Na Angela Msimbira,
Wakuu wa Wilaya wameagizwa kuzisimamia halmashauri nchini kuhakikisha kuwa zinatenga maeneo maalum ya kufanyia biashara ndogondogo (machinga) ili waweze kuendesha shughuli zao bila kuvunja sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA uliofanyika leo katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.
Alisema Wakuu wa Wilaya wana wajibu wa kuratibu na kuhakikisha kuwa maeneo ya kufanyia bishara kwa wamachinga yanatengwa na Halmashauri ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa utaratibu bila kuvunja sheria za nchi.
Aliongeza kuwa wamachinga ni watu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wadogo ndio wanaoleta muunganiko wa watu katika kada mbalimbali wakiwemo wasomi wenye shahada, astashaada, kidato cha sita, kidato cha nne, darasa la saba na wasiosoma kabisa wote huunganika na kufanyabiashara kama wamachinga.
Alisema kati ya watanzania milioni 50, walioajiriwa serikalini na sekta ya umma ni 520,000, hivyo kundi kubwa ni la watu ambao ama wamejiajiri au wameajiriwa katika sekta binafsi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na wamachinga wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania- SHIUMA leo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dodoma, Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na baadhi ya viongozi wa shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA leo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA