Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

NSSF DODOMA YATOA NJIA KWA WAJASIRIAMALI KUPATA MIKOPO

$
0
0

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) umewashauri wajasiriamali nchini kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kutambuliwa na kupata mikopo.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma wakati alipokuwa akitoa mada yake kwenye Kongamano la Wajasiriamali lilifanyika jijini Dodoma.

Chuma amesema wajasiriamali hao wakiunda na kuvisajili vikundi vyao watapata mikopo kutoka NSSF ili kukuza biashara zao.Amesema mfuko huo hautaweza kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kwani masharti ya mikopo itatolewa kupitia vikundi au Saccos mbalimbali zilizosajiliwa.

“Lengo la mikopo hii ni kuunga jitihada za serikali katika kuwainua wananchi wa kipato cha chini kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025,”amesema.Pamoja na kupata mikopo wajasiriamali hao, watapata fursa ya kujiunga na pia na kuchangia michango katika mfuko huo jambo ambalo litawawezesha wanachama kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF.

Alitaja baadhi ya mafao hayo kuwa ni fao la Afya linalomwezesha mwanachama aliyejiunga kupata huduma za afya na mafao mengine kusaidiwa wakati wa majanga ya ajali au msiba.Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali hao kuwa waaminifu katika kuchukua na kurejesha mikopo hiyo ili na waweze kukopeshwa.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akionesha kadi ya uanachama wa mfuko huo alipokuwa akizungumza na wajasirimali kwenye kongamano lililofanyika ukumbi wa vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma 
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akizungumza na wajasiriamali katika kongamano lililofanyika ukumbi wa vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma 
Wajasiriamali wakiwa kwenye kongamano uliofanyika jana Jijini Dodoma ambalo liliandaliwa na Mfuko wa NSSF.

WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KUTUMIA MASHINE ZA EFD

$
0
0
Na Veronica Kazimoto- Kibaha

Wafanyabiashara wamehimizwa kutumia Mashine za Kieletroniki za Kutolea Risiti (EFD) kwa kuwa mashine hizo kwa sasa zimeanza kufanya kazi na yeyote anayestahili kutumia mashine hiyo akiuza bidhaa au huduma bila kutoa risiti atatozwa faini ya shilingi milioni tatu hadi milioni nne na nusu. 

Akizungumza mara baada ya kukagua mashine hizo leo wilayani Kibaha mkoani Pwani ambazo hivi karibuni mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi na kusababisha baadhi ya mashine hizo kutokufanya kazi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema kuwa, wafanyabiashara wanatakiwa kutoa risiti kwa kila mauzo wanayoyafanya kwa sababu utoaji wa risiti hizo upo kwa mujibu wa sheria. 

“Sasa hivi wafanyabiashara hawana kisingizio chochote kwa sababu mashine za EFD zote zinafanya kazi na mimi mwenyewe nimejiridhisha hivyo ni lazima kila mfanyabiashara anayestahili kutumia mashine ya EFD atoe risiti kila anapofanya mauzo na wananchi wanatakiwa kudai risiti kila wanaponunua bidhaa au huduma na kwa kufanya hivyo, Serikali itapata mapato yake stahiki,” alisema Kichere.

Akizungumzia kwa upande adhabu ya kutokudai risiti, Kichere alisema kuwa, mwananchi yeyote akikamatwa amenunua bidhaa bila kuwa na risiti ya EFD atatozwa faini ya shilingi 30,000 hadi 1,500,000.“Nawakumbusha wananchi wote kwamba, Suala hili la risiti linahusu pande zote mbili yaani mfanyabiashara na mnunuzi hivyo mtu akikiuka utoaji au upokeaji wa risiti atatozwa faini kama nilivyosema hapo awali,” alisisitiza Kichere.

Naye mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi wilayani hapa Bw. Furaha Njabili amekiri kuwa, mashine hizo zinafanya kazi vizuri na amekuwa akitoa risiti kwa wananchi wanaonunua bidhaa dukani kwake bila matatizo yoyote.

Mnamo tarehe 11 Mei, 2018 Mfumo wa Kupokelea na Kuhudumia Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti ulipata hitilafu ya kiufundi na kusababisha baadhi ya mashine hizo kutokufanya kazi ambapo kwa sasa mfumo huo umetengemaa na mashine hizo za kielektroniki zimeanza kufanya kazi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsikiliza mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi Wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati alipofanya ziara ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia) akiwa ameongozana na Kaimu Meneja wa TRA, Bw. Deogratius Shuma (kushoto) pamoja na watendaji wengine wa Mamlaka wakielekea katika baadhi ya maduka Wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati kwa ajili ya kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.(PICHA ZOTE NA TRA)

MWENYEKITI MSTAAFU BAVICHA AWAGEUZIA KIBAO VYAMA VYA UPINZANI, AWATUHUMU KWA UFISADI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI mstaafu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Patrobas Katambi amevituhumu vyama vya siasa vya upinzani kuwa huko nako kuna wanasiasa mafisadi na wabadhirifu wa fedha za umma.

Amesisitiza ni jambo la kushangaza pamoja na wanasiasa wengi wa vyama vya upinzani kuwa mafisadi bado wameendelea kunyoosha vidole kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakati kwenye upinzani kuna ufisadi mkubwa unafanyika.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katambi ambaye kwa sasa ni kada wa CCM amesema kuna utafiti ambao umefanyika na kubaini kuna ufisadi mkubwa ambao unafanywa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani na anayo orodha ya wanasiasa 11 wanaongoza kwa ufisadi huo.

Katambi ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria amesema inasikitisha kuona jamii inakaa kimya wakati kuna wanasiasa wa upinzani wakiendelea kufanya ufisadi.“Tena baadhi yao wamekuwa wakijipambanua kuwa ni wazalendo na waadilifu lakini ukweli ndio wanaoongoza kwa ubadhirifu wa fedha za Watanzania.Ninayo majina 11 ya wanasiasa ambao wapo upinzani na wanaongoza kwa ufisadi.Kwa sasa sitataja majina yao ili wasivuruge ushahidi,”amesema Katambi.

Wakati anazungumzia wanasiasa hao wanaoongoza kwa ufisadi ameanza kwa kumtaja mwanasiasa namba moja kwa ufisadi nchini(akataja) huku akimtuhumu kwa kuonesha nyaraka mbalimbali.Amesema wanasiasa wa upinzani wamekuwa mstari wa mbele kunyoosha vidole pindi wanaposikia kuna masuala ya ufisadi au ubadhirifu wa fedha upande wa CCM na inapotokea upande wao wanakaa kimya.

Amesema uzuri wa CCM inapoona kuna mambo hayaendi sawa na kuna ubadhirifu au ufisadi eneo fulani wanachukua hatua kwa vitendo tofauti na upinzani ambao kuna wanasiasa wengi mafisadi lakini wanajifanya wasafi.
Hivyo ameomba haki itendeke pande zote na yupo tayari kwenda mahakamani iwapo anaowatuhumu watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo huku akitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya mafisadi waliopo upinzani.

“Nchi yetu tumepewa na Mungu ,utajiri wa rasilimali za kila aina , ila watu wake ni masikini na nchi ni masikini kiuchumi.Sababu kubwa ni makosa ya aina ya siasa, mfumo na uongozi katika uamuzi , mipango , utekelezaji ,rushwa na mgongano kati ya maslahi binafsi na uzalendo (ufisadi),”amesema Katambi.

Ameongeza ugonjwa wa kukosa uzalendo na uaminifu ndio chanzo cha Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kuamua kufanya uchunguzi na mabadiliko katika sheria , mifumo miundo na utendaji ili kuinusuru nchi yetu na taasisi washirika kiuchumi.

“Bila upendeleo wa utoaji taarifa ,vyombo vya habari kwa niaba na faida ya Watanzania leo wajue wapo mafisadi wakubwa kutoka vyama vya upinzani , walipata wapi uhalali na uhodari wa kuchambua na kutuhumu wenzao kwa ufisadi .“Sio vibaya nao Watanzania wakawajua na kutoa hukumu bila upendeleo ili kuisaidia nchi kupata viongozi wazalendo wa kweli,”amesema.
Mwenyekiti mstaafu Baraza la  Vijana wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo AVICHA)Patrobas Katambi akizungumza leo jijini Dar es Salaam.

DKT KIJAJI AFANYA ZIARA MITAANI JIJINI DODOMA KUKAGUA MASHINE ZA EFD,ABAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA HAWAZITUMII

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara katika mitaa ya Jiji la Dodoma, kukagua upatikanaji wa huduma ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs), ambazo mfumo wake ulipata hitilafu hivi karibuni ambao hivi sasa umetengemaa na kubaini kuwa licha ya hitilafu iliyotokea, wafanyabiashara wengi katika jiji hilo hawazitumii ipasavyo mashine hizo.

Dkt. Kijaji aliyeambatana na Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw. Elijah Mwandumbya, amewaonya wafanyabiashara kote nchini wanaokiuka masharti ya matumizi ya mashine hizo kuacha vitendo hivyo mara moja na kuiagiza TRA kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wasiotoa risiti za kieletroniki baada ya kuuza bidhaa zao.

"Wanauza mauzo yao vizuri lakini hawatoi risiti, tumeongea nao kuwaeleza kuwa wanapaswa kutoa risiti wanapouza bidhaa na huduma zao kwani suala hilo ni la kisheria, ni lazima litekelezwe" alionya Dkt. Kijaji.Alisema kuwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuelewa kuwa maendeleo ya nchi hayawezi kupatikana bila kukusanywa kwa kodi sahihi.

"Tunadai maji, huduma za afya, barabara nzuri, bila kukusanya na kulipa kodi haiwezekani tukayafikia haya malengo ya kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati" aliongeza Dkt. Kijaji

Kwa Upande wake, Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA Bw. Elijah Mwandumbya, amesema kuwa wafanyabiashara wasiotumia ipasavyo mashine za EFD watakabiliwa na adhabu kali inayofikia shilingi milioni nne na nusu kwa kutokutoa risiti huku mteja akikabiliwa na faini ya shilingi elfu thelathini kwa kutokudai risiti inayolingana na thamani ya bidhaa alizonunua.

"Ni kosa kuwa na mauzo ambayo hujayatolea risiti na ndio maana tunawapa fursa hii waweze kuweka kumbukumbu zao sawasawa kwa sababu tumegundua baadhi yao wanayo mauzo lakini hawajatoa risiti" aliongeza Bw. Mwandumbya.Bw. Mwandumbya ameeleza kuwa ukaguzi wao umeonesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya mashine za kieletroniki zinafanyakazi ipasavyo baada ya kutengemaa kwa mfumo wa kuchakata taarifa za mauzo kwa njia ya kieletroniki uliopata hitilafu tangu Mei 11 mwaka huu na kusababisha baadhi ya mashine hizo za EFD kutofanyakazi.

Aliwataka wafanyabiashara kuingiza mauzo yote waliyoyafanya katika kipindi chote ambacho kulikuwa na hitilafu ya kimfumo katika mashine ya EFD na kutoa risiti moja ya mauzo hayo ili yaweze kutambulika katika mfumo wa mapato wa TRA kwa ukadiriaji sahihi wa kodi za biashara zao.

AZAM KUMPELEKA NGOMA AFRIKA KUSINI KWA AJILI YA MATIBABU

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii

MCHEZAJI Donald Ngoma aliyesaini na timu ya Azam FC kwa mwaka mmoja akitoke Yanga SC anatarajiwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu yake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo Jaffary Iddy amesema Ngoma ataambatana na Dk. Mwanandi ambaye ndiye mkuu wa kitengo cha afya Azam FC kuelekea mji wa CaptTown kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya St Parot.

Amefafanua wataondoka ya saa 9:45 usiku wa leo kwa kutumia usafiri wa Shirika la Ndege la Kenya Airways.“Uongozi wa Azam unampeleka mchezaji huyo katika matibabu kwa kuwa wanaamini ana uwezo na atatoa mchango mkubwa katika klabu yetu,”amesema.

Mchezaji huyo raia wa Zimbawe alisajiliwa na matajiri hao wa chamazi akiwa majeru wa muda mrefu mpaka kupelekea kutokufanya vizuri msimu mzima uliopita kwa wajiri wake wa zamani Yanga SC.

Jaffary Iddy amesema Ngoma atafanyiwa matibabu ya vipimo vya afya yake kwa gharama zozote.

"Mchezaji huyu akikutwa na ugonjwa atatibiwa kwa gharama zozote ilimradi apone na kucheza na ikionekana hana tatizo lolote atarudi Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza mkataba mnono zaidi na kuitumikia Azam FC kwa muda mrefu katika Ligi Kuu Tanzania Bara,"amesema Jaffary.
Mchezaj Donald Ngoma aikiwa katika Jezi za waajiri wake wa zamani YangasSc.

KIGWANGALLA AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA KARIBU/KILI FAIR 2018

$
0
0
Na Hamza Temba-WMU-Moshi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa taasisi za Serikali, jamii, sekta binafsi na wadau kwa pamoja kushirikiana kuendeleza utalii katika maeneo yao ili sekta hiyo iweze kunufaisha zaidi taifa kwa kiwango kinachostahiki kuliko ilivyo hivi sasa.

Ametoa wito huo juzi katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi wakati akifungua maonesho ya kimataifa ya utalii ya Karibu/Kili Fair 2018 ambayo yameshirikisha makampuni na wadau wa utalii zaidi ya 350 kutoka nchi zaidi ya 12 duniani huku na kuvutia watu zaidi ya 4,000 kuyatembelea.

Amesema ushirikiano huo utaiwezesha sekta hiyo kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa ambao kwa sasa ni takriban asilimia 17.2 ya pato la Taifa, zaidi ya asilimia 24 ya mapato yote ya fedha za kigeni sambamba na zaidi ya asilimia 10 ya ajira zote nchini.

Amesema mchango huo bado ni mdogo ukilinganisha na aina na idadi ya vivutio vilivyopo hapa nchini.Dkt. Kigwangalla amesema Serikali ya awamu ya tano imeshaanza kuchukua hatua mbalimbali zitakazosaidia kuboresha sekta hiyo ikiwemo ujenzi unaoendelea wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, ujenzi wa Terminal 3 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Saalam na uboreshaji wa Shirika la Ndege la ATCL.

Pamoja na hayo amesema Serikali kupitia wizara yake inaendelea na mpango wa kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini ili kuongeza idadi ya watalii na mapato ambapo Mapori matano ya Akiba mkoani Kagera na Geita yatapandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa (Burigi, Biharamulo, Kimisi, Ibanda na Rumanyika).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mst. Thomas Mihayo (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 kabla ya kuzindua maonesho hayo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kilifair Promotion, Tom Kunkler (kushoto).
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Devotha Mdachi wakiwa katika meza kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Ltd,Tom Kunkler, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mkurugenzi wa Karibu Fair, Dominick Shoo na viongozi wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na viongozi wengine wa Serikali na sekta binafsi wakiwa kwenye eneo la mfano wa kilele cha Uhuru cha mlima Kilimanjaro baada ya kuzindua Maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Karibu/Kili Fair 2018 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
Waziri Kigwangalla akisalimia baadhi waoneshaji katika banda la utalii wa kiutamaduni kwenye maonesho hayo.

ABIRIA MIKOA YA KUSINI WALIA USUMBUFU WANAOUPATA KITUO CHA MABASI MBAGALA

$
0
0

*Ni baada ya mabasi ya Mashallah, Ngombare kuhamishwa kituo namba 21

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ABIRIA wanaosafiri kwenda katika mikoa ya Kusini hasa Mkoa wa Lindi na Mtwara, wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa hatua zake za kuhamisha huduma za usafiri wa mabasi ya Kampuni ya Mashalaah kutoka kituo Namba 21 kwenda kituo Namba 48 vilivyopo eneo la Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya kuhamishwa kwa mabasi hayo kumesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaotumia mabasi hayo na sasa wanaomba halmashauri hiyo kutafakari upya uamuzi huo.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la kituo namba 21 na baadae katika kituo namba 48 jijini Dar es Salaam, abiria hao walisema kitendo hicho pamoja na mambo mengine, kimekuwa kikiwasababishia baadhi yao kupoteza mizigo na wakati mwingine kulazimika kutumia fedha za ziada kwa ajili ya kukodi piki piki na hata mikokoteni kuyafuata mabasi hayo katika kituo Namba 48, ambacho kipo mbali na neo la Barabara Kuu mahali walipokuwa wakipandia hapo awali.

Abiria hao akiwemo Mustafa Salehe, alisema kubadilishwa kwa utaratibu wa mabasi hayo kutoka kituo namba 21 kwenda kituo namba 48, kumesababisha changamoto kubwa kwa mamia ya abiria hasa wale wanaotumia kituo hicho cha Mbagala, eneo ambalo ndilo linalotumika kama kituo kikuu cha daladala kutoka maeneo mbalimbali ya mji. “Zamani ulikuwa ukishuka hapa kutoka mahali popote ndani ya mji huu, moja kwa moja unaingia katika basi kuendelea na safari yako, lakini kwa sasa inashangaza kuona huduma hiyo imeondolewa tena kwa baadhi ya mabasi, suala linaloleta wasiwasi kuwa pengine kuna mgogoro unaoendelea baina ya uongozi na wamiliki wa mabasi hayo” alisema Salehe.

Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwanakopa Hassan, mbali na kudai kushangazwa na hatua hiyo, alisema hali ya usafiri katika kituo hicho imekuwa ya kutoeleweka kutokana na mkanganyiko unaojitokeza mara kwa mara mahali hapo. “Hapo zamani tulikuwa tunapandia kituo hiki kikubwa cha daladala cha Rangi tatu( kituo namba 21), baadae tukahamishwa tena kwenda huko mitaani(Namba 48),

“Lakini kabla hatujakaa vizuri huduma zikarudishwa tena eneo la mara ya kwanza, na sasa wamezipeleka tena huko huko mitaani, jambo ambalo sisi kama abiria linatuchanganya ikizingatiwa siyo kila mtu mwenyeji wa mji huu” alisema Mwanakopa .Kwa mujibu wa abiria hao, huduma hizo za usafiri zimehamishwa kituo hicho kwa kampuni mbili za mabasi ambazo ni Ngombale pamoja na Mashallah, huku mabasi mengine yakiachwa jambo lililotoa tafsiri kwa abiria hao kuwa pengine linatokana na mgongano wa kimaslahi baina ya watoa huduma hao, uongozi wa manispaa pamoja na wasimamizi wa huduma za usafiri.

Walipotafutwa kuthibitisha suala hilo, Uongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA)ulisema hali hiyo inasababisha manyanyaso kwa abiria hao na unatokana na kiongozi Ofisa mmoja wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke pamoja na kiongozi kutoka Manispaa ya Temeke, na suala hilo wanalifuatilia. “Inashangaza kuona kila siku ni kampuni hizi hizi mbili ndiyo zinayumbishwa pale katika eneo la kutoa huduma, kuna tatizo gani, nini kimejificha..kwa taarifa tulizozipata wapo watu wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, jambo ambalo sisi kama uongozi wa wasafirishaji hatuwezi kulifumbia macho” alisema Katibu Mkuu wa TABOA Enea Mrutu.

Kwa upande wa uongozi wa mabasi hayo umesema kuwa unasikitishwa na hali inayoendelea dhidi yao na kufafanua kwa sasa wanasubiri haki itendeke baada ya kupeleka malalamiko yao maeneo husika huku wakidai kuna baadhi ya maofisa wa halmashauri na polisi kikosi cha usalama barabarani ambao wanawafanyia hujuma za kibiashara.

1: Baadhi ya abiria wakipakia mizigo yao kwenye basi la Mashaalah baada ya kuletwa kwenye mikokoteni kutoka kituo namba 21 kuja kituo namba 48 ambacho kinalalamikiwa na abiria kuwa kimewasababishia usumbufu.
Mmoja wa abiria wa basi la kampuni ya Mashalaah(aliyevaa fulana nyeusi) akitoa malalamiko yake kutokana na adha ambayo wanaipata tangu kuhamishwa kituo namba 21
Mizigo ya abiria ikitolewa kituo cha mabasi namba 21 kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam ikiwa kwenye mkokoteni kwa ajili ya kupelekwa kituo namba 48.
Baadhi ya abiria wa basi la Mashalaah wakiwa wamekaa nje ya ofisini ya basi hizo wakisubiri mizigo yao ipakiwe kwenye mikokoteni ili kufuata basi linakoegesha baada ya kuondolewa kituo namba 21 ambacho ndicho kituo kwa ajili ya abiria wanaokwenda mikoa ya Kusini na kupelekwa kituo namba 48.

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI ELIMU YA JUU YASITISHA MPANGO WA KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA (DIPLOMA)


BUJORA DANCE GROUP WAREJEA NCHINI KWASHANGWE

$
0
0
Na Agness Francis,Globu ya Jamii.

KIKUNDI cha  ngoma cha Bujora Dance  kililokwenda Nchini India katika tamasha la michezo ya asili Afrika kimerejea nchini. 

Kundi hilo lililofanya vizuri zaidi katika mashindano ya Tulia Traditional Dances Festival 2018  ambao waliibuka kuwa ndio washindi limeifanya Tanzania kuwa kivutio huko nchini India.

Ambapo kundi hilo kutokea mwanza Mei 25 mwaka huu ndio lilianza kufanya kazi hiyo ya michezo  asili ya Mtanzania ambapo waliifanya nchi yetu kuwa kivutio katika tamasha la hilo iliyoshirikisha nchi nane  lenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kitamaduni.

Kiongozi wa msafara huo Hassan Ngoma amesema kuwa  tamasha hilo lililokonga nyoyo za watu wengi sana  lilifanyika katika miji mitatu  New Delhi, khairagah pamoja na Chandigarh huko nchini India.

Ambapo Usiku wa May 27 heshima nyingine ya Tanzania ilitengenezwa katika mji wa Chandigarh nchini hapo huku kundi  hilo la ngoma za asili  walionyesha tena uwezo wao katika tamasha hilo.

Ngoma amesema usiku wa Mei 30 ndio walihitimisha kufanya maonyesho yao  katika tamasha hilo la wiki ya Afrika ambapo walimalizia kwa kutoa burudani ya uhakika katika mji wa Khairagarh wakiwa ndio waalikwa pekee katika mji huo.

"Imekuwa fursa nzuri kwetu ya kuitangaza tamaduni ya kitanzania kwa nchi mbali mbali lilitoshiriki tamasha la michezo ya asili Afrika" amesema Hassan Ngoma.

 Kiongozi wa msafara Hassan Ngoma(katikati) akiwa pamoja na wanakikundi cha Ngoma cha Bujora cha Mkoani  Mwanza wakiwa wamewasili kutoka Nchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.
Kikundi cha Bujora kikiwa kimewasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakitokeaNchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti. 

MOTO WATEKETEZA MADUKA NANE LAMADI MKOANI SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Moto ambao hadi sasa chanzo chake hakijafahamika umeteketeza maduka nane , stoo pamoja na mali za wafanyabiashara ambazo thamani yake haijafahamika, katika Mji mdogo wa Lamadi wilaya ya Busega Mkoani Simiyu , usiku wa tarehe 02 Juni.

Akizungumzia jinsi moto huo ulivyoanza mmoja wa wakazi wa Lamadi aliyeshuhudia tukio hilo, Bw. John Balele amesema moto ulianza kuwaka katika moja ya chumba cha duka majira ya saa mbili usiku na baadaye ukaanza kusambaa katika vyumba vingine lakini hawakuweza kufahamu chanzo chake maana vyumba vyote vilikuwa vimefungwa.
“Huu moto umetokea majira ya saa mbili hivi tulivyouona tukapiga simu polisi, askari polisi wakaja na askari wa zimamoto, Zimamoto wamejitahidi kuwahi kufika na wametusaidia sana kutuelekeza namna ya kukabiliana na moto huu tukafanikiwa kuuzima na kuokoa baadhi ya mali japo mali nyingi zimeteketea lakini hakuna mtu aliyedhurika; binafsi nawashukuru sana wananchi wenzangu wa Lamadi kwa moyo wao wa kujitolea” alisema John Balele.

Diwani wa kata ya Lamadi, Mhe. Laurent Bija amewashukuru wananchi kwa namna walivyojitoa kushirikiana na jeshi la polisi na kikosi cha Zimamoto na uokoaji katika kuukabili moto huo na kulinda baadhi ya mali zilizookolewa kwa uaminifu .

Aidha, Diwani huyo ametoa pole kwa wafanyabiashara ambao mali zao zimeteketea na akatoa wito kwa wafanyabiashara wote katika Kata hiyo kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika maeneo yao ya biashara, ili viweze kuwasaidia katika hatua za awali za kukabiliana na moto pindi unapotokea.

Akizungumza wananchi wa Lamadi waliojitokeza kuzima moto huo wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Polisi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapa pole wafanyabiashara ambao wamepoteza mali zao katika ajali hiyo ya moto na akawashukuru wananchi wa Lamadi kwa ushirikiano na uaminifu waliounesha wakati wa kuzima moto huo.
Mtaka amesema kwa kuwa chanzo cha moto huo hakijafahamika Serikali kupitia TANESCO na Zimamoto itaendelea kutafuta na kubaini chanzo na tarehe 03 Juni, 2018 Serikali itafanya tathmini kujua madhara yaliyosababishwa na moto huo.

“ Nawapa pole wananchi wa Lamadi bado hatujajua chanzo hasa, wenzetu wa TANESCO na Zimamoto watatusaidia kujua chanzo, kuhusu madhara kwa kuwa sasa ni usiku kesho Serikali itafanya tathmini ili na sisi tuone namna ya kuzungumza na wenzetu wa benki na kuona busara gani itumike kuwasaidia wafanyabiashara waliokopa namna ya kurejesha, wakati wanajipanga upya” alisema

Mkuu huyo wa Mkoa pia ametoa wito kwa Taasisi za Bima hapa nchini kupanua wigo na kuwafikia wafanyabiashara na kuona namna sahihi ya kuwa msaada kwao pale wanapokutana na majanga yasiyoepukika yakiwemo ya moto, huku akisisitiza wafanyabiashara kuchukua tahadhari ya moto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vifaa vyote vya umeme vimezimwa wanapofunga biashara zao. 
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya majanga ya moto hasa kwenye maeneo ya masoko ili waweze kuchukua tahadhari ya moto na akawataka wale wanaojenga majengo ya biashara kupata ushauri wa kitaalam juu ya ujenzi wa majengo yao

Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Simiyu, Gervas Fungamali amesema Jeshi la polisi litaendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani juu ya umuhimu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto na kuchukua tahadhari ya moto katika maeneo yao.

SEKTA YA UFUGAJI SAMAKI INAKUA, ITASAIDIA KUONGEZA KIPATO-ULEGA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema sekta ya ufugaji samaki inakua na inasaidia katika kuongeza ajira na kipato kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na hiyo ni kutokana na ubora wa samaki wanaozalishwa nchini.

Ulega ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kutembelea Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Mbegani, shamba la ufungaji wa samaki la NFCO Ruvu,Ruvu fish farm Mlandizi,Kiwanda cha kuzaliza chakula cha kuku na samaki,Hill feeds Mapiga,wakulima wa Mwani Bagamoyo Milingotini.

Aidha amesema vijana wengi wanamaliza vyuo na kukosa ajira, hivyo wataboresha sekta hiyo ili kuongeza ajira kwani biashara ya samaki inalipa na kwa kasi iliyopo Taifa na wananchi watapata kipato kikubwa.

Akizungumzia kuhusu kutopatikana kwa vifaranga Ulega ameeleza wamejipanga katika kutatua tatizo hilo hasa katika kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika vituo vya uzalishaji wa vifaranga vya samaki kama Luhila Songea na Nyegezi mkoani Mwanza.

Pia amesema changamoto ya chakula cha samaki imetatuliwa na baada ya kutembelea kiwanda cha chakula cha Hill Package kilichopo Mpinga Bagamoyo ameridhika na utendaji na uzalishaji wa chakula cha samaki katika kiwanda hicho. Hivyo amewashauri wafugaji kutumia chakula kutoka katika kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa na badala ya kuagiza chakula kutoka nje ya nchi.

Ametoa mwito kwa wananchi kushirikiana na Serikali kutokomeza uvuvi haramu ili kuongeza kipato kwa wavuvi na taifa kwa ujumla. 
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia akiangalia sabuni pamoja na mafuta ya kupaka yanayotengenzwa na zao la Mwani katika kijiji cha Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kulia) akimsikiliza Mmiliki wa Shamba la kufugia samaki,Khumbo Kathenga
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiangalia vyakula vya kuku na samaki vinanyo zalishwa na kiwanda cha  Hill feeds kilichopo Mapiga mkoa wa Pwani.

Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kushoto) akizungumza na wamiliki wa shamba la samaki lilipo Ruvu mkoa wa Pwani.

Wanachama kuogelea wapitisha Katiba mpya

$
0
0
Dar es Salaam. baada ya kusua sua kwa muda mrefu, hatimaye Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) kimepata katiba mpya itakayo waongoza katika mchezo huo hapa nchini.

Katiba hiyo imepatikana katika mkutano mkuu uliotishwa na Kamati ya Muda ya TSA iliyoteuliwa na Baraza la Michezo nchini (BMT) hivi karibuni.
Katika Mkutano huo uliosimamiwa na BMT, wanachama kutoka klabu mbalimbali nchini walipitisha mabadiliko hayo ambayo kwa mujibu wa katiba ya sasa, Zanzibar haitashiriki katika masuala ya uchaguzi kama ilivyokuwa zamani.

Katiba ya zamani iliruhusu wanachama kutoka Zanzibar kushiriki katika uchaguzi na masuala mengine, jambo ambalo ilikuwa tofauti na michezo mingine kama mpira wa miguu, netiboli na mingineyo.

Hata hivyo, kutokana na hali ya mchezo wa kuogelea nchini kutokuwa na vyama vya mikoa na wilaya, ushiriki wa Zanzibar katika shughuli za TSA utakuwepo kupitia habibu za rejea (MoU) baina ya Kamati ya Utendaji ya TSA na Kamti ya Utendaji ya Chama Cha kuogelea cha Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa TSA, Imani Dominick amesema kuwa wamefarijika sana kukamilisha zoezi hilo lililokuwa gumu na vipingamizi vingi kutoka kwa watu ambao hawakuwa wakitaka kukamilisha zoezi hilo.

Dominick alisema kuwa baadhi ya wadau walipinga waziwazi pamoja na kusambaza ujumbe kuwa Kamati yetu siyo halali kwa lengo la kupotosha pamoja na ukweli kuwa BMT ndiyo iliyowaidhinisha kushika nyadhifa hizo baada ya wanachama kuwapitisha katika mkutano halali uliofanyika shule ya Kimataifa ya Tanganyik Upanga.

“Naomba niwapongeze kwa kazi kubwa mliyoifanya kuokoa mchezo wa kuogelea, pia nawashukuru wanachama kwa kuitikia wito wa kuijadili na kuipitisha Katiba mpya, huu ni muongozo wa kisasa na tunaamini tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa,”alisema Dominick.Pia aliwahasa wanachama walioshindwa kuhudhuria mkutano huo kutofanya hivyo tena kwani maendeleo ya mchezo yanahitaji mchango wao kubwa kwani chama si cha watu wachache zaidi ya vilabu, waogeleaji na wanachama.

Afisa Michezo wa BMT, Benson Chacha naye aliwashukuru wanachama hao kwa kufanikisha zoezi hilo na kuwaomba kujikita zaidi katika kuuendeleza mchezo huo na kuachana na masuala ambayo yatarudisha nyuma mchezo huo.“Mmefanya kazi vizuri sana kukamilisha zoezi hili ambalo lililkuwa gumu sana, mmefanya kazi kubwa na ya kupongezwa, sasa mnatakiwa kujikita zaidi kwenye maendeleo ya mchezo, BMT itawapa ushirikiano mzuri sana,” alisema Chacha.

Baadhi wa wajumbe wa Kamati ya Muda na Wanachama wa chama cha kuogelea nchini (TSA) wakiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Baraza la Mchezo nchini (BMT) mara baada ya kupitisha Katiba mpya.

DKT: DKT ABBASI: HII NDIYO MIRADI MIKUBWA YA MKAKATI WA MAGEUZI SEKTA YA NISHATI

KIJANA WA SAUDIA ASHINDA DOLA 5,000 TUZO YA KIMATAIFA YA KUHIFADHI QURAN

$
0
0
KIJANA wa miaka 18 kutoka Saudi Arabia, Ibn Rayizah Hatim Abdullah ameibuka na kitita cha dola za Marekani 5,000 kwenye fainali za 26 za tuzo ya Kimataifa ya Quran tukufu.

Kijana Rayizah ameibuka na kitita hicho baada ya kuwashinda wenzake sita waliofanikiwa kuingia fainali hizo ambao walitoka Yemen, Zanzibar, Malaysia, Mali, Marekani na Tanzania Bara.

Nafasi ya pili imechukuliwa na kijana Hamza Soukouna (25) kutoka Mali ambaye amejishindia dola za Marekani 4,000 na ya tatu imechukuliwa na Hamza El-Habashiy (18) kutoka Marekani ambaye amejishindia dola za Marekani 3,000. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, mwaka huu yalishirikisha vijana 16 kutoka nchi 16 duniani.

Akizungumza na mamia ya waumini wa Kiislamu waliofurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo mchana (Jumapili, Juni 3, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini hiyo waendelee kuwakamata vema vijana waliohifadhi Quran na kuwaendeleza kitaaluma katika fani nyingine za elimu ya kimazingira.

“Leo hii nimefarijika sana kusikia kwamba tunao vijana wetu ambao si tu wamehifadhi Quran bali pia wamehitimu fani mbalimbali katika elimu ya juu. Uwepo wa vijana wa namna hii ni muhimu katika kujenga jamii bora na yenye kuzingatia uadilifu katika kutekeleza majukumu yao,” amesema.

Amesema kazi ya kuhifadhisha Quran haiishii katika kujua kuisoma pekee. “Kuhifadhisha Quran kunapaswa kuwa msingi imara katika kujenga jamii bora kupitia mafunzo sahihi ya tabia njema, utii lakini pia kujua mipaka katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia vijana hawa tunaowahifadhisha Quran kuwa raia wema, wazalendo, wanaotambua wajibu wao, majukumu yao, kwao wenyewe na kwa nchi yao pia,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubary Zubeir (kulia) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo (watatu kulia) wakiwa na washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tanzania baada ya Waziri Mkuu kuwakabidhi washindi hao zawadi zao kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza Ibn Rayizah Hatim Abdullah wa Saudi Arabia, Mshindi wa pili Hamza Soukouna kutoka Mali na Mshindi wa tatu Hamzah El- Habashiy kutoka Marekani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi waliofika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambako Mheshimiwa Waziri Mkuu alikabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania, Juni 3,2018. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Mwenyekiti wa Haj Trust Fund, Sheikh, Swaleh Misky, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt, Mohammed Bilal, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir kabla ya kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es salaam, Juni 3, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-aan Tanzania, Sheikh Othman Kaporo (kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salum (wapili kulia) baada ya kukabidhi Tuzo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Tanzania kwenye  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MAONESHO YA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI BUSTANI YA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM


MICHUZI TV: DC HAPI ATOA ONYO KWA WAFANYAKAZI HALMASHAURI

TCCIA YAANZA KUSHEREKEA MIAKA 30 YA KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
Raisi wa TCCIA Bwana John Mayanja, akizungumza na wajumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa ambao ni wanachama wa TCCIA.

Chama cha wenye Biashara, Viwanda na Wakulima ‘TCCIA’ jana kimezindua rasmi safari ya kusherekea mafanikio makubwa waliyoyapata katika miaka 30 tangu kuanzishwa kwake. Wanachama pamoja na viongozi wa TCCIA jana walikutana kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ambao ulifanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mbalimbali yaliyotungumzwa katika mkutano huo, kulifanyika uzinduzi rasmi wa kusherekea mafanikio makubwa ya TCCIA.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group Bw. Imani Kajula ambae ni mshauri wa masuala ya masoko, Alisema ‘Huwezi kuongelea Uchumi wa nchi bila kutaja kazi kubwa iliyofanywa na TCCIA hasa katika kuleta msukumo mkubwa kwenye uboreshwaji wa sera mbalimbali ambazo zimesaidia katika kukuza Uchumi wetu. Miaka 30 hii ni hatua kubwa sana kwa shirika la kizalendo lililowakutanisha watu mbalimbali kutoka katika kada za Biashara, Uchumi pamoja na Kilimo na kuweza kukaa pamoja kwa maslahi mapana ya nchi yetu’

Pamoja na ufunguzi huo, mkutano huu pia kutoa fursa kwa Rais wa TCCIA Bw. John Mayanja kuweza kutoa taarifa rasmi ya kipindi cha Oktoba 2017 hadi Mei 2018. Akiongea katika mkutano huo aliwasihi wafanya biashara wote kuweza kutumia jukwaa hilo kuongea na serikali ili kuweza kupata majawabu ya pamoja yatakayoibua fursa zaidi za uwekezaji nchini, ‘serikali yetu ni sikivu, ni lazima sisi tuiambie tunataka nini kwa sauti yetu moja’ alisema Rais Mayanja. 
Wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya Taifa pia walipata nafasi ya kusomewa Taarifa ya Mwaka 2017, taarifa ya fedha kwa kipinndi cha Jauari – Machi 2018 pamoja na kuchagua wajumbe.

WATANZANIA WATAKIWA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA

$
0
0

WATANZANIA wametakiwa kujiunga na mpango wa bima a Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu ya uhakika wakati wanapokuwa wakiugua na hivyo kuwapunguzia mzigo wa kuingia gharama kubwa.

Hayo yalisemwa leo na Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hawa Duguza wakati akizungumza kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya biashara ya kimataifa.

Licha ya mfuko huo kutoa elimu juu ya umuhimu wa mpango wa bima lakini pia wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa afya na kutoa ushauri kwa wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesha hayo.

Alisema mpango wa bima ni mzuri kutokana na kuwapa uhakika wa matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali na hivyo ni muhimu kujiunga nao ili waweze kuona manufaa makubwa wanayoweza kuyapata.

Aidha pia aliwahamasisha kujiunga na mpango wa kikoa na toto Afya kadi ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuweza kupata huduma nzuri kipindi ambacho wanapatwa na changamoto za kuugua hususani watoto wadogo wakati wa ukuaji wao.
Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis David akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kwenye banda lao  lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifaKatibu tawala mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akipima afya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Hillary Ngonyani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kushoto ni Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Korogwe Jumanne Shauri kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa Duguza
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens kulia akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kupata elimu ya mpango wa kujiunga na bima ya AfyaKatibu Tawala wa mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akiwa na tisheti akijiandaa kuwapa watoto zawadi wakati alipotembelea banda hilo kushoto Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) .


KWA NINI NI LAZIMA UFANYIWE MASSAGE?

$
0
0
Massage ni tiba ya asili na ya kitaalamu yenye uwezo mkubwa wa kuufanya Mwili wako kuwa Imara Kiafya

Faida za Massage Katika Mwili
1. Massage inaboresha afya ya ngozi.

2.Massage hufungua mishipa ya fahamu na kuongeza uwezo wa kufikiri.
3. Massage husafisha ngozi na kuboresha mfumo wa utoaji takamwili.
4. Massage Inaondoa kovu la jeraha.
5. Massage husaidia kupona kwa wenye mivunjiko ya viungo/ mifupa.
6. Massage huondoa uchovu wa mwili na kukosa usingizi.
7. Massage huzuia kansa ya ngozi na tishu.
8. Massage huzuia Saratani ya Matiti.
9. Massage huondoa maumivu ya wakati wa hedhi.
10. Massage huboresha mmeng'enyo wa chakula na kuzuia Constipation (choo ngumu).
 11. Massage hupunguza maumivu ya uchungu kwa wamama wajawazito.
12. Massage huondoa uchovu na kuvimba kwa miguu kwa wamama wajawazito.
13. Massage huimarisha mifupa kwa kuchochea ufyonzwaji wa Madini ya Kalsiam(Calcium) na Fosforas.
14. Massage huboresha mzunguko wa damu mwilini.
15. Massage husaidia kuondoa maumivu ya misuli na majeraha.
16. Massage huchochea ufanyaji kazi wa homoni mwilini.
17. Massage huzuia Stroke/ kiharusi.
18. Massage inasaidia sana kwa wazee kuimarisha misuli na kuwapa nguvu ya kutembea.
19. Massage huondoa maumivu ya chini ya mgongo.
20. Massage husaidia kuboresha mfumo wa limfu (lymphatic system)

🌹 KARIBU UBORESHE AFYA YAKO NA HAPPINESS MASSAGE! 🌹

 Tunapatikana: Lamada Hotel-Manyara 27,
Ilala Dar Es Salaam.

Simu / WhatsApp
📞 0787 343 161
📞 0756 343 161

Fanya booking mapema ili tukuhudumie kwa wakati

Happiness Massage Tunaboresha Afya yako na kurejesha Furaha yako

WANAKIJIJI 772 WA KIJIJI CHA MLANDA WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA 1,777

$
0
0
NA FREDY MGUNDA.IRINGA.

JUMLA ya wanakijiji 772 kati ya 1890 wa kijiji cha Mlanda kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamepimiwa maeneo na mashamba yao na kukukabidhiwa hati miliki za kimila zinazotolewa kupitia Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Hati hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya wakati wa sherehe fupi za kuwakabidhi hati hizo zilizofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi na wageni mbalimbali walikuwepo katika tukio hilo.

Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo Masunya alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.

Masunya aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Masunya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye ni mlemavu 
Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda wakati wa kutoa hati za kimila 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye alikuwa anawakilisha kundi la wazee
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushirikia zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila zilizotolewa na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID),viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na baadhi ya wananchi walikuwa tayari wamepokea hati za kimila.



Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images