Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Serikali Kuendelea Kuchukua Hatua za Kisera Kuhakikisha Riba za Mikopo Zinapungua

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali imesema kuwa pamoja na huduma za bidhaa ya fedha kuamuliwa na nguvu ya soko kwa upande wake imekuwa ikichua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo zinapungua katika soko hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Khatibu Haji juu ya Serikali inachukua hatua gani ili benki ziweze kupunguza viwango hivyo vya riba?
"Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ni pamoja na kuzitaka benki za biashara kutumia mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji (Credit Reference Bureau System). Aidha, Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89," amesema Dkt. Kijaji.
Dkt. Kijaji amezitaja hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni Benki Kuu kushusha riba (Discount Rate) kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 pamoja na kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara (Statutory Minimum Reserve Requirememnt (SMR)) kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0.
Vile vile Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa kwa lengo la kupunguza kiwango cha mikopo chechefu na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Aidha, amesema baada ya hatua hizo za kisera kuchukuliwa na Serikali, baadhi ya benki za biashara hapa nchini zimeanza kupunguza riba za mikopo.
Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo katika soko zinaendelea kupungua. 
Waziri wa Madini Mhe. Angellah   Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni  Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu  Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo  Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike  na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI  hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua stahiki.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo (wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Sehemu ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni  mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.
Sehemu ya Wanafunzi waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu. ( Picha zote na Frank Mvungi-  MAELEZO)

SINGIDA UNITED YATOLEA UFAFANUZI USAJILI WAO

MAALIM SEIF ATUMA UJUMBE KUMPONGEZA KATIBU MKUU MPYA WA CCM

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi  (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad amewasilisha barua ya pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Dk. Bashiru Ally aliyeteuliwa kuongoza chama Hicho. 
Barua hiyo ya Maalim Seif ambayo imewasilishwa na msaadizi wake Bw. Mbaralala Maharagande saa chache baada ya kumalizika kwa  shamrashamra za kukabidhiana ofisi baina ya aliyekuwa katibu mkuu aliyestaafu  Ndg. Abdulrahman Kinana kwenye ofisi ndogo za CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo. 
 Maharagande amesema kuwa Maalim Seif ameandika barua ya hiyo ya pongezi mara tu baada ya Dr. Bashiru kuteuliwa kuwa katibu Mkuu mpya wa CCM. 
 “Katibu mkuu wa chama chetu ameandika barua kumpongeza Dr Bashiru na kumpongeza Katibu Mkuu aliyestaafu Ndg. Abdulrahman Kinana kwa kuweza kuimarisha demokrasia ya vyama kwa kipindi chote alichokuwa akiongoza CCM kwa kujali maslahi ya nchi kwanza kuliko mambo binafsi”amesema Maharagande. 
Amesema Dr Bashiru ni moja ya wasomi watakaoleta mabadiliko katika mfumo huu wa vyama vingi licha ya kuwa si vyema kutabiri atakachokifanya kwani watu wajue tu kuwa kiongozi huyu ni mzalendo ambaye anaamini katika mabadiliko makubwa katika masuala ya kisiasa. 
Bw. Mbaralala Maharagande, ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi  (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad, akitoka kuwasilisha barua ya pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo.

VOA SWAHILI: Duniani Leo May 31st, 2018

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO MEI 21, 2018

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 31.05.2018

Balozi Seif Ali Iddi aipongeza Jamuhuri ya Cuba kwa kumaliza Uchaguzi wa Bunge salama

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Jamuhuri ya Cuba kwa kumaliza Uchaguzi wa Bunge salama wa kuwachagua Wajumbe wa Baraza Kuu la Nguvu ya Umma lenye Mamlaka ya kumchagua Rais wa Baraza la Taifa la Nchi hiyo. 
 Alisema uchaguzi huo uliofanyika Mnamo Tarehe 11 Machi, 2018, ambapo Wajumbe wa Baraza la Taifa la Cuba walimchaguwa Bwana Miguel Diaz-Canel kuwa Rais wa Nchi hiyo aliyekuwa msaidizi wa Kiongozi wa Taifa hilo Bwana Raul Castro ulikuwa na amani na kushuhudiwa na Jumuiya za Kimataifa. 
 Balozi Seif Ali Iddi alitoa pongezi hizo wakati akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernandes kwenye Makazi yake Jijini Dar es Salaam. 
Alisema kufuatia kumalizika kwa uchaguzi huo Tanzania na Cuba zitaendelea kupata wasaa zaidi wa kushirikiana katika masuala na sekta zilizoanzishwa ambazo anamatumaini ya kuendelezwa chini ya Rais huyo Mpya wa Cuba Bwana Maguel Diaz-Canel mwenye fikra za watangulizi wake waliolenga kuona ustawi wa Bara la Afrika unaimarika na kukua siku hadi siku. 
 Akitoa shukrani zake Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernandes alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Cuba itaendelea kuiunga mkono Tanzania hasa katika masuala ya Elimu na Afya. 
 Profesa Lucas alisema miradi hiyo ya pamoja iliyoanzishwa ni pamoja na wa Afya ambao umeanza kutoa sura ya matumaini kuwatafutia baadhi ya Madaktari Wazalendo wa Zanzibar mfumo wa kuendelea na mafunzo yao ya Juu ya Udaktari Nchini Cuba baada ya kumaliza masomo yao Zanzibar chini ya usimamizi wa Wataalamu na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Matantas cha Nchini humo.
 Kiongozi huyo Mpya wa Taifa la Cuba akiwa wa Tatu tokea Taifa hilo kupata Uhuru wake alishika wadhifa huo kwa kupata Asilimia 85.65% baada ya kushinda Viti 605 
 Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa salamu za pole kwa Rais wa Cuba Bwama Miguel Diaz-Canel kupitia Balozi wa Nchi Hiyo Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo kufuatia ajali ya Ndege ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Cuba-Cubana Airlines. Ajali hiyo iliyotokea mapema wiki hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Havana wa Jose Marti ilisababisha vifo vya abiria 111 ambao walikuwemo kwenye Ndege hiyo. Balozi Seif kupitia Balozi huyo wa Cuba Nchini Tanzania aliwataka Wananchi wa Cuba pamoja na wale wenye jamaa na ndugu zao waliofariki kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu cha Msiba. 
 Alisema Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wanaungana na Serikali ya Cuba pamoja na Wananchi wake katika msiba huo uliojumuisha pia vijana ambao ndio nguvu kazi iliyokuwa ikitegemewa na Taifa hilo.
Ndege hiyo ya Abiria ilipata ajali mara baada ya kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jose Marti katika Mji Mkuu wa Havana ikielekea Mji wa Holguin ulioko Mashariki mwa Nchi hiyo. Kwa mujibu wa takwimu za Vyombo vya Habari hiyo ni ajali ya Tatu kubwa za Ndege Nchini Cuba tokea mnamo Mwaka 2010.
Habari na picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar na Ofisi ya Zanzibar ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akisalimiana na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo alipofika kwenye Makaazi yake Jijini Dar es Salaam kumpongeza kwa Cuba kumaliza Uchaguzi wa Rais Salama.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibr Balozi Seif kulia na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Prifesa Lucas Domingo  kushoto wakibadilishana mawazo kwenye makaazi ya Balozi wa Cuba Mjini Dar es Salaam.
 Balozi Seif na Profesa Lucan akiangalia baadhi ya picha na matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye maktaba ya Ubalozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi Kulia na Mke wa Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mama Melyin Suazez Alvarez  kati kati wakimfanyia mzaha mtoto wa mke wa Balozi huyo Evelyn Hernandes Suarez.

Balozi Seif akiagana na Mke wa Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Mama  Melyin Suarez Alvarez. Kati kati yao ni Balozi Lucas Domingo Hernandes na Mtoto wake  Evelyn Hernandes Suarez

MICHUZI TV: DKT. KIJAJI AITAKA BENKI YA ABC KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI KUCHOCHEA SEKTA YA KILIMO NA VIWANDA


NAIBU SPIKA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATENDAJI WA BENKI YA NBC OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Watendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Ofisini kwake Jijini Dodoma, kushoto kwa Naibu Spika ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Theobald Sabi. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto.
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) katika picha ya pamoja na Watendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma,  watatu toka kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Theobald Sabi na wapili kulia ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akiagana na Watendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara  (NBC) mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma. PICHA NA BUNGE

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi apokea vitendea kazi ubalozi wa china

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akizungumza jambo na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen wakati wakati wa mkutano baina yao uliofanyika ubalozi wa China Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza jambo wakati wa wakati baina ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi ((katikati) na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen uliofanyika Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akisaini mkataba ya makabidhiano ya vitendea kazi ikiwemo vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Idara hiyo mara baada ya kumaliza kwa mkutano baina yake na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen (kulia) uliofanyika Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akipokea sehemu ya vitendea kazi vilivyotolewa na Ofisi ya Ubalozi wa China kupitia kwa Afisa Mwandamizi wa Ubalozi huo, Xu Chen mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao uliofanyika Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi akiagana na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China, Xu Chen mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao uliofanyika leo Alhamisi Mei 31, 2018 Jijini Dar es Salaam. PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO

Swahili Fashion Week Pop Up Shop kufanyika Juni 2 mwaka huu nyumbani kwa Balozi wa Italia Dar es salaam

$
0
0

Habari Njema! Balozi wa Italia nchini Tanzania, kwa mara nyingine tena atakuwa wenyeji wa onesho hili la Swahili Fashion Week Pop Up shop litakalo fanyika tarehe 2 mwezi juni kuanzia saa sita mchana hadi kumi na mbili jioni, ni sehemu pekee utakayopata nguo na vito  vya hali ya juu kutoka kwa wabunifu mashughuli watakao simamia uuzaaji wa bidhaa zao bora.
Onyesho hili la siku moja lenye lengo la kuonesha bidhaa mbalimbali  zinazotengenezwa kwa mkono kutoka kwa wabunifu wa ndani na nje ya nchi pamoja na wasanii wa uchoraji kutoka sehemu tofauti nchini Tanzania watakuwepo nyumbani kwa balozi wa Italia  eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Onesho hili la pop up shop linawapa nafasi wafanyabiashara na wajasiriamali kuuza bidhaa zao kwa jamii ya kidiplomasia na watu wengine tofauti, pia litawakutanisha na wabunifu wa nguo, wabunifu wa vito, watengeneza mapambo ya ndani, na wasanii wa uchoraji.
Waandaaji wa Onyesho hili wanawasihii wajasiriamali wa kitanzania wanaokuza bidhaa “zinazotengenezwa Tanzania” kuchukua nafasi hii kukuza mtandao wakibiashara na kuongeza wateja na kupata nafasi ya kushiriki kwenye maonesho  ya Swahili Fashion Week Bazaar yatakayo fanyika mwezi Disemba mwaka huu. Onesho hili lina jumla ya washiriki 40, baadhi yao ni, Jamilla Vera Swai, MM Collection, Xarafa, Neste Fashion Africa, Kiwohede, Naledi Tanzania, Lulua Gems, Diana Quilt and Designs, ABLO, Yasmar Perfumes, Kekuune, Hucna designs, Zawadi Zanzibari na wengine wengi.
Onyesho la SFW Pop Up shop linawakaribisha watu wote wafike nyumbani kwa balozi wa Italia, oysterbay, jumamosi ya tarehe 2 mwezi juni, hakuna kiingilio , vinywaji vitakuwepo na utapata nafasi ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa waoneshaji.
Swahili Fashion Week Pop Up shop imeandaliwa na kampuni ya mawasiliano na uratibu matukio, 361 Degrees Africa kwa kushirikiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mh. Roberto Mengoni
Kwa taarifa Zaidi na jinsi ya kushiriki tembelea tovuti yetu
www.swahilifashionweek.com au piga simu 0769 696 633/0713 844 486

LALA SALAMA MWALIMU KASUKU BILAGO, UMEONDOKA KABLA YA NDOTO YAKO KUTIMIA.

$
0
0
Leo Mbunge wangu Mwalimu Kasuku Bilago, Mbunge wa Buyungu utalala katika nyumba yako ya milele, utalala hutaamka tena, familia yako itakukosa, wananchi wa Buyungu watakukosa, ndugu jamaa na marafiki hatutakuona tena mtu uliyefanya siasa za kistaarabu, uliyetanguliza mbele maslahi ya wananchi wake na uliyetamani chama chako cha CHADEMA kufanya siasa zenye mwelekeo wa maendeleo.

Tangu kauli yako izimike Mei 26, 2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, nimekumbuka mengi tuliyozungumza na uliyoniambia kwa dhati ya moyo wako. Mengi hayajatimia lakini hayo ndio maisha ya mwanadamu. 
Nakumbuka sana siku ile Julai 21, 2018 baada ya Rais John Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Kibondo - Nyakanazi Mkoani Kigoma, yenye urefu wa Kilometa 50 uliniambia umefurahishwa sana na kuanza kwa ujenzi huo, ulisema barabara hiyo ikikamilika italeta ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Kibondo likiwemo jimbo lako la Buyungu.

Ulinibonyeza kuwa bahati mbaya ndani ya chama chako cha CHADEMA kushabikia miradi ya maendeleo sio jambo linalopendwa sana, ulinidokeza kuwa linapokuja suala la maendeleo upo tayari kutofautiana na viongozi wako wa chama. 
Nakumbuka uliniambia kuwa hata uliposalimiana na Rais Magufuli ulimwambia upo tayari kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilimradi wananchi wako wa Buyungu wapate maendeleo. Nilikuamini kwa sababu hata maneno uliyozungumza baada ya kupewa nafasi ya kusalimu wananchi ulijikita kuzungumzia maendeleo na kumshukuru Rais Magufuli na serikali yake. 
Ndio maana nasema umeondoka kabla ndoto yako haijatimia, najua kuwa ulikuwa njiani kuhamia CCM, hukupenda kumaliza nguvu zako na muda wako kushabikia mabishano ya kisiasa badala ya kuelekeza nguvu kuwapigania wananchi wa Buyungu. Najua kwa namna Rais Magufuli alivyozungumza nawe kwa bashasha, ungekaribishwa ndani ya CCM na ungepewa nafasi ya kuwatumikia wananchi ili ukate kiu yako.

Kifo hiki kimezima ndoto zako, kimeondoa neema kwa wananchi wa Buyungu. Najua ndani ya CHADEMA ulishaanza kusemwa vibaya kutokana na kuwepo hisia kuwa ulikuwa mbioni kuhama chama. Ulianza kuwekewa maazimio mabaya, ulianza kutishwa. 
Nasikia minong’ono ya wana CHADEMA wanaotaka kifo chako kichunguzwe, kuna hofu kuwa umeuawa. Kuna wasiwasi kuwa msimamo wako wa kupingana na viongozi wakuu wa chama chako na nia yako ya kutaka kuhamia CCM vimesababisha kifo chako. 
Kuna hofu kuwa umeuawa kama ambavyo viongozi wengine wa chama chako cha CHADEMA akiwemo Mhe. Chacha Wangwe waliuawa, kuna hofu kuwa umeuawa ili usifikie uamuzi wako wa kukihama chama kwa kuwa ungekidhohofisha chama kama walivyokidhohofisha akina Dk. Godwin Mollel na madiwani lukuki wa CHADEMA waliokihama chama hicho na kujiunga na chama Tawala. 
Mimi rafiki yako nitafurahi kuona uchunguzi huu unafanywa, japo kuwa nami ulinishawishi kujiunga na CHADEMA lakini natafakari sana uanachama wangu, na kama nilivyokuahidi kuwa ukihama na mimi nitahama. Sasa umeondoka,nakuahidi kuwa nikimaliza msiba na mimi nitahamia kwenye chama kilichotayari kupigania maendeleo ya wananchi na sio porojo na kutishiana usalama. 
Mwalimu Bilago kwa heri, unalala leo milele lakini tunakulaza wakati viongozi wako wa CHADEMA wakiwa wametukwaza sana sisi ndugu na marafiki zako wa Buyungu. Kifo chako kimegeuzwa kuwa mtaji wa kisiasa, wameanzisha mabishano na Bunge bila sababu za msingi, Spika Mhe. Job Ndugai alikuja kukuzika lakini ameondoka bila kukuzika kwa sababu ya ubishi wa Mwenyekiti wako Freeman Mbowe na washirika wake.

Unazikwa huku vichwa vya habari vya magazeti vikiwa vimeandikwa bila heshima kwako “Mazishi ya Bilago yaibua utata, Ndugai aondoka” hilo ni gazeti la Mwananchi, “Mazishi ya Mbunge Chadema fugisu tupu, Spika akabidhi mwili na kuondoka, Chadema wabaki kuzika leo”hilo ni gazeti la Tanzania Daima. Natambua kuwa haya ni magazeti rafiki wa CHADEMA lakini kwangu mimi kukuzika rafiki yangu kwa kusindikizwa na vichwa hivi vya magazeti imenikwaza sana. 
Naomba kutoa pole kwa wote walioguswa na kifo chako Mwalimu Kasuku Bilago, nakuombea radhi kwa Spika wa Bunge Job Ndugai, na nakuombea radhi kwa wote waliokwazika na vitendo vya viongozi wa CHADEMA kugeuza msiba wako kuwa mtaji wa kisiasa, nakuombea Mwenyezi Mungu akupumzishe mahali pema peponi na pia awape uvumilivu, subira na ustahimilivu ndugu wote na hasa Mke wako uliyempenda sana na familia yako.
  
Saimon Michael
Kigoma.
Mei 31, 2018

MAFURIKO SAME YAKATA MAWASILIANO YA MIOUNDO MBINU ,WANACHI WATUMIA MITUMBWI NA TREKTA KUSAFIRISHA MALI ZAO

$
0
0
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour (aliyenyoosha mkono) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Maafa  ya mkoa wakiwa eneo la Ruvu Darajani ambako magari yanaishia baada ya miuondo mbinu ya barabara kujaa maji .
Moja ya barabara ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakazi wa maeneo ya Ruvu Muungano na Darajani ikiwa imejaa maji na kusababisha adha kwa wasafiri.
Baadhi ya wananchi wakijaribu kuyahama makazi yao baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji katika Vijiji vya Ruvu  Marwa na  Ruvu Mferejini.
Baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia usafiri wa pikipiki kwa maeneo ambayo bado hayajafikwa na maji mengi.
Kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika vibaya baadhi ya wafanyabiashara ya bidhaa ndogondogo wametumia kadhia hiyo kununua bidhaa kama Unga na Mchele na kuwauzia wananchi waliozingirwa na maji kwa bei ya juu.
Usafiri pekee kwa sasa katika maeneo hayo ni Trekta na Mitumbwi ambayo imekuwa ikitumika kuhamisha mali pamoja na wananchi.
Na Hii ndio hali Halisi ya wananchi katika maeneo hayo wamelazimka kutumia mitumbwi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakabidhiwa jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisaini hati ya kukubali rasmi kupokea jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri kuhusu Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika Mashariki. Kushoto ni Bw.Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye alikabidhi majukumu ya usimamizi wa Bodi hiyo kwa Wizara.Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Arusha.Bodi hii yenye makao makuu yake jijini Arusha, Tanzania, tokea kuanzishwa kwake tarehe 30/01/2013 ilikuwa chini ya uangalizi wa TAKUKURU.

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakifurahia jambo baada ya kuasaini hati za makabidhiano

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akipokea nyaraka za Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw.Valentino Mlowola
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji  na Watumishi wa Serikali, na Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika.

BancABC yazindua tawi jipya Dodoma

$
0
0
Benki ya BancABC imezindua tawi jipya jijini Dodoma kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma za kibenki kwa wateja hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi katika kanda ya kati. Hilo ni tawi la saba kwa BancABC nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema ufunguzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka kwa kuwa ofisi za serikali zimehamia Dodoma na Dodoma imepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo mahitaji ya huduma za kibenki yameongezeka ili kuwawezesha wananchi kupata mitaji kwa ajili ya biashara na shughuli mbalimbali na pia kuhamasisha watanzania wengi kuendelea kujenga hulka ya kuweka amana.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza BancABC kwa kuona umuhimu wa kuleta huduma za kibenki kwa kufungua tawi jipya jijini Dodoma. Ninaamini bado kuna watu wengi ambao hawajanufaika na huduma za kibenki na ni imani yangu kwamba mtafanya kazi kwa bidii ili kuwafikia wananchi na wafanyabiashara wengi mjini na vijijini katika ukanda huu”, alisema.

Dkt. Kijaji ameonyesha kufurahishwa na hatua ya benki hiyo ya kupunguza riba. “Hii itawavutia wafanyabiashara wengi hivyo kukuza biashara zao na kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo ya biashara na nyumba za kuishi. Upatikanaji wa mikopo kwa riba nafuu pia utasaidia kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa mkoa wa Dodoma”, alisema

Naibu WAZIRI WA Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya BANCABC Jijini Dodoma jana. Wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurungenzi benki ya BANCABC Imani John (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge. 

Naibu Waziri Fedha, Uchumi na Mipango Dr. Ashatu Kijaji (kushoto) akifungua akaunti katika Tawi jipya la Benki ya BANCABC Jijini Dodoma mara baada ya kulifungua rasmi jana, kulia ni Frida Mmmari wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.
Naibu WAZIRI WA Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya BANCABC jjijini Dodoma jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BANCABC Imani John (kulia). 


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Binilith Mahenge akiongea wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya BANCABC jjijini Dodoma jana. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi Dr. Ashatu Kijaji na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde (kushoto). 


Prof.Mkenda afanya ziara katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Namanga

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda, akizungumza na wajumbe (hawapo pichani)  waliohudhuria kikao baina yake, watendaji wa Kituo hicho na wafanyabiasha wanaozunguka eneo hilo kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo.Pro. Mkenda katika ziara hiyo aliambatana na Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya.
Wawili hao kwa pamoja sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho katika pande zote mbili za Tanzania na Kenya walipata fursa ya kuongea na watendaji wanaohudumu katika kituo hicho.
Lengo la ziara hii ilikuwa nikuangalia ufanisi wa kituo hicho katika kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kutika pande zote mbili za Tanzania na Kenya hivyo
 kurahisisha shughuli za biashara.
 Vilevile ziara hii ililenga kubaini changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi wanaotumia kituo hicho.
Aidha Makatibu Wakuu hao wamezipongeza M
amlaka na Taasisi zote zilizopo katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi. 

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa na  Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya (kushoto), kenye kikao cha wadau kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa OSBP ya Namanga 
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (watatu kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wanaohudumu katika Kituo hicho

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa nana Katibu Katawala wa Halmashauri ya Longido Bw.Toba Nguvila (kushoto) na Mwenyeketi wa Wafanyabiasha Namanga  (katikati) wakiwa katika ziara za kutembelea kituo cha  OSBD 

Mhe.Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya akizungumza katika Kikao. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

INTRODUCING "AMINI" BY AMINI, MAGIC AND NDELAH

NIMERIDHISHWA NA UTENDAJI TANRODS - DC HAPI

DC HAPI AINGILIA KATI SWALA LA TUHUMA ZA MWALIMU KUBAKA WANAFUNZI

SERIKALI YATOA BILIONI 40 KUSHUGHULIKIA TATIZO LA MAJI MUHEZA

$
0
0
SERIKALI imeanza kulishughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kwa vitendo baada ya kutoa kiasi cha bilioni 40 kwa ajili ya kutoa maji kwenye chanzo cha mto zigi kupelekwa kwenye vijiji mbalimbali ili kuweza kuondosha kero hizo iliyokuwepo muda mrefu iliyokuwa ikiwafanya wananchi kutumia muda mwingi kusaka huduma hiyo.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwele wakati alipofanya ziara wilayani humo kutembelea vyanzo vya maji Amani na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani.

Alisema kuwa mpango huo wa serikali unakusudia kuhakikisha changamoto za maji ambazo walikuwa wanakabiliana nazo wananchi hao kwa muda mrefu zinamaliza ili waweze kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao na jamii zinazowazunguka.

Waziri Kamwelwe alisema hatua hiyo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John Magufuli kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi zikiwemo za maji ili kuhakikisha tatizo la kutokupatikana kwa huduma hiyo linaondoka kwa watanzania.

“Ndugu zangu serikali tumetoa bilioni 40 kwa ajili ya kushughulikia tatizo la maji wilayani Muheza kutoka chanzo cha Mto zigi kupita vijiji vyote hadi Muheza mjini huu ni mpango wa kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji Muheza tunaipatia ufumbuzi wa kina “Alisema.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakitazama namna maji yanavyotoka kwenye Kijiji cha Mashewa Tarafa ya Amani wakati alipofanya ziara kutembelea vyanzo vya maji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi
 Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Pongwe hadi Jijini Tanga kutoka kampuni ya Koberg Contrustion Co.Limited Stephen Kingili wa pili kulia akimuonyesha jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto wakati alipotembelea na kuangalia tanki kubwa la maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambalo litakalokuwa la lita milioni saba  linalotarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwakani litakuwa limekamilika kwa ajili ya kutoa maji Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia mchanga unazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akiangalia kikoto  zinazotumika kwenye ujenzi wa tanki la maji eneo la Ngomeni

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images