Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SEKTA YA MIUNDOMBINU, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WAFANYIKA JIJINI KIGALI RWANDA

$
0
0
Mkutano wa Kumi (10) wa Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu, Mawasiliano na Hali ya Hewa unatarajiwa kufanyIka tarehe 23 Agosti, 2013 jijini Kigali. Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Wataalamu kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia tarehe 19-21 Agosti 2013 ambao utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utaofanyika tarehe 22 Agosti, 2013.

Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu, Mawasiliano na Hali ya Hewa linategemea kupokea taarifa ya utekelezaji wa Programu na Miradi mbali mbali inayotekelezwa katika nchi Wanachama katika Sekta za Barabara, Reli, Bandari, Hali ya Hewa, Mawasiliano, viwanja wa ndege pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama ya waliyoyatoa katika Retreat yao ya pili kuhusu ufadhili na maendeleao ya Miundombinu pamoja na maagizo ya Mkutano wa tisa ( 9) cha Baraza la Mawaziri wa Sekta husika wa tarehe 24 Februari, 2012.

 Baada ya kupokea taarifa husika Baraza la mwaziri linategemea kutoa miongozo na maamuzi ya kisera.
Mkurugenzi wa Miundo Mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Ndugu Wambugu 
(kushoto) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu anayehusika na Mindombinu Ndugu Enos Bukuku.
Maafisa Waandamizi kutoa nchi Wanachama wakifuatilia kwa makini Mkutano husika.

PONGEZI kwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax

$
0
0
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kumpongeza Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, kwa kuteuliwa na Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo katika Mkutano wa Viongozi Wakuu hao tarehe 18 Agosti, 2013, Jijini Lilongwe, Malawi.

Uteuzi wa Mhe. Dkt. Tax katika wadhifa huo mkubwa na nyeti sio tu ni fahari kwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambako amekuwa Katibu Mkuu, bali pia kwa Watanzania wote. Tanzania kama mmoja wa nchi waanzilishi wa SADC na mshirika muhimu, inajisikia fahari kwa kushika nafasi hii ya Katibu Mtendaji. Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax anaondoka akiwa na mafanikio makubwa katika Uendelezaji wa Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inamtakia, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, kila la kheri katika majukumu yake mapya na inajivuna kwamba SADC imepata Kiongozi shupavu, mahiri na mchapa kazi.

Imetolewa na
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Cross-border Illegal Loggers put on notice

$
0
0
From Right to Left, Tanzania Forest Services Agency Chief Executive Mr. Juma Mgoo, National Directorate of Land and Forests of Mozambique Director Mr. Simao Joaquim and WWF Head of Terrestrial Dr. Simon Anstey discuss various ways to implement an MOU signed between Tanzania and Mozambique to help manage forests resources in both countries sustainably.
Technical teams from the Tanzania Forest Services Agency and the National Directorate of Land and Forests of Mozambique agree on practical ways to implement an MOU that was signed in April last year in order to help manage forest resources in both countries effectively.

Article 0

Maeneo kadhaa ya Dar yakosa umeme baada ya moto kuunguza mitambo ya SonGas Ubungo

$
0
0
Picture
Askari wa Kikosi cha zimamoto na Uokoaji wakizima moto uliokuwa unawaka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas, hUbungo jijini Dar es Salaam. 
Picha na habari na Francis Dande
Mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas iliyopo Ubungo jijini dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo imeungua moto kabla ya kudhibitiwa na Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto kwa kushirikiana na kikosi cha Kampuni ya Knight Support.


Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Felichesim Mramba, alisema hitilafu hiyo imetokea katika kituo cha 33kv na kusababisha gridi ya taifa inayotumika jijini Dar es Salaam kuzimika, hivyo baadhi ya maeneo umeme ukawa umekatika.


“Tulipata taarifa saa 10 kuwa kuna hitilafu hapa na tukajaribu kuwasiliana na Idara ya Zimamoto kwa simu wakawa hawapatikani mpaka tulipowafuata ofisini kwao. Nashukuru baada ya taarifa walifika kwa wakati na wakafanikiwa kuudhibiti moto,” alisema.


Alisema kuwa kutokana na hitilafu hiyo maeneo mbalimbali ya jiji yaliyokuwa yakipata umeme kupitia kituo
 hicho yataathirika na kuyataja kuwa ni Kigogo, Mburahati, Magomeni, Tandale na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Meneneo mengine ni Changanyikeni, Kimara, Tabata na Riverside na kwamba juhudi zinafanyika kuangalia uwezekano wa maeneo hayo kuunganishwa katika njia nyingine kwa muda.


Aliongeza kuwa bado hawajajua thamani halisi ya hasara iliyopatikana na muda utakaotumika kufanya marekebisho huku akiainisha kuwa ukarabati wa vifaa hivyo unaweza kuchukua wiki moja mpaka mbili kutegemea na aina ya uharibifu.


Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa moshi uliokuwa ukitoka katika mitambo hiyo ulikuwa mzito na uliwasababishia kushindwa kupumua vizuri.


“Niliwaona kina mama na watoto waliokuwa wanakwenda katika kituo cha mabasi Ubungo wakipata taabu kupumua hadi tukawa tunawasaidia kuwapeleka mbali na eneo la tukio,” alisema Gervas Lutabalize, ofisa wa Chama cha kutetea abiria.


Kamanda wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji jijini Dar e s Salaam, ACP Jesward Ikonko, alisema walipata taarifa ya tukio saa 11:58 alfajiri na kufika katika tukio saa 12:5 ambapo waliwakuta wafanyakazi wa kikosi cha Knight Support wakiwa wameshaanza kazi ya kuzima moto.

KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA MJINI DODOMA KESHO

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo.


Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kinatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Agosti 24 na 25, 2013 mjini Dodoma Chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
    Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika Agosti 23,2013 mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambacho kimeketi kwa Siku tatu kuanzia Agosti 20, 21 na leo 22, 2013 mjini Dodoma.
 Kwa mujibu wa Ndugu Nape, Ajenda Kuu ya kikao cha NEC ni kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mchakato wa chama Kama Baraza la Katiba la kitaasisi  kukamilisha mjumuisho wa mchango na maoni yake Tayari kuwasilisha kwa Tume ya Katiba.
         Ndugu Nape alisema mpaka sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kujadili na kutoa maoni yao kuanzia ngazi ya Chini ya mashina na Matawi.
Mwisho

Viongozi wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania watembelea Ubalozi wa wetu Nigeria

$
0
0

Bi Fatma Rajab (katikati) anaekaimu nafasi ya Balozi nchini Nigeria akiwa katika picha ya pamoja na Mhe Mussa Azzan Zungu Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania.Wengine pichani ni Saidi Yakubu( Mratibu wa CPA Tanzania),Mhe Beatrice Shellukindo ambae ni Makamu Mwenyekiti wa CPA Kanda ya Afrika.Wa kwanza kulia ni Bw.Francis Nkayala ambae ni Mhasibu wa Ubalozi. Picha na Ofisi ya Bunge

Balozi Dr Kamala akutana na Mstahiki Naibu Meya wa Jiji la Ghen

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea zawadi ya kitabu cha Historia ya Jiji la Ghent - Ubelgiji kutoka kwa Mstahiki Naibu Meya wa Jiji la Ghent. Balozi Kamala  ametembelea ofisi za Jiji la Ghent na kufanya mazungumzo ya jinsi ya kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Jiji la Ghent na Halmashauri za Wilaya za Tanzania.

IYOMBE ATEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemhamisha Engineer Ibrahim Iyombe, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Alhamisi, Agosti 22, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa Eng. Iyombe anachukua nafasi ya Engineer John Stanslaus Ndunguru ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, taarifa imesema kuwa uhamisho huo unaanza mara moja.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.


Dar es Salaam.

ORODHA YA Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Wapya

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Jumatano tarehe 21 Agosti 2013 jioni alitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Wapya katika Press Conference iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Mawasiliano.


Ifuatayo ni orodha kamili ya majina na vituo vya kazi vya Makatibu Wakuu Wapya na Manaibu Katibu Wakuu, pamoja na waliohamishwa. 

GENN Redio Inawaletea kipindi Kipya cha ''Bongo Views'' kutoka kwa waTanzania wanaoishi Kansas City

$
0
0
Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani, inawaletea kipindi  kipya cha BONGO VIEWS kitakacho endeshwa LIVE kila Jumamosi  midaa ya Saa 5 PM za Marekani ya kati 6: PM Jioni EST na kwa saa za nyumbani Tanzania  ni Saa 1: AM (Yani Saba Usiku) kwa wale wanaopenda kukesha wasikose kutembelea HAPA Global Entertainment and News Network (GENN)
Photo
Muendesha wa kipindi cha Bongo Views Joshua Kijo Simon Madelkeka walioendelea kujadili  Mjadala kuhusu Mjadala kuhusu uraia wa nchi mblili.na mambo mengi kuhusu mstakabaliwa nchi yetu, wakiwa ndani ya Studia ya Global Entertainment and News Network (GENN)
Photo: BONGO VIEWS: ANDY MKINGA and BAVON
Wachangiaji kipindi  kushoto Mjombo Andrew Mkinga,  akiwa na Anko Bavon Mwakasungula, wakijadili Mjadala kuhusu uraia wa nchi mblili na mambo mengi kuhusu mstakabaliwa nchi yetu, wakiwa ndani ya Studia ya Global Entertainment and News Network (GENN)
Kipindi cha Bongo Views  kitaendele  tena hewani LIVE wiki hii, siku ya Jumamosi Aug 24, 2013  MIDA ya Saa 5: PM  kwa Saa za Marekani ya kati.  Saa 6:PM jioni kwa Saa za EST US.  Na Tanzania Saa 1:AM Usiku kwa wale wanaopenda kukesha wasikose kutembelea. HAPA Global Entertainment and News Network (GENN). Mhadala utakua kuhusu Madawa ya kulivya, Nchini kwa kuchangia njia ya simu piga simu number  (913) 662-1190

MKUTANO NA WANAHABARI JUU YA KUANZA KWA ZOEZI LA KITAIFA LA USAJILI WA ARDHI ZANZIBAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Ardhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE 2.
 Afisa Mtambuzi na Msajili wa Ardhi Shawana Sudi Khamis kulia akitoa ufafanuzi kwa Waandihi wa habari hawapo pichani, katikati ni Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi na kushoto ni Mshauri wa Kiufundi wa zoezi hilo Andrew Smith. Mkutano huo ulifanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE.
Baadhi ya Waandishi wa habari waliokuwepo katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar Wakimsikiliza Mkurugenzi wa Adhi na Usajili Zanzibar Januari Fusi(hayupo pichani) kuhusu kuanza kwa Zoezi la Kitaifa la utambuzi na usajili wa ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar Chini ya Mradi wa SMOLE 2. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo ZANZIBAR

Serikali kuendelea kutoa mafunzo kwa Wachimbaji Wadogo

$
0
0
 Kamishina Msaidizi wa Madini, (Leseni), John Nayopa na wajumbe alioongozana nao kutoka  Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini- Magharibi  na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mafunzo kwa wachimbaji wadogo cha Katundasi wilayani Chunya, Injinia Paul Gongo (wa pili toka kushoto) mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kituo hicho kwa ajili ya kupata taarifa ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo yanayoendeshwa na kituo hicho.

Serikali imesema kuwa itahakikisha inaendelea kutoa fursa za mafunzo kwa wachimbaji wadogo nchini ili wapate utaalam utakaowawezesha kufanya shughuli za uchimbaji madini kwa tija.

Hayo yamesemwa na Kamishina Msaidizi anayeshughulia Leseni  katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi John Nayopa, katika Kituo cha Mafunzo kwa Vitendo cha Matundasi wilayani Chunya ambacho hutoa mafunzo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo.


Mhandisi John Nayopa aliusisitiza uongozi wa kituo hicho kuhakikisha wanajitangaza kwa umma ili watu wenye uhitaji wa mafunzo waweze kufika kituoni hapo na kupata huduma zao kwani lengo la Wizara ya Nishati na Madini na Serikali ni kuhakikisha elimu kuhusu madini inawafikia wanachi wengi.

SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS ROBERT MUGABE WA ZIBWABWE, HARARE

$
0
0

 Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akila kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013
  Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akivishwa shada na medali baada ya kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013


  Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akishukuru wananchi baada ya kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013

  Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akisalimia wanannchi baada ya kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013

 JK akimpongeza Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe katika sherehe za kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Tumkumbuke Chris Kelly (RiP) wa Kriss Kross na ngoma ya 'Jump'

RATIBA YA MAZISHI YA NDUGU YETU ALEX MAGAFU

$
0
0
Kwa mujibu wa familia ya Marehemu, Mwili wa Marehemu Alex Magafu (pichani) aliyefariki dunia tar 21/8/013 utaondolewa katika Hospitali ya Amana pale Ilala leo tar 23/8/013 mida ya Saa 4 nne asubuhi na kupelekwa nyumbani Mbezi karibia na Kituo cha mabasi cha Kibanda cha Mkaa.

Saa Tano taratibu za ibada zitafanyika na kisha Saa Saba Mchana safari itaanza  kuelekea Makaburini kwa kuupumzisha mwili wa mwenyetu salama.


Kwa mawasiliano zaidi piga namba hizi; 0658431919  au 0658941941



BWANA ALITOA NA BWANA AMETWA JINA LABWANA LIHIMIDIWE. APUMZIKE KWA AMANI NDUGU YETU. AMIN

hepi besdei ya kuzaliwa mwanalibeneke mc baraka

$
0
0
LEO TAREHE  23 AUGUST NI SIKU 
BIRTHDAY YANGU BLOGGER MC BARAKA.
NI KUMBUKUMBU YANGU YA KUZALIWA NAPENDA KUWASHUKURU NYOTE MNAO NITUMIA SALAMA ZA PONGEZI PIA WOTE MNAONITUMIA ZAWADI MBALIMBALI KIUKWELI SINA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUUWEKA UPENDO WENU MOYONI MWANGU
SHUKRANI KWA  TEAM NZIMA YA BUKOBAWADAU BLOG PIA SHUKRANI KWA MABLOGGER WENZANGU KWA USHIRIKIANO MKUBWA MNAONIPA

MIMI NA TANZANIA: MAONI YA WATAZAMAJI KUHUSU KUSHUKA KWA ELIMU

NEWS ALERT: MADUKA YATEKETEA KWA MOTO SOKO KUU LA KITETO MKOANI MANYARA

$
0
0

Na Mohamed Hamad, Manyara
ZAIDI ya maduka kumi ya wafanya biashara wa soko kuu la kiteto Mkoani
Manyara yameteketea  kwa moto ulioibuka usiku wa kuamkia leo Aug 23 mwaka huu na kusababisha hasara ambayo thamani halisi haijafahamika kwa haraka


Inasemekana kuwa moto huo ulianza saa nane ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme katika moja ya maduka hayo ambayo yameteketea ibaya baada ya watu waliofika kushindwa kuudhibiti moto huo 


Kwa mujibu wa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Kibaya Fatuma Ngao amedai
kuwa miongoni mwa vitu vilivyoteketea ni pamoja na maduka hayo kumi
nyaraka mbalimbali za Serikali, ofisi ya kijiji pamoja na baraza la
ardhi la kata.
Alisema kuwa nyaraka hizo ni pamoja na vitabu mbalimbali ambazo
zilitumika kama kumbukumbu za Serikali, viti na meza ambazo zilitumika
katika kuihudumia jamii ya Kibaya na vitongoji vyake.
Ngao alisema alipata taarifa hizo kupitia matangazo yaliyotolewa
kwenye moja ya msikiti mkuu mjini hapo ya kuwaomba wananchi hao ili
waweze kufika kuokoa mali zilizokuwa zinateketea katika soko hilo.

mwenge wa uhuru waingia mkoani morogoro

$
0
0

 Baadhi ya wakimbiza mwenge wa kitaifa na askari wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wao wakipasha mwili kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa viongozi wa mkoa wa Morogoro, Augosti 22, mwaka huu
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehama Nchimbi ( kulia), baada ya kumaliza mbio zake katika Mkoa huo na kuanza rasmi Augosti 22, mwaka huu katika Mkoa wa Morogoro, makabidhiano  hayo yalifanyika kwenye mpaka kati ya Mikoa hiyo katika kijiji cha Ukwamani, kinachopatana  kati ya Wilaya ya Gairo , mkoani Morogoro na Kongwa , Dodoma, katika mkoa wa Morogoro unakimbizwa katika Halmashauri saba za Mkoa na kukabidhiwa Augosti 29, mwaka huu eneo la Bwawani, mpakani mwa wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa pwani na Morogoro.

 Kikosi cha Sungusungu cha Tarafa ya Gairo kionesha umahili wake mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Kitaifa , Juma Ali Simai akinyosha mkono juu kuashiria kwa  wananchi na viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro kuwa yenye yupi fiti kuendelea na jukumu la kuukimbiza mwenge wa uhuru hadi siku ya kilele , kabla ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehama Nchimbi , kumkabidhi mwezake wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (  hayupo pichani ) jana ( Augosti 22) baada ya kumaliza mbio zake Mkoa humo ,makabidhiano  yaliyofanyika mpakani mwa  Mikoa hiyo eneo la  kijiji cha Ukwamani,katika  Wilaya ya Gairo , ya mkoa wa  Morogoro na Kongwa , Dodoma.
 Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa akimshikisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kabla ya kuukabidhi kwa DC wa Gairo
 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Fatma Ally ( kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya mwenzake wa Bahi, mkoani Dodoma, Mhe. Betty Mkwassa 
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Anthony Mtaka ( kulia) akipokea mwenge wa Uhuru sambamba na Viongozi wengine wa Serikali wa Mkoa wa Morogoro. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images