Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

VIFO VYA PACHA: Kauli ya Consolata iliyohitimisha safari ya miaka 22


MICHUZI TV: vijana waliohifadhi Quran watakiwa kuendelezwa kitaaluma katika fani nyingine za elimu

VIDEO: MIRADI 70 YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 11. 1 KUZINDULIWA NA MWENGE MKOANI RUVUMA

0
0
Zaidi ya miradi 70 yenye thamani ya shilingi bilioni 11.1 itazinduliwa na mwenge wa uhuru uliowasili mkoani RUVUMA,ambapo mwenge huo utakimbizwa katika halimashuri nane na kuitimishwa katika wilaya ya TUNDURU tarehe 11 utakabiziwa mkoani mtwara.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa ruvuma CHRISTINA MNDEME

Wataalam Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakagua umeme vijijini Tanga na kuwasha umeme

0
0

Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiongozwa na Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati, wamekagua mradi wa umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika wilaya mbalimbali mkoani Tanga na kuzindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo, wilayani Korogwe.

Mhandisi Msembele, ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu katika uzinduzi huo, alisema kuwa, kuzinduliwa kwa huduma ya umeme katika Kijiji hicho kumewezesha wananchi zaidi ya 63 kuunganishwa na huduma ya umeme huku wateja 180 tayari wameshalipia huduma hiyo.

" Niwapongeze wananchi wa Kijiji hiki cha Bagamoyo kwa kuchangamkia huduma ya umeme, lakini niwakumbushe kuwa inapaswa kutumia umeme kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi kama kufunga mashine za kusaga nafaka na si kuwasha taa peke yake, " alisema Mhandisi Msembele.

Wataalam wengine walioambatana na Mhandisi Msembele ni  Afisa Upimaji kutoka REA, Hussein Shamdas, Meneja wa TANESCO mkoa wa Tanga,  Eng. Cecilia  Msangi na Meneja wa TANESCO, wilaya ya Korogwe, Julius Nyamarungu.

 Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakikagua transfoma zitakazotumika kusambaza umeme vijijini katika Wilaya ya Korogwe. Kushoto ni Hussein Shamdas kutoka REA na katikati ni Yusuph Msembele.
 Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati (wa Tatu kulia) akikata utepe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo wilayani Korogwe mkoa wa Tanga. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka TANESCO, REA na wawakilishi wa wananchi.
 Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo wilayani Korogwe mkoa wa Tanga. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka TANESCO, REA na wawakilishi wa wananchi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAMENEJA WA TRA NCHINI WAAGIZWA KUWATEMBELEA WAFANYABIASHARA MARA KWA MARA

0
0
Na Veronica Kazimoto-Dodoma

Mameneja wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nchi nzima wameagizwa kuwa na utaratibu wa kuwatembelea wafanyabiashara mara kwa mara ili kujua changamoto zao na kuzitatua ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara hao.

Agizo hilo limetolewa leo na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere jijini Dodoma alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya kujiridhisha utendaji kazi wa Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutokufanya kazi.

"Nimepita katika baadhi ya maeneo mengi kuanzia Dar es Salaam, Kibaha, Mlandizi, Morogoro, Gairo na sasa nimemalizia Dodoma. Katika maeneo yote niliyopita nimekuta wafanyabiashara wana changamoto ambazo zinaweza kutatulika kirahisi na Mameneja bila ya kusubiri mpaka Kamishna Mkuu apite, hivyo nawaagiza Mameneja kuwatembelea wafanyabiashara katika maeneo yao, kujua changamoto wanazozipata ili kuzitatua mara moja kinyume na hapo nitachukua hatua," alisema Kichere.

Aidha, Kamishna Mkuu Kichere alieleza kuwa, tatizo la Mashine za EFD limekwisha na tayari zimeanza kufanya kazi, hivyo Mameneja wote wa mikoa wanatakiwa kupita katika maeneo yao ili kufanya ufuatiliaji wa mashine hizo na kuzitolea taarifa zile zitakazokutwa bado zina matatizo kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi wa haraka. 

"Ninasema Mameneja wawatembelee wafanyabiashara mara kwa mara kwasababu nimepita katika maduka mbalimbali nimekuta kuna baadhi ya wafanyabiashara tangu Mfumo wa EFD upate hitilafu mpaka leo hawajawasha mashine zao na nilipoziwasha nimekuta zinafanya kazi vizuri, hivyo kinachotakiwa ni Mameneja kupita katika maeneo yao na kufanya ukaguzi wa mashine husika na kuwapa elimu," alifafanua Kichere.

Kamishna Mkuu Charles Kichere amehitimisha ziara yake iliyoanzia Dar es Salaam mpaka Dodoma akipita katika maduka na vituo mbalimbali vya mafuta kwa ajili ya kujiridhisha kama mashine za EFD zinafanya kazi vizuri baada ya mfumo wake kupata hitilafu ya kiufundi tangu Mei 11, mwaka huu kutengemaa na kuruhusu mashine hizo kuanza kufanya kazi kama inavyotakiwa.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kushoto) akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara wa Bodaboda Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia) akikagua risiti iliyotoka katika Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akikagua risiti iliyotoka katika Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti katika kituo cha mafuta kilichopo Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi kujiridhidha utendaji kazi wa mashine za kielektroniki za Kutolea risiti (EFDs) ambazo mfumo wake ulipata hitilafu ya kiufundi hivi karibuni na kusababisha mashine hizo kutofanya kazi.(PICHA ZOTE NA TRA)

BARAZA LA WAFANYAKAZI WA NIC LAKUTANA MOROGORO

0
0
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt .Steven Kabwe (kushoto) akizungumza katika mkutano wa baraza la wafanyakazi la NIC mkoani Morogoro mwishoni wa wiki.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Sam Kamanga.
Picha ya pamoja ya baraza la wafanyakazi walioshiriki katika mkutano huo.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kabwe na kushoto  kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Sam Kamanga.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt.  Steven Kabwe (katikati) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa NIC

Tamasha la Sports Music Festval 2018 kutua Kanda ya Ziwa

0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii. 

King Cash and Isbah Entertainment inawaletea burudani kabambe wakazi wa kanda ya Ziwa Tamasha la Sports Music Festival 2018 katika kusherehekea sikuku ya Idd.

Tamasha hilo la aina yake litakalosindikizwa na wasanii mbalimbali wa bongo  fleva hapa nchini.

Wasanii hao watakao tumbuiza siku hizo ni Mbunge wa Mikumi Profesa Jay, Juma Nature, Young Killer, Roma, Stamina, Fid Q, Bill Nas, Umber Lulu, Snura, Msaga Sumu, G Nako, Young Dee, Coyo Mc, Fany, B-Gwai pamoja na mkali wa singeli Shalo Mwamba.

Siku ya Idd Mosi wataanzia Geita katika viwanjwa vya Infotech ambapo kiingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 na watoto ni 3000.

Ambapo Idd pili watatapiga hodi Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM kirumba,na baada ya hapo watamalizia burudani Mjini Kahama pale Uwanja wa Taifa kwa kiingilio cha Shilingi  10000 wakubwa,huki watoto wakilipia mlangoni 5000.

Tamasha  hilo  litaanza saa 4 asubuhi mpaka majogoo ambapo pia watashuhudia michezo ya piki piki na magari yakifanya maajabu yake ya dunia.

Waziri Makamba awasihi wananchi kuunda kamati za Mazingira

0
0
Tamasha kubwa lililopewa jina la “Tulonge Mazingira na Mimi” limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo la aina yake lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na lililenga kukuza uelewa wa wananchi juu ya hifadhi ya mazingira msisitizo ukiwa ni kutumia nishati mbadala wa Mkaa kama kauli mbiu ya Siku ya Mazingira kwa mwaka huu inavyosema.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika katika viwanja hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema wananchi wana wajibu mkubwa katika kuhifadhi mazingira na kuwataka kuwa mstari wa mbele kuuliza viongozi wao ni nini wanafanya kuhusu mazingira. “Tuulizeni kuhusu Mazingira na nini tunafanya kuhusu hifadhi ya mazingira” Makamba alisisitiza.

Aidha Mhe. Makamba ameitaka jamii kutoa taarifa juu ya mtu yeyote anaechafua mazingira katika maeneo yao kwani Sheria ya Mazingira inatoa nafasi hiyo ya kumshtaki mtu yoyote. “Sheria ya mazingira  Kifungu cha 5 kimewapa wananchi nguvu ya kushtaki kwa niaba yake kama yanaharibiwa, maana kila mtu ni mdau katika suala la mazingira,  hivyo msilalamike badala yake chukueni hatua stahiki pale mazingira yanapoharibiwa katika maeneo yenu” Makamba alisisitiza. 

Wakati huo huo, Waziri Makamba ameagiza kila mtaa, kijiji na  kitongoji katika nchi yetu kuwa na Kamati ya Mazingira ambayo kisheria ina nguvu kubwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha upelelezi kwenye jambo lolote, kufunga na kufungia kitu chochote kwenye mtaa kinachoharibu mazingira.

Kampeni hiyo ya kuhifadhi mazingira itaendelea nchi nzima na imeambatana na utoaji wa tuzo za hifadhi ya Mazingira ngazi ya Mkoa, tuzo zilizotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Felix Lyaviva. Tamasha hilo pia limehudhuriwa na viongozi wa mbalimbali wa Serikali, Wabunge na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni sehemu ya shamrashamra za wiki ya Mazingira ambayo kilele kitafanyika Juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Kauli mbiu ya Siku ya Mazingira mwaka huu inasema “Mkaa ni gharama, tumia nishati mbadala”
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijumuika katika Tamasha la wananchi  katika Viwanja vya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la ‘Tulonge Mazingira na Mimi’ limefanyika mwishoni mwa wiki na kujumuisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Sehemu ya wananchi waliojumuika katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam wakifuatilia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

WILAYA YA BUHIGWE YAANZA UGAWAJI HATIMILIKI ZA KIMILA KATIKA VIJIJI

0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

HALMASHAURI ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeanza mchakato wa ugawaji wa Hatimiliki za Kimila katika Vijiji vya Mugera, Kajana na Katundu katika Kata ya Mugera na Kajana katika kaya 1025 zitakazo saidia kupunguza migogoro ya ardhi Katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

Akikabidhi hatimiliki hizo katika kaya 50 za mfano jana katika kijiji cha Muhegera Kata ya Mugera wilayani humo zinazotolewa na mradi wa usimamizi wa maliasili kwa ajili yq kuongeza kipato kwa mwananchi unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania na Ubelgiji chini ya shirika la ENABEL.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema katika kesi 10 zinazofika ofisini kwake kati ya hizo nane ni za migogoro ya ardhi na mbili ni za urithi.

Brigedia Jenerali Gaguti amesema mradi huo utasaidia usalama wa wananchi na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kubaki wakiwa walemavu, kwakuwa wananchi wakiwa na maeneo yaliyopimwa na wakiwa na umiliki wa kisheria itasaidia kesi hizo kupungua.

"Na wananchi wataendelea kufanya shughuli zao za Maendeleo na kuachana na tabia iliyokuwepo kwa wananchi wengi kuzunguka kwenye mahakama za Ardhi, na kupeleka kesi za kuibiana maeneo na kuepuka kutumia gharama nyingi kuendesha Kesi hizo,"amesema.
Ameongeza amefurahishwa kwa mradi huo ambao ameuona maeneo mengi aliyopita kukagua mchakato huo ulivyokwenda aa ameona wananchi wengi wanauelewa na wanajua umuhimu wa hatimiliki.Ametoa mwito kwa ciongozi wa Serikali za Vijiji waendelee kuwahimiza wananchi kuja kufuatilia hatimiliki hizi kwani hati hizo nje na kupunguza migogoro ya ardhi itasaidia wananchi kutumia hati hizo kuombaea mikopo kwaajili ya kuendeleza biashara zao.

alisema Mkuu huyo."Wote wanaouelewa faida ya kwanza ni usalama mtu akimiliki hati yake anauhakika wa kumiliki eneo lake kisheria kesi nyingi zinazo pokelewa wilayani kati ya kesi 10 kesi saba ni za migogoro ya ardhi na kesi nyingine ni za mirathi imepelekea kwa kiasi kikubwa watu wengi kupoteza maisha,"amesema .

Hata hivyo amesema maeneo yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za msitu wa kupanda mti kuanza mchakato wa upandaji miti msimu wa upandaji utakapo anza na kutoa rai kwa viongozi wa vijiji kusimamia ipasavyo maeneo ya huduma za kijamii yaliyopimwa kwaajili ya shughuli za ufugaji na kilimo yatumike kwa lengo lililokusudia na wananchi waelekezwe namna bora ya kuyatumia na Kuepusha migogoro kwa wananchi.

Akitoa taarifa ya mradi Mratibu wa Mradi huo wilayani Buhigwe, William Marandu amesema mpango wa matumizo bora ya ardhi ni tokeo tarajiwa namba mbili la mradi ilipima ukubwa wa ardhi ya Kijiji cha Mugera hekta 9401.856 chenye vitongoji vinne ambavyo ni Ruyange, Mugera, Kishaha na majengo na mradi huo ulianza mwaka 2016 kwa kutenga matumizi ya ardhi ya maeneo ya kilimo kekari (6117.076) Malisho ya mifugo Hekati 1207.1, vyanzo vya maji , maeneo ya maziko , maeneo ya makazi hekari 477.78, misitu ya asili 378 na misitu ya kupandwa hekari 1097.3 kwakuwa aridhi ndio chanzo kikubwa cha Mtaji wa Wananchi.
Amesema hati miliki zilizo gawiwa Kwa kaya 50 za mfano ni kati ya hatimiliki 1025 zilizo andaliwa na mradi wa (NRMLED) Kwa vijiji vitatu vya Wilaya ya Buhigwe na hatimiliki 975 zilizobaki zitaendelea kutolewa baada ya ufunguzi wa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi wengine ambao bado hawajafanya utaratibu wa kupata hatimiliki za kimila kufanya utaratibu waweze kupata hati hizo kwa kupitia Idara ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Thadeo Bitumgwa ni mmoja kati ya wanufaika wa Mradi wa ugawaji wa hatimiliki za kimilqa amesema anashukuru kwa kufahamu mipaka ya kiwanja chake anahakika ya kuwa hata pata mgogoro na mtu yeyote na anauhakika wa Kuwarithisha watoto wake eneo ambalo ni salama na bila kuwa na ugomvi na majirani wenzake.

Nae Sospiter Sabuni mkazi wa Mugera amesema hati hiyo anaweza kunufaika nayo kwa shughuli mbali mbali wananchi wengi wamekuwa wakipoteza uhai kwaajili ya kugombea maeneo, na wengine wamepoteza haki zao za kumiliki kwakuwa hawana hati lakini baada ya Kuwa na hati wanauwezo pia wa kupata fidia pindi wanapokuwa maeneo yao yeamechukuliwa kwa shughuli zingine za maendeleo kwa kutumia hati hizo wanaweza kupata fidia.
Kwa Mujibu wa Sera ya Taifa ya Ardhi na Sheria za Ardhi Namba nne ya mwaka 1999, sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba tano ya mwaka 1999 , sheria ya mpango ya matumizi bora ya Ardhi Namba sita ya mwaka 2007 kila Kijiji hakina budi kuandaa mpango wa amatumizi bora ya ardhi kwa madhumuni ya kuwezesha usimamizi na matumizi endelevu ya ardhi na maliasili na rasilimali zake zote.

Wizara yazindua mradi wa VVU na Ukimwi kwa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Nchini

0
0
Na Anthony Ishengoma Singida.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida kwa lengo la kuutambulisha kwa jamii kuhusu wasichana na wanawake vijana walio shuleni na walio nje mfumo wa Elimu.

Mradi huu unatekelezwa na  Wizara pamoja na wadau wa Maendeleo kutoka AMREF, TAYOA, TASAF, TACAIDS na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund na wakati huu mradi uko katika hatua ya majaribio katika mikoa mitatu ya Tanzania ambayo ni Singida, Dodoma na Morogoro.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mradi huu mapema leo mjini Singida Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba amesema kimsingi Wizara yake imepewa jukumu la kuandaa mazingira rafiki na wezeshi ya utekelezaji wa Mradi huu na ndiyo maana hatua ya awali ya maandalizi inaanzia kwa kujenga uwezo kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka mikoa ya majaribio ya mradi.

Aidha Bw. Katemba amesema Serikali ya Tanzania imepata ruzuku kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya  Ukimwi Nchini  kwa kipindi cha January 2018 mpaka Desemba 2020.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba  akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
 Mkurugenzi wa Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza na wajumbe wa Mkutano wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akitoa neno la shukrani kwa viongozi wa Wizara hawako pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
Uongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Taasisi za TASAF na TACAIDS na wadau wa maendeleo kutoka Amref na TAYOA wakiwa katika picha ya pamoja  wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali, NSSF wajipanga kumaliza tatizo la uhaba wa maji jiji la Dar es Salaam.

0
0
Morogoro, June 4, 2018:SERIKALI kwa kushirikikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF wamejipanga kutekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la Kidunda, hatua inayotajwa kuwa itatatua kabisa tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Dar es Salaam katika kipindi chote cha mwaka.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo katika kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi Wilaya ya Morogoro Vijijini, Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwelwe alisema mradi huo unalenga kufanikisha adhma ya Rais John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa Viwanda.
"Tunapozungumzia ustawi wa uchumi wa viwanda hususani kwa jiji la Dar es Salaam ni lazima kuwepo pia na upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika katika kipindi chote cha mwaka. Changamoto iliyopo sasa ni kupungua kwa kiasi cha maji katika Mto Ruvu hususani katika miezi ya Septemba na Oktoba, hivyo mradi huu unakwenda kuhakikisha mto Ruvu unakuwa na uhakika wa maji katika kipindi chote cha mwaka'' alisema.
Kwa mujibu wa Mhandisi Kamwene, mradi huo utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu ni wazo la zamani likiwepo tangu serikali ya awamu ya kwanza chini Mwalimu Julius Nyerere na kwamba utekelezaji wake katika kipindi hiki ni mwendelezo wa adhma ya Rais Magufuli ya kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa.
"Kukamilika kwa mradi huu tafsiri yake ni kwamba huduma ya maji katika la Dar es Salaam inakuwa ni ya uhakika katika kipindi cha mwaka mzima'' alisisitiza.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwene (alievaa kofia ngumu) akifuatilia maelezo ya Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Prof Felix Mtalo (wa pili kushoto)kuhusu mradi mkubwa wa Bwawa la Kidunda kutoka utakaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF alipotembelea eneo la mradi huo katika kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi Wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (katikati). 
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwene (kulia) akibadilishana mawazo na wadau muhimu wa mradi huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephene Kebwe (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (wa pili kushoto) Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Attilio Mwang'ingo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara hiyo.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwene (katikati) akiongozana akiongoza msafara wa wadau kuelekea eneo la mradi wakati wa ziara hiyo. Wengine ni pamoja na Mkoa wa Morogoro, Dk Stephene Kebwe (kushoto) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba (kulia). 
 Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka NSSF pamoja na DAWASA wakibadilishana mawazo wakati wa ziara hiyo.
Mchoro wa Mradi wa Bwawa la Kidunda.

UMEME NI NISHATI MBADALA ILIYO NAFUU KWA MATUMIZI YA NYUMBANI: KAMOTE

0
0

 Bw. Ally M. Koyya, (kulia), kutoka idara ya Masoko TANESCO, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea kwenye banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Nishati Mbadala yanayokwenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 4, 2018.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limesema hakuna sababu yoyote kwa wananchi kuogopa kutumia nishati ya umeme kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani kwani ni nafuu mno ukilinganisha na nishati nyingine.

Afisa Mazingira wa Shirika hilo, Bw.Yusuf Kamote, amesema hayo kwenye maonesho ya Nishati mbadala ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni 4, 2018, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mkaa ni ghali tutumie Nishati mbadala”.

“Siku zote tunasema umeme wa TANESCO ni umeme wa bei nafuu, jambo la msingi ambalo wananchi wanapaswa kuelewa ni matumizi sahihi ya vifaa vya umeme kulingana na mahitaji.” Alisema.
Alisema kwa mfano mtu anatumia kifaa kinachohitaji WATI100 (100watts) kwa saa moja lakini anatumia kifaa cha WATI 200 (200Watts) kwa saa na kwa mahitaji yanayofanana, bila shaka hayo sio matumizi bora ya umeme.
Bw. Kamote pia alishauri, wananchi wanapotaka kununua vifaa vya umeme, wanapaswa kukague kiasi cha umeme kinachohitajika kwenye kifaa husika anachotaka kununua na vifaa hivyo hupimwa kwa kutumia WATI(Watt ).

 Wanafunzi wa shule ya sekondari Kanosa ya jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya kitaalamu na wataalamu wa TANESCO (Kushoto).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Njombe, Ruvuma kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, Septemba

0
0
Na Greyson Mwase, Makambako
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako kilichopo mkoani Njombe.
Kalemani aliyasema hayo leo tarehe 03 Juni, 2018 mara baada ya kukamilika kwa ziara yake katika kituo ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya Njombe na Ruvuma kwa ajili ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme nchini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Alisema kuwa, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea mapema mwezi Septemba mikoa ya Njombe na Ruvuma itaunganishwa rasmi na Gridi ya Taifa na kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Aliendelea kufafanua kuwa, kuingizwa kwa mikoa husika kwenye Gridi ya Taifa kutalipunguzia Shirika la TANESCO gharama kubwa inayotokana na matumizi ya mitambo ya mafuta mazito. 
Katika hatua nyingine, Dkt. Kalemani alielekeza kampuni  inayojihusisha na usambazaji wa umeme mkoani Njombe na Ruvuma ya Isolux kutoka Spain kuongeza kasi ya usambazaji ili wananchi waweze kupata umeme wa uhakika.
“ Haiwezekani wananchi wanakosa huduma ya nishati ya umeme wa uhakika kutokana na kusuasua kwa ukamilishwaji wa miradi ya umeme,” alisema Waziri Kalemani.
Awali akielezea utekelezaji wa mradi wa umeme wa Makambako – Songea, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Didas Lyamuya alisema  lengo la mradi lilikuwa ni kujenga njia kuu ya usafirishaji  umeme wa msongo wa kV 220, yenye urefu wa kilomita 245 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba.
 Meneja Mradi wa Mradi wa Umeme wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya (kulia mbele) akielezea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati mbele) mara alipofanya ziara katika kituo hicho Juni 03, 
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati mbele) akiendelea na ziara katika kituo cha kupoza umeme cha Makambako kilichopo mkoani Njombe Juni 03, 2018
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mbele) akiendelea na ziara ya ukaguzi wa kituo cha kupoza umeme cha Madaba kilichopo mkoani Ruvuma.
 Kituo cha Kupoza Umeme cha Makambako kama kinavyoonekana pichani


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKADIRIO YA UJENZI WA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI MURRIET KUPITIWA UPYA

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Fabian Daqorro kuhakikisha anaunda timu ya wataalam kuchunguza ubora wa mabati yaliyotumika katika ujenzi wa kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika kata ya Murriet Halmashauri ya jiji la Arusha 

Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha Afya cha Murriet kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimepatiwa shilingi milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya wodi ya Wazazi, Maabara, chumba cha upasuaji na chumba cha kuhifadhia maiti

Mhe Kandege amemtaka kuhakikisha anachunguza gharama za ujenzi wa majengo hasa jengo la kuhifadhia maiti kwa kuwa gharama yake ni kubwa ikilinganishwa na ramani zilizotolewa na Serikali kwa nchi nzima kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo. 

Amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya kuhakikisha wanafanya mapitio mapya ya makadiri ya ujenzi yaliyofanyika katika jengo la kuhifadhia Maiti ambapo gharama iliyokadiriwa ni shilingi milioni 51. Kwa jengo hilo.

“Sijaridhishwa na makadirio ya ujenzi yaliyofanyika katika jengo la kuhifadhia maiti kwa kuwa ramani hizo zimetolewa na Serikali nchi nzima kwa ajili ya ujenzi huo, hivyo namtaka Mkuu wa Wilaya kufanya mapitio mapya ya makadirio ya ujenzi wa jengo hilo.Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini hivyo inahitaji kuona thamani ya majengo yanayojengwa yanaenda sambamba na fedha zilizotolewa na Serikali.

Mhe. Kandege ameziagiza Halmashauri zote nchini kubana matumizi ili kiasi cha fedha kitakachotolewa na Serikali kitumike kuongeza majengo mengine na kuimarisha yaliyopo ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii.Ameelekeza chumba cha kujifungulia akina mama wajawazito kitenganishwe kila kitanda ili kuwa na usiri mama mjamzito anapojifungua.

Aidha Mhe. Kandege ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Arusha kuhakikisha Ujenzi wa vituo vya afya unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma za afya karibu na maeneo wanavyoishi.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Athumani Kihamia amesema jumla ya shilingi milioni 700 zimepokelewa kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la OPD pamoja na kujenga majengo ya wodi ya wazazi, Maabara, chumba cha upasuaji na chumba cha kuifadhia maiti ambapo zaidi ya shilingi milioni 462 zimetumika.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akitoa maelekezo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua baadhi ya majengo yaliyojengwa katika Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Jengo la Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha , Jijini Arusha.

1 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege akikagua baadhi ya mabati yaliyotumika katika ujenzi wa Kituo cha afya cha Murriet kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Hotuba Ya Bajeti Wizara Ya Fedha Na Mipango 2018/19 iliyowasilishwa leo Bungeni na Dkt Mpango

0
0
 
Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Philip Mpangango (MB.) akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2018/19 mjini Dodoma leo.

RAIS MAGUFULI AZINDUA AWAMU YA PILI YA PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO (ASDP ll) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018. Anayemshikia kitabu hicho ya Programu ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassa Mwinyi nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahamoud Hassan Mgimwa nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihela Chibunda nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kukabidhiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Reginald mengi  nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kukabidhiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  

Picha na IKULU

MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP LIVE NDANI YA STARTIMES

0
0
Katika kipindi ambacho ligi zimefikia zimefikia tamati, katika king’amuzi cha StarTimes burudani bado inaendelea. Sasa ni michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inafanyika nchini Kenya na kushirkisha jumla ya timu nane kutoka Tanzania na Kenya.

Tanzania inawakilishwa na timu nne ambazo ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2017/18 Simba, Yanga, Singida United na JKU ambao ni mabingwa kwa Upande wa visiwani Zanzibar. Timu hizo zinashiriki mashindano haya kwa kuwa zote ziko chini ya udhamini wa SportPesa.

Michuano hiyo imeanza kutimua vumbi tar 3 Juni itafikia tamati tar 10 Juni, na mechi zote ziko Mubashara katika kiwango cha HD kupitia king’amuzi cha StarTimes kupitia chaneli ya michezo ya Sport Focus namba 240 na ST Swahili namba 400. 

“Ili mteja aweze kutazama mechi hizi atatakiwa kulipia kifurushi cha Mambo, pia anaweza kufanya malipo ya siku na akatizama mechi ambazo anazipenda”, alisema Meneja Masoko wa Kampuni ya StarTimes, Ndg David Malisa akizungumza na waandishi wa Habari. 

Timu za Tanzania zinaendelea na uwakilishi wake, na mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili na utakuwa Mubashara kupitia Sports Focus na ST Swahili ndan ya king’amuzi cha StarTimes. Mshindi wa mchezo wa fainali atapata nafasi ya kucheza na klabu ya Everton inayoshiriki ligi Kuu ya nchini Uingereza katika dimba lao la nyumbani ST Goodison Park huko Merseyside. 

MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA MIRADI YA THAMANI BILIONI11MKOANI RUVUMA

0
0
Na Lituh, Nyasa

Mwenge wa Uhuru umeamenza mbio zake kwenye mkoa wa Ruvuma jana katika kijiji cha Lituhi wilaya ya Nyasa ambapo utatembelea miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni11.

Akitoa taarifa ya mkoa kuhusu mbio hizo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alisema miradi 20 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.2 itazinduliwa, miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 itawekewa mawe ya msingi na miradi 13 yenye thamani ya bilioni 1.5 itafunguliwa na mwenge wa uhuru
Mndeme aliongeza kusema ipo miradi 18 yenye thamani ya bilioni 1.4 itakaguliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa mkoa huyo alimweleza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kuwa miradi yote imefanyiwa uhakiki na maandalizi ya kutosha kukidhi ubora unatakiwa.
Alionya watumishi na watendaji wa serekali ambao watabainika kuhujumu miradi ya wananchi au kutumia vibaya fedha za umma kuwa serikali haitosita kuchukua hatua haraka.
"Katika utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ya wananchi kwenye mkoa wangu sitomvumilia mtumishi atakayeharibu miradi na kufuja fedha" alisisitiza Mndeme
Mkuu wa mkoa alieleza pia kuwa mkoa unaendelea na kazi ya kauli mbiu ya mwaka huu kusimamia elimu kwa kuhakikisha sera ya elimu bila malipo inatekelezwa kote kwa watoto kupelekwa shule bila vikwazo.
Kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI mkoa wa Ruvuma una maambukizi ya asilimia 5.5 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ya kile cha kitaifa asilimia 4.7 ambapo mikakati ya kudhibiti inatekelezwa pamoja na wadau.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Chares Kabeho ameupongeza mkoa wa Ruvuma kwa kuwa miongoni mwa mikoa yenye utoro hafifu wa wanafunzi mashuleni.
Ameagiza mkoa kuhakikisha unasimamia mkakati wa upatikanaji wa chakula mashulen kama ilivyofanikiwa mikoa ya Njombe na Kilimanjaro.
"Ruvuma mnacho chakula cha kutosha lakini shule zenu nyingi hazitoi chakula kwa wanafunzi,igeni kwa Njombe na Kilimanjaro namna walivyofanikiwa" alisema Kabeho
Kabeho alisema Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli inataka wazazi na walezi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao na hii itasaidia kukuza taaluma na kuondoka mdondoko wa watoto kutimiza ndoto zao.
Mwenge wa Uhur utakimbizwa umbali wa kilometa 1,27 katika hlmashaur nane za mkoa wa Ruvuma.

MATUKIO MBALIMBALI YA SPIKA WA BUNGE JIJINI DODOMA

0
0
Wageni Mbali mbali wakiwemo Manaibu Makatibu Wakuu, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Makamishna wa Bajeti na Sera wakisikiliza hotuba ambapo Wizara ya Fedha na Mipango ilikuwa ikiwasilisha Bajeti yake leo Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Son (kulia) leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Mount Everest kutoka Jijini Dar es Salaam, leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia)akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari TUSIIME kutoka Jijini Dar es Salaam, leo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Mbunge wa Segerea, Mhe. Bonnah kaluwa

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA

0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Viongozi wa Jimbo hilo wataendelea kuwaunga mkono  Wananchi wao hasa Vijana na Akina Mama walioamua kujituma katika muelekeo wa kujitafutia Maendeleo ili kujenga hatma njema ya maisha yao.

Alisema misaada ya kuyawezesha Makundi hayo katika kuyapatia vifaa, mtaji sambamba na  maarifa itakuwa ikiendelea kila wakati kulingana na mahitaji halisi ya Wananchi ikilenga zaidi katika Vikundi vya Ushirika.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akikabidhi msaada wa  Mashine iliyoitanguliwa  na  Boti ya kuvulia Samaki  aliyoitoa kwa Kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Bahati Abeid Nassir kwa ajili ya Vijana wa  Kikundi cha Hamasa cha Jimbo la Mahonda chenye Mastakimu yake Kijiji cha Fujoni hafla iliyofanyika Nyumbani kwake Kama Kaskazini kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema hakuna Tajiri au Kikundi cha Jamii kilichopata utajiri wa kushtukia  bila ya kufanya kazi za ziada katika kujitafutia riziki ambazo Wanakikundi hao watalazimika kufanya jitihada zitakazowawezesha kujikwamua kutoka  katika mazingira magumu ya maisha.

Balozi Seif  aliwatahadharisha Wanachama wa Kikundi hicho cha Hamasa kwamba msaada huo wa Boti na Mshine yake  usije geuka kuwa chanzo cha  kuleta mifarakano baina yao.

Aliwataka Wanakikundi hao wapatao 50 walio jinsia mbili tofauti  wafanye kazi kwa juhudi zao zote ili vifaa vya msaada waliopatiwa  viwezeshe kuzaa vyengine kwa lengo la kutanua mradi wao unaopaswa kuwa wa kudumu.
  Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akimkabidhi Mashine ya Boti Katibu wa Kikundi cha Hamasisha cha Jimbo la Mahonda Bibi  Mwanapatima Othman Salum kwa ajili ya shughuli za Uvuvi za Kikundi hicho. Kati kati yao ni Mkuu wa Nidhamu wa Kikundi cha Hamasa Bwana Kichamu Haji Abdullah.
 Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Sul;eiman Iddi akitoa nasaha kwa Wanachama wa Kikundi cha Hamasa mara baada ya kukabidhiwa Mashine ya Boti hapo nyumbani kwae Kama.
 Mkuu wa Nidhamu wa Kikundi cha Hamasa Bwana Kichamu Haji Abdullah kwa niaba ya wana kikundi wenzake akitoa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Mahonda  kwa uamuzi wao wa kuwapatia  Boti pamoja na Mashine yake kwa ajili ya shughuli za Uvuvi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika pamoja na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi yake katika futari ya pamoja iliyofanyika kwenye Makaazi yake Kama.
 Baadhi na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijipatia vyakula kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa neon la shukrani mara baada ya futari ya pamoja iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Seif. Picha na – OMPR – ZNZ.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images