Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) OFISI ZA TANZANIA WATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

$
0
0
 Picha no. 1 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika mkutano na  wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ofisi za Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake  kwa ajili ya kuingia makubaliano ili  wafanyakazi wa shirika hilo waanze kutibiwa  katika Taasisi hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na   wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  ofisi za Tanzania walipomtembelea leo  ofisini kwake  kwa ajili ya kuingia makubaliano ili  wafanyakazi wa shirika hilo waanze kutibiwa  katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI


MICHUZI TV:TWENZETU RUSSIA 2018: UCHAMBUZI KUNDI A & B

ASAS DAIRIES LTD YAGAWA MAZIWA KWA WANAFUNZI MIKOA YA MBEYA, ARUSHA,IRINGA NA DODOMA MAADHIMISHO YA UNYWAJI MAZIWA DUNIANI

$
0
0
ASAS DAIRIES LTD imegawa zaidi ya pakiti 400,000 kwenye shule mbalimbali za mikoa ya IRINGA, ARUSHA, MBEYA na DODOMA. wakati wa  maadhimisho ya  wiki ya Maziwa duniani ambapo kitaifa inafanyika mkoani Arusha.
ASAS DAIRIES LTD ilianza kampeni hii Tarehe 22 mwezi wa Tano na kufikia zaidi ya shule 108 na Wanafunzi 67,000. Hii inatokana na uhamasishaji wa unywaji wa Maziwa Mashuleni ambao unafanywa na ASAS DAIRIES LTD kila mwaka.
Katika kufikia lengo la watanzania kunywa maziwa kwa wingi kampuni ya ASAS DAIRIES LTD imejikita katika kampeni hiyo ili kuwafanya watoto ambao watakuwa wazazi wa baadaye kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya zao pamoja na vizazi vyao kwa siku za baadaye.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha ASAS DAIRIES LTD Bw. Ahmed Salim Asas amesema  huu ni mwendelezo wa kampeni hiyo na lengo la kampuni hiyo kwa mwakani ni kuzifikia shule za msingi nchi nzima.
 Bw. Ahmed Asas ameishukuru Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ngazi zote  jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa kwao na kuifanya ndoto ya Tanzania ya Viwanda kwenda kutimia kwa mafanikio makubwa.
 Naibu Waziri Wa Kazi Ajira Na Vijana Mheshimiwa Anthony Mavunde Akigawa Maziwa Ya Asas Kwa Wanafunzi Waliojitokeza Kwenye Viwanja Vya Nyerere Square jijini Dodoma Kwenye Kilele Cha Unywaji Wa Maziwa Duniani Ambapo Kitaifa Imeadhimishwa Mkoani Arusha
 Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Nkuhungu Ya jijini  Dodoma Wakigawiwa Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD.
 Wanafunzi Wa Shule Ya Nkuhungu Wakifurahia Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD
 Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Na Mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Mh. Mrisho Gambo Wakipokea Maziwa Kutoka Kwa Mwakilishi Wa Asas Dairies Lipita Mtimila Kwa ajili Ya Shule Za Mkoa wa Arusha Ambapo ASAS DAIRIES LTD Wametoa Maziwa pakiti 15,000 Kwa Wanafunzi wa mkoa huo.

 Mheshimiwa Richard Kasesela Akuu wa Wilaya ya Iringa Na Mkurugenzi Wa ASAS DAIRIES LTD Ahmed Salim Asas wakiwa  Kwenye Viwanja Vya Ngombe Mjini Iringa Kwenye Kilele Cha Madhimisho Ya Wiki Ya Maziwa Duniani.
 Wanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngombe Wakifurahia Maziwa Ya ASAS DAIRIES LTD wakati Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela na Mkurugenzi wa ASAS DAIRIES LTD Bw. Ahmed Salim Asas walipokuwa wakiwagawia.

YANGA ,SIMBA NA JKU WATINGA KENYA SPORT PESA SUPER CUP,SINGIDA KUWAFUATA

$
0
0

Vikosi vya Yanga ,Simba, JKU cha Zanzibar vimeondoka nchini kwenda Nairobi nchini Kenya.Yanga ,Simba ,Singida united na JKU wanakwenda kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup itakayofanyika mjini Nakuru nchini Kenya.Michuano hiyo itaanza Jumapili ikishirikisha timu nane, nne kutoka Tanzania na nne kutoka Kenya.
Kikosi kamili cha Yanga Sports Club  kilichoelekea nchini Kenya kwenye michuano ya SportPesa Super Cup .

Kikosi kamili cha Simba SC kilichoelekea nchini Kenya kwenye michuano ya SportPesa Super Cup. Simba wanatarajiwa kufungua dimba na Kariobangi Sharks Jumapili kabla ya mahasimu wao wa jadi, Yanga kuvaana na Kakamega Homeboys Jumatatu 4, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Afraha, Nakuru, Gor Mahia itaanza na JKU Juni 3, wakati Singida United itaanza na AFC Leopards Juni 5.Kikosi kamili cha timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi(JKU)

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHANGUO CHA URAFIKI NA KUKUTA MADUDUDU

$
0
0
*Aagiza Waziri wa Viwanda, RC na Menejimenti wakae na kumpa taarifa leo jioni
*Asema tofauti ya viwango vya mishahara inatisha, ataka orodha ya watumishi
*Awataka watumishi walioko kazini, likizo wawe wastahimilivu

SERIKALI imesema hairidhiki na ubia unaoendeshwa kwenye Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Juni mosi, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wafanyakazi wa kiwanda hicho mara baada ya kukagua mitambo mbalimbali kwenye kiwanda hicho.

“Serikali haturidhiki na ubia huu, na huyu mbia aelewe kwamba Serikali haturidhishwi na ubia huu wala kinachoendelea hapa kiwandani,” amesema huku akishangiliwa kwa nguvu na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aongoze kikao baina ya wabia hao na menejimenti ya kiwanda na apewe taarifa hiyo leo saa 12 jioni baada ya kufuturu.

“Ubia wenu hauna tija. Kwa hiyo wewe Msajili wa Hazina na huyo mwekezaji, nikitoka hapa, mbaki mfanye kikao na mnipe majibu leo saa 12 jioni. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Mkuu wa Mkoa muongoze mjadala huo na nikitoka kufuturu mniambie maazimio yenu, na kama haiwezekani, mvunje kabisa ubia huo ili tujue hatuna mbia tutafute mbia,” amesema.

Waziri Mkuu amesema wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na kampuni ya Changzhou State owned Textile Assets Operations kutoka China na kwamba Serikali ilipoamua kukaribisha uwekezaji ilitarajia kupata mtaji, teknolojia na ajira za kutosha lakini hali ya sasa ni kinyume kabisa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam baada ya kukagua kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza nao kiwandani hapo, Juni1, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam, Khamis Mazugo (kushoto)  kuhusu mitambo ya kiwanda hicho iliyokoma kufanya kazi wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita katika eneo zilipong'olewa mashine za kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, Shadrack Nkelebe kuhusu mashine za kutengeneza  nyuzi za pamba wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 01.06.2018

VOA SWAHILI: Zulia Jekundu

VOA SWAHILI: Duniani Leo Juni 1, 2018


DC SHINYANGA AKABIDHI MSAADA WA BIMA ZA AFYA, SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 200 TAMASHA LA TVMC

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro leo Ijumaa Juni 1,2018 amekabidhi msaada wa nguo za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata za Chamaguha,Ibadakuli,Kizumbi, Mwawaza na Mwamalili zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
Msaada huo umetolewa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.
Akizungumza wakati wa Tamasha lililokwenda sanjari na ugawaji wa sare za shule na kadi za bima ya afya,Matiro alisema bado wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mimba na ndoa za utotoni huku miongoni mwa sababu zinachochangia ikiwa ni ugumu wa maisha.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akikabidhi msaada wa nguo za shule na kadi za bima ya afya kwa wawakilishi wa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata za Chamaguha, Ibadakuli, Kizumbi, Mwawaza na Mwamalili zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akiendelea kuzungumza wakati wa tamasha la TVMC.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akishikana mkono na mmoja wa wanafunzi wakati wa zoezi la kugawa kadi za bima ya afya watakazozitumia kwa ajili ya matibabu
Mwanafunzi akishikana mkono na Katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Rajabu Bwanga baada ya kupata kadi yake ya bima ya afya.
.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa tamasha hilo la TVMC
Afisa Elimu Sayansi Kimu na Afya Manispaa ya Shinyanga,Beatrice Mbonea akizungumza wakati wa tamasha hilo ambapo alilishukuru shirika la TVMC kutoa msaada wa sare za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 waliopo katika manispaa ya Shinyanga.




KATIBU MKUU MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA ERASTO SIMA AKABIDHIWA OFISI RASMI

$
0
0
Na Elisa Shunda 
VIONGOZI na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameungana kwa pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa jumuiya hiyo Anayemaliza Muda wake,Seif Shaban Mohamed kumpokea Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo Erasto Sima katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo zilizopo Kariakoo jijini Dar es Salaam Ijumaa. 
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi Katibu Erasto Sima alisema kuwa mojawapo ya vipaumbele vyake atakavyoenda kuvisimamia katika uongozi wake kwa nafasi hiyo ya utendaji wa jumuiya hiyo ya wazazi taifa atahakikisha anawakumbusha watendaji wenzake wa ngazi ya chini kufuatilia kwa makini ulipaji ada ya wanachama waliomo ndani ya muiya hiyo,pia ataendeleza kwa kufanya usimamizi wa kutosha katika uangalizi wa mali na miradi yote iliyopo ndani ya jumuiya hiyo. 
 "Tunao wanachama wengi katika jumuiya yetu hivyo nitalisimamia suala hili wanachama wetu walipe mapema ada zao siyo hadi kipindi cha uchaguzi ndo watu waje wawalipie ada kwa kweli hilo silipendi ukiwa wewe ni mwananchama wetu ni heri ujilipie ada mwenyewe lakini pia nitahakikisha nasimamia mali za chama na miradi yotde iliyopo katika jumuiya yetu iendelee zaidi ya hapa ilipo ili kukiongezea chama chetu kipato cha ndani" Alisema Katibu Sima. 
Akizungumza kuhusu utofauti wa nafasi aliyokuwepo awali na hivi sasa Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa,Erasto Sima alisema kuwa kwa sasa yeye ni mtendaji hivyo atamshughulikia ipasavyo mtu yoyote atakayetaka kukwamisha utendaji kazi wake na majukumu yake yasiende vizuri.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Aliyemaliza Muda Wake,Seif Shaban Mohamed (kulia) akimlaki Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima (kushoto) baada ya kuwasili katika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi.


 Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Erasto Sima (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi CCM Mkoa wa Pwani, Dk.Zainab Gama.

Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Erasto Sima (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Edwini Shunda aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka (kulia) baada ya kuwasili ofisini hapo. Kulia kwake ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Pwani,Gama Juma Gama.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Aliyemaliza Muda Wake,Seif Shaban Mohamed (kulia) akimkaribisha ofisini na kumkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima (kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Elisa Shunda.


MICHUZI TV: CRDB yawazawadia washindi wa kampeni ya “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2...

Introducing Wimbo Rasmi wa Ndondo Cup 2018 by Kayumba and Sharara

MKUTANO WA NANE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) MKOANI MOROGORO

$
0
0
MKUU  wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe amelitaka Shirika la  Bima la Taifa  (NIC) kuongeza maarifa na ubunifu wa kutafuta masoko mapya  kutokana na kuwepo zama za ushindani mkubwa wa kibiashara.
Dk Kebwe alisema  hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo uliofanyika mjini Morogoro.
Alisema , pamoja na kuongeza masoko mapya pia ni vyema shirika likajizatiti katika ulipaji wa madeni kwa wateja wao ,kwa kufanya hivyo kutadumisha imani kwa wateja na kuongeza biashara kwa kiasi kikubwa.
Mkuu mkoa alisema, baraza la wafanyakazi  ni chombo muhimu katika ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kufikia maamuzi mbalimbali na katika kuongeza tija
Pamoja na hayo alipongeza Shirika hilo kwa kukuamua kuanzisha bima ya kilimo kwa wakulima na hatua hiyo itauwezesha  mkoa wa Morogoro ambao ni  moja wenye fursa kubwa ya kilimo  kunufaika zaidi.
“ Ningependa kuwaomba bima hii ya kilimo itakapoanza mkoa wangu  upewe nafasi ya kupata elimu hii, wakulima wengi wa mkoa wa Morogoro waweze kunufaika nayo” alisema Dk Kebwe.
Pia alilipongeza kwa hatua mbalimbali za kidigitali walizofikia ikiwem matumizi  ya Tehama na mfumo wa kidigitali wa Comesa ambao wanatarajia kuanza kuutumia.
Mkuu huyo wa mkoa pia alilitaka Shirika hilo kutumia vyema rasilimali watu walizonazo na teknlojia hiyo ili kufikia malengo yaliyowekwa ya biashara .
Kwa upande wake  Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Sam Kamanga   kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Morogoro, kufungua mkutano  huo alisema , mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu isemayo “ Bima ya Kilimo ni Udondo Rutuba kwenye Kilimo Biashara na Uchumi wa Viwanda Imara”.
Kamanga  alisema , katika mkutano huo wa siku mbili  kulikuwa na mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo pamoja na mafunzo ya mfumo mpya wa kidigitali wa Comesa
 Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la  Bima la Taifa  (NIC), Sam Kamanga  ( kulia) akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( kushoto),kwa ajili ya kufungua mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa NIC.
  Wajumbe wa mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa NIC wa kimsiliza mgeni rasmi
  Wajumbe wa mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa NIC wa kimsiliza mgeni rasmi

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( kati kati mwenye koti walioketi ) akiwa na baadhi ya viongozi na wajumbe wa baraza la wafanyakazi  wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) chini ya Mkurugenzi mtendaji hilo,  Sam Kamanga  ( watatu  kutoka kushoto walioketi) 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( kati kati mwenye koti walioketi ) akiwa na viongozi na wajumbe wa baraza la wafanyakazi  wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) chini ya Mkurugenzi mtendaji hilo,  Sam Kamanga  ( watatu  kutoka kushoto walioketi) mara baada ya mkuu wa mkoa kufungua mkutano wa nane wa baraza hilo.( Picha na John Nditi).

RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amemuagiza mkuu wa Kituo Cha Polisi Gairo kuwakamata wale wote waliokula fedha za ujenzi wa maabara ya shule sekondari ya Idibo iliyiyopo katika Kata ya Idibo wilayani Gairo. 
 Akizungumza katika mkutano wa hadhara hizi karibuni Dkt. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema kuwa hawezi kuvumilia kuona shilingi Milioni 12 fedha za ujenzi wa maabara zilizotokana na nguvu ya wananchi zinaliwa na watu wachache tena bila kufanikisha malengo. 
"Hivi kuna watu bado hawaelewi umuhimu wa kutunza fedha za umma??? Haiwezekani wananchi wajichange harafu nyie viongozi wa kijiji mle hela zao za maendeleo bila aibu, siwezi kuvumilia... Nakuagiza OCD Gairo na TAKUKURU kufanya msako watu hawa wapelekwe mbele ya sheria haijalishi walishastaafu au la!," amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Katikati) akiwahutubia wakati kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo. 
.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (wa tano toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wilaya ya Gairo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (kulia kwake), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kulia kwa mkuu wa mkoa) pamoja na wengine. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea zawadi ya mahindi mara baada ya kuwahutubia (katikati) wananchi wa kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akisikiliza maelezo mafupi ya ujenzi wa shule ya Idibo ulioanza mwaka 2014 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umekwama katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi pamoja na pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya kijiji wakiwa katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo. Habari  kamili BOFYA HAPA



NIDA YAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa amezindua rasmi kuanza kwa zoezi la Ugawaji Vitambulisho kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya Usajili wa Mkupuo kumalizika kwa asilimia 82%.
Akitoa taarifa ya mwenendo wa zoezi la Usajili na Utambuzi liloanza mwezi Octoba 2017 kwenye sherehe za uzinduzi wa zoezi hilo; mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bi. Rose Joseph amesema mkoa wa Kilimanjaro umekuwa mkoa wa nne (4) kitaifa kumaliza awamu ya kwanza ya Usajili Wananchi na kuanza kugawa Vitambulisho kwa wananchi waliokidhi sifa na vigezo vya uraia.
Amesema ugawaji wa awamu ya kwanza ya Vitambulisho vya Taifa utafanyika kwenye ofisi za Watendaji wa Mitaa na Vijiji wananchi walikosajiliwa ambapo zaidi ya vitambulisho 250,000 vitagawanywa huku hatua za mapingamizi, uchakataji na uzalishaji wa Vitambulisho vingine zikiendelea kwa Wilaya zote za mkoa huo.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi; Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba amesema kukamilika Usajili wa Umma hakumaanishi wananchi hawataendelea kusajiliwa; badala yake kuwataka wananchi ambao hawajasajiliwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwenye ofisi za NIDA zilizoko kila Wilaya kwani manufaa ya Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ni makubwa na mengi, na iwapo mwananchi atakosa kuwa na hati hiyo muhimu atakwama kufanikisha mambo mengi na muhimu ya kimaendeleo ikiwemo kushindwa kushiriki katika masuala muhimu ya kitaifa.
Mkuu wa Mkoa huo amewataka Wakuu wote wa Wilaya mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha wanahamasisha wananchi na kufuatilia kwa karibu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kusajiliwa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa kabla wananchi hawajaanza kukwama kufanya shughuli zao au kukumbwa na msako kwa kwa kukosa Hati hii muhimu inayowatambulisha kama Raia.
Sherehe za uzinduzi wa zoezi la ugawaji Vitambulisho mkoa wa Kilimanjaro zimehudhuriwa na Viongozi wa Dini, Wafanya biashara, Viongozi wa kisiasa, wananchi, watu wenye mahitaji maalumu na vyombo vya habari; ambapo zaidi ya wananchi 20 wawakilishi wa makundi mbalimbali walikabidhiwa Vitambulisho vyao, huku wakuu wa Wilaya za mkoa huo wakikabidhiwa zaidi ya Vitambulisho 250,000 vya awamu ya kwanza.
 Mhe. Anna Mghirwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. Katikati ni Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour na kushoto ni mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bi. Rose Joseph.



 Baadhi ya makundi wawakilishi wa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia kwa karibu matukio wakati wa sherehe za Uzunduzi wa zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wanachi wa mkoa wa Kilimanjaro. Sherehe hizo zilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kuanza kwa ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bi. Rose Joseph na Kushoto ni Mhandisi Aisha Amour.
 Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akimkabidhi Ndg. Evance Moshi Kitambulisho chake kwa niaba ya kundi la watu wenye mahitaji maalumu.
 Mwakilishi wa kundi la viongozi wa dini Sista Eliaichi Malisa akikabidhiwa Kitambulisho chake na mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakati wa sherehe za uzinduzi


Baadhi ya washiriki wa sherehe za uzinduzi wa zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo la ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa akibadilishana mawazo na mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA -  Bi. Rose Joseph (kulia)

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) OFISI ZA TANZANIA KUTIBIWA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

$
0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika mkutano na  wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ofisi za Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake  kwa ajili ya kuingia makubaliano ili  wafanyakazi wa shirika hilo waanze kutibiwa  katika Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na baadhi ya madaktari bingwa wa taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na   wafanyakazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  ofisi za Tanzania walipomtembelea leo  ofisini kwake  kwa ajili ya kuingia makubaliano ili  wafanyakazi wa shirika hilo waanze kutibiwa  katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI

Michuzi TV: CRDB yawazawadia washindi wa kampeni ya “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCard Visa”

Introducing "IYENA IYENA" by Diamond Platnumz Ft Rayvanny

Habari za Umoja wa Mataifa leo: Tanzania yapokea medali ya ulinzi wa amani Umoja wa Mataifa

Rais Magufuli awapandisha vyeo Maafisa 9 wa Jeshi la Magereza

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images