Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 28 WA CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya hima maana Serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza kufanya mageuzi makubwa katika eneo la mazingira ya biashara kama ilivyobainishwa hivi karibuni na Waziri wa Viwanda na Biashara.


Makamu wa Rais ameyasema hayo  wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) unaotanguliwa na mafunzo endelevu ya Sheria.
“Nawapongeza TAWLA kwa namna ya kipekee sana kwa kutimiza miaka 28 ya uhai wake. Ni miaka 28 ya mafanikio makubwa sana. Nawapongeza kwa sababu, katika miaka 28 ya uhai wenu, hamjawahi kuyumba wala kutoka nje ya lengo la kuanzishwa kwenu, ambalo ni kutumia taaluma ya sheria kuwasaidia wanawake wasio na uwezo kupata msaada wa kisheria na haki zao.” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema anatambua na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) hapa nchini ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia taaluma ya sheria.Mkutano huo wa mwaka huu ambao umebeba kauli mbiu ya “Uwekezaji Wenye Tija; Kufungua Fursa kwa Mitaji ya Sekta Binafsi na Umma Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi”Makamu wa Rais amewataka Chama Cha Wanasheria Wanawake wawasaidie wanawake wajasiriamali kujua sheria, “Sisi kama wanawake kwanza ni kumnyanyua mwanamke, Ukimnyanyua Mwanamke umeinyanyua Tanzania.”
Makamu wa Rais aliwahakikishia TAWLA kuwa Serikali haina upungufu wa dhamira. “ Serikali yenu inajali na inao utashi wa kumkomboa mwanamke kiuchumi”,Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano maana maslahi ya TAWLA na ya Serikali yanakutana katikati katika suala hili.
Akimkaribisha Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile amewataka TAWLA kutumia maendeleo ya kiteknolojia kujitangaza ili wanawake wengi zaidi wapate taarifa zao na kuweza kupata msaada wa kisheria.Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka amesema TAWLA inapenda kuona mtoto wa kike na mwanamke anaendelea kupewa kipaumbele katika maendeleo ya Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Athanasia Soka wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama cha Wanasheria Wanawake TANZANIA(TAWLA) uliotanguliwa na mafunzo Endelevu ya Sheria uliofanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.




Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano mkuu wa 28 wa TAWLA. 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar yakutana leo

$
0
0
KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa  Zanzibar, leo tarehe 27 Mei, 2018 imefanya kikao chini ya  Mwenyekiti  wake ambae pia  Makamu Mwenyekiti wa  CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. 

Dk. Shein amewataka  wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC ya CCM Taifa Zanzibar kuendeleza kasi ya kuimarisha Chama kwa kutekeleza majukumu yao na kushuka kwa Viongozi na Wanachama wa ngazi mbali mbali ili CCM ishinde kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa  mwaka 2020.

Kauli hiyo ameitoa leo hii katika Kikao cha Kamati Maalum, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar. Pia kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa za Viongozi Wakuu wa kitaifa, Wakuu wa Idara wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar pamoja na mikakati ya Chama kuelekea 2020.
Vile vile kikao hicho kimejadili mambo ya utendaji ya Chama Cha Mapinduzi ambayo yamepelekwa katika Vikao vya ngazi za juu kwa ajili ya kujadiliwa.Pamoja na hayo wajumbe wa Kamati hiyo wamepongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020  inayotekelezwa kwa ufanisi zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Kikao hicho ni cha  kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108(2).

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:
CATHERINE PETER NAO
KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC
ITIKADI NA UENEZI CCM-ZANZIBAR.
 Naibu  Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza katika kikao hicho.
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein(katikati) akiongoza Kikao Cha Kawaida cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdulla Juma Saadalla (Mabodi).
 WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakifuatilia mambo mbali mbali katika kikao hicho.
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakifuatilia mambo mbali mbali katika kikao hicho.

Profesa Joseph Mbele akutana na msomaji mpya wa kitabu chake

$
0
0


Na Profesa Joseph Mbele


Jana jioni nilikutana na msomaji mpya wa kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Nilikuwa mjini St. Paul kuhudhuria darasa la Nu Skool, ambayo ni jumuia ya wa-Marekani Weusi wanaokutana mara moja kwa mwezi kutafakari na kujadili masuala mbali mbali.
Kwa kawaida, kunakuwepo na mtoa mada na kunakuwepo na masuali ya watu kuyajadili. Wakati mwingine inaonyeshwa filamu ya kuelimisha, ambayo inafuatiliwa na mjadala pia. Mada ya mkutano wa jana ilikuwa "The Language of Black America."
Jana hiyo, tulipokuwa tumemaliza darasa na baadhi yetu tukawa tunaendelea kuongea na kutambulishana, mama moja aliniambia kuwa anasoma kitabu changu na kuwa kinamgusa sana. Mama huyu m-Marekani Mweusi alisema kuwa mambo ninayoelezea yanamwezesha kujitambua ni nani kiasili. Alisema anakisoma kitabu kidogo kidogo kwa makusudi ili kuupata ujumbe vizuri, bila pupa. Alisema kuwa, katika maisha yake kama m-Marekani Mweusi alikuwa na hisia mbali mbali, lakini hakuelewa chimbuko lake, ila kitabu kimemfunulia chanzo, yaani u-Afrika. Mama huyu amenigusa kwa kauli hiyo.
Nilimwuliza alisikiaje habari za kitabu hiki, kwani hiyo ni moja ya duku duku zangu. Aliniambia kuwa alihudhuria mhadhara wangu Nu Skool na ndipo alipofahamu kuhusu kitabu changu. Alikiagiza Amazon. Alisisitiza kuwa amekiweka chumbani na anasoma kidogo kidogo kwa makusudi.
Nimeshasema katika blogu hii kuwa tangu mwanzo nilipoandika na kisha kuchapisha kitabu hiki, nilikuwa na wasi wasi na duku duku kuhusu namna wa-Marekani Weusi watakavyokipokea, kwa kuwa ninagusia tofauti baina yao na wa-Afrika kwa namna ambayo huenda ikawakwaza baadhi yao. Lakini nimeshukuru kwamba hadi sasa, inaonekana kuwa hali ni shwari.
Nimeguswa na kauli za mama huyu. Nimeguswa na furaha aliyo nayo kutokana na kusoma niliyoandika. Sina namna ya kuelezea ninavyojisikia, kwani amenifanyia hisani kubwa kwa kunijulisha kuwa niliyoandika yana maana kubwa kwake, katika kujielewa na kumfariji. Ushuhuda kama huu ni motisha kwangu, niendelee kutafakari mambo na kuandika.

kilomita 91 za mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya mkoani Mara zaimarishwa

$
0
0
Na Rehema Isango, Arusha
Jumla ya kilomita 91 za mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya mkoani Mara zimeimarishwa na sasa timu za wataalam wa upimaji ardhi na ramani zimeanza kazi hiyo wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha.
Kiongozi wa timu ya wataalam kutoka Tanzania Bw. Isaack Marwa amefafanua kuwa jumla ya alama kuu 66 zenye umbile la pembetatu zimeimarishwa ambapo kati ya hizo, 47 zimejengwa upya baada ya kung’olewa na 19 zimekarabatiwa baada ya kuchakaa katika maeneo ya mbalimbali ya wilaya za Rorya na Tarime mkoani Mara. Amesema kuwa wamefanikiwa kuweka alama mpya ndogo  takriban 900 zenye umbile la pembe nne ambazo zinaonana na kwamba sasa zinawezesha eneo la lote la mpaka wa kimataifa mkoani Mara kuonekana kwa urahisi ambapo kazi hiyo imetumia muda wa mwezi moja na majuma mawili.
Pamoja na kazi ya uwekaji wa alama, pia kazi ya usafishaji wa eneo la mpaka kwa urefu wa mita tano kwa kila upande wa nchi imefanyika  kwa kufyeka miti na kuwezesha alama hizo kuonekana kwa urahisi zaidi. Bw. Marwa amesema kuwa hivi sasa wameanza kazi mkoani Arusha baada ya kuruka kwa muda eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara lenye urefu wa kilomita 51 kutokana na mvua kuharibu barabara zinazotakiwa kufikisha vifaa vya ujenzi wa alama pamoja na wataalam.   
“Tumelazimika kuendelea na kazi hii katika kijiji cha Ololosokwan kilichopo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ambacho kimepakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kisha  tutarejea nyuma kumalizia kipande tulichokiruka baada ya njia zinazotusaidia kufikisha vifaa na wataalam hifadhini kuimarika.” Alisema Bw. Marwa
Alisema kuwa tayari kilomita 21 zimefanyiwa kazi mkoani Arusha kwa hatua za awali kwa kuwa kazi hii hufanyika kwa mpangilio wa timu zilizoundwa kitaalam hadi kufikia uwekaji wa alama za mpaka. Kazi ya uimarishaji wa mpaka kati ya Tanzania na Kenya inayolenga kuwezesha Serikali   kusimamia kwa ufanisi shughuli za mipakani, rasilimali za nchi pamoja na ulinzi na usalama  ilianza katikati ya Mwezi Machi mwaka huu ambapo Kilomita 238 zinaimarishwa kutoka kando ya Ziwa Victoria mkoani Mara hadi Ziwa Natron mkoani Arusha.  
 Bw. Nairoti Kenanda kutoka kijiji cha Njoroi katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha akishiriki kuchimba shimo lenye urefu wa mita moja kwa ajili ya kuwekwa alama ndogo ya mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya unaopita katika kijiji hiko.
Wanakijiji wa Kijiji cha Sukenya katika kata ya Soitsambu wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakisoma vipeperushi walivyopewa wakati wa utoaji elimu na uhamasishaji kuhusu uimarishaji wa mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya ulioanza mkoani Arusha.

MIPANGO YA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA BUYUNGU MAREHEMU KASUKU BILAGO

MWANAFUNZI WA ST. AUGUSTINE AJINYONGA MJINI MBEYA KWA MATOKEO YA MECHI YA REAL MADRID NA LIVERPOOL

$
0
0
Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo kikuu cha ‘St. Augustine’ kampasi ya Mbeya Moses Mashaka amejinyonga mara baadaya timu yake ya Liverpol kushindwa kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya, Polisi yathibitisha

DC TUNDURU ATOA MAAMUZI MAGUMU KWA WAFUGAJI, AWAPA RUNGU WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera ametoa maamuzi juu ya wafugaji ambao wameshindwa kufuga mifugo yao na badala yake wamekuwa wakiiachia inalalanda hovyo barabarani jambo linaloweza kusababisha ajali na kuharibu mazao mashambani.

DAGAA WILAYANI NYASA SASA KUUZWA KIMATAIFA

$
0
0
Halmashuri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imeazimia kuomba mkopo wa bilioni moja kutoka wizara ya fedha, Mkopo usio kuwa na riba kwa ajili ya mradi wa kuchakata na kuongeza ubora wa Dagaa Nyasa wanaopatikana Ziwa Nyasa kwa lengo la kuuza dagaa hao soko la kimataifa na kukuza kipato cha halmashauri na wavuvi.

NDANDA WAAHIDI KUBAKI LIGI KUU TANZANIA BARA, WASEMA USHINDI KWA STAND UNITED NI LAZIMA

$
0
0

Kikosi cha timu ya Ndanda FC kinasema maandalizi yake hadi sasa yanaendelea vizuri na kimewaahidi wanaMtwara kupambana kwa kadri iwezavyo ili kuhakikisha wanapata alama tatu kwa Stand United zitakazowabakisha ligi kuu Tanzania bara.

Siku ya Pili ya Mafunzo Ya Uandishi wa Habari za Kitakwimu kwa wanahabari mjini Dodoma

$
0
0
Washiriki wa mafunzo ya  uandishi wa habari za Kitakwimu yanayofanyika Jijini Dodoma kwa waandishi wa habari wakimsikiza  Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stephano Cosmas akiwasilisha mada kuhusu hali ya malaria hapa nchini.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir akiwasilisha mada kuhusu faida za uandishi wa habari  unaotumia takwimu.
 Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za kitakwimu Bi Sharon Sauwa akisisitiza jambo wakati wa majadiliano ya washiriki wa  mafunzo ya uandishi wa habari za Kitakwimu yanayofanyika Jijini Dodoma .

 Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO  Bibi Beatrice Lyimo akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za Kitakwimu yanayofanyika Jijini Dodoma .

Meneja wa Takwimu  Idara ya Kodi Bw. Fred Matola akisisitiza kuhusu umuhimu wa takwimu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za Kitakwimu yanayofanyika Jijini Dodoma kwa waandishi wa habari.


Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi Phausta Ntigiti akiwasilisha mada kuhusu  faida ya lugha ya kitakwimu na takwimu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za Kitakwimu yanayofanyika Jijini Dodoma. Picha na Ofisi ya Takwimu ya Taifa

MASHEIKH 11 WA SHIA ITHNA SHERIA WA KANDA YA ZIWA WASAIDIWA VYOMBO VYA USAFIRI

$
0
0
Masheikh 11 wa madhahebu ya Shia Ithna Sheria katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Kagera,Tabora,  Kigoma, Dodoma na Katavi wamepewa vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 80. 
Vitendea kazi hivyo pikipiki aina ya Freedom vilikabidhiwa jana kwa mashaeikh hao na mlezi wa taasisi ya The Bhakhiyatullah Foundation  ya jijini Mwanza Alhaji Sibtain Meghjee hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Bilal Muslim Mission of Tanzania Mwanza.
Akikabidhi pikipiki hizo Sibtain ambaye ni Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation aliwataka wakazitumie kutembelea jamii na kuibua kero na changamoto zinazoikabili bila kujali imani zao za dini kwenye maeneo yao na kisha kutoa taarifa na maoni ya utatuzi wa changamoto hizo.
“Pikipiki hizi mmekabidhiwa na nyaraka zote mkazitumie vizuri kwa kuhudumia jamii na isiwe kwa waislamu tu bali na waumini wa dini zote na sisi tunatoa huduma bila kubagua.Mzitumie vizuri ili na wengine waweze kupata lakini mkishindwa mtasababisha wakose,”alisema Meghjee na akawataka watoe mrejesho wa matokeo chanya yatakayopatikana kwenye jamii baada ya miezi sita tangu wakabidhiwe pikipiki hizo.
Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya masheikh walisema mbali na kuzitumia kuibua changamoto kwa waumini wao na jamii ya waumini wa dini zingine zitawasaidia kuwaingizia kipato.
“ Tofauti na zamani sasa kazi itakuwa rahisi kutokana na vipandwa (vifaa) hivi vya usafiri ambavyo vitaturahishia kuwafikishia ujumbe wa Allah (Mungu) waumini wetu lakini pia tutawafikia kwa urahisi watu mbalimbali kwenye maeneo yetu na kuibua kero na changamoto zao. Tunawashukuru wafadhili waliotovitoa,”alisema Sheikh Hussein Thuqumali wa TBF.
Naye Sheikh Daud Daud wa Mantare Kwimba alisema wanashukuru The Desk & Chair na BFT kutambua changamoto na mazingira magumu wanayofanyia kazi na vitendea kazi hivyo vitayarahisisha mazito na kuyafikia kwa urahisi ingawa pia wamepewa uhuru wa kuvitumia kujitafutia vipato pamoja na kuhudumia jamii kiroho na hivyo akamwomba Mwenyezi Mungu awajalie waliovitoa kwa maslahi ya jamii ya dini zote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa BTF Sheikh Hashim Ramadhan alisema vitendea kazi hivyo vimetolewa kwa lengo la kupigania amani na kusimamia maadili kwenye jamii kutokana na changamoto wanazopata watu wema waliobakia duniani na waja wa kiroho wa Mwenyezi Mungu ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Hadija, mke wa Mtume Muhamad S.A.W.
“Kwa sababu ya moyo wa imani ya Mwenyezi Mungu na mafundisho , chochote unachokitoa kwa heri, amani ili kuokoa maisha ya binadamu unakuwa umewekeza kwa Mwenyezi Mungu.Ni muhimu na hakuna jambo jema kama kusaidiana kwenye shida na taabu, kikubwa ni kusafisha nyoyo za watu wote wapate kusaidiana,”alisema Sheikh Hashim
Sheikh huyo wa Bilal Muslim Kanda ya Ziwa aliwaasa waumini wa dini mbalimbali, Waislamu na Wakristo kuacha ubahiri na badala yake watoe sehemu ya mali wanazomiliki kwa mujibu wa vitabu vyote vya dini ili wawasaidie maskini, yatima na wajane wanaoishi kwenye mazingira magumu ili wapate amani ya roho.
Akizungumzia masheikh hao kuingia mkataba na TBF kuhusu pikipiki hizo alisema wamefanya hivyo ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza baadaye na zitakuwa mali ya taasisi  na hawataruhusiwa kumpa (kummilikisha) mtu mwingine.
“Mikataba ya umiliki pamoja na matumizi ya pikipiki hizo inalenga kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza hapo baadaye. Leseni, mafuta na matengenezo itakuwa juu ya mtumiaji na pikipiki itatakiwa kuhifadhiwa kwenye kituo cha sheikh anakofanyia kazi,”alisema Sheikh Hashim.
 Mwenyekiti wa taasisi ya The Bakhiyatullah Foundation (TBF) ya jijini Mwanza Sheikh Hashim Ramadhan akizungumza na baadhi ya masheikh kabla ya kuwakabidhi pikipiki kwa ajili ya usafiri. Kulia ni mfadhili aliyetoa pikipiki hizo Sibtain Meghjee wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania na mwenye kilemba ni Maulana (waliokaa) wa pili kushoto Sayyed Amir Abass Bakri.
 Sheikh Hussein Thuqumali wa TBF akitia saini (mkataba) wa kumilikishwa pikipiki wanaoshuhudia ni Maulana Sayyed  Amir Abbas Bakri katikati na Mwenyekiti wa The Bakhiyatullah Foundation (TBF)   Sheikh Hasim Ramadhani.
 Sheikh Daud Daud wa Lamadi Simiyu akipokea hati za pikipiki aliyokabidhiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Alhaji Sibtain Meghjee kulia.
 Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee akimkabidhi pikipiki Shekh Alhamud Said Athuman wa Mantare Kwimba .Katikati mwenye kilemba cheupe ni Sheikh Hashim Ramadhani ambaye ni Mwenyekiti wa The Bakhiyatullah Foundation.
Masheikh wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa pikipiki za usafiri kutoka taasisi ya The Bakhiyatullah (TBF) pikipiki hizo zimetolewa na The Desk & Chair kwa masheikh hao ili kuwasaidia usafiri waweze kuibua kero na changamoto kwenye jamii. picha Baltazar Mashaka

MAJALIWA AHUTUBIA NA KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AAN TUKUFU AFRIKA KWENYE UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM, MTANZANIA ASHINDA

$
0
0

*Waziri Mkuu amtaka Sheikh Kishki akaonane na 
Waziri wa Ardhi atoe maamuzi ya kiwanja
          
KIJANA wa Kitanzania, Shujaa Suleiman Shujaa ameibuka kidedea na kunyakua kitita cha sh. milioni 15 katika mashindano ya 19 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30. 
Shujaa mwenye miaka 23 ambaye ni mkazi wa Morogoro, amejishindia pia laptop, kiwanja chenye hati eneo la Kigamboni kilichotolewa na kampuni ya Property International ya jijini Dar es Salaam pamoja na dola za Marekani 500 kutoka kwa Bw. Ahmed Seif “Magari” aliyetoa dola 500 kwa washindi wote watano. 
Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Mei 27, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuilinda amani iliyopo nchini kwani ikipotea hakuna atakayeweza kufanya ibada. 
“Mtakubaliana nami kuwa amani ya nchi yetu, ndiyo inatufanya tutembee vifua mbele dhidi ya wenzetu, ni neema kubwa ambayo kila muumini anapaswa kuilinda kwani ikipotea hata mkusanyiko wetu huu wa leo si rahisi kufanyika mahali kama hapa,” amesema. 
“Leo hii tuko hapa uwanjani kwa sababu tuna amani, kama Serikali isingekuwa inashirikisha Watanzania wote kulinda amani, basi tusingeweza kukutanika hapa. Kuna nchi 18 ziko hapa, na watu wake wamekuja hapa uwanjani kwa kuwa wana uhakika na amani tuliyonayo sisi Watanzania,” alisema. 
Alisema katika nchi ambazo amani imetoweka, watu wanalazimika kufanya shughuli za ibada majumbani au kwa kujificha. “Wenzetu hao, hawapati fursa adhimu kama hii ya kujumuika pamoja na majirani, ndugu, jamaa na marafiki kusikiliza na kufurahia kisomo cha Quran au kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii,” aliongeza. 
Aliwataka Watanzania waendelee kubeza na kupuuza kauli za walio wachache ambao kwao kuzungumzia amani ni kujipendekeza kwa Serikali. “Watu hao wamesahau kwamba tofauti katika Uislamu hazikuanza leo, lakini tofauti hizo hazikuwa sababu ya wema waliotangulia kuacha kuheshimiana na kushirikiana,” alisisitiza. 
Mshindi wa pili kwenye kundi hilo la juzuu 30 ni Ahmed Noor wa Sudan ambaye ameshinda sh. 12,564,750 pamoja na laptop akifuatiwa na Muzamil Awadh Mohamed wa Sudan alijishindia sh. milion 7.5 pamoja na laptop zilizotolewa na kampuni ya Camara Education.

Mshindi wa nne ni Abdulally A. Mohammed wa Kenya aliyepata zawadi ya sh. 5,711,000 na wa tano ni Ibrahim Maazur kutoka Niger, aliyepata sh. 3,426,000. Washindi hao wote watano walipewa zawadi ya kwenda hijja na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dk. Saleh Ally Sheikh. 
Washiriki wengine kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji Djibouti, Kenya, Ethiopia, Congo DRC, Nigeria, Ghana na Afrika Kusini. 
Washiriki wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watatu), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi watatu). 
Viongozi wengine waliohudhuria mashindano hayo ni Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kutoka Saudi Arabia, Comoro, Oman, Uturuki, Kenya, Msumbiji na Nigeria, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Rais wa taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Sharif Abdilkadir Al-Ahdal.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Sheikh Nurdin Mohammed Ahmad (maarufu kama Sheikh Kishki) akaonane na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi ili atoe maamuzi ya kiwanja chao kilichopo eneo la Matumbi ambacho mwaka jana aliagiza kifuatiliwe taratibu zake na kisha wapatiwe.

“Kuhusiana na suala la kiwanja mlichosema, mamlaka ya awali ni Manispaa ya Temeke na ilishakamilisha taratibu zote za kisheria, ikapeleka kwa Afisa Ardhi wa Mkoa kuona kama limepita kwenye vikao vyote ndipo wanaenda wizarani kupata kibali. Hakuna sababu ya wizara kuikatalia manispaa huku eneo lenyewe likiwa kwenye ramani kuu ya manispaa yenyewe, nenda mumuone Waziri mwenye dhamana, awape ardhi,” alisema.

Waziri Mkuu amefikia hatua hiyo baada ya kupewa taarifa akiwa jukwaani kwamba taasisi ya Al-Hikma iliwasiliana na Manispaa ya Temeke, hadi mkoani wakapewa barua zinaonyesha eneo liko sawa lakini walipofika wizarani wamekwamishwa na Afisa mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mama Mpetula.

Juni 11, mwaka jana katika mashindanio ya 18, taasisi ya Al-Hikma waliomba wapatiwe kiwanja na.118 kwenye kitalu E kilichoshikamana na kiwanja na. 117 chenye shule yao ya Al-Hikma Girls iliyoko Temeke ili waweze kujenga zahanati.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur- aan Tukufu  Afrika yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Al – Hikima, Mei 27, 2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh  Alashiek.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dr. Saleh  Alashiek   katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. 

 Baadhi ya waalikwa waliohudhuria katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
  Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
 Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dr. Saleh  Alashiek  akizungumza katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. 
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkabidhi Shujaa Suleiman Shujaa zawadi ya shilling milioni 15 baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 17, 2018. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir na watatu kulia ni Rais wa Taasisi ya Al- Hikima, Sheikh Shariff Abdukadir. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM NDG. KINANA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)) Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 27, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 27, 2018

WAAJIRI LETENI WATUMISHI WANOLEWE TPSC- MKUCHIKA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Mbeya

Serikali imeendelea kuwasisitiza waajiri wote nchini kuwapeleka watumishi wao Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kupigwa ‘msasa’ namna ya kufanya kazi za utumishi wa umma. 

Akizungumza jijini hapa mwishoni wa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika alisema kuwa ni muhimu waajiri hao wakawapeleka watumishi chuoni hapa hasa ikitiliwa maanani kwamba TPSC ndiyo chuo kilichopewa dhamana ya kuendesha mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiri wapya wa serikali.

Alisema pamoja na makujuku hayo pia Chuo hicho kina wajibu wa kusimamia mitihani ya utumishi wa umma katika program ya kuendeleza watumishi.Pia TPSC inatoa mafunzo ya kozi nyingine za muda mrefu na mfupi katika maeneo ya uongozi, Utawala na ya matumizi ya mifumo ya kisasa ya TEHAMA.

Waziri Mkuchika aliwaasa wahitimu kwamba mafunzo waliyoyapata chuoni hapo yasiishie kwenye vyeti bali yawe ni mafunzo ya kufanya kazi kwa weledi na kasi mpya yenye ufanisi wa ili kuleta tija kwa lengo kukuza uchumi wa taifa hili.

“Ninawasihi huu usiwe mwisho wa kujiendeleza kwani mafunzo huongeza ujuzi , weledi na mbinu maridhawa za ufanisi wa kazi hususan katika kujifunza teknolojia mpya,” alisema.
Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC chuoni hapo Jijini Mbeya. 
Mtendaji Mkuu wa TPSC Dkt Henry Mambo akizungumza wakati wa Mahafali hayo ya 28 ya TPSC Jijini Mbeya 
Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 28 ya TPSC wakiwa kwenye mahafali hayo chuoni hapo Jijini Mbeya 
Baadhi ya wafanyakazi wa TPSC wakifatilia mahafali hayo 

Water Mission Tanzania yazindua mradi wa maji wilayani Mwanga

$
0
0
Wakazi wa kata ya Kiruru iliyopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, wameanza kupata maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali ,kutokana na kuzinduliwa kwa mradi wa maji katika eneo lao. 

Mradi huo ambao una uwezo wa kuhudumia kaya 427 zenye wakazi zaidi ya 2,135 umejengwa na shirika la Water Mission Tanzania, wakishirikiana na shirika la Rotary Club ya Mwanga, Rotary International na Rotary Foundation. Kata ya Kiruru inayojumuisha vijiji vya Heria, Msikitini, Bhughuru na Mighareni, kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na tatizo la maji safi kutokana na kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kutokana na mazingira ya kijiografia ya eneo hilo. 

 Mkuu wa wilaya ya Mwanga,Bw. Aron Mbogho, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa kata ya Kiruru, kutokana na kuanzishwa kwa mradi huu mpya wa maji safi na salama katika eneo hili,ambao utawahakikishia wananchi kupata maji safi na salama wakati wote. 

Kwa niaba ya serikali napenda kutoa shukrani kwa shirika la Water Mission Tanzania na Washirika wake kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto ya tatizo la maji safi na salama kwenye jamii mbalimbali” Bw. Mbogho, alisema mradi huu utanufaisha wakazi wote wa kata ya Kiruru, hususani Wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji safi kwa ajili ya matumizi ya familia zao. Aliwataka wananchi wa Kiruru kutoa ushirikiano kwa wadau waliofanikisha mradi huu sambamba na kutunza miundombinu ya mradi ili uweze kuwa endelevu. 

“Kuwepo mradi huu katika eneo hili kutapunguza kwa kiasi kikubwa maradhi mbalimbali yatokanayo na matumizi ya maji yasio salama” alisisitiza. Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Mission Tanzania, Isack Abdiel alisema “Tunayo furaha kubwa siku ya leo kutokana na kukamilisha mradi huu mpya hapa wilayani Mwanga ambao unazinduliwa leo. Mradi huu ni mwendelezo wa jitihada za shirika letu kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto ya kumaliza tatizo la maji kwenye jamii. Nina imani wakazi wa eneo hili la mradi mtahakikisha mnatunza miundombinu ya mradi ili uwe endelevu kwa matumizi ya sasa na ya vizazi vijavyo”.

 Isack Abdiel pia alishukuru viongozi wa serikali wa wilaya ya Mwanga na wadau wengine kwa kuunga mkono Shirika la Water Mission Tanzania, na kwa kutoa ushirikiano wakati wote wa ujenzi wa mradi huu hadi kufikia sasa ambapo umefikia hatua ya kuzinduliwa. Shirika la Water Mission Tanzania, lilianza kufanya kazi nchini Tanzania, mnamo mwaka 2013 likiwa linajishughulisha na ujenzi wa miradi ya kukabiliana na changamoto ya maji kwenye jamii. Hadi sasa Shirika lina miradi katika mikoa zaidi ya 6 ikiwemo, Dodoma, Arusha, Geita, Kagera, Kigoma and Tanga na Kilimanjaro. 

 Ofisi za makao makuu ya shirika hili kwa hapa nchini yapo jijini Dar es Salaam ambayo inaratibu miradi yote inayoendeshwa na shirika hapa nchini. Mbali na Tanzania shirika la Water Missions International, linaendesha miradi ya kukabiliana na changamoto ya maji katika nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Haiti, Honduras, Mexico, Peru, Belize na Indonesia.
Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Bw. Aron Mbogho akikata utepe kuzindua mradi.
Mmoja wa wakazi wa kata ya Kiruru akitwishwa ndoo ya maji aliyochota kwenye mradi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wakifuatilia matukio.
Afisa mwandamizi wa Water Mission Tanzania,Isack Abdiel akiongea wakati wa hafla hiyo --- 

BENKI YA MKOMBOZI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya benki ya biashara ya Mkombozi Method Kashonda akizungumzia jinsi benki hiyo ilivyofanikiwa kupata faidi baada ya kodi ya shilingi bilioni 1.44 kwa mwaka 2017 kutoka shilingi bilioni 1.05 ilivyokuwa mwaka 2016. Sawa na ongezeko la asilimia 37.1  katika mkutano mkuu wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bank ya Mkombozi, George Shumbusho akizungumzia matarajio ya benki kuanza kutumia mfumo wa kimataifa wa ripoti za fedha wa IFRS (International Financial Report Standard), ili kumuhakikishia mteja anapata huduma za mkopo kwa uhakika.
Mhashamu baba askofu mkuu wa jimbo Katoliki la Dodoma, Beatus Kinyaiya akifafanua juu ya mkakati wa benki ya mkombozi wa kushawishi waumini wa kanisa katoliki kununua hisa kwa wingi ambapo gawio la mwaka 2017 limeongeza kwa shilingi 5 sawa na shilingi 25 kwa hisa kutoka gawio la shilingi 20 ilivyokua mwaka 2016.
Makamu mwenyekiti wa bodi ya Mkombozi Profesa Marcellina M. Chijoriga akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Wanahisa wa benki ya Mkombozi wakifuatilia mkutano kwa makini. 
Picha ya pamoja

Naibu Waziri Masauni akabidhi vifaa vya michezo kwa timu 20

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni amekabidhi vifaa vya michezo kwa Timu 20 zinazoshiriki ligi ya Masauni and Jazeera Cup.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo Masauni amesema michezo inajenga udugu kutokana na mkusanyiko wa watu mbalimbali.
Masauni amesema michezo kwa sasa ni ajira kwani wengine wataonyesha vipaji vyao na timu zikawaona na zikaweza kuingia nao mikataba.
Aidha amesema kwake ataona faida pale baadhi ya vijana watakaonyesha vipaji na timu zikawachukua.
Aidha amesema ataendelea kuwa bega kwa bega na vijana kwa kudhamini ligi mbalimbali zitaanzishwa katika jimbo la Kikwajuni
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Hamad Masauni akikabidhi vifa vya michezo jezi na Mpira kwa timu 20 zinazoshiriki ligi ya Masauni na Jazeera Cup katika Jimbo la Kiwajuni
 Sehemu ya vifaa vya michezo.
Baadhi ya viongozi wa tumu mbalimbali wakiwa wameshika jezi za timu zao zinazoshiriki ligi ya Masauni na Jazeera Cup katika Jimbo la Kiwajuni

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUTURISHA NYUMBANI KWAKE JIJINI DAR

$
0
0

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkaribisha, Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh Alashiek (wapili kushoto) na ujumbe wake wakati alipofuturisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu,  Oysterbay jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofuturisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam  Mei 27, 2018. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh Alashiek na kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir.
  Baadhi ya waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika futari aliyoiandaa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Mei 27, 2018. 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kushoto) akiagana na baadhi ya wanawake walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZAZI WASHAURIq KUWASIMAMIA WATOTO WABUNIFU ILI WAFIKE MBALI

$
0
0
--
Kiongozi wa HDIF Tanzania , David McGinty akizungumza wakati wa kufunga Wiki ya Ubunifu iliyofanyika katika Ukumbi wa Costech Jijini Dar es Salaam
 Kiongozi wa HDIF Tanzania , David McGinty akitoa cheti kwa moja ya vijana walikuwa wakijitolea kutoa huduma kwa watu walifika katika wiki ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwa ushirikiano wa UKAID na Costech
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la HDIF Hannah Mwandoloma akipokea zawadi kutoka kwa moja ya Viongozi wa HDIF mara baada ya kumalizika kwa Wiki ya Ubunifu.
 Kiongozi wa HDIF Tanzania , David McGinty akizungumza jambo na sehemu ya wadau kutoka Mashirika Mbalimbali walioshiriki wiki ya Ubunifu
Sehemu ya Wanafunzi walioshiriki Wiki ya Ubunifu  wakifatlia kwa makini hotuba mbalimbali wakati wa kufunga

NAIBU SPIKA AONGOZA WABUNGE KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA BUYUMBU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuletwa Bungeni kesho Jumanne tarehe 29 Mei, 2018 kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake Kasuga, Wilayani Kakonko, Mkoani Kigoma. Awali mapema leo, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson aliahirisha Bunge kutokana na Msiba huo.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama  akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Capt. George akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Mbunge wa kuteuliwa na Rais Mhe. Salma Kikwete  akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
 Mbunge wa Tarime Mjini , Mhe. Esther Matiko akisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.
Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago. Aliyeketi kusaini ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mhe. Mahmoud Mgimwa.
 Waheshimiwa Wabunge wakijipanga kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Mwl. Kasuku Samson Bilago.


PICHA NA BUNGE
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images