Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

KESI INAYOMKABILI WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeipiga kalenda kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka  2006, Wema Sepetu na wafanyakazi wake hadi Juni 19 mwaka 2018.

Kesi hiyo ilikuja leo kwa ajili ya Wema na wenzake kuanza kujitetea Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba huku upande wa Wakili wa Serikali Costantine Kakula na Wakili wa utetezi Albert Msendo wakiwa wapo tayari kuendelea na kesi.

Hata hivyo, Hakimu Simba anayesikiliza kesi hiyo amepata udhuru kikazi na kulazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Juni  19 mwaka 2018 ambapo washtakiwa wataanza kujitetea.Kesi hiyo imefikia hatua hiyo baada ya Hakimu Simba kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

Na kutoa uamuzi ambapo aliwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu na hivyo wanapaswa kujitetea.Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.Inadaiwa kuwa Februari 4 mwaka 2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi, mwaka 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.


BREAKING NYUZZZZZZZ......: TIMU YA TAIFA YA HISPANIA IMEMFUTA KAZI KOCHA WAKE, LOPETEGUI NDANI YA MASAA 24.

0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Ikiwa imebaki siku moja kuanza kwa Michuano ya Kombe la Dunia nchini Russia, Timu ya taifa ya Hispania rasmi imetangaza kumfuta kazi Kocha wake, Julen Lopetegui kama Kocha Mkuu wa kikosi hicho.

Spain rasmi imemfuta kazi Kocha huyo ndani ya Masaa 24 kabla yakuanza Kombe la Dunia baada yakushtushwa na taarifa ya Kocha huyo kusaini Mkataba wa miaka mitatu na Real Madrid ya Hispania siku ya Jumanne.

Julen Lopetegui alitangazwa kuchukua mikoba ya Zinedine Zidane mapema wiki hii jambo ambalo lilishangaza wengi.

"Tunatakiwa kuangalia zaidi timu ya taifa inayoshiriki Kombe la Dunia", maneno ya Rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania, Luis Rubiales. "Tumefurahishwa na tulichokipata kutokana na sehemu kubwa ya mchango wake, na lazima tumshukuru na kumtakia mafanikio.

Julen Lopetegui alijiunga na Hispania kama Kocha Mkuu Julai 2016 aliongoza kikosi hicho michezo 20, akishinda michezo 14, na kutoka sare michezo sita.

Hispania itacheza na Portugal siku ya Ijumaa na pia itazikabili timu za Iran na Morocco katika Kundi B la Michuano hiyo mikubwa Duniani.

NISHATI, JICA WAJADILI MPANGO WA MATUMIZI YA GESI ASILIA MAJUMBANI

0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Kamishna wa Nishati Tanzania, Mhandisi Innocent Luoga, ameongoza Timu ya wataalam wa nishati, kupokea Rasimu ya Mpango unaolenga uainishaji wa mahitaji na matumizi ya gesi asilia katika makazi na viwanda vya ndani ya nchi.
Mhandisi Luoga alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua kupokea rasimu husika iliyowasilishwa na wataalam kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), jana, Juni 12 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
“Mpango huu umelenga kuainisha matumizi ya gesi majumbani, viwandani, usafiri pamoja na maeneo mengine mbalimbali ndani ya nchi,” alifafanua Mhandisi Luoga.
Alisema kuwa, baada ya kupokea taarifa hiyo ya awali, Serikali itaupitia na kutoa mapendekezo yake yanayolenga kuuboresha kabla ya kuanza kutekelezwa.
Akifafanua zaidi kuhusu Mpango husika; Luoga alieleza kuwa,Timu ya wataalam hao kutoka JICA, ilikwishafanya utafiti katika Mikoa Saba (7) nchini ambayo ndiyo itahusika katika utekelezaji wake. Mikoa hiyo ni Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma, Morogoro na Mbeya.
Alieleza kuwa, awali, Serikali kupitia JICA iliandaa Mpango wa kwanza wa matumizi ya gesi nchini ujulikanao kama NGUMP (Natural Gas Utilization Master Plan), ambao ulikamilika Desemba 2016.
“Mpango huo wa kwanza uliainisha matumizi ya gesi katika maeneo mbalimbali ambayo ni pamoja na uzalishaji umeme, matumizi ya majumbani, viwandani na kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.”
Alisema kuwa, baada ya kukamilika kwa Mpango huo wa kwanza, sasa JICA wanaendelea kuandaa Mpango huu mwingine kwa ajili ya kuanisha matumizi ya gesi majumbani na viwanda vya ndani ya nchi pekee.
JICA inaisaidia Tanzania kuandaa Mpango husika kama sehemu ya misaada yake inayotoa nchini.
 Kamishna wa Nishati nchini, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akipokea rasimu ya mpango wa uainishaji wa mahitaji na matumizi ya gesi katika makazi na viwanda vya ndani ya nchi, kutoka kwa mmoja wa wataalam kutoka JICA, Shinji Omoteyama, Juni 12, mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
 Kamishna wa Nishati nchini, Mhandisi Innocent Luoga (katikati), akiongoza kikao cha wataalam wa nishati (kushoto) na wataalam kutoka JICA (kulia), ambapo iliwasilishwa Rasimu ya Mpango unaolenga uainishaji wa mahitaji na matumizi ya gesi asilia katika makazi na viwanda vya ndani ya nchi. Tukio hilo lilifanyika Juni 12 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
 Kamishna wa Nishati nchini, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza-kushoto) na wataalam wa nishati, wakifuatilia uwasilishwaji wa Rasimu ya Mpango unaolenga uainishaji wa mahitaji na matumizi ya gesi asilia katika makazi na viwanda vya ndani ya nchi; uliofanywa na wataalam kutoka JICA (hawapo pichani), Juni 12 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
Mmoja wa wataalam kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Yoshikazu Kobayashi (aliyesimama), akiwasilisha Rasimu ya Mpango unaolenga uainishaji wa mahitaji na matumizi ya gesi asilia katika makazi na viwanda vya ndani ya nchi, kwa wataalam wa nishati wa Tanzania (kulia). Tukio hilo lilifanyika Juni 12 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.

Serikali Yafanikiwa kuendeleza Madawati ya Jinsia zaidi ya 500

0
0
               Na Jacquiline Mrisho 
Serikali kupitia Jeshi la Polisi imefanikiwa kuwa na madawati ya jinsia zaidi ya 500 nchi nzima yanayosaidia kutatua na kutoa ufumbuzi wa haraka kwa mashauri ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Arusha na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika pamoja na ufunguzi wa mafunzo ya Waandishi wa Habari za watoto yaliyoandaliwa na shirika la Plan International.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inalinda haki na maendeleo ya mtoto ndio maana imeanzisha Idara, Sera na Sheria zinazomlinda mtoto hivyo haki za msingi za mtoto zikiwemo za kuishi, kuendelezwa, kulindwa, kutobaguliwa pamoja na kushirikishwa lazima ziheshimiwe na kulindwa.

”Tangu Januari hadi Disemba, 2017 jumla ya matukio 41,000 ya ukatili wa kijinsia yameripotiwa na kati ya hayo 13,457 ni ukatili dhidi ya watoto, matukio hayo ya ukatili wa kijinsia ni mengi kuliko matukio ya ujambazi kwa nchi nzima hivyo Madawati ya jinsia yana umuhimu mkubwa katika kusimamia mashauri haya na ndio sababu kubwa ya Serikali kuyaongeza” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa mbali na madawati ya kijinsia, Serikali imeboresha huduma za afya kwa kuhakikisha wakina mama wanajifungulia katika vituo vya afya na watoto wanaozaliwa wanapatiwa chanjo stahiki ili kuokoa vifo vya watoto hao.
 Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akiongea na vyombo vya habari leo jijini Arusha kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2018.
 Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akimkaribisha Naibu Waziri Dk. Faustine  Ndugulile kuongea vyombo vya habari leo jijini Arusha kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2018.

MOTO MKUBWA WATEKETEZA GHALA LA KUHIFADHIA BIDHAA KARIAKOO

0
0
 Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

TAHARUKI kubwa imeibuka katika Mtaa wa Livingstone na Agrey Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya moto mkubwa kuzuka na kuteketeza ghala la kuhifadhi bidhaa mbalimbali lililopo mtaa huo.

Moto huo ambao ulisababisha moshi mkubwa kutanda angani na kuzua hofu kubwa kwa wamiliki wa maduka ulianza kuwaka mapema leo.

Hali ya kuwaka moto huo kwa kasi ulisababisha biashara katika maeneo hayo kusimama kwa muda kutokana na mkusanyiko wa watu waliokuwa wamefika kushuhudia. 
Wakizungumzia tukio la kuwaka kwa moto huo baadhi ya wananchi wamesema kuwa walishuhudia wakiona moto mkubwa ukiwaka katika ghala hilo na hofu yao kubwa ilikuwa huenda ukaunguza na maghala na maduka mengine yaliyopo karibu na ghala lililokuwa linawaka.
Wamesema moto huo uliokuwa umeambatana na moshi mkubwa angani ambapo baadhi ya waliokuwa maeneo hayo ulisababisha baadhi ya watu kukimbia maeneo hayo.
Akizungumza moto huo, mmoja ya maofisa wa Jeshi la Zima Moto amesema wamefanikiwa kuzima moto huo na cha msingi waliudhibiti kwa kuhakikisha hauendi kuunguza maeneo mengine.
Moto huo ulifanikiwa kuzimwa mchana na ndipo baadhi ya wafanyabishara walipoanza kufungua maduka yao baada ya hali kuwa shwari.

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI CHA KUPOKEA TAARIFA YA MAJUMUISHO KATI YA KAMATI YA BAJETI NA SERIKALI

0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza na Mawaziri, Wenyekiti wa kamati za kudumu za Bunge na Watendaji wakuu kutoka Serikalini (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
 Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia (wa pili kulia) akizungumza na Mawaziri, Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge na Watendaji wakuu kutoka Serikalini (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Katikati  ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye U​​lemavu, Mhe. Jenista Mhagama (kulia)
Baadhi ya Mawaziri na Wenyekiti wa kamati za kudumu za Bunge wakiwa  kwenye kikao cha kamati ya uongozi kilicholenga kupokea Taarifa ya majumuisho yaliyofanyika kati ya kamati ya Bajeti na Serikali, kilichofanyika leo tarehe 13 Juni, 2018 katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu wakamilika

0
0
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Wachezaji watatu waliobaki katika kinyang'anyiro hicho ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni wote wa Simba, ambapo kamati ya Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora imeandaa utaratibu wa kupiga kura kuwashirikisha Wahariri wa Habari za Michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom na makocha wa timu za Ligi Kuu. 

Pia kamati imekamilisha uteuzi wa wachezaji watakaowania tuzo katika kategori mbalimbali kwenye sherehe hizo za Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL itakayofanyika ukumbi wa Mlimani, City Dares Salaam Juni 23 mwaka huu.

Tuzo 16 zinatarajiwa kutolewa siku hiyo, ambapo baadhi ni za kikanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo tayari washindi wake wamefahamika, ambazo ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji bora.Ukiacha hizo tano za kikanuni, zipo tuzo 10 ambazo zimefanyiwa kazi na Kamati ya Tuzo kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo, ambapo tuzo moja nyingine ya Mchezaji Bora chini ya umri wa miaka 20 (Tuzo ya Ismail Khalfan), inayohusisha vikosi vya vijana vya timu za Ligi Kuu yenyewe inaendelea kufanyiwa kazi kwa vile mashindano yanaendelea mkoani Dodoma na itakapokamilika watatangazwa wateule watatu.

Tuzo nyingine zitakazotolewa siku hiyo ni Timu yenye Nidhamu inayowaniwa na Kagera Sugar, Simba na Mtibwa Sugar, wakati Mchezaji Bora Chipukizi inawaniwa na Shaaban Idd Chilunda, Yahya Zayd (Azam) na Habibu Kiyombo (Mbao).

Mwamuzi Msaidizi Bora inawaniwa na Helen Mduma, Mohammed Mkono na Ferdinand Chacha, wakati Mwamuzi Bora wateule ni Elly Sasii, Jonesia Rukyaa na Hans Mabena.

Tuzo ya Kipa Bora wanaowania ni Aron Kalambo (Prisons), Aishi Manula (Simba) na Razack Abalora (Azam), huku Kocha Bora wateule ni Abdallah Mohamed (Prisons), Zuberi Katwila (Mtibwa) na Pierre Lechantre (Simba).

Goli Bora ni Seif Karihe (Lipuli) na Shaaban Idd Chilunda (Azam) ambaye ameingiza mabao mawili.

Tuzo nyingine ambazo zitatolewa Juni 23 ni Mchezaji wa Heshima ambayo licha ya kuwa kamati ina majina ya wachezaji mbalimbali inaoona wanastahili tuzo kwa mwaka husika, lakini haitangazi majina hayo, isipokuwa hutaja jina la aliyepewa tuzo siku ya sherehe. 

Pia kutakuwa na kikosi bora (VPL Best Eleven), ambacho kitatangazwa siku ya sherehe.

CAF YATAJA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO

0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani Julai 18,2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba 2 Suleiman Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.

Mtathmini waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo Nomsa Jacobeth Mahlangu.

Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa July 29,2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius. 

Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Cauvelet Louis Ralph Fabian,Mwamuzi msaidizi namba 2 Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.

Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru Sarkintudu Jibril.

MICHUZI TV: MOTO WATEKETEZA GHALA LA KUHIFADHIA BIDHAA KARIAKOO JIJINI DAR

MAHAKAMA YAELEZWA 'MHASIBU TAKUKURU' ALIVYOKUWA AKIFANYA MIAMALA YA UONGO KUFICHA UMILIKI WA MALI ZAKE

0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji na kumiliki utajiri kuliko kipato chake inayomkabili, aliyekuwa Mhasibu wa Takukuru Godfrey Gugai na wenzake umeieleza Mahakama kuwa, uchunguzi umeonesha kuwa, Gugai alifanya miamala ya uongo ili kuficha umiliki wa mali zake.

Hayo yameelezwa leo mahakamani hapo wakati watuhumiwa hao wakisomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo wamekubali maelezo yao binafsi na kuyakana mashtaka yote yanayowakabili.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.Washtakiwa wamesomewa maelezo hayo leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na Wakili wa serikali Awamu Mbagwa.

Akiwasomea PH washtakiwa hao, wakili Mbagwa alidai kuwa Gugai anakabiliwa na makosa mbalimbali ikiwamo kumiliki mali isiyoelezeka, kughushi na kutakatisha fedha ambayo anadaiwa kuyatenda kati ya mwaka 2005 na mwaka 2006.Alidai kuwa Gugai aliajiriwa na Takukuru kama mchunguzi daraja la tatu mwaka 2001 na baadae 2009 aliteuliwa kuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru kazi alïyoendelea nayo hadi Agosti 2016 alipofukuzwa kazi.

Alidai washtakiwa wenzake wote ni marafiki zake wa karibu na kwamba katika kipindi chote cha ajira Gugai hakuwa na chanzo cha mapato ambacho kingeweza kumpatia kipato zaidi ya ajira yake.Alidai kwenye mishahara ya mshtakiwa na malupulupu mengine alijipatia kipato halali cha Sh.852,183,160.46 kutoka kwa mwajiri wake.

BAKWATA YATOA MAELEKEZO KUUTANGAZA MWANDAMO MWEZI WA RAMADHAN KESHO

0
0
*Watoa shukrani kwa Rais Magufuli kufuatilia ujenzi wa msikiti mkuu Bakwata


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

BARAZA Kuu la Waislam Tanzania(BAKWATA)limetoa maelekezo ya kuutangaza mwandamo wa Ramadhan huku likifafanua kuna kamati maalum inayoongozwa Mufti wa Tanzania Aboubakar Zuber ndio itakayotangaza mwandamo huo baada ya kuthibitika kuonekana.

Akizungumza leo Dar es Salaam Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata na Msemaji wa Mufti wa Tanzania Sheikh Hamis Mataka amesema kuwa mwandamo wa mwezi unatarajiwa kutangazwa kesho kwa utaratibu maalumu uliowekwa na baraza hilo.

Amefafanua kote duniani kumekuwa na utaratibu wa kuufuatilia mwandamo wa mwezi na kisha kuutangaza na hivyo utaratibu pia unafanywa na Bakwata kupitia kamati maalum ya kufuatilia mwandamo.

"Zanzibar wanacho chombo cha kufuatilia mwanandamo wa mwezi na kuutangaza, pia Kenya wanachombo cha kutangaza. Kwa Tanzania Bara kuna kamati maalum ya kufuatilia na kuutangaza mwezi na kamati hiyo inaongoza na Mufti wa Tanzania,"amesema.

Amesema kesho Alhamis ndio tarehe 29 ya Ramadhan na magharibi yake mwezi utafuatiliwa kama umeandama na kisha kuuutangaza. Amefafanua pamoja na kuwepo kwa kamati ya kufuatilia mwandamo bado umma nao unayo nafasi ya kuufuatilia na kisha watatoa taarifa kupitia utaratibu uliopo.

"Bahati nzuri Bakwata ina mtandao mkubwa kote nchini kuanzia msikiti, hivyo kinachotakiwa ni kutoa taarifa kwa imamu ya msikiti,"amesema.Ameongeza mwezi haundami chumbani bali ni hadharani, hivyo anayeuona anatoe taarifa kwa imamu wa msikiti ambaye naye baada ya kuuthibitisha atatoa taarifa makao makuu Bakwata na kisha kuutangaza rasmi.

MUFTI AMSHUKURU RAIS MAGUFULI

Wakati huo huo Sheikh Mataka amesema Mufti wa Tanzania anatoa shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kutokana na jitihada zake za kuufuatilia ujenzi wa msikiti mkubwa unaojengwa katika eneo la Bakwata.

"Jana Rais alifanya ziara ya kuja kuangalia ujenzi wa msikiti unaoendelea kujengwa .Baada ya kukagua ujenzi alitoa mchango wa Sh.milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huu unaojengwa na Mfalme wa Moroco.

"Tunafahamu hata ujenzi huu kuanza kwake umetokana na jitihada za Rais ambaye alitoa ombi kwa mfalme Mohamed wa VI ambaye alikubali kujenga msikiti huo ambao utakuwa mkubwa.Pia kutakuwa na kumbi za mikutano na vitega uchumi.Mufti wa Tanzania kwa niaba ya Bakwata na Waislamu nchini anatoa shukrani nyingi kwa Rais,"amesema.

WAKURUGENZI SITA BODI YA MIKOPO WAACHISHWA KAZI KUTOKANA NA TUHUMA MBALIMBALI DHIDI YAO

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BODI ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELB) imewachia kazi wakurugenzi sita kutokana tuhuma mbalimbali dhidi yao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi wa Bodi hiyo Abdulzaq Badru amewataja waliofukuzwa ni Juma Chagonja( Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo)na Onesmus Laizer(Mkurugenzi wa Upangaji na Ugawaji Mikopo).

Amewataja wengine ni John Elias(Mkurugenzi Msaidizi wa Ugawaji Mikopo) Robert Kibona(Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo),Heri Sago(Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu) na Chikira Jahari (Mkurugenzi Msaidizi wa Upangaji Mikopo).

Amefafanua kati ya hao waliochishwa kazi wakurugenzi ni wawili na wakurugenzi wasaidizi wanne (4). 

Amesema watumishi hao walikuwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo; uzembe uliokithiri, kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma 2002 na Kanuni zake, Sheria ya Bodi ya Mikopo Na. 9 ya mwaka 2004, Kanuni za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zinazo ongoza majukumu yao; na kusababisha hasara ya upotevu wa fedha za Serikali;

Badru amesema kuwa sheria na kanuni za utumishi wa Umma zinavyotaka, baada ya taratibu za ndani kukamilika.Amesema Februari mwaka huu bodi ya Wakurugenzi ambayo iliunda Kamati ya Uchunguzi iliyojumuisha wataalamu wa sheria, fedha na utumishi wa umma kwa lengo la kufanya uchunguzi na mahojiano na watuhumiwa hao. 

Amefafanua kamati hiyo imefanya kazi kwa kuwasilisha taarifa yake kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya uamuzi. Baada ya Uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo na utetezi uliotolewa na watumishi hao, Bodi ya Wakurungezi imejiridhisha kuwa watumishi hao walitenda makosa ya kinidhamu na hivyo kustahili adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazosimamia utumishi wa umma.

AZANIA BANK YAWAFUTURISHA WATEJA WAKE NA WATOTO YATIMA DAR

0
0
AZANIA Benki inajivunia uzalishaji wa huduma kwa kila mmoja kwa wateja wake bila kujali dini, kabila na jinsia kwa faida na hasara kwa kuandaa futari pamoja na waislamu walioungana na wateja wa benki hiyo.

Akizungumza juzi katika hafla ya futari iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki hiyo, Rhimo Nyansaho alisema wameungana na waislam katika futari hiyo ikiwa ni sehemu yao ya kushirikiana na jamii.

Nyansaho alisema benki hiyo inasonga mbele kwa sababu ya michango ya jamii katika benki hiyo ndio maana kipindi cha mfungo wakaona ni sahihi kurudisha pato hilo kwa kufuturu na jamii yenye uhitaji kama watoto yatima na wengineo.

Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuisifia benki yake kwamba wanatoa huduma bora na ndio maana faida inayoongezeka wanairudisha kwa jamii.Aliipongeza serikali kwa kuweka mazingira ya kushuka kwa riba katika benki mbalimbali ingawa wao walishashusha riba zao muda mrefu.

Mwakilishi wa wateja wa benki hiyo, Deogratius Kifumani aliipongeza benki hiyo kwa huduma zake inazotoa na kutoa wito kwa jamii kuelekeza mikakati yao ya kiuchumi huko.Kifumani alisema ubora wa huduma zao ndio maana inafanikisha matukio muhimu kama hayo katika jamii kwa kurudisha sehemu ya pato lao. 
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, akizunguma katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Azania Bank, Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Maulid Kidebe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Azania Bank kwa ajili ya wateja wake pamoja na watoto yatima.
Sheikh wa Wilaya ya Ubungo, Shjeikh Maulid Kidebe. akiwaongoza wateja wa Azania Bank wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo iliyowahusisha watoto wa kituo cha watoto yatima cha Ijango zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wateja wa Azania Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo na kuwahusisha watoto wa kituo cha yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KWA UMMA

MAMIA WAMLAKI KATIBU MKUU WA CCM ALIPOWASILI JIJINI DODOMA LEO

0
0

Mamia ya wananchi na wanachama wa CCM asubuhi ya leo wamemlaki Ndg. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipowasili kwa mara ya kwanza jijini humo kama Katibu Mkuu wa CCM na ikiwa ni kituo chake kikuu cha kazi.

Mamia ya wananchi na wana CCM walikusanyika katika uwanja wa ndege wa Dodoma na katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House).

Akizungumza na wananchi wa jiji la Dodoma waliofika kumlaki, wanachama wa CCM, viongozi wa CCM kutoka Mkoa wa Dodoma na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Bashiru amesema amepewa dhamana kubwa na wana CCM, dhamana ya kusimamia Mageuzi Makubwa ambayo yanakirejesha Chama chetu kwa wanachama na katika misingi ambayo kwayo Chama Cha Mapinduzi kiliasisiwa.

Ndg. Bashiru amegusia kwa ufupi kazi kubwa iliyo mbele ya wana CCM kwa ujumla kuwa ni kuhakikisha kazi nzuri ya kuendelea kuhuisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Mashina, Matawi na Kata inaimarishwa maradufu, na kwamba uhai wa Chama uende sambamba na vikao vya Chama kukaa ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali zetu za Chama kote nchini.

Aidha Ndg. Bashiru amezuangumzia hali ya maslahi ya watumishi wa Chama Cha Mapinduzi bado si ya kuridhisha, na akatumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa CCM kwa moyo wao wa kujitolea, utii na nidhamu ya hali ya juu licha ya changamoto walizonazo.
“… nitafanya kazi kwa bidhii kuimarisha misingi ya Chama kujitegemea na tutaboresha maslahi ya watumishi, hiki ni kipaumbele namba moja na ndio Maelekezo na msimamo wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)” amesema Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM. 
 Mapokezi ya Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM Ofisi ya Makao Makuu ya CCM 
 Ndg. Bashiru Ally Kakurwa akihutubia mamia ya wananchi walifika kumlaki katika Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma
Kutoka Kulia Ndg. Rodrick Mpogolo Naibu Katibu Mkuu (Bara), Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Mkanwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Ndg. Lubinga Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Ndg. Pereira Silima Katibu wa NEC Oganaizesheni.



MICHUZI TV: Katibu Mkuu wa CCM ataka uhai wa Chama uende sambamba na vikao vya Chama

Meet Mark Ethan Mutunji in an Interview with Leon Senyange

MOTO WATEKETEZA GHALA LA KUHIFADHIA BIDHAA KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM

Next: 2:13 Kim Jong-un takes private jet to China; getting ready for Singapore meeting with Trump? ARIRANG NEWS 133K views 7:57 Nguzo ya kwanza Daraja la Treni ya Umeme linalojengwa kuanzia Stesheni Posta hadi Ilala yasimikwa. TRC RELI TV 74K views 10:51 10 Coolest Strongest Toys Which Actually Exist ! TOP 10 INFORMATION - TTI Recommended for you 1:33 Tourism facilitated by SGR: Number of tourists to Taita Taveta increases by 40% NTV Kenya 322 views New Citizen TV Live 🔴 Kenya CitizenTV 3.4K watching LIVE NOW ALICHOWAFANYIA Waislamu Rais Magufuli Hakitasaulika kabisa Habari Mpya 167K views New MFAHAMU BEKI PASCAL WAWA ANAYETUA YANGA Global TV Online 140 views New WABUNGE CCM, UKAWA WATOFAUTIANA AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUHAMIA DODOMA MCL Digital 719 views New BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 12.06.2018 BBC News Swahili 14K views New Ahsanteni Serikali na TRC Tulidhani hatutolipwa, Mamia wapewa Fidia,Vijana waomba ajira Ujenzi SGR TRC RELI TV 3.9K views Hii ni Treni itakayo kumbukwa na Vizazi Vyetu Vyote katika Historia ya Nchi yetu. TRC RELI TV 17K views Video ya Dakika 10 ikionesha Ripoti ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kwa Mwezi April 2018 TRC RELI TV 14K views Ujenzi wa Reli ya Kisasa Umefikia hatua hii ,Tazama Full Video. TRC RELI TV 23K views Reli ya kisasa SGR Waziri wa Uchukuzi wa Uganda asema ni faida hata wa Uganda afurahishwa na kasi TRC RELI TV 7.9K views New Nguzo ya Saba Ujenzi Daraja la Treni Ilala yasimikwa, Nigeria yaipongeza Tanzania kwa Ujenzi wa SGR TRC RELI TV 17K views Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR-Shuhudia Mtambo Maalum wa Kumwaga Zege unao Tumia Computer TRC RELI TV 5.8K views Ujenzi wa Reli ya kisasa SGR utumike kama shule kwa Vijana wakiTanzania, Waziri Mbarawa aiagiza Bodi

2:13 Kim Jong-un takes private jet to China; getting ready for Singapore meeting with Trump? ARIRANG NEWS 133K views 7:57 Nguzo ya kwanza Daraja la Treni ya Umeme linalojengwa kuanzia Stesheni Posta hadi Ilala yasimikwa. TRC RELI TV 74K views 10:51 10 Coolest Strongest Toys Which Actually Exist ! TOP 10 INFORMATION - TTI Recommended for you 1:33 Tourism facilitated by SGR: Number of tourists to Taita Taveta increases by 40% NTV Kenya 322 views New Citizen TV Live 🔴 Kenya CitizenTV 3.4K watching LIVE NOW ALICHOWAFANYIA Waislamu Rais Magufuli Hakitasaulika kabisa Habari Mpya 167K views New MFAHAMU BEKI PASCAL WAWA ANAYETUA YANGA Global TV Online 140 views New WABUNGE CCM, UKAWA WATOFAUTIANA AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUHAMIA DODOMA MCL Digital 719 views New BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 12.06.2018 BBC News Swahili 14K views New Ahsanteni Serikali na TRC Tulidhani hatutolipwa, Mamia wapewa Fidia,Vijana waomba ajira Ujenzi SGR TRC RELI TV 3.9K views Hii ni Treni itakayo kumbukwa na Vizazi Vyetu Vyote katika Historia ya Nchi yetu. TRC RELI TV 17K views Video ya Dakika 10 ikionesha Ripoti ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kwa Mwezi April 2018 TRC RELI TV 14K views Ujenzi wa Reli ya Kisasa Umefikia hatua hii ,Tazama Full Video. TRC RELI TV 23K views Reli ya kisasa SGR Waziri wa Uchukuzi wa Uganda asema ni faida hata wa Uganda afurahishwa na kasi TRC RELI TV 7.9K views New Nguzo ya Saba Ujenzi Daraja la Treni Ilala yasimikwa, Nigeria yaipongeza Tanzania kwa Ujenzi wa SGR TRC RELI TV 17K views Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR-Shuhudia Mtambo Maalum wa Kumwaga Zege unao Tumia Computer TRC RELI TV 5.8K views Ujenzi wa Reli ya kisasa SGR utumike kama shule kwa Vijana wakiTanzania, Waziri Mbarawa aiagiza Bodi

VOA SWAHILI: Duniani Leo Juni 13, 2018

Previous: 2:13 Kim Jong-un takes private jet to China; getting ready for Singapore meeting with Trump? ARIRANG NEWS 133K views 7:57 Nguzo ya kwanza Daraja la Treni ya Umeme linalojengwa kuanzia Stesheni Posta hadi Ilala yasimikwa. TRC RELI TV 74K views 10:51 10 Coolest Strongest Toys Which Actually Exist ! TOP 10 INFORMATION - TTI Recommended for you 1:33 Tourism facilitated by SGR: Number of tourists to Taita Taveta increases by 40% NTV Kenya 322 views New Citizen TV Live 🔴 Kenya CitizenTV 3.4K watching LIVE NOW ALICHOWAFANYIA Waislamu Rais Magufuli Hakitasaulika kabisa Habari Mpya 167K views New MFAHAMU BEKI PASCAL WAWA ANAYETUA YANGA Global TV Online 140 views New WABUNGE CCM, UKAWA WATOFAUTIANA AZIMIO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUHAMIA DODOMA MCL Digital 719 views New BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 12.06.2018 BBC News Swahili 14K views New Ahsanteni Serikali na TRC Tulidhani hatutolipwa, Mamia wapewa Fidia,Vijana waomba ajira Ujenzi SGR TRC RELI TV 3.9K views Hii ni Treni itakayo kumbukwa na Vizazi Vyetu Vyote katika Historia ya Nchi yetu. TRC RELI TV 17K views Video ya Dakika 10 ikionesha Ripoti ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kwa Mwezi April 2018 TRC RELI TV 14K views Ujenzi wa Reli ya Kisasa Umefikia hatua hii ,Tazama Full Video. TRC RELI TV 23K views Reli ya kisasa SGR Waziri wa Uchukuzi wa Uganda asema ni faida hata wa Uganda afurahishwa na kasi TRC RELI TV 7.9K views New Nguzo ya Saba Ujenzi Daraja la Treni Ilala yasimikwa, Nigeria yaipongeza Tanzania kwa Ujenzi wa SGR TRC RELI TV 17K views Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR-Shuhudia Mtambo Maalum wa Kumwaga Zege unao Tumia Computer TRC RELI TV 5.8K views Ujenzi wa Reli ya kisasa SGR utumike kama shule kwa Vijana wakiTanzania, Waziri Mbarawa aiagiza Bodi
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images