Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

Zaidi ya Sh 253 milioni kutumika kwa Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya jirani

$
0
0
 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
 Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya jirani, unatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kuanza mradi maalum wa Faru kufungwa vifaa vya technolojia za kisasa na hivyo kuwalinda na matishio ya ujangili ama kupotea. 
 Faru ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini, kutoweka duniani, kutokana na kuwindwa na majangili, ambao wamekuwa wakiuza pembe zao na hivyo serikali imekuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha ulinzi wao. 
 Mwakilishi mkaazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa la Frankfurt zoological Society moja ya mashirika yanayoratibu mradi huo, Gerald Bigulube alisema mradi huo wa aina yake barani Afrika, unatarajiwa kuimalisha ulinzi na ufatiliaji wa faru katika eneo la Seregeti. 
Alisema mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya sh 253 milioni, zilizotolewa na shirika la uhifadhi la Friedkin Conservation Fund(FCF) na unaratibiwa pia na Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) na Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI). 
 Bigulube alisema, tayari utekelezaji wa mradi huo, umeanza, ambapo mwaka jana faru 21 walifungwa vifaa maalum digital VHF na mwaka huu wengine watafungwa vifaa vya kisasa zaidi kutumia mfumo wa LoRa(LoRa System). 
 "Lengo letu kama wahifadhi ni kuhakikisha Faru waliopo nchini wanaongezeka zaidi sambamba na wanyama wengine ambao maisha yao yamekuwa hatarini wakiwepo Tembo ambao nao tayari kuna miradi ya kuwafunga vifaa vya kisasa ili kuwafatilia "alisema.
 Alisema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu wameanza kuwapeleka kwenye mafunzo wahifadhi nchini Uholanzi ambao ndio watakuwa wakiratibu matumizi ya technolojia katika ulinzi na ufatiliaji wa faru. 
 "Hivi karibuni tutaanza kuwafunga vifaa Faru, zoezi ambalo litatumia techolojia za hali ya juu,helkopta na vifaa vingine vya kisasa kama ilivyokuwa mwaka jana"alisema.
Akizungumzia mradi huo, Mhifadhi Mkuu wa hifadhi za Taifa ya Serengeti, William Mwakilema alisema, mpango huo ambao unashirikisha wizara ya maliasili na utalii na wadau wengine utasaidia sana ulinzi wa Faru. 
 "Ulinzi wa Faru ni jambo ambalo ni nyeti na serikali na vyombo vyake imekuwa ikifatilia kwa makini hivyo,lengo kuu ni kuhakikisha wanahifadhiwa"alisema 
 Mtafiti kiongozi wa taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI),Dk Edward Kohi ,alisema ili kuimarishwa ulinzi wa faru, technolojia mbali mbali zinatakiwa kutumika. "hii ni technolojia ya kuwafunga vifaa maalum, itawezesha kujulikana kila siku wapo wapi na hivyo ni rahisi kuwafatilia na kuwapa ulinzi"alisema 
 Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani, ambayo bado yana idadi kubwa wa faru ambao wamehifadhiwa katika hifadhi kadhaa za taifa, tofauti za nchini nyingine ambazo zimehifadhi Faru katika mashamba maalum



  


BAJETI KUU YA SERIKALI 2018/2019 YAPITA KWA KISHINDO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Baadhi ya wabunge wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 Bungeni, Dodoma ambayo imeweka kipaumbele katika maendeleo ya  uchumi wa viwanda.  
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto), akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Kilimo  Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati), na Mhe. Janeth Masaburi baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wakiwa na furaha katika viwanja vya Bunge baada ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 kupita Bungeni Dodoma.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono wa pongeze na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, Jijini Dodoma.
Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, (kulia) akibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi wa Bajeti wa Wizara hiyo Bw. Pius Mponzi (katikati), nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa pili kushoto), pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Bunge kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

SERIKALI YATOA UFAFANUZI SAKATA LA KOROSHO

HOJA YA HAJA: WABUNGE WA KUSINI MSILIGAWE TAIFA ACHENI UPOTOSHAJI KUHUSU SUALA LA MFUKO WA KOROSHO NA FEDHA ZA USHURU WA KOROSHO GHAFI INAYOSAFIRISHWA NJE YA NCHI (EXPORT LEVY)

$
0
0

Na Habib Mchange
Wananchi watambue kuwa, Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho “Cashewnut Industry Development Trust Fund (CIDTF)" ni chombo  binafsi  ambacho kilinzishwa mwezi  Juni, 2010 na kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Miunganisho ya Wadhamini, sura ya 318. 
Ni Mfuko wa Wakfu tu kama ulivyo mifuko mingi binafsi na sio chombo cha Umma au Serikali. Wadau wa Korosho wa wakati huo waliamua kuanzisha Mfuko huo ili kushirikiana kwa pamoja katika ugharimiaji wa maendeleo ya zao la korosho ikiwa ni pamoja na utafiti, elimu kwa mkulima huduma za ugani, masoko na kuhamasisha ubora wa korosho.  
Kabla ya kuanzishwa Mfuko huu, miaka ya 1990, kulikuwa na Mfuko kama huo ambao uliitwa “Cashewnuts Industry Development Trust Fund”. Mfuko huo nao haukuanzishwa na Serikali bali ulikubaliana na Serikali kupata fedha za ushuru wa Korosho zilizokuwa zikisafirishwa nje ya Nchi kiasi cha 2% ya bei ya FoB (thamani ya mzigo uliouzwa kabla ya kusafirishwa). 

Lakini kutokana ubadhirifu mkubwa wa fedha zilizoingizwa katika Mfuko huo kutoka Bodi ya Korosho Serikali ikasitisha kuupa fedha Mfuko huo na mwanzoni mwa miaka ya elfumbili, Mfuko huo ulikufa ukiwa umepoteza fedha nyingi za umma kutokana na ushuru wan korosho.
Serikali ilipozuia wakulima wasitozwe ushuru kuanzia mwaka 2005, Wakulima, Wabaunguaji, Bodi ya Korosho, Halmashauri za Wilaya na Wawakilishi wa Serikali Kuu walikutana mwezi Mei, 2010,  na Randama ya Maelewano ya kuanzisha Mfuko wa Korosho mpya ambao jukumu lake lilikuwa ni kushughulikia maendeleo ya korosho nchini. 

Wadau hao walikubaliana pia, kuiomba Serikali Kuu kuwa fedha ambazo zilikuwa zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2006 kwa lengo la kusaidia viwanda vya ubanguaji korosho, ziinghizwe kwenye Mfuko huo. 
Fedha hizo zilikuwa zinakusanywa kwa kwa kuzingatia  marekebisho ya Sheria ya Korosho ya mwaka 1984 ambayo iliweka kiasi cha 10% ya ushuru kwa korosho ghafi kwenda nje ya nchi.  TRA ilitakiwa itoe 6.5% kwenda Halmashauri za Wilaya zinazolima Korosho na 3.5% kwenda Mfuko Mkuu wa Hazina. Kusoma yote BOFYA HAPA

KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA MPANGO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA CHATEMBELEA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA DODOMA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Salome Kassanga akitoa maelezo kuhusu wodi maalum ya viongozi wa Serikali iliyopo katika hospitali hiyo kwa wajumbe wa Kikosi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea Juni 25, 2018.
 Baadhi ya wajumbe wa Kikozi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakipata maelezo ya kuhusu hospitali ya Benjamini Mkapa kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa hospitali hiyo Dkt. walipotembelea Juni 25, 2018 Dodoma.
 Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika dirisha la mapokezi hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Chuo kikuu cha Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Salome Kassanga akitoa maelezo kwa baadhi ya wajumbe wa Kikozi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea hospitali hiyo kuona namna walivyojipanga katika utoaji wa huduma ya afya nchini.
 Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Salome Kassanga akitoa maelezo ya matumizi ya mitambo ya kuchunguza, kuzibua na Kutibu mishipa ya moyo  iliyopo katika Hospitali hiyo walipotembelea kuona namna walivyojipanga katika utoaji wa huduma ya afya nchini.
 Muonekano wa mashine za upasuaji wa matundu madogo (endoscopys) vilivyofungwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma kwa ajili ya kuhudumia wananchi.
 Muonekano wa mashine ya CT-Scaniliyofungwa katika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
 Muonekano wa Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Vodacom Tanzania yaongezewa masafa na TCRA

$
0
0
Kampuni ya simu inayoongoza nchini Vodacom Tanzania Plc, imepokea kwa furaha tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority) ambapo Vodacom imepewa masafa ya kuongeza nafasi ya kuboresha na kuwafikia mamia ya wateja wake baada ya mnada uliofanyika tarehe 08 Juni 2018.

““Mgao wa eneo la mawasiliano ni hatua ya kimaendeleo kwa taifa na kwa uchumi. Ni jambo la kuleta mabadiliko makubwa kwa mtazamo wa upatikanaji wa mawasiliano na matumizi ya wigo wa mawasiliano uliopangwa utaiwezesha Vodacom kuchangia miundombinu ya mawasiliano ya simu ya mkononi ambayo ni kipengele muhimu cha maendeleo ya kiuchumi kama ilivyoelezwa katika Sera ya Taifa ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, 2016”, anasema Bw. Ali Mufuruki, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania PLC.

“Tunakaribisha taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na tumefurahia mafanikio yetu katika mnada huo na kuweza kupata wigo uliokuwa unahitajika kwa kiasi kikubwa katika mawasiliano. Hili linatuwezesha kuanza kutekeleza mipango yetu ya kuongeza kasi ya kupanua mtandao na utoaji wa mawasiliano ya kasi zaidi, tukitoa mawasiliano bora ya 4G nchi nzima,” amesema Bw. Diego Gutierrez, Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Biashara ya Kimataifa wa Vodacom.

Vodacom Tanzania PLC inaipongeza serikali kwa kusimamia mchakato na kuendesha mnada kwa mafanikio. “Ushiriki wetu kwenye mnada na mipango yetu ya kuwekeza kwenye mtandao wa 4G, vyote vinaonyesha dhamira tuliyonayo ya kutoa huduma bora nchini. Tunafurahi sana kutoa mchango wetu katika mipango ya maendeleo ya Tanzania,” alihitimisha Mufuruki.

RAIS DK.SHEIN AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WIZARA YA ARDHI,NYUMBA,MAJI NA NISHATI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Zura Bw.Haji Kali Hajii  akitoa ufafanuzi kuhusu namna Uagiziaji wa Mafuta yanayofika Nchini na hatimae kuuzwa kwa Wananchi wakati wa Kikao cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika mkutano wa siku moja katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini zanzibar.
 Wizari wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati  Mhe. Salama Aboud Talib akisoma muhtasari wa taarifa yake katika mkutano wa siku moja katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
 Mrajis wa Ardhi katika  Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Dk.Abdul-Nasser Hikmany alipokuwa akitoa maelezo yanayohusu masuala ya viwanja vinavyotolewa kwa Wananchi katika  mkutano wa siku moja katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,Mwenyekiti wake akiwa   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
 Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ahmeid Rashid akitowa maelezo   katika  mkutano wa siku moja katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,Mwenyekiti wake akiwa   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) Naibu Waziri wa  Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati  Mhe. Juma  Makungu Juma.
 Mhandisi Mji Mkongwe Nd,Mussa Awesu (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo yanayohusu idara yake hasa Mradi wa Green Corridor unaoanzia Mkunazini hadi Posta Kijangwani wakati wa  mkutano wa siku moja wa Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd,hassan Ali Mbarouk alipokuwa akitoa ufafanuzi wa kuhusu masuala ya Umeme  wakati wa  mkutano wa siku moja wa  Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati  katika utekelezaji wa Mpango kazi kwa mwaka 2017-2018 na mpango Kazi kwa mwaka 2019-2019 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu)

Waziri mkuu ashiriki sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akigonganisha glasi kumtakia afya njema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli na Mtukufu Agakhan, katika sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan, kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai na katikati ni   Mwakilishi Mkazi wa Mtandao wa Mashirika ya Maendeleo ya Agakhan (AKDN) Amin Kurji. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa na Bw. Mehboob Chamsi pochi iliyotengenezwa Tanzania, katika  sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan, zilizofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia shati lililotengenezwa Tanzania, katika sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan, zilizofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, kutoka kushoto ni Muwakilishi Mkazi wa Mtandao wa Mashirika ya Maendeleo ya Agakhan (AKDN) Amin Kurji akifuatiwa na Bw. Mehboob Chamsi. 


Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-Office)

$
0
0
 Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa (katikati) akifuatilia mafunzo ya mfumo wa ofisi mtandao yaliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Utumishi wa Walimu jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu, Bibi Christina Hape na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Nidhamu na Maadili ya Walimu.
  Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA Bibi, Devota Gabriel akitoa maelezo kwa wajumbe waliohudhuria mafunzo ya mfumo wa Ofisi Mtandao.
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya mfumo wa Ofisi Mtandandao kutoka Wakala ya Serikali Mtandao, Bw. Simba Hussein akielezea matumizi ya mfumo huo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu, Bibi. Mectildis Kapinga (wa kwanza kushoto) akifuatilia mafunzo ya Ofisi Mtandao. Wa pili (kutoka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Elia Malaki, akifuatiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi, Bibi Shani Kamala na pembeni ni Afisa Utumishi Bw. David Igogo.
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mafunzo ya Ofisi Mtandao katika ukumbi wa ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu Dodoma.

SEKTA YA KILIMO ZANZIBAR YAENDELEA KUKUA

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uagizaji wa baadhi ya bidhaa zikiwamo za chakula na Matunda nje ya Zanzibar umepungua kutokana na hamasa kubwa walionayo wananchi hasa wakulima katika muelekeo wa kuwekeza zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

Alisema Sekta ya Kilimo ni miongozi mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele cha kwanza na Chama Cha Mapinduzi wakati kilipoomba ridhaa ya kutaka kuongoza Dola kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kilipokuwa kikitangaza Sera na Ilani yake.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kuli hiyo wakati alipofanya mahojiano maalum na Timu ya Wanahabari wa Redio Uhuru pamoja na Magazeti ya Chama cha Mapinduzi ya Uhuru na Mzalendo waliotaka kujua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa upande wa Zanzibar kwenye Ofisi ya Uratibu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Jijini Dar es salaam.

Alisema kutokana na Serikali za CCM kusamehe ushuru wa forodha kwa vifaa vya kilimo vinavyoingizwa nchini sambamba na kuendeleza mafunzo ya kisasa kwa wadau wa kilimo, wakulima wengi nchini hasa wale wanaojishughulisha na kilimo cha matunda wameongeza mara dufu uwezo wa uzalishaji.

Balozi Seif alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wakulima wengi wamekuwa wakilalamikia ufinyu za soko la bidhaa wanazozalisha jambo ambalo limefikisha baadhi ya bidhaa hizo kusafirishwa kupelekwa upande wa Tanzania Bara.

Alisema hatua hiyo imeonyesha mabadiliko makubwa yaliyokuwa yamezoelekea kwa muda mrefu katika kushuhudia bidhaa nyingi hasa zile za nafaka, mizizi, mboga mboga pamoja na matunda ziliingizwa Zanzibar zikitokea mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba kwa vile kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa, Wananchi na hasa Wakulima wanapaswa kuendelea kuzalisha mazao yao katika kiwango kinachokubalika kitaalamu ili Taifa liendelee kupunguza kasi ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akifanya mahojiano maalum na Wanahabari wa Redio Uhuru pamoja na Magazeti ya Chama cha Mapinduzi ya Uhuru na Mzalendo waliotaka kujua utekelezaji wa ilani ya CCM kwa upande wa Zanzibar kwenye Ofisi ya uratibu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Jijini Dar es salaam.
Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Asia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bibi Justa Matari Nyange Ofisi ya Uratibu wa SMZ Jijini Dar es salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuangalia hatua zinazoendelea katika maandalizi ya Ushiriki wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayotarajiwa kufanyika katika Jimbo la Guangzhou Nchini China mnamo Mwezi wa Septemba Mwaka huu. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TaGLA YAENDELEA NA MAFUNZO YA UPANGAJI MIJI, YAJIZATITI KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKALA wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) wameendelea na mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Wakala hiyo Charles Senkondo ameeleza kuwa huo ni mdahalo wa pili kati ya saba inayotarajiwa kufanyika hadi kufikia oktoba mwaka huu, na mdahalo wa kwanza ulifanyika mapema mwezi huu na hii ni katika kujifunza jinsi ya kutunza mazingira na kupanga miji kisasa zaidi.

Senkondo ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatolewa na profesa Heungsuk Choi kutoka chuo cha maendeleo cha korea kusini katika kueleza namna ya upangaji wa miji na majiji kisasa na kuzingatia usafi na miundombinu iliyo bora zaidi.Imeelezwa kuwa Korea Kusini ilikuwa sawa na Tanzania ya sasa katika miaka 1960 ila hadi sasa Korea kusini imepiga hatua kubwa sana hivyo kama wakala inajifunza hatua zilizochukuliwa katika uboreshaji wa miundombinu hiyo na usalama kwa ujumla.

Pia Senkondo amewaomba wadau wa serikali na taasisi binafsi kuitumia wakala hiyo ili kuweza kushirikiana na Serikali katika kujenga miji na kutunza mazingira.Naye mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche ameeleza kuwa wao kama taasisi ya serikali inayohusika na masuala ya mazingira semina hiyo inawasaidia sana katika uboreshaji wa mazingira na ulinzi hasa katika masuala ya usafi kwa kuzoa taka ili kuweza kupambana na magonjwa ya mlipuko sambamba na kuwa tayari katika kujipanga na mlipuko wa majanga kama mafuriko.

Aidha Manchare amesema kuwa changamoto kubwa katika suala la upangaji wa miji ni kutopanga mapema maeneo maalumu kama makazi na yale ya viwanda hivyo wamejipanga katika kulitatua hilo hasa katika jiji la Dodoma ambalo limekuwa makao makuu ya nchi.

Pia mdau wa mazingira ambaye pia ni mkurugenzi wa Legendary International Limited Kamugenyi Luteganya,  ameeleza kuwa semina hiyo ni muhimu sana katika jamii katika kuishi mazingira yaliyo bora na safi kama Korea wanavyofanya na kuboresha kwa kila hatua hivyo ni lazima wachukue ujuzi ili kuweza kuboresha makazi  nchini.
 Mwanasheria wa Mwandamizi (NEMC) Manchare Heche akichangia mada katika mkutano  wa mtandao uliofanyika jana jijini Dar,ambao ulihusisha nchi mbalimbali huku Nchi mwenyeji ikiwa ni Korea kusini 
 Mkurungenzi Mtendaji wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao,Charles  Senkondo akizungumza na waandishi wa habari  mbalimbali waliohudhuria mkutano wa mtandao uliohusisha nchi  mbalimbali ,mwenyeji ikiwa Nchi ya Korea kusini  jana  jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Mkutano wa mafunzo kwa njia ya mtandao ukiendelea, huku mada kuu ikiwa ni upangaji wa miji na majiji sambamba na utunzaji wa mazingira.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mjadala wa moja kwa moja kutoka Korea kusini.

FINCA Microfinance kutoa zaidi ya Milioni 10 kwa Wamiliki wa Biashara ndogo ndogo

$
0
0
· Shindano la miezi mitatu lina lengo la kutoa elimu ya fedha na biashara kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo. 

· Benki ya FINCA Microfinance inaendelea kuwa benki ambayo inahamasisha ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi ya uwepo wake nchini Tanzania. 

Tarehe 26 Juni, 2018 Dar es Salaam - Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania, Benki ya FINCA Microfinance leo imetangaza uzinduzi wa programu ya miezi mitatu na shindano ambalo linalengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa. 

Shindano linalojulikana kama 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege. 

Akiongea wakati wa uzinduzi jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John alisema kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao, Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo. 

"Shindano hili litashirikisha wateja wa FINCA wenye akaunti na wale ambao wanapenda kushiriki watatakiwa kufungua akaunti ya FINCA, ambao pia watatakiwa kuweka kiasi cha TZS 20,000 (Salio jipya katika akaunti zao) Watatakiwa kujaza fomu katika matawi ya FINCA ambapo watabainisha katika fomu hizo kuwa wataenda kufanyia nini zawadi hiyo katika biashara zao iwapo wataibuka kuwa washindi. Baada ya hapo fomu hizo zitawasilishwa katika matawi yetu, mpaka hapo watakuwa wametimiza vigezo vya hatua ya kwanza ya shindano". 

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance, Nicholous John (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la Kuza Ofisi na FINCA linalenga kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao. Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, Emmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam.

Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba. Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Biashara wa Benki ya FINCA Microfinance, mmanuel Mongella (katikati) akieleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya ushindani wa Kuza Ofisi na FINCA katika uzinduzi wa shindano hilo leo uliofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John na kushoto ni Mtalaam wa Masoko wa Benki ya FINCA Microfinance, Noel Mulumba.

Shindano la 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.


NAMNA YA KUKATA RUFAA KWA WALIOFUKUZWA KAZI KWENYE UTUMISHI WA UMMA.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.

Wapo watumishi wa umma ambao wameachishwa kazi kwasababu mbalimbali na wanahisi kuwa pengine haki haikutendeka lakini hawajui la kufanya. Basi waelewe la kufanya lipo na ni rufaa. 

Na wengine wanajua kuwa ni rufaa yumkini wasijue rufaa yenyewe inakatwa kwa utaratibu upi. Nitaeleza hapa, lakini kwanza tujue nani mtumishi wa umma anayeongelewa hapa.

1.NANI MTUMISHI WA UMMA.
Sheria namba 8 ya 2002, Sheria ya Utumishi wa Umma , iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 18 ya 2007 imemueleza mtumishi wa umma. Kifungu cha  3  kinasema kuwa mtumishi wa umma ni yule anayefanya kazi katika ofisi yoyote ya umma. Ili uelewe vizuri mtumishi wa umma anayeongelewa katika sheria hii na katika makala  haya ni yule mfanyakazi/mwajiriwa wa serikali.  Kwahiyo watumishi wa bunge, maafisa wa mahakama, na wafanyakazi wa taasisi/kampuni binafsi  taratibu hizi za rufaa zinazoelezwa humu haziwahusu.

Tunaongelea watumishi wa serikali kuu, za mitaa, mashirika ya umma, idara na taasisi zote zilizopo chini ya serikali tukiondoa wale wa uteuzi japo nao wanaongozwa na sheria hii. 

2.  HAKI YA RUFAA.
Unapokuwa umesimamishwa kazi rufaa ni haki yako ewe mtumishi. Rufaa sio kuonesha ukorofi, sio kuwa mjuaji, sio kupingana na serikali, na sio kukosa utiifu. Rufaa ni haki kama zilivyo haki nyingine za mshahara, likizo, nk. Usiogope kukata rufaa kwani hata huyo aliyekusimamisha kazi naye akisimamishwa anakata rufaa.
Kifungu cha 25( 1 ) (b) cha Sheria ya utumishi wa umma ndicho kinachoeleza haki hii. Kadhalika kwenye barua yako ya kuachishwa kazi  au siku ya kusimamishwa, yafaa na ni haki uelezwe haki hii ya rufaa. 

                   KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com



TRA YAKAGUA MASHINE ZA EFD

$
0
0
JOSEPH MPANGALA, MTWARA 

Mamlaka ya mapato mkoani Mtwara wamefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya maduka kukagua mashine za kutolea risiti na kujionea kama wafanyabiashara wanatoa risiti lakii pia kama wateja nao wanadai risiti baada ya kufanya manunuzi.

Operesheni hiyo ambayo imeongozwa na kamishna msaidizi wa kodi za ndani operesheni ,Abdul Zuberi wamefanya ukaguzi katika maduka mbalimbali na kutoa elimu kwa baadhi ya wateja waliokuwa wakifanya manunuzi.

Zuberi amesema zipo changamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na baadhi ya wafanyabiashara ikiwemo mashine hizo kusumbua katika utoaji wa risiti

Pia amewataka wafanyabiashara ambao mashine zao zinapowasumbua kuwasiliana na wasambazaji wake na pindi wakikosa ushirikiano waende TRA kwa ajili ya ufumbuzi kwani mashine hizo zinakuwa hazina tatizo.

“Mkiona hampati huduma nzuri kutoka kwa wasambazaji mje TRA, kuna bwana mmoja alikuwa analalamikia mashine yake lakini kupata ushirikiano kutoka kwa msambazaji tumefika tumekuta ile mashine haina tatizo,”amesema Zuberi.
Kaim Kamishna wa Kodi za Ndani Operesheni Abdul Zuberi wakiwa na Meneja wa Kodi TRA Lucas Igembe Wakijadiliana Jambo mara baada ya kumaliza Ziara ya Kutembelea Maduka ya wafanyabishara kwa lengo la Kuhakiki Utumiaji wa Mashine za EFD Mkoani Mtwara.
Kaim kamishna waKodi za ndani Operesheni Abdul Zuberi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Duka la uzwaji wa Vipuli la Prashant Mkoani Mtwara Sunil Janaksihn Gandhi wakati akitoa maelezo juu ya Utoaji wa risiti kwa wateja wake Mkoani Mtwara.
Mfanyabishara wa uuzaji wa Duka Kubwa {Supermarket} Dickson Mroso akitoa maelezo jinsi ya Utoani wa risisti kwa Wateja kwa Kutumia Mashine ya EFD kwa Kaim kamishna wa Kodi za Ndani Operesheni Abdul Zuberi mara baada ya Kutembelea katika Duka Hilo kwa Lengo la kutazama Matumizi sahihi ya Risisiti Mkoani Mtwara. 
Lucas Igembe Afisa Kodi TRA akihakiki Utoaji wa Risisti Uliotolewa kuanzia mwezi Juni kwa Kutumia mashine za EFD katika Duka Kubwa,Pembeni yake ni Meneja wa duka Hilo Dickson mroso. 

NEWS ALERT: Mchezaji wa kimataifa wa IVORY COAST Wilfried Bony kuongea na wanahabari jijini Dar es salaam leo

$
0
0
 Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Westham ya Uingereza Wilfried Bony akiwa na watoto wenye mahitaji maalumu huko Kigamboni jijini Dar es salaam alipowatembelea Jumatatu na kuwapa misaada mbalimbali. Bony, ambaye amewahi kuchezea pia Swansea na Manchester City, yupo nchini kwa ziara binafsi na anatarajiwa kuondoka baadaye leo. Kwa mujibu wa msemaji wake, Bony ataongea na vyombo vya habari saa tano na nusu hoteli ya Protea Oysterbay jirani na kanisa la mtakatifu Peter.
 Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Westham ya Uingereza Wilfried Bony akiwa kwenye pantoni ya MV Magogoni akivuka kutoka kwenye kambi ya watoto wenye mahitaji maalumu huko Kigamboni jijini Dar es salaam alipowatembelea na kuwapa misaada mbalimbali.

TANTRADE YAZUNGUMZIA KUKAMILIKA MAANDALIZI MAONESHA YA BIASHARA SABASABA, KUANZA ASUBUHI HADI SAA TATU USIKU, WASHIIKI WAONGEZEKA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) imesema tayari maandalizi ya Maonesho ya biashara yamekamilika huku idadi ya washiriki ikiongezeka kwa kiwango kikubwa. Pia imesema mwaka huu wameongeza muda wa maonesho kwa lengo la kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kuyashuhudia,hivyo yataanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade Injinia Christopher Chiza baada ya kukagua na kisha kujiridhisha na maandalizi ya maonesho hayo ya biashaara."Nimefurahishwa na maandalizi ya maonesho ya mwaka huu. 

"Hata hivyo nieleze kuwa tumetekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ambapo alitutaka tuongeze muda wa kufanya maonesho haya na hivyo mwaka huu tumeongeza muda.Tutaanza Juni 28 na tutamaliza rasmi Julai 13 mwaka huu. "Cha kufurahisha zaidi idadi ya kampuni za nje zimeongezeka kutoka 30 mwaka jana hadi kampuni 33.Na kwa hapa nchini kutakuwa na 2900,"amesema. 

Pia amehoji kwanini watu wanapenda maonesho ya biashara , ambapo jibu ni kwamba kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu inasema Ukuzaji wa biashara kwa Maendeleo ya viwanda, hivyo uwepo wa viwanda lazima uendane na biashara na ndio maana washiriki wameongezeka. 

Amefafanua kwenye maonesho kama hayo ndiko ambako teknolojia wengi waniona na ni njia mojawapo ya kukuza biashara.Pia ametoa rai kwa Watanzania kupenda bidhaa zinazozalisha nchini kwani zina ubora wa kiwango kikubwa. Mhandisi Chiza amezungumzia pia mchakato wa eneo la TanTrade kuendelea kutumika kibiashara hata baada ya maonesho ya Sabasaba kumalizika na watazungumza rasmi wakikamilisha hatua zote. 

Amesema wanataka kulifanya eneo hilo kuendelea kutumika kwa biashara wakati wote.Hiyo itatoa nafasi ya wananchi kuendelea kulitumia eneo hilo kibiashara lakini mchakato wa mazungumzo unaendelea. 

Kwa upande wake Mkurugezi Mkuu wa TanTrade Edwin Ntagaruka amesema wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maonesho hayo kutakuwa na shughuli za aina mbalimbali za kibiashara. Pia amesema wanatambua kuwa wakati maonesho yakiendelea kuna michuano ya kombe la Dunia inaendelea nchini Urusi, hivyo licha ya muda wa kumaliza ni saa 12 jioni ,wameamua kuongeza hadi saa tatu usiku.

Kuhusu maandalizi amesisitiza yamekamilika na wanachojivunia kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia kwa mwaka huu. Pia amesema TanTrade imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyabishara na mwaka huu wanatarajia kuzindua kliniki ya biashara ambayo jukumu lake itakuwa ni kuwasaidia wafanyabiashara nchini. Amesema kwenye kliniki hiyo ya biashara kutakuwa na madaktari bingwa wa kutibu magonjwa ya biashara na hiyo itasaidia katika kutatua changamoto zinazojitokeza. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade Injinia Christopher Chiza (kushoto),akizungumzia maandalizi ya Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu hadi Julai 13 katika Viwanja vya Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Edwin Rutageruka akifafanua jambo kuhusu maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam

Rais wa Zimbabwe kufanya ziara ya kikazi nchini

$
0
0

Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29 Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.

Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Botswana.

Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hii pia itatoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili ya kikanda na kimataifa.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Rais Mnangagwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Mnangagwa anatarajiwa pia kutembelea Chuo cha Sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na Mhe. Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho. Mhe. Rais Mnangagwa anatarajiwa kuondoka tarehe 29 Juni 2018 kurejea chini Zimbabwe.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam, 27 Juni, 2018

WAGONJWA 20 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA MOYO

$
0
0
Jumla ya wagonjwa 20 ambao ni watu wazima wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita iliyofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India .

Wagonjwa hao wamefanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) tumefanya kwa wagonjwa nane (8), kubadili valvu mbili za moyo (Valve Replacement) kwa wagonjwa 10, upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair/Bental Procedure) na mgonjwa mmoja alitolewa damu iliyokuwa imeganda kwenye mshipa wa moyo (Blood Clot).

Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wote wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu pamoja na kufanya mazoezi. Ndani ya siku chache zijazo tutaanza kuwaruhusu baadhi ya wagonjwa ambao hali zao zimeimarika kurudi nyumbani.

Aidha katika kambi hiyo iliyoanza tarehe 18 hadi tarehe 23 mwezi huu wa Juni kwa mara ya kwanza tumefanya upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu ndani ya kifua upande wa kulia na kushoto na kuunganisha kwenye misuli ya moyo ili kuuongezea moyo damu.

Kambi hiyo pia ilienda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kati ya wageni na madaktari wetu pamoja na wauguzi.

Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri hivyo basi tunawaomba wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na kama wanamatatizo wataweza kupata tiba kwa wakati.

Kutokana na matibabu ya moyo kuwa ya gharama kubwa tunaendelea kuwasisitiza wananchi wajiunge na mifuko ya bima ya afya ambayo itawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapohitaji kutibiwa. Pia itasaidia Hospitali yetu kuendelea kujiendesha yenyewe kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine.

Tunawaomba wananchi waendeleee kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji kuongezewa damu kati ya chupa sita (6) hadi saba (7) wakati wanapatiwa matibabu. Taasisi inamkaribisha mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ambao wanapenda kuchangia damu waweze kufanya hivyo ili tuokoe maisha ya ndugu zetu wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

RAIS WA ZIMBAMBWE KUWASILI NCHINI KESHO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

RAIS wa awamu ya tatu wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa anataraji kuwasili nchini mapema kesho kwa ziara ya siku mbili kuanzia June 28 hadi 29 mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuwa Mnangagwa atapokelewa katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere na mwenyeji wake Rais John Magufuli majira ya saa tano kamili asubuhi.

Aidha ameeleza kuwa ujio huo wa Rais wa Zimbabwe una lengo kuu ambalo ni kudumumisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya Tanzania na Zimbabwe tangu wakati wa kupigania uhuru wa taifa hili la kusini mwa Afrika.

Makonda amesema kwamba Mnangagwa ataondoka nchini june 29 asubuhi akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Magufuli na ametoa wito kwa wakazi wa Dar es salaam kumkaribisha mgeni na wageni wote waingiao nchini kwa kuwafanya wajisikie wako nyumbani kwa muda wote watakaokuwa jijini.

Ikumbukwe kuwa hii ni ziara ya kwanza ya Rais Mnangagwa wa Zimbabwe kufika nchini Tanzania tangu alipoingia madarakani Novemba 2017.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu ziara ya kikazi  ya Rais wa Zimbabwe Mh. Emerson Mnangagwa.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

ASAS YAJIPANGA KUWAHUDUMIA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA , WAKAMILISHA MAANDALIZI KWA AJILI YA WATEJA WAO

$
0
0
ASAS imeamua kupiga kambi katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayotarajia kuanza kesho Juni 28 mwaka huu katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo maandalizi ya banda lao kwa ajli ya kuwahudumia wateja wao limekamilika.

Kwa sasa nchini maziwa ya ASAS ndio yamekuwa  yakipendwa kila ya nchi yetu na katika kuhakikisha wanawahudumia watanzania kokote walipo wameamua kuweka banda lao kwa kuhakikisha wanaendelea kuwahudumia wote  watakaofika kwenye maonesho hayo.

ASAS kutokana na kutambua kuwa kwenye viwanja vya Sabasaba idadi ya watu itakuwa kubwa nao wameamua kuchukua banda lenye uwezo wa kuingiza watu ndani na uamuzi huo ni kuhakikisha wanamhudumia kila anayeingia katika banda hilo.

Mmoja waaandaaji wa banda la ASAS  ameiambia Michuzi Blog kuwa mwaka huu wameamua kuweka maeneo mengi ya kuhuduma wateja watakaofika huku wakihakikisha hali ya hewa muda wote inakuwa rafiki kwa wote.

Mkazi wa Mtoni kwa Aziz Alli jijii Dar es Salaam ambaye alifika kujionea maandalizi ya maonesho hayo Juma Shaban amesema kuwa maziwa ya Asas yamekuwa na ladha ya aina yake ambayo inasababisha watu wengi kuyanunua.

Hivyo anaamini idadi kubwa ya watu watakaokwenda kwenye maonesho hayo lazima watafka katika banda hilo kama si wakubwa basi watoto ambao wengi wao wanapenda maziwa ya ASAS.
Muonekano wa nje wa banda la ASAS 

Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images