Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

Dk. Shein kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliawa na NBC

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza Benki ya taifa ya biashara NBC kwa kasi  na juhudi za kukuza  Uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza mkuu wa mkoa wa  mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud kwa niaba ya Rais  katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort,amesema kuwa pato la Taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka  kutoka na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali ikiwemo benki hiyo ya NBC.

Dkt Shein ameipongeza  benki hiyo kwa kuonyesha umuhimu kwa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo ya kufutirisha na kutoa huduma nyingine mbali mbali kwa jamii.

Aidha akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NBC  Dk Kassim Hussein amesema kuw kwa huduma za kifedha kisiwani Zanzibar ni kutokana na juhudi  bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake.

Dk Hussein amesema kuwa mazingira salam yaliopp Zanzibar yanayoimarishwa na viongozi wakuu wa nchi imewezesha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma za kifedha kwa ufanisi zaidi.

Vile vile amesema kuwa benki hiyo imeanzisha huduma  za kibenki  kiislam ambayo inatoa huduma za mikopo kwa misingi ya sheria ya kiislamu.

Katika hafla hiyo  ya futafi iliyoongozwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein,Mawaziri,Jaji Mkuu,Mufti mkuu wa Zanzibar  viongizi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wateja wa benki ya NBC.
 Kaimu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki ya NBC Dk.Kasim Hussein wakati wa kufutu katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki akizungumza  kuwa benki hiyo imeshaanzisha huduma ya kibenki ya kiislamu ambayo itatoa huduma  za mikopo kwa misingi ya sheria ya Kiislamu.
Raiz wa Zanzibar na Maenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein akichukua chakula  wakati wa kufuturu futari iliyoandaliwa na na Benki ya NBC,mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

WALINZI WA HIFADHI WATAKIWA KUWA MAKINI NA WADILIFU KUTOKANA NA WANYAMA KUTOKA NJE YA HIFADHI

$
0
0
WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA).Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.

Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo."La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike," alisema.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game Tracker Safaris (TGTS).

Wataalam hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya Friedkin inayomiliki TGTS ililiyofadhili fedha, vifaa pamoja na helikopta, kazi ijayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine.Katika ziara hiyo TAWA imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA) Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko, Akikagua Gwaride la Askari wa Wanyamapori wa pori la akiba Maswa.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA),Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko akiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa Wizara ya Maliasili washirika wake.

KANDEGE APONGEZA USIMAMIZI WA UJENZI WA VITUO VYA AFYA ARUSHA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege amepongeza usimamizi mzuri uliofanyika katika ukarabati na ujenziwa vituo vya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Jijini Arusha.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara hivi karibuni ya kukagua maendeleoya ujenzi wa vituo vya afya vya Nduruma kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Jijila Arusha na Kituo cha afya cha Usa River Kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Meru, Jijini Arusha.

Mhe. Kandege amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya Jijini Arusha, na kuwapongeza kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo ni imara na yanaendana na dhamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.

“Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya katika Jiji la Arusha ipo vizuri na kazi inayofanyika inaridhisha ukilinganishwa na fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini.

Mhe. Kandege ametoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili huduma za afya ziweze kutolewa kwa wananchi.Amezitaka Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri ya vituo vya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuweka uzio, kupanda miti hasa ya matunda ili kutengeneza mandhari inayovutia kwa wagonjwa pindi wanapohitaji kuaptiwa huduma ya afya.

Akiongelea kuhusu vyumba vya kujifungulia wanawake wajawazito Mhe Kandege ameelekeza chumba cha kujifungulia kitenganishwe kila kitanda ili kuwa na usiri wamama mjamzito anapojifungua.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akikagua jengo akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha .
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege akipatiwa maelezo wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Jiji la Arusha
Moja ya jengo lililojengwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Jiji la Arusha.

Umeme wa Gridi kuokoa bilioni 30 kwa mwaka Njombe, Ruvuma

$
0
0
Na Greyson Mwase, Ruvuma

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa umeme utakaopelekea mikoa ya Njombe na Ruvuma kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa Septemba, 20 mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litaweza kuokoa shilingi bilioni 30 zilizokuwa zikitumika kama gharama ya kuendesha mitambo ya kuzalishia umeme inayotumia mafuta mazito katika mikoa hiyo.

Waziri Kalemani aliyasema hayo mapema jana tarehe 04 Juni, 2018 kwa nyakati tofauti kupitia mikutano na vijiji vya Suluti kilichopo wilayani Namtumbo na Lukumbule na Mkowela vilivyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwenye ziara yake ya kukagua njia ya Makambako – Songea, vijiji vinavyotakiwa kuunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa pamoja na miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Katika ziara hiyo Waziri Kalemani aliambatana na wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakandarasi pamoja na wakuu wa wilaya husika.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, shirika la Tanesco limekuwa likitumia gharama kubwa ya shilingi bilioni 30 kwa mwaka kama  gharama ya uendeshaji wa mitambo inayotumia mafuta mazito katika mikoa ya Njombe na Ruvuma na kusababisha hasara badala ya faida.

Alisema kuwa, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea mapema mwezi Septemba mikoa ya Njombe na Ruvuma itaunganishwa rasmi na Gridi ya Taifa na kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 30 kinachotumika kuendesha mitambo ya mafuta mazito gharama ambazo ni kubwa tofauti na mapato ya shirika hilo ya shilingi bilioni tisa kwa mwaka kwa mikoa husika.

Aidha, aliongeza kuwa kuingizwa katika Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Njombe na Ruvuma kutapelekea uwepo wa nishati ya uhakika na kuchochea ukuaji wa uchumi.
 Kazi ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Songea kilichopo mkoani Ruvuma ikiendelea.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake katika kituo cha kupoza umeme cha Songea kilichopo mkoani Ruvuma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema na kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Makambako – Songea, Mhandisi Didas Lyamuya.
 Sehemu ya wananchi wa kijiji cha  Suluti kilichopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokuwa akiwaelezea mikakati ya serikali katika upelekaji wa huduma ya umeme vijijini.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akielezea matumizi ya kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa kijiji cha  Suluti kilichopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma (hawapo pichani)

WATAALAMU WA MADINI NCHINI WAJIFUNZA UZOEFU KUTOKA AUSTRALIA

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma

Wataalam mbalimbali kutoka sekta ya madini nchini wameshiriki warsha maalum iliyotolewa na wataalamu kutoka Australia, kwa lengo la kujifunza uzoefu kutoka nchi hiyo ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta husika. Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alifungua rasmi warsha hiyo ya siku mbili, Juni 4 jijini Dodoma na kusema kuwa Tanzania inahitaji kujifunza zaidi kutoka nchi zilizofanikiwa katika sekta ya madini kama Australia, ili iweze kukuza zaidi mchango wake katika katika Pato la Taifa.

“Wenzetu Australia, sekta yao ya madini ina mchango mkubwa sana; zaidi ya asilimia 40 kwenye Pato lao la Taifa. Kwa hiyo, tunakutana nao kubadilishana uzoefu, ni namna gani wao wamefanya kuwezesha sekta husika kuchangia kwa kiasi hicho kwenye Pato la Taifa.”

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa, suala muhimu ambalo Wizara ya Madini inalisimamia ni kuhusu usimamizi wa rasilimali za madini. Alisema kuwa, lengo jingine la warsha hiyo ni kujifunza Australia imefanya nini katika kusimamia na kutatua migogoro kwenye sekta ya madini, ili Tanzania itumie mbinu hizo kutatua migogoro iliyopo kwenye sekta husika.

Biteko alitumia fursa hiyo kuiomba serikali ya Australia kuangalia uwezekano wa kuendesha warsha husika kwa wachimbaji wadogo nchini ili wapate maarifa ya namna bora ya usimamizi wa rasilimali za madini. Akizungumzia mchango wa sekta ya madini kwenye uchumi wa viwanda, Biteko alieleza kuwa, rasilimali za madini ni tegemeo kubwa katika kukuza uchumi huo.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya madini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
Mtaalamu wa Madini kutoka Australia, Rick Rogerson, akiwasilisha mada katika warsha ya wataalam wa madini nchini (hawapo pichani), iliyofanyika Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
Kutoka kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi David Mulabwa; Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania, Prof Shukrani Manya wakijadiliana jambo, wakati wa ufunguzi rasmi wa warsha ya wataalam wa madini nchini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), akijadiliana jambo na Mtaalamu wa Madini kutoka Australia, Rick Rogerson, muda mfupi baada ya Naibu Waziri kufungua rasmi warsha ya wataalam wa madini nchini, iliyotolewa na wataalam kutoka Australia; Juni 4 na 5 mwaka huu, jijini Dodoma.

VIDEO: MADEREVA WASIO NA LESENI MKOA WA RUVUMA KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA

$
0
0
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa RUVUMA kimejipanga kikamilifu katika kuhakikisha madereva wanaoendesha vyombo vya moto vyenye miguu miwili maarufu kama bodaboda wanafuata sheria,ikiwemo kuwa na leseni pamoja na kuvaa kofia ngumu pamoja na abiriwa wake. Hayo yamebainishwa na maratibu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa RUVUMA SALUMU MORIMORI wakati akitoa elimu kwa baadhi ya madereva bodaboda mjini SONGEA.

VIDEO: MAKAMU WA RAIS AZINDUA UKUTA WA FUKWE WA BAHARI- BARABARA YA BARACK OBAMA DAR ES SALAAM

RC MGHWIRA ATOA ONYO KALI KWA WANAOHARIBU MIUNDOMBINU YA TANESCO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Mghwira ametoa onyo kali kwa wakazi wa mkoa huo wanao jihusisha na uhabifu wa miundombinu ya Shirka la Umeme Tanzania (Tanesco) na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema, serikali inatumia gharama kubwa sana kuendesha shirika hilo hivyo kulihujumu kwa kuharibu miundimbinu sio sahihi na halivumiliki. 

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na waandisi wa habari, katika kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya athari za kuhujumu miumbombinu ya shirika hilo. 

“Hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya baadhi ya watu kupoteza maisha baada ya kujaribu kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi. naagiza wakazi wa mkoa huu kuacha kabisa tabia hiyo kwani matukio ya aina hiyo ni sawa na matukio ya uhujumu uchumi, ambayo yanarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana na hivyo kufikia uchumi wa kati kupita viwanda,” alisema 

Aliongeza kuwa uhujumu wa miundombinu sio tu inaleta hasara kwa shirika lakini pia inapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa kupitia maafa mbalimbali ikiwemo vifo na ulemavu kwa watu wanaohusika na matukio hayo. Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro Mahawa Mkaka alisema changamoto ya uharibifiu wa miumbombinu unatokana na uelewa mdogo kuhusiana na madhara yatokanayo na umeme. 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza na waandishi wa habari katika kampeni maalumu ya kuzuia uharibifu wa miundombinu ya umeme mkoani humo. 
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi inayoendelea mjini Moshi 
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Salama
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Salama.
Mafundi wa Tanesco wakikata miti iliyopita katika njia za umeme Moshi. 



Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma(Epicor 10.2) kuboresha usimamizi wa mapato na matumizi kwenye Halmashauri nchini

$
0
0
Daudi Manongi- MAELEZO, Iringa
Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) utawajengea uwezo wahasibu na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ili kusimamia vyema mapato na matumizi ya fedha za umma kwenye halmashauri zao.
Hayo yamesemwa leo Mkoani Iringa na Katibu tawala wa mkoa huo Bi Wamoja Ayubu wakati akifungua mafunzo ya mfumo huo  Mkoani hapa.
"Mfumo wa Epicor 10.2 umeandaliwa mahsusi kuungana na mifumo mingine ili kukidhi matakwa ya maboresho yanayoendelea, Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo ili muweze kusimamia fedha za umma na kuwapatia uelewa wa mabadiliko ya msingi yaliyofayika bila kukwamisha  utoaji wa huduma kwa wananchi" Alisema Bi.Ayubu
Aidha ameeleza kuwa kupitia mafunzo haya wahasibu na maafisa usimamizi fedha wa mikoa wataelekezwa kwa ufupi namna mfumo wa epicor 10.2 utakavyobadilishana taarifa na mifumo ya mipango na bajeti (PlanRep) pamoja na mfumo wa FFARS na hivyo kuleta utejelezaji wa dhana nzima ya uwazi,uwajibikaji  na  utawala bora katika usmamizi wa fedha za umma.
Pamoja na hayo katibu tawala huyo ameishukuru TAMISEMI kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo ambao ni mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma(PS3), kwa kazi nzuri inayofaywa na mradi huo kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika  mkoani Iringa.
 Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya TEHAMA-TAMISEMI Bw.Baltazar Kibola akifuatilia jambo wakati wa  Mafunzo ya usimamizi wa fedha za umma kwa watumishi  wa mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa yaliyofanyika leo Mkoani Iringa.
 Muhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi.Catherine Kiyuo akimwelekeza jambo mshiriki wa mafunzo ya usimamizi wa fedha za umma kwa watumishi kwa watumishi wa mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa jinsi mfumo huo unavyofanya kazi leo Mkoani Iringa.
 Washiriki wa Mafunzo ya Usimamizi wa fedha za Umma ambao wanajumuisha wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo leo Mkoani Iringa.
 Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha akielezea jinsi mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma ujulikanao kama Epicor 10.2 unavyofanya kazi kwa wahasibu na Maafisa usimamizi wa Fedha wa Mikoa mbalimbali leo Mkoani Iringa.
Mhasibu kutoka Mkoa wa Songwe Bw.David Johnson akielezea jinsi gani wahasibu na Maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa wanavyoweza kusimamia mapato kwa kutumia mfumo wa Epicor 10.2 leo Mkoani Iringa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Sekta ya Afya Rukwa yatakiwa kuja na mikakati ya kumaliza matatizo ya uzazi

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali ameitaka sekta ya afya mkoani humo kuhakikisha wanaandaa mkakati wa kupunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la vifo vya watoto wachanga na akinamama vitokanavyo na matatizo ya uzazi.

Amesema kuwa mkakati huo utakamilika endapo kutakuwa na ufuatiliaji wa kila mwezi katika ngazi ya halmashauri pamoja na ufuatiliaji wa kila robo mwaka katika ngazi ya Mkoa ili kubaini changamoto mbalimbali zinazoibuka kila siku na kuona namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

“Kwa mkoa wetu wa Rukwa, kwa mwaka 2017 kinamama 62 walipoteza maisha hii ni sawa na vifo 132 kati ya vizazi hai 100,000, na vifo vya watoto wachanga 15 kati ya vizazi hai 1,000. Kwa takwimu hizi hata kama tunaonekana tuna vifo vichache ikilinganishwa na viwango vya kitaifa bado sio nzuri, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kubuni na kutekeleza njia mbalimbali za kupunguza vifo hivi,” Alisema.

Aliyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili cha kujadili vifo vya watoto wachanga na akinamama vitokanavyo na matatizo ya uzazi kilichowashirikisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu wa wilaya na timu za afya ngazi ya mkoa na wilaya.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inatekeleza haya kwa vitendo juhudi za kupunguza vifo hivyo kwa kuendesha zoezi la ukarabati na upanuzi wa vituo vyote vya afya nchini ambapo Mkoa wa Rukwa umepatiwa shilingi Bilioni 2.9 kukarabati na kujenga vituo vya afya 6 ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri.

Kwa upande wake akisoma risala kbala ya kumkaribisha mgeni rasmi mratibu wa huduma ya afya na uzazi mkoa wa Rukwa Asha Izina amesema kuwa madhumuni ya mkoa ni kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi kwa wanawake na watoto chini ya umri wa miaka mitano na hasa wa chini ya mwaka mmoja na kuhakikisha makundi haya yanapata huduma muhimu Mkoa unatekeleza sera ya serikali ya kutoa huduma bila ya malipo.

“Katika kutekeleza maelekezo ya serikali, Mkoa kupitia ofisi ya mganga mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na mradi wa UZAZI SALAMA Rukwa, tumeanza kufanya vikao vya kujadili vifo vya akinamama na watoto wachanga kila robo mwaka tangu mwanzoni mwa mwaka 2017 tukiwa na lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na vifo hivyo na hatimae kuokoa maisha ya akinamama na watoto wachanga,” Alisema.

Takwimu za mwaka 2015 – 2016 za utafiti wa viashiria vya huduma za afya na Malaria zinaonesha kuwa, vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi kitaifa ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 na vifo vya watoto wachanga ni 39 kwa kila vizazi hai 1,000.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali ( wa Nne kutoka kulia) kwatika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Rukwa, Wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu wa mikoa na timu za afya ngazi za halmashauri na mkoa.

Balozi wa Kuwait nchini aanda iftar jijini Dar

$
0
0
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akiongozana na Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakati wakiwasili kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam kwa Iftar iliyoandaliwa na Balozi huyo kwa heshima ya Dkt. Waliyd Shuaib Msaidizi Waziri wa Wakfu nchini Kuwait anayeshughulika na maswala ya Quran Tukufu.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza machache katika Iftar aliyoiandaa kwa wadeni mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ikiwa kwa heshima ya Dkt. Waliyd Shuaib Msaidizi Waziri wa Wakfu nchini Kuwait anayeshughulika na maswala ya Quran Tukufu.
 Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya frame yenye nembo ya Kuwait kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem baada ya hafla ya Iftar aliyoiandaa kwa wageni mbalimbali waliofika. Kushoto ni Dkt. Waliyd Shuaib Msaidizi Waziri wa Wakfu nchini Kuwait anayeshughulika na maswala ya Quran Tukufu na Kulia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana.
 Baadhi ya wageni wakipata Iftar iliyoandaliwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akisalimiana na baadhi ya wageni wake waliofika kwenye Iftar aliyoiandaa kwa heshima ya Dkt. Waliyd Shuaib Msaidizi Waziri wa Wakfu nchini Kuwait anayeshughulika na maswala ya Quran Tukufu.
picha ya pamoja.

Matumizi ya TEHAMA Kuboresha Huduma za Afya Katika Halmashauri

$
0
0
Mkuu wa Timu ya Mifumo ya Rasilimali Watu Dkt. Josephine Kimaro akisisitiza umuhimu wa matumizi ya mfumo unaotoa taarifa kuhusu uhitaji wa watumishi katika kituo cha kutolea huduma (WISIN) na Mfumo unaogawa watumishi kulingana na vipaumbele (POA) leo Jijini Mbeya, ambapo mafunzo hayo yatawashirikisha watumishi wa sekta hiyo wa mikoa yote Tanzania Bara.

Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya

Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imetajwa kuwa chachu ya kuboreshwa kwa huduma za Afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) kote nchini.

Akizungumza leo Jijini Mbeya wakati wa mafunzo ya matumizi ya mifumo ya WISN na POA kwa Watumishi wa Sekta ya Afya, Utawala, na Serikali za Mitaa, Mkuu wa Timu ya Mifumo ya Rasilimali Watu kutoka mradi wa kuimarisha mifumo ya sekta za umma (PS3) Dkt. Josephine Kimaro, amesema kuwa lengo la mifumo hiyo ni kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi kupitia vituo vya kutolea huduma za afya.

PS3 ni mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi huu wa miaka mitano unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
Mkuu wa Timu ya Mifumo ya Rasilimali Watu Dkt. Josephine Kimaro akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya matumizi ya Mfumo unaotoa taarifa kuhusu uhitaji wa watumishi katika kituo cha kutolea huduma (WISN ) na Mfumo unaogawa watumishi kulingana na vipaumbele (POA) leo Jijini Mbeya.

“Mifumo ya WISN na POA inatumika kubaini mahitaji ya watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya na vipaumbele katika maeneo husika, hivyo itasaidia kuleta mgawanyo wa watumishi kwa kuzingatia mahitaji ya kila kituo,” alisisitiza Dkt. Kimaro Akifafanua, Dkt. Kimaro amesema kuwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na mradi wa PS3 wanafanya kazi ya kuhakikisha watumishi katika sekta ya afya wanapelekwa kwenye maeneo yenye uhitaji, ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Mafunzo hayo katika ngazi ya Halmashauri yanawashirikisha Waganga Wakuu wa Wilaya, Maafisa Utumishi na watumishi wengine katika kada ya afya kama Makatibu wa Afya.

Aidha, mafunzo hayo yanayoendelea mkoani Mbeya yameanza kwa kushirikisha Mkoa wa Mbeya na kufuatiwa na Mikoa ya Katavi na Songwe. Pia, mafunzo hayo yanaendelea katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Mtwara na Mwanza.
Katibu wa Afya wa Jiji la Mbeya Bi. Kalunde Mbeyu (Katikati) akifurahia Kiongozi cha Mafunzo ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Mamlaka za Serikali za Mitaa sekta ya afya, wakati wa mafunzo kwa Watumishi wa Sekta ya Afya, Utawala na Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Mbeya ambapo mafunzo hayo yatawashirikisha watumishi wa sekta hiyo mikoa yote Tanzania Bara ili waweze kutumia mfumo wa WISN na POA kwa ufanisi , kushoto ni mtaalamu wa Takwimu za afya wa Jiji la Mbeya Bi. Claudia Kaluli na kulia ni Afisa Afya wa Jiji hilo Bw. Johnson Ndaro.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu mkoa wa Mbeya, Bw. Marko Masaya, amesema kuwa mifumo hiyo imekuja wakati muafaka na itasaidia kurahisisha uandaaji wa mipango ya ajira kwa watumishi wapya kulingana na mahitaji, na kubainisha maeneo watakapopelekwa baada ya kuajiriwa.

“Mifumo hii inaongea, hali itakayosadia kubainisha uwiano wa majukumu kati ya mtumishi mmoja na mwingine katika vituo vya kutolea huduma, hivyo tutabaini watumishi wanatekeleza majukumu mengi zaidi kuliko inavyotakiwa ili tuweze kuongeza watumishi wengine katika eneo hilo,” alisisitiza Masaya Akieleza zaidi amesema kuwa moja ya hatua zitakazochukuliwa ili kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inaleta matokeo chanya, Mkoa huo utaongeza usimamizi kwa watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma ili takwimu zinazokusanywa kupitia mifumo hiyo ziwe halisi na hivyo kusaidia katika kuimarisha huduma kwa wananchi.

Mifumo ya WISN na POA iko chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, pamoja na Ofisi ya Rais Utumishi, ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Mfumo unaotoa taarifa kuhusu uhitaji wa watumishi katika kituo cha kutolea huduma (WISN ) na Mfumo unaogawa watumishi kulingana na vipaumbele (POA) wakifuatilia namna mfumo huo unavyofanya kazi leo Jijini Mbeya.
Mtaalamu wa mifumo ya taarifa za sekta ya Afya kutoka Wilaya ya Rungwe Bw. Melchizedeck Stephen akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Timu ya Mifumo ya Rasilimali Watu Dkt. Josephine Kimaro kutoka Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) wakati wa mafunzo ya Mfumo unaotoa taarifa kuhusu uhitaji wa watumishi katika kituo cha kutolea huduma (WISN ) na Mfumo unaogawa watumishi kulingana na vipaumbele (POA) leo Jijini Mbeya.

MAkamu wa Rais azindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikagua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam mara baada ya kuuzindua mapema hii leo, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Sehemu ya kupumzika iliyojengwa katika ukuta wa ufukwe wa bahari ya Hindi uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Msanii Beka Fleva akitoa burudani kwa wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wananchi mara baada ya kuzindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO 

BODI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YAJIONEA JUHUDI ZA KUDHIBITI UJANGIRI PORI LA AKIBA MASWA

$
0
0
BODI ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko imefanya ziara ya kujionea shughuli za uhifadhi na juhudi za kudhibiti wa vitendo vya ujangiri zinazodaiwa kufanywa na mwekezaji Mwiba Holding aliyepo Pori la Akiba Maswa lililopo wilayani Meatu mkoani Simiyu. 

Mbali ya kujionea vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangiri anavyotumia mwekezaji Mwiba Holding, Mwenyekiti wa Bodi akiwa ameongozana na wajumbe wake pia alitembelea kambi ya askari wa doria na kujionea changamoto na mafanikio kadhaa. 

Akizungumza na askari hao amewataka kufanya kazi kwa bidii kwani tayari Bodi yake imefanyia uamuzi baadhi ya masuala ili kuruhusu mabadiliko ya kimfumo wa uendeshaji Mamlaka hiyo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Bariadi juzi kuhusu umuhimu uhifadhi kupitia Pori ya Akiba Maswa linavyochangia maendeleo hususani sekta ya elimu na afya kwa wananchi
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu Paul Susu akiwaonyesha maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) na maofisa Elimu Mkoa shughuli za ufyatuaji tofali ambao fedha zake zilichangiwa na TAWA kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za shule ya vipaji maalumu ya  Sekondari ya Ufundi Simiyu inayojengwa mjini Bariadi.
 Meneja wa Pori la Akiba Maswa Lusato Masinde akiwaonyesha wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) pichani mazingira yalipo kambi ya askari wanaoshiriki kufanya doria kwenye pori hilo upande wa Kijiji cha Butuli wilayani Meatu mkoani Simiyu.

 Mkurugenzi wa Utalii Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Iman Nkui akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bodi ya mamlaka hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake mwenye koti jeusi Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko.
 Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Luteni Jenerali Mstaafu Samweli Ndomba akizungumza na askari waliopo Pori la Akiba Maswa wilayani Meatu mkoani Simiyu kuhusu kujituma na kuibenda kazi yao.
 Mkurugenzi wa Utalii Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Iman Nkui akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo wakati Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali alipotembelea na kujionea changamoto zinazowakabili akari katika Pori la Akiba Maswa lililopo wilaani Meatu mkoani Smiyu, aliongozana na wajumbe wa bodi hiyo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA),  Meja Jenerali Hamis Semfuko akizungumza na akari wa Pori la Akiba Maswa lililopo wilayani Meatu mkoani Simiyu, kushoto kwake ni Mjumbe wa Bodi hiyo Luteni Jenerali Mstaafu Samweli Ndomba na pembeni ni Meneja wa pori hilo Lusato Masinde.

MAPACHA WALIOUNGANA MARIA NA CONCOSALATA KUZIKWA KATIKA KABURI MOJA

$
0
0
*Tayari maandalizi ya jeneza la kipekee na kaburi kubwa yakamilika, kaburi lao kuzungukwa na makaburi ya mapadre, masista

 Na Ripota Wetu,Iringa

Tayari Maandalizi ya kuipumzisha Miili ya mapachaa hao yamekamilika baada ya jeneza la kipekee na kaburi kubwa lililochimbwa katika makaburi wanayozikwa masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga kukamilika. 

Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Shule ya Seminari ndogo ya Tosamaganga Padre Benedict Chavala amesema uamuzi wa mapacha hao kuzikwa Tosamaganga, kutawasaidia kuendelee kuwaombea. Awali kulikuwa na msuguano wa eneo watakalozikwa mapacha hao uliohitimishwa na Mkuu wa Masista wa Shirika la Maria Consolata, Jane Nugi kudai walichagua kuzikwa wanakozikwa viongozi wa kanisa hilo. 

Msuguano huo pia ulitokana na hatua bibi wa marehemu upande mama yake, kudai miili hiyo isafirishwe kwa ajili ya maziko Bukoba jirani na alipozikwa marehemu mama yao. Alipoulizwa endapo kama itatokea wakasema miili hiyo izikwe Bukoba wakati tayari Iringa wameshachimba kaburi Padre Chavala alisema kuwa itategemea watu hawa wana hoja nzito kiasi gani. 

“Muda mwingi wamechukuliwa ni watoto wetu nahivyo tunapenda watuelewe kwamba tangu mwanzo kama kanisa liliamua kuwachukua kutokana na mazingira waliokuwa nayo na kuwalea tunasikia ni wanetu na kama ni wanetu basi tubaki nao hapa ambapo wapo mama na bibi zao ambao ni masista ili tuweze kuwakumbuka muda wote.”alisema Padre Chavala na kuongeza: 

“Wanaendelea kuwa karibu nasi kuliko kupelekwa huko hata pengine hawajawahi kufika,kila mmoja atawashangaa inakuwaje hawa watu wanakuja wakiwa wamefariki wakati wakiwa wazima hawajawahi kufika,na kilio ni kilio,msiba ni msiba wakubali tu wazikwe hapa ni pazuri zaidi hata wao wenyewe waje tulie pamoja.”alisema Padre Chavala 

Alisema masista walio walea kwa muda mrefu tayari ni wazee kuwapeleka hukombali hao masista watajisikia wapweke zaidi kwa sababu wameachana na wapendwa wao halafu kuwapeleka mbali ambapo wao hawawaoni. “Jambo lote hili lina uzito wake,kule nako wakipelekwa kuna uzito wake lakini hapa pia pana uzito zaidi.”alisema Padre Chavala 

Chavala akizungumzia utofauti wa kaburi la maria na Consolata alisema kuwa wanaweka pana kwasababu wapo watu wawili,lazima ukubwa wake utofautiane na kaburi linalozikwa mtu mmojammoja. “Wapo watu wawili,tumeamua kuwaweka mahali pamoja lakini upekee wa kaburi ni kwamba watu hawa tunaendelea kuwalea katika vituo vyetu,ni wenzetu,tunawaweka hapa ambapo wanalala Masista,Mapadre,Mabrother na hata walei sasa hawa wamepata upekee sana kwa sababu wamebaki wakilelewa na masista.”alisema Chavala 

Naye sista Calista Ludega ambaye ni mkuu wa shirika la mtakatifu Theresa wa mototo Yesu jimbo katoliki la Iringa alisema kuwa wanawazika Maria na Consolata mahala wanapolala masista wa consolata kwa ajili ya kuwaenzi masista wa mishionari wa consolata kwa kuwa wao wamechukuwa sehemu kubwa ya malezi tangu walipozaliwa watoto hao hadi wanapomaliza maisha yao hapa duniani. 

Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista ambao walikwisha fariki Maraia Lorenta,Masweta Pagosi na Maria Saglio. Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu. 

Vifo vya mapacha hao vimeleta simanzi na huzuni kubwa kwa Watanzania walio wengi akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.John Pombe Magufuli ambapo baada ya kupata taarifa za vifo hivyo alisema na hapa namkunukuu “Nimesikitishwa na kifo cha maria na Consolata .Nilipokwenda hospitali waliliombea taifa.Walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa .Poleni familia , masista wa maria Consolata na wote walioguswa , pumzikeni mahali pema wanangu .Bwana alitoa na bwana ametwaaa.Jina la bwana lihimidiwe.
 Baadhi ya Ndugu na Jamaa wakishiriki kuchimba kaburi ambalo Mapacha walioungana Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa hapo kesho 
 Sehemu ya Makaburi yaliyolizunguka kaburi la Mapacha walioungana ,Marehemu Maria na Consolata,ambapo Masista na Mapadre wamezikwa
 Baadhi ya Ndugu na Jamaa wakiendelea kushiriki kuchimba kaburi ambalo Mapacha walioungana,Marehemu Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa hapo kesho .
Zoezi la uchimbaji wa kaburi kwa ajili ya maziko ya mapacha walioungana, marehemu Maria na Consolata linaendelea katika Makaburi ya Masista wa Shirika la Bikira Maria wa Consolata Tosamaganga,  Jimbo Katoliki la Iringa.


KIGWANGALLA AAGIZA MSAKO MKALI KWA WALIOUA SIMBA TISA SERENGETI

$
0
0
Na Hamza Temba-Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Serengeti kuwasaka watu waliohusika na mauaji ya simba tisa katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo ofisini kwake Jijini Dodoma jana baada ya kupokea taarifa rasmi ya mauaji hayo ya kikatili yaliyoripotiwa hivi karibuni kwa simba hao kulishwa sumu kali katika kijiji hicho huku mmoja akikatwa miguu, mkia, ngozi ya juu ya mgongo na kuchukuliwa baadhi ya viungo vyake ambapo amesema mauaji hayo hayavumiliki kwa kuwa yana athari kubwa kiikolojia, kiutalii na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

"Bahati mbaya sana ni kuwa anapouawa simba kwa sumu hafi peke yake, inakufa familia nzima ya simba, na mara nyingi wanakufa pia wanyamapori wengine wanaodowea nyama na wanaokula mizoga. Walipouawa simba wa Ruaha hivi karibuni walikufa fisi zaidi ya 70 na ndege mbeshi zaidi ya 100, achilia mbali wadudu," amesema Dkt. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.

Amesema pamoja na faida kubwa za simba kwa Taifa kiuchumi, Kijiji cha Nyichoka pekee walikouwawa simba hao ni katika sehemu iliyofaidika sana na miradi ya ujirani mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti."Wanyama hawa jamii ya paka wakubwa ni muhimu sana kwa kuweka mizania ya ikolojia sawa, maana wanadhibiti idadi ya wanyama wala nyasi kwa kuwala, bila hivyo hifadhi zote zinaweza kugeuka kuwa jangwa. 
Baadhi ya simba kati ya tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara
Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.
Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.

UONGOZI SHULE YA ST FLORENCE WAMZUNGUMZIA MWALIMU ANAYETUHUMIWA KWA KUDHALILISHA WANAFUNZI WA KIKE

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Shule ya St Florence Academy ya jijini Dar es Salaam umesema umesikitishwa na habari za mmoja wa walimu wake kutuhumiwa kuwadhalilisha wanafunzi wa kike kijinsia huku ikifafanua kuwa umejipanga kuongeza CCTV Camera katika sehemu mbalimbali za shule ili kuimarisha usalama

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Shule hiyo, Flora Damas Assey amesema kuwa wao kama uongozi, wazazi na walezi wamesikitishwa mno na taarifa hizo.

"Hii ndio mara ya kwanza mwalimu wa shule yetu ambayo ilianzishwa zaidi ya miaka 25 iliyopita kupatwa na tuhuma kama hizi na tumekuwa tukijitahidi kuajiri walimu makini na kujenga imani kwa wazazi na jamii nzima kwa ujumla kutokana na matokeo mazuri ya wanafunzi wetu na nidhamu ya hali ya juu ambayo inaendana na sera ya shule yetu,"amesema Assey.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uongozi wa shule hiyo umetoa ushirikiano mkubwa kwa Jeshi la Polisi ambalo linachunguza suala hilo na tayari uongozi na kamati ya shule umekutana na kukubaliana kutekeleza masuala kadhaa.

"Tunapenda kukanusha taarifa zilizozagaa hivi karibuni kuwa shule imemficha mwalimu huyu anayetuhumiwa kwani hata sisi hatujui aliko na tunaendelea kushirikiana na Polisi katika suala hili,"amesema huku akitoa mwito kwa wananchi pia walisaidie Jeshi la polisi ili sheria ichukue mkondo wake.

Mkurugenzi huyo amesema baadhi ya mambo walioazimia kufanya ni kuongeza CCTV camera katika sehemu mbalimbali za shule ili kuimarisha usalama,  kuimarisha uchunguzi wa ndani mara kwa mara na kuimarisha kitengo cha ushauri ili wanafunzi wapate usimamizi wa karibu na waendelee kupata ushauri  (counseling) pale inapohitajika.

"Kama uongozi wa Shule ya St. Florence tunatoa rai kwa wazazi wote wawe na subira wakati huu ambao polisi wanaendelea na uchunguzi na shule itatoa ripoti mara kwa mara kuhusu suala hili,"amesema.

Pia amesema shule inaendelea na maandalizi ya mtihani wa darasa la saba na kuwataka wazazi na walimu washirikiane na uongozi kuhakikisha matokeo mazuri yanapatikana.

"Tumekuwa tukifanya vizuri katika mitihani mbalimbali inayosimamiwa na Baraza la Mitihani Tanzania na kupokea vyeti na tuzo mbalimbali kutoka serekalini na taasisi mbalimbali kutokana na matokeo haya ambayo tuko tayari kuhakikisha tunayaendeleza,"amefafanua na kuongeza St.Florence Academy, ambayo ni moja ya shule bora nchini, ilianzishwa  mwaka 1993.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kijitoupele Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama, akijadili jambo na Waziri wa Elimu Profesa Joice Ndalichako, Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Elimu Profesa Joice Ndalichako, Bungeni jijini Dodoma, Juni 5, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma, Juni 5, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar Asha Abdullah Juma, Juni 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Halotel yazindua laini mpya za watu mashuhuri (VIP).

$
0
0

-Ni laini zenye gharama nafuu Zaidi, hazihitaji kujiunga kifurushi

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua laini mpya za watu mashuhuri zilizopewa jina la VIP zitakazo wawezesha wateja wa mtandao huo kufanya mawasiliano kwa makato ya gharama nafuu zaidi kwa kila dakika na MB za intaneti watakazo tumia.

Laini hizo za VIP zitawawezesha wateja wa mtandao wa Halotel nchi nzima kuweza kupiga simu au kutumia intanenti kwa gharama nafuu kwa kutumia salio la muda wa kawaida wa maongezi bila kuwa na ulazima wa kujiunga na kifurushi chochote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, uzinduzi huo wa laini za VIP ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama ambapo badala ya mteja kutumia muda na gharama kujiunga na vifurushi vya kupiga simu kwa mtandao wa Halotel na mitandao yote au vifurushi vya intaneti mteja ataweza kutumia salio la muda wa maongezi kupiga simu au kutumia intaneti bila kuhofia matumizi makubwa ya makato kwa gharama nafuu zaidi.

“Huduma hii inawalenga wateja wa vipato vya aina zote, wale wenye matumizi ya kati, na matumizi makubwa, ambapo katika laini hii ya VIP makundi hayo yamegawanywa kwa kupewa majina ambayo ni Silver kwa wateja wenye matumizi madogo, Gold kwa wateja wa matumizi ya kati na Diamond kwa wateja wa matumizi makubwa. Makundi haya yana lengo la kukidhi mahitaji ya kila mteja kulingana na kundi alilomo.” Alisema Semwenda na kuongeza.

“Mfano kwa mteja atakayenunua laini ya VIP ya Silver yenye thamani ya shilingi elfu tano (5,000) kwa pesa hiyohiyo anaweza kupiga simu Halotel kwenda Halotel kwa gharama ya makato ya shilingi thelathini (30) tu kwa dakika ambapo kwa makato ya gharama ya kawaida ni shilingi (228) kwa dakika ambapo ni mara punguxo la mara saba(7) ya gharama za kawaida. 

Vile vile mteja katika kundi hili anaweza kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya makato ya shilingi arobaini na tano (45) tu kwa dakika tofauti na makato ya gharama ya kawaida ambayo ni shilingi (228) kwa dakika ambapo ni punguzo mara tano (5) ya gharama za kawada. Kwa MB 1 mteja atatumia intanenti kwa gharama ya shilingi nne (4) tu akiwa na laini ya Silver ya VIP gharama ambayo ni mara saba(7) pungufu ya makato ya gharama ya kawaida ya shilingi 30.72 kwa MB huku akifurahia kutumia Facebook bure.” Alisema Semwenda.

Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia kupiga simu Halotel na mitandao yote pamoja nakutumia Mb za intanenti kwa kupiga *148*66# kisha anachagua namba tisa (9) na hivyo kuendelea kuchagua kundi atakalohitaji kujiunga, si hivyo tu mteja wa Halotel wa kawaida anaweza kuendelea kujiunga na vifurushi kama kawaida endapo atahitaji.

Hii ni moja ya maendeleo ya teknolojia katika kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wetu ambao wamekuwa na imani kubwa ya huduma zetu siku zote” alisema Tito.

“Tunatarajia huduma hii ya VIP itaongeza nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wetu na kwa watanzania wote, na kuokoa kiasi kikubwa cha gharama za mawasiliano zinazokatwa wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana, biashara na kupata taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia intaneti kwa uhakika. Alihitimisha Semwenda.”
Meneja wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta, Halotel akiwaeleza waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi wa huduma ya VIP ambapo Mteja yeyote wa Halotel wa kawaida ana uhuru wa kuweza kubadili laini yake na kuwa laini ya VIP na kuweza kufurahia huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akiwaeleza waandishi wa Habari, akitoa ufafanuzi mbele ya waandish wa Habari katika uzinduzi wa huduma ya VIP, ambayo ni mwendelezo wa ubunifu na maboresho ya huduma za mawasiliano kwa wateja wa Halotel kwa kuwaokolea muda na gharama katika matumizi yao ya kila siku. Kulia ni Meneja wa idara ya ushirika Halotel Emmanuel Tito Malyeta. 

AAR YAPANDA MITI SHULENI KUSAIDIA UTUNZAJI BORA WA MAZINGIRA

$
0
0
Kampuni ya bima ya afya nchini ya AAR imepanda miti katika Shule ya Msingi ya Ushindi iliyoko eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono kwa vitendo utunzaji wa mazingira.

AAR imefanya zoezi hilo Jumanne wiki hii ikipanda jumla ya miti sitini (60) katika shule hiyo ya umma iliyo kwenye eneo lililo karibu na ofisi zake za makao makuu, katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani.

Akizungumza baada ya upandaji miti, Msemaji wa AAR, Hamida Rashid amesema kuwa kuboresha na kulinda afya ya jamii ni sehemu muhimu ya jukumu la kampuni hiyo, hivyo haina budi kusaidia na kuhamasisha kwa vitendo utunzaji wa mazingira katika jamii inayoizunguka kwani ndio msingi wa uhai.

“Tunafamu mazingira ni muhimu katika maisha yetu kwani ubora wa afya na uhai wetu unategemea hali ya mazingira yetu.  Kama kampuni ya bima ya afya ambayo hujikita katika kuboresha na kulinda afya ya jamii, tunaamini kwamba ni jambo lisilowezekana kuwa na jamii yenye afya bora bila kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwenye mazingira bora yanayohifadhiwa vizuri,” alisema Hamida 

“Ndio sababu tumeamua kuhamasisha jamii kwa vitendo kupanda miti. Tunaamini elimu ya mazingira ikitolewa vizuri kwa jamii kuanzia kwa watoto shuleni tutajenga taifa la wachapakazi ambalo ni rafiki wa mazingira,” Hamida aliongeza. 
 Meneja wa Maendeleo na Biashara wa AAR Insurance, Hamida Rashidi (kulia) akishiriki katika zoezi la kupanda miti lililoandaliwa na Kampuni ya Bima ya AAR katika siku ya kusheherekea siku ya mazingira duniani
 Wafanyakazi wa AAR Insurance, Sammuel Budodi (kushoto) na Geophray Peter(katikati) wakipanda mti pamoja na mwanafunzi wa shule ya msingi ya Ushindi katika siku ya Mazingira Duniani
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ushindi Mikocheni wakipanda Miti katika zoezi liloandaliwa na Kampuni ya Bima ya AAR ikiwa ni ishara ya kusherekea siku ya Mazingira Duniani
 Wafanyakazi wa AAR Insurance wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ushindi Mikochi mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti  ikiwa ni ishara ya kusherekea siku ya Mazingira Duniani.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ushindi, Mikocheni wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda Miti lililoandaliwa na Kampuni ya Bima ya AAR ikiwa ni ishara ya kusherekea siku ya Mazingira Duniani.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images