Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amteua Jaji Wambali na Jaji Kwariko kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani


MAMA YAKE MZAZI HUSSEIN BASHE AZIKWA WILAYANI NZEGA LEO

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake mzazi aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Selukamba. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa mama yake mzazi mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyezikwa leo wilayani Nzega.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wa tatu kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla (wa sita nyuma kutoka kulia), Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (wa nne kulia), viongozi wengine wa chama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa wilaya ya Nzega wakishiriki kusalia jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) muda mfupi kabla ya kupelekwa makaburini kwa ajili ya maziko wilayani Nzega leo.
 Jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) likiondolewa kwenye eneo la makaburi kupisha mwili huo kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milelel (kaburini) wilayani Nzega leo.
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele yake kulia) na viongozi wengine wa vyama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Nzega wakishiriki kumzika mama yake mzazi, Hussein Bashe katika makaburi wilayani humo leo.

MAVUNDE AWAOMBA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Peter Mavunde amewaomba waamini wa Dini ya kiislamu kuliombea Taifa,Rais Dk.John Magufuli na Viongozi wote wa Serikali ya awamu ya Tano ili waweze kutimiza majukumu yao kwa Haki na Usawa na kuendelea kuwahudumia Watanzania wanyonge.

Mavunde ameyasema hayo leo katika Masjid Gaddafi alipokuwa akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini ambapo Mbunge huyo amegawa Speaker 20 za misikitini,mikeka,mabusati,Mifuko ya Saruji,matofali,tende,maboksi matano ya Juzuu & Misahafu,Jezi,Mipira vyote vyenye thamani ya Tsh 15,000,000 na fedha taslimu kwa Tsh 1,000,000 kwa kikundi cha Vijana cha UWAZAM na kuwataka wanufaika wa Vifaa hivyo kuvitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

“Rais wetu pamoja na viongozi wetu wakuu wanafanya kazi nzuri sana ambayo inapaswa kuungwa mkono,tuliombee Taifa na Viongozi wetu ili waendelee kututumikia na kutatua changamoto zetu”Alisema Mavunde.

Aidha akimkaribisha Mh Mavunde,Sheikh wa Mkoa Wa Dodoma Al-ahi Sheikh Mustafa Rajab amemshukuru sana Mbunge Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na Waislamu na kuwataka waamini wa Dini ya Kislamu kumuombea na kumpa ushirikiano muda wote.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza alipokuwa akikabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini
Vifaa mbalimbali vilivyokabishiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde kwa ajili ya misikiti ya Jimbo hilo.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya misikiti ya Jimbo la Dodoma Mjini Shekhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab
Shekhe wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab akizungumza katika Hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya misikiti ya Dodoma.
Waumini wakiwasikiliza viongozi mbalimbali

HABIB HAJI KYOMBO RASMI ASAINI KANDARASI YA MIAKA MITATU SINGIDA UNITED.

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Aliyekuwa Mshambuliaji wa timu ya Mbao FC msimu uliopita, Habib Kyombo leo amesaini mkataba wa miaka mitatu na Singida United.

Kyombo ambaye ameitumikia Mbao FC kwa mwaka mmoja na nusu alifanikiwa kufunga mabao 16 kwenye mashindano yote aliyocheza akiwa na timu hiyo. 

Ujumbe wa shukrani aliondika kupitia mtandao, amesema anawashukuru Mbao FC na mashabiki wake, kwa kusema kuwa tangu amevaa Jezi ya timu hiyo  walimpa sapoti yakutosha. 

Bila kusahau amemshukuru, Aliyekuwa Kocha wa timu ya Mbao, Ettiene Ndayirajige kwa imani yake nakuonyesha kumuamini katika nafasi ya ushambuliaji ambao imesaidia kumsogeza karibu na ndoto zake. 

Amesema hatosahau na itabaki kumbukumbu kwake baada yakuisaidia timu hiyo kufika Fanali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) msimu uliopita ambapo walipoteza kwa kichapo cha bao 2-1 mbele ya Simba SC.

RAIS MAGUFULI KUZINDUA PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ASDP II)

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) tarehe 4 June 2018.

Katika dhifa hiyo inayotarajiwa kuanzia Saa 2.00 asubuhi katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Rais Magufuli ataambatana na wageni wengine wa kitaifa na kimataifa akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dara es salaam Mhe Paul Makonda, Mawaziri wa sekta za kilimo pamoja na wadau wote wa sekta hiyo.

Taarifa ya uzinduzi wa Programu hiyo ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini imetolewa jana 1 June 2018 na waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.

Dkt Tizeba alisema, Wizara za kisekta zikijumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ndizo zenye jukumu la kuhakikisha ASDP II inakuwa na mafanikio makubwa nchini na kuwa mkombozi wa wananchi katika kilimo.

Alisema kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa miaka kumi (10) kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ambapo kipindi cha kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24. 

Katika hatua nyingine Dkt Tizeba ametaja lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi; kuongeza pato la Taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na lishe. 

Aidha, Programu hii itatekeleza sera mbalimbali kama vile Sera ya Kilimo ya Taifa, Sera ya Mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa Chakula na Lishe, Sera ya Ugatuaji Madaraka, Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sera ya Mashirikiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi.

Katika hatua nyingine Mhe Dkt Tizeba ameuarifu umma wa watanzania kuwa endapo mpango huo utatekelezwa kama ilivyopangwa hadi kufikia mwaka 2022 Tanzania itakuwa katika uchumi wa kati.Katika utekelezaji wa ASDP II washiriki ni wadau wa sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Ushirika, Wizara, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na wananchi wote.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP II) katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, jana 1 June 2018. Wengine ni Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Dkt. Thomas kashililah. Picha zote Na Mathias Canal-WK
Wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018.
Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kulia), Mratibu wa ASDP II Mhandisi Januari Kayumbe (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa zana za kilimo Mhandisi Joseph Lubilo wakifatilia mkutano wa waziri wa kilimo na waandishi wa habari. Jana 1 June 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati wa maandalizi ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo ASDP II katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018.

WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUUNDA VYAMA VYA USHIRIKA

$
0
0
Angela Msimbira OR-TAMISEMI


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege  amewaagiza wafugaji nchini kuunda  vyama vya ushirika imara ambavyo vitawezesha  kupata huduma za mifugo na kuboresha ukusanyaji na masoko ya maziwa. 



Mhe Kandege ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maziwa iliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nanenane, Themi Mkoani Arusha Mhe. Kandege amesema uwepo wa ushirika imara utaboresha ukusanyaji wa  maziwa kwa wingi kwa ufanisi zaidi na hatimaye  kuongeza kiasi cha usindikaji kwa viwanda. 



“Napenda kutoa pongezi kwa wafugaji wa Mikoa ya Tanga na Njombe kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mafanikio yanayoonekana katika kuendeleza tasnia ya maziwa kupitia ushirika” Amesema Kandege.Amesisistiza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na idara zake nchini kuhakikisha zinawezesha uundwaji wa vyama vya ushirika imara na pia wanaimarisha vyama vya ushirika vilivyopo.

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Joseph Kandege akikagua moja ya machine inayotumika katika usindikaji wa maziwa kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akikabidhiwa maziwa kwa ajili ya shule mbalimbali katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akiwa na baadhi ya viongozi wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye  kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kandege akiongea na wadau wa ufugaji katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maziwa kilichofanyika leo katika viwanja Nanenane Themi, Mkoani Arusha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTIBWA SUGAR MABINGWA ASFC, WAIPIGA SINGIDA UTD 3-2.

$
0
0
Wakata miwa wa Morogoro Mtibwa Sugar wamefanikiwa kunyakua ubingwa wa mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2018 baada ya kuifunga Singida United.

Mtibwa imewachukua miaka 18 kunyakua ubingwa baada ya mara ya mwisho mwaka 2000 walipotawazwa ubingwa wa ligi kuu.

Mtibwa Sugar imefanikiwa kutwaa taji hilo la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Singida United. .

Mtibwa imewachukua miaka 18 kuchukua ubingwa kwa kuwafunga Singida United magoli matatu kwa mawili huku magoli ya Mtibwa sugar yakifungwa na Salum kihimbwa dk 22, Issa Rashidi dk 37 na Ismail mhesa dk ya 90 huku magoli ya Singida United yakifungwa na Chuku dk ya 43 na Kutinyu dk ya 71.
Picha na Mwaisabula.blogspot



PRECISION AIR YANG’ARA MAONESHO YA KARIBU KILI FAIR MOSHI

$
0
0

Waziri wa Mali Asili na Utalii Mh.Dkt.Hamisi Kigangwala akipokea maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa Precision Air Bw.Hillary Mremi , alipotembelea banda la Precision Air katika Maonyesho ya utalii Karibu/Kili Fair.
 Meneja Mauzo wa Precision Air Kanda ya Kaskazini, Bi.Lydia Kibonde akitoa maelezo kwa mmoja ya wageni waliofika katika banda la Precision Air katika maonyesho ya Karibu/Kili Fair yaliyofanyika mjini Moshi
Wateja wa Precision Air wakipata huduma katika banda la Precision Air katika maonyesho ya utalii Karibu/Kili Fair
 Timu ya Precision Air katika maonyesho ya utalii ya Karibu/Kili Fair Kushoto ni Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini Bi.Lydia Kibonde, Katikati Meneja Masoko and Mawasiliano Bw.Hillary Mremi and Afisa Mauzo Bi. Monica Massawe.





Balozi Wilson M. Masilingi atembelea Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing, Seattle, Jimbo la Washington, Marekani.

$
0
0

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akiwa na Bw. Kevin G. McAllister, Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing, Seattle, Jimbo la Washington, Marekani. Kampuni hiyo ya kutengeneza Ndege ya Boeing imedhamiria kuendelea kushirikiana na Tanzania kujenga Shirika la Ndege lenye Ndege za teknolojia ya kisasa

Kutoka kushoto ni Bw. Christopher M. Cook, Mkurugenzi wa Mauzo ya Kimataifa, (Business Director International Sales); Bw. Ihssane Mounir, Naibu Rais wa Mauzo (Senior Vice President Commercial Sales & Marketing); Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi; Bw. Kevin G. McAllister,  Mkurugenzi Mwandamizi (President & CEO Boeing Commercial Airplanes) na Bw. Alfred Swere, Mwambata Fedha wa Ubalozi

Daily News Digital: AFYA YAKO - Mambo ya kufahamu maambukizi ya Ebola Afrika

OPERESHENI YA POLISI YANASA WATU 35, SILAHA 5 MIKOA YA KUSINI.

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 35 katika Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa mikoa ya  Kusini unaojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza mkoani katika eneo la Kilambo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya watuhumiwa 35, wawili wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi, 16 wapo chini ya Upelelezi na 17 wapo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee).

Sabas amezitaja Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Rifle mbili na Gobore moja ambapo amebainisha kuwa ufuatiliaji bado unaendelea ili kuwabaini wafadhili wa uhalifu hapa nchini.

“Kama nilivyosema kipindi kilichopita kuwa Operesheni hii ni endelevu na matokeo ndio kama haya hivyo hata wale waliokimbilia nchi jirani ya Msumbiji hawapo salama kwa kuwa hata kule operesheni zinaendelea na tunashirikiana na Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuhakikisha kuwa wote wanakamatwa“. Alisema Sabas.

Aidha Kamanda Sabas amewataka wakazi wa mwambao wa mto Ruvuma kuendelea kutoa taarifa mapema mara tu waonapo watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao kwa kuwa uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakitumia vipenyo vya mto huo na kufanya uhalifu kati ya nchi yetu na Msumbiji.

Pia amesema Operesheni hiyo inashirikisha vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa wito kwa raia wema kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na usalama hapa nchini.

Kufuatia mafanikio hayo, baadhi ya Wananchi katika mkoa wa Mtwara wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa inayofanya ya kuhakikisha kuwa wahalifu wanaosumbua wananchi wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.
 Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas akionesha baadhi ya silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo
Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas akiongea na wananchi katika eneo la Kilambo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara

KAMATI MAALUM ZA BUNGE ZA KIUCHUNGUZI KUHUSU SEKTA ZA UVUVI WA BAHARI KUU NA GESI ASILIA ZAWASILISHA TAARIFA ZAKE NA MHE. SPIKA KUZIPOKEA NA KUZIKABIDHI SERIKALINI

$
0
0
 Spika wa Bunge (Mb), Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla ya uwasilishwaji na kukabidhi taarifa za Kamati Maalum alizounda  kuchunguza na kushauri kuhusu sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi asilia. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na mara baada ya kuzipokea taarifa hizo Mhe. Spika alizikabidhi Serikalini ambapo zilipokelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu.
 Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Gesi Asilia Mhe. Dustan Kitandula (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
 Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  kuchunguza na kushauri kuhusu Uvuvi wa Bahari Kuu Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akikabidhi taarifa ya Kamati hiyo kwa Mhe. Spika mara baada ya kuiwasilisha mbele ya Waheshimiwa Mawaziri, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa kitaifa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (kushoto) kwa Mhe. Spika
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akipokea taarifa za Kamati Maalum za Bunge kwa niaba ya Waziri Mkuu zilizoundwa kuchunguza na kushauri kuhusu Sekta za Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia kutoka kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Wengine katika picha kutoka kushoto kwa Mhe. Spika ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Kamati Maalum ya Bunge aliyounda kuchunguza na kushauri kuhusu sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu (waliosimama) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kutoka kushoto waliokaa ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwepo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Anastazia Wambura, Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi.  PICHA NA OFISI YA BUNGE

NEWZ ALERT: WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA WAFARIKI DUNIA MJINI IRINGA

$
0
0
Pichani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alipokwenda kuwajulia hali watoto hao wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao walikuwa wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa 
 
Watoto Maria na Consolata ambao ni mapacha walioungana wamefariki Dunia usiku huu katika hospitali ya Rufaa mkoani Iringa.Chanzo cha taarifa ya kufariki kwa watoto hao imetolewa usiku huu na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela kupitia ukurasa wake wa Twitta kama unavyoonekana hapa chini.

TAARIFA ZAIDI TUTAWAJULISHA KADIRI YA ZIKAVYOKUWA ZIKIENDELEA KUPATIKANA.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN

HESHIMA ZA MWISHO KWA JOSIAH CHACHA ZILIZOKUWA ZIFANYIKE LEO JUMAMOSI SASA KUFANYIKA SIKU ITAKAYOTANGAZWA TENA

$
0
0
Familia ya marehemu Josiah Chacha inaendelea kufarijika na kuwashukuru wote kwa Sala, simu rambirambi za kifedha ambazo imekuwa ikizipokea. MUNGU na aendelee kuwabariki wote.

Kutokana na ughafla wa tukio hili, Familia ya marehemu imeridhia kusogeza mbele siku ya Last respect kwa hapa Marekani. Tutawapa taarifa Maalumu mipango itakapo kamilika.

Badala ya memorial service tutakutana leo Jumamosi June 2nd kuanzia saa nane mchana for fundraising ili tuweze kukamilisha taratibu za kumsafirisha mwenzetu.
Address ni 
26, South Hadley , MA 01075

-Bado tunakabiliwa na changamoto la kufikia gharama halisi za kumsafirisha marehemu kwenda Tanzania. Tutakuwa tukishare status ya pale tulipofikia kila siku usiku. Gharama za funeral home na ushafirishaji kwa ujumla ni $20,000. Tunaamini kwa msaada wenu tutafanikiwa lengo la kumsafirisha mwenzetu Josiah Chacha akapumzishwe kwenye nyumba yake ya milele Tanzania.
Ndugu zangu Watanzania tunaopendana kwa utaifa wetu,familia ya Watanzania New England tumepatwa na msiba wa mwenzetu Josiah Chacha. Michango yetu inahitajika ili mwenzetu Josiah Chacha aweze kwenda pumzishwa katika nyumba yake ya milele.
 Tuungane ndugu na tulichonacho ili tuwasaidie familia yake kukamilisha mipango ya mazishi yake. Tusaidie pia kuarifu wanajumuiya wenzetu ili nao wasaidie. 
Kwa taarifa zaidi Unaweza wasiliana moja kwa moja na: 
Aida (Fiancee) : 413-693-5432 
Sada (Dada wa marehemu): 413-204-1321 
Richard Mwandemani: 413-262-0400 

Msiba upo nyumbani kwa marehemu: 
540 Grandy Rd, 
South Hardley MA 01075 

Kwa Rambirambi Kuisindikiza familia hii kwa rambirambi, tafadhali tumia njia yeyote kati ya hizi: 
CashApp 
Aida Mwangaka: 413-693-5432 
Amina Makoko : 413-204-1321

Bank Account 
Bank of America (BOA)
acct;004648822691 
routing;011000136
jina;VeronicaBisege

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA,
NA JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMINA

MISSY TEMEKE NA MUMEWE WAFUTARISHA HILTON HOTEL, ROCKVILLE, MARYALAND, MAREKANI

$
0
0
Missy T (kati) akiwa na Loveness Mamuya (kushoto) na Shamis siku ya Ijumaa June 1, 2018 katika hotel ya Hilton iliyopo Rockville, Maryland siku Missy Temeke na mumewe Mohamed Matope walipofutarisha. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa udhamini wa Kilimanjaro studio.
Wageni waliofika kwenye futariiliyoandaliwa na Missy T na mumewe Mohamed Matope siku ya Ijumaa June 1, 2018 katika hotel ya Hilton iliyopo Rockville, Maryland nchini Marekani.
Wageni waalikwa wakipata futari siku ya Ijumaa katika hotel ya Hilton iliyopo Rockville, Marylanda nchini Marekani.
 Wageni waliofika kwenye futari iliyoandaliwa na Missy T na mumewe Mohamed Matope
 Futari ikiendelea

 Futair lililoandaliwa na Missy T na mumewe Mohamed Matope.
Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolphh Mutta akiwa na mkewe Agnes Mutta kama moja ya wageni walioalikwa kwenye futari ya Missy T na mumewe Mohamed Matope siku ya Ijumaa June 1, 2018 Rockville, Maryland.

MICHUZI TV: DKT. MWAKYEMBE AZINDUA BODI YA USHAURI YA BODI YA FILAMU, ATOA MAAGIZO KWA VIBANDA UMIZA

Rais Magufuli amteua Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi kuwa Jaji Kiongozi Mahakama Kuu Tanzania

TANZIA: RAIS DKT. MAGUFULI AOMBOLEZA VIFO VYA MABINTI MAPACHA WALIOUNGANA MARIA NA CONSOLATA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na vifo vya mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. 
Mhe. Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam tarehe 06 Januari, 2018. Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake. 
Mhe. Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo. 
Amewaombea Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi.
Amina.

WAZIRI JAFFO ATOA NENO KWA UONGOZI WA BENKI YA PBZ, AWATAKA KUJITANUA ZAIDI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

WAZIRI wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jaffo ameishauri Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),kuhakikisha wanafungua matawi mengi zaidi Tanzania Bara.

Amesisitiza kufunguliwa kwa matawi hayo kutatoa fursa ya Watanzania wengi kuchukua mikopo fedha na hatimaye kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo hasa katika kipindi hiki cha ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Waziri Jaffo ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa shukrani zake kwa uongozi wa benki ya PBZ iliyokuwa imeandaa futari kwa ajili ya wateja wao, vingozi wa ngazi mbalimbali, watendaji wa benki hiyo na wananchi.

"Nitoe shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa PBZ kwa kuandaa futari hii ambayo kimsingi imetukunanisha watu wengi na wa kada tofauti.Nitumie nafasi hii kuwaomba muendelee kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli.

"Kwa sasa mmendelea kushuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikiendelea kufanyika nchini kwetu, hivyo ni vema mkaendelea kuuunga mkono juhudi za ujenzi wa viwanda unaotekelezwa."Uwepo wa benki hii ni muhimu kwani mchango wake ni mkubwa hasa pale inapotoa mikopo ya fedha kwa Watanzania wengi ambao nao kwa namna moja au nyingine wataweza kushiriki katika maendeleo ya nchi yetu,"amesema Waziri Jaffo.

Aidha amefafanua miradi ya ujenzi wa Reli ya kisasa(Standard Gauge), pamoja na mradi kuzalisha umeme katika Mto Rufiji (Stiggler’s Geogre) ni sehemu ya matokeo mazuri yanayoendelea kufanywa na Serikali ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Ameongeza tangu kuingia madarakani Serikali imepiga hatua kadhaa ili kuinua uchumi, ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na ununuzi wa ndege."Hii ni mikakati inayofanywa na Serikali yetu kuhakikisha inaboresha uchumi wake.Bila ya kuwa na uchumi imara itakuwa ngumu vijana kupata ajira."Hivyo ujenzi wa viwanda ni matokeo mazuri ya kufikia dhamira hiyo ambayo mbali na mambo mengine itawasaidia vijana wengi kupata ajira,"amesema.

Amesema kuna idadi kubwa ya wanaohitimu ngazi mbalimbali za masomo waliopo mitaani kutokana na kukosa ajira, hivyo ujio wa viwanda vya kutosha kwa kiasi kikubwa utasaidia vijana hao kutoka mitaani na kupata kazi.Kuhusu benki ya PBZ Waziri Jaffo amesema imejiapambanua vema kutokana na utoaji wa huduma bora na uwepo wa dirisha la Islamic ndani ya benki hiyo kumefungua milango kwa wale wanaotaka kukopa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam.

Hata hivyo wameshauri kujitanua mikoani kwa kufungua matawi maeneo mbalimbali nchini ili kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi nchini."Uwepo kwa dirisha la Islamic kumetoa fursa kwa waumini wa dini ya kiislamu kulitumia kupata huduma za kibenki.Kwa nafasi hii naombe muone fursa ya kuwasaidia vijana wengi kupata mikopo ya benki yenu ili kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi hasa uchumi wa viwanda,"amesema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Dirisha la Islamic la benki hiyo Said Mohammed Said akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa PBZ,amesema wanatoa shukrani kwa wateja wa benki hiyo kwa hatua zao za kuendelea kuunga mkono benki hiyo.

Amesema umefika wakati watanzania wachague huduma za benki hiyo ili waweze kunufahika na huduma mbalimbali ambazo wanazitoa kwa kutanguliza weledi wa hali ya juu katika kutoa huduma bora za kibenki."Tunatambua mchango wa wateja wetu katika kutuunga mkono na futari hii imetokana na wao kuwa pamoja nasi na ndio maana tumejumuika sote mahala hapa ,"amesema.

CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA SOKO WAKWAMISHA MAPATO WILAYA YA BUHIGWE

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

CHANGAMOTO ya ukosefu wa soko Katika Kijiji cha Manyovu Kata ya Munanila wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, imekuwa kero ya muda mrefu ambayo imesababisha wafanyabiashara wengi wa eneo hilo kukimbilia Kasulu na mikoa mingine.

Wanafanya hivyo kwa lengo kuendeleza biashara zao hali inayo sababisha kushuka kwa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

Wakizungumza na Michuzi Blog mkoani Kigoma mwananchi na mfanyabiashara wa Manyovu , Jackson Hemana amesema Soko litakapojengwa watapata faida kubwa na kwamba Warundi wamekuwa wakija Tanzania na kwenda kuchukua bidhaa katika Wilaya ya Kasulu kwa kuwa Manyovu hakuna soko.

Amesema litakapo jengwa wananchi wana muamko wa kufanya biasha na itasaidia pia hata kuongeza pato katika Wilaya na wananchi wote.Azalia Ashery amesema wao kama kafanya biashara wa mazao ya ndizi na nanasi pamoja na vyakula vingine wanapata shida na wanalazimika kuuzia biashara zao juani na mvua kuwanyeshea, hali inayosababisha mazao yao kuharibika na kupata hasara.

Pia amesema wafanya biashara wengine wanaamua kuuzia mazao yao shambani kutokana na ukosefu wa soko ambapo wanalazimika kuuza kwa bei ya chini kwani hakuna mahali watakapo kwenda kuuzia.

"Edapo Serikali itajenga jengo la soko itawasaidia sana wakulima kuinuka na kufanya biashara pamoja na kuinua Wilaya ya Buhigwe kwakuwa eneo hilo ni eneo maarufu kwa wakulima wa , Kahawa , Ndizi , Nanasi na Mazao mengine ya chakula na biashara hivyo yatapa soko na kuinua uchumi wa Watanzania," amesema.

Akizungumza ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia General Marko Gaguti amesema kutokana na changamoto hiyo wao kama viongozi wa Wilaya walishirikiana na kuandaa andiko la kuomba fedha serikalini kwaajili ya ujenzi wa soko la kimataifa litakalo wakutanisha wananchi wa Burundi na Tanzania kufanya biashara Katika soko la kimataifa ambalo litajengwa mpakani.

Amesema mradi huo umekubaliwa na hatua za awali zimekwisha kamilika ambapo Serikali kuu imetoa fedha Sh.bilioni 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa soko lenye ghorofa moja litakalo kuwa na Ofisi 300 na maeneo ya vibanda vya wazi 500 na ujenzi utaanza mwaka wa fedha 2018/2019 na Julai mwaka huu watatangaza zabuni ya awali na ujenzi utatumia mwaka Mmoja.

"Sababu Kubwa ya kuuweka mradi huu Manyovu katika Wilaya ya Buhigwe eneo hilo ni eneo maarufu kwa Wilaya hiii na Mkoa kwa ujumla linalo wakutanisha Wafanya biashara Wengi kutoka Nchi za jirani kutokana na mpaka huo kutumiwa na Watu wengi ,soko hilo litakapo kamilika litatoa chagizo kubwa Kwa Wananchi wa Buhigwe na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kupata Fulsa ya Biashara na kuongeza pato katika Halmashauri ya Wilaya hiyo", alisema Brigedia Jenerali Gaguti.

Aidha aliwaomba Wananchi washiriki kwa pamoja katika ujenzi wa soko hilo pamoja na usimamizi ili malengo ya serikali ya kukamilisha mradi huo unao tarajiwa kuingizia kiasi cha shilingi milioni 230 kwa halmashauri hiyo ukamilike kwa wakati ilikuongeza ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.

Baraka Lupori ni Diwani wa Kata ya Munanila alisema anaishukuru sana Serikali kwa kuweza kuweka mradi mkubwa wa soko katika eneo hilo ambalo lilikuwa kilio kikubwa Kwa Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe na Kata hiyo ,ambapo Wafanya biashara wengi wa eneo hilo walikimbia kutokana na kukosa soko hali iliyopelekea kushuka kwa Mapato kupelekea kata hiyo kukusanya Kiasi cha shilingi milioni tatu tu kwa mwezi.

Alisema Munanila ni mpaka unaokutanisha Wananchi wa Nchi tatu za Burundi, Rwanda na Congo, na Wananchi wa Burundi wengi wa Burundi wanategemea sana Bidhaa za chakula kutoka Katika Vijiji vya Manyovu na Wilaya ya Buhigwe kwa ujumla soko hilo litakapo kamilika litasaidia sana wafanya biashara wengi walioondoka Manyovu na kuhamia maeneo Mengine kwaajili ya kuendeleza Biashara zao kurejea na kufanya biashara na kipato cha halmashauri na wananchi kitaongezeka.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images