Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO JUNI 13, 2018


DKT. NDUGULILE AAGIZA MADAKTARI KUCHUNGUZA UKATILI KWA WATOTO WACHANGA

Introducing "Vurugu na Papara" (Official Video ) by Genevive

$
0
0
Vurugu na Papara is the fifth debut single for the African Glamour and beauty Queen Genevieve who claimed the title of the most beautiful girl in Tanzania and crowned Miss Tanzania in the year 2010. The song was solely written by Barnaba Classic Boy and produced by Deey Classic at High Table Sound back in 2016. Vurugu na Papara is Genevieve's second recorded single after Bonnie and Clyde but it is the Fifth to be released and the sixth in total ( including a Diamonds by Rihanna cover) After a successful release of Nana, Bonnie and Clyde, Naringa and Hoi, here is another classic single #VuruguNaPapara by your one and only Genevieve. The song is available on all platforms

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 13.06.2018

INTRODUCING FIFA WORLD CUP 2018 "GO AFRICA" SONG

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 14, 2018

IGP SIRRO ASAIDIA KUOKOKOA MAJERUHI ALIYEPATA AJALI WAKATI AKIWA SAFARINI KUELEKEA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa na baadhi ya wananchi na abiria waliokuwa safarini wakisaidiana kuokoa majeruhi kutoka kwenye roli aina ya Scania lenye namba T 396 CCY iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam baada ya kupata ajali na kuanguka katika eneo la Bwawani mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi mmoja ambaye ni dereva wa roli hilo. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wa Pili kulia), akiwa na dereva wa roli aina ya Scania (wa pili kushoto)  aliyeokolewa muda mfupi uliopita kutoka kwenye roli alilokuwa akiliendesha baada ya kupata ajali na kuanguka katika eneo la Bwawani mkoani Morogoro na kusababisha majeruhi mmoja ambaye ni dereva wa roli hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto, muda mfupi baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati), akizungumza na kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto na kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mugabo Wekwe alipokutananao katika mpaka unaotenganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kabla ya kuwasili mkoani Dodoma kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.


Waziri afanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Maziwa Makuu Mhe. Said Djinnit alipomtembelea Wizarani terehe 13 Juni 2018, Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez.

Mjumbe huyo alifika Wizarani kwa lengo la kuzungumzia hali ya usalama na amani katika nchi za Maziwa Makuu.Aidha, mjumbe huyo alimuomba Mhe. Waziri kufikisha shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa mchango mkubwa wa Tanzania katika kusaidia kutunza amani ya nchi za Maziwa Makuu.

 Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mhe.Djinnit.
Mkutano ukiendelea, wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bw. Salvatory Mbilinyi(wa kwanza kulia kwa Waziri), Bw. Ally Ubwa Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi Katibu wa Waziri na kushoto ni Ujumbe wa Mhe. Djinnit alioongozana nao.

Mjumbe wa Katibu Mkuu UN ahimiza ushirikiano kukabili uhalifu

$
0
0
Na Mwandishi wetu
MJUMBE maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), Said Djinnit ametaka nchi wanachama wa Umoja wa Ushirikiano katika masuala ya kisheria katika nchi hizo za ICGLR , kuongeza kasi ya mashirikiano ili kukabiliana na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Nchi zinazounda umoja wa ICGRL pamoja mwenyeji Tanzania ni Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya kati, Congo, Kenya, Rwanda, Sudan, South Sudan, Uganda na Zambia.
Alisema pamoja na kufikia maendeleo ya kutosha katika ushirikiano wa kisheria nchi hizo kwa sasa zinatakiwa kuungana zaidi kutokana na watenda uhalifu dhidi ya ubinadamu kuendelea kujificha katika nchi mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano wa pili wa umoja huo uliofanyika jijini Dar es salaam jana, Djinnit alisema kwamba mambo makubwa mazuri yamefanyika miongoni mwa nchi hizo tangu kuuanzishwa kwa ushirikiano huo, na kutaka wazidi kujiimarishwa sanjari na ushirikiano mwingine wa kukomesha uhalifu.
Alisema bila kukomeshwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu mataifa ya Maziwa makuu yatakuwa katika hekaheka na hiyvo kukosa maendeleo kutokana na kukosekana kwa amani.
Awali akmimkaribisha mjumbe huyo kufungua mkutano, Naibu Mkurugenzi Mwendesha Mashtaka nchini Tanzania, Frederick Kapela Manyanda alishukuru ushiriki wa wajumbe wa wataalamu wa sheria kutoka nchi za ICGLR akisema ujio wao ni neema ya kufanikisha ushirikiano dhidi ya vitendo vya kihalifu.
 Naibu Mkurugenzi Mwendesha Mashtaka nchini Tanzania, Frederick Manyanda akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
 Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa ICGLR, Bi. Eliane Mokodopo akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa ICGLR, Balozi Zachary Muburi-Muita (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), Said Djinnit akizungumza wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Uholanzi nchini, Mh. Jeroen Verheul akitoa salamu za taifa la Uholanzi wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja (UNDP), Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mwendesha Mashtaka nchini Tanzania, Frederick Manyanda, Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa ICGLR, Bi. Eliane Mokodopo pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Mh. Jeroen Verheu wakati mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Natalie Boucly (kulia) na wajumbe wengine wakifuatilia kwa umakini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiwasishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa Marekani nchini Immi Patterson (kushoto) akiandika mambo muhimu wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja (UNDP), Alvaro Rodriguez akipitia makabrasha wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ECOBANK YAPANDA MITI 130 UFUKWE WA BARABARA YA BARACK OBAMA JIJINI DAR

$
0
0
BAADA ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kufungua ukuta uliojengwa katika ufukwe wa barabara ya Barack Obama jijini Dar es salaam, leo June 14 Ecobank wamepanda miti ipatayo 130 ili kutunza  mazingira yanayozunguka eneo hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee ameeleza kuwa benki hiyo ni ya watu na inajali jamii inayowazunguka hivyo suala la mazingira linapewa kipaumbele kwa kiwango cha juu.

Ameeleza kuwa zoezi hilo la upandaji miti linafanywa na nchi 33 Afrika ambazo Ecobank inatoa huduma zake wakiwa na kauli mbiu ya  "Panda leo, Uilinde kesho."

Mwanahiba amesema kuwa kwa Tanzania wameandaa miti 500 katika shule ya awali na msingi iitwayo kisimani iliyoko Arusha na leo wamepanda miti 130 katika fukwe hizo.

Aidha ameeleza kuwa wamejikita katika kubadilisha mfumo wa kibenki wa Afrika katika kuwahudumia wateja kwa ufanisi, rahisi na kwa gharama nafuu kama vile, utumiaji wa aplikasheni ya simu (mobile app) ambayo hadi sasa imepakuliwa na zaidi ya wateja Milioni 5.

Pia amewashukuru wafanyakazi wa Ecobank kwa kwa ushirikiano wao katika kuungana na jamii kwa kuhakikisha watoto na vizazi vijavyo wanafurahia matunda ya utunzaji wa mazingira katika sayari hii adimu.

 Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee(kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Sea View, Victor Angelo Muneni(kulia) wakipanda mti kwenye fukwe ya barabara ya Barack Obama wakati wa hafla ya upandaji miti katika eneo hilo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee pamoja na Mwenyekiti wa Sea View, Victor Angelo Muneni na Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala Feada Magesa wakimwagilia maji moja ya mti walioupanda wakati wa zoezi wa upandaji miti 130 katika eneo la fukwe ya barabara ya Barack Obama.
   Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti 130 katika eneo la fukwe ya barabara ya Barack Obama. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Furaha Samalu na kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Sea View, Victor Angelo Muneni

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIJANA MTWARA WANUFAIKA NA UJASILIAMALI

$
0
0
JOSEPH MPANGALA , MTWARA 

Zaidi ya Vijana 200 wa Mkoa wa Mtwara wameunufaika na Ujasiliamali Kupitia Mradi wa KIJANA JIKWAMUE unaotekelezwa na Shirika la Africare na kufadhiliwa na Kampuni ya Uchimbaji na Uzalishaji Nishati ya Gas na Mafuta ya Shell. 

Vijana hao waliopo katika Makundi 12 ambapo wanajishulisha na Ufugaji wa nyuki,Ufugaji wa Kukubora,Kilimo,Biashara Ndogondogo pamoja na kuongeza thamani Bidhaa mbalimbali na kuzitafutia masoko kwe lengo la kujipatia Kipato cha kila siku. 

Frank Lyimo meneja Mradi anasema Mradi umeanza kuonesha mafanikio kutokana na baadhi ya Vikundi wameanza kuzalisha Bidhaa Bora ambazo zimeonekana kuwa na Ushindani katika Masoko tofauti kutokana na Kupata Vifungashio Bora na vyenye Nembo inayovutia. 

“Mradi wa Kijana Jikwamue Unashughulika na kuwajengea uwezo wajasiliamali ambo kwa sasa umeonesha mafanikio kutokana na baadhi ya vikundi wanaweza kuzalisha Bidhaa Bora kwa mfano kuna kikundi kinafuga Kukumiatano mpaka Elfmoja ambao wanapelekwa sokoni wafikapo kuanzia kilo 1.3 na Tumewawezesha mabanda ya kutosha lakini wengine wanaongeza thamani Kilimo cha Mboga mboga pamoja na Asali” amesema Frank. 

Naye Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna anasema Kunaonekana kuwa na mafanikio kutoka Mradi wa awam ya kwanza na sasa awam ya Pili ambapo lengo kubwa ni kuwawezesha kupanua Biashara ili kuweza kupata masoko sio tu kwa mkoa wa Mtwa balinchi Nzima. 

“Nimefurahi sana kutembelea miradi hii na kuona manufaa ambayo Wananchii wameyapata kutoka kwenye awam ya kwanza na sasa hivi awam ya Pili na Tunaimani kuwa kwenye hii awam ya Pili watu watapata mafunzobora zaidi na waweze kupata masoko kwa sababu lengo la Awam ya Pili ni kuwawezesha waweze kupanua Biasha na kupata masoko Nje ya Mkoa wa Mtwara” 

Abdulah Mkumbila ni mmoja wa wajumbe kutoka kikundi cha Jikomboe Kilichopo Mtaa Lwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani anasema walianza na Mizinga mitano{5} kwa ajili ya kufuga Nyuki lakini kwa sasa wanamizinga Sitini{60}ambayo inaweza kuzalisha Asali Lita Miambili na Ishiriri{220} 

“ Kutokana na Kupata Mizinga hii tayari baadhi ya wajumbe wameweza kujenga Nyumba Bora kwa utaratibu wa kukopa pesa na kurejesha na wengine wamenunua Pikipiki lakini Bado Kikundi kipo kwenye Mchakato wakuongeza Miradi Mingine kama Vile Ulimaji wa Bustani za Mboga Mboga ili kuongeza kipato”
Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna akitoa Ufafanuzi Kuhusiana na Ushiriki wa kampuni yake katika Mkutano kamati ya utendaji ya mradi wa Kijana Jikwamue Unaoendeshwa na Shirika la Africare na Kufadhiliwa na Kampuni ya Shell Mkutano Ulifanyika Mkoani Mtwara
Wajumbe wa kamati ya Utendaji wa Mradi wa Kijana Jikwamue Wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya Kumaliza Kikao cha kupokea Taarifa za Mradi wa Awam ya Kwanza pamoja na Mapendekezo na Mpango kazi wa Mradi kwa awamu ya Pili kwa ajili ya kuwawezesha Vijana wa Mkoa wa Mtwara
Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna akipokea Taarifa ya Utendaji Kutoka kwa Abdulah Mkumbila ambaye ni Mjumbe wa Kikundi cha Jikomboe Kilichopo Mtaa wa Lwilo ambacho kinajishughulisha na Uzalishaji wa Asali Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Shirika la Africare Alfred Kalaghe. 
Kutoka Kushoto Muweka hazina wa Kikundi cha Jikomboe Salum Nampaya akitoa Maelezo Kuhusiana na Uvunaji wa asali kwa Viongozi wa Africare Walipotembelewa Mtaa wa Lwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo tangu walipoanza kikundi kilikuwa na Mizinga Mitano kwa ajili ya ufugaji nyuki lakini kwa sasa wameweza kuwa na Mizinga Sitini {60} ambapo wanaweza kuvuna Asali Lita Miambili na Ishirini 220}

WAGANGA WAKUU WAAGIZWA KUKAGUA WATOTO WACHANGA KUBAINI UKEKETAJI

$
0
0
                 Na Jacquiline Mrisho - 
SERIKALI imewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha wanawafanyia uchunguzi watoto wachanga wanaopelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kubaini kama wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji.

Agizo hilo limetolewa leo Jijini Arusha na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoazimishwa kitaifa jijini humo katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume.

Dkt. Ndugulile amesema kutokana na watoto kuendelea kujengewa uwezo kuhusu hasara za ukeketaji wamekuwa wanajitahidi kutoa taarifa  sehemu husika hivyo wazazi wameamua kuanzisha mbinu mpya za kuwakeketa watoto wachanga jambo ambalo haliwezi kuvumilika.

“Suala la ukeketaji watoto wachanga liko ndani ya uwezo wangu hivyo naagiza kutolewa kwa waraka kwa Waganga Wakuu wote nchini  kuwakagua watoto wanaoenda kliniki ili kubaini kama wamekeketwa na kuwachukulia hatua za kisheria wazazi waliohusika na vitendo hivyo,” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa ukeketaji bado ni changamoto kubwa nchini ambapo takwimu za mwaka 2015 zimeonyesha bado kuna mikoa mitano ambayo iko juu ya wastani wa kitaifa katika suala la ukeketaji hivyo ni lazima agizo hilo litekelezwe kwa haraka ili kukomesha tatizo hilo.

Ameitaja mikoa inayoongoza kwa ukeketaji kuwa ni Mkoa wa Manyara unaongoza kwa asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha asilimia 41, Mara asilimia 32 na Singida asilimia 31.

Vile vile Dkt. Ndugulile ameelezea kukithiri kwa mimba za utotoni ambapo Mkoa wa Katavi unaongoza kwa asilimia 45, Tabora asilimia 43, Mara asilimia 37 na Shinyanga asilimia 34.

Ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa kuhakikisha Mabaraza ya Watoto yanasambazwa katika ngazi zote nchini ili watoto wapate uwakilishi mkubwa wa masuala mbalimbali yanayowahusu.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Plan International, Benatus Sambili amesema kuwa shirika hilo linafanya kazi pamoja na Serikali katika kuziba mianya iliyopo katika jamii ambayo inazuia watoto kupata haki zao zikiwemo za kuwapa elimu na stadi za maisha pamoja na elimu ya kujitambua.

“Shirika letu lina miradi ambayo inawasaidia watoto ikiwemo miradi ya kupinga ndoa za utotoni katika mikoa ya Mara, Morogoro, Geita na Rukwa lenye lengo la kuwafikia zaidi ya watoto 28,755, mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia mashuleni ambapo tumelenga kuwafikia watoto 35,000 pamoja na mradi wa kupunguza na kuondoa ajira za watoto katika maeneo ya migodi kwa watoto zaidi ya 22,000” alisema Sambili .

Maadhimisho hayo hufanyika kila Juni 16 ambapo kwa mwaka huu yameadhimishwa Juni 13 kwa sababu siku husika itakuwa na muingiliano wa ratiba zingine, kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘kuelekea uchumi wa viwanda, tusiwaache watoto nyuma’.
 Watoto wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika Maaandamano ya Siku ya myoto wa Afrika yenye Kauli Mbiu isemayo Kuelekea uchumi wa Viwanda Tusimuache Mtoto Nyuma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na watoto waliokusanyika katika kiwanja cha mpira cha Shkeih Amri Abed Jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Sihaba Nkinga akielezea chimbuko la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Jijini Arusha.

MRADI UBORESHAJI RELI YA KATI DAR ES SALAAM - ISAKA (TRC) WANANCHI WAANZA KUELIMISHWA

$
0
0
Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Uongozi wa TRC wamedhamiria kukarabati reli ya kati kipande cha kuanzia Dar es Salaam – Isaka (km970). Mradi huu umefadhiliwa na Benki ya dunia na kutekelezwa na Shirika la Reli Tanzania katika kipindi cha muda wa miaka miwili kuanzia juni 2018 hadi juni 2020. 

Lengo la uboreshaji wa reli ya kati ni kutoa usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora Nchini. Na maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mzigo toka chini ya tani 13.5 za uzito wa eskeli hadi tani 18.5 kwa kufanya yafuatayo: 

I. Kutandika upya njia za reli zenye uzani wa paundi 80 kwa urefu wa kilometa 312 

II. Kufanya ukarabati wa njia ya reli iliyosalia kwa urefu wa kilometa 658 

III. Kufanyia ukarabati makaravati na madaraja 442 

IV. Kuboresha mfumo wa mawasiliano 

V. Kuboresha vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam, ilala na Bandari kavu ya Isaka. 

VI. Ununuzi wa vichwa vitatu vya treni (vipya) na mabehewa mapya 44 ya mizigo 

Katika kufikia malengo haya TRC itaingia mikataba 64 kati ya hiyo 32 ni ya kuajiri Washauri mbalimbali, 6 ni ya ujenzi na 24 ununuzi wa vifaa mballimbali na mikataba miwili ni ya huduma. Mpaka sasa zaidi ya 50% ya mikataba hii imeshasainiwa. 

Kupitia Mradi huu TRC pia imetengeneza mpango endelevu wa matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya usafiri huu kuwa wa uhakika na kuaminika. Kuimarika kwa usafiri wa reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo serikali kuelekeza bajeti iliyookolewa kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii. 
 Afisa maendeleo ya jamii TRC Bi Catherine Mroso, , akitoa maelezo katika kampeni ya uhamasishaji wa uelewa wa uboreshaji wa reli ya kati Dar es Salaam – Isaka katika mkutano na viongozi wa Halimashauri ya kibaha vijijini, Magindu, Mkoani Pwani. 
Wanakijiji wa Halmashauri ya kibaha vijijini, wakifuatilia kwa makini maelelezo yanayotolewa katika mkutano unaoendeshwa na wataalamu kutoka shirika la reli Tanzania - TRC Kuhusu uboreshaji wa Reli ya kati Dar es salaam- Isaka
Mratibu wa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dares Salaam- Isaka, kutoka TRC Mhandisi Mlemba Allen Singo ni  akitoa maelezo katika mkutano wa wananchi wa Halmashauri ya Kibaha vijijini, Magindu, Mkoani Pwani
Muonekano wa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dares Salaam- Isaka ukiendelea.

Serikali Yatumia TEHAMA Kuokoa Mabilioni ya Shilingi

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Serikali inaokoa takribani shilingi bilioni moja kutokana na kutumika kwa mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kuwachagua na kuwapingia shule wanafunzi   wanaojiunga na kidato cha tano katika shule zote hapa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Mbeya, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick  Kitali amesema kuwa mfumo huo umejengwa kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ukilenga kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo malalamiko kutoka kwa wanafunzi wakati wa kupangiwa shule kulingana na ufaulu wao.
“Kwa sasa Serikali inatumia watumishi wasiozidi 20 wakati awali walitumika zaidi ya 300 katika kuwapangia wanafunzi shule za kidato cha tano hali ambayo imepelekea kupungua kwa gharama za uendeshaji wa mchakato huo kwa kiasi kikubwa.” Alisisitiza Kitali.
Akifafanua Bw. Kitali amesema kuwa mfumo huo tangu uanze kutumika umeondoa malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo wakati wa kuwapangia wanafunzi shule kwa kuwa kinachozingatiwa ni sifa za mwanafunzi husika na mchepuo anaotaka kuchukua anapojiunga kidato cha tano na si vinginevyo.
 Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza jambo kwa  washirki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 jijini yanayoendelea jijini   Mbeya.
 Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka  PS3 Bw. Desderi  Wengaa akisisitiza jambo kwa Meneja wa Fedha  PS3  Perpetua Ngogo wakati wa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 leo jijini  Mbeya.
 Afisa Usimamizi  Fedha Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Mmaka Mwinjaka akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo wa EPICOR 10.2 leo jijini Mbeya kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya.
Sehemu ya awamu ya pili ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa EPICOR 10.2 yanayoendelea Jijini Mbeya ikiwa ni siku ya tatu ya mafunzo hayo.n(Picha  zote na Frank Mvungi- MAELEZO)
 
 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI MKUU KUTOKA BENKI YA NMB OFISINI KWAKE BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya NMB, Ndg. Ineke Bussemaker alipomtembelea leo Tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu na Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya NMB, Ndg. Ineke Bussemaker alipomtembelea leo tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Wageni kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu kutoka NMB, Ndg. Ineke Bussemaker (kushoto kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wageni kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Ndg. Ineke Bussemaker (wa pili kulia) walipomtembelea leo tarehe 14 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Hatimiliki za kimila 747 kutolewa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

$
0
0
Shirika la PELUM Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeanza zoezi la kutoa hatimiliki za kimila zipatazo 747 kwa wananchi wa vijiji vitano ambao wamefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo ulio chini ya watu wa marekani 

Hatimiliki hizo zinatarajia kunufaisha wanawake 250, wanaume 385, wenza wenye ushiriki wa pamoja 97 pamoja na maeneo ya Taasisis 97 toka vijiji vya Usokame, Ugesa, Magunguli, Isaula na Makungu

Simon Mbago Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mufindi anayesimamia zoezi hili, mbali na kulishukuru Shirika la PELUM Tanzania kwa kufanya nao kazi kwenye vijiji hivyo amesema kufanyika kwa mpango wa matumzi ya ardhi hadi kufikia utoaji wa hatimiliki imesaidia kutekeleza majukumu ya Halmashauri ambayo yalipaswa kutekelezwa na Halmashauri husika.

“Ni jukumu la kila Halmshauri kuhakikisha inatenga fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ili kufanyia vijiji vyake mpango wa matumizi ya ardhi lakini uwepo wa mashirika binafsi kutekeleza jukumu hili ikiwemo PELUM Tanzania imesaidia kwa kiwango kikubwa kuchochochea maendeleo katika Halmashauri yetu.”

Hivyo basi uwepo wa hatimiliki hizi tunazogawa zitasaidia wananchi wa Halmashauri yetu kuzitumia kuomba mikopo kwenye taasisi za fedha kwa kuweka dhamana maeneo yao jambo ambalo wamekuwa wakilisubiri kwa kipindi kirefu ili kuwawezesha kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kupita fedha watakazopata.
Evance Kibasa Mwananchi kutoka kijiji cha Usokame akiwa na Hatimiliki yake ya kimila baada ya kukabidhiwa.
Mmoja wa wananchi toka kijiji cha Usokame akikabidhiwa hatimiliki ya kimila na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Simon Mbago
Asafu Mgelekwa na Mkewe Atuganule Lunyungu wakiwa na hati yao yenye umiliki wa pamoja
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ugesa wakiwa na hatimiliki zao za kimila

ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA

$
0
0
Na Dixon Busagaga-MOSHI.

MWANAMKE aliyejifungua watoto Mapacha akiwa Mahabusu ,Marry Lukumay ameendelea kusota Gerezani na watoto wake baada ya kukosekana kwa wadhamini wenye sifa zinazokidhi masharti yaliyotolewa na Mahakama.

Miongoni mwa masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu mkazi ,Moshi ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watakaosaini Fungu la Dhamana la kiasi cha sh laki tano kila mmoja.Marry Lukumay mkazi wa Babati mkoani Manyara kwa mara nyingine alifikishwa mahakama ya hakimu Mkazi ,Moshi baada ya kukamatwa Oktoba 15 mwaka jana kwa madai ya kukutwa na Mirungi kilogramu 10.

Katika shauri hilo namba 182 la mwaka 2017 ,mwendesha mashtaka upande wa Jamhuri ,Lilian Kowelo aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo kutokana na upelelezi kutokamilika .Hakimu anayesikiliza shauri hilo ,Pamela Meena alikubaliana na ombi hilo na kupanga June 27 mwaka huu ,mtuhumiwa kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Akizungumza na mwanahabari wetu nje ya Mahakama ,Mwanamke huyo aliyewapa majina watoto wake ya Nora na Noreen wenye umri sasa wa miezi miwili sasa alisema alikamatwa mwaka jana katika eneo la Himo Oktoba mwaka jana.Alisema kuwa, Oktoba 24 Mwaka jana alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka linalomkabili na kuelezwa kuwa dhamana yake ipo wazi huku akitakiwa kuwa na wadhamini wawili.

Mary anayeshikiliwa katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro alisema wakati anakamatwa tayari alikuwa na ujauzito wa miezi miwili na Aprily 8 mwaka huu alijifungua watoto hao Mapacha katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi .

NAY WA MITEGO KUPAMBA DODOMA BUILDERS EXPO 2018

TMA YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA NCHINI KWA KIPINDI CHA MWEZI JUNI – AGOSTI (JJA), 2018

$
0
0
Na. Monica Mutoni 


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa mwelekeo wa hali ya hewa nchini kwa kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka 2018. Taarifa hiyo imetoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa, joto, upepo na mvua, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Mamlaka imeeleza kuwa uwepo kwa hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi inatarajiwa katika maeneo ya miinuko ya nyanda za juu Kaskazini mashariki (Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Nyanda za juu kusini Magharibi (hususani mkoa wa Njombe) pamoja na maeneo ya miinuko ya mkoa wa Tanga (hususan wilaya za Lushoto na Bumbuli). 

Kuhusu hali ya mvua na upepo taarifa hiyo imeeleza kuwa maeneo mengi yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla,pamoja na vipindi vifupi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo. Aidha, vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya pwani hususan katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Juni, 2018 na vipindi kadhaa kwa mwezi Julai, 2018. 

Wananchi wameendelea kushauriwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kama vile hali ya baridi inayotarajiwa katika maeneo mengi ya nchi hususan maeneo ya miinuko nakuweza kusababisha kudumaa kwa mazao kama vile ndizi pamoja na mazao ya nje ya msimu, na kuathiri mifugo. Vile vile, kutokana na hali ya joto katika bahari ya Hindi kuwa juu ya wastani kiasi, ongezeko la siku zenye tija katika shughuli za uvuvi katika kipindi cha msimu wa JJA linatarajiwa. 

Kwa taarifa zaidi temebelea tovuti www.meteo.go.tz

VODACOM YASHEREKEA MIAKA 10 YA M-PESA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
KATIKA kuadhimisha miaka kumi ya M-PESA kampuni ya simu ya mkononi Vodacom Tanzania imesherekea hafla hiyo ya kwa kutoa futari kwa wateja wake na kuwahamasisha waendelee kutumia huduma hiyo ya haraka na uaminifu.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika Mlimani City jijini Dae es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula, amesema serikali itaendelea kuwa bega kwa bega, kusimamia fedha za wateja na kuhakikisha hakuna wizi au utapeli kupitia mitandaoni.

Pia amewapongeza Vodacom kwa kuwa kinara wa wateja wengi wanaofanya miamala ambapo kwa mwezi Machi tu wateja zaidi ya milioni nane walifanya miamala ya kifedha.

Nae Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao amesema sherehe hizo zitaendelea kufanyika katika mikoa tofauti nchi nzima kwa kuwa huduma M-PESA ndiyo inayoongoza nchini Tanzania ikiwa imekamata asilimia 42 ya soko, watumiaji hai zaidi ya milioni 8.2.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula ( wa sita kushoto) akiiongoza meza kuu kushuhudia magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa  yaliyotolewa wakati wa hafla ya kutimiza miaka kumi ya M-Pesa iliyofanyika jana Jijini Dsm. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema (wa tano kushoto), Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary na Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi.
 Mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 10 ya M-Pesa, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula (wa kwanza kushoto),  Mkurugenzi wa Mifumo ya malipo ya Kitaifa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Benard Dodi, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Raymond Mfungahema  na Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,  wakifuatilia moja ya burudani wakati wa sherehe ya kusherehekea mika 10 ya M-PESA iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula (kulia)   akimsikiliza Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia (katikati)  wakati wa hafla ya kusherekea miaka 10 ya M-pesa iliyofanyika  katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Ian Ferrao.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia  akimsikiliza mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mary Majula  wakati wa  hafla ya kusherekea miaka 10 ya M-pesa  iliyofanyika  katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (kulia) akisalimiana na balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thomsanga Msekelu  wakati wa Sherehe ya Kusherehekea miaka 10 ya M-pesa iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Moja ya magari mawili kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-Pesa  yakiwa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuzinduliwa  wakati wa sherehe kusherehekea miaka 10 ya M-pesa .Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara wa M-Pesa, Polycarp Ndekana  na mshereheshaji Taji Liundi.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalyn Mworia (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha M-pesa Ashutosh Tiwary  (katikati) na Mkuu wa kitengo cha Mwendelezo  wa Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya gari kati ya 10 yatakayoshindaniwa na wateja wa M-pesa  wakati wa sherehe ya kusherehekea miaka k10 ya M-pesa  iliyofanyika  katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images