Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Wizara ya Ulinzi ya Tanzania yasaini Mkataba wa Makubaliano na Serikali ya Israel

$
0
0
Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali, Nicodemus Elias Mwangela pamoja na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye masuala ya Ulinzi katika Wizara ya Ulinzi ya Israel, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Ben-Baruch wakiwekeana saini katika Mkataba wa Makubaliano ya pamoja ya Ulinzi kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania na Wizara ya Ulinzi ya Taifa la Israel, tukio hilo limehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania, Mhe. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dkt. Florens Turuka, Balozi wa Israel nchini Kenya awakilisha pia Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Salehe pamoja na viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania.Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao Makuu ya Jeshi 
Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (kulia) pamoja na Brigedia Jenarali Mstaafu Michael Ben-Baruch wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kuwekeana saini. 
Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela akimkabidhi Brigedia Jenerali Michael Ben- Baruch zawadi ya Nembo ya Jeshi la Kujenga Taifa la JWTZ 
Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela (wa sita kulia) pamoja na Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Ben- Baruch (wa saba kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Israel pamoja na Balozi wa Israel nchini Kenya ambaye anawakilisha Tanzania. 

KAMPUNI YA ORYX GAS YAJIVUNIA KUWA RAFIKI WA MAZINGIRA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

KAMPUNI ya mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX nchini ijulikanayo kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao umeonekana kuwa wa gharama sana.

Akizungumza katika kuadhimisha Wiki ya mazingira leo viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kampuni ya gesi ya ORYX Jeffrey Nasser amesema kuwa ORYX GAS amekuwa rafiki mkubwa wa mazingira pale walipoamua kuletea nishati mbadala ya ges.

"Na haikuishia hapo tu bali tuliwawezesha wananchi wengi sana nchi nzima kuipata kwa gharama ndogo na hata yale maeneo ya wananchi wa hali ya chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini tumeokoa miti mingi ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia,"amesema.

Amefafanua kwa ORYX GAS kwa nyakati tofauti wamekuwa wadau muhimu katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutunza mazingira, na kwa muda mrefu wamekuwa na kampeni yao ya ORYX GAS "Rafiki wa Mazingira". 
 Mkuu wa Kitengo cha Mauzo  ORYX GAS,Jeffrey Nasser akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu yakuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu  ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akimzikiliza 
Menejacha wa Maendeleo ya Biashara Oryx Gas,Mohamed Mohamed ambabo akifafanua juu  ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu  ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira,leo jijini Dar as Salaam katika kilele cha maadhimosho ya wiki ya mazingira Duniani.

MAHAKAMA YAELEZWA JALADA HALISI KESI VIGOGO WA UTHAMINI MADINI NA ALMASI WA SERIKALI LIPO KWA DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada halisi la kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa Serikali lipo kwa Mkurugenzi wa mashtaka ( DPP).

Wakili wa Serikali Esterzia Wilson ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja mahakamani hapo kwa kutajwa.Amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na jalada halisi lipo kwa DPP, hivyo akaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.

Wote wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh.bilioni 2.4. Kalugendo na Rweyemamu wanasota rumande kutokana na DPP kuzuia dhamana zao.Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na ashtaka la kuisababishia serikali hasara ya Sh. 2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, mwaka 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo ni sawa na Sh.2,486,397,9.

YANGA , SIMBA VUTA NIKUVUTE CECAFA

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya Jamii

WATANI wajadi Yanga Sc na SimbaSc wamepangwa kundi moja katika michuano ya Kombe la Kangame (CECAFA).

Simba na Yanga wamepangwa kundi C la michuano hiyo inayojumuisha timu 12 za Afrika Mashariki na Kati ambayo itaanza kutimua vumbi Juni 28 mpaka Julai 13 mwaka huu ambapo Tanzania watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.Mashindano hayo yataonyeshwa kupitia Azam TV.

Michuano hiyo itachezwa nchini Tanzania kwa mitanange yake kupigwa kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa (Tanzania Main Studium) na Uwanja wa Azam Chamazi Complex.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam Rais wa shirikisho la mpira wa MiguuTanzania (TFF), Wallece Karia ametoa shukura kwa CECAFA pamoja na Azam kuleta tena mashindano hayo hapa nchini.

Karia amesema kuwa hiyo ni mara ya pili mfululizo kuwa wenyeji wa michuno hiyo ambapo ilifanyika kwa mara ya mwaka 2015 na matajiri wa Chamaz Azam Fc ndio walikuwa mabingwa wa kikombe hicho.

"Sisi tumepata tena fursa hii ya kuwa ndio wenyeji wa michuano hii iwe chachu kwa nchi zingine kuendeleza kufanyika kila mwaka bila kusimama"amesema Karia.

Katibu Mkuu Kagame Cup (CECAFA) Nicholas Musonye ameweka wazi timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwa makundi ambapo mshida wa kwanza atajinyakulia kitita cha Dola za Marekani 30, 000, wa pili dola 20, 000 na wa tatu kupata dola 10,000.

"Kundi A ni Azam (Tanzania), Uganda Reps (Uganda),JKU (Zanzibar), KatorFC (Sudani Kusini ), ambapo kundi B ni Rayon (Rwanda),Gor Mahia (Kenya),Lydia Ludic (Burundi),ports (Djibouti) Huku kundi C ni Yanga (Tanzania),Simba (Tanzania),St.George (Ethiopia) na Dakadaha (Somalia)" amesema Musonye.

STAMICO KUJA NA NISHATI YA MAKAA YA MAWE KWA MATUMIZI YA MAJUMBANI,VIWANDANI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limesema makaa ya mawe yakianza kutumika kama nishati ya kupikia kutapunguza matumizi ya mkaa kwa asilimia 15.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Madini na huduma za Kiuhandisi, Zena Kongoi wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Dunia yaliyohitimishwa, leo Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam amesema Stamico katika miradi mbalimbali wameweka kipaumbele cha utuzaji wa mazingira katika kulinda vizazi vya leo na vijavyo.

Amesema kuwa katika ripoti ya Trido inaonyesha hekta 300,000 za miti zinakatwa kwa ajili mkaa hivyo matumizi ya makaa ya mawe kutumika nishati ya kupikia itapunguza ukataji wa miti hiyo.Kongoi amesema makaa ya mawe kuna taasisi ambazo zitakuwa za kwanza kufikiwa na nishati ya makaa ya mawe ni Magereza , Kambi za Wakimbizi pamoja na vyuo vikuu.

Amesema kuwa nishati hiyo watauza kati ya Sh.350 hadi 500 ambapo kila mtu anaweza kumudu na kuachana na matumizi ya mkaa kutokana na gharama iliyopo katika mkaa.Amesema majaribio ya makaa ya mawe yana gesi hivyo kazi kwa ushirikiano kati ya Stamico na Trido katika kutoa gesi hiyo na kemikali zingine zilizo katika makaa ya mawe.

Kongoi amesema stamico iko bega kwa bega na wadau mbalimbali katika shughuli za madini katika kuangalia masuala ya mazingira ikiwemo kufanya tathimini ya uhalibifu wa mazingira katika miradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Madini na huduma za Kiuhandisi, Zena Kongoi akizungumza na waandishi habari katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria wa Baraza la Mazingira (NEMC), Heche Suguta akiwapa vipeperushi pamoja na kuwapa maelezo wananchi waliotembelea maonesho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja

HILI NDILO SANDUKU LITAKALOBEBA MIILI YA MAREHEMU MARIA NA CONSOLATA

$
0
0
Hili ndilo sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata likiwa tayari limekamilika kwa maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa

Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.

Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista waliokwishafariki.Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.
Baadhi ya Mafundi wakitengeneza  sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata,kwa maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa.

Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.

Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista waliokwishafariki.Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.
Sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata likiwa tayari kwa maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa
Baadhi ya Mafundi wakiendelea na maandalizi ya kutengeneza Sanduku litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata,kwa ajili ya maziko hapo kesho katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa

UGANDA YADHAMIRIA KUPITISHA SHEHENA ZA MIZIGO KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege amesema, nchi hiyo imedhamiria kupitisha shehena nyingi za mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya vivutio vingi vilivyopo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam Mhandisi Mtege amesema bandari hiyo ni njia rahisi kwao ya kupitisha mizigo yao na pia usafiri wa kutumia njia ya maji ni wa bei nafuu.Alisema vivutio vilivyopo katika bandari ya Dar es Salaam hawaoni sababu itakayo wakwamisha kupitisha mizigo yao na kuendeleza uchumi wa nchi yao.

" Kufika Bandari ya Dar es Salaam ni mara yangu ya kwanza lakini nimeshuhudia mambo mengi ikiwamo maboresho ya miundombinu hivyo napongeza Serikali ya Tanzania ambazo zimechukuliwa hasa za kufungua njia ya ukanda wa kati jambo lililorahisisha kufika kwa mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Uganda," alisema Monica.

Amesema tayari wamejiandaa kuhakikisha wanasafirisha shehena kwa wingi kutoka Uganda kuja Dar es Salaam.Amesema tayari wameandaa makampuni makubwa yenye nia ya kuja Dar es Salaam kupitia njia ya ukanda wa kati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Lydia Malya amesema, tayari bandari wameanzisha kikosi kazi maalum ili kuhakikisha wanapata mizigo mingi zaidi ya Uganda.Amesema watatumia fursa mbalimbali kutangaza njia hiyo kwa faida ya nchi mbili.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege akizungumza katika mkutano wa menejimenti ya TPA wakati alipotembelea bandari hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akitoa maelezo wakati  Waziri wa Uganda alipotembelea banadari ya Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Banadari , Mhandisi Karim Mataka akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa ujenzi na Uchukuzi wa Uganda alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignatus Rubaratuka akizungumza kuhusiana na mamlaka hiyo kuhakikisha inatoa huduma bora kutokana na ushirikiano kati ya Uganda na Tanzania

MISS UBUNGO MWAKA 2014 DIANA KATO ASHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA KWA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA AMANA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii.

ALIYEKUWA Miss Ubungo jijini Dar es Salaam mwaka 2014-2016 Diana Joachim Kato ameshiriki kuadhimisha wiki ya mazingira kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini.

Miss huyo ambaye ana mradi wake wa maji safi na salama amefanya usafi huo kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Ilala jijini Saady Khimji.Hivyo ameamua kushiriki siku ya mazingira duniani kwa kuamua kuitumia siku ya leo kufanya usafi hospitalini hapo ikiwa pamoja na kupanda miti.

Akizungumza baada ya kufanya usafi huo Diana Kato amesema ameamua kushiriki siku ya mazingira duniani kwa kufanya usafi katika hospitali hiyo pamoja na kupanda miti huku akiweke akitoa mwito kwa Watanzania kuendelea kutunza mazingira.

"Nimeona ni vema leo nikawa katika hospitali ya Rufaa ya Amana kwa ajili ya kufanya usafiti na baada ya hapo nikashiriki kupanda miti .Hii yote ni katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani .Kubwa zaidi nitoe rai kwa Watanzania tuwe sehemu ya kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha tunatunza mazingira yetu ili nayo yatutunze.
Aliyekuwa Miss Ubungo 2014/16,  Diana Joachim Kato akipanda mti katika  Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa  maadimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo
Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji  akipanda mti katika  Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa  maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika leo.
Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji(wa pili kushoto) na Aliyekuwa Miss Ubungo 2014/16,  Diana Joachim Kato(kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja walipofika katika Hospitali ya Rufaa ya Amana  kwa ajili ya kupanda miti pamoja na kufanya usafi wa mazingira yanaoizunguka hospitali hiyo leo.


KOCHA MSAIDIZI SIMBA SC AKANUSHA KUJIUZULU

MICHUZI TV: TEKNOLOJIA YA NISHATI MBADALA IMEBADILIKA - PROF DOS SANTOS SILAYO

MICHUZI TV: NCHI ZA NORDIC ZALIDHISHWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI KWENYE MAPAMBANO YA RUSHWA

Michuzi TV: Vibweka vya JOTI kulekea mchezo wa Juni 9 kati ya Team Samatta vs Team Kiba

Michuzi TV: WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AFANYA ZIARA BOHARI KUU YA JESHI LA POLISI

AZAM TV 2: TAARIFA YA HABARI JUNI 5, 2019

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 05.06.2018


MAJAMBAZI NANE NA WAHAMIAJI HARAMU SABA WAKAMATWA MKOA WA PWANI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
 JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu nane wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji wa gari. 
 Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu saba kutoka nchi ya Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Tukio hilo lilitokea Juni 4 mwaka huu, katika eneo la Vigwaza ambapo watu wawili waliojifanya wasamaria wema walisimamisha gari hiyo yenye namba za usajili T 311 DHS aina ya Fuso lililokuwa likiendeshwa na Abeid Victor likitokea Dar es Salam kwenda Iringa. 
 Kamanda wa Polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna alithibitisha kutokea kwa tukio hilo . Alieleza watu hao wawili walimsimamisha dereva huyo wakihitaji msaada lakini baadae walimgeuka na kumpora gari hilo. 
 Shanna alisema, gari hilo lilikua limebeba unga wa ngano kilo 205, baada ya tukio hilo Jeshi hilo kwa kushirikiana na polisi wa mkoa wa Morogoro waliendesha msako ambao ulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kwenye mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Dar es Salam. "Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na mzigo huo wa unga na vifaa mbalimbali vya gari hilo waliloliteka" 
 "Baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika katika tukio hilo na kisha kuonyesha walipohifadhi mzigo huo na vifaa vya gari vilivyokua vimekatwa ambavyo ni kichwa cha gari, kadi ya gari, namba za usajili wa gari, giabox na engine" alisema. 
 Shanna aliwataja watuhumiwa hao ni pamoja na Juma Chilala, Edgar Musa, Abdallah Mohamed, Ashama Bakari, Said Selemani, Kassim Nassoro na Masumbuko Selemani . Alisema anatarajia kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa. 
 Katika tukio lingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu . Wahamiaji hao walikamatwa katika msako unaoendeshwa na Jeshi hilo katika eneo la wilaya ya Kipolisi ya Chalinze ambapo raia hao wa Ethiopia walikutwa kwenye nyumba ambayo haijakamilika huko Pingo. 
 Shanna aliwataja wahamiaji hao kutoka Ethiopia kuwa ni Malakwi Abala(20),Elias Tadela(40), Mohamed Awole(31), Degafa Hanadamo(22)Sadebo Cakebo(38),Abraham Lamango(35) na Mahalu Tahifae wote watakabidhiwa kwa idara ya Uhamiaji kwa taratibu za kisheria. 
 Aliwaonya wahamiaji ambao wanaingia nchini bila kibali na yeyote atakayekamatwa Sheria itachukua mkondo wake.
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu tukio la ujambazi /utekaji gari pamoja na kukamatwa kwa wahamiaji haramu .

BUNGE LAIDHINISHA BAJETI YA TRILIONI 12.058 KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA 2018/19

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akionesha kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa wa Taifa wa Miaka Mitano, wakati wa kuhitimisha hoja za Wabunge kuhusu bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango Bungeni, Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu hoja za Wabunge kuhusu Uhimilivu wa Deni la Taifa ambapo alieleza kuwa bado Deni hilo ni himilivu kwa vigezo vya kimataifa.
 Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya Bajeti ya Wizara hiyo, ya shilingi trilioni 12.058, kuidhinishwa na  Bunge, Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), viongozi wengine wa Wizara hiyo na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakishangilia baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kuidhinishwa na Bunge.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (tai ya rangi ya Bendera ya Taifa), viongozi wengine wa Wizara hiyo na Maafisa Waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Bunge kuridhia na kuidhinisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19.
 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
-Wizara ya Fedha na Mipango-Dodoma)

DC SHINYANGA AIBUKIA STENDI YA MABASI MAADHIMISHO SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro ametembelea maeneo ya Stendi ya Mjini Shinyanga kukagua mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka. 
g 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza na wafanyabiashara na wasafiri katika Stendi ya Shinyanga Mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro katika Stendi ya Shinyanga Mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akiwa katika Stendi ya mabasi ya Shinyanga Mjini akielekea katika choo kilichopo katika stendi hiyo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA


NAIBU WAZIRI WA ARDHI ANGELINA MABULA AANZA ZIARA MKOA WA LINDI NA KUHIMIZA ULIPAJI KODI YA ARDHI, ASULUHISHA MGOGORO BAINA YA WANANCHI WA KIJIJI CHA KICHONDA LIWALE MKOA WA LINDI NA MUWEKEZAJI

$
0
0
Na Munir Shemweta, Liwale 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesuluhisha mgogoro ulipo katika kijiji cha Kichonda kilichopo wilayani Liwale mkoa wa Lindi baina na wakazi wa kijiji hicho kuhusu uhawishaji wa ardhi ya kijiji ekari 1000 kwenda kwa muwekezaji M/S KSM & AGL EXPORT FARM C LTD. 
Wananchi wa kijiji cha Kichonda wamekataa uhawishaji wa ardhi ya kijiji hicho kwenda kwa muwekezaji kwa madai kuwa muwekezaji huyo ameshindwa kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa kwa wakazi hao kabla ya kumilikishwa rasmi eneo hilo. 
Kwa mujibu wa wakazi wa kijiji hicho, muwekezaji huyo aliwaahidi wakazi hao kuwajengea msikiti, kuwachimbia kisima cha maji, kusaidia magodoro katika zahanati ya kijiji lakini wamedai kuwa kutotekelezwa kwa ahadi zote hizo kumewafanya kukosa imani naye na kueleza kuwa hastahili kumulikishwa eneo hilo. 
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walieza kuwa, muwekezaji huyo kwa sasa hapaswi kulaumiwa kwa kuwa eneo lenyewe hajapewa jambo linalomuwia vigumu kwake kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi alizotoa hivyo walitaka akubaliwe kumilikishwa ndipo waanze kumlaumu.
 Naibu Waziri Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Lindi kuhusiana na masuala ya Ardhi alipowasili mkoani humo jana kwa ziara ya siku mbili.
e
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa halamshauri ya Manispaa ya Lindi, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemaga na kushoto ni mbunge wa Viti Maalum Hamida Abdallah (Picha na Munir Shemweta- WANMM).
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kichonda wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi  wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji hicho kwa muwekezaji.
.
 Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kichonda akichangia maoni wakati naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi alipotembelea kijiji hicho kuhakiki zoezi la uhaishwaji ekari 1000 kwa muwekezaji.
.

 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kichonda wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (hayupo pichani) wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji.



MWENYEKITI WA TAWA AKAGUA UHIFADHI SERENGETI, AWATAKA WALINZI WA WANYAMAPORI WATAKIWA KUWA MAKINI NA WAADILIFU

$
0
0
WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA) Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.
Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo.
"La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike," alisema.
Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society  ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika  eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game    Tracker Safaris  (TGTS).
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA), Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko (wa pili kushoto mwenye miwani), akizungumza na walinzi wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa mkoani Simiyu alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo. 
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images