Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KRANTZ MANTEPELE ni miongoni mwa Bloggers 50 duniani walioalikwa kiushuhudia kombe la dunia Urusi

$
0
0
Mwanablogu kutoka Tanzania Krantz Mwantepele kutoka blog ya Mwanaharakati Mzalendo amechaguliwa na serikali ya Russia kuwa miongoni mwa Bloggers na social media influencers 50 dunia nzima kutembelea nchi hiyo kabla michuano hiyo haijaanza mapema Juni 14.
Mtanzania huyo pamoja na wenzake atapata fursa ya kutembelea viwanja vyote 5 ambavyo ni Krestovsky Stadim, Fisht Olympic Stadium, Cosco Arena, pamona na Ekaterinburg Arena.z
Krantz ambaye pia ni Katibu wa Tanzania Bloggers Network (TBN), alisema yeye aliomba nafasi hiyo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kutumiwa link na marafiki zake.
“Nafurahi kuwa mmoja ya Bloggers na social media influencers 50 dunia nzima kualikwa na serikali ya Urusi kufanya Coverage ya kombe la dunia na vivutio mbali mbali vya nchini humo,” alisema Krant.

Krantz akikabidhiwa bendera na Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi. 
Aliongeza, “Nitakuwa balozi mzuri pia wa utalii wa hapa nchini kwa udhamini mkubwa wa Wonderfultanzania, Nitawakilisha vizuri huko ughaibuni Endelea kufuatilia na koncept_tv na Mwanaharakati Mzalendo Blog nitakupa exclusive zote kupitia huko,”
Mwanabloger huyo pia alipongezwa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali pamoja na kukabidhiwa bendera ya Tanzania na Mkurungezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi.

WAKULIMA KUNUFAIKA NA BIMA YA KILIMO KUANZISHA MWAKA HUU- KAMANGA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

SHIRIKA la bima la Taifa la Tanzania (NIC), limelenga kuanzisha bima ya kilimo mwaka huu, ambayo itasaidia kuwapa usingizi wakulima mbalimbali nchini, waweze kunufaika kwa kujikinga na majanga .

Mkurugenzi mtendaji wa NIC ,Sam Kamanga (pichani), aliweka bayana juu ya mpango huo ,wakati akitolea ufafanuzi masuala ya bima za majanga, wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Alieleza, wamelenga kuanzisha program hiyo wakati wa siku ya wakulima, nanenane na sabasaba mwaka 2018.

"Katika program zetu tunaianzisha program hii ya bima ya kilimo ,kusudi kumpa mkulima nafuu ,kwani ni asilimia 75 ya watanzania wananufaika na kilimo"

"Kukitokea majanga wakulima hao huwa wakipoteza muelekeo ,tunataka kumpa usingizi mlaji ,hata akitokewa na janga shambani ama gari lake limeangukiwa na mti awe anajua atakingwa na kulindwa na bima yake" alifafanua Kamanga.

Akielezea baadhi ya gharama za kukata bima , Kamanga alisema nyumba ya yenye thamani ya Tsh.mil 30 bima yake kwa mwaka haizidi 150,000 .#

" Bima zetu zinaendana na uwiano na kutokana na gharama na thamani, mfano gari uliyonunua kwa gharama ya Tsh.milioni 400 unakatiwa bima ya mil.13 "

"Ni gharama kidogo na nafuu sana ,nikikupa hapa dada yangu 150,000 ambayo ni bima ya nyumba ukienda salun unaweza kusema 150,000 haitoshi ,maana wengine mnanunua wigi la milioni moja ,sasa kwanini usijikatie bima ya nyumba, kilimo ama gari yako  ??!alihoji Kamanga.


Aidha Kamanga alieleza ,bado uelewa kwa wananchi haujawa mkubwa ,kwani wengi wao wanajua bima hizo zinawahusu watu walio matajiri pekee.


Kwa mujibu wake, hakuna elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa bima ya majanga kama ilivyo bima ya afya. Aliwataka wananchi ,kubadilika  na kujiwekea utamaduni wa kujilinda na mali zao kabla ya hatari.

"Tatizo utamaduni tuliojiwekea tunataka kusaidiana likitokea janga la moto, msiba  ,wakati inatakiwa kujiwekea mwenyewe pia kabla ya janga ama shida ,:;"Kizazi kinachokuja inabidi tubadilike na utamaduni huu kama ilivyo kwa wenzetu katika baadhi ya nchi" alisema.

Hata hivyo ,Kamanga alisema ,wamejiwekea kuwa karibu na wananchi kwenye changamoto zao za kijamii ikiwemo afya na elimu. Alisema wameanza kutekeleza katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Sumbawanga na wilaya ya Kisarawe -Pwani ikiwa ni miongozo ya utawala bora kwa kushiriki kutatua changamoto ndani ya jamii.

DKT. KIJAJI AITAKA BENKI YA ABC KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI KUCHOCHEA SEKTA YA KILIMO NA VIWANDA

UKUSANYAJI WA MAPATO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAONGEZEKA HADI KUFIKIA ASILIMIA 16

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Zanzibar 

Wastani wa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha miezi 10 ya Mwaka wa Fedha 2017/18 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki umeongezeka hadi kufikia asilimia 16 ukilinganisha na asilimia 14 katika kipindi kama hicho cha 2016/17. 

Hayo yamesemwa na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere baada ya kumaliza Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya hiyo kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambacho TRA ilikuwa mwenyeji.

"Katika kikao hiki tulichomaliza leo, tumejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafanikio tuliyoyapata ambayo ni kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato katika Jumuiya yetu kutoka asilimia 14 kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 hadi kufikia asilimia16 katika kipindi kama hicho cha Mwaka huu wa Fedha wa 2017/18", alisema Kichere. 

Kichere alieleza kuwa, pamoja na mafanikio hayo, kikao hicho kimejadili na kukubaliana masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha utozaji kodi kwa watu binafsi na wafanyabiashara wadogo na kuweka mipango mahususi ya kutoza kodi stahiki kutoka kwa wafanyabiashara hao. 

"Pia, tumekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupeana taarifa na kuonyeshana mianya ya ukwepaji kodi ili kudhibiti na kukomesha hali hiyo," alibainisha Kichere.

Makubaliano mengine ni pamoja na kuweka mikakati mahususi ya kushughulikia masuala ya uadilifu kwa kuwa, Mamlaka za Mapato za Afrika Mashariki kama ilivyo kwenye taasisi nyingine za Serikali ndani ya Jumuiya, kumekuwa na changamoto hiyo ya uadilifu. Hivyo, Makamishna Wakuu hao wamekubaliana kuongeza ufanisi katika kukagua mwenendo wa maisha wa watumishi wa Mamlaka zao ikiwa ni pamoja na kuwashitaki wale wote ambao si waadilifu kama sehemu ya kupambana na rushwa. 

"Ndugu waandishi wa habari, pamoja na kupambana na rushwa, tumekubaliana pia kupunguza gharama za mifumo ya TEHAMA kwa kuwajengea uwezo watumishi wa ndani ya Mamlaka ili kupunguza gharama ambazo zinatumika kuwalipa watalaam kutoka katika mataifa mengine," aliongeza Kichere.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambapo TRA ilikuwa mwenyeji. Kushoto ni Mhe. Audace Niyonzima wa Mamlaka ya Mapato Burundi na kulia ni Bi. Doris Akol, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA).

 Mwenyekiti wa Kamati ya Watalaam wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mahariki Bi. Martine Nibasumba kutoka Mamlaka ya Mapato Burundi (OBR) akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo kwa Makamishna Wakuu (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya hiyo kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambapo TRA ilikuwa mwenyeji.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wakuu wenzake na baadhi ya wajumbe wa Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambapo TRA ilikuwa mwenyeji.


Balozi Seif afanya mazungumzo na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Jamuhuri ya Cuba kwa kumaliza Uchaguzi wa Bunge salama wa kuwachagua Wajumbe wa Baraza Kuu la Nguvu ya Umma lenye Mamlaka ya kumchagua Rais wa Baraza la Taifa la Nchi hiyo.

Alisema uchaguzi huo uliofanyika Mnamo Tarehe 11 Machi, 2018,  ambapo Wajumbe wa Baraza la Taifa la Cuba walimchaguwa Bwana Miguel Diaz –Canel kuwa Rais wa Nchi hiyo aliyekuwa msaidizi wa Kiongozi wa Taifa hilo Bwana Raul Castro ulikuwa na amani na kushuhudiwa na Jumuiya za Kimataifa.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa pongezi hizo wakati akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernandes kwenye Makazi yake Jijini  Dar es salaam.

Alisema kufuatia kumalizika kwa uchaguzi  huo Tanzania na Cuba zitaendelea kupata wasaa zaidi wa kushirikiana katika masuala na sekta zilizoanzishwa ambazo ana matumaini ya kuendelezwa chini ya Rais huyo Mpya wa Cuba Bwana Maguel Diaz – Canel mwenye fikra za watangulizi wake waliolenga kuona ustawi wa Bara la Afrika unaimarika na kukua siku hadi siku.

Akitoa shukrani zake Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernandes alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Cuba itaendelea kuiunga Mkono Tanzania hasa katika masuala ya Elimu na Afya.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akisalimiana na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo alipofika kwenye Makaazi yake Jijini Dar es salaam kumpongeza kwa Cuba kumaliza Uchaguzi wa Rais salama.
Balozi Seif akitia saini Kitabu cha Wageni mara baada ya kukaribishwa kwenye Ubalozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Jijini  Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziabr Balozi Seif  Kulia na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Prifesa Lucas Domingo  Kushoto wakibadilishana mawazo kwenye Makaazi ya Balozi wa Cuba Jijini Dar es salaam.
Balozi Seif na Profesa Lucan akiangalia baadhi ya Picha na matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye Maktaba ya Ubalozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi Kulia na Mke wa Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mama Melyin Suazez Alvarez  Kati kati Wakimfanyia mzaha Mtoto wa Mke wa Balozi Huyo aitwae Evelyn Hernandes Suarez.
Balozi Seif akiagana na Mke wa Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Mama  Melyin Suarez Alvarez. Kati kati yao ni Balozi Lucas Domingo Hernandes na Mtoto wake  Evelyn Hernandes Suarez. Picha na – OMPR – ZNZ.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Airtel na itel wazindua SMARTPHONE mpya ya A32 F na Bando la Airtel BURE miezi sita

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel leo kwa pamoja wamezindua simu mpya ya itel A32 F iliyoambatanishwa na offer ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 12, dakika 300 pamoja na sms 300 kwa muda wa miezi 6 mfululizo.

Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel  na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A32F. Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia  wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuuu, Hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na  uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel.  

Simu ya A32 F itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa  na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 12GB chenye muda wa miezi sita ambapo kila mwezi ni 2GB pamoja na nyongeza ya sms 300 na dakika 300 zote kutoka Airtel Tanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam kutoka itel Mobile Mr. Walle XU, alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A32 F ambayo ni smartphone ya kwanza kutumia alama za vidole (finger print) yenye AndroidTM  Oreo™ ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima. Simu ya A32 F ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu, alisema Khosla.

Bwana Walle aliongeza kuwa itel A32 F ina usalama na uhakika kwa kuwa inauwezo wa kutambua vidole vya mwenye simu na iweza kuweka programu nane ambazo zinatumika kwa matumizi mbalimbali kama kupiga picha, kupiga video, kupokea simu, stop alarm pamoja kusajili vidole vitano ambavyo kila kidole kinakuwa na kazi yake maalum

Alisema vifaa vingine ni ukumbwa wake wa inch 5.0 pamoja na kamera ya kisasa ya 5mp kwa nyuma na mbele 2mp na inaweza kupiga picha kwa mazingira yeyote yale. Pia simu hiyo ina memory ya 8GB+1GB ambazo zinaweza kuzidi mpaka 32GB.
 Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu  na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
 Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu- kulia Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kati ni  Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo  na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu  baada ya kuzindua simu mpya ya A32 F ya smartphone kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania.  Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MAONESHO YA MADINI BUNGENI DODOMA

$
0
0
Na Veronica Simba
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo Mei 30, amefungua rasmi maonesho ya madini katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma na kuipongeza Wizara ya Madini kwa kuyaandaa.
Akitoa hotuba ya ufunguzi, Ndugai alimpongeza Waziri mwenye dhamana, Angellah Kairuki pamoja na watendaji wa Wizara, kwa juhudi kubwa za kutangaza na kulinda rasilimali ya madini hapa nchini. Alisisitiza kuwa, anatumaini juhudi hizo zitaendelezwa ili kuiwezesha sekta husika kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa letu.
Alisema kwamba Wizara ya Madini inalo jukumu kubwa la kuufahamisha umma kuhusu sekta husika kupitia njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari na maonesho mbalimbali.
“Maonesho haya yamekuja wakati muafaka kwa sababu kipindi hiki nchi yetu iko katika mageuzi makubwa katika sekta ya madini; na ninyi wizara mnawajibika kuifanikisha azma hii kwa njia mbalimbali, hususan vyombo vya habari na maonesho kama haya.”
Aidha, Spika aliwataka wadau mbalimbali wa madini kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo, ikiwa ni pamoja na usalama wa wafanyakazi wao na kulipa kodi za Serikali.
Kuhusu suala la uongezaji thamani madini kabla ya kuyauza, Ndugai alisema kwamba hilo ni suala muhimu sana kwa kuzingatia sera ya nchi ya kuwezesha uchumi wa viwanda. “Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo tutajenga viwanda ambavyo vitatoa fursa ya ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi yetu,” alisisitiza.
Akizungumzia mchango wa Bunge katika kukuza sekta ya madini, alisema Bunge limekuwa makini katika kuhakikisha uwekezaji kwenye sekta husika unakuwa wenye tija na manufaa kwa pande zote; yaani Serikali, Taifa na wawekezaji.
“Tuliunda Kamati mbalimbali za ufuatiliaji wa sekta ya madini. Nafurahi kuwaambia kwamba mambo yamekuwa yakiboreka siku hadi siku. Nawasihi tuendelee hivyohivyo kwa manufaa ya pande zote.”
Awali, akimkaribisha Spika kufungua maonesho husika; Waziri Kairuki alisema kuwa, Wizara imeandaa maonesho hayo kwa kuzingatia kuwa ni Wizara mpya hivyo inahitaji kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake; yakijumuisha dhima na dira.
“Baada ya Bunge lako tukufu kuifanyia marekebisho Sheria ya Madini Namba 14 ya Mwaka 2010, kupitia marekebisho ya Sheria Namba 7 ya Mwaka 2017, Wizara yangu imekuwa na jukumu kubwa la kutekeleza maelekezo ya Sheria hiyo.”
Maonesho hayo ya siku tatu, yaliyoanza Mei 30 na kutarajiwa kuhitimishwa Juni Mosi; yameshirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali, Shirikisho la Wachimbaji Wakubwa (TCME) na Kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji na uongezaji thamani madini.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya madini katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 31 mwaka huu. Wengine pichani (kutoka kulia), ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Simon Msanjila.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (katikati), akiangalia aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini, alipotembelea Banda la Chuo cha Madini (MRI) wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 31 mwaka huu.
 Mjasiriamali anayejishughulisha na uongezaji thamani madini kwa kutengeneza na kuuza bidhaa mbalimbali za urembo, Susie Kennedy (mwenye blauzi nyeupe), akimwonesha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, moja ya bidhaa anazotengeneza kutokana na madini; wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 31 mwaka huu. Kushoto ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, akiangali bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya Tancoal, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 31 mwaka huu. Pamoja naye pichani ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu wa Wizara, Prof Simon Msanjila na Kamishna wa Madini Prof Shukrani Manya.

BREAKING NEWS:: ZINEDINE ZIDANE AACHIA NGAZI REAL MADRID

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane 'Zizzou' mchana wa leo ametangaza kuachia ngazi kama Kocha Mkuu wa kikosi hivyo baada yakutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).

Zidane (45) alijiunga na Real Madrid mwaka 2014 akianza kukinoa kikosi cha Castilla (Real Madrid B).

Zidane alichukua mikoba ya Rafael Benitez aliyeondoka kwenye Kikosi cha kwanza hapo January 2016 .

Kwenye Mkutano wake na Waandishi wa Habari nchini Hispania, Zidane ameeleza kwamba: "Kila kitu kina mabadiliko na ndio maana nimefanya maamuzi haya, naipenda Madrid".

"Nafikiri Madrid inahitaji kushinda mataji zaidi, nafikiri pia mabadiliko yanahitajika", ameongeza Zizzou. 

Alipata mafanikio na Real Madrid kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuiondoa Atletico Madrid kwenye Fainali ya Michuano hiyo barani Ulaya, alipatetea Kombe hilo mwaka unaofuata na kuweka historia mpaka sasa licha yakukosa taji la La Liga msimu wa 2017-2018

TASWIRA MBALIMBALI MARA BAADA YA BUNGE KURIDHIA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI

$
0
0
Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimpongeza Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (kushoto) Dorothy Mwanyika akimpongeza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt. Angeline Mabulla mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (kushoto) Dkt. Moses Kusiluka akimpongeza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt. Angeline Mabulla mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19.
  Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwapongeza Waziri wa Ardhi na Naibu wake mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19
 Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimpongeza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt. Angeline Mabulla mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19.
 Baadhi ya Makamishna wa Ardhi wa kanda 8 zilizopo nchi nzima kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (katikati) Dorothy Mwanyika akimpongeza Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi  mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo Sh73.07 bilioni kwa ajili ya mwaka 2018/19.
Picha zote na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.

UNESCO TO SUPPORT ONE MONTH ANTI FGM CAMPAIGN IN 5 REGIONS

$
0
0
UNESCO is supporting the organization of a one-month anti-FGM campaign in selected districts within the five regions with high prevalence namely Manyara, Dodoma, Arusha, Mara and Singida. The campaign is organized with financial support from SDC project, Sida O3 Project and UNDAP II- VAWC One UN fund. 
The campaign kicked off in Ngorongoro on May 28 and will include a 3-day capacity-building workshop to be conducted in collaboration with Loliondo FM, a UNESCO supported community radio, followed by official launch of the campaign on 31st May and an intergeneration dialogue on ending FGM practices and traditional to be aired live by Loliondo FM. 
The workshop is meant to orient key anti-FGM campaigners including media practitioners with key messages where a major public campaign through five community radios within the top five regions will be carried out there after expected to reach 1 million people. 
Community radios for the public campaign with regions in brackets include Loliondo FM (Arusha), ORS (Manyara), Dodoma FM (Dodoma will also cover Singida), Triple A FM (Arusha), Mazingira FM (Mara). 
The key approaches for the Ngorongoro anti-FGM campaign include a Public Campaign through Community Radios highlighted where a series of community radio sessions will be developed and broadcasted targeting community leaders, law enforcers, medical personnel, religious leaders, Ngaribas and young people (particularly out of school girls. 
The other approach will involve a School-based campaign, specifically targeting pupils, students, 
teachers, and school-parent committees from 20 schools in Loliondo division.. 
Simultaneously, a Community-based campaign will take place specifically targeting parents and caretakers in 14 selected villages in Loliondo division and will take the form of parent/caretakers village/sub-village sensitization meetings. 
The campaign comes in June, a month considered as high season where parents utilize the long school holidays to circumcise their girls. 
UNESCO organizes the anti FGM campaign in close collaboration with the Ngorongoro District Council, the Council of Masaai traditional leaders and the Network of Community Media in Tanzania (TADIO) 
Through its socio-cultural approach, UNESCO’s initiatives have gained community support and achieved notable impact including change of mind-set of some of the traditional leaders and Ngaribas (the female 
circumcisers). 
The anti-FGM campaign is a continuation of similar ones conducted in June and December 2017 where 10 girls were rescued from the cut, with two being rescued from being married off to old men as old as 
68 years old. Toggle screen reader support

TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG

$
0
0
SHIRIKA la hifadhi za Taifa nchini ( TANAPA ) limemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, zahanati itakayowasaidia wananchi wa Kiijiji cha Gijedabung kata ya Endakiso Wilbayani Babati, kupata huduma ya afya hivyo kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa kilomita 15 kufuata huduma hiyo eneo la Endakiso.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, Meneja  wa ujirani  mwema Ahmed Mbugi wakati akimkabidhi mkuu huyo wa Mkoa alisema ujenzi wa jengo la zahati hiyo hilo ni wakati wa makabidhiano ya zahanati hiyo ni ushirikiano kati ya hifadhi za Taifa Tanzania kupitia  hifadhi ya Tarangire na wananchi wa kijiji cha Gijedabung.

Mbugi alisema Halmashauri ya wilaya ya Babati chini ya mkurugenzi wake Hamis Malinga ni miongoni mwa wilaya nne zinazopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, ambapo wamekua wakishirikiana katika mambo mbalimbali  yakiwemo ya uhifadhi  wa maliasili na mazingira pamoja na maendeleo ya wananchi.

"Naomba nikujulishe kwamba mpango wa ujirani mwema katika shirika la hifadhi za Taifa Tanzania kuwa ulianzishwa mwaka 1988 katika hifadhi ya Taifa Serengeti  kama mradi wa majaribio ukiwa na malengo makuu manne, moja kuweza na kuanzisha uhusiano mzuri kati ya hifadhi na jamii inayoizunguka, pili kuwezesha mpango wa kufikisha Faida za uhifadhi kwa jamii kwa urahisi zaidi, tatu kusaidia jamii kuweza kupata elimu  ya uhifadhi kwanjia rahisi, nne kubuni mpango wa kitaalam wa ushirikishwaji wadau wote wa uhifadhi kwa pamoja," alisema Mbugi.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akipanda mti kwenye eneo la zahanati ya Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati Mkoani Manyara, iliyojengwa kwa shirilingi milioni 83 ambpo shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) imechangia shilingi milioni 65 na nguvu za wananchi wa eneo hilo shilingi milioni 18.
 Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Esta Mahawe akipongezwa na Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti na viongozi wengine wa Wilaya ya Babati, baada ya mbunge huyo kumkabidhi mkuu huyo wa mkoa mashuka 10 yatakayotumika kwenye zahanati ya kijiji cha Gijedabung iliyozinduliwa na Mnyeti.
 Meneja  ujirani mwema wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi, akisoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Gijedabung kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, ambapo TANAPA ilitumia shilingi milioni 65 kujenga zahanati hiyo na nguvu za wananchi zikathaminishwa kwa shilingi milioni 18 hivyo jumla kutumika kiasi cha shilingi milioni 83 hadi kukamilika kwake.
 Kikundi cha ngoma cha Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati Mkoani Manyara, wakicheza ngoma wakati shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) lilipokabidhi zahanati ya kijiji hicho kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akimkabidhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho cheti cha kutambua mchango wake wa kusimamia maendeleo baada ya TANAPA kumkabidhi zahanati waliyojenga kwenye Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KITENGO CHA LISHE KUTOA MATONE YA VITAMIN A NA DAWA ZA MINYOO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA SITA

$
0
0
 Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya Zanzibar itaanzisha zoezi la mwezi mmoja la utoaji matone ya Vitamin A na Dawa za Minyoo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kuanzia Juni 1, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa jengo la Malaria Mwanakwerekwe, Msimamizi wa Lishe Wilaya za Magharibi Salama Makame amesema zoezi hilo litafanyika katika vituo vyote vya afya kwa siku za kazi na siku za Jumamosi na Jumapili zoeli hilo litaendelea ndani ya shehia katika vituo maalum vitakavyopangwa.

Aliwataka wazazi na walezi ambao hawatapata nafasi ya kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya kwa siku za kazi kuwapeleka katika vituo vitakavyopangwa kwenye shehia zao ili kupata matone ya Vitamin A na Dawa ya Minyoo.

Alisema lengo la Wizara ya afya kutoa matone ya ya Vitamin A na Dawa ya Minyoo kwa watoto wenye umri kuanzia miezi sita mpaka miaka mitano ni kuwaepusha na maradhi mbali mbali na kuwawezesha kukua vizuri wakiwa na afya bora.

Bi. Salama aliongeza kuwa tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa tokea kuanzishwa zoezi la kutoa matone ya Vitamin A na Dawa ya Minyoo kwa watoto imesaidia kupunguza  idadi ya vifo vya watoto hao kwa asilimia 33.

Alisema Wizara ya afya imejiandaa kuwafikia zaidi ya watoto laki mbili elfu sita Unguja na Pemba, hivyo amewashauri wazazi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao ili kufikia malengo ya yaliyowekwa.

Alikumbusha kwamba katika zoezi lililofanyika mwezi Novemba mwaka jana, watoto waliopatiwa Matone ya Vitamn A na Dawa ya Minyoo ilifikia asilimia 98 na ametaka zoezi la mwaka huu lizidi matokeo ya mwaka jana.
 AFISA Msimamizi wa Chanjo Wilaya ya Magharibi ‘A’ na ‘B’ Salama Makame Ashrak akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana zoezi la utoaji wa Matone ya Vitamen A  na dawa za Minyoo linaloanza tarehe 1 June 2018 na kumalizika tarehe 30 Juni 2018. katika ukumbi wa Malaria uliopo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
MWANDISHI wa habari wa Star TV Abdalla Pandu akiuliza Maswali  kuhusu zoezi la   utolewaji Matone ya Vitamen A na dawa za Minyoo katika ukumbi wa Malaria uliopo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar( Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar

Wakurugenzi wa Bodi wa TPA wafanya ziara bandari ya Dar es Salaam

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (wa pili kulia) akionyesha moja ya maghara yatayovunjwa ili kupisha maboresho ya kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya kisasa na yenye uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi aina ya ‘Panamax’. Wanaomsikiliza pichani ni Wakurugenzi wa Bodi ya TPA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Prof. Ignatus Rubaratuka (katikati) mara baada ya kufanya ziara bandarini hapo kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa huduma ya shehena bandarini hapo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu) wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kwa Wakurugenzi wa Bodi wa TPA mara baada ya kufanya ziara bandarini hapo kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa huduma ya shehena katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akionyesha moja ya maeneo yatakayofanyiwa ukarabati wa kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya kisasa na yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuhudumia meli kubwa aina ya ‘Panamax’ kwa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, mara baada ya Bodi hiyo kufanya ziara bandarini hapo kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa huduma ya shehena bandarini. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof. Ignatus Rubaratuka na Naibu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu), Mhandisi Karim Mattaka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof. Ignatus Rubaratuka (kulia) akikagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa huduma ya shehena ya Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Wakurugenzi wake wa Bodi na Menejimenti ya TPA.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akionyesha Wakurugenzi wa Bodi ya TPA eneo litakalojengwa mizani ya kisasa kwa ajili ya kupima uzito wa mizigo inayotoka na kuingia bandarini mara baada ya Bodi ya Wakurugenzi kufanya ziara bandarini hapo kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa huduma ya shehena bandarini.

JAFO AAGIZA KASI YA UJENZI KITUO CHA AFYA CHAMWINO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi katika kituo cha Afya Chamwino. 

Jafo ameyasema hayo alipofanya ziara kituoni hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu unaofanyika katika kituo hicho.  

Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amefurahishwa na ubora wa majengo yanayojengwa na kwamba ni vyema ikaongezwa kasi ya ujenzi ili yakamilike kwa haraka."Mafundi ongezeni kasi ya ujenzi kituo hichi cha Afya kikamilike haraka ili wananchi wapate huduma.  

Katika Zara hiyo, waziri Jafo pia amefanikiwa kufanya ukaguzi katika kituo cha Afya chamwino wilayani Chamwino pamoja na kituo cha Afya Mlali kilichopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma. 

Vituo hivyo viwili ni miongoni mwa vituo vya afya 208 vinavyoboreshwa na serikali ya awamu ya tano.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino  Athumani Masasi
 Jengo la upasuaji linalojemgwa katika kituo cha afya chamwino
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe.  Deo Ndejembi katika ukaguzi wa miundombinu ya kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa.
 Baadhi ya majengo mapya katika kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifurahishwa na uwekaji wa Tiles katika majengo mapya ya kituo cha afya Mlali Kongwa.

KINANA AKABIDHI RASMI MIKOBA KWA DK. BASHIRU OFISI NDOGO YA CCM LUMUMBA

$
0
0

 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akipunga  mikono kuwaaga wafanyakazi na Viongozi wa Ofisi ndogo ya CCM Lumumba mara baada ya kukabidhi ofisi kwa Katibu Mkuu mpya Dkt. Bashiru Aliy ambaye ameanza kazi rasmi leo.
  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukabidhi ofisi kwa katibu Mkuu mpya wa CCM.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi DK. Bashiru Ali akiwaeleza Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali vipaumble vyake katika uongozi alioupata ndani ya CCM katika awamu hii ya tano .
  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya Watendaji wa Chama Cha Mapindzui waliofika katika hafla ya kukabidhi Ofisi iliyofanyika  katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba.
  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana, akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogoro mara baada ya kumaliza kukabidhi ofisi kwa katibu mkuu mpya .
  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa CCM Lumumba.

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU KUZINDUA KAMPENI YA KUPIMA VVU NCHINI

WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA – WAZIRI MKUU

$
0
0
*Aagiza viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wabadilike
*Ataka wasimamie wananchi waachane na matumizi ya mkaa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, mashirika na taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni na mkaa.

“Wizara, taasisi na mashirika yote ya Serikali na binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji wanaotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli za uzalishaji waanze kutumia nishati mbadala ili matumizi ya mkaa yaishe na ikiwezekana yatoweke kabisa,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Mei 31, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Mkaa ni Gharama: Tumia Nishati Mbadala.”

Waziri Mkuu amesema teknolojia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala ambayo ameiona kwenye maonesho hayo, ikuzwe na kusambazwa kote nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi waachane na matumizi ya mkaa wa kawaida na badala yake watumie mkaa-mbadala kwa lengo la kuhifadhi misitu na kupunguza uharibifu wa mazingira.

Ili kufanikisha matumizi ya teknolojia hiyo, Waziri Mkuu amesema vibali vya ujenzi wa majengo makubwa na taasisi kama shule, vyuo, hospitali navyo pia vianze kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala katika taasisi na majengo makubwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya  Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu  mkaa uliotengenezwa kutoka na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Neema Matemba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabada ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda la Kituo cha Utengenezaji magari cha Nyumbu  na kujionea mashine ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kituo hicho. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Opwani Mhandisi, Evarest Ndikilo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole  wakati alipotoa maelezo kuhusu majiko makubwa yanayotumia  gesi kidogo  katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es alaam, Kate Kamba,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori  na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA NI MKOMBOZI WA WANANCHI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ilizindua sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ili kuhakikisha wakopaji wakiwemo wajasiriamali wadogo wanalindwa na kupata haki zao bila kudhurumiwa wanapo hitaji mikopo na huduma zingine za kifedha zitakazowasaidia kujiendeleza kiuchumi.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge Mhe. Khatibu Said Haji aliyetaka kujua hatua za Serikali kuhusu taasisi za huduma ndogo za kifedha (Microfinance) kuwatoza wananchi riba kubwa wanapochukua mikopo.

Dkt. Kijaji, alisema kuwa  mwezi Desemba, 2017 Serikali ilizindua sera ya huduma ndogo ya fedha itakayosaidia  kuwatambua wakopeshaji  na kuwalinda wakopaji wanaohitaji huduma katika taasisi hizo zikiwemo za mikopo.

“Tunataka kuhakikisha tunawalinda wakopaji na kuhakikisha wanakopa kwa kuzingatia sheria na taasisi hizo za fedha zinazingatia sheria, utaratibu na kanuni za utawala bora”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kukamilika kwa sheria ya huduma ndogo ya fedha hivi karibuni kutakua ni muarobaini wa kutatua changamoto za kifedha kwa wananchi wanaohitaji mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo kuhusu hatua za Serikali za kuhakikisha Benki nchini zinapunguza riba ili kuchochea shughuli za biashara, Dkt. Kijaji alisema kuwa Sekta ya Benki inafanya biashara huria na ilianza tangu mwaka 1991 baada ya kupitishwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Benki na Vyombo vya Fedha ya Mwaka 1991.

“Kupitia Sheria hiyo, wawekezaji walifungua benki binafsi nchini na gharama za huduma na bidhaa kuamuliwa na nguvu ya soko hivyo Serikali haina mamlaka ya moja kwa moja ya kupunguza viwango vya riba katika soko”, alisisitiza Dkt. Kijaji.

Hata hivyo alizitaja hatua ambazo Serikali imezichukua kwa upande wake kuwa ni pamoja na kuzitaka benki za biashara kutumia Mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji, Benki Kuu kuanza kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89 na pia kushusha riba kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0.

Hatua zingine ni Benki Kuu kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa  na Benki za biashara  kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0  na pia Serikali kuendelea kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa kwa lengo la kupunguza kiwango cha mikopo chechefu na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Aidha Naibu Waziri huyo ameipongeza benki ya CRDB, NMB na Benki ya ABC kwa kupunguza riba ya mikopo kutoka asilimia zaidi ya 20 hadi kufikia asilimia 17 hivyo kuwa na tumaini kuwa Benki zingine zitaendelea kufanya hivyo.

Serikali Yatoa Milioni 700 kwa vijana mwaka 2017/18

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa takribani shilingi milioni 700 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa vijana nchini ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuweza kuepuka utegemezi katika jamii.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana - ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Juma Abubakari alipokuwa akifungua kikao cha Jukwaa la Vijana Kitaifa cha vijana waliowezeshwa Kiuchumi kupitia mradi wa YEE unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Shirika la Plan International – Tanzania.

Abubakari amesema kuwa mradi huo ni muhimu kwa sababu unaenda sawa na Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2017 ambayo inahimiza suala la uwezeshaji vijana kiuchumi ambapo shirika hilo limejitahidi kushirikiana na Serikali kwa kuwawezesha vijana zaidi ya 10,000 kwa kuwapa stadi za ujasiriamali pamoja na elimu ya ufundi.

“Serikali inawasaidia vijana kwa kuwapa elimu kuhusu Sera, kuwatengea maeneo ya kufanyia biashara zao pamoja na kuwapa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na asilimia 4 ya mapato ya halmashauri ambayo ni kwa ajili ya vijana hivyo kwa mwaka wa fedha unaoishia tumeshatoa takriban shilingi milioni 700 kwa ajili ya kuwainua vijana,” alisema Abubakari.

Abubakari amefafanua kuwa Serikali kupitia mfuko huo ulianza kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana tangu mwaka 1993 ambapo kuanzia mwaka 2003 hadi 2018 mfuko huo umefanikiwa kutoa jumla ya shilingi bilioni nne kwa vijana nchini.

Ametoa rai kwa vijana hasa waliopata mafunzo kupitia mradi wa YEE kuendelea kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo kirahisi pamoja na kuziomba taasisi za fedha  na mabenki kuendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa YEE kutoka Shirika la Plan International, Simon Ndembeka amesema katika mradi huo shirika linajivunia kuvuka lengo na   kuwawezesha vijana 10,132 mbali na vijana 9100 waliopanga kuwafikia pamoja na kuhamasisha vijana kuunda vikundi vya uzalishaji mali zaidi ya 849 ambavyo vimepatiwa vitendea kazi vya kuanzia.

Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la vijana walionufaika na mradi wa YEE, Mwajuma Chamkono amesema kuwa lengo la jukwaa hilo ni kuishawishi Serikali na wadau wa maendeleo ya vijana kuhusiana na sera, changamoto na fursa za vijana ili kuweza kupata njia mbadala za kuwawezesha vijana kujikwamua.

“Jukwaa hili linapendekeza Serikali na taasisi za fedha zinazoingia mikataba ya utoaji mikopo kwa vijana kuweka bayana masharti na vigezo visivyosababisha vijana kuogopa kuchangamkia fursa ya mikopo kutokana na mkanganyiko wa taarifa”, alisema Bi Mwajuma.

Mradi wa YEE ni wa miaka mitatu ulianza tangu mwaka 2015, unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).  
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana - ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Juma Abubakari (aliyesimama mbele) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Jukwaa la Vijana Kitaifa cha vijana waliowezeshwa Kiuchumi kupitia mradi wa YEE unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Shirika la Plan International – Tanzania.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la vijana walionufaika na mradi wa YEE, Mwajuma Chamkono akichangia hoja wakati wa kikao cha Jukwaa la Vijana Kitaifa cha vijana waliowezeshwa Kiuchumi kupitia mradi huo unaofadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Shirika la Plan International – Tanzania.

MAFANIKIO YA ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI TIC NCHI ZA UJERUMANI NA UHOLANZI

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images