Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Soccer Eclipse 2018


RC MAKONDA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI UJENZI WA BARABARA KINONDONI SHAMBA

VODACOM YAMWAGA MAGARI 10, MAMILIONI YA PESA KUSHINDANIWA WAKATI IKISHEREHEKEA MIAKA 10 YA M-PESA

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula ( wa sita kushoto) akiiongoza meza kuu kushuhudia magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa  yaliyotolewa wakati wa hafla ya kutimiza miaka kumi ya M-Pesa iliyofanyika jana Jijini Dsm. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema (wa tano kushoto), Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary na Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi.
 Mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 10 ya M-Pesa, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula (wa kwanza kushoto),  Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema  na Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,  wakifuatilia moja ya burudani wakati wa sherehe ya kusherehekea mika 10 ya M-PESA iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Moja ya magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa  yakiwa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuzinduliwa  wakati wa sherehe kusherehekea miaka 10 ya M-pesa .Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara wa M-Pesa, Polycarp Ndekana  na mshereheshaji Taji Liundi.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary  (katikati) na Mkuu wa kitengo cha Mwendelezo  wa Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya gari kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-pesa  wakati wa sherehe ya kusherehekea miaka k10 ya M-pesa  iliyofanyika  katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.





HOSPITALI YA MAMC, MLOGANZILA YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MACHO KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

$
0
0
Madaktari wa Macho walioshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika katika kutoa huduma ya upimaji wa macho katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi Idara ya Macho ya Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili -MAMC, Mloganzila wametoa huduma ya upimaji macho katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa yaliyofanyika katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi kuanzia tarehe 12 mpaka 14 mei 2018. 
Akiongea katika maadhimisho ya siku hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. John Kisimbi amesema kuwa katika maonesho haya, Idara ya Macho imeazimia kutoa elimu kwa wazazi na watoto hususani kwenye magonjwa ya macho. 
"Vile vile, kwa kupitia zoezi hili la upimaji macho wanafunzi wetu wanajifunza mambo mbalimbali na pia tunapata nafasi ya kutangaza huduma mbalimbali zinazotolewa katika hospitali ya MAMC, Mloganzila,” Dkt. Kisimbi aliongeza. 
Mbali na kutoa elimu kwa magonjwa mbalimbali ya macho, Dkt. Kisimbi amesema katika maadhimisho haya Idara inatoa huduma ya kupima uwezo wa kuona, kujua hali ya jicho kwa ujumla kama ni zima au linauma, vipimo vya miwani hasa kwa watoto waliokuwa na uhitaji wa miwani pamoja na huduma ya dawa kwa watoto waliokuwa hawana shida kubwa ya macho na pia kutoa ushauri wa kwenda Hospitali kwa watoto wenye matatizo makubwa ya macho kwa ajili ya uchunguzi wa kina na matibabu. 
Katika maadhimisho haya Siku ya Mtoto wa Afrika zaidi ya watoto mia mbili (200) waliweza kupata huduma ya upimaji wa macho kutoka Idara cha Macho ya Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MAMC). Baadhi ya watoto wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya upimaji macho katika banda la Hospitali ya Taaluma na Tiba, MAMC wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika duniani katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi. Dkt. Nicholaus Benedicto akiwa anampatia huduma ya kipimo cha miwani kwa mtoto aliyetembelea banda la Hospitali ya MAMC wakati ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani katika viwanja vyaTANESCO, Kinyerezi. Dkt. Ally Omari akimgagua mtoto kujua tatizo gani la macho linamsumbua baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa mama yake wakati ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi. Dkt. Edwin Greyson akifanya kipimo cha fundoscopia (kuangalia pazia la macho kama linaona vizuri kwa mtoto aliyejitokeza kushiriki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi. Dkt. Nicholaus Benedicto akimuelekeza mtoto aliyepata huduma ya macho katika banda la Hospitali ya MAMC jinsi ya kuweka dawa kwenye macho wakati ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Duniani Picha ya pamoja ya Madaktari wa Macho walioshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika katika kutoa huduma ya upimaji wa macho katika viwanja vya TANESCO, Kinyerezi Idara ya Macho ya Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili -MAMC, Mloganzila 

Introducing KENYA & TANZANIA COLLABO = Bahati EMB & Mbosso Wasafi "FUTA"

Afrika Jambo Band na BongoDeejays Kutikisa Coventry, Uingereza, siku ya Jumamosi Hii katika Eid Party

$
0
0
Karibu Jumamosi hii Club Junction Coventry CV1 3JZ, Ucheze Muziki Mzuri na bendi yako ya Africa jambo na BongoDeejays mafundi wa Muziki Mzuri Usiozeeka wa Kizazi Kipya na zamani..Watakuwepo Club Junction Coventry Jumamosi hii Kusherekea Siku kuu ya Eid, Saa tatu mpaka Majogoo Mwambie na Mwenzako.
Kwa Tickets piga +447853482158/07469015174

BONGO DEEJAYS EVENTS LIMITED
EVENT ORGANISER / TALENT /ARTIST MANAGEMENT
we also offer professional Djs,Sound  and Light for your events indoor and outdoor we do it all full setup included
For Booking & any enquiriesplease contact us
 info@bongodeejays.com For Entertainment News || Music logon @ www.bongodeejays.com
Check Us Out on Social Media

Bongo Deejays Quality through Experience

EID MUBARAK WADAU WOTE WA GLOBU YA JAMII

KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ametoa mwito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha siasa na badala yake kufanyakazi kwa kwaajili ya maendeleo.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya maendeleo katika jimbo lake la Ubungo na kuikabidhi.

Miradi aliyoitembelea Kubenea ni ujenzi wa kibanda cha kupumzikia katika Zahanati ya Mavurunza iliyopo Kimara ambao umegharimu Sh. milioni 7.7, miradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mabibo ambao umegharimu Sh. milioni 17,mradi wa kisima katika soko la Mabibo uliogharimu sh. milioni 12 pamoja na ujenzi wa ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kawawa.

Akizungumza baada ya kutembelea na kuikabidhi miradi hiyo, Kubenea amesema ni vyema kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kuangalia chama."Mimi sifanyi mambo haya kwaajili ya siasa, ninafanya kwaajili ya maendeleo ya wananchi....ninajua hata siku nikiondoka itabaki historia kwamba Kubenea alifanya kitu fulani.

"Kwahiyo niwaombe viongozi wote, tusiangalie siasa eti huyu chama tawala, huyu Chadema...tufanye kazi pamoja katika kuleta maendeleo ya Taifa letu," amesema Kubenea.Amefafanua kuwa maendeleo yana safari ndefu hivyo maeneo ya jospitali na shule yanahitaji kuboreshwa.

Akizungumzia miradi hiyo Kubenea amesema fedha zake zimetoka katika mfuko wa jimbo ambapo ni sehemu ya fedha za bajeti ya mwaka 2017/18.Akitoa shukrani kwa ujenzi wa Kibanda cha mapumziko, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mavurunza amesema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wagonjwa ambao ulisababishwa na kutokuwa na sehemu ya kupumzika.

Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa kata ya Mavurunza Kimara mara baada ya kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Mavulunza lililojengwa na fedha za mfuko wa jimbo
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisoma gharama za ujenzi wa Mnara wa kupandisha maji juu katika kisima kilichojengwa katika soko la Mabibo Garment kwa fedha za mfuko wa jimbo
Mwalimu wa shule ya Msingi Mkwawa Mabibo akimueleza Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea kiasi cha fedha zinazohitajika katika umaliziaji wa ofisi za walimu.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisalimiana na wananchi na Makada Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.


RC GAMBO:WAANDISHI KUWENI WAZALENDO KWA MKOA NA TAIFA LENU

$
0
0
Na. VERO IGNATUS ARUSHA

Mkuu wa mka wa Arusha Mrisho Ghambo amefanya mkutano wa siku moja na waandishi wa habari ukiwa na lengo la kuimarisha na kuboresha mahusiano kati ya Serikali na wanahabari.

Katika mkutano huo wa siku moja ambao  ni wapili tangia kuingia madarakani  umewajumuisha wadau mbalimbali wa Taasisi za serikali mkoani hapa katika kueleza mafanikio changamoto mbalimbali za maendeleo na namna ya kuzitatua.

Katika ufafanuzi zaidi Gambo amesema kuwa asilimia 80%ya mapato mkoani hapo yanatokana na utalii hivyo amewataka wanahabari kuwa makini  taarifa ambazo wanaandika wazichuje kabla ya kuzipelea katika jamii."Mfano habari ya mtalii kutekwa, mwandishi unapoaiandika hiyo habari na kuitoa katika vyombo vya habari, itasomwa na inaweza kuleta madhara, kuwaogopesha wageni kutokuja nchini kwaajili ya utalii, kuweni makini tangulizeni uzalendo kwanza"

Amewataka viongozi mkoani hapa Kuwapa ushirikiano wa kutosha waandishi kwani kuna baadhi ya viongozi wanawakimbia waandishi na kuwalazimisha waandike kadri wanavyoona inafaa,amekemea na kuwataka kutoa ushirikiano. RC Gambo amepongeza juu ya jambo la kujiendeleza kielimu kwa waandishi ambapo ameutaka uongozi wa, APC kupeleka data base ili uongozi wa mkoa waone ni namna gani unaweza kuandika andiko kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kuwasapoti kielimu. 

Gambo amewataka wanahabari mkoani hapo kutokukubali kurubuniwa au kutumiwa na mtu awae yeyote yule ili kuharibu amani badala yake watangulize Uzalendo kwanza kwaajili ya mkoa na Taifa kwa ujumla. 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiendesha mazungumzo pamoja na mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika kikao. Cha siku. Moja cha waandishi wa habari pamoja na wadau wa taasisi za serikali mkoani hapo. Picha na Vero Ignatus. 
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku moja ulioitishwa na mkuu wa mkoa huo. Picha na Vero Ignatus
 Katibu Tawala  wa Mkoa wa Arusha Charles Kwitega akizungumza katika mkutano huo katika Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Arusha. Picha na Vero Ignatus.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha AICC Arusha Eliashialia Kaaya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO KUUNDA TIMU MAALUM YA WATAALAM KUCHUNGUZA MIGODI YOTE ILIYOPO WILAYA YA ULANGA

$
0
0
Na Freddy Mgunda, Morogoro
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa ataunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote nchini ikiwa ni pamoja na utambuzi wa aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika sekta ya madini.

Akizungumza wakati wa ziara ya siku mbili Mkoani Morogoro Mh Biteko alisema kuwa madini yote yaliyopo katika ardhi ya Tanzania ni mali ya watanzania hivyo yanapaswa kuwanufaisha watanzania kwanza ndipo watu wengine wafuate.
“Naombeni watanzania wote mjue kuwa madini haya ni mali ya watanzania wote hivyo tunapaswa kuyalinda na kutoa taarifa sahihi kwa serikali kama kuna mtu anaiibia serikali kwa namna moja au nyingine ili serikali iweze kuchukua hatua za kisheria dhidi yake, Na mimi nawaambieni watanzania tuache uoga tuseme ukweli kama Rais wetu Mhe Dkt John Pombe Magufuli anavyosisitiza utendaji wa uwazi na uwajibikaji katika serikali” Alikaririwa Mhe Biteko.
Biteko amepiga marufuku wawekezaji kutumia fedha zao kuwanyanyasa wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo kuna migodi kwa ajili ya kuwaibia watanzania ambao bado wana kipato cha chini katika maeneo yanapopatikana madini.
“Najua hawa wawekezaji wanapesa nyingi sana hivyo isiwe sababu ya kuwarubuni baadhi ya wananchi na kuwatesa wananchi wengi hususani waliopo kwenye maeneo ya madini na leo nataka niwaambie ukweli wawekezaji wote nchini najua ambavyo mnatumia pesa zenu kuwanyanyasa wananchi, sasa ndio mwisho wenu maana serikali ya awamu ya tano inataka haki kwa kila mwananchi” alisisitiza Biteko.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Bitoke alifanya ziara ya kikazi katika kijiji cha Ipanko kilichopo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kugundua kuwa kuna wawekezaji wanaidanganya serikali na wananchi kwa kutoweka wazi kiasi gani ambacho wanakipata kwenye migodi iliyopo katika kijiji hicho.
“Jamani wana Ipanko nchi hii tumeibiwa sana sasa ifike mwisho tusema hapana haiwezekani tena kwenye serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli tuendelee kuibiwa madini yetu na kuwanufaisha watanzania ambao wapo nje ya nchi yetu, Rais kashasema na sisi wasaidizi wake tunaungana naye kwamba iwe mwisho kuchezewa kwa rasilimali zetu”
“Chonde chonde nyie viongozi wetu wa ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa tunaomba msituangushe kwa kupokea rushwa kutoka kwa wawekezaji na kuisaliti nchi yako kuendelea kuibia kirahisi namna hii” alisema Biteko

Biteko alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inawapenda sana kuwa na wawekezaji wengi wenye tija ambao sio wababaisha na ambao wamekuja nchi kuiba rasilimali za watanzania.
Aidha, Biteko alisema kuwa haiwekani muwekezaji akawekeza Bilioni 42 halafu akachangia madawati na mifuko ya saruji katika jamii kama ndio mchango wake, haiwezekani wanapaswa kuchangia kulingana na kiasi ambacho wamewekaza kwa faida na manufaa ya wananchi.

“Mimi binafsi hainiingi akilini kuona muwekezaji amewekeza pesa nyingi kama hizo halafu kwenye shughuli za kimendeleo amechangia kiasi kidogo namna hiyo kwangu nasema haiwezekani na nchi hii kwa sasa sio yakuchezewa tena” alisema Biteko
Lakini pia Naibu waziri huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe Goodluck Mlinga kwa kuwapigania wananchi wake kwa kuzifikisha kero mahali husika na kutafutiwa ufumbuzi.
Nao baadhi ya wananchi akiwemo Pangarasi Kanyali, Cyprian Kanyali, Micky Sengo, Doedatus Moholeli, Hilda Linoma na Fredrick Kazimoto  walimpongeza Naibu Waziri wa Madini Mhe Biteko kwa kufika kijiji hapo na kusiliza kero zao kwani wana amini zitatafutiwa ufumbuzi kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.

“Toka sisi tuzaliwe hatujawahi kutembelewa na waziri na kusikiliza kero zetu kama ambavyo wewe umefika kijijini kwetu leo hii tunajisikia wenye amani na furaha kwa kuwa tunajua kero zetu tunazifikisha moja kwa moja kwa kwa Rais wetu kupitia wewe waziri” Walisema wananchi hao

Awali Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga alisema kuwa lengo la waziri kufika katika kijiji hapo ni kujionea kero wanazokumbana nazo wananchi kupitia wawekezaji wa sekta ya madini na kuzitafutia ufumbuzi.

“Huku ni mbali sana Mheshimiwa Naibu Waziri lakini kuna madini mengi ambayo ndio utajiri wa nchi hii hivyo tunapaswa kuwa makini na hawa wawekezaji maana wamekuwa wakiibia sana serikali yetu” Alisema Mlinga
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Naibu waziri wa madini mheshimiwa Doto Bitoke alifanya ziara ya kutatua mgogoro baina ya wawekezaji na wananchi kwenye sekta ya madini
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wananchi wa kijiji cha Ipanko juu ya changamoto ambazo wanakabiliwa nazo na kuunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote na aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika seckta ya madini. 
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akiendelea kuongea na wananchi wa kijiji cha Ipanko 

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA YAFANA WILAYA YA MKURANGA

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Filberto Sanga amewataka wazazi kuwajali na kuwapenda watoto wao kwani waliwaleta duniani kwa mapenzi yao wenyewe yawapasa kuwalea na kuwakinga na ukatili wa kijinisia.

Hayo aliyasema jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayofanyika kila mwaka na kwa Wilaya ya Mkuranga walifanya katika kijiji cha Magoza  Kata ya Kiparang'anda na watoto 108 wanaoshi kwenye mazingira magumu kuzawadiwa  zawadi mbalimbali.

Sanga amesema kuwa, wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha masomo watoto hao.
"Hakuna mtoto aliyeomba kuja duniani bali ni sisi wazazi kwa starehe zetu tumewaleta hawa watoto na lazima tuwajali na kuwalinda, kuwapa elimu na pia kutowakatisha masomo yao na kupelekea ndoa za utotoni," amesema Sanga.
Na kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake na mke wa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega amesema kuwa yeye pamoja na mumewe wameamua kusherehekea maadhimisho haya kwa kuwapatia watoto zawadi.

Mama Ulega amesema kuwa watoto ni tuni ya taifa yapaswa kulindwa kwani kauli mbiu ya mwaka huu katika siku ya mtoto wa Afrika kwa hapa nchini inayosema KATIKA UCHUMI WA VIWANDA WATOTO WASIACHWE NYUMA inalenga katika kuhamasisha watoto wasome kwa bidii ili baadae na wao waje kuwa wabunge na mawaziri.

Mama Ulega amesema, "Kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu, wazazi hawana budi kuwasisitiza watoto wasome kwa bidii ili baadae waje kuwa wabunge na mawaziri kama Ulega na cha zaidi ni kuwa watoto ni tunu ya taifa hili kuelekea uchumi wa viwanda," 

Pia, Mama Ulega alisema mbali na zawadi hizo kwa watoto pia Mh Ulega aliweza kutoa zawadi kwa watendaji wa kata na vijiji 36 kwa utendaji wao mzuri wa na kuwataka wasikatishwe tamaa na changamoto baadhi zinazojitokeza.
Mbali na Ulega kutoa zawadi hizo kwa pia Wabunge wa viti maalum mkoa wa Pwani Subira Mgalu, Zainab Vulu na Hawa Mchafu waliweza pia kuchangia  kiasi cha fedha na kufanikisha kupatikana kwa kilo 750 za mchele, sabuni na baadhi ua zawadi zingine walizopatiwa watoto hao ikiwemo doti 30 za kanga walizowapatiwa wazee wanaoishi na watoto yatika kutoka vijiji sita.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka duniani kote na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zimekuwa zinajitolea kuhakikisha wanapigania haki za watoto na kutoa elimu zinazohusu umuhimu wa kuwapatia elimu watoto wote na kutowakatisha masomo na kuwaozesha.

Maadhimisho haya yalienda sambamba na kukabidhi misaada kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo vifaa vya shuleni na Bima za Afya kwa familia 150 zinazoishi katika Mazingira Magumu. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akimkabidhi  cheti Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake la uwezeshaji wa Kiuchumi Mariam Ulega  kama ishara ya shukrani kwa kusapoti Harakati mbalimbali za Maendeleo katika Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungunza na wanachi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake la Uwezeshaji wa Kiuchumi Mariam Ulega akitoa salumu za Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mbunge wa Mkuranga wakati wa maadhimisho ya siki ya mtoto wa Afrika.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akimkabidhi  cheti Mkurugenzi wa Mwanamke na Uongozi Shamira Mshangama kamama ishara ya shukrani kwa kusapoti Harakati mbalimbali za Maendeleo katika Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akikabidhi cheti.


Matukio mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Mkuranga.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ashiriki swala ya Eid kwenye Msikiti Anwar, Msasani, jijini Dar es salaam

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika swala ya Eid kwenye Msikiti  Anwar, Msasani, jijini Dar es salaam leo  Juni 15, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika  swala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani,  jijini Dar es salaam leo Juni 15, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Waislamu baada ya kushiriki katika swala ya Eid  kwenye Msikiti wa Anwar, Msasani,  jijini Dar es salaam leo Juni 15, 2018. 
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kushiriki katika swala ya Eid kwenye Msikiti wa Anwar,  Msasani,  jijini Dar es salaam leo Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SWALA EID EL FITRI UWANJA MAISARA SULEIMAN MJINI UNGUJA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali katika swala ya Eid  El Fitri  baada ya kukamilika kwa ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan iliyoswalishwa na Sheikh Khalid Ali Mfaume katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo
 Sehemu ya Waumini wa Kiisalamu mbali mbali wakiwa  katika swala ya Eid  El Fitri  baada ya kukamilika kwa ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan   iliyoswalishwa na Sheikh Khalid Ali Mfaume katika Uwanja wa Maisara Suleiman  Mjini Zanzibar leo
 Sehemu ya kinamama Waislamu wakijumuika pamoja  katika swala ya Eid  El Fitri  baada ya kukamilika kwa ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan   iliyoswalishwa na Sheikh Khalid Ali Mfaume katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo
 Waumini wakisikiliza Hotuba ya baada ya Swala ya    Eid  El Fitri iliyotolewa na  Sheikh Khalid Ali Mfaume leo katika  katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Zanzibar baada ya Idaba ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na  Viongozi na Waislamu mbali mbali waitikia dua iliyoombwa baada ya  swala ya Eid  El Fitri  kwa  kukamilisha  ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan   katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo. Picha na IKULU.

DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amesema hairuhusiwi katika duka la dawa kuwa na dirisha la ushauri kwani huo si utaratibu huku ikielezea sababu zinazosababisha usugu wa dawa.

Dk.Faustine Ndugulile amesema hayo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Famasi yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumzia maduka ya dawa kuwa na dirisha kwa ajili ya kutoa ushauri, Dk.Ndugulile amesema kisheria hairuhusiwi kwani kuna mgawawanyo wa majukumu.

"Kuna baadhi ya maduka ya kuuza dawa wameweke na madirisha kwa ajili ya kutoa ushauri.Hairuhusiwi na hivyo baraza la famasi linatakiwa kusimamia hili kwa kuhakikisha hakuna duka la dawa ambalo limeweka dirisha la ushauri,"amesema Dk.Ndugulile.

Akizungumzia usugu wa dawa kwa mtumiaji, Dk.Ndugulile amefafanua zipo sababu nyingi ikiwamo ya matumizi ya dawa yasiyo sahihi na ulaji holela wa dawa.Amefafanua mbali ya kuwapo kwa sababu hizo kuna tafiti ambayo imebaini kuna vimelea ambavyo ni sugu wa hali ya juu kwa dawa zote zilizopo duniani.

Wakati huohuo Dk.Ndugulile ameliezea baraza la Famasi kuwa anao ushahidi wa baadhi ya watalaam wa famasi si waaminifu kwani wamekuwa wakiiba dawa na hivyo hao wachache kuharibu sifa ya famasi.

Ameliomba baraza la famasi kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria za famasi kwani kukaa kimya kunatoa nafasi ya baadhi yao kukika sheria zilizopo, hivyo wafuatilie.Hivyo amesema wenye tabia hiyo ya kuiba dawa waache mara moja kwani Wizara yao inafuatilia huku akielezea kwa sasa hakuna tatizo la uhaba wa dawa kwani zipo za kutosha.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akionesha juu Bango Kitita la famasia baada ya kulizindua wakati  wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Bakari.

WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya jamii.

WASANII mbalimbali wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya Tamasha la Sport Music Festival ambalo linatarajia kufanyika leo Kanda ya Ziwa.
Lengo la tamasha hilo ni kuhakikisha wananchi wa Kanda ya Ziwa katika Sikuu ya Eid Elfitri wanasheherekea siku hiyo kwa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.Tamasha hilo la aina yake litafanyika maeneo ya Geita,Mwanza na Kahama.

Kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo ni kwamba pia kutakuwa na michezo ya pikipiki pamoja na magari huku wakisindikizwa na wasanii mbalimbali wa Bongo fleva.Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro Profesa Jay(Chadema)ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya amewataka mashabiki zake wafike kumshuhudia akitoa burudani.

"Tangu niwe mbunge sijafanya shoo kubwa, hivyo hii ndio ya kwanza nitafanya maajabu kwenu,"amesema Prof. Jay.Kwa upande wa Snura Mushi a.k.a Snura amesema amejipanga kwa kufanya mazoezi licha ya kukaa mwezi  mzima wa mfungo bila kufanya shoo. "Nimewaandalia vitu vingi na vipya mashabiki zangu,nimejipanga kutengeneza vitu vipya tofauti na mlivyovizoea,"amesema.

Wakati huohuo Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Weusi G Nako amewasili nchini ambako naye atashiriki katika tamasha hilo kwa kufanya shoo ya kibabe , hivyo amewataka mashabiki kjitokeza kwa wingi. Burudani hizo kwa siku ya leo zitaanzia Geita, kesho Mwanza na kumalizikia Kahama keshokutwa.
 Mbunge wa jimbo la mikumi ambaye ni msanii wa kizazi kipya prifesa jay akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika viwanja vya ndege jijini Mwanza,akizungumzia ujio wake mpya kwa wakazi wa kanda ya ziwa,ambapo amesema bado yupo fiti   licha ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya shoo kubwa.
 Msanii wa kizazi kipya kutoka weusi G Nako akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutua katika viwanja vya ndege jijini Mwanza kuhusu ujio wake tena kwa wakazi wakanda ga ziwa  ambapo amewataka wajitokeze kwa wingi kushudia burudani ya uhakika kutoka kwake na shangwe zakutosha.
Mama wa chura snura mushi akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika  Viwanja vya ndege leo jijini mwanza ambapo amewataka mashabiki wa kanda ya ziwa wajitokeze kumshuhudia akitoa buruda yake ambayo itakua na vitu vingi vipya kwenye tamsha hilo la sport music festival litakalofanyika,Geita,Mwanza,Kahama katika kusheherekea sikukuu ya Iddy.

MWENYEKITI WA WAZAZI KINONDONI AHIMIZA UMAKINI SIKUKUU YA EID ELFITRI

$
0
0
Na Emmanel Massaka ,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Said Subety amewataka madereva wote wa gari, pikipiki na bajaji kuwa makini katika Sikukuu ya Eid Alfitri kwani siku hiyo kunakuwa na watoto wengi barabarani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Subety amesema katika Sikuu ya Eid ni vema jamii ikachukua tahadhari kwa kuhakikisha hakuna ajali ambazo zinatokea na hasa kwa watoto na kwamba vipengele vya umakini vimegawanyika katika maeneo matatu katika sherehe ya sikuku hiyo. 

Amesema kwanza ni umakini kwa wazazi na walezi ambapo amefafanua jinsi watoto wanavyokuwa wengi wakisheherekea sikuku hiyo kwa kurandaranda sehemu mbalimbali wakiwa na furaha na hata bila ya tahadhari yoyote, bila wazazi au uangalizi makini wanahitaji kuangaliwa kwa umakini.

Amesema na mara nyingi kiongozi wao ni mtoto mwenzao na hakika matembezi yao wanatembelea sehemu nyingine ni hatarishi kama baharini ambako watoto wengi hupenda kwenda huko kwa ajili ya kuogelea na barabarani, hivyo amewasisitiza wazazi wasiwaache watoto wakienda bila uangalizi wa maana.

Pia kwa wenye kumbi za starehe ambazo zitachukua watoto washeherekee nao wawe makini na wasifanye biashara kwa tamaa kubwa kwa kuwajaza watoto kupita uwezo wa kumbi zao kwani ni hatari.

"Tunawapongeza sana Waislamu wote hususani wale waliofunga Mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwenyezi Mungu apokee swaumu zetu, kwa baraka za funga zao, Mungu atujalie ulinzi wa amani wa nchi yetu, Rais wetu Dk. John Magufuli na wananchi wote, Amen,"amesema. 
 Mjumbe wa kamati ya utekelezaji baraza la Wilaya ya Wazazi Kinondoni,kwege Nyangunda asisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za sisi Kinondoni.
 Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Kinondoni wa Chama cha Mapinduzi,Said Dubety (kulia)akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mandereva waendeshai vyombo vya moto kuwa makini barabarani,siku ya sikukuu ya (Eid Elfri) .kulia ni Mjumbe wa mkutano mkuu wazazi Taifa,Hassan Kaniki.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Picha ya pamoja

Wahasibu Mamlaka za Serikali za Mitaa Watakiwa Kuzingatia Matumizi Sahihi ya Fedha za Umma

$
0
0
Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Waweka Hazina na Wahasibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha za Umma kupitia mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) unaotarajia kuanza kutumika na mamlaka hizo kuanzia  Julai 1 mwaka huu.
Hayo yameelezwa leo, Jijini Dodoma na Mhasibu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jeremiah Mtawa alipokuwa akifunga mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara.
“Kuanzia Julai 1 mwaka huu mfumo wa epicor 10.2 ndio utakaotumika katika kuonesha mapato na matumizi ya fedha za Umma katika Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini, hivyo mfumo huu ukatumike kama ulivyopangwa na kwa usahihi,” alisema Mtawa.
Aidha amewataka Wahasibu hao kutumia mfumo huo vizuri kwani umeunganishwa na mfumo unaowezesha mabenki kulipana Tanzania (TISS) ambao utaruhusu malipo yote kufanyika kwa njia ya kielektroniki. Hivyo basi, kama mfumo huo utatumika vibaya basi Mhasibu husika atafunguliwa kesi.
Kwa upande wake, Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bibi Mariamu Nkanyanga ambaye ni mshiriki wa mafunzo hayo amesema epicor 10.2 itasaidia kutekeleza kwa asilimia kubwa shughuli ambazo zimeelekezwa katika bajeti ya mwaka husika kutokana na mfumo huo kutoruhusu malipo nje ya bajeti na ikiwa malipo yoyote yatafanyika  nje ya bajeti basi yataonekana kwenye mfumo huo tofauti na mfumo unaotumika sasa.
Nae, Mhasibu wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Ajuaye Jasho amesema mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) utaondoa matumizi holela ya fedha za Umma kutokana na matumizi yote ya Halmashauri kuidhinishwa na Mweka Hazina tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo kuna matumizi yalikuwa yakiidhinishwa na Mweka Hazina na matumizi mengine yalikuwa yakiidhinishwa na Mhasibu yeyote wa Halmashauri husika.
Mafunzo ya mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) yanaendelea kutolewa katika vituo Sita nchini ambavyo ni Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza, Kagera na Mtwara yakihusisha Waweka Hazina, Wahasibu, Maafisa Manunuzi, Wakaguzi wa Ndani na Maafisa TEHAMA, lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo watumiaji wa mfumo huo namna ya kutumia mfumo huo unaotarajia kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini.
 Mhasibu Mwandamizi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jeremiah Mtawa akiongea na Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya mfumo wa epicor 10.2, alipokuwa akifunga mafunzo ya siku Nne ya mfumo huo kwa Waweka Hazina na Wahasibu, leo Jijini Dodoma. Mfumo huo unaotarajia kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini.
 Mhasibu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Simeon Mwanjwango  (aliyesimama) ambaye ni mwenyekiti wa darasa la mafunzo ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) kwa Waweka Hazina na Wahasibu wa Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi Bw. Jeremiah Mtawa (hayupo pichani) namna walivyopokea mafunzo ya epicor 10.2, wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo,  leo Jijini Dodoma.
Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara wakimsikiliza mgeni rasmi Bw. Jeremiah Mtawa (hayupo pichani) alipokuwa akifunga mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo Wahasibu hao namna ya kutumia mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) unaotarajia kuanza kutumika na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini kuanzia Julai 1 mwaka huu.

WAISLAM TABORA WAMPONGEZA JPM KWA MISAADA YAKE

$
0
0
SHEIKH wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi amemupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kusaidia shughuli mbalimbali za kuendeleza miradi ya madhehebu mbalimbali ikiwemo  ya Waislamu hapa nchini.
Alitoa kauli hiyo mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora

Sheikh Mavumbi alisema misaada anayochangia ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za Ibada ni jambo zuri na linamuonyesha kuwa yeye sio mbaguzi  na ameonyesha mapenzi makubwa aliyonayo kwa watu wote bila kujali tofauti zao , hali inayosaidia kuimarisha umoja wa Kitaifa ulioasisiwa tangu uhuru wa Nchi ya Tanzania.

Sheikh huyo wa Mkoa aliwataka Waislamu wote nchini kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli na Serikali yake katika jitihada zake mbalimbali za kuwaletea wananchi maendeleo hapa nchini.

Alitoa wito kwa wakazi wote Mkoani hapa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kudumisha mshikamano na upendo ili amani iliyopo iendelee kudumu na waumini waendelea kusali bila wasiwasi katika nyumba zao za Ibada.

Aidha Sheikh Mavumbi aliwataka Masheikh wa ngazi zote na Maimam kuhakikisha kuwa ndoa wanazofungisha zingatie maandiko matakatifu ili kuepuka kusababisha kuwepo na ndoa za utotoni mkoani humo.
 Sheikh  wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi (mbele) akiongoza Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislaam wakiwa katika Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.
 Baadhi wakimama wa dini ya Kiislam wakisikiliza salamu za Eid El Fitri kwa niaba ya Serikali kutoka kwa  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza (hayupo katika picha) mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.
Baadhi ya Wakinababa wa dini ya Kiislam wakisikiliza salamu za Eid El Fitri kwa niaba ya Serikali kutoka kwa  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandizi wa Magereza(SACP) Hamza Hamza (hayupo katika picha) mara baada ya Swala ya Eid El Fitri iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana (leo) mjini Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA

$
0
0
* Ni baada ya kumalizika kwa  Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
RAIS Dkt. John Magufuli amewaasa Waislam na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kutenda mema baada ya kuwa wamejisahihisha na kutubu makosa yao ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Juni 15, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli kwenye Baraza la Eid El Fitr lililofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Viongozi wanaendelea kuwasihi Waislam wote na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuonesha upendo, umoja na kuvumiliana  hasa baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema huruma, ukarimu na ucha Mungu ulioneshwa katika kipindi cha mfungo wa ramadhani, uendelee na uwe sehemu ya maisha ya kila siku na kamwe usiwe umeisha baada ya mwandamo wa mwezi wa mfungo mosi.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa upendo, umoja, utulivu, mshikamano na subra uliooneshwa kipindi chote cha mfungo wa ramadhani ni vema ukaendelezwa kwa sababu ucha Mungu si katika mwezi huo pekee.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameniagiza kwa kusema ‘’Waislam ni kielelezo cha taasisi za dini zinazozingatia maadili mema, hivyo wachache wasijipenyeze na kuharibu taswira yao. Ninawahakikishia kuwa Serikali iko tayari kushirikiana taasisi yeyote ya dini ambayo itakuwa tayari kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na taratibu tulizojiwekea nchini’’
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir  (wapili kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salim (wapili kushoto) baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika  Baraza la Eid, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) kuingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Baraza la Eid Juni 15, 2018. Wapili kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salim.
Baadhi ya waliohudhuria katika Baraza la Eid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo akimwakilisha  Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 15, 2018.
aziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiteta na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir katika Baraza la Eid kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoj jijini Dar es salaam Juni 15, 2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli . 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Baraza la Eid kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 15, 2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKINA MAMA 925,342 NCHINI WASAJILIWA NA MRADI WA TUMAINI LA MAMA

$
0
0
WAKINA mama 925,342 nchini wamefanikiwa kusajiliwa na mradi wa “Tumaini la Mama tokea ulipoanza mwaka 2012 na kuweza kunufaika huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga kilichofanyika mjini Korogwe.

Alisema idadi hiyo ni kuanzia mpango huo ulipoanza hadi mwezi Mei mwaka huu huku wakina mama wapatao 323,797 wakitokea mkoani Tanga pekee ambao wamesajiliwa.

Aidha alisema pia kaya 323.797 zimenufaika na kulipiwa fedha kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo sh.milioni 48,077,859,434 zimelipwa kwa watoa tokea mradi huo ulipoanza huku vituo vya mkoa wa Tanga vikilipwa kiasi cha sh.milioni 12,449,902,412.

“Pia vifaa tiba vyenye ya sh. milioni 900 vimenunuliwa na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma pia mradi umesaidia upatikanaji wa computers katika vituo vyenye mahitaji kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa kumbukumbu”Alisema.

“Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana mfuko utakaa na mfadhili kuona uwezekano wa kupata fedha zaidi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi sisi viongozi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba mradi unatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili mfadhili aone umuhimu wa kuongeza muda zaidi”Alisema.
Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa akizungumza wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga kilichofanyika mjini Korogwe katikati ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
 MKUU wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akifungua kikao hicho kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Ally Mwakababu
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mbaruku Mgawa
Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita
 Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona,Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Jairy Khanga
 Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia kwa umakini kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Luiza Mlelwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images