Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 232 | 233 | (Page 234) | 235 | 236 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Goodluck Ole Medeiye,Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,Abdulkarim Shah na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Grace Kiwelu wakijadiliana jambo wakati walipotembelea eneo litakalojengwa mji mpya wa Kigamboni.
  Bi Mwajuma Ramadhan Pazi Mkazi wa Kibada Kigamboni akitoa maoni yake Kwa Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeiye na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,Maliasili na Mazingira Abdulkarim Hasani Shah kuhusu kushirikishwa kwa wananchi katika uendelezaji wa mji Mpya wa Kigamboni ili kupata maendeleo endelevu ya mradi huo.
  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Goodluck Ole Medeiye na Makamu Mwekeiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira Mh Abdulkarim Hassan Shah pamaoja na wajumbe wengine wa kamati wakiangalia ukutu uliojengwa kuzuia mmomonyoko wa Bahari katika makazi yaliyojengwa bila kufuata utaratibu wa hifadhi ya bahari wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo litakalojengwa Mji mpya wa Kigamboni.
  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba,na Maendeleo ya Makazi Mh Goodluck Ole Medeiye akifafanua jambo kwa wakaazi wa kibada huko Kigamboni,ili weweze kupisha katika maeneo ambayo yameshatathminiwa kwa ajili ya ulipaji fidia ili kupisha ujenzi wa Mji mpya wa Kigamboni. Picha na Clarence Nanyaro - Afisa habari Wizara ya Ardhi.

  0 0

  STATE HOUSE ZANZIBAR
  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
  PRESS RELEASE
        Zanzibar                                                                                     20.8.2012

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika Wizara nyengine. Marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki Wizara 16.

  Shughuli za Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ zimeondolewa katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuundiwa Wizara mpya.

  Shughuli za Utawala Bora zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora na 
  kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

  Shughuli za kazi zimeunganishwa na shughuli za utumishi na kuundiwa Wizara mpya.

  Shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika zimeondolewa kutoka Wizara ya Kazi,  Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika na kuunganishwa na shughuli za ustawi wa jamii, vijana, wanawake na watoto.

  Shughuli za Tume ya Mipango zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

  Aidha, kufuatia kuundwa kwa Wizara hizo mpya Rais Dk. Shein amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Wizara kwa kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora anakuwa Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame na katibu Mkuu wake anakuwa ndugu Salum Maulid Salum ambapo Naibu Katibu Mkuu ofisi hiyo anakuwa Said Abdulla Natepe.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, anakuwa Mhe. Haji Omar Kheir na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anakuwa ndugu Joseph Meza ambapo Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa ni ndugu Mwinyiussi A. Hassan na Naibu Katibu Idara Maalum za SMZ anakuwa CDR Julius Nalimy Maziku.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma anakuwa Mhe. Haroun Ali Suleiman na Katibu Mkuu wake anakuwa ndugu Fatma Gharib Bilal na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma anakuwa ndugu Yakout Hasan Yakout.

  Wizara ya Fedha itakuwa chini ya Waziri Mhe. Omar Yussuf Mzee na Katibu Mkuu wake ni ndugu Mussa Omar na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo atakuwa ndugu Juma Ameir Hafidh.

  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto anakuwa Mhe. Zainab Omar Mohamed ambapo Katibu Mkuu wake atakuwa ndugu Asha Ali Abdalla na Naibu Katibu Mkuu Uwezeshaji na Ushirika atakuwa ndugu Ali Khamis Juma na Naibu Katibu Mkuu Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto atakuwa ndugu Msham Abdalla Khamis.  0 0

  Na Eleuteri Mangi – MAELEZO

  Serikali imeanzisha mkakati wa kutokomeza wimbi la tatizo la dawa za kulevya nchini kwa kudhibiti viwanja vya ndege na sehemu mbalimbali za mipakani zinazotuhumiwa kupitisha dawa za kulevya.

  Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo.

  “Kwa yeyote aliyekuwa anafikiria kufanya biashara ya dawa za kulevya ajue muda wake umekwisha” alisema Mwambene.

  Mwambene alisema kuwa tatizo hili litakuwa historia kwani ulinzi umeimarishwa, hivyo ametoa rai kwa mtu yeyote mwenye nia ya kufanya biashara hiyo aache mara moja.

  Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Serikali imeweka jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa watumiaji na waathirika wa dawa za kuelevya ili waweze kubadili tabia zao za kutumia dawa hizo na kuwa watu wema katika jamii.

  Aidha Mkurugenzi Mwambene amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter” kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.

  “Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, ameongeza Mwambene.

  Assah Mwambene amefafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha Umma na si kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.

  0 0


  0 0

  Na Ally Changwila

  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imetoa zawadi mbalimbali katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha New Life kilichopo Kigogo jijini Dar Es Salaam.

  Zawadi hizo ambazo ni pamoja na mchele , sukari , mafuta na biscuit ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa TCAA ambayo licha ya kuhakikisha kuwa Anga ya Tanzania inaendelea kuwa salama pia hutoa sehemu ya mapato yake kufurahi kwa pamoja na watoto wanoishi katika mazingira magumu ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii .

  Akipokea msaada huo kutoka TCAA, Mkurugenzi wa Kituo hicho Bibi Mwanaisha Magambo aliishukuru sana TCAA kwa kitendo hicho cha kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

  Kwa mujibu wa Bibi Magambo kituo hicho hivi sasa kina jumla ya watoto 103, miongoni mwao wakiwemo wasichana 38 na wavulana 65 wenye umri kati ya miaka 3 na 21, waliopo katika hatua mbali mbali za masomo kuanzia msingi hadi vyuoni.

  Aliongeza kuwa changamoto anayokumbana nayo sana kituoni hapo ni Elimu na Matibabu na kutoa wito kwa wenye moyo wa kukisaidia kituo hicho kujitokeza.

  Bibi Magambo alisema Kituo cha New Life kilianzishwa mwaka 1998 na kutambuliwa rasmi kwa kupata usajili wa Serikali mwaka 2009 na sababu ya kuanzisha kituo hicho ni mapenzi yake ya kupenda watoto pamoja na moyo wake wa kutaka kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.Bibi Magambo ni mama wa watoto saba wote wa kiume na hivi sasa wanajitegemea .
  Bibi Mwanaisha Magambo (Kushoto), Mkurugenzi wa kituo cha New Life akipokea zawadi kutoka kwa Bw.Ally Changwila Afisa Habari Msaidizi kutoka TCAA.Wengine pichani ni wawakilishi kutoka TCAA pamoja na baadhi ya watoto wanaoishi kituoni hapo.


  0 0
 • 08/20/13--10:11: Article 13


 • 0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Bw.Teo Siong Seng Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore ikulu jijini Dar es Salaam leo .
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Teo Siong Seng Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore(wanne kushoto) na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Baadhi ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda kukabidhi mwenge kutoka wilaya ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika wilaya ya Mpwapwa wakiangalia moja ya magari yaliyoharibika baada ya kutokea ajali hiyo Gari namba DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) ambayo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma, Mrakibu wa Jeshi la Polisi Bw. Bonventure Nsokolo Akikagua moja ya gari iliyoharibika katika ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa.
  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo.

  ===============
  Mnamo tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.

  Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
  1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
  2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
  3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
  4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
  5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
  6. STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.

  Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
  1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
  2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
  3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
  4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.

  Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
  1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
  2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
  3. JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
  4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.

  0 0

  Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimlaki kwa furaha Katibu Mtendaji mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),  Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax mara baada ya kuwasili Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Mhe. Membe akimkabidhi shada la maua Dkt. Tax kwa niaba ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kuwasili Wizarani hapo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule nae akimkarisha Dkt. Tax kwa furaha Wizarani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


   
  Abiria wapatao 60 waliokuwa wanasafiri na basi la Turu linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Singida na Haydom mkoani Manyara, walilazimishwa kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu, ambao baadae walilichoma moto basi hilo.
  Taarifa toka eneo la tukio zinasema wananchi hao  wa vijiji vya Singa, Idabagadu. na Nkungi. mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.  
  Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita

  0 0


  Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  Bw. Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News for Rwanda na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.

  “Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
  Madai  hayo  yaliandikwa  jana  na  mitandao  ya  Rwanda  wakidai  kuwa  mama  Salma  Kikwete  ni  Mnyarwanda  na  ni  binamu  wa  aliyekuwa  rais  wa  zamani  wa  Rwanda. 
  Wakati huo huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mmakonde  wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu na kushangaa zaidi kuona mitandao hiyo ya udaku ya Rwanda haijaonesha jinsi Rais Kagame alivyovurumishiwa mawe na Wanyarwanda wenzake alipokuwa Chuo Kikuu ya Oxford nchini Uingereza.

  "Unajua ustaarabu wa Watanzania ni wa hali ya juu ndio maana mitandao yake iliamua kuacha kuripoti habari za kutukanwa na kupigwa mawe Rais Kagame na Wanyarwanda wenzake wanaomchukia (angalia video) alipotembelea Chuo Kikuu cha Oxford hivi karibuni", amesema mdadisi mmoja  wa Uingereza, James Parker wa North London.

  Mdadisi mwingine wa Uingereza, Bw. Mark Sutton, amesema hiyo ni moja ya njia chafu za Wanyarwanda katika kujaribu kulipiza kisasi kwa kutimuliwa maelfu ya ndugu zao waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania, na sasa wanahaha wapi kwa kuwaweka kwenye ka-nchi hako kadogo ka Afrika Mashariki.
  "Kutimuliwa kwa Wanyarwanda nchini Tanzania kutaleta vituko vingi sana, na hii ya kumsingizia Mama Salma Kikwete kuwa anahusiana nao ni mojawapo - mengi yatakuja na Watanzania wasishangae maana Wanyarwanda wametaharuki na hawajui wafanyeje kwa kupokea zaidi ya wenzao 10,000 waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania," amesema mdadisi mwingine, Adam Hayes.

  0 0
 • 08/20/13--17:15: viwanja vinauzwa Kimbiji


 • 0 0

   Hawa ni Bwana Joseph Lyimo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (kulia) na Bi. Zuwena Ibrahim mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini ambao wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la vijana kutoka mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) litakalofanyika Lilongwe, Malawi kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2013 ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia umuhimu wa kuwashirikisha vijana mapema katika vyombo vya maamuzi.

   Rais wa CPA Kanda ya Afrika na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb), akiwakabidhi Waheshimiwa Wabunge hao wateule bendera ya Tanzania akiwataka waiwakilishe na kuipeperusha vema bendera hiyo ya Tanaznia katika Bunge la Vijana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb),  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Mhe. Mussa Zungu Azzan, (Mb) na Kamishna wa Bunge Mhe. Beatrice Shilukindo (Mb).
   Wahadhiri waandamizi kutoka katika Vyuo Vikuu vya Mzumbe na Tumaini walioambatana na wanafunzi wao katika hafla ya kuwaaga. Hapa wapo kwenye picha ya pamoja na Mhe. Spika Makinda.
      Spika Makinda akimpa mkono wa heri na baraka Mhe. Zuwena kama ishara ya kuwaaga vijana hao
  Mhe. Joseph Lyimo akizungumza na wanahabari mara baada ya hafla hiyo ambapo ameahidi kuiwakilisha Tanzania vyema.Picha na Prosper Minja - Bunge

  0 0
 • 08/20/13--19:51: JIUNGE NA FLATBELLY TANZANIA
 •             Neema  Herbalist  & Nutritional  Foods  Clinic  kwa  ushirikiano  mkubwa  na  Taasisi  ya  Flatbelly  Tanzania  wamedhamiria   kuwasaidia  wadada  kwa  wakaka  wanao  taka  kutengeneza  shape  za matumbo  yao   kwa  kuyafanya  kuwa  flat pamoja  na  watu  wote  wenye  nia  ya  kuondoa  vitambi  vyao, kupunguza  unene  na  uzito   kwa  njia  ya  tibalishe  na  mazoezi,  kuhakikisha  wanafikia  malengo  yao. 
  Hili  litafanyika  kupitia  mradi  wa    Flatbelly   Project  unao  ratibiwa  na  Neema  Herbalist  kwa  kushirikiana  na    Flatbelly  Tanzania.
  Programu   hii  inafanyika  kwa  lengo  la  kusogeza  huduma  zetu  kwa  wananchi  walio  wengi    kwa  urahisi  na  ukaribu  zaidi.  Kupitia  program  hii, tutahakikisha  kuwa, kila  memba  anaye  jiunga  na  program  anaya  fikia  malengo  yake   kwa  asilimia  mia  moja. Tutakuwa   tukiweka  picha  za    memba  kabla  na  baada  ya  kujiunga  na  program  ili  kuwaonyesha  watanzania  ni  kwa  namna  gani  tumedhamiria  kuimarisha  afya  za  watanzania  kupitia  program  hii. Gharama  za  kujiunga  na  programu  hii  ni  rahisi  sana  na  mtanzania  wa  rika  lolote  lile  anaweza  kujiunga.  
  Unapo chukua  uamuzi  wa  kuja kujiunga  na  programu  hii, unapaswa  kuwa  na  uhakika   kwamba   utayafikia  malengo  yako  kwa  asilimia  mia  moja.
   Kwa  wewe  unayetaka  kujiunga  na  program  hii, fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  jijini  Dar  Es  salaam, katika  eneo  la  Changanyikeni, karibu  na  Chuo  Cha  Takwimu, au  tuandikie  barua  pepe :neemaherbalist@gmail.com  au   tupigie   0766538384.
  Kauli  mbiu  ya   program  hii  ni 
             “ FLATBELLY  IS  SEXY!
  Kwa  maelezo  zaidi, tembelea 

  0 0
 • 08/20/13--20:01: ngoma azipendazo ankal
 • Odyssey wakaja na ngoma ya 'Going Back to My Roots'

  0 0

  IMG_3248
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jinsi waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari nzuri zenye kuelimisha kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu wanazoweza kutumia ili kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
  Akizungumza katika warsha ya siku nne inayoshirikisha waandishi na maripota wa redio za jamii inayofanyika Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Bi. Ledama ameongeza kuwa upo umuhimu wa kuwajengea uweze watendaji katika redio hizo ikiwemo kuwafundisha namna ya kutumia mtandao wa Intaneti kwa ajili ya kuboresha uandishi na utangazaji , haswa katika maeneo muhimu yanayoigusa jamii ikiwemo Elimu, Afya na Kilimo na pia jinsi redio hizo zinavyoweza kuandaa vipindi vitakavyoigusa jamii moja kwa moja.
  Kwa jumla warsha hiyo ya siku nne kwa waandishi wa habari wa redio za jamii imeangalia kwa mapana mambo muhimu ya kijamii, na kuchambua mambo hayo ni yapi ambapo imegusia masuala ya Afya na Kilimo pamoja na mambo mengine na kuangali fursa zinazopatikana, pia changamoto zinazokabili masuala hayo na kutathmini nini kifanyike ili kuboresha utendaji na utoaji huduma katika sekta hizo.
  IMG_3079
  Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara ya Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari wa redio za jamii inayofanyika mkoani Mwanza ambapo fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo na jinsi ya kuzitumia ili kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo Kwanza na pia amezungumzia changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo na namna gani maafisa wa Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza wakafanya kukabiliana nazo ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.


  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.

  Wanariadha wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO nchini Namibia wameanza vyema mbio hizo baada ya kufanikiwa kunyakua medali za Dhahabu na fedha katika mbio za mita elfu 10000 wanaume.

  Aliyenyakua medali ya dhahabu ni Mwanariadha Fabian Nelson ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe,Namibia,Botwasana na Angola.

  Wengine walioipatia Tanzania Medali ni pamoja na Basili John mita 800 (Shaba ) na Mohamed Ibrahim mchezo wa kurusha kisahani (shaba).

  Katika mpira wa miguu mechi ya ufunguzi ilizikutanisha wenyeji Namibia na Msumbiji ambapo Namibia iliichapa Msumbiji mabao 2 kwa 0 huku kwenye mpira wa miguu wanawake Namibia na Angola zilitoka suluhu ya bila kufungana.

  Tanzania itaanza kutupa karata yake katika mpira wa miguu dhidi ya Zambia ambapo Tanzania imepangwa kundi B ikiwa na timu za Zambia, Angola ,DRC na Lesotho huku Kundi B lina timu za Namibia, Msumbiji, Botswana na Zimbabwe.
  Mbio zikiendelea
  Mwanariadha Fabian Nelson akivishwa Medali ya Dhahabu baada ya kushika nafasi ya kwa katika mbio hizo,ambapo alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe,Namibia,Botwasana na Angola.
  Furaha ya ushindi.

  0 0

  Kamati ya Hesabu za Serikali imekutana na Wizara ya Ardhi kwa madhumuni ya kupitia Hesabu za Wizara kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2012. Changamoto za Wizara ni nyingi sana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amehoji mambo mengi sana na mengi ni wizi, upotevu wa mapato ya Serikali na malalamiko ya wananchi kuhusu ardhi. CAG alitoa hoja za ukaguzi maeneo ya mapato kutokusanywa, kulimbikizwa na hata kukusanywa bila kuyawasilisha Wizarani.

  Katika Mwaka wa Fedha 2011/12 Wizara ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni tisini na tisa (99 bilioni) lakini ilikusanya shilingi bilioni ishirini tu (20 bilioni) sawa na asilimia 21 ya makadirio.

  CAG pia alihoji masuala ya viwanja vilivyopimwa, kugawiwa watu lakini watu hawakupewa hati ambapo zaidi ya viwanja 7, 342 vilikutwa ni viwanja vyenye shaka. Pia viwanja 160 jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 555.8 milioni viligundulika ni viwanja ambavyo walijigawiwa maafisa wa Ardhi maana haoakuwa na ushahidi wowote wa mauzo ya viwanja hivyo. Hoja nyingine ni pamoja na ukiukaji wa sheria kwa kujengwa kwenye fukwe nk.


  0 0  0 0

   Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.

  Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.

  Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo.

  Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.

  Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.  Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.

  Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.

  Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.

  Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.

older | 1 | .... | 232 | 233 | (Page 234) | 235 | 236 | .... | 3272 | newer