Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

AAR YAANDAA FUTARI KWA KIKUNDI CHA TUSHIKAME NA KUTOA MSAADA WA VITANDA

$
0
0
Kampuni ya Bima ya Afya ya AAR imewafuturisha wazee wanaotunzwa katika ‘Kituo cha TUSHIKAMANE PAMOJA cha jijini Dar es Salam na kuwapa msaada wa vitanda kama sehemu ya mchango wao katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mkuu wa Itifaki wa BAKWATA, Shekh Mohammed Nassor akiambatana na viongozi wengine wa kidini waliongoza futari hiyo, iliyofanyika jana jioni, Juni 13, 2018 katika Ofisi za Makao Makuu ya AAR yaliyoko Mikocheni jijini Dar.

Akizungumza katika hafl hiyo, Shekh Mohamed ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza AAR kwa kuwajali watu wenye uhitaji hususan wazee ambao alisema wanahitaji uangalizi maalum na faraja. 

Aidha, aliitaka jamii kwa ujumla kushiriki katika kutatua matatizo yanayowakabili wazee, akifafanua kuwa hata Mtume Muhammad (S.W.A) alionesha mfano katika hili akieleza kuwa, “Kama kijana atamheshimu mzee wakati wa umri wake, Mwenyezi Mungu atamteulia mtu atayemheshimu na kumjali wakati wa uzee wake pia.”

“Tunapotumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kutafakari afya za roho zetu, tunapaswa kuhakikisha mazingira ya upendo na kuwajali wenye mahitaji maalum na hata wapita njia. Ninawapongeza AAR kwa kujali hali za wazee ambao ni kisima cha busara ambazo kama taifa tunaweza kuzitumia kuepuka migogoro isiyo ya lazima,” alisema Shekhe Mohammed.
 Mkuu wa Itifaki wa BAKWATA, Shekh Mohammed Nassor akizungumza na Wazee wa Kikundi cha Tushikame Pamoja kilichohudhuria Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Bima ya AAR.
  Mwenyekiti wa Kikundi cha Tushikame, Bi. Rose Mwapachu akitoa shukrani kwa Uongozi wa Kampuni ya AAR kwa kuwakaribisha Futari hiyo pamoja nakusaidia baadhi ya vitu kama Vitanda.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya AAR, Bi. Violet Modichai akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Wazee hao wa Kikundi cha Tushikame kilichopo Kwembe.
Sehemu ya Wazee wa Tushikame Group waliohudhuria Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya AAR kwenye Makao Makuu yaliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HATUA YA VIONGOZI KUANDAA FUTARI NA KUWAALIKA WATU INAJENGA UMOJA –SHEIKH MAVUMBI

$
0
0
Na Tiganya Vincent- Tabora
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amepongeza hatua ya viongozi mbalimbali wa umma na sekta binafsi kwa kuandaa futari kwa kuwa jambo linasaidia kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri.

Alisema ni kweli Serikali haina dini lakini wananchi wanazo dini na hivyo hatua hiyo inaoonyesha mapenzi makubwa waliyonayo kwa watu wote bila kujali tofauti zao , hali inayosaidia kuimarisha umoja wa Kitaifa ulioasisiwa tangu uhuru wa Nchi ya Tanzania.

Sheikh Mavumbi aliwataka watu wengine ambao Mwenyezi Mungu amejalia kuwa na uwezo wa kifedha kuigia mfano ulionesha na baadhi ya viongozi wakiwemo wa Kitaifa wa kutoa futari kwa watu bila kujali rika na uwezo wao aua hali zao za kimaisha.

Aidha Sheikh huyo wa Mkoa aliwaomba umma wa kiislamu katika Mkoa wa Tabora endapo watafanikiwa kuuona mwezi muandamo kushiriki Swala ya eid El fitri itakayoswaliwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni baada ya kukamilika mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akisalimia na Sheikh wa Mkoa wa Tabora wa Ahamadiyya  Musilim Jamaat Tanzania  Shafi Mohamed Memon (kulia) jana mjini hapa wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa mara baada ya kufuturisha jana mjini hapa. 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akitoa salamu za Waislamu wa Mkoa huu baada ya futari iliyoandaliwa  jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Aggrey Mwanri.
 Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini na Serikali walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakifuatilia hotuba ya Sheikh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi(hayupo katika picha)
  Baadhi ya Viongozi wa dini walioshiriki futari iliyoandaliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA CRDB YATOA SH. MIL 100 KUSAIDIA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA MOYO JKCI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa tatu kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil.100, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (wa tatu kulia), kwa ajili ya kusaidia ukarabati wodi ya wagonjwa wa moyo, katika Taasisi hiyo, Muhimbili jijini Dar es Salaam.Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya ya Moyo, Dkt. Tulizo Shemu, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa pamoja na Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza jambo katika mkutano wake na uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ulioambatana na kuchangia fedha kiasi cha sh. mil 100 kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya wagonjwa wa moyo, katika Taasisi hiyo, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza jambo wakati akitoa taarifa ya Taasisi yake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei aliyeambatana na ujumbe wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Mafunzo ya Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) kwa wahasibu na waweka hazina Iringa

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) chasaini mkataba wa ushirikiano na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO)

$
0
0
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), ambayo pia ni mtandao wa radio zenye maudhui ya kijamii nchini. Mtandao huu una radio 31 wanachama zilizopo Tanzania bara na visiwani.
 Chini ya mkataba huo, OUT itatumia wataalam wake (wahadhiri) kushiriki katika vipindi mbalimbali vyenye manufaa kwa umma wa watanzania hususan wananchi wanaoishi vijijni, ambapo radio jamii zinafanya shughuli zake. Pia TADIO kupitia radio wanachama, itawajibika kurusha vipindi hivyo kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya. 
Mkataba huo unaipa fursa TADIO kuwa na ofisi zake katika majengo ya Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria, Kinondoni Dar es Salaam. Pia unatoa fursa kwa wanafunzi wa OUT wa taaluma ya habari na mawasiliano, kutumia studio zilizopo katika majengo hayo zinazomilikiwa na TADIO kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
 Pamoja na kutumia studio hiyo, wanafunzi wa OUT watapata pia nafasi ya kushiriki mafunzo kwa vitendo katika radio wananchama zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda akitoa rai juu ya mkataba huo amesema “OUT itatumia mtandao wa radio wanachama wa TADIO kuifikia jamii na kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali za kiuchumi na maendeleo zilizopo kwa kuzingatia vigezo vya utafiti.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha UNESCO Bi. Nancy Kaizilege, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda pamoja na Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda wakibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria (OUT) na TADIO wakati wa hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Ndg. Prosper Kwigize na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda wakionyesha hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Huria (OUT) na TADIO mara baada ya kusainiwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa (kulia).
Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, UNESCO na OUT baada ya hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya OUT na TADIO. Kutoka kushoto walioketi ni Bi. Nancy Kaizilege (UNESCO), Prof Elifas Bisanda (VC OUT), Prosper Kwigize (Mwenyekiti TADIO) na Marco Mipawa (Katibu TADIO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

POLISI YATAJA KILICHOSABABISHA AJALI YA AMBULANCE DAR

TBS NA FCC WATOA ELIMU KWA WAFANYABISHARA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA,MTWARA

Shirika la Viwango Tanzania TBS kwa kushirikiana na Tume ya ushindani FCC Imetoa mafunzo kwa wafanyabishara mbalimbali mkoani Mtwara yenye lengo la kuwajengea Uwezo wa kutambua Bidhaa Feki ambazo zinaingia sokoni pamoja na Kuwawezesha waweze kuzingatia sheria ya Ubora wa bidhaa Wanazonunua na Kuuza.

Mafunzo HAYO yamepita Duka kwa Duka na kutembelea wajasiliamali na Wauzaji wa Bidhaa mbalimbali na hivyo kubaini kuwa Kwa kiasi kikubwa Bidhaa zinazouzwa zinakidhi Viwango vya Ubora lakni kuna baadhi ya Sehemu kumeonekana kuwa na matatizo.

Frank mndimi ni Afisa mwandamizi mawasiliano na Mahusiano ya Uma kutoka Tume ya Ushindani FCC anasema Elimu hiyo inayopelekwa kwa wananchii na wafanyabiashara inaumuhim kwa sababu inajenga uwezo mkubwa katika kukuza Biashara hasa kwa wajasiliamali.

“Wafanyabiashara wengi wametaka Elim hii Ifanyike mara kwa mara lakini pia tumebaini Bidhaa zinazouzwa kwa kiasi kikubwa kwa sasa zinakidhi Viwango na zinakidhi matarajio na Bidhaa Halisi Kuna sehem Kidogo Bado Bidhaa zinamatatizo matatizo lakini Tumewaelimisha nini cha kufanya kuangalia na kuzingatia kwamba wanaweka bidhaa ambazo ni nzuri,bidhaa zinazo kizi matwakwa ya Sheria ya miliki Bunifu “alisema Frank.

Naye Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi TBS Stiphen Minja amesema madhara ambayo mfanyabishara yanaweza kumtokea Pindi anapouza Bidhaa isiyokuwa Bora ni pamoja madhara ya kiuchumi pamoja na Uchafuzi wa Afya.

“Mfanyabishara anapoweka Bidhaa sokoni ambayo haikidhi matakwa ya Ubora kwanza atapata madhara ya Kiuchumi,Kiafya na kimazingira,kama Mtu atanunua Bidhaa kwenye eneo lake Supermarket yake au duka la vifaa vya ujenzi popote pale ile bidhaa atakaposhindwa kuitumia hatarudi kwenye Duka lile kwenda kununua Bidhaa kwa sababu ameshakutana na Bidhaa yake ambayo Haina Ubora”.
 Mfanyabishara  wa Bidhaa za Rejareja Hemen Bajaria akimweleza Afisa mwandamizi mawasiliano  na Mahusiano ya Uma  kutoka Tume ya Ushindani FCC Frank Mdim Juu ya Elim aliyoipta katika Kutambua Bidhaa zenye Viwango na Nembo ya TBS
 Stiphen Minja Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi TBS akitoa elim  kwa  mmoja wa wafanyabiashara wa Spea za Mabari  Mkoani mtwara Mbarak Mabrouk juu ya Uagizwaji wa Bidhaa Kutoka nje ya Nchi na Jinsi ya Kutambua Bidhaa hizo kama zinaubora uanaohitajika kwa Wanunuzi.
Stiphen Minja Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi TBS akiwa na Afisa mwandamizi mawasiliano  na Mahusiano ya Uma  kutoka Tume ya Ushindani FCC Frank Mndami wakitazama moja ya Kopo la Asali lililofungashwa Vizuri na mmoja wa wajasiliamali kisha kupelekwa katika moja ya Soko kubwa liliko Mkoani Mtwara. 

MAGARI YA SERIKALI NDIO YANAYOONGOZA KWA KUVUNJA SHERIA-KAMANDA MAMBOSASA

$
0
0
*Apiga marufuku magari ya vyombo vya ulinzi na usalama kupita barabara ya mwendo kasi


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema magari ya Serikali ndio yanayoongoza kuvunja sheria kwa kupita kwenye barabara ya mabasi ya mwendo kasi na hivyo limesema ni marufuku gari hayo kupita kweye baabara hiyo.

Kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo jeshi hilo limesema litaanza kufanya operesheni maalum kukomesha hali hiyo na kwamba dereva ambaye atakamatwa atachukuliwa hatua.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ambapo amefafanua kumwekuwa na tabia ambayo sasa inaota mizizi ya madereva kuhama kwenye barabara inayohusika na kuingia barabara ya mabasi ya mwendo kasi.

"Vyombo vya ulinzi madereva wake wengi wanapita katika barabra hiyo,magari ya wagonjwa nayo wakati yanapeleka mgonjwa na hata wakati wa kurudi pamoja na dereva kuwa peke yake bado anapita katika barabara hiyo. Matokeo yake inakuwa vurugu kwani ni matumizi ambayo hayakukusudiwa"amefafanua.

Hivyo Kamanda Mambosasa ametoa rai na onyo kwamba ni vema barabara zikatumika kwa mujibu wa sheria na hakuna sababu ya kulazimisha kubadilisha matumizi ya barabara hiyo ya mwendo kasi.

"Juzi Ambulance imesababisha mauaji au vifo vya wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutokana na uzembe ulifanywa na dereva wa Ambulance hiyo kwa kulazimisha kupita katika barabara ambayo hakuwa anaruhusiwa na matokeo yake akawa anapambana na magari yanayokuja mbele yake.

"Katika kulazimisha kupita akaligonga gari iliyokuwa imesimama na matokeo yake akasababisha ajali hiyo ambayo imepoteza maisha ya wanafunzi hao."Hatuwezi kuacha hali hii ikaendelea kuota mizizi, hivyo tutafanya operesheni na dereva ambaye tutamkamata asipige mayoe .Magari ya Serikali yanaoongoza kwa kuvunja sheria na kupita kwenye barabara za mwendo kasi,"amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza operesheni hiyo inaanza leo kwa kuwachukulia hatua wote wanaovunja sheria na kwamba matokeo yake yataonekana.

Wakati huohuo Kamanda Mambosasa amepiga marufuku mchezo wa kuvaa viatu vya matairi na kisha kukimbia barabarani huku magari yakipita kwa kasi na kwamba wanaofanya mchezo huo waache mara moja kwani polisi itawakamata na kuwachukulia hatua.

Amesema kila mchezo una maeneo yake ya kuchezea hivyo hakuna sababu ya barabara za Serikali kutumika kwa mchezo huo na ole wao watakaokamatwa.

DK. BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUSOMA KURANI JIMBONI KIKWAJUNI

$
0
0
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akizungumza wakati wa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akimkabidhi zawadi, Salha Mohamed Khamis, baada ya kuibuka  mshindi wa juzuu tano wa  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Saleh Nassoro Jazeera  na  Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia).
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Salha Juma Sadalla akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika  leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Abdilbaswit Hamis Hassan, akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar. Picha na Mpiga Picha Wetu
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal (watano kulia mstari wapili) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na washindi wa Mashindano ya Kusoma Kurani baada ya kuwakabidhi zawadi.Mashindano hayo yamefanyika katika Kiwanja cha Mapinduzi visiwani Zanzibar. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANAFUNZI WA CHUO CHA MT.AUGUSTINO MWANZA WATEMBELEA MAKABURI YA HISTORIA YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA

$
0
0
WANAFUNZI wa chuo cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza(SAUT) wa mwaka wa kwanza na wapili wanaosoma kozi ya mawasiliano ya umma watembelea kituo cha kumbukumbu na Makaburi ya halaiki ya wahanga wa mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda.

Kituo hicho ambacho kimebeba historia ya nchi ya Rwanda pamoja na baadhi kumbukumbu ya vitu mbalimbali vya watu wa nchi ya Rwanda kabla na baada ya mauaji ya kimbari.

Baadhi Kumbukumbu zilizopo katika jengo la kumbukumbu ni picha za watu waliofariki dunia pamoja na picha za watoto ambao waliuwawa bila hatia yoyote mauaji na makaburi yalitokea Aprili 7, 1994.

Pia katika ziara hiyo wanafunzi wa chuo cha MT. Augustino walitembelea televisheni ya Taifa ya Rwanda, Rwanda Bordicasting Agency (RBA) na kujifunza vitu mbalimbali katika shirika hilo la utangazaji nchini Rwanda.
Lango la kuingilia katika makumbusho na Makaburi ya mauji ya kimbari Kigari nchini Rwanda. Baadhi ya Wananfunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustino Mwanza wakiingia katika eneo la kumbukumbu.
 Mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha kumbukumbu ya makaburi ya mauaji ya kimbari, Kazinimana Pacifique akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha MT Augustino jijini Mwanza mara baada ya kufika katika kituo cha kumbukumbu na makaburi ya pamoja ya mauaji ya Kimbari ambayo walitokea nchini Rwanda Mwaka 1994 ambapo mpaka kwaka huu 2018 wametimiza miaka 24 ya kumbukumbu ya mauaji hayo.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(HOD), Peter Mwidima.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Austine wakiingia  katika chumba cha kuangalia moja ya sinema.
  Baadhi ya wanafunzi wanafunzi wakipiga picha nje ya Jengo ambalo limebeba historia ya nchi ya Rwanda pamoja na picha za wahanga wa mauaji ya kimbari na vitu mbalimbali ambavyo vimehifadhiwa humo.
 Moja ya kaburi la pamoja la wahanga wa mauaji ya Kimbari Kigari nchini Rwanda.
Wanafunzi wa chuo cha Mt. Augustino jijini Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri mkuu Mtendaji wa Kituo cha Utangazaji cha Rwanda Broadcasting Agency. na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chuo cha Mtakatifu Augustino,(HOD), Peter Mwidima. 

NEWZ ALERT:ASKARI 12 JKT WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MBEYA

$
0
0
Wengine 25 wajeruhiwa...Kamanda Polisi Mbeya alezea ajali ilivyotokea

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.

Akizungumza leo kwa njia ya simu na Michuzi Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.

Amesema kutokana na mwendo mkali aliokuwa anaendesha dereva wa basi gari hiyo yenye namba T 755 BAB aina Scania alishindwa kumudu kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao

Amesema kuwa askari hao walikuwa wakitokea Igunga kwenda Mbeya kwa ajili ya kuendelea na mafunzo mengine ya jeshi baada ya kumaliza mafunzo katika kambi ya Igunga.Amefafanua kuwa dereva wa gari hiyo naye amepoteza maisha na kwamba miili ya merehemu hao ipo chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Mbeya.

Amesema waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni askari 25 na wanne hali zao ni mbaya na sasa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya huku majeruhi waliobakia wakipatika matibabu katika hospitali ya JKT Mbeya kwani majeraha yao si makubwa.
Baadhi ya Askari wa JWTZ na JKT wakishriki kutoa msaada kwa Majeruhi  waliopata ajali iliyotokea katika eneo la Kawetele mkoani Mbeya mapema leo mchana.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.ASKARI 12 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Kawe Tele mkoani Mbeya.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 8:30 mchana katika eneo hilo na kwamba gari hiyo iliyokuwa na askari hao ilikuwa ikitokea Igunga.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi vifo vya vijana wa JKT 11, Askari JWTZ 1 na Dereva vilivyotokea Mbeya

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/1

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (MB) akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya mapato na Matumizi kwa Mwaka 2018/19

TATU MZUKA YAZINDUA ‘SUPA MZUKA CUP’ YA MILIONI 300

$
0
0
• Pia yazindua ushirikiano na VODACOM ambapo wateja wa MPESA wataweza kushinda dakika za bure, intaneti na bidhaa mbalimbali kwa kipindi chote cha kampeni.

Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini Tanzania leo umezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.

Wachezaji wote wa Tatu Mzuka kuanzia leo mpaka fainali, wataweza kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda milioni 300 ambapo kwa kila shilingi 500 unayocheza inakupa tiketi ya kushiriki droo siku ya fainali.

‘Mpaka sasa hii ndiyo kampeni inayosisimua zaidi kwa sababu hakuna ushindi mkubwa namna hii wa jackpot ambao ulishawahi kutolewa nchini Tanzania’ alisema Bwana Sebastian Maganga, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka

Kwa kuwa huu ni msimu wa kucheza na kushinda na marafiki, Tatu Mzuka kupitia droo ya Mzuka Deile wanatotoa fursa kwa mshindi kuchagua marafiki wanne ambapo kila mmoja atapewa 500,000 katika ushindi wa milioni 10 zinazotolewa kila siku.

Katika droo ya Jumapili, marafiki 5 kila mmoja atapata milioni 1 kutoka katika ushindi wa jackpot ya kila Jumapili. Siku ya fainali, mshindi wa milioni 300 atatoa milioni 1 kwa marafiki zake kumi ili kukamilisha timu ya ushindi ya watu 11.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati wakizindua ushirikiano na VODACOM, ambapo wateja wa MPESA wataweza kushinda dakika za bure, intaneti na bidhaa mbalimbali kwa kipindi chote cha kampeni pichani kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana,mbali ya kushirikiana huko 
Tatu Mzuka wamezindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga Tatu Mzuka pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana wakionesha kombe wakati wa wakizindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga Tatu Mzuka pamoja na Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya biashara na Masoko wa MPESA, Bwana Polycarp Ndekana wakionesha jezi maridhawa wakati wa wakizindua kampeni mpya ya ‘SupaMzuka Cup’ ambapo siku ya fainali tarehe 15 Julai 2018 mshindi mmoja ataondoka na milioni 300 za kitanzania.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 14.06.2018


Tunasoma "Homegoing," Riwaya ya Yaa Gyasi

$
0
0

Na Profesa Joseph Mbele


Tarehe 4 Juni, nilianza kufundisha kozi ya kiangazi hapa chuoni St. Olaf juu ya fasihi ya Afrika (African Litterature). Nimefundisha kozi hiyo mara kadhaa miaka iliyopita. Baada ya mimi kutoa utangulizi siku mbili za mwanzo, tulianza kusoma riwaya ya Yaa Gyasi iitwayo Homegoing.

Yaa Gyasi alizaliwa Ghana akakulia hapa Marekani. Nilikutana naye katika tamasha la Hemingway mjini Moscow, katika jimbo la Idaho akiwa ni mgeni rasmi wa tamasha kufuatia riwaya yake kushinda tuzo ya PEN/Hemingway kwa mwaka 2017.

Homegoing, inaturudisha nyuma karne tatu zilizopita, kwenye nchi ambayo leo ni Ghana. Tunaona jamii inavyoishi mila na desturi zake na mahusiano ya watu, lakini tunaona pia shughuli ya biashara ya utumwa. Tunaona jinsi watu walivyokuwa wakitekwa kufanywa watumwa na wengi kupelekwa pwani kwenye kasri ya Cape Coast kuhifdhiwa humo katika mazingira ya ovyo kupindukia, wakisubiri kuvushwa bahari kwenda Marekani.
Homegoing inafaa kusomwa sambamba na tamthilia ya The Dilemma of a Ghost, ya Ama Ata Aidoo, ambayo iliigizwa mara ya kwanza mwaka 1964, ikachapishwa mwaka 1965. Tungo hizi zinafaa kulinganishwa hasa kwa kuwa zinahusika na dhamira ya watu kuchukuliwa kutoka Afrika Magharibi kwenda utumwani Marekani. Vile vile zote zinatumia vipengele vya sanaa ya fasihi simulizi. Wanafunzi wangu nami bado tunaisoma riwaya hii, na tutajua mengi zaidi kadiri tunavyoendelea kusoma. 

KAMPUNI YA BIMA YA AFYA YA AAR YAFUTURISHA WAZEE JIJINI DAR ES SALAAM

VOA Swahili: Duniani leo Juni 14, 2018

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO JUNI 12, 2018

TRC-RELI TV: Ujenzi wa Reli SGR, Wananchi Dodoma wapewa fidia,wataja FURSA watakazo zitumia ikiwemo kuuza Vyakula

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images