Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Takwimu Zatajwa Kuchochea Maendeleo Endelevu

$
0
0
Na Mwandishi  wetu
Warsha ya Wadau Kuhusu  hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa wa Kijinsia, Utawala na  Amani .
Akizungumza wakati wa warsha ya siku mbili   Mjini Dodoma Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Kutoka Ofisi  ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Bibi Ruth  Minja amesema kuwa  warsha hiyo ni muhimu  na itasaidia  katika kubainisha  maeneo yanayotakiwa kufanyiwa tafiti na kuzalisha takwimu zitakazotumika katika kuchochea maendeleo mara baada ya kubaini maeneo ambayo bado takwimu zake hazijakusanywa.
"  Warsha hii itatusaidia  kuona ni wapi kuna takwimu ambazo hazijafikiwa kweye maeneo mbalimbali ya kisekta ili ziweze kukusanywa na kusaidia katika kuleta maendeleo" Alilisisitiza  Bibi Ruth.
Akifafanua  amesema kuwa jukumu kubwa la Ofisi hiyo ni kukusanya na kuchambua na hatimaye kutoa takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ili kuchochea maendeleo .
Kwa upande wake  mmoja wa wawezeshaji katika warsha hiyo Davis  Adieno kutoka nchini Kenya amesema kuwa wanapongeza hatua iliyochukuliwa ya kuwa na warsha hiyo ya wadau kwa kuwa itasaidia takwimu zinazokusanywa zitasaidia wadau katika kupanga mipango ya maendeleo.
Aliongeza kuwa wadau wamekusanyika katika warsha hiyo ili kujifunza na wataweza kushiriki kikamilifu katika kuondoa  umasikini.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Usawa wa Kijinsia wa wanawake ( UN Women) Bibi Usu Mallya amesema kuwa uchambuzi wa Takwimu unasaidia kuonesha upungufu  wa takwimu zinazotakiwa kukusanywa  katika sekta mbalimbali.
Aliendelea kusema kuwa  Takwimu zilizopo zimenyumbulishwa kijinsia na kupitia warsha hiyo washiriki  wataweza kuendeleza takwimu za kijinsia.
Warsha ya ya Wadau Kuhusu  hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa wa Kijinsia, Utawala na  Amani  inafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili ikiwashirikisha wadau kutoka sekta ya umma , Binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo.
 Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi  ya Taifa ya  Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama  Jijjini Dodoma.
  Mtaalamu kutoka Taasisi ya Africa Regional Manager, Global  Partnership for Sustainable Development   Data Bw. Davis Adieno akiwasilisha mada katika Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama Jijjini Dodoma ikiratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshighulikia Usawa  wa Kijinsia wa Wanawake (UN Women) Bibi  Usu  Mallya akizungumzia maana ya  takwimu za kijinsia wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama Jijjini Dodoma.
 Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi  ya Taifa ya  Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo Bw. Said  Ameir wakati  wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala,  amani na usalama Jijjini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala,  amani na usalama Jijjini Dodoma.
 Mratibu wa Mpango Kabambe wa kuboresha na kuimarisha  Takwimu Nchini  (Tanzania Statical Master Plan ) Bw. Philemon  Mahimbo  akiwasilisha mada  wakati wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya Maendeleo  Endelevu,  Usawa wa Kijinsia,  Utawala,  Amani na Usalama  Jijjini Dodoma.  (Picha na Frank Mvungi- MAELEZO)

Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba

$
0
0
 Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella amewataka viongozi na watendaji mbalimbali wakiwemo wa vyama vya msingi vya ushirika AMCOS kuwahamasisha wakulima kuongeza kasi ya uvunaji wa zao hilo ili kunufaika na msimu mpya wa ununuzi ambao tayari umeanza.

Mongella ametoa rai hiyo hii leo baada ya kufanya ziara wilayani Misungwi ili kujionea hali ya ununuzi wa pamba baada ya msimu mpya kuzinduliwa Mei Mosi mwaka huu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bukama wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya kutembelea maghala mbalimbali ya vyama vya msingi vya ushirika AMCOS wilayani Misungwi, Mongella amewataka wasimamizi wa zoezi hilo kuhakikisha mizani haichezewi kwa minajili ya kuwapunja wakulima.

Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania, James Shimbe amesema tayari bodi hiyo imetoa leseni za ununuzi wa zao la pamba kwa vyama vya msingi vya ushirika AMCOS ambapo amewataka wanunuzi wote kuhakikisha wanachukua leseni hizo ili kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Naye John Masalu ambaye ni Meneja Shughuli, Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza amesema maandalizi yote yamekamilika hivyo ni wakati mwafaka wakulima kunufaika na zao la pamba kupitia AMCOS ambazo zinasimamia zoezi hilo.

Issa Malando ambaye ni mwandishi AMCOS ya Mwalu Mabuki amesema bei ya pamba hivi sasa ni shilingi 1,100 kwa kilo moja hivyo matarajio ni wakulima kuanza kuuza pamba kwa wingi licha ya kwamba baadhi yao bado wanaendelea kuvuna.

Awali akitoa taarifa kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Misungwi, Katibu Tawala wilaya hiyo Peter Michale amesema zaidi ya vituo 100 vya ununuzi wa pamba vimejiandaa vyema kusimamia zoezi hilo ambapo tayari vituo 18 vimepokea zaidi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya malipo ya wakulima.

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA SH. 240 MIL KUSAIDIA SEHEMU YA UKARABATI WA JENGO LA WAGONJWA WA DHARULA HOSPITALI YA BUGANDO, MWANZA

$
0
0
Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (katikati) akikabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Beki ya CRDB, Dk. Charles Kimei mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na arobanini (240 mil) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bungando, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dkt. Abel Makubi na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akitoka hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Beki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na arobanini (240 mil) kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Bungando, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi akizungumza machache wakati akitoa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya CRDB, kwa msaada wa shilingi milioni mia mbili na arobanini (240 mil) kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ukarabati na upanuzi wa Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dkt. Abel Makubi (kushoto) akimueleza jambo Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (koti jeusi) aliyeambatana na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo pindi walipotembelea sehemu ya Jengo la Huduma za wagonjwa wa dharula (Emergency Medicine Department) inayofanyiwa ukarabati katika Hospotali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza Mei 25, 2018. Wengine pichani ni baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU AKIWEMO RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kushoto) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kulia) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Phillip Mangula (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa   Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Article 0

IDARA YA UHAMIAJI YAZINDUA PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI DAR ES SALAAM, WAKAZI WAHIMIZWA KUZICHANGAMKIA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jami
PASIPOTI ya kieletroniki imezinduliwa leo na Idara ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa na Rais mapema Januari mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameeleza pasipoti hiyo ina manufaa makubwa hasa katika teknolojia, kukidhi viwango vya kimataifa na kufafanua ukiwa nayo unakuwa na nakala ya pasipoti kwenye simu mara baada ya kupakuwa applicationi hiyo.

Mhandisi Ndikilo ameeleza gharama za kupata pasipoti hiyo ni Sh.150,000 na kueleza kuwa pasipoti za kawaida zitaendelea kutumika hadi Januari 2020.

Aidha ametoa rai kwa wananchi hasa katika utunzaji wa pasipoti hizo ili zisiangukie kwa wahalifu na gharama kwa pasipoti iliyopotea mara ya kwanza ni shilingi laki 5 na ikipotea kwa mara ya pili italipiwa shilingi laki 7 na nusu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewaomba wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam wachangamkie fursa hiyo, pia ametoa wito wa kada mbalimbali hasa wafanyabiashara wadogo kupata pasipoti hizo ili kuweza kufanya biashara kwa uhuru na kuvuka mipaka hii itawasaidia kutangaza biashara zao.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Chrispin Ngonyani amehaidi kusimamia kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa na amewaomba wananchi kueleza changamoto wanazokumbana nazo ili ziweze kutatuliwa mara moja.

Pia, Kamishina wa Uhamiaji, uraia na pasipoti Gerald Kahiga ameeleza kuwa pasipoti hizo zinatolewa kwa raia wa Tanzania pekee na zikitolewa wazitunze kwa usalama wa hali ya juu na wamejipanga na harufu yoyote ya rushwa katika utoaji wa pasipoti hizo na ametoa rai kwa wananchi kutotumia mawakala kama daraja la kupata pasipoti hizo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Cathy Kamba amefurahishwa na uzinduzi huo kwani hata katika ilani ya uchaguzi walisisitiza suala la ulinzi na usalama na amemshukuru Rais kwa kuendelea kuboresha maisha ya watanzania.

TABOA YADAI KUSIKITISHWA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU KUPUUZWA

$
0
0
*Sasa waomba kukutana naye ili wamueleze malalamiko yao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TUMESIKITISHWA kupuuzwa kwa maagizo ya Waziri Mkuu!Hiyo ndio kauli ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA) kwa madai licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra), kukutana na wadau wa usafiri kujadili malalamiko mbalimbali lakini hadi sasa wameshindwa kufanya hivyo.
Taboa wamedai Waziri Mkuu Majaliwa Mei 10 mwaka huu akiwa Bungeni alitoa maagizo kwa Sumatra kukutana na wadau wa usafirishaji  kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi wa malalamiko yao yakiwamo ya faini kubwa  wanazotozwa wamiliki wa mabasi kwani imekuwa kero na kusababisha kuifanya shughuli hiyo kwa hasara.

Katibu Mkuu wa Taboa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa kitendo cha Sumatra kuendelea kukaa kimya bila kuitisha kikao kimewavunja moyo na wanasikitika kuona maagizo yaliyotolewa yameshindwa kufanyiwa kazi huku wao wakitozwa faini kubwa ambazo wamezilalamikia muda mrefu.

"Tulitarajia baada ya maagizo tungeitwa wadau wa usafirishaji ili tujadiliane kwa pamoja na kupata muafaka badala ya kuendelea kukaa kimya. Sisi tumeendelea kuumia kwa kutozwa faini kubwa.Ombi letu ni moja tu hizi faini haramu ambazo zinatutesa ni vema zikaachwa kwanza hadi Sumatra watakapotuita.

 "Kwanza kanuni ambazo wanazitumia kututoza faini tunaziita haramu kwani wakati wa mchakato wake hatujashirikishwa na kibaya zaidi tukaona tu zinaanza kutumika.Kwa sasa matumaini yetu ni kwa Waziri Mkuu na hivyo ombi letu kwake tuaomba kumuona ili atusikilize, imani yetu tutapata muafaka na haya manyanyaso ya Sumatra yatakwisha,"amesema Mrutu.

Amesisitiza Mrutu kuwa kwa muda mrefu Taboa wamekuwa katika kusigana na Sumatra kuhusu sheria ya makosa mbalimbali iliyopitishwa Bungeni  waliyodai kutozingatia usawa na hivyo kuathiri utendaji wao katika sekta hiyo.

"Tunashumkuru Waziri Mkuu kwa kauli yake aliyoitoa bungeni kwani ameelezea hali halisi ilivyo kati yetu na Sumatra na akaomba wadau wote wa usafirishaji tuitwe ili kutafuta ufumbuzi wa yale ambayo tunayalalamikia,"amesema.

Katika mkutano huo wa Bunge unaoendelea, Waziri Majaliwa alisema mgogoro uliopo baina ya Sumatra na Taboa  unaohusu faini mbalimbali wanazotozwa wasafirishaji, ulishafika katika Ofisi yake, ambapo aliagiza Sumatra kukaa chini na Taboa na kupitia upya kanuni za uendeshaji ili kufikia muafuaka, jambo ambalo halijatekelezwa na Sumatra hadi sasa.

 Kwa kukumbusha tu Waziri Mkuu aliamua kutoa maagizo hayo kutokana na swali la Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Singida Martha Mrata, kumuuliza ni mgogoro uliopo kati ya Taboa na Sumatra  utamalizika ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara ya Taboa hadi kufikia hatua ya kuitisha migomo.

"Waziri Mkuu alijibu swali hilo la mbunge na kutoa maagizo wiki mbili mbili zilizopita lakini hakuna hatua ambazo zimechukuliwa.Kinachoendelea kwa sasa ni kulipishwa faini kubwa ambazo ndizo tunazilalamikia,"amesisitiza Mrutu.

Awali wasafirishaji hao waliilalamikia Sumatra kwa hatua yake ya kuandaa kanuni bila kuwashirikisha na baadae kuipeleka Bungeni na kuwa sheria, ambayo pamoja na  mambo mengine inawapa maumivu  ya kuwatoza faini kuanzia Sh 20,000 hadi Sh 500,000 kwa makosa ambayo kimsingi hayawahusu.

Mrutu amefafanua wanachotaka haki iwe inatendeka pindi yanapotokea makosa ya barabarani , lakini ni jambo la kushangaza hata kosa ambalo linafanywa na dereva lakini adhabu inakwenda kwa mmiliki na kusisitiza dawa ya kuondoa ajali ya barabarani si faini pekee yake,hivyo wakae wajadiliane.

Alipoulizwa iwapo ombi lao la kukutana na Waziri Mkuu limepokelewa Mrutu amesema ni mapema mno kulizungumzia suala hilo lakini ifahamike tu wameomba kumuona na wanaamini watakubaliwa kwani nia yao ni njema na ndio maana wamekuwa na subira.

TCRA WATOA LESENI KWA WATOA HUDUMA ZA HABARI MTANDAONI

$
0
0
*Mkurugenzi TCRA asema 45 ndio wamekidhi vigezo kati ya waombaji 262
*Asema mchakato bado unaendelea, atoa sababu kuweke gharama za usajili

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAMLAKA ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania(TCRA)imesema leo ni siku muhimu katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na kushuhudiwa wadau wa habari wakiwa wamekamilisha hatua za usajili ili watambulike na kutumia fursa hiyo ya utoaji na upashaji habari kupitia mtandao wa intanenti.

Kutokana na kukamilisha mchakato huo TCRA imetoa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti 45 kati ya watoa huduma 262 walioomba na kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa.Miongoni mwa waliopewa leseni baada ya kukamilisha taratibu hizo ni pamoja na Michuzi Media Group(MMG)

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba wakati akikabidhi cheti cha usajili kwa wamiliki 45 wa Blogs, Redio na televisheni za mtandaoni na kusema kuwa zipo faida nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo zinafahamika kwa wengi.

"Kama tunavyofahamu kwa miongo mingi sasa sekta ya habari na utangazaji imekuwa ikipata habari kwa njia ya redio na televisheni kupitia majukwaa mbalimbali kama mitambo iliyojengwa ardhini,Satellite na Cable.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao , iliyofanyika leo  katika ukumbu wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Blogers , Krants Mwantepele akizungumza kuhusiana na mwitikio ulionyeshwa kwa wamiliki kujisajili TCRA iliyofanyika , jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (MMG), Ainde Ndanshau katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mkurugenzi wa Blogu ya Wananchi , William Malecela ‘LE MUTUZ ‘ Vkatika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mwakilishi wa  Mtandao wa Bongo 5, Yassin Ng’itu katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa Mmiliki wa Habari Mseto , Francis Dande katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA),  Mhandisi James Kilaba akikabidhi  leseni kwa  watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao kwa  Mmiliki wa Radio Seven ya Mtandaoni,  Atu Mandoza katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TCRA , jijini Dar es  Salaam.
 Baadhi ya waandishi na wamiliki wa watoa huduma kwa njia ya mtandao

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Mussa Zungu akiongoza kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa zao la korosho  linaendea kuwanufaisha wakulima Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita  wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
 Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akitolea ufafanuzi tofauti iliyopo kati ya shule za Serikali na Binafsi na kusisitiza kwamba mitaala ya kimataifa imeruhusiwa ili kukidhi mahitaji ya raia wa kigeni wanaoishi nchini.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philip Mpango akizungumza jambo na Mbunge wa Bunda Mjini wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Jacqueline Ngonyani akiomba ufafanuzi kwa Serikali kuhusu ulipaji wa Mawakala wa pembejeo wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiwasalimie wabunge wakati wa utambulisho wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Juma (kushoto)  wakati wa kikao cha thelathini na saba cha mkutano wa kumi na moja Jijini Dodoma leo.
Picha zote na Daudi Manongi, DODOMA

BALOZI WA POLAND NCHINI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

$
0
0
Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski akilakiwa na wenyeji wake alipo wasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam yaliyopo wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Balozi huyo ametembelea Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.
Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (kulia) akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi. (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye aliyeketi (mbele) akisoma taarifa ya Jeshi hilo kwa Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kulia) alipotembela Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Balozi huyo alifika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (kushoto), akimsikiliza kwa makini msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi. (Wa pili kulia) ni Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (wa pili kushoto), wengine ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (wa pili kulia), Kamishna wa Usalama Dhidi ya Moto, (CF) Jesuald Ikonko (wa kwanza kushoto) na msaaidizi wa Balozi wa Poland hapa nchini, Bi. Ewelina Lubieniecka (kulia).
Picha ya pamoja.
(Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

RAIS Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya Chai na Mkurugenzi Mkuu wa RARI

$
0
0
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chai Tanzania (Tea Board of Tanzania – TBT).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote umeanza tarehe 21 Mei, 2018.
Mhandisi Steven Daudi Malekela Mlote anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Research Institute – TARI).
Uteuzi wa Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo umeanza tarehe 22 Mei, 2018 na kabla ya uteuzi huu, alikuwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Mashariki, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ilonga Mkoani Morogoro.
Dkt. Geofrey Suleiman Mkamilo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fidelis Angelo Myaka ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

23 Mei, 2018

TFDA YAKAMATA VIPODOZI, POMBE KALI VILIVYOPIGWA MARUFUKU

TIB CORPORATE BANK WASHIRIKI TAMASHA LA BIASHARA JIJINI ARUSHA

TMRC YAZINDUA MPANGO WA HATIFUNGANI WA MIAKA MITANO WENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 120

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Utoaji Mikopo kwa Mabenki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC), imezindua mpango wa hatifungani wa miaka mitano kwenye Soko la Hisa (DSE).

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo Ammish Owusu-Amoah ameongoza uzinduzi huo ambao pia umeshuhudiwa na wawekezaji pamoja na wadau mbalimbali toka sekta za fedha, nyumba na sekta nyingine.

Hivyo uzinduzi wa utoaji wa dhamana ya TMRC ulifanyika baada ya TMRC kupokea kibali kwa ajili programu ya utoaji wa dhamana ya miaka 5 yenye thamani ya Sh. Bilioni 120. Mpango huo ulipata kibali kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji (CMSA) pamoja na Soko la Hisa (DSE). Kampuni hiyo ya TMRC itaorodheshwa kwenye DSE.

Aidha, CMSA na DSE, zilijumuisha kuendelea kwa TMRC kutoa dhamana ya ushirika wake ambayo itakuwa kiasi cha Sh Bilioni 12.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC) Oscar Mgaya akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB Plc, Ineke Bussemaker( wa tatu kutoka kulia) pamoja na Mwenyekiti wa TMRC ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya BOA Tanzania, Ammishaddai Owusu-Amoah, wakikata kwa pamoja utepe wa uzinduzi wa mpango wa hatifungan.
 Mtendaji Mkuu wa Fedha wa TMRC, Oswald Urassa akiwaelezwa wadau mambo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa kampuni ya TMRC.
 Mwenyekiti wa kampuni ya TMRC, Ammishaddai Owusu-Amoah, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mpango wa hatifungani wa miaka mitano kwenye Soko la Hisa (DSE).
Baadhi ya wageni walioshiriki wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Utoaji Mikopo kwa Benki na Taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo wa nyumba Tanzania (TMRC) Oscar Mgaya  kwenye uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam .

PASPOTI YA KIELETRONIKI YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM


WAZIRI MKUU AHIMIZA MATUMIZI YA MIFUMO YA ULINZI WA MIJI YA KIELEKTRONIKI

ALIKIBA VS SAMATA...

GP SIRRO ATOA ONYO KWA WAFUNGWA WALIOPATA MSAMAHA WA RAIS NA KUENDELEA KUFANYA UHALIFU

MKURUGENZI JIJI LA DODOMA ATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA VIWANJA

$
0
0
Na Ramadhani Juma
Ofisi ya Mkurugenzi, Dodoma

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeongeza muda wa kulipia Viwanja kwa wateja wake wote walionunua Viwanja kuanzia Aprili 20, mwaka huu kutoka siku 30 yaani Mwezi mmoja hadi siku 90 yaani miezi mitatu.
Aidha, Halmashauri hiyo inatarajia kuendelea kuuza Viwanja vya eneo la Iyumbu kuanzia tarehe 5 Juni, 2018 kwani tayari imeshamaliza kazi ya kushughulikia malalamiko ya Wakazi wa Ngaloni walioibuka na kudai kutolipwa fidia hapo awali.
Hayo yametangazwa na Mkurugenzi wa Jiji hilo Godwin Kunambi wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini humo leo ambapo amesema Halmashauri imefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na mwenendo wa wateja kulipia Viwanja vyao ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi bilioni 4 zimeshalipwa kwa Wananchi kama fidia ya maeneo yao yaliyotwaliwa wakati wa upimaji.
Alitoa wito kwa wateja wote walionunua viwanja na wanaoendelea kununua kutumia muda ulioongezwa kama fursa ya kukamilisha malipo yao ili kuepuka usumbufu usio wa lazima baada ya muda huo kumalizika.
“Kwa wale wote waliokuwa wanasubiri Viwanja vya Iyumbu wafike katika eneo letu la kuuzia Viwanja ambalo ni Ofisi za Manispaa ya zamani jirani na Sabasaba siku ya tarehe 5 mwezi ujao…tutaanza kuviuza siku hiyo” alisema Kunambi.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa Jiji ametoa muda wa miezi mitatu kwa watu wote waliopewa Viwanja na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) katika maeneo ya Njedengwa, Miganga, Mkonze, Iyumbu New Town Center, na Mkalama na hawajakamilisha malipo ya Viwanja hivyo kukamilisha ndani ya kipindi hicho vinginevyo Halmashauri itavitwaa kwa mujibu wa Sheria na kuviuza kwa wateja wengine wenye mahitaji.  
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo ambapo ameongeza muda wa wateja wa Viwanja kulipa gharama za Viwanja vyao kutoka Mwezi mmoja wa awali hadi miezi mitatu sasa.

TFDA YAKAMATA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU ZENYE THAMANI YA MIL 72/-

$
0
0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
 VIPODOZI ambavyo vimepigwa mrufuku vyenye thamani ya milioni 72,406,500 pamoja na Pombe kali zilizopigwa marufuku zenye thamani ya Sh.Milioni 11,356,000 vimekamatwa vikiwa kwenye maduka wakiuziwa wananchi.

Hayo yamebainiswa leo Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) , Agnes Kijo ,wakati alipokuwa anatoa taarifa kuhusu  ukaguzi maalum wa kukagua na kuondoa katika soko  vipodozi visivyosajiliwa,pombe kali zisizosajiliwa pamoja na kufuatilia uhalali wa biashara ya vipodozi kwenye mitandao ya kijamii.

Kijo ameseka katika ukaguzi huo ambao ulishirikisha Jeshi la Polisi,TFDA,Shirika la Viwango nchini (TBS),Wakala  wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Ofisi ya Rais,

Amesema katika ukaguzi huo walifanya katika mikoa ya Dar es Salaam,Pwani,Mwanza,Shinyanga,Geita,Mara na Arusha ambapo ukaguzi huo ulichukua mda wa siku mbili.

Kijo amevitaja vipodozi vilivyokamatwa ni Carolight cream,Citrolight Crem,Sivoclaire Cream,Max light cream,dawa zinazodaiwa kuongeza maumbile kwa wanaume(Maxman capsules) sabani za kurudisha usichana ( Virginity soap).

Vipodozi vengine ni Dawa za kuongoeza ukubwa wa maziwa kwa wanawake (Papaya breast enlarging crem) pamoja na dawa za kutibu magonjwa ambazo zimekuwa zikitumika kimakosa.

Sanjari na Vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku pia katika ukaguzi huo wamekatamata  pombe kali zenye ujazo milimita 200  ambazo  zinazofungaswa kwenye viroba.

"Tumekamata pombe hizi ni imperial blue whsky,White mischief vodka,contessa preimium dry gin vodka,Konyagi (Ladha ya pesheni)magic movement vodka,officers choice ,Dewer's white label,Officers can spirit,sinature vodk "amesema Kijo.

Hata hivyo Kijo amesema baada ya ukaguzi huo wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga majadala 24 ya kesi katika vituo vya  Polisi dhidi ya watuhumiwa  na majengo ya biashara 29 yamefungwa.

"Baada ya uchunguzi wa makosa kukamilika hatua za kisheria zinatachukuliwa ikiwa pamoja na kuwapeleka mhakamani watuhumiwa na kutoa dhabu kulingana na sheria ya Chakula,Dawa na Vipodozi ,Sura  219.Adhabu hizo zinajumuisha kufutwa leseni ya biashara na kuharibu bidhaa zilizokamatwa kwa gharama ya mtuhimiwa,"amesema

Kijo amewataka wananchi kuendendelea kutoa taarifa za wale wote wanaojihusisha na biashara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku ,Biashara harany ya vipodozi na dawa katika mitandao ya kijamii ili hatua zichukuliwe na Mamlaka husika.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na operesheni walioifanya hivi karibuni.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images