Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

Shangwe za M-Pesa zahamia Jijini Mbeya, gari ya pili yaenda Tukuyu

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika (kushoto) akimkabidhi namba ya gari mshindi wa Mpesa Mkazi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe, Mbeya, Tumaini Msosi (kulia) jana baada ya kuibuka mshindi katika shindano ya mtumiaji bora wa Mpesa kutoka Vodacom wakati wa sherehe za Mpesa kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambazo zilifanyikia Jijini Mbeya. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mpesa kutoka Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwaryg.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika (katikati) akionesha funguo ya gari kabla ya kukambidhi wa mshindi wa gari hilo kutoka Mpesa katika sherehe ya kutimiza miaka 10 ya Mpesa tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika jana jijini Mbeya.
Mshindi wa gari kutoka promosheni ya 'Tumia Mpesa ushinde gari', Mkazi wa Tukuyu Wilayani Rungwe, Mbeya, Tumaini Msosi(kulia) akionesha funguo ya gari mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari. Kushoto ni  Mkurugenzi wa M-Commerce kutoka Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika.
 Mkurugenzi wa M-Commerce kutoka Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa gari kutoka promosheni ya 'Tumia Mpesa ushinde gari', Mkazi wa Tukuyu Wilayani Rungwe, Mbeya, Tumaini Msosi baada ya kukabidhiwa gari hilo juzi mchana wakati wa hafla ya kusherekea miaka 10 ya Mpesa tangu kuanzishwa kwake.

MUHOGO SASA RASMI KWENYE MAZAO YA BIASHARA-MAJALIWA

$
0
0

*Ni baada ya kupata soko kubwa nchini China  
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya China imetoa fursa ya kufungua soko la muhogo mkavu kutoka Tanzania, tukio ambalo  linafungua ukurasa mpya wa zao la muhogo kuwa miongoni mwa mazao ya biashara. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) bungeni jijini Dodomakatika hotuba yake aliyoitoa wakati wakuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge. 

Amesema ili kuwezesha wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania kunufaika na fursa hiyo, Mei, 2018 ulisainiwa mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China kuruhusu bidhaa za muhogo mkavu kutoka Tanzania kuingia katika soko la China.  

Amesema kufuatia hatua hiyo, mwezi huu wa Juni 2018, tani 74 za muhogo mkavu kutoka Tanzania zimeingia China kupitia Bandari ya Qingdao iliyopo katika jimbo la Shandong. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kiasi cha muhogo kilichofanikiwa kuingizwa katika soko la China bado ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji ambayo yanazidi tani 150,000 kwa mwaka. 

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wachangamkie fursa ya kilimo cha muhogo ambacho kimeonesha kuwa na tija kubwa, pia amevitaka vituo vya utafiti wa kilimo viwawezeshe wakulima kupata mbegu bora na mbinu za kisasa ili waongeze uzalishaji na kukidhi mahitaji ya soko hilo. 

Waziri Mkuu amesema kutokana na zao la muhogo kuonekana kuwa na matumizi menginezaidi ya chakula, Serikali inaendelea kuvutia uwekezaji wa viwanda vya kuchakata muhogo na kuzalisha bidhaa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwamba umekuwa na mafanikio katika maeneo mengi nchini kwa sababu wakulima wadogo na wa kati wapo kwenye ushirika, hivyo kuwa na nguvu ya soko na bei nzuri ya mazao yao. 

“Mathalani, kwa kutumia mfumo huo, mwezi huu bei ya ufuta imeongezeka kutoka shilingi1,500 hadi shilingi 2,800 kwa kilo na kuua mfumo usio rasmi wa uuzaji wa zao hilo ujulikanao kama ‘chomachoma’ ambao  ulimpunja mkulima kwa ujazo na bei,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amesema mfumo huo unasaidia kuzuia upotevu wa mazao unaotokana na uhifadhi dhaifu, pia unasaidia kuhifadhi mazao ili kusubiri kuuza wakati muafaka na kuyaongezea thamani mazao kabla ya kuyauza. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa mfumo huo unatekelezwa kikamilifu na kuleta tija kwa wakulima. 

Amesema hatua hizo ni pamoja na ushirikishwaji wa wadau, kuimarisha ushirika, kuweka miundombinu ya masoko na kuboresha muundo wa taasisi na vitendeakazi vya Bodi ya Stakabadhi za Ghala. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watendaji Serikalini kuhakikisha kuwa mazao mengi zaidi yanaingizwa katika stakabadhi za ghala ili kuwe na tija kwa wakulima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge, jijini Dodoma Juni 29, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na baadhi ya wabunge baada ya kusoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge jijini Dodoma Juni 29, 2018.
Bendi ya JKT Makutupora ikiongoza  Wimbo wa Taifa wakati Bunge lilipoahirishwa  jijini Dodoma Juni 29, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya Bendi ya JKT Makutopora kuongoza Wimbo wa Taifa wakati wa kuahirisha  Mkutano wa 11 wa Bunge  jijini Dodoma Juni 29, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Madini,  Angela Kairuki, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mahagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuiu)

Young Killer aachia video ya ‘Hunijui’ akiwashirikisha Dully Sykes na Ben Pol

$
0
0
Rapper Young Killer Msodoki ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Hunijui’ aliomshirikisha mkongwe kwenye muziki wa Bongo Flava, Dully Sykes pamoja na mfalme wa R&B Tanzania, Ben Pol.


Kwa historia yake ya kutengeneza hits, haikuwa ngumu kuwapata wakubwa zake kuiwekea nakshi ngoma hii. Young Killer anasema alianza kumshirikisha Ben Pol kwanza na alipomtembelea Dully Sykes ili kumsikiliza wimbo,  muda huo huo staa huyo akaupenda na yeye kuridhia kuweka mchango wake.



“Nimempa nafasi Dully kwenye ngoma sababu ni legend na ni inspiration kwa watu wengi na niliowafuatilia tangu kitambo,” anasema Young Killer. “Na Ben Pol ni moja kati ya watu niliokuwa nawasikiliza wakipiga chorus za watu ambao walikuwa wamenitangulia, unasikia kabisa kuna kitu amekifanya na bila uwepo wake kisingekuwa. Nimewashirikisha sababu niliamini watafanya kitu kizuri ambacho wamekifanya,” ameongeza.



Young Killer anasema Hunijui ni ujumbe kwa watu wanaodhani kumjua vizuri wakati si kweli. Anasema neno ‘Hunijui’ limetoka kwenye uumbaji wa chorus wa Dully Sykes na kuwa na nguvu ya kubeba maudhui ya wimbo.



Huu ni mradi wake wa pili chini ya label ya Wanene Entertainment aliyosaini nayo miezi kadhaa iliyopita, baada ya ule aliomshirikisha staa wa Kenya, Khaligraph, ‘Shots’ ambao na unaendelea kufanya vizuri Afrika Mashariki. “Maendeleo ni mazuri,” anasema Young Killer kuhusiana na kuwa chini ya label hiyo maarufu nchini, nyumbani pia kwa rapper Chin Beez.



“Ni kutokana na ukweli kuwa tunafanya kazi ambayo inaonekana.”



Hunijui imetayarishwa na Bin Laden akishirikiana na Gonche na mastering kufanywa na Chizan Brain kupitia Wanene Studios. Video imeongozwa na Destro wa kampuni ya Wanene Films.

zifahamu faida za kuwa Mwanachama wa IMEI Community

MULTICHOICE TANZANIA YAWEKA NGUVU KWENYE RIADHA

$
0
0
MultiChoice Tanzania imetangaza kuendelea kudhamini mchezo wa riadha hapa nchini huku ikisaini makubaliano maalum ya kumdhamini mwanariadha kinda Francis Damiano Damasi. Udhamini huo unahusisha fedha ya kujikimu kwa mawanariadha huyo na mafunzo yake na wanariadha wengine katika kambi maalum ya mafunzo inayotarajiwa kuwa wilayani Mbulu.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini kwa mwanariadha huyo, Mkuu wa Mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana, amesema kuwa dhamira kubwa ya MultiChoice ni kuhakikisha kuwa mchezo wa riadha unakuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa, kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.

“Tunataka taifa hili lijulikane ulimwengu mzima kama chimbuko la mabingwa, na tumeanza na riadha. Tumedhamiria kukuza mchezo huu na kuufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo, ni burudani, na ni sekta nyeti kiuchumi kama ikiendelezwa” alisema Mshana na kuongeza “Tunataka kuusikia wimbo wetu wa taifa katika mashindano makubwa ya kimataifa, tunataka kuiona bendera yetu ikipepea juu katika kila mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa, tunataka mamia ya vijana wetu wenye uwezo mkubwa katika riadha washiriki kwenye mashindano makubwa, waweze kujipatia kipato, kuwekeza na kuwa chanzo cha maelfu ya ajira na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu”

Amefafanua kuwa udhamini huo utakuwa wa mwaka mmoja na utaendelezwa na kuboreshwa kulingana na hali itakavyokuwa pamoja na mafanikio yatakayopatiokana. “ Huu ni mkakati wetu endelevu, ni mpango wetu maalum unaojulikana kama ‘Ni Zamu Yetu’! ambao umejikita katika kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika riadha.” Amesema Mshana.

Mbali na kumdhamini Damiano, MultiChoice pia itadhamini kambi maalum ya mafunzo itakayokuwa wilayani Mbulu ambayo inatarajiwa kuanza mafunzo rasmi hivi karibuni. Amebainisha kuwa taratibu za kuanza kwa kambi hiyo zipo katika hatua nzuri na kambi inatarajiwa kuanza rasmi Agosti mwaka huu na itakuwa na wanariadha kinda wasiopungua sita – wasichana na wavulana.

Kwa upande wake mwanariadha Damiano ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas, amesema udhamini huo utamfanya aweze kufanya mazoezi yake vizuri kwani sasa hyo ndiyo itakuwa kazi yake ya kudumu. Amesema kilicho mbele yake ni ushindi tu. “Nashukuru sana kwa udhamini wa MultiChoice, na mimi naahidi kuwa nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa siwaangushi MultiChoice na siwaangushi watanzania.”

Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida-Buday, amesema wamefarijika sana kuona kuwa MUltiChoice inaendelea kudhamini riadha na akasema udhamini huo siyo tu utamsaidia mwanariadha husika, bali pia ni chachu hata kwa wanariadha chipukizi kuwa na moyo na ari ya kushiriki katika mchezo huo.

Amesema Shirikisho la Riadha Tanzania litahakikisha kuwa udhamini huo unakuwa wa manufaa na unazaa matunda yaliyotarajiwa ya kuleta medali zaidi kutaka katika mashindano ya kimataifa. “Ufadhili wa aina hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa riadha. Tunaahidi ushirikiano wetu wa hali na mali ili kufanikisha malengo na tutahakikisha kuwa tunatoa ushirikiano unaostahili kwa wadhamini wetu” alisema Gida.

Mwanariadha Francis Damiano Damasi, anatarajiwa kushiriki mashindano makubwa ikiwemo Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki yanayofanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam, Mashindano ya vijana ya Dunia (World Junior Championship) mwezi Julai nchini Finland, Mashindao ya vijana ya Olympic kanda ya Afrika mwezi Julai nchini Algeria, Mashindano ya vijan ya Olympic (Youth Olympic Games) mwezi Oktoba nchini Argentina, na mashindano ya nyika ya vijana (World Junior Cross-country) mapema mwakani nchini Denmark.
Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wapili kushoto) na Kocha wa riadha Meta Petro (kulia) ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano wakisaini mkataba maalum wa udhamini wa mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha. Kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida Buday na wa pili kushoto ni mwanariadha Fracis Damas Damiano.
Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wapili kushoto) na Kocha wa riadha Meta Petro (kulia) ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano wakiwa Tayari kubadilishana nyaraka punde baada ya kusaini mkataba maalum wa udhamini wa mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha. Kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida Buday.
Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (kushoto) akimkabidhi nakala ya mkataba mwanariadha chipukizi Francis Damiano mara tu baada ya kusainia mkataba wa udhamini kwa mwanariadha huyo. Kulia ni Kocha wa riadha Meta Petro ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha.

TBL YAPELEKA WASHINDI WAKE NCHINI URUSI KUSHUHUDIA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA

$
0
0




Meneja Masoko na udhamini wa TBL group, George Kavishe akiwa katika Uwanja wa Spartak jijini Moscow nchini Urusi pamoja na washindi wa ticket za Kombe la dunia kutoka Tanzania kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakiendelea kufuatilia mechi za Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi.



Meneja Masoko na udhamini wa TBL group, George Kavishe akila selfie na baadhi ya washindi wa ticket za Kombe la dunia kutoka Tanzania kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakiendelea kufuatilia mechi za Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi.


Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara

$
0
0
Na MwandishiWetu
Wakulima wa ufuta nchini wametakiwa kuachanana kilimo cha mazoe and kufanya kilimo biashara. Hasa katika kuongeza tija ya uzalishaji ili kukabiliana na changamoto wakati bei inaposhuka pamoja na kuweka kumbukumbu na kuwasiliana na wanunuzi kabla ya kulima mazaoyao. 

Hiyo ni pamoja na wakulima kujiunga katika vikundi rasmi au katika vyama vya ushirika ili kuweza kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha nchini ambapo serikali itawapatia dhamana kupitia vikundi hivyo.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba alisema hayo jijini Dar es Salaam katika kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilayaz a Bahi, Babati na Manyoni, kongamano hilo liliandaliwa na shirika la Farm Africa kwa kushirikiana na mashirika wenza ambayo ni INADES Tanzania, COSITA na MVIWATA. 

 “Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli mara kadhaa amekuwa akisisitiza umuhimu wa wakulima nchini kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kujikwamua kutoka kwenye kilimo kisicho na tija kwa sababu vyama vya ushirika vina fursa ya kupata dhama na ya serikali moja kwa moja,” alisisitiza.

Wadau wa walioshiriki kongamano hilo ni wakulima, wanunuzi wakubwa na wakati, halmashauri za Babati Manyara , Manyoni Singida, Bahi Dodoma na Kilwa, wakala wa mbegu ASA, wizara ya TAMISEMI, Viwanda   na wadau wengine ni Shirika la TOSCI watoa huduma kwa njia ya tehama ambao ni wawakilishi kutoka mashirika ya Esoko na Sibesonke .
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen kushoto aliyesimama  akifafanua jambo wakati wa wakati wa  kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta kutoka wilaya za Kilwa, Bahi, Babati na Manyoni na liliandaliwa na shirika hilo, kulia ni  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida Manyoni, Bw.Charles Fussi, wa pili kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki. 
 Meneja Mwandamizi wa Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki aliyeye simama akieleza jambo wakati wa  kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilaya za Bahi, Babati, Kilwa na Manyoni lililoandaliwa na shirika hilo, kulia kwake mwenye laptop ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen na wengine ni wadau wa zao hilo. 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba wa pili kulia akifafanua jambo wakati wa  kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilaya za Bahi, Babati na Manyoni na liliandaliwa na shirika la Farm Africa, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen, kushoto Meneja Mwandamizi Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki na wa pili kushoto Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida  Manyoni,Bw.Charles Fussi.
 Wadau wa zao la ufuta kutoka wilaya za Kilwa, Bahi, Babati na Manyoni wakiwa katika  kongamano la siku mbili la wadau wa zao hilo lililoandaliwa na shirika la Farm Africa.

SPRITE BBALL KINGS HATUA YA MCHUJO KUFANYIKA KESHO

$
0
0



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanaanza kutimua vumbi kesho kwa michezo 25 kuchezwa katika hatua ya mtoano kwenye Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu Jijini Dar es salaam.

Michezo hiyo katika hatua ya mtoano itazikutanisha timu 50 kutoka sehemu mbalimbali za Jijini Dar es Salaam ili kuweza kupata timu 15 zitakazoungana na bingwa mtetezi Mchenga BBall Stars walioingia moja kwa moja kwenye hatua ya 16 bora.

Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya pili imeandaliwa na kituo cha Televishen cha East Africa na Radio yakidhaminiwa na kinywaji cha Sprite.

Mechi ya kwanza itaanza saa 2 asubuhi na mpaka kufikia 11 jioni michezo yote 25 itakua imemalizika na kupatikana timu zitakazoingia hatua inayofuata ya mchujo.a.

Mshindi wa kwanza anajinyakulia Shiling Milion 10 na kikombe, mshindi wa pili milion 3 na mchezaji bora wa miachuano anajinyakulia milion 2 na kikombe.


RATIBA YA MASHINDANO SPRITE BBALL KINGS 2018 HATUA YA MTOANO                                                                      TEAM VS TEAM
1.Dream Chaser  VS  Temeke Heroes
2.The Fighter  VS  Force One 
3.Flying Dribblers VS Kurasini Worriours
4.TMT VS Street Ballers
5.God With Us VS External Heroes
6.DMI VS Madale State
7.Ardhi Univ  VS The Kazi 8 Lycans
8.Ukonga Worriours VS Little Saints
9.Oysterbay VS Ilala East Zone
10.BTP  VS Grounders
11.Oratory VS Mbezi Beach KKKT
12.The Snipers VS Young Boys
13.Eagle Wings VS Portland
14.Goldernt Talents VS  Montfort Kings
15.Ukonga Hitmen VS Yombo Patriot
16.The Hashtag VS BV
17.Bankers VS Water Institute (W.I)
18.NIT Ballers VS Air Wings
19.Fast Heat VS Street Worriours
20.Stlylers VS Denthshoppers Bball Team
21.Loyolight  VS Kigamboni City
22.K Worriors Kijichi VS Team Kiza
23.Madena Ballers VS St Joseph
24.The Magic VS Raptors
25.Weusi Basket Ball Club VS Kichangani

JAJI IMANI ABOUD WA TANZANIA ASHINDA UCHAGUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

$
0
0
Mkutano wa 33 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaoendelea Jijini Nouakchott, Mauritania kwa siku mbili, leo tarehe 29 Juni, 2018 umefanya uchaguzi wa Majaji wanne wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Mgombea wa Tanzania Mhe. Jaji Imani D. Aboud ameshinda uchaguzi huo kwa kura 47 kati ya kura 50 zilizopigwa na kufanikiwa kuchukua nafasi ya Jaji Solomy Balungi Bossa wa Uganda aliyejiuzulu nafasi hiyo kabla ya kumaliza kipindi chake.

Kwa ushindi huo, Mhe. Jaji Aboud atakuwa Jaji wa Mahakama hiyo akiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka miwili.

Majaji wengine walioshinda kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Jaji Kioko Ben (Kenya), Jaji Tchikaye Balise (Jamhuri ya Congo), na Jaji Anukam Stella Isibhkhomen (Nigeria).

Ushindi huu unadhihirisha uwezo mkubwa alionao Mhe. Jaji Aboud na heshima kubwa iliyonayo nchi yetu katika Bara la Afrika.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 29 Juni, 2018

SERIKALI YATENGA 4.3bn/- KUJENGA VITUO VYA KUHIFADHI DAMU SALAMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 4.3 ili kujenga vituo vya kuhifadhi damu (satellite blood banks) kwenye mikoa 12.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Manyara, Katavi, Rukwa, Ruvuma na Njombe. Mingine ni Tanga, Arusha, Pwani, Singida, Songwe, Geita na Simiyu.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) bungeni jijini Dodoma katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge.Bunge limeahirishwa hadi Septemba 4, mwaka huu.

Amesema lengo la mpango huo ni kuboresha upatikanaji wa damu hasa kwa akinamama wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua. “Serikali imedhamiria kupunguza vifo vya akinamama na watoto vitokanavyo na uzazi. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea kufanya ukarabati na ujenzi wa majengo ya upasuaji, maabara, wodi za wazazi, nyumba za watumishi na wodi za watoto,” amesema.

Amesema kukamilika kwa majengo hayo, kutaboresha huduma za uzazi kwa akinamama na watoto wachanga. “Hatua hii itawezesha upatikanaji wa huduma kamili za uzazi na kupunguza vifo vya mama na watoto. Katika mwaka 2018/2019, eneo litakalopewa kipaumbele ni kuimarisha upatikanaji vifaa na watumishi katika vituo 208 vinavyoendelea kuboreshwa,” amesema.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi watumishi wa afya, waongeze juhudi ya kuhamasisha wananchi wajitolee damu na pia akawaomba wananchi nao wawe na utamaduni wa kuchangia damu ili kuwezesha upatikanaji wa damu salama itakayohifadhiwa kwenye benki hizo.

BARAZA LA UUGUZI LAWATIA HATIANI WAUGUZI WAKUNGA SITA

$
0
0
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewakuta na hatia na kuwapa karipio kali la maandishi Wauguzi Wakunga sita katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya kitaaluma wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa.

Katika kikao chake cha 193 kilichofanyika tarehe 28 Juni, 2018 katika Ofisi za Baraza hilo zilizopo Kibaha, Mkoani Pwani, chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bw. Abner Mathube, lilisikiliza shauri la ukwiukwaji wa maadili ya kazi lililotokea katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambapo mama mjamzito alilalamika kutokupatiwa huduma stahiki alipowasili hospitalini hapo hali iliyosababisha mama kukosa mtoto.

Pamoja na karipio hilo, Wauguzi Wakunga wameonywa kuwa endapo watarudia kosa hilo, Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania, halitasita kuwachukulia hatua kali zaidi za ikiwemo kuwafutia usajili.

Akizungumza na wanahabari, Msajili wa TNMC Bi. Agnes Mtawa amesema katika kikao hicho, Baraza limejadili suala la baadhi ya watu wanaogushi vyeti na leseni za taaluma ya uuguzi na ukunga ambapo limebaini kuwa katika robo mwaka Aprili-Juni, 2018 watu watano walitambuliwa kugushi vyeti na leseni hivyo wamepelekwa kwenye vyombo vya dola ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Aidha, Baraza limewabaini watu 15 wanaojitambulisha kuwa ni wauguzi lakini kanzi data ya Baraza hilo imeonesha kuwa vyeti hivyo siyo halali na leseni wanazotumia ni za kugushi. Kwakuwa watu hawa wapo mikoa mbalimbali hapa nchini Baraza linawataka kujisalimisha mara moja kabla halijawafuata huko waliko.

Baraza linatoa onyo kali na kuwataka watu wanao ghushi vyeti na leseni za kitaaluma ya Uuguzi na Ukunga kuacha kuacha tabia hiyo mara moja kwani hatua kazi zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Bw. Abner Mathube akiongoza kikao cha baraza hilo, Kibaha Mkoani Pwani. Kushoto kwake ni Msajili wa Bazara Bi. Agnes Mtawa

Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Takribani wanawake milioni 2.6 wanategemea kunufaika na mradi ujulikanao kama 50 Million Women Speak Project’ unaolenga kuwawezesha wanawake kupata taarifa za kiuchumi kupitia mtandao wa mawasiliano.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Julius Mbilinyi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini.

Bw. Mbilinyi amesema kuwa takwimu za Hali ya Afya na Demografia za mwaka 2015 zinaonesha asilimia 51 ya Watanzania ni wanawake ambao kati ya wanawake hao, asilimia 70 wanajihusisha na shughuli za kilimo na ujasiriamali hivyo mradi huo utatumika kusaidia kuimarisha shughuli zao.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Julius Mbilinyi akifungua kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini kilichofanyika jijini Dodoma.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mary Makoffu na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji Kiuchumi, Esther Riwa.
Msimamizi wa Mradi huo kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Wilson Muyenzi akitoa mada katika kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini kilichofanyika jijini Dodoma.
Wadau wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha kujadili kuhusu mradi ujulikanao kama 50 Million Women Speak Project’ unaolenga kuwawezesha wanawake kupata taarifa za kiuchumi kupitia mtandao wa mawasiliano kilichofanyika jijini Dodoma.

RAIS WA ZIMBABWE ATEMBELEA CHUO CHA KILIMO NA MIFUGO CHA KAOLE AMBACHO MIAKA YA 1960s ILIKUWA SHULE YA MAFUNZO YA UFUNDI YA WAPIGANIA UHURU WA CHAMA CHA FRELIMO

$
0
0
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili katika chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani. Rais huyo wa Zimbabwe alisoma Shuleni hapo mwaka 1963 pamoja na wapigani Uhuru wa Chama cha FRELIMO na ilijulikana kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya  wapigania Uhuru wa Chama cha FRELIMO.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza na wafanyakazi pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole ambapo miaka ya nyuma alisoma hapo wakati huo ikijulikana kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO.
 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiangalia moja ya sufuria waliokuwa wakiitumia katika matumizi yao ya kila siku  wakati wakisoma katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa katika picha na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa, Viongozi wengine wa Tanzania na Zimbabwe pamoja na wanafunzi wanaosoma katika chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati alipokuwa akielekea katika moja ya madarasa ambayo walikuwa wakiyatumia kuanzia mwaka 1963.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoka katika moja ya mabweni waliyoyatumia katika mwaka 1963 wakatika wakiwa katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kina julikana kama chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kukagua baadhi ya madarasa na mabweni waliyokuwa wakiyatumia katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kinajulikana kama chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akipunga mkono kwa kikundi cha ngoma za asili wakati akiondoka katika eneo la chuo hicho cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani. 
PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI AMUAGA MGENI WAKE RAIS EMMERSON MNANGAGWA WA ZIMBABWE LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe aliyemaliza ziara yake rasmi ya siku mbili nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kiongozi huyo kuondoka kurejea nchini kwake leo Ijumaa Juni 29, 2018 l eo Ijumaa Juni 29, 2018 leo Ijumaa Juni 29, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgeni wake Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe alipokuwa akimtambulisha kwa baadhi wa wajumbe alioambatana nao.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe akiwa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dkt. Raymond Mndolwa  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka kurejea nchini kwake eo Ijumaa Juni 29, 2018   l eo Ijumaa Juni 29, 2018.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe akiwa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa CCM mkowa wa Dar es salaam katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka kurejea nchini kwake eo Ijumaa Juni 29, 2018   l eo Ijumaa Juni 29, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe aliyemaliza ziara yake rasmi ya siku mbili nchini  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka kurejea nchini kwake eo Ijumaa Juni 29, 2018   leo Ijumaa Juni 29, 2018.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 29.06.2018


NHC YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0

 Afisa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC  Bw. Augustino Sanga akiongea na mmoja ya Wateja waliofika katika banda la NHC katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendlea Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa  Bi. Aika Benson akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika katika banada la NHC
 Afisa Masoko Bw. Wistone Sanga akitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda la shirika hilo kwenye viwanja vya Maonesho Sabasaba.
Banda la Shirika la Nyumba la Taifa NHC  Kama linavyoonekana kwa nje katika Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba.

Matukio ya mbalimbali ya maonesho ya Sabasaba

$
0
0
 WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji , Charles Mwijage (wa pili kushoto), akipata maelezo  kutoka kwa Mtafiti Msaidizi  wa  Kampuni ya Camartec ya Arusha,  Mhandisi  Noela  Byabachwezi kuhusu zana za kilimo zinazotengenezwa na    kampuni hiyo, katika viwanja vya Maonyesho ya  42 ya Biashara ya Kimataifa, yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere,  Dar es Salaam, jana.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara ya Kimataifa Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka
 .Meneja  Biashara wa Kampuni ya Tigo, Wande Shisael, akiongea na waandishi wa habari, kuhusu kampuni hiyo kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya  Biashara ya Kimataifa Tanzania (TANRADE) kuandaa maonyesho  42 ya  kimataifa ya Biashara iashara maarufu kama Sabasaba, yanayofanyika kiatika viwanja vya  maonyesho vya  Mwalimu Julius Nyerere, , Dar es Salaam, jana. Kushoto ni  Meneja  Ukuzaji Biashara  wa TANTRADE, Stephrn Koberou.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Dr.Mathias  Lugoye, (kulia) akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la chuo hicho,  katika Maonyesho ya Kimataifa ya 42 ya Biashara, yanayofanyika katika Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana, kuhusu teknolojia  ya usindikaji bidhaa inayobuniwa na chuo hicho.
 Meneja wa Mawasiliano wa VETA, Sitta Peter akitoa maelezo kwa wananchi wanaotembelea Maonyesho ya Kimataifa ya 42 ya Biashara, yanayofanyika katika Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, , kuhusu nafunzo ya ufundi yanazalishwa na VETA
 Wananchi wakipata maelezo kuhusiana na ufundi mbalimbali unaotolewa na vyuo vya VETA. Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii

INFINITY GYM YAWASHAURI WANAOFANYA MAZOEZI KUNYWA MAZIWA YA ASAS

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
WATANZANIA ambao wanafanya mazoezi wameshauriwa baada ya kumaliza mazoezi wanywe Yoghurt(maziwa) ya Asas kwani husaidia kulainisha misuli.
Ushauri huo umetolewa na Meneja Masoko wa Infinity Fitness Gym Sia Ndaskoi wakati anazungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi sambamba na unywaji wa maziwa ya Asas.
Amesema wanafahamu kuwa baada ya kufanya mazeozi mhusika hupata kiu , hivyo badala ya kunywa maji ni vema akanywa maziwa hayo ambayo kwa sehemu kubwa yatamfanya mwili wake misuli kuachia haraka na kumuondelea maumivu ya mwili.
Amesema mtu anayefanya mazoezi mwili wake unakuwa imara na hausumbuliwi a magonjwa na hivyo ametoa mwito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kasha wasisahau kunywa maziwa ya Asas.
Ndaskoi ambaye pia amewahi kushiri mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2009 amesema  kwa anayefanya mazoezi inakuwa ngumu kuzeeka mapema , hivyo ushauri wake ni watanzania kujikita kufanya mazoezi ambayo pia husaidia kuondoa mafuta mwilini na hata kwa aliye na msongo wa mawazo akifanya mazoezi yanamsaidia kuuondoa mawazo.
Meneja wa Infinity Fitness Gym Sia Ndaskoi wa Infinity Fitness Gym Sia Ndaskoiwa pili kutoka kushoto akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye banda la ASAS kwenye  maonyesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam leo.
Meneja wa Infinity Fitness Gym Sia Ndaskoi wa Infinity Fitness Gym Sia Ndaskoi wa pili kutoka kushoto akiwa na wafanyakazi wenzake wakionyesha baadhi ya vifaa vya mazoezi kwenye banda la ASAS kwenye  maonyesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam 

MKUTANO WA WANASAYANSI KUFANYIKA JULAI 2 JIJINI DAR ES SALAAM

MWANAFUNZI CHUO CHA MAABARA SINGIDA AKIRI KUSAMBAZA ZA UONGO MATUMIZI YA PANADOL

$
0
0
*Ajisalimisha Mamlaka ya Chakula na dawa, awaomba radhi watanzania wote

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MWANAFUNZI wa Chuo cha Maabara Singida, Elia Mhina amekiri kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu dawa aina ya Panadol kwamba si salama kwa matumizi ya binadamu.

Hatua ya mwanafunzi huyo ambaye aliambatana na mzazi wake Mchungaji Emmanuel Mhina jana katika Ofisi za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ilitokana na jitihada za mamlaka hiyo za kumtafuta hadi walipomkamata.

Mhina ambaye anafanya mafunzo kwa vitendo Temeke, amesema alisambaza taarifa hizo alizozitafsiri kwa lugha ya kiswahili bila kufanya uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mhina alisema alipokea taarifa za uvumi kutoka kwende video iliyotumwa kwenye kundi moja  la WhatsApp na kuifanya kuwa taarifa ya uhakika.

"Nilipokea video kweye kundi la Medical ambayo ilikuwa kwa lugha ya Kiingereza nami niliitafsiri kwa lugha ya Kiswahili na ndani ya siku tatu baada ya kuisambaza ilienea Tanzania nzima," alisema Mhina.

Pia alieleza kuwa aliamini taarifa hizo bila ya kufuatilia kitendo ambacho kimesababisha hofu kwa watumiaji wa dawa hiyo.

"Niwaombe radhi watanzania kwa ujumla, taasis na Kampuni ya Paracetamol kwa makosa niliyofanya ambayo kimsingi sio mazuri.

"Hivyo naahidi hata nikipata ajira nitakuwa mwaminifu pia niwasihi vijana wenzangu watumie vyema mitandao tusisambaze taarifa bila kujua ukweli wake," alisema.

Kwa upande wa Baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Avest Kibaha, Emmanuel Mhina alisema alipewa taarifa kuwa mtoto wake amefanya makosa ya mtandao kwakusambaza taarifa zisizo na ukweli na alikiri kufanya hivyo.

Alisema ni lazima watumiaji wa mitandao wawe makini na waangalifu kwani sio kila taarifa inatakiwa kusambazwa.

"Nawaomba vijana wajitawale na kuwa na mopaka katika kutumia mitandao ya kijamii kwani inaweza kubadili taswira ya kitu chochote. 

"Pia wazazi tunapaswa kuwafuatilia watoto wetu ili kujua viashiria vyovyote vinavyoweza kusababisha taharuki kwa jamii," alieleza Mchungaji Mhina.

Wakati  huo huo Mwanasheria Mshauri wa TFDA, Iskari Fute alisema kitendo cha kusambaza uvumi ni kosa kisheria na kwamba likithibitishwa zipo adhabu mbalimbali ikiwemo kifungo jela au kulipa faini.

Fute alisema kwa mtu atakayebainika kutenda kosa hilo atatozwa faini ya kuanzia Sh laki moja hadi Sh milioni 10 au kifungo kisichopungua chini ya wiki mbili na kuendelea.

"Sayansi ya jinai inaelekeza kuwa mtu akikiri au kutambua kosa lake mbele ya umma inamaanisha kwamba kitu alichokifanya hakikuwa na nia ovu. Tumeangalia kitendo na nia ya kufanya kitendo hiki tumeona kuwahakuwa na nia ovu," alisema  Fute.

Pia aliwataka vijana kutumia somo hilo kuhakikisha wanatumia vyema mitandao ya kijamii na kwamba taarifa zozote zinathibitishwa na mamlaka husika.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agnes Kijo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu dawa aina ya Paracetamol inayojulikana kama Panadol kwamba si salama kwa matumizi ya binadamu uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Maabara Singida, Elia Mhina akizungumza na kuhusiana na kuhusika kusambaza taarifa za uongo za dawa aina ya Panado na kukiri kosa hilo kwa kuombaza msamaha kwa kile alicho kifanya katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mshauri wa TFDA, Iskari Fute akizungumza kuhusiana na sheria za kwa mtu anayesambaza taarifa za uongo katika masuala ya dawa na chakula Panado  katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images