Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

BREAKING NEWZZZZ: BASI LAGONGA TRENI KIGOMA MJINI

$
0
0
 Habari tulizozipata Globu ya Jamii  hivi punde kutoka mkoani Kigoma mapema leo asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018, inaelezwa kuwa Basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD lililokuwa likitoka Kigoma kwenda wilaya ya Nzega mkoani Tabora limegonga treni ya mizigo (Garimoshi la mizigo) katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.

Ripota wetu aliyekuwepo eneo la tukio na kushuhudia mandhari halisi ya jali hiyo,ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri, na mpaka sasa idadi ya vifo na majeruhi bado haijafahamika.

Ripota wetu yupo eneo la tukio,hivyo tutaendelea kuwaleta habari kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia.
 Baadhi ya vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa eneo la tukio la ajali
 Baadhi ya Askari wa JWTZ wakiwa tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa namna moja ama nyingine
 Baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio la ajali hiyo wakishuhudia majeruhi wakipakizwa kwenye gari  ya Wagonjwa ya JWTZ tayari kupewa huduma ya kwanza na baadae kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi
Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa

SDA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
JOSEPH MPANGALA -MTWARA
Shirika la msaada wa  maendeleao ya Michezo SDA Mkoa wa Mtwara Limefanikiwa kutoa Mafunzo pamoja na Vifaa vya michezo kwa Shule Mbili za Msingi Libobe Pamoja na Sekondari zilizopo Kijiji cha Libobe Kilichopo Wilaya na Mkoa wa Mtwara.
Mafunzo hayo yamelenga Kujenga uwezo kwa wanafunzi hasa wa kike katika maswala ya Afya Kupitia Michezo pamoja na kujua haki zao ili kuweza kujiamini katika kutoa maamuzi mbalimbali ya maisha yao.
Meneja Mradi wa Mradi wa Kuwezesha wasichana Kupaza sauti  Unaoendeshwa na SDA Thea Swai  amesema Mradi huo unaendeshwa katika kata Tisa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara manispaa kwa lengo la kuelimisha na kujengea Uwezo wa Umuhimu wa Umuhim wa Elim kwa wasichana na Jamii kwa ujumla .
“Lengo kuu la Mradi huu ni kuelimisha na Kujengea Wasichana na Jamii kuhusu Umuhim wa Elimu kwa ujumla juu ya upatikanaji Ushiriki na ufikiwaji wa elim ya msingi na sekondari hasa kwa watoto wakike ambao wamekuwa wahanga wa matatizo ya ufaulu mdogo wanapomaliza elim ya sekondari na wakati mwingine kwa idadi ndogo ya wasichana wanaomaliza shule za sekondari”
Lakini naye Afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmahauri ya Mtwara Vijijini Maisha Mlaponi amewaomba wazazi kuhakikisha wanawajengea Uwezo wa Kijamini wanafunzi ili waweze kufanya Vizuri wawapo darasani.
“Wazazi naombeni Muwasaidie watoto wenu wa Kike waweze kujiamini katika Maisha yao na wakiweza kujiamini hata darasani wataweza kufanya vizuri  kwa sababu watakuwa na uwezo wa kuuliza maswali kwa walim na hivyo wataweza kuelewa na kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho’”.

Mkurugenzi wa Shirika la SDA Adolph Kanda akimkabidhi Mwalim wa Shule ya msingi Libobe Mwanaidi Mtanda Vifaa vya Mchezo wa Mpira wa Pete kwa ajili ya kufanyia mazoezi Shuleni hapo.

Mkurugenzi wa Shirika na Msaada wa Maendeleo ya mischezo SDA Adolph Kanda akinyanyua Juu kuonesha medali walizokabidhiwa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Libobe mara baada ya Kumaliza mchezo wa mpira wa Miguu.







Kutoka Kulia ni Mratibu wa Mradi Anu Nieminen katikati Mratibu wa Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Mtwara Adelina Ndyamukama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Paralegal Mkoa wa Mtwara Mullowellah A.Mtendah wakiwa wanajadiliana jambo katika mafunzo yaliyofanyika kwa wanafunzi wa Libobe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mtwara Paralegal Mullowelh A.Mtendah akitoa mafunzo yakisheria kuhusu haki za watoto pamoja na haki za walemavu katika kuhakiksha zinasimamiwa na kutekelezwa na wanakijiji wa Libobe Mkoani Mtwara.

Meneja wa Mradi wa Kuwawezesha wasichana Kupaza sauti Thea Swai akitoa mafunzo ya kujiamini kwa wanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha waweze kupaza sauti katika Kutetea haki Zao. 

IGP SIRRO AFUNGA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MAAFISA WA POLISI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi wakati alipowasili katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu mkoani Morogoro, kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya wiki nne ya Utayari ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu Wakuu wa Polisi Wilaya (OCDs) na Maafisa Operesheni. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wa pili kushoto), akiwa ameongozana na Naibu Kamishna wa Polisi Msataafu (DCP) Vennance Tossi (katikati) Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu (DCP) Mpinga Gyumi na baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo wakati alipowasili katika Chuo hicho kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya wiki nne ya Utayari ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu Wakuu wa Polisi Wilaya (OCDs) na Maafisa Operesheni. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mmoja kati ya askari Polisi 203 wanaoshiriki mafunzo ya Utayari ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Polisi Wilaya (OCDs) na Maafisa Operesheni katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu mkoani Morogoro akiwa katika onesho la namna ya kukabiliana na uhalifu, mafunzo hayo ya wiki nne yalifungwa jana na  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DK. SHEIN AWAFUTARISHA WANANCHI WA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Futari aliyowaandalia jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni Wilaya ya Micheweni ikiwa ni katika mpangilio wake kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar,(kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa (wa pili kulia) na Mzee Haji Nasibu Nyanya (kulia).
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika  Swala ya Magharibi Iliyoswalishwa na Sheikh Ukasha Hijja Shariff (mbele) kabla ya Futari aliyoiandaa  jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akijumuika na Viongozi akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Futari aliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni.
 Baadhi ya Akinamama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni,  Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
 Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
 Baadhi ya  Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, Wilaya ya Micheweni  ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
 Sheikh Omar Hamad (kushoto) alipokuwa akitoa Shukurani kwa Niaba ya  Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba jana  katika Futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Micheweni, ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AWASISITIZA WABUNGE WADUMISHE MSHIKAMANO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasisitiza wabunge waendelee kudumisha  mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa nchi tulivu na yenye amani.

Amesema mshikamano na upendo walionao wabunge hao ni vema wakauendeleza ili waweze kutekeleza shughuli zao za kuishauri Serikali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Juni 5, 2018) katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma wakati wa futari aliyowaandalia wabunge. Futari hiyo ilihudhuriwa na wabunge wa vyama vyote.

"Mshikamano na upendo huu tuliouonesha kuanzia mwanzo wa mkutano wa Bunge naomba tuudumishe ili tuweze kuishauri vizuri Serikali na tufikie malengo tuliyojiwekea,” alisema. 

Naye,Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye alitoa neno   la shukurani kwa niaba ya wabunge wote alimshukuru Waziri Mkuu kwa heshima aliyowapa.

"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii heshima uliyotupa ni kubwa, kualikwa na wewe si jambo dogo si kila mtu anaweza kupata nafasi hii," alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mgogoni, Mheshimiwa Dkt. Suleiman Ally Yussuf ambaye alisoma dua alisema watu wanatakiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliowapa.

“Kuna wenzetu tulioshirikiana nao kwenye mfungo wa Ramadhani mwaka uliopita lakini leo hatunao sababu wametangulia mbele ya haki, hivyo sisi tunatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliotupa,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Malindi Zanzibar, Ally Abdullah Saleh, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 5, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, wakati wa futari aliyowaandalia wabunge, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018, kushoto ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, baada ya futari aliyowaandalia, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson, baada ya futari aliyoiandaa kwa wabunge, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

POLISI TANZANIA KUANDAA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.
Michezo ya pili ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018) inatarajia kutimua vumbi jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  ambapo nchi 14 tayari zimethibitisha kushiriki. 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maandalizi ya Michezo hiyo kinachofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili, Mkuu wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Leonard Paul amesema lengo la michezo hiyo kuimarisha ushirikiano na kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu kupitia michezo.
DCP Paul amesema Jeshi la Polisi Tanzania tayari limeanza maandalizi ili kuhakikisha kuwa michezo hiyo inafana na ushindi unabaki hapa nyumbani na ili kufikia lengo hilo wanamichezo hao wanatarajia kuingia kambini hivi karibuni ili wapate muda mrefu wa kujiandaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo hiyo Naibu Kamishna wa Polisi DCP Daniel Nyambabe alisema wadau mbalimbali wanakaribishwa kufadhili michezo hiyo  ambapo alizitaja nchi zinazotarajia kushiriki kuwa  ni pamoja na Burundi, Comoro, Djibout, DRC Congo, Elitrea, Ethiopia, Kenya , Uganda, Rwanda, Sudan, Sudani kusini, Somalia, Shelisheli na mwenyeji Tanzania.
Mwaka jana michezo hiyo ilifanyika Kampala Uganda na Polisi Tanzania walishika nafasi ya tatu katika ushindi wa jumla na nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwenyeji Uganda na ya pili ilikwenda Kenya.
Mkuu wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Leonard Paul akizungumza katika  mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Michezo ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018). Michezo hiyo inatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 katika Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa   mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Michezo ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018). Michezo hiyo inatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 katika Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
Washiriki wa   mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Michezo ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018) wakiwa katika picha ya pamoja. Michezo hiyo inatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 katika Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).

UBONGO TIME: SAMAKI MTU (NGUVA) KWELI NI NUSU MTU NUSU BINADAMU...???

Mafunzo ya Mfumo wa Uhasibu na uandaaji wa taarifa (Epicol 10.2) yanayoendelea mkoani Mwanza

$
0
0
Mhasibu Mwezeshaji OR TAMISEMI, Melkizedeki Kimaro, akiwasilisha mada kuhusu mchakato wa Imprest kwakutumia mfumo wa Uhasibu na utoaji wa taarifa wa (Epicol) kwenye ukumbi wa Victoria Palace Jijini Mwanza.
Mmoja ya Wawezeshaji wa mafunzo ya mfumo wa Uhasibu na utoaji wa taarifa (Epicol 10.2) kutoka OR TAMISEMI, Stanslaus Msenga, akiwa anatoa msaada wa kiufundi kwa mmoja ya wahasibu wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea kwa siku ya tatu.
Watunza Hazina na Wahasibu kutoka katika Halmashauri za Mikoa ya Mwanza na Simiyu wakiwa wanafatilia kwa ufasaha mafunzo ya Uhasibu na utoaji taari kwa njia ya kieletroniki (Epicol) wakifatilia kwa makini mafunzo hayo.
Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri ya Meatu, Laurent Mguma, akifanya nukuu muhimu za mafunzo hivi leo kuhusu mfumo wa Epicol, kama alivyokutwa na Kamera yetu kwenye ukumbi wa Viktoria Palace.
Washiriki wakiwa makini kuhakikisha mara baada ya mafunzo wanaanza kutumia vema mfumo wa Uhasibu na utoaji wa tarifa.
Washiriki wakiwa makini kuhakikisha mara baada ya mafunzo wanaanza kutumia vema mfumo wa Uhasibu na utoaji wa tarifa.

PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KAMBI YA SOGA YA UJENZI WA RELI YA MWENDOKASI ‘SGR’…ATOA MAAGIZI MAZITO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa ( kulia) akipatiwa maelezo ya maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ Juni 5, 2018, usiku eneo la kambi ya Soga ,iliyopo wilaya ya Kibaha , mkoani Pwani kutoka kwa Meneja mradi wa Kampuni ya Yapi Merkezi , Kemal Artuz.

Na John Nditi, Kibaha

WAZIRI wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa ameitaka  Kampuni ya Yapi Merkezi  ya nchini Uturuki inayojenga  reli ya kisasa (Standard Gauge)’SGR’  kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro urefu wa kilomita 300 kuongeza kasi na  kufanya kazi mchana na usiku ili ujenzi huo ukamikike kwa wakati  kulingana na makubaliano ya kimkataba.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushitukiza  Juni 5, mwaka huu ( 2018) majira ya saa tano siku kwenye  kambi ya Reli ya Mwendokasi  iliyopo Soga , wilayani  Kibaha mkoani   Pwani na kuendesha  ukaguzi hadi saa sita usiku  maeneo mbalimbali  ya  ujenzi  wa njia ya SGR.

Alisema , lengo la kufanya ziara ya kushitukiza ni  kujionea namna walivyojipata kuhakikisha kazi zinafanyika saa 24 mchana na usiku ndani ya siku saba za juma.

Profesa Mbarawa alisema , lengo ni kuona makubaliano kati ya mkandarasi na Serikali ya kukamilishwa kwa ujenzi huo ifikapo Novemba mwaka 2019 unatimizwa na wananchi kunufaika na mradi huo mkubwa.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa akijandaa kuelezea maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ Juni 5, 2018 usiku eneo la kambi ya Soga ,iliyopo wilaya ya Kibaha , mkoani Pwani .

Hata hivyo , Waziri aliwakuta wafanyakazi na wahandisi wa mradi huo wa kiwa maeneo yao ya kazi , ambapo aliwataka watanzania walipata fursa ya kusimamia kazi hiyo kuwepo eneo la mradi kipindi chote cha saa 24 na kupangiana zamu za kazi .

Alisema , hatua hiyo itawezesha shughuli ya ujenzi iendelee kwa kasi zaidi na kwa muda wote kama ilivyopangwa  ndani yamakubaliano  na kazi hiyo inafanyika  kwa viwango vya ubora na ufanisi mkubwa.

Pamoja na hayo alitumia fursa hiyo kumkata mkandarasi wa ujenzi huo kupitia Meneja mradi  , Kemal Artuz kuogeza kasi ya ujenzi ili kufikiwa makubaliano ya kukamilishwa kwa ujenzi wa reli hiyo  kwa wakati  kuwezesha watanzania kunufaika na matunda hayo.
Kwa mujibu wa Waziri  ,njia ya reli ya mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro  urefu wa kilometa 300 na  kati ya hizo, kilometa 205 ni eneo la njia ya reli na nyingine 95 ni za kupishana na mradi  huo  utagharimu kiasi cha Sh trrioni 2. 7.9.

“ Tayari wameanza kujenga tuta na sehemu nyingine wameweka kokoto kabla ya kuweka mataaluma  , kazi inaenda vizuri “ alisema Profesa Mbarawa na kuongeza .

“ Tuta linalojengwa linapaswa liwe na vipimo na viwango vilivyokubalika kwa pamoja  kimkataba ili reli hii ya kisasa inayotumia umeme itakuwa na uwezo wa  kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni ya abiria ” alisema Profesa Mbarawa.

 Waziri alisema , treni ya mizigo itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa kilometa 120 kwa saa na kubeba mizigo  tani 10,000 kwa wakati mmoja na kwa maana hiyo itaweza  kuondoa barabarani mizigo tani 20 kwa magari 500 wakati mmoja. Profesa Mbarawa alitaja kipande cha reli kingine kitakachojengwa ni kutoka  Morogoro- Makutupola chenye  urefu  kilometa 422 .

 Waziri Mbarawa alisema ,reli ya kwendo kasi itakayokuwa imejengwa kutoka Dar es Salaam hadi Makutupola itakuwa na  urefu wa  kilometa 722  na  ujenzi wake utagharimu kiasi cha  Sh trrioni 7.06.7 fedha  zinagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.
Naye Mhandisi  na Msimamizi wa mradi  wa Ujenzi wa Reli ya kisasa  , Josephat Rutaihwa alisema, kazi za ujenzi huo inaenda kwa kasi kutokana na vifaa kuwepo eneo la mradi  hadi kufikia  Juni 5, 2018 kazi zilizofanyiwa ni asilimia 13 ya ujenzi wa mradi mzima  wa kilometa  205 kutoka Dar es Salaam hadi Ngerengere.Hata hivyo alimhakikishia Waziri kuwa , kazi hiyo inakwenda kama ilivyoangwa  na kwamba mradi huo utakamilishwa  ndani ya mkataba Novemba 2, 2019.

 “ Kazi niafanyika mchana na usiku kama mlivyotukuta na mheshimiwa Waziri … na inafanyika kwa ubora na umakini na sasa tumefikia kwa baadhi ya maeneo kumwaga kokoto  na baada  kuweka mataaluma “ alisema Mhandisi Rutaihwa.

Article 16

WAZIRI MWAKYEMBE ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MSANII MCHONGAJI FOCUS SENYA

KAMPUNI YA REGUS YAFUNGUA KITUO KIPYA CHA BIASHARA DAR ES SALAAM

$
0
0
Kampuni ya kimataifa ya Regus, ambayo inajihusisha na kupangisha ofisi za kisasa za muda na za kudumu imefungua kituo kipya cha nne cha ofisi za kupangisha jijini Dar es Salaam . 

 Jengo jipya la ofisi za Regus kwa ajili ya matumizi ya kupangisha ofisi zisizo na usumbufu wa masharti liko eneo la Msasani Penisula, na linazo ukubwa wa mita za mraba 590 kwa ajili ya matumizi ya ofisi za kisasa. 

 “Tumefungua jengo la nne la kituo cha biashara lenye maeneo ya ofisi za kupangisha,hii ni fursa pekee kwa Mashirika Yasio ya Kiserikali,na makampuni ya kimataifa kujipatia sehemu za ofisi za kisasa. Eneo hili la biashara limelenga makundi yote ikiwemo wajasiriamali wanaoanza biashara kwa kuwa bei zake za pango ni za kawaida na rahisi kuzimudu” alisema Joanne Bushell,Meneja wa Regus nchini. 

 Regus imepanua huduma zake kutokana na ongezeko la mahitaji ya ofisi kwa matumizi mbalimbali na kwa gharama nafuu bila kuhangaika kununua samani za ofisi, kuingia mikataba ya kipindi cha muda mrefu na kulipia huduma mbalimbali za matumizi ya ofisi kama umeme na maji. 

 Kituo hicho cha biashara cha Regus kinazo ofisi za kupangisha, kumbi za mikutano zenye huduma mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya uhakika kupitia mtandao wa internet na simu za mezani, majiko na sehemu za kupumzikia, huduma za usafi, huduma za mapokezi na utawala. 

 Kampuni inao mpango wa kuendelea vituo vingine vya biashara katika siku za usoni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya ofisi zisizo na masharti na usumbufu,Regus inaendesha vituo vya biashara katika miji ipatayo 900 kwenye nchi zaidi ya 120 duniani,ikiwa inahudumia wajasiariamali wa kawaida, watu binafsi na makampuni makubwa ya kimataifa.

Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Ecobank katika barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza. Kushoto ni viongozi mbalimbali wa benki hiyo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella amefungua tawi jipya la Ecobank Jijini Mwanza ambapo amesema benki hiyo ina nafasi kubwa ya kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia viwanda kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Amesema mikoa ya Kanda ya Ziwa ina utajiri mkubwa wa mazao, madini pamoja na viwanda hivyo benki hiyo inapaswa kushirikiana na wananchi kuchangia maendeleo ya viwanda kupitia huduma zake.

Aidha amesema mkoa wa Mwanza una fursa nyingi za uwekezaji ukiwa ni mkoa wa pili baada ya Dar es salaam kwa kuchangia pato la taifa hivyo miaka michache ijayo Mwanza itakuwa mshindani mkubwa kiuchumi na mkoa wa Dar es salaam ambapo tayari Mamlaka ya Bandari nchini inajiandaa kujenga bandari kavu katika eneo la Fella wilayani Misungwi hatua itakayosaidia uchumi wa mkoa kukua kwa kasi.

Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee amewahimiza wananchi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kujiunga na benki hiyo ili kufurahia huduma zake ambapo ina matawi saba nchini, matano Jijini Dar es salaam na mawili Arusha na Mwanza huku ikiwa na ATM mashine zenye uwezo wa kupokea VISA, Master Card, China Union, Union Pay pamoja na Pan African Card.

Awali Ecobank tawi la Mwanza lilikuwa barabara ya Karuta na sasa limehamishiwa barabara ya Kenyatta jirani na mzunguko wa samaki Jijini Mwanza ambapo Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo nchini Peter Machunde amesema maamuzi hayo yamelenga kuboresha huduma, kuongeza ufanisi pamoja na kuwa karibu zaidi na wateja. 
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella akizungumza hii leo Mei 31, 2018 kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la Ecobank katika eneo la mzunguko wa Samaki barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza. Awali tawi hilo lilikuwa barabara ya Karuta na sasa limehamishiwa barabara ya Kenyatta ili kukidhi ili kufikisha kwa urahisi huduma bora kwa wateja.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amebainisha kwamba benki hiyo ilianzishwa mwaka 1988 katika mji wa Lome nchini Togo na hadi sasa inaongoza kwa kuwa benki kubwa barani Afrika iliyoanzishwa na Waafrika kwa ajili ya Afrika ambapo ina matawi saba nchini, matano Jijini Dar matawi mawili Arusha na Mwanza.
Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Tanzania, Peter Machunde akizungumza kwenye uzinduzi huo. 

Baadhi ya watendaji wa Ecobank wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo tawi la Mwanza.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

KUTOKA BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Juni 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe (kushoto ) na Lucy Mayenga kwenye viwanja vya Bunge jijjini Dodoma Juni 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania, Deus Seif kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Juni 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde akijibu maswali bungeni jijini Dodoma, Juni 6, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI,Joseph Kakunda , Bungeni jijini Dodoma, Juni 6, 2018.

TANI 160 ZA NISHATI YA KUNI NA MKAA ZINATUMIKA KILA SIKU KAMBI ZA WAKIMBIZI KIGOMA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma

IMEELEZWA zaidi ya tani 160 za matumizi ya nishati ya  kuni na mkaa  hutumika katika  kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kwa siku moja, kwa  matumizi ya kupikia.

Hivyo hali ina sababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo yaliyokaribu na kambi hizo.Hayo yalibainika jana wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ,  yaliyofanyika kimkoa katika Kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani humo.

Akizungumza  Mratibu wa mradi wa utunzaji wa mazingira  kambini CEMDO Tanzania Frank Kayegameni akitoa taarifa ya mradi huo amesema kutokana na  idadi kubwa ya wakimbizi  kambi ya Nyarugusu ambayo imesababisha uhitaji mkubwa wa matumizi ya mazao ya misitu.Amefafanuana  wakimbizi huenda kutafuta kuni nje ya kambi kwa kukata miti ambapo kwa siku inakadiriwa mtu mmoja anatumia kiasi cha kuni kilo moja na kambi inakadiriwa kuwa na wakimbizi 152,309 hivyo kusababisha  uharibifu mkubwa.

Amesema katika kupambana na hali hiyo Shirika la uhifadhi wa mazingira  na utunzaji wa mazingira kambini ( CEMDO) Tanzania,  kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa utaratibu wa upandaji wa miti 1,425,223  katika Vijiji 13 vinavyozunguka Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa mwaka 2017/2018 , kugawa majiko banifu kwa kaya 9600 za wakimbizi.

Pamoja na majaribio ya ugawaji wa gesi  kwa kaya 3180 lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni  yanayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na  kuboresha mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili  unaotokana na ukataji miti ovyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea  Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira
 Mmoja wa Wakimbizi akimuelezea Mkuu wa Wilaya namna wanavyo yatumia Majiko banifu kuhakikisha hawaharibu mazingira
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Ndagala  akioneshwa na Afisa wa Shirika la CEMDO majiko banifu yanayotumia kuni chache kwa lengo la kutokomeza uharibifu wa mazingira.


WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI

$
0
0
*Kamanda wa Polisi Kigoma aelezea hatua kwa hatua namna ilivyotokea

 Na Ripota Wetu, Kigoma

WATU 10 wamefariki dunia na wengine 26 wamejeruhiwa baada  ya basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Tabora kuligonga treni. 

Akizungumzia ajali hiyo leo Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kigoma Martine Otieno amesema  imetokea eneo la kivuko Bungo Relini mkoani humo.Amefafanua dereva wa  basi licha ya kupigiwa honi na  treni hakusimama eneo la kivuko na hivyo akagongwa. 

Ameongeza baada ya kutokea ajali hiyo  abiri 10 wamepoteza maisha wakiwamo saba waliofariki eneo la tukio na wengine watatu walifariki dunia wakiwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu. 

Kamanda Otieno amesema ndani ya basi kulikuwa na jumla ya abiria 18 pamoja na dereva na utingo wake na kufanya jumla ya idadi waliokuwamo kufikia 20.Ameeleza kiss kati ya  hao waliofariki dunia wanaume ni saba na wanawake watatu. 

Pia amesema baada ya basi holiday kugonga treni liliburuzwa umbali wa mitambo 100 na hivyo kusababisha majeruhi wengine 17 waliokuwamo pembezoni mwa reli. "Katika ajali  hiyo waliokuwamo ndani ya basi ni watu 20,waliopoteza maisha ni 10,maheruhi tisa na mmoja amenusurika na majeruhi wengine 17 hawa waliokuwamo pembezoni mwa reli.

"Hivyo idadi ya  majeruhi wote ni 26 na chanzo cha ajali  ni uzembe wa dereva wa  basi ambaye aliamini atawahi kuvuka kivuko cha reli na matokeo yake amesababisha kutokea kwa ajali hiyo, "amesema Kamanda Otieno.
 Baadhi ya majeruhi wa ajali wakiendelea na matibabu katika hospitali  ya mkoa wa kigoma.

Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution, AnnMary Mugo akinena jambo.

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kuzikatia bima nyumba zao ili wanufaike na fidia pindi nyumba hizo zikipatwa na majanga ya aina mbalimbali kama vile kuungua, kuharibiwa na mafuriko au majanga yoyote yale.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution, Maryanne Mugo wakati akizungumzia bima ya nyumba itolewayo na kampuni hiyo.

Alisema, jamii inatakiwa kuwa na mwamko katika kujiunga na bima hiyo ambapo malipo yake sio makubwa ikilinganishwa hasara inayoweza kutokea pindi nyumba ikikutwa na majanga mbalimbali.

Alisema,“ jamii inapaswa kutambua kuwa kuna amani na faida kubwa iwapo wakizikatia bima nyumba zao na hiyo inajidhihirisha pindi pale ambapo nyumba zikipatwa majanga iwe kuungua moto, kuvunjwa, kuharibiwa na mafuriko au majanga yoyote yale huwa bima inalipa”

Akizungumzia kuhusiana na mwamko wa watu kutumia huduma ya bima ya kampuni hiyo, alisema mpaka sasa wanao wateja 210 ambapo kati yao ni wawili tu ndo wamepatwa na majanga, mmoja ameshalipwa na mwingine anakaribia kulipwa.

Aliongeza, kuwa kuna dhana kati ya watu mbalimbali wakifikiria kuwa inachukua muda mrefu sana tangia nyumba ikipatwa majanga na kulipwa fidia ambapo alisema kwa kampuni hiyo huchukua muda mchache tu iwapo taratibu za malipo zikishakamilishwa.

Alisema, mteja hulipwa iwapo tu atakamilisha nakala muhimu kama vile ripoti ya Polisi, Makadirio ya vitu vilivyopotea au kuharibiwa ambavyo vinatokana na ripoti ya mpimaji au mkadiriaji wa bima.

“Hivi ni vitu muhimu na vya haraka vinavyotakiwa kuwakilishwa na mteja pindi nyumba yake itakapopatwa na majanga ya aina yoyote ile na kampuni za bima zinashughulikia kwa wakati”alisema.

MADIWANI NA WAKUU WA IDARA NA VITENGO KATIKA HALMASHAURI ZOTE ZA DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA MAADILI

$
0
0
Afisa Uchunguzi Mwandamizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda Dodoma, Bibi Jasmin Awadh akiwasilisha Mada ya Mgongano wa Maslahi kwa Waheshimiwa Madiwani naWakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri za Jiji la Dodoma wakati wa Mafunzo ya Maadili kwa Viongozi wa Umma wanawake yalifanyika ukumbi wa VETA Dodoma juni 5, 2018.
Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri za Jiji la Dodoma wakifuatilia kwa makini Mada ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyokuwa ikitolewa na mkufunzi wakati wa Mafunzo ya Maadili kwa Viongozi wa Umma wanawake yalifanyika ukumbi wa VETA Dodoma juni 5, 2018.
Wanahabari kutoa TBC1, Star TV, Redio A FM na Global TV wakifanya mahojiano na Mhe. Asia Halamgha ambaye ni diwani Viti Maalum Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika mafunzo ya Maadili kwa Viongozi wa Umma wanawake yalifanyika ukumbi wa VETA Dodoma juni 5, 2018.

TFS YAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUTUMIA NISHATI MBADALA ILI KULINDA MAZINGIRA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)umesema ipo haja kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia nishati mbadala na hasa mkaa mbadala kwa lengo la kulinda mazingira na hasa misitu iliyopo nchini huku akielezea namna ambavyo kasi ya ubaribifu mazingira ikiendelea kuongezeka.

Hayo yamesemwa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Dos Santos Silayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo kwa Tanzania kitaifa yamefanyika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi Blog, Profesa Silayo amesema takwimu zinaonesha bado kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na hivyo kuiomba jamii kutumia nishati mbadala ili kulinda mazingira na kubwa zaidi ameshauri kutumia mkaa mbadala kwa ajili ya kupikia.

Akizungumzia Siku ya mazingira duniani ambayo yameambatana na maonesho ya nishati mbadala, Profesa Silayo amesema Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wameshiriki kwasababu msitu inabeba dhamana kubwa katika mazingira na unapozungumza mazingira basi yanaonekana maeneo ya misitu na ekolojia yote.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos akiteta jambo jana akiwa katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyofanyika kitaifa Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos akiangalia mkaa mbadala ambayo unatengenezwa kwa mabao ambao haujatokana na miti asili baada ya kutembelea banda la Accaso International Ltd jijini Dar as Salaam Jana. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)


Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 10 ajali ya basi na treni Kigoma

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>