Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

NHIF YAWAHAMASISHA WANAUSHIRIKA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA

$
0
0


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga(NHIF) umewahamasisha wanaushirika mkoani Tanga kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kupata kadi za matibabu ambazo wanaweza kunufaika na huduma ya matibabu nchini nzima kwani bila afya imara mipango wanayopanga inaweza kushindwa kufanyika kwa ufanisi mkubwa. 

Uhamaishaji huo ulifanywa na Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi. 

Alisema bila wana ushirika hao kuwa na afya imara mipango yao wanayopanga itashindwa kufanikiwa kwa sababu wanapokuwa wakiungua wanaweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha nyingi kuweza kujitibu lakini wanapokuwa kwenye mpango huo wataweza kupata matibabu kwa gharama nafuu. “Lakini niwaambie kuwa mkijiunga na mpango wa ushirika mnaweza kunufaika na huduma za matibabu nchi nzima lakini pia utawawezesha kuweza kuwa na uhakika wa matibabu wakato wote bila kujali kama utakuwa na fedha wakati unapougua “Alisema. 

Alisema mpango wa ushirika afya ni mpango maalumu unaomuwezesha wana ushirika kwa umoja wao kuchangia huduma za matibabu kabla ya mwanachama kupata majanga yakiwemo maradhi,kuunguliwa au magonjwa mbalimbali wakati wakiendelea na shughuli zao. Hata hivyo aliwataka wanaushirika hao kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye mpango huo ili kuweza kupata huduma za matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali ambayo yanaweza kuwapelekea kushindwa kutekeleza wajibu wao kama ilivyokuwa awali. 

“Ndugu zangu niwaambieni bima ya afya ndio mambo yote bila kuwa na afya imara mipango tunayopanga haiwezi kukamilika hivyo niwaase tujiunge na mpango huo wa Ushirika Afya ambao ni mpango maalumu unaowawezesha kuchangia huduma za matibabu kabla ya kupata majanga”Alisema.
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia Kaku akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi. 

KAA TAYARI KWA TAMASHA LA ASAS MTOTO DAY OUT VIWANJA VYA POSTA

TANZANIA NI KIMBILIO KWA WALIOKOSA AMANI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuvumiliana na kustahamiliana ndiko kunakolifanya Taifa la Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao. 

Kadhalika, uwepo wa amani nchini si tu unatoa fursa ya kutekeleza majukumu ya kiuchumi na kijamii bila hofu bali pia ni sababu muhimu ya wenzetu wengine kutoka nje kuona fursa ya kuwekeza na kushirikiana nasi katika kujenga maendeleo ya nchini. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 28, 2018) wakati akizindua Umoja wa Kimataifa wa  Wabunge Wapenda Amani tawi la Tanzania (IAPP), kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni, jijini Dodoma.

Amesema amani na utulivu ni tunu kubwa sana katika jamii yoyote ile Duniani na Tanzania muda wote imeendelea kuenzi tunu hiyo iliyojengwa kwenye misingi imara kupitia waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu Shirikisho la Amani kwa Wote  (Universal Peace Federation (UPF), ambalo lilianzishwa kwa lengo la kumkomboa binadamu kutoka katika udhalili wa kukosa mahitaji muhimu. 

“Hili linadhihirika kupitia mipango ya shirikisho hilo ya kushirikiana na jamii nyingine katika kuimarisha sekta zenye kugusa maisha ya watu wengi kama vile kilimo, mazingira, afya, elimu, miundombinu na nyinginezo,” amesema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa tuzo ya Balozi wa Amani na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mbunge wa Tabora Mussa Ntimizi katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018 katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh, katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NSSF YAKABIDHI MASHINE 12 ZA KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KATIKA HOSPITALI YA TEMEKE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam limetoa mashine za kupima shinikizo la damu 12 zenye thamani ya Sh.5,000,000 kwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa lengo la kuboresha utoaji huduma hospitali hapo.

NSSF imesema vifaa tiba hivyo vitatumika kwa Watanzania wote watakaofika kupata tiba Hospitali ya Wilaya ya Temeke.Pia vitatumika kutoa huduma kwa wanachama wao wapatao 4000 ambao wanatibiwa hapo.

Akizungumza leo katika hosptali hiyo baada ya kukabidhi mashine hizo Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke Barnabas Ndunguru amesema wametoa msaada huo kutokana na maombi ya hospitali hiyo.

Pia amesema msaada huo ni moja ya jukumu la NSSF katika kurudisha fadhila kwa jamii ikiwa ni jitihada za kuisaidia Serikali katika juhudi za kuboresha sekta ya afya nchini.

Amefafanua NSSF Mkoa wa Temeke idadi ya wanachama wake wanaopatiwa huduma katika hospitali hiyo ni 4000 na kwa mwezi wanatoa fedha Sh.milioni 42 kwa ajili ya kulipia matibabu hayo."Hivyo tunaamini kutoa msaada huu wa BP Mobile Machine utasaidia katika kuwatibu wanachama wetu pamoja na wananchi wote ambao watakwenda kupata tiba,"amesisitiza.

Ameongeza msaada huo si mwisho na kuahidi kuendelea kusaidia kadri watakavyoweza kulingana na nafasi yao na kueleza wamekuwa wakisaidia jamii katika maeneo mbalimbali.Pia Ndunguru amesema NSSF wanalo fao la matibabu na kinachofurahisha zaidi wanachama wao wamekuwa wakipata huduma za afya za magonjwa yote isipokuwa TB na Ukimwi ambayo hayo huduma zake Serikali inatoa bure.

Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam Barnabas Ndunguru (wa pili kulia) akimkabidhi Ofisa Muuguzi wa Hosptali ya Temeke,Deodata Msoma vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi  milioni tano
Picha ya pamoja
Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam Barnabas Ndunguru (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi vifaatiba kwenye Hosptal ya Wilaya ya Temeke vyenye thamani ya shilingi Milioni tano .(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

SPIKA NDUGAI APOKEA TUZO YA BALOZI WA AMANI BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipewa tuzo ya Balozi wa amani na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge wapenda amani, Dkt. Thomas Walsh katika hafla ya kuzindua tawi la Wabunge wapenda amani iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson  (kushoto) akipewa tuzo ya Balozi wa amani na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge wapenda amani, Dkt. Thomas Walsh katika hafla ya kuzindua tawi la Wabunge wapenda amani iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge (hawapo kwenye picha) wakati wa hafla ya kuzindua tawi la Wabunge wapenda amani iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge wapenda amani, Dkt. Thomas Walsh, Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na Katibu Mkuu wa Chama cha Wapenda amani Duniani Afrika, Ndg. Adama Doumbia wakifuatilia video inayoelezea mambo mbali mbali yanayohusiana na amani katika tukio lililofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwa katika hafla ya kuzindua tawi la Wabunge wapenda amani iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Hafla hiyo Ilihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto), Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kulia), Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge wapenda amani, Dkt. Thomas Walsh (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya hafla ya kuzindua tawi la Wabunge wapenda amani iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati) akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge wapenda amani, Dkt. Thomas Walsh (kushoto) baada ya hafla ya kuzindua tawi la Wabunge wapenda amani iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai

(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

MAKANDARASI FANYENI KAZI KWA BIDII NA UADILIFU-KWANDIKWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amezungumzia umuhimu wa Makandarasi kuungana ili kupata miradi mingi inayotekelezwa na Serikali na hivyo kuwezesha fedha nyingi zinazopelekwa kwenye miradi kuwanufaisha makandarasi wazawa.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa mwaka wa siku mbili wa wakandarasi jijini Dodoma, Mhe. Kwandikwa amesema ni wakati sasa kwa wakandarasi kuwa waadilifu katika kutekeleza miradi ya Serikali ili kunufaika na upendeleo unaofanywa na Serikali kwa makandarasi wazawa.
“Tumieni wataalamu wenye weledi wa kutosha katika miradi mnayopewa na Serikali muijenge kwa ubora na kuikamilisha kwa wakati kulingana na mikataba ili kuiwezesha Serikali kuwaamini na kuwapa miradi mingi na mikubwa ya ujenzi makandarasi wazawa’, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Mhe. Kwandikwa amesema Serikali inaendelea kulipa madeni ya nyuma ya Wakandarasi na itaendelea kufanya hivyo ili kuhakikisha hali za uchumi kwa wakandarasi wazawa inaimarika na kumudu kujenga miradi mingi zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi Nchini (CRB) Eng. Consolata Ngimbwa ameiomba Serikali ifanye mabadiliko yatakayowezesha makandarasi wazawa kupata kazi nyingi zaidi hususani katika miradi mikubwa inayoendelea kujengwa Nchini.
Amesema hali za wakandarasi wengi kwa sasa si nzuri sababu hawapati miradi mingi ya kuwawezesha kufaidika na utekelezaji wa miradi hiyo hivyo ni wakati wa Serikali kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa ili kukuza uchumi na kuimarisha kampuni za wazawa kimtaji.
“Tunaomba Serikali itenge miradi mingi ya upendeleo kwa wakandarasi wazawa ili kuwajengea uwezo lakini kuwezesha fedha nyingi kubaki nchini” amesema Eng. Ngimbwa.
Naye Msajili wa bodi ya CRB, Bw. Reubeni Nkori amesema kwa sasa makandarasi wenyeji ambao ni wengi wanapate fedha chache kutoka kwenye miradi ya ujenzi inayoendelea nchini ikilinganishwa na wakandarasi wachache kutoka nje wanaopata fedha nyingi.
Mkutano wa mwaka wa siku mbili wa Makandarasi ulioanza leo jijini Dodoma unawakutanisha Makandarasi wote nchini kujadili na kujitathmini ukiongozwa na kauli mbiu isemayo “Ukuaji wa Makandarasi kwa uchumi endelevu, fursa na changamoto”.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Usajili Makandarasi (CRB), Eng. Light Chobya, kabla ya kufungua Mkutano wa mwaka wa siku mbili wa Bodi hiyo unaofanyika mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akifungua Mkutano wa mwaka wa siku mbili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), unaofanyika mjini Dodoma.
 Sehemu ya Makandarasi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa siku mbili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), hiyo unaofanyika mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati), katika picha ya pamoja na Makandarasi mara baada ya kufungua  Mkutano wao wa mwaka mjini Dodoma. Wa pili kulia waliokaa ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Eng. Joseph Nyamuhanga.

JAFO ATOA WITO KUSAIDIA WANAFUNZI WASIOJIWEZA ILI KUINUA ELIMU

$
0
0
Na. Zulfa Mfinanga na Fred Kibano,

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo, leo amekabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza wa shule ya msingi na sekondari za Kata ya Sejeli kijijini Mbande wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Msaada huo utanufaisha zaidi ya wanafunzi mia tisa ni pamoja na madaftari 9,000, kalamu 4,000, penseli 2,800, vifutio 1,200 na vichongeo 1,200 vyote vikiwa ni msaada kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Makao makuu kwa lengo la kuunga mkono Programu ya  “Nipekalamunadaftarinamiminisome” iliyozinduliwa mwezi Februari mwaka huu na Mhe Jafo ili kuwasaida wanafunzi wanaotoka katika familia duni.

Akikabidhi msaada huo katika shule ya sekondari Sejeli Mhe Jafo amesema licha ya kuwa serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu lakini gharama za vifaa vya shule pamoja na sare za shule zinatakiwa kugharamiwa na wazazi au walezi, hivyo baada ya kuona kuna changamoto ya kipato kwa baadhi ya familia ndio sababu pekee ya kuanzisha Programu hiyo.

“Leo wadau wameamua kurudisha fadhila kwa watoto ambao wazazi ama walezi wao hawana uwezo, hili jambo ni kubwa sana tena ni jambo la Ibada, nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwaombea, niwasihi watanzania wote waunge mkono jitihada hizo ili Sera ya Elimu Bila Malipo isaidie kuondoa tofauti kati ya wanaojiweza na wasio jiweza” Alisema Mhe Jafo.

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo alipokea msaada wa vifaa kama hivyo kutoka kwa Chama cha Umoja wa Waganga wa Tiba Asilia Tanzania (UWAWATA (T)) waliochangia madaftari elfu mbili, huku walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakichangia daftari 120, kalamu 115 na penseli 70 pamoja na ahadi ya daftari 4,400 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza kwa shule za msingi na sekondari Kata ya Sejeli wilayani Kongwa mkoani Dodoma leo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akitoa msaada kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kata ya Sejeli kama sehemu ya kampeni ya
Nipe kalamu na daftari na mimi nisome
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akipokea msaada wa daftari na penseli kutoka kwa wawakilishi wa walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo walichangia daftari 120, kalamu 115 na penseli 70
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jafo akiongea na walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) waliofika kijijini Mbande wilayani Kongwa Dodoma kuunga mkono kampeni ya nipe daftari na peni na mimi nisome.
Rosemary Chimya mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Sejeli kijiji cha Mbande akisalimiana na waziri Jafo baada ya kutoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo kwa msaada wa vifaa vya kusomea, ameiomba Serikali kuwajengea mabweni ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni pia kuwaongezea walimu wa masomo ya sayansi.

TANZANIA KUNUFAIKA NA VIPAUMBELE VYA MPANGO MKAKATI WA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO) KWA KIPINDI CHA MWAKA 2015-2019

$
0
0
Tanzania  kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeshiriki katika Mkutano wa Sabini wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization Executive Council WMO-EC 70) uliofanyika makao makuu ya Shirika hilo, Geneva nchini Uswisi kuanzia tarehe 20 hadi 29 Juni, 2018. 

Kupitia mkutano huo Tanzania imepata nafasi ya kushiriki katika kujadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Duniani sambamba na kutimiza makubaliano ya Kikanda na Kimataifa katika kukabiliana na athari zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. 
Akielezea manufaa yaliyopatikana katika mkutano huo, Dkt. Agnes Kijazi mjumbe wa kamati kuu akiwa miongoni mwa wajumbe 37 (wanaowakilisha Dunia nzima) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa  TMA  alisema masuala yanayojadiliwa ni sehemu ya Mpango Mkakati wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani na vipaumbele vyake katika kipindi cha mwaka 2015-2019 unaojumuisha utekelezaji wa programu za utoaji wa huduma bora zaidi za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for Climate Services (GFCS)”.

 Uboreshaji wa huduma za hali ya hewa kwa maeneo ya Dunia yenye barafu ya asili ikiwa ni pamoja na milima mirefu kama Kilimanjaro (Polar and High mountain regions)., utoaji wa tahadhari za mapema ili kukabiliana na maafa (Disaster Risk Reduction, Resilience and Prevention), uboreshaji wa huduma za usalama na usafiri wa anga (Aviation meteorological services), sambamba na  kujenga uwezo wa rasilimali watu na vitendea kazi hasa kwa nchi zinazoendelea na kuweka msisitizo katika tafiti za hali ya hewa. 

Vile vile Mkutano huu umejadili namna ya kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa kama njia ya kuboresha huduma za hali ya hewa kote duniani na kutatua changamoto za athari zitokanazo na matukio ya hali mbaya ya hewa hususani yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
‘Tanzania imeweza kunufaika mojamoja kupitia programu za utoaji wa huduma bora zaidi za hali ya hewa kwa jamii (Global Framework for Climate Services (GFCS)) ambapo Tanzania na Malawi ni miongoni  mwa nchi mbili barani Afrika zinazotekeleza program hiyo, Aidha  mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza umejumuishwa katika program ya kuboresha huduma za hali ya hewa kwa maeneo ya Dunia yenye barafu ya asili (Polar and High mountain regions)’, Alisema Dkt. Kijazi. 
Aidha, Dkt. Kijazi katika Mkutano huu amewasilisha ripoti ya Mkutano wa Jopo la Wataalamu wa Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani wanaoshughulikia mafunzo (WMO EC Panel of Experts on Education and Training) uliofanyika Nairobi, Kenya mwezi Aprili 2018. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), hivyo Dkt. Kijazi alimwakilisha Rais wa Shirika la Hali ya hewa Duniani akiwa Mwenyekiti wa Mkutano huo. Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais wa Shirika la Hali ya hewa Duniani alimshukuru Dkt. Kijazi kwa kumuwakilisha vema katika Mkutano huo.
Kupitia  Mkutano huo Balozi na Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Dkt. James Msekela alipata fursa ya kukutana na Katibu Mkuu wa WMO, Prof. Petteri Taalas na kufanya mazungumzo mafupi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusiana na uwakilishi wa Tanzania katika masuala ya hali ya hewa katika Shirika hilo na namna ya kuendelea kusaidia nchi zinazoendelea kama Tanzania katika kuboresha zaidi huduma za hali ya hewa kwa manufaa ya wananchi wote.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu Umoja wa Mataifa Balozi Dkt. James Alex Msekela(kushoto) na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Prof. Petteri Taalas.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,  Dkt. Agnes Kijazi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO Excecutive Council) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Sabini wa Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Excecutive Council-70) unaondelea, Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 20-29 Juni 2018.

Halotel, StarTimes waleta kombe la dunia kiganjani

$
0
0
Bando hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana.

Huku mshike mshike wa kombe la dunia ukiendelea kukolea, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel kwa kushirikiana na Kampuni ya StarTimes wameleta wamezindua huduma mpya itakayo wawezesha wateja wa mtandao huo kuangalia mechi za kombe la dunia kupitia simu zao za kiganjani kwa gharama nafuu.

Huduma hii itawawezesha wateja wa Halotel na StarTimes kutazama Soka kwenye simu zao kwa gharama nafuu sana, huduma hiyo inawapatia wateja intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda amesema huduma hiyo itawawezesha wateja wa Halotel nchini nzima kufurahia kutazama mechi za kombe la dunia kupitia simu za mikononi (Smartphone) kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwa kutumia intaneti ya uhakika tena yenye kasi kwa masaa 24 bila kikomo.

“Kuanzia sasa wateja wa Halotel wanaweza kupakua Application ya Startimes kupitia simu zao za Android na watalipia kuanzia shilingi 2000 na watapata GB 1 ambayo wanaweza kuitumia kuangalia mechi zote za kombe la dunia kwa intaneti yenye kasi. Alisema Semwenda.“Jinsi ya kufanya malipo mteja wa Halotel anapaswa kufungua Application ya Star times na baada ya hapo atafuata maelekezo ya kununua vifurushi kuanzia vya siku, wiki hadi mwezi mzima,” Alihitimisha Semwenda.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa StarTimes Ndg. David Malisa Alisema, “Ukiwa unatumia intaneti ya Halotel ni rahisi zaidi kulipia na kutumia StarTimes App ambayo ina burudani na mechi zote za Kombe la Dunia. Kwa watumiaji wa mitandao mingine wanalipia maudhui pembeni na intaneti au data pembeni, ukilipia huduma hii unakuwa umelipia maudhui na intaneti kwa pamoja. Pia unaweza kutumia Intaneti hii bila kikomo kwa masaa 24 hata bando inapoisha utaendelea kupata Intaneti ya kutumia kwenye StarTimes App”. Alisema Malisa. 

Hii ni huduma ya kwanza kabisa Tanzania ambayo itamruhusu mteja kuendelea kupata intanenti hata baada ya bando lake kuwa limekwisha. Ushirikiano baina ya StarTimes na Halotel ni katika hatua ya kusogeza Burudani ya kandanda la kimataifa katika Simu za Mkononi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel (kulia) akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kushoto ni Meneja Masoko wa Startimes David Malisa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa kwa pamoja wakionesha namna ambavyo mteja wa Halotel anavyoweza kuangalia mpira kwenye simu yake ya mkononi kupitia App ya Star times. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa pamoja katika uzinduzi wa Halotel na Startimes kuonyesha ishara ya ushirikiano.

Bei ya Ufuta katika wilaya ya Kibiti yazidi kupaa

$
0
0
*Ni kutokana na mfumo wa stakabadhi ghalani

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BEI ya ufuta katika wilaya ya Kibiti imezidi kupaa kutoka shilingi 2750 hadi 3100 kwa kilo na kufanya wakulima kunufaika na kilimo hicho.

Kupanda kwa bei hiyo kunatokana na serikali kutaka mazao ya korosho, pamba pamoja na ufuta kuuzwa kwa mfumo wa mnada wa stakabadhi ghalani ikiwa ni kumsaidia mkulima kunufaika na kilimo anachokifanya.

Akizungumza wakati wa mnada wa zao la Ufuta Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Milongo Sanga amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa mnada zao la Ufuta limekuwa na soko kubwa na kufanya wananchi kunufaika kilimo hicho.

Amesema kuwa baadhi ya wachuuzi walikuwa wakinunua zao la Ufuta kwa shilingi 1200 hali ambayo kuliwafanya baadhi wakulima kuachana na kilimo lakini mfumo wa mnada kutokana na maagizo ya serikali wakulima wameanza kunufaika na mfumo huo.

Sanga amesema kuwa wananchi waachane na wachuuzi wa zao la ufuta kwani hawana nia njema na wao katika kuwakomboa kiuchumi.Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti, Alvera Ndabagoye amesema kuwa tangu kuanza kwa mnada huo bei imekuwa ikipanda kila mnada unapofanyika pamoja na tani za ufuta zikiongezeka.

Amesema mnada wa kwanza waliuza ufuta wa Tani 90 kwa shilingi 2750, Mnada wa pili waliuza ufuta wa Tani 118 kwa shilingi 2781 huku mnada wa tatu wameuza ufuta wa tani 454.8 kwa shilingi 3100.Amesema kuwa anategemea mnada wa Julai 4 mwaka huu bei inaweza kupanda huku akisisitiza wanunuzi wanaoshinda mnada kulipa kwa wakati ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wakulima.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti , Milongo Sanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mnada wa zao la Ufuta uliofanyika katika viwanja makao makuu ya wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Khatib Chaulembo akizungumza kuhusiana wanunuzi wa ufuta kulipa malipo kwa wakati kabla ya kuingia mwaka mpya wa fedha 2018/2019 katika mnada wa zao la Ufuta uliofanyika katika viwanja Makao makuu ya wilaya hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti, Alvera Ndabagoye akizungumza kuhusiana na kuongezeka kwa makampuni ya kununua Ufuta katika Wilaya ya Kibiti katika mnada wa zao la Ufuta uliofanyika katika viwanja Makao Makuu ya wilaya hiyo.
Sehemu ya wakulima na kampuni ziliozoomba ununuzi wa zao la Ufuta.
Viongozi wa Ushirika wakifungua sanduku la zabuni za maombi ya kampuni za kununua ufuta

DKT TIZEBA AZINDUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA KILIMO JIJINI DODOMA

$
0
0
Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba leo 28 Juni 2018 amefungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo, mkutano utakaotuama kwa siku mbili kuanzia leo mpaka kesho 29 Juni 2018 katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo Dkt Tizeba aliwasisitiza wajumbe wa baraza hilo kwa umoja wao kujadili kwa muktadha wa kutatua changamoto na kuboresha sekta ya kilimo kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa ikiwa ni pamoja na kuhusu elimu ya majukumu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi, Elimu juu ya watumishi wa Umma na hoja kutoka vyama vya wafanyakazi sambamba na wajumbe kupitishwa katika bajeti ya wizara kwa mwaka 2018/2019.

Alisema kuwa Baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu ambacho kimepewa nguvu kisheria ili kuwapa watumishi nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusu utendaji na ufanisi wa Taasisi ili kuongeza tija mahali pa kazi hivyo wajumbe hao wanapaswa kujadili mada hizo kwa ufanisi na tija.

Alisisitiza kuwa Baraza hilo linapaswa kuzaa matokeo mazuri ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya kazi huku akisema kuwa serikali imekuwa ikisisitiza kila taasisi ya umma kuunda mabaraza ya wafanyakazi ili kuongeza ufanisi na tija katika mchango wa mapinduzi ya uchumi wa viwanda.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Katikati) na Katibu wa Baraza la wafanyakazi Wizara ya kilimo Bi Agnes Hugo wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa mkutano na uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.



TPW YATOA SH MILIONI 40 KWA WANAWAKE 250 WILAYANI MONDULI KUFANIKISHA UFUGAJI WA NYUKI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Arusha

MAISHA ya wanawake 250 waliopo Kata ya Lemooti na Mswakini Monduli mkoani Arusha yanataraji kubadilika baada ya Asasi ya Watu na wanyama(TPW) kuwapatia Sh.milioni 40 za mradi wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki.

Kupitia mradi huo wanawake hao kutoka kwenye vijiji sita vya Mswakini Juu, Mswakini chini, Lengolwa, Lemooti, Oldonyo na Naitolia watapatiwa mizinga 475 itakayofungwa kwenye maeneo ya vikundi 25 vya watu 10. Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo leo, Msimamizi wa miradi Asasi ya TPW Revocatus Magayane amesema mradi huo wanautekeleza kwa ushirikiano na Baraza la Wanawake wa Kifugaji Monduli (BAWAKIMO).

Magayane amewataka wanawake hao kutoa taarifa za maendeleo ya mradi kila wakati hatua itakayowawezesha kuwa na mwanzo mzuri wa utekelezaji. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta aliwataka wanawake hao kutoingiza siasa kwenye shughuli zinazohusiana na maendeleo kwani kufanya hivyo kutawafanya wakwame kufikia ndoto zao.

“Uchumi hauna itikadi ya kisiasa, mkiingiza siasa kwenye masuala haya mtahawanyika na kushindwa kufikia mnachokihitaji kama kuwa na maisha mazuri kusomesha watoto na kujenga nyumba bora na kisasa,” alisema Kimanta. Naye Katibu wa BAWAKIMO Nai Zakayo ameishukuru TPW kwa kuwawezesha kupata na kuanzisha mradi huo wa nyuki kwenye kata mbili za wilaya hiyo.

Aidha ameiomba TPW kuwafikia wanawake wengi zaidi kwani bado wanayo maeneo mengi katika Kata nyingine ambazo zinaweza kufanya miradi ya uhifadhi wa mazingira na ufugaji wa nyuki.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akipokea mfano wa Hundi ya zaidi ya Sh milioni 40 kutoka kwa Msimamizi wa Miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama (TPW),Revocatus Magayane kwa ajili ya mtaji wa mradi wa ufugaji nyuki kwa wanawake 250.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akibadilishana mawazo na Msimamizi wa Miradi wa TPW Revocatus Magayane mara baada ya kukabidhi mradi wa ufugaji nyuki kwa wanawake 250 wa Kata ya Lemooti na Mswakini.
Mratibu wa Miradi kutoka BAWAKIMO Angela Kagashe akizungumza na baadhi ya wanawake wanachama wa baraza hilo juu ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji wa nyuki wilayani Monduli. 

Makamu wa Rais aelekea Mauritania kumuwakilisha Rais kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka jioni ya leo kuelekea nchini Mauritania ambako atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika .

Mkutano huo wa siku 2, utakaoanza tarehe 1-2 Julai 2018, utafanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa AU. 
Kaulimbiu ya waka huu ni Kushinda Vita Dhidi ya Rushwa chini ya Uenyekiti wa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.

Ujumbe wa Makamu wa Rais unajumuisha Mheshimiwa Dkt. Balozi Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais na ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini Julai 5, mwaka huu.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
28 Juni, 2018

RAIS WA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS MAGUFULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Zimbabwe zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akipunga mkono kwa wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya ziara ya kazi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha pamoja na  Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

TANZANIA NI KIMBILIO KWA WALIOKOSA AMANI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuvumiliana na kustahamiliana ndiko kunakolifanya Taifa la Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao. 

Kadhalika, uwepo wa amani nchini si tu unatoa fursa ya kutekeleza majukumu ya kiuchumi na kijamii bila hofu bali pia ni sababu muhimu ya wenzetu wengine kutoka nje kuona fursa ya kuwekeza na kushirikiana nasi katika kujenga maendeleo ya nchini. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 28, 2018) wakati akizindua Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani tawi la Tanzania (IAPP), kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni, jijini Dodoma.

Amesema amani na utulivu ni tunu kubwa sana katika jamii yoyote ile Duniani na Tanzania muda wote imeendelea kuenzi tunu hiyo iliyojengwa kwenye misingi imara kupitia waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu Shirikisho la Amani kwa Wote (Universal Peace Federation (UPF), ambalo lilianzishwa kwa lengo la kumkomboa binadamu kutoka katika udhalili wa kukosa mahitaji muhimu. 

“Hili linadhihirika kupitia mipango ya shirikisho hilo ya kushirikiana na jamii nyingine katika kuimarisha sekta zenye kugusa maisha ya watu wengi kama vile kilimo, mazingira, afya, elimu, miundombinu na nyinginezo,” amesema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa tuzo ya Balozi wa Amani na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mbunge wa Tabora Mussa Ntimizi katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018 katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wabunge Wapenda Amani, Dk Thomas Walsh, katika hafla ya kuzindua tawi la Tanzania la Wabunge wapenda amani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, jijini Dodoma Juni 28, 2018.




Zimbabwe Kuendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania

$
0
0
Na. Immaculate Makilika –MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangangwa amesema serikali yake itaendelea kushirikiana na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo, Rais Mnangagwa amesema kuwa Tanzania imesaidia kwa kiasi kikubwa katika harakati za ukombozi wa nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini, Namibia na Msumbiji na hivyo ni jukumu lao kuimarisha uhusiano huo mzuri.

“Sisi kizazi cha zamani ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunakieleza kizazi cha sasa kuhusu jitihada za Tanzania katika harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika”

“Tulikuwa tunakuja hapa, jengo hili na Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wakati huo, ambapo aliweza kusuluhisha migogoro iliyokuwepo kati ya chama cha ZANU na ZAPU” aliongeza Rais Mnangangwa.

Rais Mnangagwa alisema kuwa serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali yatakayosaidia kukuza uchumi wake na kuahidi kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu kuisha utaotarajiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu, Tume ya Ushirikiano itakutana kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo ya kibiashara.

Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema Tanzania na Zimbabwe ni nchi marafiki tangu harakati za uhuru mwaka 1960.Ambapo mwaka 1982 ilianzishwa Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe kupitia taasisi mbalimbli za kimataifa ikiwemo SADC.

Aidha, Rais Magufuli ametaja mikakati ya kukuza na kuimarisha ushirikiano wa uchumi katika maeneo ya sita ambayo ni biashara ambapo nchi hizo zimedhamiria kutumia fursa za SADC za kulegeza masharti ya biashara.Maeneo mengine ni la kukuza uwekezaji , utalii, usafiri wa anga na barabara, kushirikiana kupitia SADC kwa maana ya fursa za wanachama. Pamoja na eneo la ulinzi, usalama, afya, utamaduni, sanaa na michezo.

Vilevile, Rais Magufuli amesema wanawakaribisha Wazimbabwe kuja kuwekeza nchini Tanzania hasa ukizingatia kwamba kuna kiwango kidogo cha uwekezaji baina ya nchi mbili ambazo ni marafiki wa muda mrefu.

“Mwaka 2006 kiwango cha uwekezaji cha Zimbabwe nchini kilikuwa na thamani ya biashara ya sh. bilioni 18.3, huku mwaka 2017 ikiwa sh. bilioni 21.1, hivyo tumekubaliana kuimarisha baadhi ya maeneo ili kuleta mkakati wa kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili” alisema Rais Magufuli.

Rais Mnangagwa ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, kesho juni 29 anatarajiwa kutembelea Chuo cha Sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika. Ambapo Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho.

NIDA KUTOA VITAMBULISHO VYA URAIA MSIMU WA SABASABA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAMLAKA ya vitambulisho vya taifa (NIDA) itatua muda wa wiki mbili za msimu wa sabasaba kuanzia June 28 hadi Julai 2 kutoa vitambulisho vya uraia kwa wakazi wa Dar es salaam.

Akizungumza na Michuzi blog Mkuu wa kitengo cha mawasiliano (NIDA) Rose Joseph ameeleza kuwa kama mamlaka wamejipanga kuhudumia wananchi wote watakaojitokeza katika viwanja vya sabasaba kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho hivyo.

Akieleza taratibu za kupata kitambulisho cha utaifa bi. Rose ameeleza kuwa lazima mwombaji ajaze fomu ya maombi inayotolewa na mamlaka hiyo sambamba na kuambatanisha na vyeti vya elimu, pasipoti, leseni, kitambulisho cha mkazi Zanzibar au kati ya vilivyoorodheshwa na nakala hizo zitakazoambatanishwa zisipungue tatu.

Pia amesema kuwa vyeti vya kuzaliwa na muhimu na lazima kwa waliozaliwa kuanzia miaka ya 1980 kushuka chini, na nakala za vivuli zitakazoambatanishwa ni muhimu mwombaji kwenda na nakala halisi ili waweze kujiridhisha.
 Jaji Mkuu kiongozi Dkt. Eliezer Mbili Feleshi akisalimia na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano (NIDA) Rose Joseph alipo tembelea banda la Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa mapema leo .(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa(NIDA)Rose Joseph  akizungumza Globu ya jamii  leo jijini Dar as Salaam
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa (NIDA) Rose Joseph akimueleza jambo Jaji mkuu kiongozi Dkt. Eliezer Feleshi namna walivyojipanga kuwahudumia wananchi katika maonesho hayo ya saba saba.picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
 Baadhi ya Wananchi walio fika kwenye banda la (NIDA) wakijaza fom ili kupata vitambulisho vya Taifa

ASAS DAIRIES PAVILLION AT MWALIMU NYERERE SABASABA GROUNDS

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 28.06.2018

MICHUZI TV: WAMILIKI WA KAMPUNI YA UTALII NCHINI WAPEWA DARASA LA VITUTIO VYA UTALII...

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images