Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 28, 2018

MAJALIWA AZINDUA VITUO 51 VYA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA WILAYNI BAHI

$
0
0
WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji watumie taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.Amesemakuwa kuongezeka kwa vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87 kama inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”.

“Vituo hivi ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”. Amesema kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa maji kwenye mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini ambavyo vinajiendesha vyenyewe.

“Pia, mradi huu umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na taarifa za mafuriko na ukame na taarifa za hali ya hewa na kuondoa ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja kwenda Wizara nyingine,” amesema. Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili ziweze kufuatilia na kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza muda wao.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa vituo na mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa usimamizi bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, Wabunge na Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bibi Natalie Boucly.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wanne kushoto ni Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo cha kupima wingi wa mvua baada ya kuzindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama,Waziri wa Maji, Mhandisi Isaack Kamwele, Mwakilishi Mkaazi wa  Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Dodoma, Felista Bura.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe wakati alipozindua vituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Airtel announces AMSHA AMSHA NA AIRTEL MONEY USHINDE winners

$
0
0
Airtel Tanzania the smartphone network in partnership with SportPesa has today announced the first winners of The “AMSHA AMSHA NA AIRTEL MONEY USHINDE” promotion which was launched on 14th June this year. The winners have won their prizes as a result of betting through Airtel Money.

Speaking in Dar es Salaam today during a draw to announce the winners, Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando said that the draw to select winners under the supervision of the Gaming Board of Tanzania which is authorized to control all gaming games in the country.

As you can see, the draw has been open to everyone and is very fair which means every Airtel customer betting through Airtel Money stands a chance to be a winner. ‘ All what Airtel Money customer will need to do is simply place a bet within the promotion period to enter the draw, said Mmbando adding that customers must make sure that the SportPesa wallet is prefunded with funds for betting.

Mmbando said that the first winners of the draw are ten customers who have won each a brand new latest smartphone; ten others have each won original jerseys for Simba and Yanga Sports Club while ten others have each won a ticket to attend Simba and Yanga matches for the entire season of 2018/2019. I call upon Airtel customers to come up and participate to this AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion as there are other many prizes yet to be won, said Mmbando adding that one customer has also won a brand new 32 inch color televisions.

AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL gives an opportunity for Airtel to reward its loyal Airtel Money users through this consumer promotion. ‘Airtel has been introducing innovative services and products that are exciting and interactive to create a firm bond with our customers. We are aware of the love for sports and betting that has become a lifestyle for most of our customers, said Mmbando.

On his part, SportPesa Public Relations Manager Subrina Msuya said since the launch of AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion launch on 14 June this year, the entry for each day starts at 00.00 HRS and close at 23.59 HRS for the whole duration of the promotion and what Airtel customer will need to do to participate is to bet on the day that there is a draw and automatically their number will enter into the weekly draw. ‘

Ms Msuya named prizes which are being won on daily basis as smartphones, Jerseys for Simba and Yanga clubs, match tickets to watch Simba and Yanga games for the entire season while weekly draws are 32 inch color televisions and Decoders from Star Times.All what a customer will be required to do is to enroll, top up SportPesa wallet using Airtel Money Waller and proceed to place a bet said Msuya adding that winners can collect their prizes from any Airtel Shop branch across the country.

Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando displays some of winning prizes that where won by winners of the first draw of the AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion today in Dar es Salaam. He is flanked by SportPesa Public Relations Manager Sabrina Msuya – left and Tanzania Gaming Board official Ahmed Hemed. To participate, a customer will be supposed to dial *150*60# then transfer money to SportPesa wallet 150888 and press a bet.
SportPesa Public Relations Manager Sabrina Msuya speaks during the first draw of the AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY promotion today in Dar es Salaam. She is flanked by Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando - center and Tanzania Gaming Board official Ahmed Hemed. To participate, a customer will be supposed to dial *150*60# then transfer money to SportPesa wallet 150888 and press a bet.
Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando speaks to one of the winners of the AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY today in Dar es Salaam. To participate, a customer will be supposed to dial *150*60# then transfer money to SportPesa wallet 150888 and press a bet. He is flanked by Tanzania Gaming Board official Abdallah Hemed.

Benki ya Barclays yazindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao kwa wateja wake wadogo na wa kati

$
0
0
Mtaalamu wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya Barclays Tanzania (BBT), Jesse Jackson (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma za kinbenki kwa njia mtandao wa intaneti kwa wateja wadogo na wa kati jijini Dar esSalaam jana. Kushoto ni Msimamizi wa Hduma za Kidigitali, Emmanuel Wangwe na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakati, Ahmed Khamis. 

BALOZI SEIF ALI IDD APONGEZA UTENDAJI KAZI WA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASAF.

$
0
0
Na Estom Sanga- TASAF

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema mchango unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF katika shughuli za maendeleo hususani katika jitihada za kupunguza umaskini wa wananchi ni za kupongezwa kwani unatekelezwa kwa kuzingatia sera za serikali za kupambana na umaskini.

Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Maafisa Waandamizi wa Benki ya Dunia waliokuwako kisiwani Zanzibar pamoja na mambo mengine kuona namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAFwanavyonufaika , amesisitiza kuwa maisha ya Walengwa wanaonufaika na huduma za Mpango huo yameboreshwa na kuwawekea msingi imara wa kujitegemea.

Amesema TASAF ni kielelezo stahiki cha namna serikali inavyowajali wananchi hususani wanaoishi katika umaskini uliokithiri kwa kuwawekea mazingira ya kufanya kazi za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato huku pia mkazo ukiwekwa katika sekta za Elimu, Afya na Lishe kwa kaya za Walengwa.

Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pia amesema mchango wa kaya za Walengwa katika ukuaji wa uchumi umeanza kuonekana kutokana na shughuli wanazozifanya hasa katika nyanja za kilimo cha Mpunga, bustani ,ususi na ufugaji wa kuku wa kienyeji na mbuzi kwa kutumia ruzuku kutoka TASAF masuala ambayo amesema yanawaongezea kipato .

Akitoa mfano,Balozi Seif amesema miradi mingi iliyoanzishwa na Wananchi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} na kupata msukumo wa Benki ya Dunia imeleta ukombozi kwa Wananchi walio wengi kisiwani humo.Mapema Mkurugenzi Mtendaji TASAF} Ladislaus Mwamanga amesema kazi kubwa inayofanywa na Wananchi wa Zanzibar kwenye miradi ya Maendeleo kupitia programu zinazosimamiwa na Mfuko huo imeleta mafanikio makubwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Maafisa wa Benki ya Dunia,TASAF na serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya mchango muhimu wa TASAF katika kukabiliana na umaskini nchini. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akishukuru ushirikiano uliopo kati ya SMT,SMZ na Benki ya Dunia uliosaidia kuzikomboa Kaya Maskini Nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga akipongeza usimamizi mzuri wa serikali katika kufanikisha shughuli za taasisi hiyo kwenye hafla iliyohudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Maafisa wa Benki ya Dunia.
Mkurugenzi na Mkuu wa Mtandao wa Masuala ya Kijamii na Ajira wa Benki ya Dunia Bwana Michal Rutkowski akizungumza kwenye hafla iliyohudhuriwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Balozi Seif Ali Idd (walioketi katikati )akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Benki ya Dunia baada ya kutoa hotuba kufuatia ziara ya maafisa hao ksiwani Zanzibar kuona shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUMALIZA TATIZO LA MAFUTA YA KULA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kufanya mageuzi makubwa katika zao la michikichi, alizeti na ufuta.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Balozi Dkt. Ramadhan Dau ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.’’Tunataka kufanya mageuzi makubwa ya zao la michikichi, tunataka kuondoa miti ya zamani na kupanda miche mipya. Tutafanya kampeni ya kuhamasisha upandaji wa miche mipya ya michikichi ili tuondoe tatizo la upatikanaji wa mafuta nchini,’’.

Waziri Mkuu amesema licha ya kuwepo kwa michikichi mingi nchini ila uzalishaji wake unafanyika kwa njia kienyeji, hivyo Serikali imedhamiria kuboresha kilimo hicho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili liweze kuleta manufaa makubwa kwa Taifa na wakulima.

Amesema mbali na zao la michikichi, pia Serikali imedhamiria kuboresha mazao mengine ya mbegu za kukamua mafuta kama alizeti na ufuta, ambayo itayafuatilia kuanzia hatua za awali za uandaaji wa mashamba hadi masoko.Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania bado ipo chini kwenye uzalishaji wa mbegu za kukamulia mafuta na inahitaji wawekezaji katika mazao hayo, hivyo amemuagiza Balozi wa Tanzania nchini Malaysia atafute wawekezaji hao.

’’Inawezekana kujitosheleza kwa mafuta ya kula kwa sababu Tanzania tuna ardhi ya nzuri yenye rutuba na watu ambao kilimo ndiyo shughuli yao kubwa. Na hivi karibuni nitafanya ziara mkoani Kigoma kwenda kuhamasisha kilimo cha michikichi,’’.Kwa upande wake, Balozi Dkt. Dau amesema Malaysia ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kilimo cha michikichi na inatengeneza zaidi bidhaa 400 kutokana na zao hilo, yakiwemo mafuta ya kuendeshea magari.

Balozi Dkt. Dau amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba atatafuta wawekezaji kutoka nchi za Malaysia na Indonesia ili waje kuwekeza kwenye mashamba na viwanda vya mafuta na sukari.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Juni 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MEYA TEMEKE ATAKA WANAOPEWA MIKOPO KUITUMIA KWA MALENGO WANAOPEWA MIKOPO TEMEKE WATAKIWA

$
0
0

MEYA wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Chaurembo amevitaka vikindu vya ujasiriamali vilivyopo ndani ya halmashauri ya hiyo kutumia mikopo wanayopata kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi.

Chaurembo amesema hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi vikundi vya ujasiriamali wilayani Temeke na kukabidhi hundi ya mkopo ya Sh.6000,000 ambazo zilitolewa kwenye vikundi vitatu vya Jitihada, Ismail, pamoja na maendeleo ambao umetolewa na taasisi ya muungano wa vikundi vya vicoba Tanzania (VIGUTA)

Chaurembo amevitaka vikundi hivyo kwenda kutumia vizuri fedha hizo ili kufikia malengo yao huku akiwataka kuepuka kutumia fedha hizo kwa anasa na starehe zingine zisizonafaida.

" Tunawapongeza Viguta kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya kwani wamekuwa ni mkombozi kwa wajasiliamali wadogo wadogo hivyo niwaomba ndugu zangu wanavikundu mkatumie fedha hizi kwa malengo ambayo mmejiwekea,"amesema Chaurembo. Pia ameongeza kuwa mikopo hiyo wanayopewa ni ya riba nafuu hivyo kila mmoja akawe mlinzi wa mwingine ili kuhakikisha marejesho yanarejeshwa kwa wakati ili kuwezesha wengine kupata mikopo hiyo.

Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaurembo, katikati akimkabidhi hundi ya mkopo ya shilingi milioni 6,000,000 Mwenyekiti wa kikundi cha ujasiliamali cha Simle Vikoba, Emaculata Mbassa (kushoto), katika uzinduzi wa vikundi vya ujasiliamali wilayani Temeke Dar es Salaam jana. ambazo zilitolewa kwenye vikundi vitatu vya Jitihada, Ismail, pamoja na maendeleo kutoka kwa taasisi ya muungano wa vikundi vya vicoba Tanzania (VIGUTA)

Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti Taifa VIGUTA Dkt. Dauda Salmin,akifafanua jambo mbele ya wana chama wa vikundi mbalimbali vya (VIGUTA) Wilayani Temeke Dar es Salaam jana,katika uzinduzi wa vikundi vya ujasilia mali.
Baadhi ya wanachama wakimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti Taifa VIGUTA Dkt. Dauda Salmin,hayupo pichani katika uzinduzi vikundi vya ujasiliamali wilayani Temeke Dar es Salaam jana.



UPELELEZI SHAURI LA MAUAJI MMILIKI WA SHULE YA SEKONDARI SCOLASTICA WAKAMILIKA

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ,Moshi imeelezwa upelelezi wa shauri la mauaji linalomkabili mmiliki wa shule ya sekondari ya Scolastica umekamilika.

Wakili wa serikali anayeiwakilisha Jamhuri katika shauri hilo, Agatha Pima aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo la mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi Humphrey Makundi umekamilika kwa asilimia 100.

Baada ya maelezo hayo,wakili wa upande wa utetezi anayemtetea mtuhumiwa wa pili katika shauli hilo,Edward Shayo,Elikunda Kipoko aliwasilisha ombi mbele ya mahakama hiyo kutoa kibali cha kuruhusu mteja wake kupatiwa matibabu kutokana na ugonjwa unaomsumbua.Hata hivyo ombi hilo lilikataliwa na Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi,Julieth Mawole akieleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa kibali kwa mtuhumiwa huyo.

Hakimu Mawole ameeleza kuwa kila mtu ana haki ya msingi ya kupatiwa matibabu lakini mahakama hiyo haina mamalaka ya kutoa kibali kwa mtuhumiwa huyo na kwamba suala hilo liko Magereza.Aidha Mawole alieleza kuwa mchakato wa kuhamisha jalada la kesi ya mauaji kwenda mahakama kuu utafanyika June,29 mwaka huu.

Hatua ya upelelezi kukamilika unafikiwa baada ya watuhumiwa hao kukaa rumande kwa zaidi ya miezi saba wakati wakiendelea kusubiri kukamilika kwa upelelezi huo.Shauri hilo la mauaji ya kukusudia linawakabili, mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scholastica pamoja mlinzi wa shule hiyo,Hamis Chacha na mwalimu wa shule hiyo Laban Nabiswa .

Mnamo Novemba 6,mwaka jana Mwanafunzi huyo ,mwili wake ulikutwa umetupwa mto Ghona mita 300 kutoka eneo la shule hiyo ambapo mwili huo ulizikwa katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Novemba 12,mwaka jana.

MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma amewaongoza wananchi na viongozi wa CCM na Serikali wa mkoa wa Simiyu katika mazishi ya aliyewahi kuwa mbunge wa Bariadi, Mkuu wa Wilaya katika maeneo mbalimbali hapa nchini,ambaye pia alikuwa Katibu wa Itikadi  na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. Danni Makanga, ambayo yamefanyika katika Mtaa wa  Kidulya Mjini Bariadi .

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Gachuma ametoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huo, huku akiwaasa ndugu na familia kuendelea kuishi maisha ya umoja na kushirikiana.

Aidha, Gachuma amepongeza mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano uliopo kati ya Viongozi wa Chama na Serikali katika masuala yote ikiwa ni pamoja na misiba na akikiri kuwa yeye pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wake(Mara) walioongozana naye wamejifunza jambo hilo kutoka Simiyu.

"Napenda niupongeze uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa namna  mnavyoshirikiana, msiba wa ndugu yetu Makanga mmeubeba wote kwa pamoja  tumeona kuna umoja na ushirikiano kati ya viongozi wa Chama na Serikali hili ni jambo jema sana ,  bahati nzuri nimefuatana na Katibu Mwenezi wangu wa Mkoa utaratibu huu na sisi tunaubeba kama somo" alisema Gachuma.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za rambirambi ametoa pole kwa familia na kuwaomba ndugu na familia waendelee kuwa wamoja na wasikubali kugawanywa kwa namna yoyote, huku akielezea kuwa CCM imempoteza mtu muhimu makini sana ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika Chama, Serikali na Taifa kwa ujumla.
 Vijana wa Green Guard wa CCM akiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga kuelekea eneo la mazishi ambayo yamefanyika katika Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi Mkoani humo.
 Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga likiteremshwa kaburini kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika katika Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi Mkoani humo
 Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, . Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma wakiweka udongo katika kaburi alizikwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga amabye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kupitia Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe. Tano Mwera na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga Mjini Bariadi.
 Padri wa Kigango cha Mtakatifu Michael Kidulya, Parokia ya Mtakatifu Luka Bariadi, James. Kitasanja akitoa mahubiri katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa la aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KIGWANGALLA APOKEA TAARIFA YA AWALI YA KAMATI YA KOVA KUHUSU TUHUMA ZA MAUAJI YA TEMBO

$
0
0


VIDEO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda (kulia). Tuhuma hizo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Naibu Waziri, Japhet Hasunga (katikati) wakipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) na Naibu Waziri, Japhet Hasunga (wa pili kulia) wakipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Julius Kibebe, Kresensia Swai na Emmanuel Musamba (kushoto). 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda taarifa hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa mapendekezo ya kamati hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wajumbe wa kamati maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma za mauaji ya Tembo ambazo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili. (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii).

NEWZ ALERT: NOAH YAUA WATANO MTWARA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA- MTWARA

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujerehiwa Vibaya kutokana na ajali ya gari kuacha barabara Kuanguka na kisha Kuwaka moto katika barabara ya Mangaka/Tunduru kijiji cha chigweje Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 10 jioni ikihusisha gari aina ya Toyota Noah yenye namba  za usajili T.485 DJE iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka Mangaka kwenda Tunduru ambapo Gari hiyo iligonga Gema na kupinduka eneo Lumesule ambalo lina kona na mteremko mkali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amesema Jumla ya watu watano wameungua mmoja ni dereva wa gari lakini wengine wanne hawajatambulika hivyo kuwaomba wananchii kujitokeza na kwenda kuwatambua Ndugu zao.

“Tunaomba wananchi wanaohisi kupotelewa na ndugu zao ambao walikuwa wanatambua kwamba nduguzao jana walikuwa na safari ya kutoka mangaka kwenda Tunduru na kama hawajafika nyumbani basi waende Hospital ya Mkoamaindo wilaya ya masasi kwa ajili ya kutazama miili yao.Amesema kamanda Mkondya.

Aidha Kondakta wa gari hiyo Khalid Maneno aliruka kutoka kwenye gari hiyo kabla ya kutokea ajali na hivyo anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa lengo la kusaidia kukamilisha Upelelezi

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva na kutokana na mteremko na kona kali na hivyo kushindwa kuimudu na kupelekea ajali hiyo.
.Muonekano wa gari aina ya Noah iliyokuwa ikufanya safari zake kutoka Manganka kwenda Tunduru baada ya kuungua na kuteketea.
 Baadhi ya wananchii wa kijiji cha Chingweje wilaya ya nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakitazama Gari aina ya NOAH mara baada ya kugonga gema la barabara na Kupinduka kisha kuwaka moto na kusababaisha watu watano kufariki.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI SIMIYU FESTIVAL 2018

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu,

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio kubwa linalojulikana kwa jina la Simiyu Jambo Festival, ambalo linatarajiwa kufanyika Julai 8 mwaka huu katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo kwa mwaka huu 2018 linafanyika kwa mara ya pili

Tukio hilo ambalo linafanyika kwa mara ya pili , limebeba vipengele vikuu vinne vya mashindano ambavyo ni mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili( wagika na wagalu), mbio fupi kilomita 10 kwa wanaume na wnawake, mbio za uwanjani kwa watoto na uandishi wa insha ambapo kauli mbio yake ni Familia Yangu, Afya Yangu, Furaha Yangu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati ya uzinduzi wa tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kuwa tukio hilo, linalengo la kukuza vipaji kwa vijana wa Mkoa wa Simiyu na kutangaza tamaduni za kabila la Kisukuma na kwamba litahusisha wananchi wote kutoka mikoa mbalimbali.

“Tutakuwa na mashindano ya mbio za baiskeli kilomita 150 wanaume, kilomita 100 wanawake, kilomita 11 watu wenye ulemavu, mbio fupi za kilomita 10 wanaume na wanawake, mbio za watoto za uwanjani, uandishi wa insha kwa wanafunzi na zaidi ya shilingi milioni 22 zitashindaniwa nitoe wito kwa Watanzania wote hususani vijana kuchangamkia fursa hii” alisema Mtaka
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo kuhusu, Simiyu Jambo Festival inayotarajiwa kufanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Vinywaji Bariadi ya Jambo (Jambo Food Products Company), Anthony Paul akisoma zawadi zitakazotolewa kwa washindi watakoashiriki katika matukio tofauti ya Simiyu Jambo Festival,ambalo litafanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia idadi ya watu (UNFPA) Mkoa wa Simiyu Dkt Amir Ibrahimu akitoa taarifa ya ushiriki wa Shirika hilo katika Simiyu Jambo Festival, ambalo litafanyika Julai 08, 2018 mjini Bariadi.

AGIZO LA WAZIRI UMMY MWALIMU LAANZA KUTEKELEZWA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu – Dodoma

Agizo alililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu la kuanzishwa kwa madawati ya kijinsia katika shule za Msingi na Sekondari nchini alilotoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike Novemba 2017 Mkoani Mara limeanza utekelezaji wake.

Utekelezwaji wa agizo hilo umeanza kwa kuanzishwa kwa Programu ya kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi wa shule za Sekondari katika kukabiliana na  ukatili shuleni ambapo ndipo vitendo vingi vya ukatili ufanyika.

Programu hiyo iliyoanzishwa na Shirika la World Education na kuishirikisha Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye lengo la kuwajenga uwezo watendaji wanatekeleza afua za ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kuwa na mbinu za kuzuia, kuchukua hatua na kushughulikia wahanga wa ukatili shuleni.

Akifungua kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu hiyo jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Marcel Katemba amesema kuwa Programu hiyo itasaidia kwa asilimia kubwa  kuweka mazingira salama na rafiki kwa watoto kusoma bila kusumbuliwa na  aina yoyote ya ukatili shuleni.

Ameongeza kuwa kupitia vitini vilivyopo katika Programu hiyo vitasaidia kuongeza weledi wa walimu kwa kubadili mitazamo na tabia zao na kuwa zenye nia ya kupinga vita ukatili na kuwa tayari kushughulikia vitendo vya ukatili punde vinapotokea.
 Kaimu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba akifungua kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Margareth Mussai akielezea jinsi ukatili kwa watoto unavyoleta  athari kubwa kwa watoto wakiwa wadogo na wanapokuwa watu wazima katika kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Mtaalamu wa masuala ya Elimu kutoka Shirika la World Education, Grace Muro akitoa taarifa ya hali ya ukatili kwa watoto ya mwaka 2011 ikionesha kuwa msichana 1 kati ya 3 na mvulana 1 kati ya 7 walifanyiwa ukatili wa kingono kabla hawajafikisha miaka 18 katika kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la World Education Tanzania, Lilian Badu akielezea dhumuni la Shirika lake kutekeleza Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni katika kikao kati ya Serikali na Shirika hilo kujadili Programu hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Mtaalamu wa Masuala ya Kijinsia kutoka Shirika la Plan International Tanzania Dkt. Katanta Simwanzi akielezea masuala mbalimbali ya ukatili wa kijinsia na jinsi uanvyoleta madhara kwa jamii katika kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wadau kutoka Shirika la World Education wakijadilaina kuhusu utekelzaji wa Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 sambamba na Mpango kazi wa Mwaka 2018-2019, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma (katikati) akisoma muhtasari wa  Utekelezaji wa Mpango kazi  wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 katika kikao cha siku moja cha Uongozi kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Mmanga Mjengo Mjawiri.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Dkt.Idrisa Muslim Hija (kulia) akifafanua jambo wakati wa  kikao cha siku moja cha Uongozi katika utekelezaji wa Mapngo kazi wa Mwaka 2017-2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwepo na Mshauri wa Rais Ushikiano wa Kimataifa na Uchumi Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto).
 Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na  Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee akichangia pamoja na kutoa maelezo wakati wa  kikao cha siku moja cha Uongozi cha utekelezaji wa Mapngo kazi wa Mwaka 2017-2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma (kushoto).
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akisisitiza jambo wakati wa  kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika utekelezaji wa Mapngo kazi wa Mwaka 2017-2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Wasaidizi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakiwa katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 na Mpango kazi wa Mwaka 2018-2019 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Wakurugenzi katika Idara za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kikao cha utekelezaji wa Mapngo kazi wa Mwaka 2017-2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu)


Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika

$
0
0
Takribani wateja 500,000 wanatembelea Jumia ndani ya mwezi katika mwaka huu 2018, kutoka wastani wa wateja 250,000 kwa mwezi mwaka 2017.Makampuni ya Kiafrika zaidi ya 60,000 na wafanyabiashara wamejiunga na Jumia. 

Ikiwa na dhamira ya kutengeneza mustakabali wa mazingira mazuri ya masoko na fursa za kuuza na kununua bidhaa pamoja na huduma za mtandaoni na kifedha, Jumia inaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya huduma za manunuzi ya mtandaoni barani Afrika.

Ikiwa imeanzishwa mwaka 2012, Jumia inajivunia kufanya kazi na makampuni zaidi ya 60,000 ya Afrika pamoja na wafanyabiashara wa kiafrika kwenye mtandao wake.

Akizungumzia juu ya shamrashamra za maadhimisho haya yakatakayodumu kuanzia Julai 2 mpaka Julai 15 mwaka 2018, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott amebainisha kuwa sherehe za mwaka huu zimekuja sambamba na sikukuu za Sabasaba hivyo kutoa fursa zaidi kwa wateja kununua bidhaa mbalimbali kwa gharama nafuu na ofa lukuki.

“Sabasaba ni maonyesho makubwa ya kibiashara siyo tu nchini Tanzania bali kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ujumla. Ni muhimu kwa wafanyabiashara na wateja ambapo hupata fursa ya kufanya maonyesho ya bidhaa na huduma tofauti, kuuza na kununua bidhaa mbalimbali. Kwa maneno mengine, Jumia ni kama maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika kwa njiaya mtandao. 

Siku zote Jumia ina aina tofauti za bidhaa zinazopatikana kwa bei nafuu kabisa. Kwa hiyo sherehe za Jumia kwa mwaka huu itashiriki maonyesho ya Sabasaba, na kuwapatia wateja (watakaokuwepo Sabasaba na maeneo mengine) fursa ya kununua bidhaa kwa punguzo kubwa la bei, kujishindia zawadi, vocha za manunuzi na ofa kemkem kutoka mtandaoni na washirika wetu,” alisema Bw. Prescott.
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 6 ya Jumia barani Afrika na uzinduzi wa kampeni ya Sabasaba. Kulia ni wawakilishi kutoka kampuni ya simu ya FERO, ambao ni mojawapo ya washirika wa Jumia katika maonyesho ya Sabasaba mwaka 2018.

  Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionesha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba katika banda  la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini katikati ni muwakilishi mwenza kutoka FERO huku kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James.
 Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionEsha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba katika banda  la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini kutoka kulia ni muwakilishi mwenza kutoka FERO huku akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James na Msimamizi wa Atsoko, Bi. Lisa Kameja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza

$
0
0
          Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka wahandisi nchini kujiongeza katika kutafuta fursa mbalimbali zikiwemo za ujasiriamali ili kujiongezea kipato.

Mwijage ameyazungumza hayo jijini Dodoma wakati akizindua Kongamano la Wahandisi zaidi ya 300 lililohusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). 

Waziri Mwijage amesema kuwa hakuna mtu anaezuiliwa kufanya kazi nyingine tofauti na aliyosomea hivyo hata Wahandisi wanaweza kufanya ujasiriamali wa aina yoyote.  ”Nawaomba Wahandisi kuchangamkia fursa pindi zinapotokea, mjitahidi mpate elimu ya ujasiriamali kwani Serikali itawatumia hata mkiwa katika Taasisi Binafsi", alisema Mwijage.

Aidha, Waziri Mwijage ametoa rai kwa Wahandisi kuungana kufanya kazi kwa pamoja bila ubaguzi ili kuwa pamoja katika ujenzi wa viwanda utakaopelekea nchi kuwa na uchumi wa kati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema amesema kuwa moja ya majukumu ya CRB ni kuhamasisha shughuli za uhandisi hasa katika shule na Vyuo Vikuu mbalimbali ili kwa miaka ijayo nchi ipate Wahandisi wengi watakaojenga miundombinu mbalimbali.

”CRB imesajili jumla ya Wahandisi 21,746, tunatoa rai kwa Serikali kuendelea kutuamini kwa kutoa fursa zaidi kwa Wahandisi wa ndani kujenga miradi ya ujenzi inayoanzishwa nchini,” alisema Prof. Lema.

Bodi ya Usajili wa Wahandisi imeanzishwa kisheria mnamo Oktoba 10, 1968 kwa lengo la kusajili na kusimamia aina zote za Wahandisi na kukuza maendeleo ya uwezo wao kwa lengo la kulinda watumiaji wa huduma za ujenzi nchini.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na Wahandisi (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). Kongamano hilo limefanyika jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akitoa neno fupi la kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). Kongamano hilo limefanyika jijini Dodoma.
 Kaimu Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi akizungumza na Wahandisi (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). Kongamano hilo limefanyika  jijini Dodoma.
Baadhi ya Wahandisi walioshiriki katika Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). Kongamano hilo limefanyika jijini Dodoma.

WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT

$
0
0


JOSEPH MPANGALA,MTWARA

Wawakilishi wa Baraza la usafirishaji Korosho Kutoka Nchini India (CEPCI) wamefanya ziara Mkoani Mtwara na kukutana na wadau wa usimamizi,ununuzi na usafirishaji wa zao la Korosho kwa leno la kujadiliana namna bora ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Biashara ya zao la Korosho kati ya nchi ya Tanzania na India.

Mkutano huo wa siku moja, umefanyika katika ofisi za Bodi ya Korosho TanzaniaCBT Mkoani Mtwara na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Vyama vya ushirika, wanunuzi wa Korosho, Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA),pamoja na Mjumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini India.

Aidha Mkutano huo umejikita katika kujadili changamoto zinazojitokeza wakati wa kununua na kusafirisha Korosho kutoka Tanzania kwenda Nchini India ambazo ni pamoja na kuzingatia kwa ubora na uaminifu wa wasafirishaji. Mwenyekiti wa CEPCI Ktuoka Nchini India Raghavanpillai Bhoocles ameishukuru Bodi ya Korosho Tanzania kwa juhudi inazozifanya katika kusimamia Sekta ya Korosho Nchini,Na kushauri kufanyika kwa mikutano ya Mara kwa Mara kwa lengo la kuondoa changamoto chache zinazojitokeza.

Kwa upande wake Meneja wa udhibiti Ubora kutoka CBT Bw.Ray Mtangi amewahakikishia wawakilishi hao kutoka Nchni India kwamba tayari Serikali imeshaanza kushughulikia changamoto zilizojitokeza katika msimu wa Korosho uliopita wa 2017/2018 na kuahidi Kuzifanyia kazi

“Changamoto Chache zilizojitokeza katika Msimu Uliopita tayari Serikali imenza kuzifanyia kazi na tayari Tumejipanga ili kuhakikisha Changamoto Hizo Kutojitokeza tena katika Msimu Unaokuja”Amesema Mtangi

Meneja Uthibiti Ubora Kutoka Bodi ya Korosho CBT Ray Mtangi Akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya CBT na wajumbe wa Wakala wa Usafirishaji wa korosho kutoka nchini India uliofanyika Mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Cashew Export Promotioncouncil of India {DEPCI} akizungumza katika mkutano wa pamoja na Bodi ya Korosho Jinsi ya Kuondokana na Changamoto katika Ununuzi na Usafirishaji wa Korosho.

Washiriki wa Mkutano wa wakijadili juu ya namna ya kuimarisha Uhusiano na kuboresha usafirishaji wa korosho kutoka Tanzania kwenda nchini India.

RC Wangabo ashauri gereza la Mollo kutumia ekari elfu 11 kwa kilimo cha alizeti na kahawa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameshauri jeshi la magereza kuhakikisha wanazitumia ekari 11,000 zinazomilikiwa na jeshi hilo kwaajili ya mazao ya alizeti pamoja na kahawa ili jeshi hilo liweze kujipatia fedha za kutatua changamoto mbalimbali walizonazo na kuongeza uzalishaji wa mazao hayo katika taifa.

Amesema kuwa nchi ya Tanzania huagiza asilimia 60 ya mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi wakati jeshi la magereza lina ardhi nzuri na ya kutosha kwaajili ya kuzalisha zao la alizeti kwa wingi na hatimae kupunguza uwingi wa mafuta unaoagizwa kutoka nje na kuokoa mabilioni ya fedha yanayotumiwa na serikali katika kununua mafuta hayo.

 “Pamoja na kuinua uchumi lakini pia tunaweza kulisha nchi yetu kwa mafuta, sisi mkoa wa Rukwa tupo katika hali nzuri ya kulima alizeti na kuchangia kupunguza pengo la mafuta yasiendelee kuagizwa kutoka nje, tumejipanga kama Mkoa, karibu kila kaya inayolima iweze kuwa na angalau ekari moja ya alizeti, na kwenye majeshi yetu hapa mna ekari hizi 11,000 mnaweza kuzalisha na kupata ekari za kutosha kutatua changamoto mlizonazo,”Alisema.  

Ameongeza kuwa kwa kuanzia jeshi hilo linaweza kutumia ekari 1000 kuanza kulima na kuona mafanikio yake ndani ya mwaka mmoja kwani kwa mujibu wa Great African Food Company (GAFCO) wanaofanya kilimo cha mkataba hununua kilo moja ya alizeti kwa shilingi 900 huku gunia moja likiwa na kilo 70 na kila ekari moja hupata gunia zisizopungua 15 matokeo yake tunaweza kupata 945,000,000/= na kuwataka magereza kushirikiana na GAFCO ili kufanikisha zozi hilo.

Ameyasema hayo alipofanya ziara fupi katika gereza la Mollo lililopo katika kata ya Mollo, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ili kujionea miradi ya maendeleo ya gereza hilo linalomiliki ekari 11,000 huku wakitumia ekari 400 kwaajili ya kilimo cha mahindi na maharage pamoja na uzalishaji wa mbegu za mahindi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(mwenye kofia nyekundu) akisalimiana na mmoja wa maafisa wa gereza la Mollo lililopo Manispaa ya Sumbawanga muda mfupi kabla ya kutembelea miradi inayoendeshwa na gereza hilo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo(kulia) akiwashauri Mkuu wa Gereza la Mollo ACP John Mwamgunda pamoja na Kaimu Mkuu wa magereza mkoa wa Rukwa ACP Ihunja juu ya kujikita na kilimo cha alizeti kwa faida ya gereza na faida ya nchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo pamoja na maafisa wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfana Haule (kaunda suti ya kijivu) wakiaangalia moja ya majosho ya mifugo ya gereza hilo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Waogeleaji wa Bluefins kushiriki mashindano ya Kenya

$
0
0
Jumla ya waogeleaji 11 wa klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins watashiriki mashindano ya Mombasa yaliyopangwa kuanza leo.

Mashindano hayo ya kimataifa, yanashirikisha waogeleaji mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki na klabu hiyo ndiyo pekee inayoiwakilisha nchi.

Muasisi na kocha mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja wachezaji ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano hayo kuwa ni Aminaz Kachra, Lina Goyayi, Muskan Gaikwad na Aliyana Kachra ambao ni wanawake.

Waogeleaji wa kiume ni Delbert Ipilinga, Christian Fernandes, Parth Motichand, Isaac Mukani, Sahal Harunani, Aaron Akwenda na Hassan Harunani.Alisema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo pamoja na kushiriki kwa mara ya kwanza katika historia.

“Haya ni mashindano yetu ya kwanza ya nje ya nchi tokea klabu yetu ianzishwe, na tumeamua kufanya hivi baada ya kupata mafanikio makubwa sana katika michezo ya ndani kwa kushika nafasi ya pili na ya tatu, tumeona kuwa ni wakati sasa kwa waogeleaji wetu kuvuka mipaka ya nchi na kupima uwezo wao,” alisema Alidina.

Alifafanua kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo ili kuiletea sifa Tanzania.“Napenda kuishukuru BMT na Kamati ya Muda ya chama cha kuogelea nchini kwa kutupa msaada mkubwa pamoja na vibali, tumefarijika sana na tunahidi kuleta ushindi katika mashindano hayo,” alisema Alidina.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images