Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA WA IRINGA AWAFUNDA MAKANDARASI WANAWAKE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, amewataka makandarasi wanawake wote nchini kufanya kazi kwa kujiamini na kutooneana wivu katika maeneo yao ya kazi.

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwawezesha makandarasi wanawake kufikia madaraja ya juu ya ukandarasi ili kuwawezesha kuchukua kandarasi kubwa, na hivyo kuinua kipato chao kitakachopelekea kuondokana na umaskini katika familia na jamii zinazowazunguka.

Ametoa wito huo mkoani Iringa, wakati akifungua mafunzo elekezi kwa makandarasi wanawake wa mikoa ya nyanda za juu kusini katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara hapa nchini na kusema kuwa mashindano yao yawe ni ya kutimiza wajibu na siyo kushindana katika kuvaa wala kusuka.

"Nataka mwanamke wa kitanzania ujiamini na kusimama vyema na kusonga mbele kwani sifa yetu kubwa ni kuhakikisha tunatunza familia kwa hali yoyote, wajibikeni ipasavyo katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara bila woga wowote", amesema Mhe. Masanze.

Aidha Mhe. Masenza, amesisitiza umuhimu wa makandarasi hao kujaza nyaraka za zabuni na mikataba wenyewe ili kuepukana na utapeli na baadhi ya watu wanaojidai wanawasaidia shughuli hizo. Amewataka makandarasi wanawake hao kufanya kazi kwa ushirika na sio mmoja mmoja ili kuweza kumiliki kampuni au vikundi vya ujenzi ambavyo vitawasaidia kupata zabuni za miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, akihutubia makandarasi wanawake kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo. 
Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake kutoka Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Rehema Myeya, akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia), kufungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo makandarasi wanawake katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.
Baadhi ya makandarasi wanawake kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Katavi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani Iringa.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole, akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, mara baada ya kufungua rasmi mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo kwa makandarasi wanawake katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani Iringa. 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza akiwa katika picha ya pamoja na makandarasi wanawake kutoka mkoa wa Iringa baada ya kufungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ushiriki wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, yaliyofanyika mkoani humo.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


INFINIX IMEZINDUA INFINIX NOTE 5 YENYE TEKNOLOJIA YA ANDROID ONE.

$
0
0
KAMPUNI ya simu ya Infinix imeweka dhamira ya kuzalisha simu zenye teknolojia ya hali ya juu na muonekano mzuri kwajili ya kizazi kipya. Infinix NOTE 5 inaendeshwa na mfumo wa Android wenye kuifanya kuwa simu ya pekee yenye sifa zenye kushawishi ukilinganisha na simu yoyote ya Infinix kwa sasa. 
Kupitia mfumo wa Android One Infinix NOTE 5 imethibitika kuwa simu yenye ulinzi zaidi wa software na inayopokea updates katika muda mfupi.

Baada ya kuzinduliwa jijini Dubai, Infinix NOTE 5 itazinduliwa katika nchi zaidi ya 30 ikiwemo Nigeria, Egypt, India, Morocco, Kenya, Uganda Cote d’ voire na nyengine nyingi.

Na katika kuhakikisha kampuni inatimiza ahadi ya kuzalisha simu zenye muonekano mzuri kuendana na wakati Infinix NOTE 5 inamuonekano wa tofauti ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 na nchi 6.0 FHD.

Pamoja ya kuwa na mfumo pendwa hasa kwa wale wenye matumizi makubwa kama ya kiofisi, lakini pia Infinix NOTE 5 imempendelea mpenzi wa kamera pia kwa kupitia pixel 16 low light selfie na pixel 12 nyuma zenye kupiga picha nzuri hata katika mwanga hafifu.

Infinix NOTE 5 inauwezo wa kukaa na chaji kwa siku tatu pasipo kuzima data kutokana na ujazo wake wa chaji kuwa 4500.

Akiongea na vyombo vya habari makamu wa raisi wa TRANSSION HOLDINGS Bwana Arif Chowdhury alisema kwamba, “nikiwa miongoni mwa wazalishaji na wasambazaji wa simu za Infinix katika masoko mbalimbali tunawahakikishia bidhaa zetu zinawafikia idadi kubwa ya watu na kuongeza utandawazi kupitia njia ya mawasiliano”.

Na mkurugenzi wa Android, Bwana Mahir Sahin alisema, “unaponunua simu mpya unategemea kuona sifa mpya katika simu hiyo na hii ndio sababu iliyotufanya tushirikiane na GOOGLE na kuwaletea simu yenye maajabu yanayotokana na Android One kupitia GOOGLE Lens na GOOGLE Assitant”.

WAHANDISI CHANGAMKIENI UWEKEZAJI WA VIWANDA-MWIJAGE

$
0
0

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amewataka wahandisi nchini kuchangamkia fursa za uwekezaji katika viwanda nchini ili kuiwezesha Serikali kufikia lengo la uchumi wa kati na jumuishi ifikapo 2025.

Akifungua kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo, Mhe Mwijage amesema mchango wa wahandisi ni muhimu sana katika kipindi hiki ili kuwezesha taifa kufikia uchumi wa kati wenye uwiano kati ya pato la nchi na uchumi wa mwananchi. “Tumejipanga kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na hivyo kugusa uchumi wa wananchi wengi” amesema Mhe. Mwijage.

Amesema uwekezaji katika viwanda vya sukari, mafuta na vifaa vya ujenzi ambavyo vyote malighafi zake zinapatikana nchini, utawezesha idadi kubwa ya wananchi wa Tanzania kupata ajira na hivyo kufikia lengo la Taifa la uchumi wa kipato cha kati. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini (ERB), Eng. Profesa Ninatubu Lema ameiomba Serikali kuthubutu kuwaamini wahandisi wazalendo kusimamia na kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi hapa nchini.

Prof. Lema amesema wahandisi wako tayari hata kupewa sehemu kidogo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya (Standard Gauge), ili nao waweke alama ya uzalendo katika mradi huo mkubwa unaotekelezwa nchini. “Tunapoadhimisha miaka 50 ya ERB tuko wahandisi tuliosajiliwa zaidi ya Elfu 21 tunaweza kufanya kitu kama alama kwa taifa na vizazi vijavyo”, amesema Prof. Lema.

Amewataka wahandisi kutathmini namna gani wanaweza kuendeleza kilimo na viwanda nchini ili kuweza kubadili uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla katika miaka ijayo.

Kaimu Msajili wa ERB, Eng. Patrick Barozi amesema kongamano la wahandisi kuhusu uchumi wa viwanda ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya wahandisi yanayofanyika katika sekta mbalimbali za kihandisi yatakayofikia kilele chake mwezi Septemba mwaka huu yakiwa na lengo la kuwaweka wadau wa uhandisi pamoja kutafakari na kuhamasishana kuhusu namna bora ya kuendeleleza taaluma ya uhandisi kukuza uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini (ERB) Eng. Profesa. Ninatubu Lema kabla ya kufungua kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano la siku moja la wahandisi (hawapo pichani) lililowakutanisha kujadili kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo. Kulia ni Kaimu Msajili wa Wahandisi, Eng. Patrick Barozi.
Sehemu ya wahandisi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akifurahia jambo na wahandisi mara baada ya kufungua kongamano la siku moja la wahandisi kuhusu mchango wa Wahandisi katika Sekta ya viwanda jijini Dodoma leo.

 

RC Wangabo ashauri gereza kutumia ekari elfu 11 kwa kilimo cha alizeti na kahawa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameshauri jeshi la magereza kuhakikisha wanazitumia ekari 11,000 zinazomilikiwa na jeshi hilo kwaajili ya mazao ya alizeti pamoja na kahawa ili jeshi hilo liweze kujipatia fedha za kutatua changamoto mbalimbali walizonazo na kuongeza uzalishaji wa mazao hayo katika taifa.

Amesema kuwa nchi ya Tanzania huagiza asilimia 60 ya mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi wakati jeshi la magereza lina ardhi nzuri na ya kutosha kwaajili ya kuzalisha zao la alizeti kwa wingi na hatimae kupunguza uwingi wa mafuta unaoagizwa kutoka nje na kuokoa mabilioni ya fedha yanayotumiwa na serikali katika kununua mafuta hayo.

“Pamoja na kuinua uchumi lakini pia tunaweza kulisha nchi yetu kwa mafuta, sisi mkoa wa Rukwa tupo katika hali nzuri ya kulima alizeti na kuchangia kupunguza pengo la mafuta yasiendelee kuagizwa kutoka nje, tumejipanga kama Mkoa, karibu kila kaya inayolima iweze kuwa na angalau ekari moja ya alizeti, na kwenye majeshi yetu hapa mna ekari hizi 11,000 mnaweza kuzalisha na kupata ekari za kutosha kutatua changamoto mlizonazo,”Alisema. 

Ameongeza kuwa kwa kuanzia jeshi hilo linaweza kutumia ekari 1000 kuanza kulima na kuona mafanikio yake ndani ya mwaka mmoja kwani kwa mujibu wa Great African Food Company (GAFCO) wanaofanya kilimo cha mkataba hununua kilo moja ya alizeti kwa shilingi 900 huku gunia moja likiwa na kilo 70 na kila ekari moja hupata gunia zisizopungua 15 matokeo yake tunaweza kupata 945,000,000/= na kuwataka magereza kushirikiana na GAFCO ili kufanikisha zozi hilo.

Ameyasema hayo alipofanya ziara fupi katika gereza la Mollo lililopo katika kata ya Mollo, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ili kujionea miradi ya maendeleo ya gereza hilo linalomiliki ekari 11,000 huku wakitumia ekari 400 kwaajili ya kilimo cha mahindi na maharage pamoja na uzalishaji wa mbegu za mahindi.

Kwa upande wake akisoma risala ya gereza Mkuu wa Gereza la Mollo ACP John Mwamgunda amesema kuwa gereza hilo limekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo uchakavu wa vifaa vya kilimo, sare za wafungwa na majengo amabyo ni ya siku nyingi lakini alikubali kuwa uzalishaji wa alizeti ni rahisi zaidi ukilinganisha na uzalishaji wa mahindi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji, Tanzania hutumia Shilingi bilioni 189.6 kila mwaka kununua mafuta ya kula nje ya nchi huku ikizalisha tani 91,000 ambayo ni sawa na asilimia 40 za mafuta hayo tofauti na makadirio ya tani 200,000 hadi 300,000 ya uhitaji wa bidhaa hiyo kwa mwaka.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) akisalimiana na mmoja wa maafisa wa gereza la Mollo lililopo Manispaa ya Sumbawanga muda mfupi kabla ya kutembelea miradi inayoendeshwa na gereza hilo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) akiwashauri Mkuu wa Gereza la Mollo ACP John Mwamgunda pamoja na Kaimu Mkuu wa magereza mkoa wa Rukwa ACP Ihunja juu ya kujikita na kilimo cha alizeti kwa faida ya gereza na faida ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) pamoja na maafisa wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfana Haule (kaunda suti ya kijivu) wakiaangalia moja ya majosho ya mifugo ya gereza hilo.

NICOLAUS WADADA NDANI YA KOMBE KAGAME AKIWA NA KIKOSI CHA AZAM

$
0
0
Na Agness Francis,globu ya Jami.

MABINGWA watetezi wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wapo kambini kujinoa kwa ajili ya maanadalizi ya mwisho kuhakikisha wanatetea kombe lao.

Kikosi hicho kiko tayari kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Kagame kipo chini ya Kocha Iddy Cheche na Juma Mwambusi.

Mashindano hayo yataanza rasmi Juni 29 hadi Juni 13 ambayo siku hiyo kutafanyika ufunguzi rasmi wa michuano hiyo katika dimba la Azam Complex lililopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Ambapo Azam itavaana na timu ya Katori ya Sudani ya Kusini kuanzia saa 10 jioni huku Singinda United wakivaana na APR ya Rwanda Uwanja wa Taifa saa moja usiku.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Azam Jaffary Maganga amesema kikosi chao kipo vizuri na wapo tayari kwa mashindano hayo ambayo kila timu inaliwania kombe hilo.

Amesema kutakuwa na ushindani wa hali ya juu ambapo timu zote zinazoshiriki zina uwezo mkubwa wa kuweza kufanya lolote katika michuano hiyo."Sisi kama mabingwa watetezi wa kombe hilo macho ya watu na timu zingine yanatuangalia sisi tutafanya nini,tutahakikisha tunafanya vizuri katika mashindano haya ili kulietea heshima nchi yetu pamoja na klabu yetu kwa ujumla,"amesema Jaffary.

Msemaji huyo amesema kuwa mchezaji wao mpya Nicolaus Wadada ambaye pia ni miongoni mwa watakaoshiriki mashindano hayo ya Kagame Cup (CECAFA) kutokea nchini Uganda katika klabu ya vipers ameshawasili nchini."Tayari amejumuika kikosini na wenzake kwa ajili ya maandalizi.Pia katika michuano hiyo kuna badhi ya wachezaji watashindwa kushiriki mashindano kutokana na sababu mbalimbali,"amesema.

Amewataja baadhi ya wachezaji hao ni Donald Ngoma,Tafadwa Kuntinyu, Yakubu Mohammed na Daniel Amor.

'UMASIKINI NI MOJA YA SABABU INAYOCHANGIA MIMBA, NDOA ZA UTOTONI'

$
0
0
Na Woinde Shizza ,Mwanza

 IMEELEZWA sababu kubwa inayosababisha mabinti wadogo kujiingiza kwenye vitendo vya kujamiana na hatimaye kupata mimba na ndoa za utotoni ni umasikini katika jamii wanazotoka.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa Kampeni  ya Binti wa kitaa Angello George wakati akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya BINTI  WA KITAA iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mwanza .

Kampeni hiyo inakuja ikiwa ni siku chache toka Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsi ,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndungulile kueleza kuwa tangu Januari hadi Aprili Mkoa wa Shinyanga takribani mimba 18,000 za utotoni zimepatikana.

Hivyo amesema kampeni hiyo itahusisha mikoa yote ya Kanda ya Ziwa naitafanyika kwa muda wa zaidi ya  mwaka mmoja kwa lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba na ndoa za utotoni  nchini.
"Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazosababisha mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,"amesema.

Ameongeza Binti wa kitaa imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 18 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani.
Amesema wanatarajia kwenda kuifanya kampeni katia mikoa zaidi ya 20 nchini huku ikiwa na ajenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa kitanzania.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF) inayoendesha  kampeni ya BINTI WA KITAA   Angelo David George akiwa anazungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Mwanza,namna ya kuepuka mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni  .
Wanafuzi wa shule ya  Mwanza Sekondari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) ambaye pia ni Balozi wa kampeni ya BINTI WA KITAA  Angelo George  wa pili kushoto (Picha na Woinde Shizza,Mwanza) 
Mmoja wa Wazazi alieyehudhuria katika uzinduzi huo, Bi Carol Nzogere akizugumza na wanafunzi

RC MAKONDA VIFAA TIBA KUTOKA KOREA KUSINI

$
0
0
Na Emmaenul Masaka, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amepokea shehena ya vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.milioni 100 kutoka Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika la KOICA.

Makonda amepokea vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam ambavyo ni Digital X-ray tatu, Ultrasound moja, Kabati la usalama wa viumbe (safety cabinet) moja, Mashine tatu za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto watoto njiti (baby warmer) pamoja na mashine ya utakitshaji.

Baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa Balozi wa Korea kusini Bwana Geum Young Song RC Makonda amekabidhi vifaa hivyo kwenye vituo vya Afya vya Sinza, Mnazi Mmoja na Mbagala ambako kuna uhaba wa vifaa. 

Kabla ya kupokea vifaa hivyo RC Makonda alifanya mazungumzo na Balozi huyo wa Korea Kusini na kuwasilisha ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo ya udaktari na uuguzi ambapo Balozi Geum Young Song amepokea kwa mikono miwili ombi hilo.

Makonda pia amemueleza Balozi ombi la kujengwa kwa kituo kikubwa cha upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi kwenye eneo moja ambapo pia Balozi amepokea ombi hilo na kumsifu RC Makonda kwa moyo wake wa kujali wananchi. 

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Geum Young Song amesema wametoa vifaa hivyo kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar es salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya na wataendelea kusaidiana na Serikali.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa makabidhiano ya shehena ya vifaa Tiba mablimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka serikali ya Korea Kusini kupitia shirika lake la KOICA.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Balozi wa Korea kusini,Geum Young Song (kushoto) akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda vifaa hivyo leo jijini Dar as Salaam.
Barozi wa Korea kusini,Geum Young Song (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda vifaa tiba

MCL YAZINDUA JUKWAA LA FIKRA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa “Jukwaa la Fikra” litakalokuwa linakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na wananchi ili kujadili Mada mbalimbali za Kitaifa , Kizalendo,kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu baadhi ya matatizo na changamoto tunazokabiliana nazo kama Nchi.Kulia ni Mkurugenzi wa masoko wa Itv na Redio One, Joyce Luhanse na Mkurugenzi Mtendaji wa Itv na Redio One, Bi Joyce Mhavile.
Mkurugenzi Mtendaji wa Itv na Redio One, Bi Joyce Mhavile(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa “Jukwaa la Fikra” litakalokuwa linakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na wananchi ili kujadili Mada mbalimbali za Kitaifa , Kizalendo,kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu baadhi ya matatizo na changamoto tunazokabiliana nazo kama Nchi.Kushoto ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa magazeti ya Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai.
Picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa “Jukwaa la Fikra” litakalokuwa linakutanisha wadau wa sekta mbalimbali na wananchi ili kujadili Mada mbalimbali za Kitaifa , Kizalendo,kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu baadhi ya matatizo na changamoto tunazokabiliana nazo kama Nchi.

PROGRAMU YA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU NA WANAFUNZI KUKABILIANA NA UKATILI

VOA SWAHILI: New Duniani Leo Juni 27, 2108

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO JUNI 27, 2018

Nimehudhuria Mhadhara Kuhusu Frantz Fanon

$
0
0
Na Profesa Joseph Mbele
Jioni hii nilikuwa St. Paul kuhudhuria mhadhara juu ya Frantz Fanon uliotolewa na Dr. Moustapha Diop. Mhadhara uliandaliwa na Nu Skool, jumuia ya wa-Marekani Weusi ambayo nimewahi kuiongelea katika blogu hii.
Niliona ni lazima nikahudhurie mhadhara huu, ambao mada yake ilikuwa "Becoming Fanon: A Portrait of the Decolonized" kwa kuzingatia umuhimu wa fikra za Fanon katika harakati za ukombozi sehemu mbali mbali za dunia, hasa ukombozi wa fikra.
Nilikutana  na fikra za Fanon kwa mara ya kwanza nilipokuwa mwanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam, katika idara ya Literature. Aliyetufundisha ni mwalimu Grant Kamenju, na vitabu vya Fanon alivyotumia ni The Wretched of the Earth na Black Skin White Masks. Katika kufundisha fasihi ya Afrika, ninaona umuhimu wa kurejea katika firka za Fanon mara kwa mara. Sielewi utakosaje kurejea kwenye fikra za Fanon.

Katika mhadhara wake, Dr. Diop alielezea kifupi maisha ya Fanon, akajikita zaidi katika kufafanua jinsi baina ya mwaka 1956 hadi 1961 Fanon alivyobadilika na kuwa Fanon tunayemjua kama mwanamapinduzi. Fanon alikuja kuwa mwanaharakati hadi akafukuzwa nchini Algeria. Alikwenda Tunisia, ndipo alipoendesha harakati, ikiwemo kuwapiga msasa wapiganaji wazalendo wa Algeria kabla hawajaingia nchini mwao kupambana na jeshi la wakoloni.
Jambo jingine ambalo nimejifunza katika mhadhara huu ni kuwa The Wretched of the Earth hakukiandika, kutokana na hali ya afya yake, bali alimwelezea mke wake kwa mdomo, naye akaandika. Ilichukua miezi kadhaa. Dr. Diop alitoa muhtasari wa mambo muhimu aliyotufundi. Kusoma mengi mengine BOFYA HAPA

JOE WARIOBA AZUNGUMZIA TUKIO LA KIHISTORIA LA KUUNDWA KWA JUMUIYA MPYA UINGEREZA

$
0
0
Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha
Joseph "Joe" Warioba akifafanua kifupi jitihada za kuunganisha Watanzania wa kila aina Uingereza chini ya ulezi wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Dk Asha-Rose Migiro. 
Mkutano huu wa kipekee ulikutanisha Watanzania na marafiki zao zaidi ya 300 mjini Reading Jumamosi 23 Juni 2018 bila ubishani na migongano ya miaka iliyopita. Tukio hili la kihistoria limeweka mikakati ya kimaendeleo- kuacha siasa (na hisia) za kibinafsi na kilafi zilizotupaka matope Walowezi tunaoishi nchi ya Malkia Elizabeth...

WILFRIED BONY AOMBA WARUHUSIWE KUPIGA PICHA KATIKA VIVUTIO ILI KUITANGAZA TANZANIA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Swansea City ya nchinu Uingereza Wilfried Bony akamatwa na polisi baada ya kupiga picha feri.

Bony alikamatwa na polisi baada ya kupiga picha kwenye pantoni feri wakati hairuhusuwi  kupiga picha na kuachiwa baadae.Mshambuliaji huyo alikuja nchini kwa ziara binafsi ikiwemo kufungua  kituo cha michezo , burudani pamoja na kusaidia watoto yatima hususani wanaoishu na ugonjwa wa upungufu wa damu (selimundu).

Akizungumza na Globu ya Jamii, Bony ameiomba  serikali ya Tanzania itoe fursa kwa wageni  wanapofika nchini kupiga picha ili kuweza kutangaza vivutio vya Utalii duniani. Bony amesema kuwa alipata msukosuko wa kushikiliwa na wanausalama akiwa katika pantoni Ferry baada ya kupiga picha ambapo kikawaida hairuhusiwi kufanya kitu hicho.

"Niliambiwa niwafuate baada ya mimi kupiga picha katika pantoni, sikuwa nafahamu kama siruhusiwi kupiga picha ila kwa upande wangu napenda kuwaomba serikali waruhusu watu hususani wageni wapige picha na kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania,"amesema Bony.

"Nimepata changamoto nyingine nikiwa katika mbuga ya wanyama Mikumi nilikataliwa kupiga picha kabisa ila nipate fursa ya kutangaza vivutio hivyo na kama tukija watu wengi basi nchini itakuwa imetangazwa zaidi na watalii kuongezeka,"

Amesema kuwa, anatarajua kurudi tena nchini kwani ameamua kuja kuwekeza nchini kwenye michezo, burudani na kuendelea kutoa misaada kwa watoto yatima na wanaosumbuliwa na ugonjwa wa upungufu wa damu (selimundu).

Kwa upande wa mwenyeji wake Yasmine Razaq amesema kuwa anaomba serikali iweze kuondoa vikwazo mbalimbali kwa wageni ili waweze kutangaza utalii wetu duniani ikiwemo kupiga picha kwenye maeneo yanayoweza kuvutia watalii.Mbali na hilo amepanga kuwaleta wachezaji wengine nchini kutoka Ligi Kuu ya Uingereza kwa ajili kusaidia uwekezaji wa michezo hususani watoto wadogo.

Kampuni ya Asas Diaries waliowezesha mkutano huo wa waandishi wa habari, Msimamizi wa kampuni hiyo Fahad Alli amesema wameamua kutilia mkazo kauli ya serikali ya Hapa Kazi Tu kwa kuamua kujiwekeza kwenye kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo burudani na michezo na tayari wameanza kwa Ali Kiba na Samatta.
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na timu ya Swansea City ya Uingereza Wilfried Bony akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wake uliofanyika leo akielezea madhumuni ya safari yake ya kuja Nchini Tanzania,kulia ni mwenyejiw wake Yasmine Razaq.
Msimamizi wa kampuni ya Asas Diaries  Fahad Alli akiwa na mshambuliaji Wilfried Bony baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi TV: MWANZILISHI WA ZIFF ASIMULIA KILICHOPELEKEA KUANZISHA TAMASHA HILO


Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mh Stephen Masele mkutanoni Nouakchott, Mauritania

$
0
0
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Mh Stephen Masele, akiwasilisha ripoti ya kazi ya Bunge hilo katika kikao cha Umoja wa Afrika (AU)kilichoanza tarehe 25 Juni 2018 huko Nouakchott, Mauritania. 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais PAP.

Mradi wa TASAT nchini umesaidia kujenga Umoja wa Wazanzibari - Mitawi

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdallah Hassan Mitawi alisema kwamba uwepo wa Mradi wa TASAT nchini umesaidia kujenga Umoja wa Wazanzibari bila ya kujali itikadi na imani zao za Dini.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdallah Hassan Mitawi wakati akitoa shukrani kwa Ujumbe wa Wakurugenzi wa Benki ya Dunia katika hafla iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hapo Hoteli ya Sea Cliff Kama.
Alisema tokea kuanza kwa Miradi hiyo wa Kaya Maskini Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Awamu ya Tatu umesaidia kujenga Umoja na kuleta mwamko mpya  wa maendeleo chini ya program ya uwezeshaji wa Kaya hizo.
Akizungumzia umuhimu wa Mradi huo Naibu Katibu Mkuu huyo Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Mfuko huo umesaidia kupunguza Umaskini na kutoa fursa pana kwa Jamii kujiajiri wenyewe.
Ujumbe wa Wakurugenzi 80 kutoka Benki ya Dunia ulikuwepo Nchini Tanzania kwa ziara ya siku Tatu kukagua Miradiinayotekelezwa Nchini ambapo wameeleza kuridhika kwao na jinsi miradi hiyo inavyosimamiwa.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Nd. Abdallah Hassan Mitawi akitoa neno la shukrani kwa Ujumbe wa Wakurugenzi wa Benki ya Dunia baada ya kukamilika kwa Tafrija waliyoandaliwa hapo Sea Cliff  Kama.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia pamoja na wale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali ya Muungano wakiwa katika Tafrija ya pamoja ya kupongezana baada ya kumalizika kwa ziara ya Ujumbe huo wa Benki ya Dunia.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga  akibadilishana mawazo na Mmoja wa Wakurugenzi wa Benki ya Dunia wakipata chakula baada yakumaliza ziara ya Siku Tatu kukagua Miradi ya Maendeleo Visiwani Zanzibar.

TASUBA YATOA UFADHILI KWA WANAFUNZI 20 WA KIKE AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imezindua mpango wa ufadhili wa masomo ujulikanao kama Sanaa tuition fee waiver scholarship kwa wanafunzi 20 kwa mwaka wa masomo 2018/2019.ambapo kwa upande wa Tanzania ufadhili huo utahusu wasichana 10 ,wanafunzi wengine kumi watatoka nchi wa washiriki wa jumuia ya Afrika Mashariki. 

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo wilayani Bagamoyo, Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema “Taasisi imekuja na mkakati wa kutoa ufadhili wa ada ya masomo ili kuweza kuziba mapengo makubwa mawili ambayo yamedhihirika katika utoaji wa mafunzo. 

Kwanza kuna uwiano hasi kati idadi ya wanachuo wa kike na wale wa kiume. Wanachuo wa kike wanaodahiliwa kila mwaka na Taasisi ni wachache sana (chini ya 30%) ikilinganishwa na wa kiume. Pili, pamoja na kupata hadhi ya kuwa kituo cha ubora uliotukuka kwenye ufundishaji katika nyanja za utamaduni na sanaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Taasisi haijaweza kudahili wanachuo kutoa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”alisema Makoye 
 Aliongeza kuwa malengo makuu ya utoaji wa Ufadhili wa ada ya masomo ni Kuwezesha vijana wa kike wa Kitanzania wenye vipaji vya sanaa kupata nafasi ya kunoa vipaji vyao kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa kwenye Taaisisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Lakini pia ni fursa kwa Taasisi kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania na kuingia katika soko na kuuza bidhaa zake kwa raia wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki 
 Naye mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TaSUBa ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Ndg.George Daniel Yambesi aliishukuru TaSUBa kwa ufadhili huo Kwa kuwa umeonyesha njia, kwa sababu ni kweli kabisa kuwa kuna vijana wengi wenye vipaji hasa wa kike ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za masomo. 
 Aidha ndugu Yambesi aliitaka TaSUBa ihakikishe ufadhili huu kweli unakwenda kwa walengwa; yaani vijana wenye vipaji vya sanaa na wana uhitaji wa ufadhili. 
Kwa kufanya hivi matunda ya ufadhili huu yataweza kweli kuonekana baada ya vijana hawa kuhitimu masomo yao. Wakati huo huo ,baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza zimejitolea kufadhili malazi na Chakula kwa kipindi chote cha masomo kwa wanafunzi kumi wa kike kutoka Tanzania watakao faidika na ufadhili huo. Uzinduzi huo ulisindikazwa na onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa na Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa

 Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa  Ndugu George Daniel Yambesi ,akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.

 Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Francis Makoye  akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi.Edda Sanga akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 . Mwenyekiti wa chama cha wabunifu mitindo Ndugu.Merinyo Desumbuka akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.

 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fisoo akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Mwakilishi kutoka Basata Ndugu Onesmo Kayanda akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.

 Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa  Ndugu George Daniel Yambesi akibofya kitufe kuashiria uzinduzi wa ufadhili wa masomo.

 Onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa
 Onyesho la Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa


 Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa  Ndugu George Daniel Yambesi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa tasuba pamoja na waalikwa

DKT. KIMEI AFANYA ZIARAKATIKA MATAWI YA BENKI YA CRDB PLC NYANDA ZA JUU KUSINI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei (wa tatu toka kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa (wa kwanza kushoto) pamoja Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mkwawa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tawi hilo wakati wa ziara ya Mkurugenzi huyo kutembelea matawi ya nyanda za juu kusini katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) akielekezwa jambo na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa wakati walipofika katika tawi la Mkwawa -Iringa kujionea utendaji kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) akipata maelezo machache kutoka kwa meneja wa Tawi la Mkwawa - Iringa Kissa.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei akiwaafa wafanyakazi wa Tawi la Mkwawa - Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kulia) huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei (Kulia) wakati walipofika kumtembelea katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William wakati Dkt. Kimei alipokuwa ziara katika matawi ya nyanda za Juu Kusini.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia picha ya juu) akizungumza na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dkt. Charles Kimei na ujumbe wake walipofika kumtembelea katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William wakati Dkt. Kimei alipokuwa ziara katika matawi ya nyanda za Juu Kusini.

KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA AWATAKA WAAJIRI KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAAJIRI nchini watakiwa kutumia fursa ya uboreshwaji ya mazingira kazi ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje hususani kwenye viwanda kwani Serikali ya awamu ya tano imejizatiti kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua kupitia viwanda.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Ole Sante Gabriel wakati wa mkutano wa mwaka wa 59 wa chama cha waajiri nchini uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Mkutano huo wa mwaka huu ukiwa ni wa 59 uliolenga katika mageuzi ya udhibiti ili kuboresha mazingira ya biashara ikiwemo katika kudhibiti na kupitia sera ya serikali ya awamu ya tano imeweka mkakati wa kuboresha mazingira ya biashara ambayo yatavutia wawekezaji wa ndani na nje.

Ole Sante amefungua mkutano huo uliohudhuriwa na wadau kutoka sekta tofauti alisema ili uchumi ukue unabidi kuwe na mafiga matatu, waajiri, wafanyakazi na serikali kwa pamoja wanashirikiana kukuza uchumi.

"Katika bajeti ya mwaka 2018/19 Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango amezitaja changamoto zinazokwamisha uwekezaji na mazingira ya kibiashara ikiwemo sheria na kanuni za uanzishaji wa biashara, gharama kubwa za kodinna ada," amesema Prof Ole Sante Gabriel.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dr Aggrey Mlinuka amesema kuwa kila mwaka wamekuwa wanafanya mkutano huu wa wanachama na mwaka huu wameangalia zaidi mageuzi ya kibiashara ili kuweza kuyaboresha kwa kusaidana na serikali ili kuvutia zaidi wawekezaji.

Dr Mlinuka amesema kuwa umedhamiria kuboresha mazingira mazuri kwa wafanyakazi ikiwemo mifuko ya jamii ya wafanyakazi na sekta ya afya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof Ole Sante Gabriel akizungumza na waajiri kutoka sekta mbalimbali Nchini wakati wa mkutano wa 59 wa mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Jayne Nyimbo akizungumza na waajiri kutoka sekta mbalimbali Nchini wakati wa mkutano wa 59 wa mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Nchini (TUCTA) Dr Yahya Msigwa akizungumza na wadau kutoka sekta mbalimbali za waajiri na kuelezea changamoto wanazokabiliwa nazo wafanyakazi kwenye mkutano uliofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dr Aggrey Mlinuka akizungumza na waandishibwa habari kuhusiana na mkutano wa 59 wa mwaka wa Chama cha Waajiri ukiwa na madhumuni ya mageuzi katika kuboresha utendaji kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezekaji Prof Ole Sante Gabriel akiwa katika Picha ya pamoja na wadau wa sekta ya waajiri nchini.


Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images