Msimba akiwa katika kampeni ya kuhimiza wananchi kujiunga na Ushirika na kupinga vita utoro na mimba za utotoni.

Alisema hivi sasa kumeibuka tabia ya watu kuanza kuchoma ovyo moto ambao umekuwa ukisababisha hasara kubwa katika mistu na hata kuunguza miti iliyopandwa hivi karibuni.

Mwanri alisema kuanza ni marufuku kuandaa mashamba yao kwa kuchoma moto kwani wamekuwa wakiuacha na kusambaa maeneo mengine na hivyo kuleta athari katika mistu ya asili na viumbe wengine.

Aliwataka wananchi na wakulima mkoani humo kuandaa mashamba kwa njia ya kisasa bila kuathiri mazingira pamoja na viumbe hai wengine hatua ambayo itawezesha kutunza na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Katika kukabiliana na tabia hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo  amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kwamba wanawachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kufanya uharibifu huo kwa kuwa haiwezekani mtu akachoma moto asijulikane .

Alisema katika kijiji au Kata ambayo atakuta watu wamechoma moto na umeteketeza miti iwe ya kupanda au asili kiongozi huyo atawajibika kwa kushindwa kusimamia sheria.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa misitu mingi ya asili na miti mingi iliyopandwa katika kipindi cha mvua za masika ipo hatarini kutokana na baadhi ya watu ambao wameanza kuchoma ovyo mistu. 

Alitaja sababu  kubwa ya uchomaji moto huu wengine ni kwa sababu ya uvivu wa kuandaa mashamba yao  kwa kupalilia na wengine kuadai kuwa wanapochoma moto wanapata malisho mapya ya mifugo jambo ambao sio rafiki kwa mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwahotubia wakazi wa Kijiji cha Msimba wilayani Uyui wakati akiwa anendelea na kampeni jana katika vijiji mbalimbali ya kusisitiza vita dhidi ya  utoro na mimba za utotoni na uchomaji moto ovyo mistu mkoani humo.Picha na Tiganya Vincent


JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI ZAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

$
0
0
Jumuiya za Watumia Maji nchini zimeaswa kufanya kazi kwa uadilifu ili kuweza kulinda na kuhifadhi rasilimali za maji kwa ajili ya manufaa ya taifa katika warsha ya siku mbili iliyoshirikisha Jumuiya za Watumia Maji zinazotoka kwenye mabonde matano ya Pangani, Wami-Ruvu, Rukwa, Ruvuma na Rufiji iliyoandaliwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo IWaSP-GIZ, UNDP, WWF, IUCN, 2030 WRG, SNV, Shahidi wa Maji, Waridi na mashirika mengine.

Warsha hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Salinero, mkoani Kilimanjaro ilishirikisha viongozi wa jumuiya hizo na maafisa Maendeleo wa Jamii, ambao kimsingi ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha ufanisi katika usimamizi wa rasilimali maji kwenye ngazi ya jamii, ililenga kufikia makubaliano ya pamoja kwenye masuala muhimu yatakayowezesha kupata ufumbuzi wa pamoja wa changamoto mbalimbali zinazozikabili jumuiya za watumia maji, na kutoa fursa kwa wadau kujadiliana na kupeana uzoefu kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo katika maeneo ya utendaji kazi ya jumuiya hizo.

Akizungumza katika kuhitimisha warsha hiyo mwakilishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhaidrolojia Mkuu, Bernad Chikarabani amesema kuwa wizara inawashukuru wadau wa maendeleo kwa mchango mkubwa katika kutunza na kuhifadhi rasilimali za maji nchini kwani mafanikio ya jambo hilo yanahitaji ushirikiano na wadau wote na si la wizara pekee.

Vilevile, aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kutengeneza mwongozo utakaosaidia jumuiya kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, lakini pia utaisaidia wizara kupata maoni kutoka kwa wahusika kwenye ngazi ya jamii na kuyaingiza katika sera na miongozo mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za maji na jinsi ya kuimarisha jumuiya hizo.

Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii toka Bonde la Pangani, Patrice Otieno amesema warsha hiyo imelenga kubadilishana uzoefu kwa lengo la kutatua changamoto zinazozikabili jumuiya hizo ambazo zimetofautiana kulingana na maeneo husika. Huku akisisitiza nia ya Serikali ni kuona jumuiya hizo zikiimarika na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili  rasilimali za maji zitunzwe na kunufaisha taifa kwa miaka mingi ijayo.

Baadhi ya matokeo ya msingi yatayotokana na warsha hiyo ni pamoja na uandaaji wa mpango kazi wa utekelezaji kitaifa iliyoshirikisha wadau wa maendeleo na pia mipango kazi katika ngazi za Jumuiya za Watumia Maji ambayo itatoa fursa katika kuandaa miongozo ya uundwaji na utendaji kazi wa Jumuiya za Watumia Maji.

Uundwaaji wa Jumuiya za Watumia Maji ni matokeo ya ushirikiano baina ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika maeneo mbalimbali ya usimamizi wa rasilimali za maji. Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na kuzipatia jumuiya hizo mafunzo mbalimbali na vitendea kazi pamoja na kuandaa warsha na majukwaa ya kubadilishana uzoefu. 
 Mwakilishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhaidrolojia Mkuu, Bernad Chikarabani akizungumza na washiriki katika warsha ya siku mbili iliyoshirikisha Jumuiya za Watumia Maji zinazotoka kwenye mabonde matano ya Pangani, Wami-Ruvu, Rukwa, Ruvuma na Rufiji 
 Mmoja wa wawezeshaji akitoa mada kwa washiriki katika warsha ya siku mbili iliyoshirikisha Jumuiya za Watumia Maji zinazotoka kwenye mabonde matano ya Pangani, Wami-Ruvu, Rukwa, Ruvuma na Rufiji 
Washiriki wa warsha ya Jumuiya ya Watumia Maji wakiwa kwenye picha ya pamoja.

BALOZI WA KUWAIT ALIVYOADHIMISHA SIKU YA ALBINO DUNIANI

$
0
0
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (katikati waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana wenye Ualbino katika kushirikiana nao kuadhimisha siku albino duniani 'International Albinism Awareness Day 2018' iliyofanyika hivi karibuni. Balozi huyo alikula nao chakula vijana hao katika kituo cha TYPF  kilichopo Upanga, jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya Humanity Action for Children iliyo chini ya Mama Shamim Khan (wa tatu kulia waliosimama).
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem akiwapatia zawadi mbalimbali vijana hao wenye ualbino ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku albino duniani 'International Albinism Awareness Day 2018' iliyofanyika hivi karibuni. kushoto kwake ni Muanzilishi wa Taasisi ya Humanity Action for Children, Mama Shamim Khan. 


MSIMU WA SABASABA 2018 UMEWADIA, MAONESHO YAMEANZA TOKEA JANA

Tigo yatoa ofa murwa kwa simu janja za kisasa zenye vifurushi vya intaneti katika maonesho ya sabasaba

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipotangaza kuwa kwa mwaka wa tatu mfululizo, Tigo ndio mdhamini mkuu wa mawasiliano katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) ambayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade). Kushoto ni Meneja wa Ukuzaji wa Biashara wa Tantrade, Stephen Koberou.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo ndio mdhamini mkuu wa mawasiliano katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) ambayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji wa Biashara Tanzania (Tantrade). Kauli mbiu ya maonesho hayo almaarufu Sabasaba yanayofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2018 ni ‘Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda’.

Akitambulisha udhamini huo jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Tigo kudhamini maonesho hayo. Ushirikiano huu ni sehemu mojawapo ya azma ya Tigo kuchangia juhudi za serikali kukuza biashara kama njia mojawapo ya kukuza uchumi wa viwanda nchini.

‘Tigo inatambua kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi za Afrika ambapo uchumi wake unakua kwa kasi ya juu na kuwa bado kuna fursa nyingi zinazopatikana nchini. Kila mwaka kwa kipindi cha miaka 42 sasa, Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya Biashara (DITF) yamekuwa chachu kubwa ya kukuza uchumi wa viwanda kwani yanatoa fursa kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wa kati kuonesha ubunifu katika bidhaa na huduma, pamoja na teknologia mpya kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Vilevile, Sabasaba ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwani inatoa fursa za ajira na mapato kwa sekta tofauti,’ Woinde alisema.

Aliwahamasisha Watanzania kujiandaa kupokea ofa kabambe za simu janja za kisasa zenye ofa murua za vifurushi vya intaneti kwa kipindi cha hadi miezi sita kutoka Tigo. ‘Tumeingia ubia na watengenezaji wakubwa wa simu duniani kama vile Tecno, Samsung, Nokia na Freetel kuhakikisha kuwa wateja na wananchi watakaofika katika viwanja vya Sabasaba, Dar es salaam au katika maduka yote ya Tigo nchi nzima wanafaidika na simu janja kwa bei nafuu kuanzia TSH 69,000 pekee katika msimu huu wa Sabasaba.’

Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Biashara wa Tantrade, Stephen Koberou aliwashukuru Tigo kwa kuchukua jukumu la kuthamini maonesho ya mwaka huu ya Sabasaba ili kukuza biashara. Pia aliwahamasisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili waweze kujionea ubunifu na teknologia mpya, kujifunza, kujenga mahusiano mapya ya kibiashara pamoja na kuwa sehemu ya fursa kubwa zaidi ya kufanya manunuzi na kupata huduma muhimu kwa bei nafuu.

‘Maandalizi yako tayari na nawakaribisha wafanyabiashara wote kujitokeza kwa wingi kuunga mkono wafanyabiashara wenzao wa ndani na nje ya nchi ambao wameleta bidhaa na huduma zao katika maonesho ya mwaka huu, huku wakipata fursa ya kujionea hatua kubwa tulizopiga katika kukuza uchumi wa viwanda nchini,’ alisema.

Sabasaba imejizolea umaarufu kama maonesho yanayoongoza nchini kwa kuvutia mamia ya wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na maelfu ya wageni wanaovutiwa na bidhaa bora na bei nafuu zinazopatikana katika maeonesho hayo.

Kazi ya kiongozi ni kujua matatizo ya wananchi- Diwani Nuru Awadh

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala , Nuru Awadh amesema kuwa kazi ya kiongozi ni kujua matatizo ya wananchi na sio kujifungia kwa kizingizio uchaguzi ulishapita huku wanancho wakiwa na kero ambazo zinakosa majibu kutoka kwa watendaji.

Diwani huyo ameyasema hayo wakati mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Buguruni, amesema kuwa masuala yaliyoibuka kutoka kwa wananchi kuhusiana na uzoaji taka na sungusungu kuwanyanyasa wananchi kuhakikisha yanapatiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa wananchi wanakabiliwa na changamoto lakini bila ya watendaji kushughulikia yanafanya wananchi kukosa sehemu ya kusemea kutokana na viongozi kutoitisha mikutano ya hadhara ya kujua matatizo ya wananchi.

Awadh amesema kuwa seriikali inatambua watu wenye ulemavu akiwa nay eye kuwa mwenye ulemavu wa kuona hivyo kwa watu wenye ulemavu katika kata hiyo waendelee kuwa na imani na serikali kutokana n mipango iliyowekwa kwao.

Nae Diwani wa Kata ya Buguruni, Adam Fugame amesema kuwa diwani wa viti maalum amekuwa na udhubutu kwa kuamua kufanya mkutano wa hadhara wa wananchi.

Amesema kuwa matatizo yaliyoibuka watendaji wafuatilie na kupata ufumbuzi ili kuwafanya wanachi kuondokana na  kero.
 Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Ilala, Nuru Awadh akizungumza katika Mkutano wa hadhara aliouandaa kwa ajili ya kusikiliza changamoto za wananchi wa kata ya Buguruni uliofanyika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo.
 Diwani wa Kata  ya Buguruni, Adam Fugame akizungumza na wananchi wa Buguruni katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo.
 Mwananchi wa Kata ya Buguruni, Siasa Ramadhan akiuliza kuhusiana na walemavu kubaguliwa kufanya biashara katika maeneo ya vituo vya daladala.
 Mwananchi wa Kata ya Buguruni, Sijali Salum akiuliza kuhusiana na walemavu kuhusiana na watu kwenda kuchukua taarifa zao lakini hakuna matokeo na taarifa zinazochukuliwa.

Wananchi wakimsikiliz Diwani wa Viti Maalum, Nuru Awadh katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ofisi ya Mtendaji kata ya Buguruni.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images