Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2017/2018 kufikia tamati Jumatatu Mei 28, 2018

$
0
0
Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2017/2018 inafikia tamati Jumatatu Mei 28, 2018 kwa timu zote 16 kuingia viwanjani kukamilisha raundi ya 30, ambayo ndiyo itakayokamilisha jumla ya mechi 240 za msimu huu.

Mechi hizo zitachezwa kama ifuatavyo;
Lipuli vs Kagera Sugar- saa 10 kamili
Tanzania Prisons vs Singida Utd- saa 10 kamili
Ndanda vs Stand Utd- saa 10 kamili
Mtibwa Sugar vs Mbeya City- saa 10 kamili
Yanga vs Azam- saa 2 kamili usiku
Njombe Mji vs Mwadui- saa 10 kamili
Mbao vs Ruvu Shooting- saa 10 kamili
Majimaji vs Simba- saa 10 kamili

IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA

VOA Swahili: Zulia Jekundu S1 Ep 174

BALOZI WA POLAND NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

$
0
0
 Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski akilakiwa na wenyeji wake alipo wasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam yaliyopo wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Balozi huyo ametembelea Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa ya Jeshi hilo kwa Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kulia) alipotembela Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kushoto), wengine ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (wa pili kulia), Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, (CF) Jesuald Ikonko (wa kwanza kushoto) na msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia).
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (kushoto), akimsikiliza kwa makini msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi. (Wa pili kulia) ni Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye akiwa na Balozi wa Poland hapa nchini Mhe. Krzysztof Buzalski (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA UWANJA MPYA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki kazi za ujenzi wa uwanja mpya wa michezo wilayani Ruangwa kwa kubeba zege na matofali pamoja na wananchi.

Waziri Mkuu ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa, ameshiriki zoezi hilo leo (Ijumaa, Mei 25, 2018) kwenye uwanja huo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Akizungumza na wananchi na viongozi waliojitokeza kushiriki zoezi hilo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi inayoendelea hadi sasa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wana-Ruangwa kwa kurejesha moyo wa kufanya kazi kwa kujitolea.

“Ninawashukuru sana wana-Ruangwa kwa sababu mmeanza kufanya kazi za kujitolea, haya matofali ni matokeo ya kazi yenu, hakuna hata mtu mmoja amelipwa kwa kazi hii. Nimeambiwa yanahitajika matofali 60,000 kwa ajili ya kujenga uzio lakini hadi sasa mmeshafyatua 57,000 na zaidi, ninawashukuru sana,” amesema.

“Nimeambiwa madiwani walipiga kambi ya wiki moja hapa, Umoja wa Vijana wa CCM nao walipiga kambi, UWT walikuja kusomba matofali, watumishi wa Halmashauri nao walipiga kambi, hongereni sana kwa kurejesha moyo wa kujitolea miongoni mwa wananchi,” amesema.

Katika zoezi la leo, walijitokeza wananchi wengi wakiwemo wazee, vijana na watoto. Baadhi ya watoto walikuwa wakibeba tofali moja kwa kushirikiana wawili wawili, watatu watatu hadi wanne.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akichimba msingi wa  jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwana wananchi  kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua nyasi zilizooteshwa kitalaam wakati alipshiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mai mdogo wa Ruangwa, Mei 25, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofali, Bibi Mariam Bakari wakati aliposhiriki katika ujenzi wa  wa msingi wa uwanaja wa michezo unaojengwa na wananchi kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Rungwa mkoani Lindi, Mei 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na wanne kushoto ni  Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba tofari Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala wakati aliposhiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa na wananchi  katika eneo la Dodoma kwenye  mji mdogo wa Ruangwa,Mei 25, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Bi. Khadija Madoa ambaye ni Mama lishe anayeuza chakula katika mji mdogo wa Ruangwa mkopo usiokuwa na riba wa sh. 200, 000/=  baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo wa unaojengwana wananchi katika eneo la Dodoma, Ruangwa mkoani Lindi Mei 25, 2018. Jumla ya sh. milioni 9 zilitolewa na mfanyabiashara Abdallah Mang'onyola na kutolewa mkopo kwa Mama lishe 42.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika ujenzi wa msingi wa jukwaa kuu la uwanja wa michezo unaojengwa kwenye eneo la Dodoma katika mji mdogo wa Ruangwa mkaoani Lindi Mei 25, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Mei 25, 2018. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


RUDI NYUMBANI, KUMENOGA - TTCL

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

LEO NI LEO LIVERPOOL VS REAL MADRID JIJINI KIEV

$
0
0

Na Sultani Kipingo
Vilabu viwili vya soka vikubwa barani Ulaya leo vinaingia uwanja wa Olimpiysky Stadium jijini Kiev huku Real Madrid wakipania kunyakua kombe la UEFA Champions kwa mara ya 13 - kwa mara ya tatu mfululizo - kwa kuishinda Liverpool FC iiliyoingia fainali kwa mara ya kwanza katika miaka 11 wakiwinda ubingwa huo kwa mara ya sita.
Ushindi huko Kiev utaifanya Real Madrid timu ya nne kushinda mataji matatu ya Ulaya na ya kwanza kufanya hivyo mara mbili, kufuatia ushindi wao wa fainali kati ya miaka 1956 na 1960. Ajax (1971-73) na FC Bayern Munich (1974-76) zikiwa timu pekee zilizoshinda kombe hilo mfululizo.
Zinadine Zidane wa Real Madrid anaweza pia kuwa kocha wa kwanza kushinda makombe ya Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo, akiwa wa kwanza kushinda ligi ya UEFA mfuluizo mwaka 2017.
Mafanikio ya Real Madrid leo yatamaanisha ushindi wa mara tano kwa mara ya kwanza kwa mfungaji bora wa michuano hiyo, Cristian Ronaldo, ambaye pia atakuwa mchezaji wa  tano kushinda  fainali za Ulaya na wa kwanza katika zama za UEFA Champions kama atacheza na timu yake kushinda. Wachezaji wengine ni magwiji watatu wa Real Madrid Paco Gento (mchezaji pekee aliyecheza fainali hizo mara sita), Alfredo Di Stefano na Maria Zarraga pamoja na Paolo Maldini wa AC Milan.
Mchezo huu unakumbushia fainali za kombe la Ulaya mwaka 1981, ambapo Liverpool ilishinda bao 1-0 jijini Paris kuwapa ushindi wa mara ya tatu wa mashindano hayo katika miaka mitano. Hiyo ilikuwa ni mechi ya mwisho kwa Real Madrid kushindwa kwenye michuano hiyo.
Ushindi huo wa Liverpool ni wa pekee kwa timu ya Uingereza dhidi ya timu ya Spain  katika kombe la ubingwa wa Ulaya. Vilabu vya La Liga vimeshinda mara tatu zilizotangulia dhidi ya timu za Uingereza - FC Barcelona ikiifunga Arsenal FC 2-1 mwaka 2006 na Machester United FC mwaka 2009 (2-0) na 2011 (3-1).
Liverpool na Real Madrid wameshakutana mara tano huko nyuma kwenye michuano ya Ulaya, Liverpool wakishinda michezo yao   mitatu na Madrid mara mbili, huku klabu hiyo ya Uingereza ikiwa imefunga magoli sita dhid ya manne ya Madrid.

Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji waendelea jijini Arusha

$
0
0
Mkutano wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Biashara,Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea kufanyika jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika kwa kipindi cha siku saba (7) kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018. Pamoja na mambo mengine yatakayojili, Mkutano huu unatarajia kufanya yafuatayo:-

Kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maagizo na maamuzi yaliyofanywa na mkutano uliopita wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji; 
Kupokea na kajadili taarifa ya majadiliano ya awali ya bajeti ya Baraza la Mawaziri wa Fedha la Jumuiya ya Afrika Mashariki; 
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Forodha 
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Kisekta ya Biashara; 
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Mamlaka ya Ushindani; 
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; na 
Kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Kisekta ya Viwanda. 

Mkutano huu anafanyika katika ngazi tatu ambazo ni ngazi ya waalam, ngazi Makatibu Wakuu, na ngazi ya Mawaziri. Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji akichangia wakati wa Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda,Fedha na Uwekezaji unaondelea jijini Arusha. 
Bw. Raymond Agaba Kamishna wa Biashara za Ndani (kushoto) kutoka Jamhuri ya Uganda akiongoza mkutano. Kulia ni Bibi Flavia Busingye Afisa Mkuu wa Forodha,ufuatiliaji na utekelezaji kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano ukiendelea.

Mwanri awatangazia kiama wale wanaoshiriki kula ubwabwa na kusherekea ndoa za watoto wadogo

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametanga kiama kwa watu wote wanaoshiriki kuwaoza watoto wadogo wakiwemo wa Shule kwa kuwakata na kuwafikisha Mahakamani ili waweze kuadhibiwa.

Hatua hiyo inalenga kukomesha mimba na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ikiwa ni sehemu ya kutetea haki za watoto wa kike kupata elimu kama walivyo wavulana na vile kuokoa maisha yao ambayo yanaweza kupotea wakati wa kijifungua kwa kuwa bado ni wadogo.

Mwanri alitoa amri hiyo jana katika vijiji vya Wilaya ya Igunga na Urambo mbalimbali wakati wa kampeni yake ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni.

Aliwaagiza Vyenyeviti wa Serikali za Mitaa , vijiji au  kuanza mara moja zoezi la kuwakamata watu wote ambao wataokutwa wakila  wali au kushabikia sherehe za ndoa ambayo Bibi harusi ni motto mdogo au mwanafunzi.

Mwanri alisema ni jambo la aibu kuona mfumo wa serikali upo kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa lakini bado Tabora inaendelea kutajwa kuwa miongoni mwa vinara wa mimba na ndoa za utotoni.

Mwanri alisema kuwa kiongozi wa ngazi yoyote akiwemo polisi akikuta kuna harusi ya mtoto aliye chini ya miaka 18 awe mwanafunzi au sio akamate watu wote wanaosherekea tukio hilo haramu kwa sababu linarudisha nyuma juhudi za kumkomboa mtoto wa kike kutoka mfumo dume.

“Ukifika katika harusi kabla ujaanza kula chakula ulinza binti aliyefunga ndoa ana umri gani…kama ni chini ya miaka 18 usile chakula ondoka…OCD , Mtendaji ukikutana aliyefungishwa ndoa ni chini ya miaka 18 …wapambe somba… mashangazi somba…bibi harusi na bwana harusi somba” alisisitiza

“Waliokula ubwabwa somba…aliyebeba ubwabwa wa harusi hiyo na kupeleka kwake somba…tutachambua mmoja baada ya mmoja ili kujua mwenye hatia na asiye na hatia tutamwachia ili watu wanyoke na waache kuwafuata watoto wadogo”alisema .

Mkuu huyo wa Mkoa alisema ili kuepuka kuingia katika matatizo ni vema vijana na watu wazima wanaonyemelea watoto wa kike na wale wanaoshabikia ndoa za utotoni kuacha mara moja na kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapoona mtu mwenye tabia chafu kama hizo ili awe kuchukuliwa hatua.

Alisema akiwa amepewa dhamana ya kuongoza Mkoa wa Tabora hatakubali kuendelea kupata aibu ya kunyoshewa vidole kwa mambo mabaya kama vile kuongoza katika mauaji , watoto kuwa watoro , mimba na ndoa za utotoni.

Mwanri aliwaonya viongozi na watendaji ambao watashindwa kusimamia utekelezaji wa kukomesha tabia hizo atawachukulia hatua ikiwemo kuwasimamisha na hatimaye kupendekeza wafukuzwe kazi ambao wako katika Mamlaka za juu.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM-ZANZIBAR- RAIS WA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AFUNGUA MKUTANO WADAU WA WCF KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA

$
0
0


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, jijini Mbeya leo Mei 26, 2018 wakati akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Mvunde alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri.

Aidha Mhe. Mavunde alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akipeana mikono na mama mjane, Atulehemu Kiduko, ambaye analipwa fidia ya kila mwezi kufuatia kifo cha mumewe wakati akiwa kazini kwenye kiwanda cha karatasi Mgololo kilichoko Mufindi mjini Iringa. mama huyo alitoa ushuhuda wa huduma anayopata kutoka WCF wakati wa kutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijini Mbeya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijinmi Mneya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akizungumza.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUSIMAMIA IPASWAVYO SAFARI ZA MAHUJAJI - WAZIRI MAHIGA

$
0
0
Waziri ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Augustine Mahiga amesema Wizara hiyo itasimamia ipasavyo na kuhakikisha kwamba nia ya Mahujaji wa Tanzania waliojiandikisha kwenda kutekeleza Ibara ya Hijja Nchini Saudi Arabia Mwaka huu inatimia.
Amesema Wizara yake inafuatilia hatua za mwisho katika kuona tatizo lililojitokeza kwa Baadhi ya Taasisi za Usafirishaji Mahujaji Upande wa Tanzania Bara kukabiliwa na madeni Nchini Saudi Arabia linapata ufumbuzi wa haraka kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho wa uthibitisho wa Mahujaji wa Mwaka huu.
Dr. Augustin Mahiga amesema hayo wakati alipofika katika Makazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya Hijja yaliyoleta usumbufu kwa Mahujaji wa Tanzania.
Amesema atalazimika kuzungumza na Mufti  Mkuu wa Tanzania pamoja na Uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) ili kujua hatua walizofikia katika kuona Taasisi zinazosimamia Usafirisdhaji Mahujaji upande wa Bara wamemaliza matatizo yanayowakabili.
Balozi Mahiga alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa Wizara yake utalazimika kutoa baraka kwa Mahujaji wanaosimamiwa na Taasisi za Zanzibar pekee iwapo zile za Tanzania bara mpaka hatua ya mwisho zitashindwa kumaliza changamoto zao.
Hatua ya Balozi Mahige imekuja kufuatia baadhi ya Taasisi za Usafirishaji Mahujaji za Tanzania Bara kushindwa kulipa Madeni na kupelekea Wizara inayosimamia masuala ya Mijja Nchini Saudi Arabia kutishia kuzuia Mahujaji wa Tanzania kuingia Nchini humo kwa Ibada ya Hijja Mwaka huu.
Akigusia Miradi ya Kiuchumi inayolenga kustawisha Maendeleo ya Tanzania Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Afrika Mashariki Balozi Mahige alisema ipo haja ya kufuatilia Miradi iliyopata Mikopo na Ufadhili wa Kimataifa ili kujua maendeleo yake.
Balozi Mahige aliitaja baadhi ya Miradi hiyo ni ni pamoja na ile ya  Ujenzi wa Gati ya Mpiga Duri Kisiwani Unguja na ile ya Gati ya Wete Kisiwani  Pemba ambayo imo ndani ya Mpango Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimpongeza Balozi Maige kwa hatua alizoamua kuzichukuwa katika kukabiliana na changamoto zilizojitokeza kwenye masuala ya Hijja.
Balozi Seif alisema Ibada ya Hijja ni miongoni mwa nguzo Tano wanazowajibika Waumini wa Dini ya Kiislamu wenye uwezo kuzitekeleza ambayo imo ndani ya Imani za Waumini jambo ambalo wasimamizi wa masuala hayo wanalazimika kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akielezea furaha yake kutokana na uamuzi wa Tanzania kuweka nia ya kutaka kufungua Ubalozi wake Nchini Jamuhuri ya Cuba Balozi Seif  alisema hatua hiyo muhimu itaongeza chachu ya uhusiano wa Kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba.
Balozi Seif alisema Cuba ni Taifa la kwanza lililoyatambua na kuyaunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 imekuwa mshirika mkubwa kwa Tanzania hasa katika kusaidia Taaluma kwenye miradi iliyomo ndani ya Sekta za Kilimo, Afya na hata masuala ya Viwanda.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dr. Augustine Maiga kwenye Makaazi yake barabara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam. Habari na picha na OMPR

Makatibu Tawala wa Mikoa Waagizwa Takwimu za Wazee ifikapo 30 Juni, 2018

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo, akizungumza wakati wa Hafla ya kuwapatia Vitambulisho Wazee wa Jiji la Dodoma.

Na. Atley Kuni-OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb), amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara kuwasilisha taarifa za takwimu za wazee ifikapo 30, Juni 2018.

Waziri Jafo, alitoa kauli hiyo mapema leo alipokuwa akizindua zoezi la kuwapatia vitambulisho maalum wazee wapatao 1,118 wa Jiji la Dodoma kutoka kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru, Madukani, Makole na Majengo. Vitambulisho hivyo, pamoja na mambo mengine vitawawezesha wazee hao kupata huduma za afya bure na kwa wakati.

“Ifikapo tarehe 15 Juni, 2018 kila kata iwe imetambua wazee na ifikapo tarehe 22 Juni, 2018 kila Halmashauri iwe imeunganisha taarifa za wazee kutoka katika kata zake zote” alisema Waziri. Aidha Waziri Jafo aliagiza kuwa, “ifikapo Juni, 26, 2018 kila Mkoa uwe umeunganisha taarifa zote na kuzituma kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI”. Aliwaonyawale wote watakaoshindwa kutimiza agizo hilo kuchukuliwa hatua kulingana na miongozo, kwasababu watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akitoa salam za jiji muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa wazee halifanyika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndugu Godwin Kunambi akizungumza katika hafla hiyo alisema shabaha ni kuwafikia wazee wote kwenye Jiji hilo, na kubainisha kwamba, vitambulisho wanavyo vitoa kwa wazee hao vitatumika pia kuwapa kipaumbele wazee sehemu zote za kutolea huduma hususan ofisi za serikali.

“Mhe. Waziri tunataka vitambulisho hivi tunavyo wapatia wazee wetu leo viwasaidie pia kupata huduma kwa haraka na kwa wakati pindi wanapofika kwenye ofisi zingine za Serikali” alisema Kunambi.

Mbali na kutolea ufafanuzi wa matumizi ya vitambulisho hivyo, Mkurugenzi Kunambi alisema juu ya Jiji hilo lilivyo jipanga katika suala zima la makusanyo ya mapato ya ndani, ambayo ndio yamekuwa chachu ya kuboresha huduma za afya kwa makundi maalum hususan wazee.
Mmoja ya Wazee akipokea kitambulisho mara baada yakuzinduliwa kwa zoezi lakuwapatia vitambulisho wazee Jiji la Dodoma.

“Mhe. Waziri, Jiji limepanga kukusanya Bil. 68 katika mwaka wa fedha ujao ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha ambapo tulijiwekea lengo la kukusanya Bil. 20 nahadi kufikia mwezi Februari tulikuwa tumekusanya Bil. 14”. Kunambi ameongeza kuwa, katika mwaka ujao wa fedha wametenga kiasi cha Mil. 58 kwaajili yakuwezesha huduma za wazee kwenye Jiji hilo.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi, ametumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya watendaji wanao waambia wazee kwamba hakuna dawa.

“Kumekuwepo na malalamiko mengi siku za nyuma kutoka kwa wazee kuwa, baadhi ya watendaji wa afya wanawanyanyapaa wazee na kuwaambia hakuna dawa wafikapo vituoni, sasa Mhe Waziri, mimi niliseme kwa uwazi kabisa hatuta mvumilia mtu yeyote atakaye onekana ni kikwazo kwa wazee hawa kadi zimetoka wazee wahudumiwe, sio mnajiwekea vijiduka karibu na vituo halafu mnawaambia waende waka nunue” alionya Ndejembi
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri Viongozi wa Halmashauri na wazee waliopatiwa vitambulisho.

Awali akitoa taarifa ya uandaji wa vitambulisho Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Mohamed Nyembea, alisema utekelezaji wa zoezi hilo ulianza kwa hatua za awali kwa kuwatambua wazee katika Kata 41 za Jiji la Dodoma, ambapo jumla ya wazee 15,885 kutoka kata 33 miongoni mwa 41 wamekwisha tambuliwa na miongoni mwao wanawake ni 9,132 na wanaume ni 6,753 ambapo ni sawa na asilimia 80.5 ya kata zote 41 za Jiji la hilo.

Utoaji wa vitambulisho kwa wazee ni utekelezaji wa sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003 ambapo inazungumzia mambo muhimu ya wazee ikiwepo kutenga dirisha maalum katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Diwani wa Kata ya Mkonze akishukuru kwaniaba ya wananchi wa Mkonze.

Introducing "SUPU YA MJUSI" BY FATHER B FT. DJ TIFFA XR

INTRODUCING "JIBEBE" BY FRIDA AMANI FT. G. BOY


DC KAKONKO APIGA MARUFUKU UNYWAJI POMBE ZA KIENYEJI ASUBUHI,ATOA MAAGIZO KWA POLISI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma ,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala ameagiza kukamatwa watu wote wanajihusisha na unywaji wa pombe za kienyeji nyakati za kazi huku akifafanua ulevi kupita kiasi ni moja ya mambo yanayochangia kukwamisha maendeleo.

Amesema inasikitisha kuona baadhi ya wananchi kunywa asubuhi badala ya kwenda kwenye shughuli za kimaendeleo.

Hali hiyo ilimlazimu Kanali Ndagala kuagiza Ofisa wa Polisi kuwakamata watu wote waliokuwa wanakunywa pombe katika vilabu vya pombe ya kienyeji nyakati za asubuhi. Pia ametoa maagizo ya Mgambo wawili kunyang'anywa vitambulisho vyao katika Kijiji cha Muhange baada ya kuwashuhudia wakinywa pombe asubuhu.

Ametoa maagizo hayo jana alipokwenda kijijini hapo kwa ajili ya kukagua na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.Amesema anasikitishwa kuona watu wana shindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuanza kunywa pombe asubuhi na wengi wao wakiwa ni vijana.

"Wakati wenzao wakijitolea katika ujenzi wa shule ya Sekondari ili kutatua changamoto ya wanafunzi wa kata hiyo kutembea umbali mrefu ili kufuata shule ilipo ambapo wananchi wameanza juhudi zao na serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za wananchi,wao wanakwenda kwenye ulevi na hili hatuwezi kulivumilia," amesema.

Aidha Mkuu huyo amewataka wenyeviti wa vijiji vyote kuhakikisha vilabu vya pombe vyote vinafunguliwa kuanzia saa 10 jioni baada ya watu kumaliza kazi zao na wazingatie hilo na kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote wanaokiuka sheria hiyo kwani ndio chanzo cha kuwa vibaka na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na Serikali kwa ujumla.

" Ni aibu sana kuona vijana wadogo ambao mnanguvu za kufanya kazi kuja kunywa pombe asubuhi mnashindwa kufanya kazi.Ofisa wa Polisi hakikisha unawakamata hawa wote wanaokunywa na waliolewa muda wa kazi, sisi tunakuja kuhimiza maendeleo, wao wanaendelea katurudisha nyuma.


Baadhi ya Wananchi waliokamatwa kufuatia unywaji pome asubuhi badala ya kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akijionea mazingira halisi ya unywaji pombe asubuhi subuhi kwa baadhi ya wananchi kwenye moja ya vilabu vyao vya pombe
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi huku akiagiza kukamatwa kwa watu wote wanaojihusisha na unywaji wa pombe za kienyeji nyakati za kazi huku akifafanua ulevi kupita kiasi ni moja ya mambo yanayochangia kukwamisha maendeleo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akishiriki ujenzi na kuunga mkono shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo hilo.Amesema anasikitishwa kuona watu wana shindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuanza kunywa pombe asubuhi na wengi wao wakiwa ni vijana.

BALOZI WA KUWAIT AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  Ijumaa 25 Mei 2018, yaliyojikita juu ya namna ya kuimarisha uhusiano kati ya Kuwait na wilaya hiyo kwa sifa ya kipekee, na baina ya Tanzania na Kuwait kiujumla. 

Katika mazungumzo hayo, Balozi Al-Najem alisema kuwa ubalozi uko tayari kushirikiana na Uongozi wa Kigamboni katika kusaidia nyanja mbalimbali husasan afya na elimu, aidha alifungua milango ya kuwasaidia watu wenye ulemavu katika wilaya ya Kigamboni kwa kuwapatia vifaa. Yafaa kueleza kuwa ubalozi wa Kuwait ushawahi kuchimba visima vya maji safi na salama huko Kigamboni vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule na wakaazi wanaoishi karibu na shule hizo.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ameishukuru Kuwait kwa misaada inayoitoa kwa Tanzania akitoa mifano msaada wa hivi karibuni kwa Taasisi ya Mifupa ya MOI Dar es Salaam na Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Kando ya mazungumzo, Balozi Al-Najem alimkabidhi Mkuu wa Wilaya vikapu vyenye vyakula vya futari vitakavyogaiwa kwa baadhi ya wakaazi wa Kigamboni wenye mahitaji ambapo Al-Najem alisema vyakula hivyo ni zawadi kutoka kwa raia wa Kuwait kwenda kwa ndugu zao na marafiki zao wa Tanzania, zawadi ambayo ni kutoka Chombo cha Baytu Zakat, Wakfu na Mali ya Amana cha Kuwait.


Baada ya mazungumzo hayo, Mkuu wa Wilaya Hashim Mgandilwa aliongozana na mgeni wake Al-Najem katika ziara ya kukagua Hospitali Kuu ya Wilaya na Kituo cha Afya cha Kigamboni kinachodumia takriban watu 36982 ambapo walitembelea wodi mbalimbali na kusikiliza matatizo na changamoto zinazokabili hospitali na kituo hicho.
Wakiwa katika hospitali ya Wilaya, Balozi Al-Najem aliahidi kusaidia wodi ya wazazi na chumba cha watoto njiti kwa kutoa vifaa vya kisasa vitakavyochangia utoaji wa huduma bora kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga ikiwa ni kuitikia wito wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt John Magufuli wa kuimarisha huduma za afya nchini.

Kabla ya kuondoka Kigamboni, balozi Al-Najem na mwenyeji wake Hashim Mgandilwa walijumuika na wakaazi wa Kigamboni kusali sala ya Ijumaa katika moja ya misikiti ambapo mara baada ya Sala, Mhe. Balozi aliahidi kurudi tena msikitini hapo kwa kuandaa futari.

Balozi wa Kuwait nchini Mheshimiwa Jasem Al-Najem (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakimkabidhi mmoja wa wakazi wa Kigamboni, kikapu cha chakula kwa ajili ya ftari.

NIDA YAPONGEZWA KWA UTENDAJI KAZI UNAOENDANA NA KASI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) na kusifu jitihada kubwa za Kaimu mkurugenzi Mkuu NIDA ndugu Andrew W. Massawe ambaye ndani ya kipindi kifupi ameweza kuleta mabadiliko makubwa ikiwemo kuongezeka kwa kasi ya kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa.

Hayo ameyasema wakati alipofanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida ofisi kwake; katika ziara ya Mkurugenzi huyo kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu linaloendelea mkoani Manyara.  

Akitoa majumuisho ya maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu linaloendelea mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara amesema mpaka sasa zaidi ya wananchi 650,000 wameshasajiliwa katika wilaya zote tano za mkoa wake.

“ Idadi hii ni zaidi ya  asilimia 84 ya makisio ya idadi halisi ya wananchi wenye umri wa miaka 18 wanaotazamiwa kusajiliwa, idadi iliyobaki tumejipanga kukamilisha usajili mwishoni mwa mwezi Juni, 2018” alisisitiza.

Amesema mwitikio wa watu ni mkubwa kutokana na wananchi wengi kutambua umuhimu wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa, ambapo mpaka sasa Wilaya ya Hanang’ na Mbulu zimeshamaliza zoezi la Usajili huku wilaya za Babati, Kiteto na Simanjiro zitakamilisha zoezi hilo mwishoni mwa mwezi Juni,2018. Kwa zile Wilaya ambazo usajili umekamilika wananchi ambao hawakusajiliwa watapashwa kwenda makao makuu ya Wilaya hizo kupata huduma.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wa Manyara wanasajiliwa pamoja na kufanikisha Usajili wa wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya Tanzanite - Mererani ambapo jumla ya wachimbaji wadogo 10,495 walisajiliwa na kupatiwa Vitambulisho.

Amesema hatua hii imeleta mafanikio makubwa katika kuhakikisha kupitia Kitambulisho cha Taifa, watakaonufaika na Uchimbaji na biashara katika migodi hiyo wanakuwa watanzania hususani katika kipindi hiki ambacho ukuta katika machimbo hayo umekamilika.

Akifafanua mipango ya Mamlaka kwa sasa; Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA amesema moja ya malengo ya ziara yake Manyara ni kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na kuanza kazi kwa vituo vya Uchakataji taarifa ambavyo vitawezesha taarifa za wananchi zilizokusanywa kuhakikiwa na kutumwa kwenye kituo kikuu cha Uzalishaji makao makuu kwa ajili ya hatua za uzalishaji Vitambulisho. Lengo ni kuhakikisha malengo tuliyojiwekea yanakamilika ndani ya wakati.

“ kiujumla nimeridhishwa sana na utendaji katika mkoa wa Manyara; na jinsi Mkuu wa Mkoa na wakuu wa Wilaya walivyojipanga katika kuhakikisha zoezi la Usajili mkoa wa Manyara linakamilika na wananchi wanapata Vitambulisho. Ndiyo maana umeona hata kituo cha kuchakata taarifa kipo kwenye ukumbi karibu kabisa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuonyesha uwepo wa ufuatiliaji wa karibu wa zoezi hili. Kwa hili nimefarijika sana….” alisisitiza

Katika ziara hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) aliambatana na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho ndugu Alphonce Malibiche, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Joseph na Meneja Mifumo ndugu Edson Guyai ambaye pia ni msimamizi wa usajili mkoa wa Manyara.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Bw. Andrew W. Massawe ofisini kwake
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Alexander Mnyeti akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Bw. Andrew W. Massawe ofisini kwake
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu likiendelea Mkoani Manyara ambapo mpaka sasa zaidi ya wananchi 650,000 wameshasajiliwa katika wilaya zote tano za mkoa huo.
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu likiendelea Mkoani Manyara ambapo mpaka sasa zaidi ya wananchi 650,000 wameshasajiliwa katika wilaya zote tano za mkoa huo.

WAKULIMA KAKONKO WAHIMIZWA KULIMA KILIMO CHA BIASHARA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WAKULIMA wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wametakiwa kulima kilimo cha biashara na kuachana na kilimo cha kujikimu wenyewe ili kuweza kuondokana na umasikini.

Mwito huo ulitolewa jana katika Kijiji cha Kiga wilayani hapo na Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kigoma, Josephu Lubuye wakati wa ugawaji wa mashine ya kuchakata Muhogo kwa kikundi cha Mwendo wa saa, iliyo tolewa na Shirika la BTC kupitia mradi wa kilimo wa ENABEL unaotekelezwa na Serikali ya Ubelgiji na Tanzania.

Lengo ni kuendeleza kilimo cha muhogo na maharage kwa kuwakopesha wakulima mashine na kuwapatia mafunzo ya namna ya kulima kitaalamu.

Hivyo Lubuye amesema wakulima wanatakiwa kubadilika na kuanza kilimo cha biashara na mashine hiyo waliyoipata itumike kuchakata mazao mengi ya mihogo waliyolima kutokana na maombi na aandiko lao la kuomba mashine ya kuchakata mihogo.

Amesema hiyo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wingi ili wakulima wengine wajifunze kupitia kikundi hicho kutokana na uzalishaji watakaoufanya kupitia mafunzo ya kilimo cha biashara waliyo yapata kuongeza uzalishaji na ubora.

Akikabidhi mashine hiyo yenye thamani ya Sh.milioni mbili na yenye uwezo wa kuzalisha kilo 700 kwa saa moja na hufanya kazi kwa muda wa saa nane, Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagala amewataka wakulima kuacha kuuza mazao ambayo hayajaongezwa thamani.
 Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagala akikabidhi  mashine  ya kuchakata muhogo,yenye thamani ya Sh.milioni mbili na yenye uwezo wa kuzalisha kilo 700 kwa saa moja.DC Ndagala amekabidhi hiyo mashine ya kuchakata Muhogo kwa kikundi cha Mwendo wa saa, iliyo tolewa na Shirika la BTC kupitia mradi wa kilimo wa ENABEL unaotekelezwa na Serikali ya Ubelgiji na Tanzania.
 Sehemu ya shamba ka Muhogo. 
 Mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagala akitumbukiza muhogo kwenye mashine ya kuchakata muhogo,ili kujionea ufanyaji wake kazi,mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha kilo 700 kwa saa moja.
Mihogo ilioandaliwa tayari kwa kuchakatwa na mashine.

RC KIGOMA AWAPONGEZA VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO YA JKT KATIKA KIKOSI CHA KJ 824 KWA AANDIKO LAO LA KUTENGENEZA SABUNI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Kikosi cha KJ 824 Kanembwa wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Amosi Mollo amewapongeza vijana wa oparesheni Melelani walio hitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa( Jkt ) kwa andiko walilolifanyia kazi la utengenezaji wa sabuni ambalo litapelekea kuanzishwa kiwanda cha utengenezaji wa sabuni kikosini hapo.

Akizungumza jana wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa vijana 732 wanaojitolea yaliyofanyika kwa miezi mitano, Mollo amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya tano wameandaa mpango wa kuanzisha kiwanda cha sabuni za kufulia.

Pia sabuni za kuogea na kunawia mikono ilikuhakikisha falsafa waliyowafundisha vijana hao ya kujitegemea katika ujasiriamali kwa kuwa vijana hao wamemaliza mafunzo ya awali wataendelea kujifunza stadi za maisha wakiwa kambini hapo.

Amesema anawapongeza vijana hao kwa kujitolea kuandaa andiko la utengenezaji wa sabuni ambalo wameanza kulifanyia kazi na sasa linaingiza pato kwa Jeshi la Kujenga Taifa ambapo ni matokeo mazuri ya kujifunza na kutumia elimu walioipata ya ujasiriamali, uzalendo, kujituma na kujitegemea inayotolewa kambini hapo kuhakikisha wanaondokana na falsafa ya kwamba hakuna ajira jambo ambalo limekuwa wimbo kwa vijana wengi mitaani.

Amesema nje na utengenezaji wa sabuni kikosi hicho kinajihusisha na ukulima wa alizeti, mahindi, kahawa na ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali, ufugaji wa mifugo mbalimbali na utengenezaji wa mafuta ya kupikia ya Alizeti.Amesema lengo ikiwa ni kuwajenga vijana wanaoingia kambini hapo kwa ajili ya mafunzo kuanza kujifunza namna ya ujasiliamali na kujitegemea hata watakapo rudi uraiani wakawe mfano na fundisho kwa vijana wenzao .

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuja kujifunza namna ya ujasiliamali kikosini hapo, na kuwataka vijana walio hitimu mafunzo hayo kutumia mafunzo hayo kulinda amani ya Nchi na kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kuondokana na umasikini uliopo katika familia zao.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura aliwapongeza wakufunzi wa kikosi hicho kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwanoa wahitimu hayo na kuwataka vijana kuyaishi yale mema yote waliojifunza pamoja na mafunzo waliyo yapata waendelee kuonesha nidhamu na utii watakapo endelea kuwepo kambini hapo.

Aidha alimuomba mkuu wa kikosi kuhakikisha anatafuta soko la kuuza bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wakurugenzi wa halmashauri kununua sabuni za kusafishia vyoo na kunawia mikono katika kambi hiyo ili kuuunga Mkono jitihada za vijana na jeshi la kujenga taifa.

"Ntoe pongezi zangu za dhati kwa wakufunzi wote najua mnafanya kazi katika mazingira magumu lakini kwa uzalendo mlionao mmehakikisha vijana wetu wAnajifunza namna bora ya maisha ikiwa ni pamoja na ujasili, uzalendo wa kujitoa kwa ajili ya Nchi yetu pamoja na ujasiliamali hii ndiyo falsafa tuliyo achiwa na waasisi wetu", alisema Bura.

Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi mmoja wa Wahitimu hao Deogratiusi Mgaya amesema mafunzo hayo yamewajenga kuwa wazalendo na walipoanza mafunzo hayo walianza vijana 739 baadhi ya hao walishindwa kumaliza mafunzo yao kwa sababu ya Kifo cha mwenzao mmoja na utoro wa baadhi na kupelekea idadi ya walio hitimu kuwa 732 ambao wamepata mafunzo hayo ya awali.

Hata hivyo amewaomba wazazi kuwahimiza watoto wao kuingia jeshi la kujenga taifa ili kuwafanya vijana kuwa wazalendo na kuepukana na vitendo viovu pamoja na kujijenga katika kutegemea kujiajiri wenyewe na bila kusubili mpaka Serikali itoe ajira kwao.

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images