Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MO AANZISHA TUZO SIMBA, KUANZA KUTOLEWA JUNI 11 MWAKA HUU

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

MWEKEZAJI katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'MO' ameanzisha tuzo zitakazotolewa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa klabu ya Simba ambazo amezipa jina la Mo Simba Awards.

Kwa mara ya kwanza tuzo hizo zitatolewa Jumatatu ya Juni 11 mwaka huu katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 16, ambavyo ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Shabiki Bora wa Mwaka na Tuzo ya Heshima.

Pia tuzo zingine ni Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka, Tuzo ya Benchi la Ufundi, Kiongozi Bora wa Mwaka, Tuzo ya Wasimamizi wa Mchakato wa Mabadiliko, Mhamasishaji Bora wa Mwaka katika Mitandao ya Kijamii, Mhamasishaji Bora wa Mwaka na Tawi Bora la Mwaka.

Washindi wa tuzo hizo watatokana na kura ambazo zitapigwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii na tovuti ya mosimbaawards.co.tz na kamati maalumu ya tuzo ambayo itahusisha wadau mbalimbali wa mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Akizungumza kuhusu tuzo hizo, Dewji amesema ameanzisha tuzo hizo kwa lengo la kutambua mchango wa wachezaji, viongozi na mashabiki ambao juhudi zao zimeiwezesha Simba SC kupata mafanikio iliyonayo sasa.

Dewji amesema tuzo hizo ni sehemu ya mikakati yake ya kuifanya klabu ya Simba kuwa timu kubwa barani Afrika, ambayo itakuwa na uwezo wa kifedha ambao utaiwezesha kuwa na wachezaji na benchi la ufundi bora ambalo litaiwezesha kushinda mataji makubwa.

"Simba ni timu kubwa inastahili kuwa na tuzo zake ambazo zitakuwa zinatolewa kwa kutambua mchango wa wenzetu ambao umetuwezesha kupata mafanikio haya ikiwepo kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ni jambo ambalo litawatia moyo kuendelea kujituma lakini hata kwa ambao watakosa itawatia hamasa na hivyo kuongeza juhudi," amesema Dewji.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo itakuwa mbashara kupitia Azam.

Mafunzo ya Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) yafanyika Mkoani Iringa

$
0
0
Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha akifuatilia jambo kwa washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) yanayoendelea Mkoani Iringa yakiwashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) yanayoendelea Mkoani Iringa yakiwashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia mfumo mpya wa Epicor 10.2 leo Mkoani Iringa ambapo mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia mfumo mpya wa Epicor 10.2 leo Mkoani Iringa ambapo mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia mfumo mpya wa Epicor 10.2 leo Mkoani Iringa ambapo mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) wakifanya mtihani wa tathmini katika magrupu leo Mkoani Iringa ambapo mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw.Juma Shaha(kushoto) akifuatiia jambo na Mtaalamu mshauri wa Masuala ya rasilimali fedha Bi.Hellen Nyagwa wakati wa mafunzo ya Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) yanayofanyika kwa wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Washiriki wa mafunzo  wa Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma (Epicor 10.2) wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia mfumo mpya wa Epicor 10.2 leo Mkoani Iringa ambapo mafunzo hayo yanawashirikisha wahasibu,waweka hazina na maafisa usimamizi wa fedha wa mikoa ya Tanga,Iringa na Morogoro.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO, IRINGA

ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa askari wake mmoja ameuawa na wengine watano hali zao si nzuri baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi kinachojulikana kwa jina la Siriri kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Taarifa ya kifo cha mwanajeshi huyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Kanali Ramadhan Dogoli ambapo akifafanua kuhusu kifo hicho amesema Juni kuwa 3 mwaka huu kikundi chetu cha wanajeshi , maofisa na askari ambao idadi yao ilikuwa 90 kikiwa katika uwajibakaji kilishambuliwa na kikundi hicho cha waasi.

Amefafanua sehemu ya kikosi hicho cha kulinda amani kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati(TANZBATT-1 CAR)baada ya kuanza kushambuliwa na waasi hao kwa kushtukizwa kiliamua kujibu mapigo.

"Kikundi chetu kilijihami kwa kujibu mapigo kijasiri na kufanikiwa kuwashinda nguvu washambuliaji na kwa bahati mbaya katika mapambano hayo askari wetu mmoja alipoteza maisa na wengine 18 walipata majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao,"amesema.

Ameongeza kati ya hao waliojrehiwa askari watano hali zao si nzuri sana na kuongeza kuwa "askari wetu waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo Bangui katika Mji mkuu wa nchi hiyo".

Kanali Dogoli amesema mipango ya kuurejesha nyumbani mwili wa askari aliyepoteza maisha inafanywa na Umoja wa Mataifa na ikikamilika mwili huo utawasili nchini kwa taratibu za maziko

WAJUMBE KAMATI ZA BAJETI NA UONGOZI WASHAURIANA NA SERIKALI KUHUSU HOJA ZENYE MASLAHI KWA TAIFA

$
0
0

 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia akizungumza wakati wa Mashauriano kati ya kamati ya Bajeti, kamati ya Uongozi  na Serikali kuhusu Hoja zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti na Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Uongozi (hawapo kwenye picha) wakati wa  Mashauriano na Serikali kuhusu Hoja zenye.
 Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu akizungumza wakati wa Mashauriano na Serikali kuhusu Hoja zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019  yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mhe. Mwanne Mchemba
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa kigoma kaskazini, Mhe. Peter Serukamba (katikati) akizungumza wakati wa Mashauriano kati ya kamati ya Bajeti, kamati ya Uongozi  na Serikali kuhusu Hoja zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mwanza Mhe. Kemirembe Lwota na kushoto ni Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mhe. Oran Njeza.
Mjumbe wa kamati ya Bajeti na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa Mashauriano kati ya kamati ya Bajeti, kamati ya Uongozi  na Serikali kuhusu Hoja zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Wajumbe wa Kamati ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki na Mhe. Martha Umbulla na nyuma ni Mhe. Ruth Mollel
 Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Uongozi wakifanya Mashauriano na Serikali kuhusu Hoja zenye Maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

YANGA WAANIKA AJENDA ZA MKUTANO MKUU, YA UCHAGUZI YAWEKWA KANDO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

KUELEKEA Mkutano mkuu wa Yanga Juni 10 mwaka huu, uongozi umeweka wazi ajenda kuu zitakazojadiliwa huku ajenda ya uchaguzi ikiwa imewekwa kando kwanza.

Maandalizi ya mkutano huo kwa wanachama wa Klabu ya Yanga yameshika kasi sasa zikiwa zimesalia siku nne kuelekea mkutano huo muhimu utakaotoa dira kwa klabu hiyo.

Akielezea masuala mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano huo leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wako hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema wanakusudia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

"Tunatarajia kuwaalika watu mbalimbali akiwemo Yusuph Manji ambaye alikua mwenyekiti na mfadhili wa klabu hii, Baraza la Michezo,TFF  pamoja na wizara husika,"amesema Mkwasa.

Mwaliko utapelekwa pia kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Moja ya ajenda katika Mkutano huo maalumu kwa wanachama ni kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo, ikiwa pamoja na suala zima la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Katika ajenda zingine zinazotarajiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kujadili ushiriki wa Yanga katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua waliyofika kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, Mapato na Matumizi, bila ya kusahau Mabadiliko kuhusu mfumo wa uendeshaji.

Pia katika suala la uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi huenda litawasilishwa kupitia mengineyo.Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa ajenda hiyo kuondolewa ili kuwapa nafasi wanachama kujadili masuala muhimu.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amesema mkutano huo utakuwa na lengo la kuwaeleza wanachama matatizo yanayoikabili timu yao, kuhusu uchaguzi wa kuziba nafasi zililizo wazi utatangazwa baadaye.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) kuweka vipimo viwanja vya ndege

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wametia saini na wizara ya afya kutekeleza mpango wa kuzuia magonjwa ya kuambukizwa kupitia viwanja vya ndege. Mpango huo ni endelevu ulioanzishwa na shirika la ndege la kimataifa la usafiri wa anga duniani.

Ambapo kama wanachama wa shirika hilo ambao ni wadhibiti wa mamlaka ya afya nchini wanajukumu la kuchukua mpango huo na kuuandaa kwa kushirikiana na wizara ya afya pamoja na wadau mbalimbali wizara nyingine mbalimbali.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari amesema kuwa dhumuni ni kuhakikisha uboreshaji ili kujihakikishia Tanzania inapambana na magonjwa ya maambukizi yanayotokana na usafiri huo wa anga kwa njia ya muingiliano wa watu kutoka sehemu mbalimbali,  ukizingatia nchi jirani ya Jamuhuri Kidemokrasia ya Congo mlipuko wa ungojwa wa ebola umeshaua watu takribani 15.

Johari amesema pia ni utaratibu huo utawezesha watumiaji wa usafiri wa anga kusafiri kwa usalama.

Mkuu wa vituo vya afya wiwanja vya ndege, bandari na mipaka Remidius Kakulu amesema kuwa mpango huo ukianza utekelezaji wake itasaidia kupambana na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama ebola.

"Katika viwanja  vyetu vyote vya ndege tumefunga vipimo vya kupima joto ambapo abiria  wote wanaoingia nchini watapimwa,kwa atakaeonekena na joto kali atawekwa pembeni kwa ajili ya uchunguzi zaidi"amesema Kakulu.

Aidha kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa kiuchumi na biashara mamlaka ya  usafiri wa anga Tanzania Daniel Malanga amesema kuwa usafiri huo ambao wa haraka kuliko yote ndio unaoweza kusambaza magongwa kwa kasi zaidi kwa kutumia mpango huo muhimu kwa kushirikiana na wadau wengi wa viwanja vya ndege mbalimbali hapa nchin utasaidia kuzuia maambukizi hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari akitia saini leo ikiwa ni makubaliano ya kutekeleza mpango wa kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuambukizwa kupitia viwanja vya ndege hapa nchini katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari(katikati) pamoja na Kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa kiuchumi na biashara wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Daniel Malanga kushoto mara baada ya zoezi la utiaji sani kumalizika leo Jijini Dar ea Salaam.
Picha ya pamoja wadau mbali mbali mara baada ya zoezi la uwekaji wa saini kumalizika leo jijini Dar es Salaam.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 06.06.2018

INTRODUCING NEW SONG "PATRICE LUMUMBA" BY MR TEACHER

$
0
0
Chini ya usimamizi wa JUA Inc, Mr. Teacher ameachia nyimbo mpya iitwayo, “Patrice Lumumba”. Nyimbo hii itaanza kupatikana katika maduka 33 ya mtandaoni siku ya Jumatano, Tarehe 30 May, 2018. Maduka hayo ni haya yafuatayo: Akazoo , Amazon Music, Apple Music, Anghami, Boomplay Music, ClaroMusica, Deezer, Google Play, Gracenote, iHeartRadio, iTune, Juke, KKBox, Kuack, MediaNet, Music load , Napster, Neurotic Media, Q.Sic, Saavn, Shazam , Slacker, SimfyAfrica, , Spinlet, Spotify, Target Music, Tidal, You Tube Music, VerveLife, Yandex, Zvooq, 7Digital, and 8tracks.
 Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia:
 Instagram@muonambali 
Twitter@kolihombi 
Thanks for supporting conscious music.



HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

$
0
0
Na Shani Amanzi, 

Mkuu wa Wilaya wa Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Watendaji na Wataalam wa Halmashauri kusimamia Sheria ndogo za katika ngazi za kata na vijiji katika kuendelea kuisimamia ili kuthibiti uharibifu wa mazingira.

Mhe.Saimon Odunga amesema “ikiwa leo ni siku ya Mazingira Duniani na utaratibu huu hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe moja mpaka sita ,mwezi Juni hufanyika maadhimisho haya, kwa hiyo ni lazima kuzuia viashiria hivyo ikiwemo ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa na kuni,uchomaji moto ovyo misitu,utupaji takataka ovyo,kilimo katika maeneo ya miteremko mikali na uchimbaji wa mawe”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Halmashauri ya Chemba kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wanaendelea na Kampeni ya kupanda miti ndani ya Wilaya ya Chemba.

“Kwa mwaka huu wa 2018-2019 tunatarajia kupanda miti laki tano ,hii ni utekelezaji wa mpango ulioasisiwa na Makam wa Rai,Mhe Samiah Suluhu wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani sambamba na kuisaidia jamii kupata nishati ya kupikia kama vile kuni”aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara wa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Chemba ,Mohamed Semdoe amesema kwa kushirikiana na Viongozi katika ngazi za Kata na Vijiji ,tunaendelea kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Pia Idara ya Usafi na Mazingira imeanzisha mkakati wa kutenga maeneo ya dampo katika ngazi za vijiji pamoja na kuhamasisha jamii zishiriki katika kuchangia gharama za uzoaji taka kutoka katika maeneo ya makazi na biashara.

Kauli mbiu ya mwaka huu Kitaifa ni “MKAA NI GHARAMA;TUMIA NISHATI MBADALA” ambapo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa dampo la Kijiji cha Kidoka ,Kata ya Kidoka, Tarafa ya Goima wilayani Chemba,tarehe 5/6/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba,Saimon Odunga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa dampo la Kidoka,katika kijiji cha kidoka wilayani Chemba

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI

$
0
0
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.

Wameyasema hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.


Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.


Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.


Amesema huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.


“Kwa mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu      ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo.

Rais Magufuli amteua Athuman Selemani Mbuttuka kuwa Msajili wa Hazina

$
0
0
Ndugu Athuman Selemani Mbuttuka alieteuliwa kuwa Msajili wa Hazina


INTRODUCING SIMULIZI YA "KINYAGO"

$
0
0
Kwa  nafasi ya upendeleo New Talents tunachukua fursa hii kukupa nafasi ya kwanza kuitazama hii video ya Simulizi mpya iliyo beba ujumbe mkubwa unaotakiwa kuwafikia Wanadamu, kwani Dunia inamambo mengi  ndio maana wengi wanajikatia tamaa kwa kuikosa thamani yao hapa Duniani.

Amini na kwambia Dunia bila changamoto haiwezi kunoga, ndio maana kila kukicha tumekuwa tukikutana na changamoto za hapa na pale kama vifo,ajali na manyanyaso.

 New Talents Tanzania Crew tunakuletea Simulizi ambayo imepewa jina la ‘KINYAGO’ Simulizi hii imegusa pande nyingi  katika maisha ya wanadamu, imeandikwa na Mrembo Rose Peter Maarufu kwa jina la ‘PUKUU’ chini ya usimamizi wa Director Mr.Super News  tunaomba Support yako katika kuufikisha ujumbe uliyomo ndani ya Simulizi hii kwa jamii Asante.

INTRODUCING "MARUKUTU" BY VATRIMA FT. SOKOMOKO

Tanzania kuwa mwenyeji wa Michezo ya pili ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018)

$
0
0
Michezo ya pili ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018) inatarajia kutimua vumbi jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo nchi 14 tayari zimethibitisha kushiriki. 

 Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maandalizi ya Michezo hiyo, Mkuu wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Leonard Paul  (angalia video) amesema lengo la michezo hiyo kuimarisha ushirikiano na kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu kupitia michezo.

Katibu Mkuu mpya UWT akabidhiwa Ofisi rasmi,awataka wanawake kushikamana kujiletea maendeleo.

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa Katibu Mkuu mpya wa Umoja huo Mwalimu Queen Mlozi pamoja na kukabidhiwa Ofisi rasmi hapo jana jijini Dar.
Katibu Mkuu UWT aliemaliza muda wake Amina Makilagi akimuelekeza jambo Katibu Mkuu mpya UWT Mwalimu Queen Mlozi wakati wa mabdhiano ya Ofisi hapo jana Jijini Dar es salam,Mlozi ,amewataka wanawake kuwa wamoja na kushikamana katika mambo mbalimbali ya kujiletea maendeleo.
Katibu Mkuu UWT aliemaliza muda wake Amina Makilagi pichani kulia akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu Mpya Mwalimu Queen Mlozi hapo Jana katika ofisi za Umoja huo Jijini Dar es salam.
Wakiwa katika picha ya pamoja Uongozi wa sasa na Uliopita wa UWT

DC CHEMBA AWASHAURI WANAWAKE KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KUJENGA UCHUMI, UJASIRIAMALI

$
0
0
Na Shani Amanzi-Chemba.

MKUU wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga amewataka wanawake washiriki  kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ukiwamo ujasiriamali  hasa kwa kuzingatia sehemu kubwa ya viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.

Odunga ametoa kauli hiyo leo wilayani hapo ambapo amesema shughuli ndogondogo za kiuchimi zinampa faida kubwa mhusika hasa akiwa mbunifu mzuri  na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli unaendelea kuwapa kipaumbele wakina mama na vijana kwa kuwapa mitaji.

"Na kwa hapa Chemba Serikali yetu inaendelea kuangalia ni namna gani wanaweza kuzidi kuwasaidia wakinamama.Ni vema kutumia muda wao kujifunza zaidi kuhusu ujasirimali una faida kubwa ,"amesema.

Kwa upande wa Mratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Ulingo, Saum Rashidi amesema lengo la kwenda Chemba ni kuwafikia wanawake walioko pembezoni ili kuwawezesha katika mafunzo ya uongozi, jinsia na ujasirimali.

Amesema lengo wanapokuwa viongozi wamudu majukumu yao kama wanawake viongozi na wawe mfano wa kuigwa ndani ya jamii husika.

Amefafanua taasisi hiyo ipo jijini Dar es Salaam na ni jumuiya ya wanawake na kwamba  wanatoa mafunzo kwa wanawake wote bila kujali itikadi za vyama.

"Na kwa hapa Chemba mafunzo hayo ya ujasirimali yamefanyika ndani ya siku mbili kuanzia Juni 5 hadi Juni 6 mwaka huu katika ukumbi wa Godown, Chemba,"amesema.
MKUU wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza kwenye semina ya Ujasirimali huku akiwataka wanawake washiriki  kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ukiwamo ujasiriamali  hasa kwa kuzingatia sehemu kubwa ya viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.
Mratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Ulingo, Saum Rashidi akizungumza kwenye semina ya ujasiriamali iliyohusu mada mbalimbali ikiwemo kuwafikia wanawake walioko pembezoni ili kuwawezesha katika mafunzo ya uongozi, jinsia na ujasirimali.
Baadhi ya akina Mama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Semena hiyo ya Ujasiriamali.

WAFANYABIASHARA KATIKA MINADA WILAYANI WATAKIWA KULIPA USHURU

$
0
0
Na Shani Amanzi

WANANCHI wa Wilaya ya Chemba wameshauriwa kutumia fursa ya minada midogo inayozunguka wilayani humo kwa lengo la kufanya shughuli za kimaendeleo ili kukuza uchumi hasa katika shughuli za kibiashara huku wakihamasishwa kulipa kodi.

Hayo yamesemwa na Ofisa Minada wa Wilaya ya Chemba Elisante Sendato wakati alipokuwa katika mnada wa Paranga hivi ambapo amefafanua kwa upande wao watasimamia vema shughuli za mnada ili ziende sawa hasa kwa watendaji na wataalam wanaokusanya mapato kwa kutumia mashine maalum.

Sendato amesema kuwa " pia tunaendelea kutekeleza agizo la Halmashauri kwa kila mnada lazima uwe na choo ambapo agizo hilo lilitoka Januari mwaka huu na kwa upande wa Paranga ujenzi wa vyoo upo kwenye hatua za mwisho,"

Kuhusu mafanikio amesema ni makubwa kwani huduma ya kisoko majumbani, ajira kwa wakazi wa Paranga na kupatia mapato Halmashauri ya Chemba imeongezeka.

Wakati huohuo Diwani wa Kata ya Paranga Hamis Ninga amewataka wafanyabiashara wawe na moyo wa kulipia ushuru wa bidhaa wanazouza na kuhakikisha .Pi wamefanya mkutano na viongozi wa minada ili kuhamisisha wenye biashara kutambua wanao wajibu wa kulipa ushuru.
 Ofisa Minada wa Wilaya ya Chemba Elisante Sendato

RAIS DK.SHEIN AWAFUTARISHA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemedi Suleiman (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Mhe.Rashid hadid Rashid mara baada ya Swala ya Magharibi jana kabla ya Futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini  Pemba jana katika Futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar kabi
 Baadhi ya  Mashekhe wakiwa katika Futari iliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pembaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya mbali mbali katika Mikoa ya Zanzibar.
 Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake,Wilaya ya Chakechake ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.
 Baadhi ya Akinamama wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chake chake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akijumuika na Viongozi akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.
 Baadhi ya  akinamama na Wananchi wengine wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman akitoa Shukurani kwa Niaba ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kwa ushiriki wa Wananchi wa Mkoa huo katika Futari  aliyoiandaa jana katika Viwanja vya Ikulu Ndogo ya  Chakechake Wilaya ya Chakechake Pemba ikiwa ni mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Wilaya na Mikoa ya Zanzibar(Picha na Ikulu)

Why you should watch the World Cup on a Smart TV

$
0
0
Smart TVs are the rave of the season and rightly so. Gone are the days when you turn on the television waiting for the channel to start broadcasting. 

Now, the power is in your hands! These devices earned their place by distinguishing themselves from the rest with key features. They have integrated internet and interactive web features. Smart TVs are a combination of flat screen televisions and computers. However, as beautiful and aesthetically appealing as these devices are, they are high-end devices and so come with a hefty price.

For smart TVs, their operating system is preloaded i.e. software apps can be preloaded to the device and updated through an app store similar to smartphones. These devices provide access to content stored on external devices such as an external hard drive and internet applications like YouTube such that one can connect to the internet on the smart TV to watch a YouTube video. Some even enable speech recognition and gestures. The possibilities on these devices are endless!

Features of Smart TVs

Shape: The smart TV is slim. It has no bulge at the back and this makes it easy to fit to the wall. Some have a small stand beneath and can be balanced on a TV stand.HD Picture Quality: This is perhaps one of the best features of the smart TV. Its high definition picture quality helps the viewer to see a much clearer picture. The picture is brightened than ever before.
Internet access: 
Operating system.

MAHAKAMA YARUHUSU HABINDER SETH KUONANA NA MKEWE AKIWA MAHABUSU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mshtakiwa Habinder Seth kuonana na mke wake anapokuwa mahabusu gerezani.

Ruhusa hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi ya utakatishaji dhidi ya Habinder Seth na James Rugemalira ilipokuja mahakani hapo kwa kutajwa.

Mapema, Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai aliieleza Mahakama kuwa, upelelezi wa ndani katika kesi hiyo umekamilika walikuwa wanafanya mawasiliano na nchi husika na katika mawasiliano hayo baadhi yamefanikiwa. Hivyo akaomba muda ili waweze kukamilisha upelelezi.

Aidha alidai kuwa, wamepokea taarifa kutoka kwa jopo la madaktari waliomfanyia uchunguzi Seth na wameelezwa kuwa mshtakiwa huyo hana shida isipokuwa anatakiwa kutolewa balloon tu lililopo tumboni mwake hivyo wanasubiri daktari wake kutoka Afrika Kusini afike kama matakwa ya mshtakiwa.

Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, Wakili wa utetezi, Dorah Malaba aliiomba mahakama iwapatie kibali cha kumruhusu mke wa mshtakiwa Seth, kwenda kumuona mume wake gerezani na kudai kuwa walipeleka barua kwa mkuu wa magereza kwa ajili ya kupata kibali hicho lakini ilishindikana.

Pia ameuomba upande wa mashtaka wajitahidi kukamilisha upelelezi ili haki iweze kutendeka.Aidha wakili utetezi wa Rugemalira, Didas Respicious alidai, "Ni mwaka sasa washtakiwa tangu wafikishwe mahakamani upelelezi bado, tunaomba haki itendeke kwa kuleta ushahidi kwani washtakiwa bado hawajapatikana na hatia, ili tujue kama wateja wetu wanashtakiwa au la.

Kutokana na taarifa ya Seth na mkewe, Hakimu Mashauri amesema" Hapaswi kuingikia taratibu za magereza lakini mshtakiwa anahaki ya kuonana na mkewe, hivyo naruhusu mshtakiwa aonane na mke wake. " amesema Hakimu Shahidi.Washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 21mwaka huu.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images