Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

BALOZI SEFUE KUSHIRIKI BONANZA LA MICHEZO YA WATUMISHI WA SERIKALI

$
0
0
Na Happiness Shayo

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la michezo (sports bonanza) la uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI litakalowashirikisha Watendaji Wakuu wa Serikali na watumishi wa umma litakalofanyika siku ya jumamosi Agosti 24 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Moshi Makuka akiwa ofisini kwake mapema leo.

Alisema dhumuni la michezo hiyo ni kujenga na kulinda afya za viongozi na watumishi,kuboresha mahusiano kazini,kujenga mshikamano kwa watumishi,kujenga utaifa na kuondoa tofauti baina ya watumishi.

Alifafanua kuwa bonanza hilo litaambatana na matembezi na mazoezi ya viungo.

“Bonanza litahusisha matembezi (jogging) kutoka Uwanja wa Taifa kupitia Klabu ya Sigara,mataa ya Chang’ombe polisi hadi Uwanja wa taifa pamoja na mazoezi ya viungo yatayoendeshwa na wakufunzi wa michezo”

Aidha,amewahimiza watendaji wakuu wa Taasisi za Serikali na watumishi wa umma kuhudhuria tamasha hilo la michezo lililoandaliwa kwa ajili yao.

Kufanyika kwa tamasha hilo ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue ambapo aliziagiza taasisi zote za serikali nchini kushiriki kwenye michezo ili kuimarisha afya zao.

MUHIMBILI YALITEMBEZEA NYUNDOZZZ JENGO LA REGENT STORE

$
0
0
Shirika la Afya Muhimbili liliingia mkataba wa pango na REGENT STORE mnamo mwaka 1987 ambapo katika mkataba huo makubaliano yalikuwa kwa REGENT STORE kujenga jengo ili litumike kuendesha biashara ya SUPERMARKET katika eneo la Hospitali kwa ajili ya mahitaji ya wagonjwa pamoja na wafanyakazi.
Mkataba huo ulikuwa wa miaka mitano yaani kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1992 ambapo REGENT STORE alitakiwa kuwa ameishajenga jengo husika pamoja na kuendesha biashara ya SUPERMARKET katika hilo jengo kwa kipindi cha miaka mitano na kukabidhi jengo kwa Hospitali.
Kilichotokea:

Hata hivyo, baada ya miaka hiyo mitano kuisha, REGENT STORE hakukabidhi jengo hilo kwa Hospitali kwa mujibu wa mkataba kwa madai kuwa alikuwa hajarudisha gharama zake za ujenzi. Kutokana na madai hayo kuwa alikuwa hajarudisha gharama zake za ujenzi, Hospitali ilikubali kumwongezea muda wa miaka mitatu kuanzia 1992 hadi 1995.

Pamoja na Hospitali kumwongenzea miaka mitatu, ilipoisha miaka hiyo mitatu, REGENT STORE hakuonesha nia ya kukabidhi jengo kwa Hospitali, na badala yake aliendelea kulitumia bila ya mkataba wa aina yoyote na bila kukubali kukaa mezani kuzungumza na kutatua suala hilo. REGENT STORE aliamua kuendelea kutumia jengo hilo kinyume na taratibu na sheria za nchi kwa kuwa mkataba ulikuwa umeisha na nyongeza ya muda aliopewa pia ilikuwa imeisha.

ALHAJ MWINYI NA MZEE MKAPA WAWASILI ZIMBABWE KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MUGABE

$
0
0
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Harare, Zimbabwe, kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Agosti 22, 2013
Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa na wake zao, Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, wakiwasili katioka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare, Zimbabwe, walikoalikwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zimbambwe, Mhe Robert Mugabe, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Agosti 22, 2013.PICHA NA IKULU

YALE YALEEE........ :UKUSANYAJI USHURU KWENYE MAEGESHO YA FUKWE YA COCO BEACH

$
0
0

Mfanyakazi wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari. Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.

Na alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na nikishakusanya nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza kukusanya ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu tupo wengi katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.

Hata hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi, hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''. alisikika akilalama jamaa mmoja

Imeelezwa kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo, ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo wanapofuatwa kulipia parking hiyo.

Na hata ukiitazama kwa makini Risiti hii haionyeshi Adress kamili ya wahusika, haina mhuri wala namba za simu zaidi ya kuandika jina la Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa kuna kila haja ya kuwahoji Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua Mapato na Matumizi ya ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia Jumatatu hadi Jumapili bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo. 
 Hii ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
 Mkusanyaji akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
 Akienda kuweka risiti  katika gari
 Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....

MAKATIBU WAKUU, MANAIBU MAKATIBU WAKUU WAPYA NA WANAOHAMA, KUPANGIWA KAZI INGINE, KUSTAAFU

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Y. Sefue akijiandaa kuongea na Waandishi wa Habari waliojikusanya jioni hii kuhusu Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Wapya, jijini Dar es Salaam.   Pembeni kushoto ni Bw. Salvatore Rweyemamu, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. 

NAIBU MAKATIBU WAKUU

Vijana wapewa changamoto ya kuweka akiba

$
0
0
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa semina ya siku mbili kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu na kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa Mwl. Gebo Steven Lugano.
Meneja Mkuu wa Masuala ya Jamii kutoka benki ya NBC akitoa mada kuhusu namna ya kuweka akiba kwa manufaa ya baadaye kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa leo jijini jijini Darc es Salaam.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa akichangia mada wakati wa mafunzo kuhusu umuhimu wa kuweka akiba benki, mafunzo ambayo wanafunzi hao wanawezeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel mwenye suti nyeusiakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya umuhimu wa kuweka akiba benki mafunzo ambayo yanaendeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC kote nchini.Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu.Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa Mwl. Shanina Athman na Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Gebo Steven Lugano.PICHA NA MAELEZO.

WAZIRI MKUU PINDA AONGOZA KIKAO CHA KUTATHIMINI BIG RESULT NOW LEO JIJINI DAR

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongoza kikao cha kutathimini` maeneleo ya Mkakati wa serikali wa Big Result now kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Agosti 21, 2013. Wapili kulia ni Wazri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo, Watatu kulia ni Waziri wa Kilimo na Ushirika, Mhandisi Chiza na kushoto ni naibu Waziri wa Maji, Dr. B. Mahenge.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Shalamar walitisha na ngoma yao ya 'Make That Move'

Wananchi waipokea kwa kishindo huduma ya Airtel money mitaani

$
0
0
Afisa kitengo cha rasilimali watu Airtel Tanzania bi Josephine Kajembe akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel money yatosha na promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu hapa wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja sokoni katika maeneo mbalimbali jijini Dar es saalam.
Meneja huduma kwa wateja Godfrey kavishe akitoa elimu kwa wateja juu ya huduma ya Airtel money yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es saalam na kutoa elimu juu ya huduma ya Airtel Money yatosha kwa watanzania.
Mfanyakazi wa Airtel akimuunganisha moja ya wateja katika maeneo ya msasani katika huduma ya Airtel money wakati Airtel ilipowatembelea wateja wake sokoni kuitambulisha promosheni ya Airtel money yatosha Hakatwi mtu hapa.

Wananchi katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam leo wamepokea kwa kishindo promosheni ya Airtel money yatosha inayofahamika kwa jina la Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo

Promosheni hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wa Airtel kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaa na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali na kuitambulisha rasmi sokoni promosheni ya Airtel money yatosha hakatwi mtu hapa.

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya Temeke walisema kuwa huduma hiyo ya Airtel money Hakatwi mtu hapa imeweza kurahisisha baadhi ya kazi zao na kuwawezesha kuhifadhi kiasi flani cha fedha ambacho awali kilikuwa kinakatwa kutokana na kutuma na kutoa pesa.

“Katika biashara zangu mimi huwa natuma na kupokea pesa mara nyingi tu, lakini awali nilikuwa nakatwa kiasi flani cha pesa ambacho mtu mwingine anaweza akaona kidogo lakini si kidogo ni kikubwa sana. Naishukuru Airtel kwa huduma hii ya Hakatwi mtu maana inanisaidia kiuchumi pale ninapotuma na kupokea pesa bure,” alisema Said Mrisho mfanyabiashara ndogondogo katika soko la Tandika.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso alisema “ Airtel tunawajali wateja wetu na kwetu mteja ni namba moja na ndio maana kwa mara nyingine tena wafanyakazi wote wa Airtel leo wanaingia sokoni ili kutoa elimu na kuwaelimisha watanzania na wateja wetu juu ya huduma zetu haswahaswa promosheni maalumu ya Hakatwi mtu hapa .

Tunazo huduma nyingine nyingi ambazo tunazitoa kwa wateja wetu kama vile Data 3.75G, Airtel Yatosha , na Huduma ya Airtel money ambayo sasa tunaendelea kuiboresha zaidi na kuwapa wateja wetu fulsa ya kutuma na kupokea pesa bure bila makato yoyote.

Lengo letu ni kuhakikisha Airtel inaendelea kutoa huduma zilizo na ubunifu, za kisasa zinazokithi mahitaji ya wateja wake na tunaamini Airtel money hakatwi mtu ni suluhisho sahihi na litaleta unafuu katika huduma za kifedha nchini.

Akizungumza katika ziara Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano Bi Beatrice Singano alisema” watu wameonesha muitikio mkubwa sana katika kuipokea huduma yetu ya Airtel money hususani promosheni ya Airtel money Hakatwi mtu na hiyo inaonesha wazi ni jinsi gani Airtel inavyotoa huduma zilizo bora na zinazokubalika kwa wateja wake na jamii nzima kiujumla.

“Promosheni hii ya Hakatwi mtu hapa inawawezesha mtu kutuma na kupokea pesa bure, yaani bila makato yoyote hivyo nachukua fulsa hii kuwahimiza watanzania kutumia huduma zetu za Airtel money ambazo ni rahisi , salama na zinapatikana nchi nzima.

Ili kutumia huduma ya Airtel money mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja na menu ya Airtel money kisha kufanya miamala mbalilimbali ikiwemo kutuma pesa, kulipa bill, kuongeza salio kununua LUKU, USA visa na nyingine nyingi. Aliongeza Singano.

Safari ya Mwisho ya Marehemu Nemela Phillip Mangula

$
0
0
Hii ndio safari ya Mwisho ya Dada yetu Nemela Phillip Mangula aliezikwa jana huko Kijijini kwao,Mkoani Njombe na mazishi yake kuhudhuliwa na watu mbali mbali.
Baba mzazi wa Marehemu Nemela,Mzee Phillip Mangula akisoma wasifu wa Marehemu mwanae wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jana huko kijijini kwao,Kushoto ni Mama Mzazi wa Marehemu.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano Uratibu wa sera Mhe. Stephen Wasira akitoa salamu za Chama wakati wa Mazishi hayo.
Baadhi ya viongozi wa Chama,Serikali na Bunge walishiriki mazishi ya Nemela Phillip Mangula huko Mkoani Njombe.
Viongozi wa Chama kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Vijana Taifa Mhe. Sadifa , Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndg. Bulembo, Mjumbe wa NEC -Temeke Ndg. Magesa na Katibu wa uchumi wa Vijana wakijadiliana mambo muhimu ya Kitaifa huko Mkoani Njombe wakati wa mazishi ya Nemela Phillip Mangula.

WAKULIMA WA SHAYIRI BABATI WANUFAIKA NA MSAADA WA PEMBEJEO ZA TBL

$
0
0
 Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto), akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji
cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000.Kulia ni mwandishi wa habari,Eliya Mbonea. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.
 Mhasibu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Octaty Minja (kushoto),akioneshwa na mkurugenzi wa kampuni ya Agric Evolution inayomiliki shamba la kuzalisha shayiri katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, .David Bagereza  (wa pili kushoto), ubora wa shayiri ambayo amekuwa akiilima katika shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3000. Maofisa wa TBL na wageni wengine wakiwemo waandishi wa habari walitembelea hivi karibuni shamba hilo la shayiri inayotumika kutengenezea bia katika viwanda vya TBL nchini.TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo wakulima  zao hilo.
 Machine ya kuvuna shayiri ikimwaga shayiri iliyokwishavunwa hivi karibuni katika shamba lenye ekari 3000 la David Bagereza lililopo katika Kijiji cha Sigino, Kata ya Sigino, , wilayani Babati, Manyara, kabla ya kupakiwa kwenye magunia na kusafirishwa kwenda viwanda vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  kutengeneza bia. Kampuni ya TBL imekuwa ikiwasaidia pembejeo  wakulima zao hilo.
Wafanyakazi wa shamba la kampuni ya Agric Evolution lililoko katika Kata ya Sigino, Kijiji cha Sigino,wilayani Babati, Manyara,wakiweka shayiri iliyokwisha vunwa kwenye magunia tayari kusafirishwa kwenda kiwanda cha biacha TBL jijini Arusha hivi karibuni.

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article4692-live.html

Mpiganaji Sunday Shomari wa Radio VOA amuweka Kamanda Ras Makunja chini ya Ulinzi wa mahojiano

$
0
0
ilikuwa majira ya saa 11.00 alfajiri kwa saa za afrika mashariki, Mtangazaji wa Radio VOA-Kiswahili,mpiganaji Sunday Shomari alisikika akimuhoji Kiongozi wa Ngoma Africa band a.k.a FFU ughaibuni almaarufu "Watoto wa Mbwa" mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mwenye makao kule Ujerumani. 

Katika mahijiano hayo mpiganaji Sunday Shomari alikuwa anataka kujua nini haswa siri ya mafanikio ya Ngoma Africa band, na kwanini ? bendi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwateka washabiki wa kimataifa kwa kutumia muziki wa dansi. Kamanda Ras Makunja anakumbana na maswali ya asubuhi ! Asubuhi ! tena kawekwa mtu kati na Sunday Shomari ! msikilize at http://www.voaswahili.com/audio/audio/177582.html

SWAHILI TV KUTOKA WASHINGTON ILIKUWEPO LIVE KWENYE SHEREHE ZA WATANZANIA WAISHIO DC,MD,VA AMBAPO PIA WALICHANGIA MAONI YAO YA KATIBA MPYA

$
0
0

Swahili TV inakuletea kipindi maalumu sherehe za watanzania waishio DC, Maryland na Virginia walipokutana kwa siku maalum ya familia (Picnic Day) iliyofanyika Wheaton Reginal Park, MD, jumamosi August 17, 2013. Muhimu zaidi waliweza pia kuchangia rasimu ya marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania. 

BENKI YA CRDB YAZINDUA KADI MPYA YA TEMBO CARD CHINA UNIONPAY

$
0
0
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akipeana mkono na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa hafla hiyo.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiingiza kadi kwenye mashine ya kutolea fedha wakati wa uzinduzi wa kadi mpya ya Tembo Card China Union Pay ambayo itamuwezesha mteja wa benki ya crdb kufanya malipo yake akiwa China. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, CRDB, Martin Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati)
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda, (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu, balozi wa China, Dk. Lu Youqing, Rais wa China UnionPay, Xu Luoude wakizindua kadi mpya ya Tembo Card China UnionPay, itakayomuwezesha mteja wa benki ya crdb kufanya malipo yake akiwa China. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WIZARA YA MALIASILI KUWAHABARISHA WAHARIRI WA HABARI

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0

FAMILIA ya Mzee Augustino Mgonja wa Pugu Kajiungeni Dar es Salaam na Familia ya Marehemu Bwana na Bibi Henry Kitosi (Mwakitosi) wa Iringa zinasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao, VICTORIA KITOSI  (DOTTO) kilichotokea Alfajiri ya leo Agosti 22, 2013 katika Hopitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikolazwa baada ya kuugua ghafla.

Mipango ya Mazishi inafanyika Pugu Kajiungeni nyumbani kwa Mjomba wake Agustino Mgonja.

Habari ziwafikie, Mama Mdogo wa Marehemu, Mary Nathan wa Kinyenze Kipera Mkoani Morogoro, Kaka wa Marehemu Bosco Kitosi wa Mwanza,Doris KitosiA wa Iringa, Bibi wa Marehemu,Balozi  Christina Shogholo wa Kisiwani Same-Kilimanjaro, Mjomba John Mgonja wa Kabuku Tanga, Ukoo wote wa Mwakitosi na Shogholo, Ndugu Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

Marehemu ameacha Mume na watoto wawili, Sanden na Sabri.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN.

WANANCHI KILOMBERO WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI YA VISIMA

$
0
0
Haya twende! Timu ya Help for Underserved Communities (HUC) ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakichimba moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, huku wakiangaliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni. HUC ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayochimba visima kwa kushirikiana na jamii kusaidia upatikanaji wa maji ya kunywa safi na salama mashuleni, vijijini na jamii kwa ujumla.
Wachimba visima toka Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., kama walivyokutwa na kamera yetu Wilaya ya Kilombero, Morogoro, wakati wa uchimbaji visima vya msaada uliotolewa na taasisi hizo hivi karibuni.
Wakazi wa Kilombero wakiangalia kisima kilichochimbwa na Help for Underserved Communities (HUC) kwa ushirikiano na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni.
Uchimbaji ukiendelea.
Dalili ya matumaini, maji bwelele.
Uchimbaji ukiendelea. Zaidi kuhusu mradi huu, bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA. (Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC)

TIGO YACHEZA DROO YAKE YA TANO NA KUWAZAWADIA WASHIDI WAKE SITA!

$
0
0
  Msimamizi wa Masoko na Biashara wa Tigo, Gaudens Mushi  akimtazama mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Furaha Hasani akipunga mkono kwa watu mara baada ya kukabidhiwa Bajaji yake katika eneo la Tandika  Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Uzalishaji Tigo, Hussein Seif akimkabidhi funguo ya Bajaji mmoja ya washindi wa droo ya tano ya Promotion ya Miliki Biashara yako na Tigo, Bi Happines Ndeki Mkazi wa Kinondoni (Kushoto) mara baada ya kukabidhiwa Bajaji yake katika eneo la Tandika  Jijini Dar es Salaam.

Balozi Seif Ali Iddi akutana na watendaji wa shirika la Bima la Zanzibar jijini dar leo

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na watendaji wa shirika la Bima Zanzibar Tawi la Lumbumba Jiijini Dar es salaa alipofanya ziara ya kuzitembelea Taasisi za SMZ zilizopo Dar.
Meneja wa Benki ya watu wa Zanzibar { PBZ } Tawi la Kariakoo Jijijni Dar es salaam Badru Idd akitoa maelezo ya utendaji wa tawi hilo na Lile ya Benki ya Kiislamu liliopo Lumumba mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyekuwa katika ziara maalum ya kutembelea Taasisi za SMZ zilizopo Jijini Dar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na watendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar wa Matawi ya Kariakoo na Lumbumba kwenye ukumbi wa Tawi la Benki hiyo inayotoa huduma za Kiislamu uliopo Lumumba Jijini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images