Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 LAITIKISA KIGOMA

$
0
0
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu wakiburudika na Wasanii wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013
 Burudani ya kutosha kabisa
 Hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu.
 Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi,Christian Bella akikamua jukwaani usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkoani Kigoma ambapo watu wamefurika ile mbaya.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
 Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu. PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Marvin Gaye akikupa 'Lets Get It On' live

MAAZIMIO YA MAFUNZO YA KAMATI ZA BUNGE ZINAZOSIMAMIA FEDHA ZA UMMA NA BAJETI (PAC, LAAC NA BC) OCEANIC BAY HOTEL BAGAMOYO 17th AUGUST, 2013

$
0
0

1)      Kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa kuna umuhimu wa kukutanisha wadau wakuu wanaohusika hususani BOT, HAZINA, Kamati za Bunge na CAG ili kuweza kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa deni hilo.  Vile vile imeamuliwa kuwa Serikali ishauriwe kuunda chombo huru kitakachosimamia deni la taifa.

2)      Baada ya kuanzisha mfumo mpya wa bajeti ya Serikali mwaka huu kuna umuhimu wa kuandaa mkutano wa kutathimini mafanikio na changamoto za mfumo huu na kujadili mambo ya kuboresha zaidi mfumo mzuri wa bajeti ya Serikali.

3)      Kamati za Bunge zinazoshughulikia usimamizi wa fedha na rasilimali za taifa zishughulikie zaidi Maafisa Masuuli hatarishi (risk based) ili kuleta thamani ya fedha katika utendaji wao.  Kamati zishirikiane na CAG katika kuamua ni Afisa Masuuli yupi aitwe kukutana na Kamati.

4)      Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge na TAMISEMI waanzishe utaratibu wa kuratibu mikutano na mafunzo ya Wakurugenzi wa Halmashauri kwa pamoja kuliko kila Wizara kuwaita watendaji hao katika sehemu mbalimbali kwa muda tofauti na kuwafanya kutokuwepo ofisini kwa kipindi kirefu.

5)      Mfumo wa kutunza kumbukumbu za hesabu na nyaraka mbalimbali katika Serikali Kuu na Halmashauri uboreshwe ili zinapohitajika zipatikane kwa wakati muafaka bila kisingizio cha aina yoyote.

6)      Kuhusu ukaguzi wa ufanisi CAG asisubiri mpaka asikie malalamiko kutoka kwa wananchi au kwenye magazeti bali akague mara kwa mara sehemu zote zenye matatizo.

7)      Taarifa za mwaka za Kamati za Bunge ziwe na kipengele cha kiwango cha utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati yaliyotolewa awali. Kamati ziwezeshwe kifedha ili ziweze kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yao. Kanuni za Bunge zieleze utaratibu wa ufuatiliaji wa Maazimio ya Bunge na namna utekelezaji wake utavyowasilishwa Bungeni.  Vile vile Bunge litenge siku ya kujadili Serikali ilivyoshughulikia hoja za Kamati za Bunge.  Spika ashauriwe kuhusu umuhimu wa kuunda Kamati ya Bunge ya kufuatilia ahadi za Serikali.

8)      Mikataba katika ngazi ya Serikali za Mitaa iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

9)      Serikali inatakiwa kufanya jitihada za ziada kuzalisha wataalam wa fani ya manunuzi.  Kuna umuhimu wa PPRA kuongezewa nguvu za ziada za kiutendaji ikiwa ni pamoja na fedha na wafanyakazi.
10)  Bajeti ya Bunge iongezwe kupitia Mfuko wa Bunge na iwasilishwe Bungeni na Naibu Spika na sio Ofisi ya Waziri Mkuu.

11)  Serikali iandae mjadala wa kitaifa wa kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na vitendo vya rushwa na mmomonyoko wa maadili vinavyoongezeka kwa kasi hapa nchini. Vilevile viongozi wa umma na watendaji waongoze kwa mfano kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza majukumu yao.

12)  Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangaza umiliki wa mali za viongozi.  Hii inapelekea viongozi kutoweka wazi mali wanazomiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa ukweli.  Ni vyema Sekretarieti wakafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa Umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili kuwawezesha wananchi kuweza kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao; na pale ambapo kiongozi hatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi taarifa hiyo itolewe kwa Tume.

13)  Kwa kuwa leseni za udereva za sasa zinaweza kuweka kumbukumbu za makosa ya usalama barabarani, basi TRA ikishirikiana na  Wizara ya Mambo ya Ndani zihakikishe ya kuwa Askari wa Usalama Barabarani wanatumia utaratibu huu wa kisasa wa kutoa  “notification” na kutoa risiti za malipo za elektroniki.

14)  Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki.  Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.

15)  TRA ihamasishe wananchi na wafanya biashara umuhimu wa matumizi ya risiti za elektroniki, wafanyabiashara waelimishwe umuhimu wa kutoa risiti hizo na wananchi waelimishwe umuhimu wa kudai risiti kila wanapofanya manunuzi. Elimu na uhamasishaji huo unaweza kufanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo sanaa, timu za michezo, bendi za muziki, redio, TV, mbao za matangazo n.k.

16)  Serikali idhibiti makampuni ya uwakala wa kupakia na kupakua mizigo (clearing and forwarding) yaliyopo Bandarini ili kudhibiti mapato ya forodha.

17)  Sheria ya “Anti Money Laundering” ya 2006 irekebishwe ili iweke viwango vya fedha ambazo mtu anaweza kuingia au kutoka nazo nchini bila kuzitaja  (declare). Kuna umuhimu wa Waziri wa Fedha kutengeneza kanuni za kutekeleza Sheria hiyo.

18)  Benki Kuu iandae mfumo thabiti wa usimamizi wa Maduka ya Fedha (Foreign Bureau de Change), na kuhakikisha kutungwa kwa sheria inayozuia matumizi ya fedha za kigeni katika shughuli za kibiashara hapa nchini.

19)  The Proceeds of Crime Act, 1991” ifanyiwe marekebisho na kuweka kifungu kinachomwezesha AG/DPP kuwa na mamlaka ya kuomba mahakama kufungua kesi ya madai (Civil Forfeiture) kwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

20)  Imesisitizwa kwamba CAG akague misamaha ya kodi na kuweka taarifa hiyo kwenye taarifa za kila mwaka.

21)  Serikali iimarishe Taasisi zinazoshughulikia maadili utawala bora na uwajibikaji kama vile Sekretariati ya Maadili ya Viongozi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Takukuru, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Kamati ya Maadili ya Bunge ili ziweze kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizoanzisha Taasisi hizo.


22)  PCCB na vyombo vingine vinavyohusiana na kushughulikia masuala ya jinai wawe waalikwa kwenye vikao vya Kamati za Bunge ili waweze kutoa ushauri kwenye kamati hizo.

Maalim Seif amuaga Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen Qi Man

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen Qi Man, nyumbani kwake Mbweni. Balozi Chen alikutana na Maalim Seif kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi zawadi Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen Qi Man, nyumbani kwake Mbweni. Balozi Chen alikutana na Maalim Seif kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea zawadi kutoka kwa  Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen Qi Man, nyumbani kwake Mbweni. Balozi Chen alikutana na Maalim Seif kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej akipokea  zawadi kutoka kwa  Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen Qi Man, wakati wakiaagana kufuatia balozi huyo kumaliza muda wake wa utumishi nchini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Chen Qi Man, nyumbani kwake Mbweni, kufuatia balozi huyo kumaliza muda wake wa utumishi nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej na kushoto ni Afisa ubalozi wa China aliyepo Zanzibar. Picha na Salmin Said, OMKR.

UZINDUZI WA SERENGETI FIESTA 2013 ULIVYONOGA MJINI KIGOMA USIKU KUAMKIA LEO

DIAMOND MUSICA, FIVE STAR MODERN TAARAB ZILIVYOUMANA DAR LIVE

$
0
0
Wanamuziki wa Diamond Musica wakiwajibika jukwaani.
Wanamuziki wa Five Star wakiwajibika stejini.
Didi Namba wa Diamond Musica akiimba.
Wanenguaji wa Diamond wakionyesha umahiri wao wa kunengua.
Ally J wa Five Star akifanya mambo stejini.
Baadhi ya mashabiki wakiserebuka.
Mashabiki wakilishana keki kwa upendo.
Husna Semhando akionyesha umahiri wake wa kunengua.
BENDI ya Diamond Musica na Five Star Modern Taarab usiku wa kuamkia leo ziliwapagawisha vilivyo mashabiki waliohudhuria katika onyesho la pamoja lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

wadau jihadharni na kanyaboya hii, ukiletewa katika email ipige chini

$
0
0
Dear Sir/Madam....!!

We are starting a very big research project in USA and Canada. This project takes place every month.
We are leading agency specialized in (Global) Customer Service Research.

We need to recruit mystery shoppers to join our project to work as a surveyor. Should you interested,
your wages would be US $200 per assignment.

Payment check or money order will be in a certain amount that you will be asked for your bank cash
and then garnish your wages and have the rest for evaluation.

Please provide the following information below if you interested.
All fields are required in order to serve you better.

1.Full Name :
2.Full A.d.d.r.e.s.s :
3.StateCityZip :
4.A.g.e :
5.Phones :
6.Gender :
7.CurrentJob :

Thank you, we waiting for your response.

Sincerely,
M`S - G R O U P

Huduma ya Mawasiliano ya Vodacom yarejeshwa.

$
0
0
*Ni Baada ya moto kuungunza mitambo  ·      
*Mtandao ulizimwa kwa saa 16 nchi nzima
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) kuhusiana na kurejeshwa kwa huduma za mtandao wa Vodacom baada ya kukosekana kwa saa 16 kufuatia moto kuzuka katika kitovu cha kuendeshea mitambo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena. Pamoja nae ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa.

Dar es Salaam, Agosti 18, 2013: Baada ya kukosekana kwa huduma za mtandao wa Vodacom kwa takribani masaa 16, huduma hizo zimerejeshwa katika hali yake ya kawaida asubuhi  ya Jumamosi ya Agosti 17.
Akizungumzia tatizo lililosababisha kukosekana kwa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wa mtandao huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema chanzo cha kukatika kwa mawasiliano nchi nzima siku ya Ijumaa ni moto uliotokea katika mtambo mkuu wa kuendeshea mtandao (Main Switch) uliyoko Dar es Salaam.

 “Kufuatia hatua hiyo, hatukuwa tena na uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote kuanzia siku ya Ijumaa jioni hadi Jumamosi asubuhi, hali hii iliathiri wateja wetu wote kwa ujumla kwani walishindwa kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki ambao wote ni wateja wetu, alisema Meza.

 Aidha, Meza aliomba radhi kwa jamii ya Watanzania na wateja wa Mtandao wa Vodacom kwa kukosa mawasiliano katika kipindi hicho, na kusema kuwa wateja wote wa mtandao wa Vodacom watarudishiwa gharama zote kwa huduma yoyote walionunua na kuhitaji kuitumia wakati ambapo mtandao  haukuwa unapatikana.
“Fidia hizi kwa wateja wetu wote zitatolewa siku ya Jumatatu ya Agosti 19, 2013 alisema Meza.
 “Tunaishi katika dunia ambayo mawasiliano ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku hivyo tunaelewa kuwa tatizo hili limekuwa kikwazo kikubwa kwa wateja wetu, Na tunawashukuru kwa kuwa waelewa na wavumilivu katika kipindi chote ambacho tumekuwa tukikabiliana na tatizo hili, alisema Meza.
Meza alihitimisha kwa kuhakakikishia Watanzania na wateja wa Vodacom kwa ujumla kuwa Vodacom imedhamiria kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya hali ya juu nchini.
 “Ninapenda kuwashukuru wafanyakazi wetu wote na washirika wetu ambao kwa pamoja wamefanya kazi bila kuchoka katika kuhakikisha huduma zote zinarejea hadi katika hali ya kawaida hadi kufikia Jumamosi asubuhi, Jitihada zao na kazi kubwa waliyoifanya imewezesha huduma zote kurejea katika hali ya kawaida, alihitimisha Meza.

Article 20

TAARIFA TOKA TFF LEO Agosti 18, 2013

$
0
0
25 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TFF
Wanamichezo 25 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Fomu hizo zilianza kutolewa juzi (Agosti 16 mwaka huu) ambapo wawili wamechukua nafasi ya Rais na wengine wawili Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

Waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea urais ni Jamal Malinzi na Omari Musa Nkwarulo wakati umakamu wa rais hadi sasa umewavutia Wallace Karia na Ramadhan Nassib.

Waliochukua fomu za ujumbe ni Athuman Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe na Khalid Mohamed.

Wengine ni Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir, Omari Walii, Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidao.

Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechukua fomu mpaka sasa ni Hamad Yahya anayeomba kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti.

Fomu za maombi pia zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni saa 10 kamili jioni ya Agosti 20 mwaka huu.

Fomu zikiambatanishwa na risiti ya malipo (receipt) au malipo ya benki (deposit slip) kupitia akaunti ya TFF namba 01J1019956700 iliyoko CRDB tawi la Holland House zirejeshwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa mkono au kwa barua pepe (email) ambayo ni tanfootball@tff.or.tz .

MECHI YA NGAO YA JAMII YAINGIZA MIL 208
Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2013/2014 iliyochezwa jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 208,107,000. Washabiki 26,084 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga kushinda Azam bao 1-0.

Mgawanyo wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 31,745,135.59, asilimia 10 ya mchango wa kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama ya tiketi sh. 7,309,866.

Uwanja sh. 22,236,194.76, gharama za mchezo sh. 13,341,716.86, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,188,445.44, TFF sh. 13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MAZOEZI YA JOGGING LEO YAZIKUTANISHA TENA KLABU ZA BIAFRA NA NAMANGA

$
0
0
Katika kuimarisha mahusiano na ujirani mwema kwa vilabu vya jogging, wanamichezo kutoka vilabu vya Biafra na Namanga vilifanya mazoezi ya pamoja ambayo yalianzia mtaa wa Isere na kuingia barabara ya Kawawa hadi barabara ya kuelekea kwa Kopa mpaka kwenye makutano ya barabara ya Mwananyamala kuelekea Viktoria, kisha barabara ya Bagamoyo hadi Sayansi kwenye makutano ya barabara ya Rose Garden (Tembo Avenue) kutokea kwa Nyerere, kisha kufuata barabara ya Mwai Kibaki hadi Moroko kuelekea Biafra na kumalizia klabuni. Fuatilia matukio kwa picha.
Tulikutana na vijana wa Mwendo Kasi Jogging (wenye jezi nyekundu)

Tulipata bahati ya kukutana na bibi ambaye alituunga mkono kwa kukimbia pamoja nasi. Kwa picha zaidi
BOFYA HAPA

Zungu: Uchawi katika mpira hakuna

$
0
0


Mbunge wa Ilala Mhe Mussa Azzan Zungu (katikati), akizungumza wakati wa kufungua semina ya viongozi wa Ligi kuu na Daraja la Kwanza leo kwenye uwanja wa Taifa.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu (DRFA), Almas Kassongo na kushto ni Katibu mkuu wa DRFA Msanifu Kondo.
MBUNGE wa Ilala Mussa Azzan Zungu leo amefungua semina kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema uchawi katika mpira hakuna.
Zungu alisema hayo wakati akifungua semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Alisema mpira unataka maandalizi mpira wa miguu unahitaji maandalizi na pesa na kwamba pia unahitaji ghrama kubwa ili kuuendesha.
“Miaka ya nyuma tulikuwa tukicheza mpira kienyeji ingawa kulikuwepo na sheria 17, sasa msione wale wanaoshindwa kucheza hawajui, tatizo hawajawekeza na ndio maana washuka madaraja,” alisema.
Zungu pia alitumia fursa hiyo kumpongeza nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa kutojisikia na kuhudhuria semina hiyo licha ya uchovu wa mechi ya jana ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam walioshinda bao 1-0.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo alisema bado ataendelea kupambana na kutowaangusha wadau wa mpira wa miguu Mkoa wa Dar es Salaam.
“Nipo katika mapamabano ya mpira kwa muda mrefu na nitahakikisha timu mojawapo ya Dar es Salaam inaendelea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya  Vodacom.

IGP MWEMA AKABIDHI UENYEKITI WA SARPCCO NCHINI NAMIBIA.

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akiongozwa na Askari wa Namibia kuingia katika ukumbi wa mkutano ambapo alitumia fursa hiyo kukabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akimkabidhi kitara Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga kama ishara ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) baada ya Tanzania kumaliza uongozi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja.Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano maalumu wa wakuu hao uliofanyika nchini Namibia.

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania IGP Said Mwema akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga baada ya kumkabidhi uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO). 


Habari na picha na Frank Geofray
Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia

Inspekta Jenerali wa Polisi wa Tanzania IGP Said Mwema amekabidhi uenyekiti wa Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika SARPCCO baada ya kumaliza kipindi chake cha mwaka mmoja cha kuongoza umoja huo.
IGP Mwema amekabidhi uongozi huo kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Nchi ya Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga wakati wa mkutano mkuu maalumu wa viongozi hao uliofanyika jana katika jiji la Windhoek na kuhudhuriwa na Wakuu wa Polisi kutoka nchi wanachama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka INTERPOL na SADC.
Akizungumza katika mkutano huo IGP Mwema alisema katika kipindi cha uenyekiti wake walifanikiwa kufanya Operesheni kubwa iliyojulikana kama Operesheni Usalama ambayo ilijumuisha umoja wa SARPCCO na ule wa Afrika Mashariki EAPCCO,operesheni ambayo ililitea manufaa makubwa katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.
Alisema Nchi wanachama wanapaswa kuendeleza ushirikiano wao ili kuhakikisha kuwa ukanda wa kusini mwa Afrika unakuwa salama kwa kukabiliana na uhalifu hasa kwa kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu.
Aidha alisema katika kipindi hicho Tanzania iliweza kuandaa mikutano yote ya kamati tendaji za SARPCCO ambazo ziliweza kuibua maazimio mbalimbali ya kupambana na uhalifu ambayo yaliweza kupitishwa na kuwa mikakati endelevu katika kukabiliana na uhalifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga alisema atahakikisha umoja huo unakuwa imara na kupambana na uhalifu unaovuka mipaka kama vile wizi wa magari, wahamiaji haramu, usafirishaji wa fedha haramu na binadamu, wizi wa mitandao pamoja na madawa ya kulevya.
Naye Mgeni rasmi katika mkutano huo Waziri wa Usalama na ulinzi wa Namibia Immanuel Ngatjizeko alisema serikali ya Namibia itaendelea kushirikiana na umoja huo kwa kila hali ili kuhakikisha Nchi wanachama na Afrika kwa ujumla zinakuwa salama.
IGP Mwema alikabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO mwezi Septemba mwaka 2012 mjini Zanzibar kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika kusini ambapo kutokana na uenyekiti huo mikutano yote ya umoja huo ilikuwa ikifanyikia nchini Tanzania.

katibu Mtendaji mpya wa SADC Dkt.Stergomena Tax apongezwa

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza katibu Mtendaji mpya wa SADC Dkt.Stergomena Tax wakati wa kikao cha 33 cha wakuu wa nchi za SADC kilichofanyika jijini Lllongwe Malawi leo kikao hicho kimeisha leo. Kushoto ni Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Rais wa  Dkt. Joyce Banda(wa pili kushoto) Jaji Mkuu wa Malawi Mhe. Anastazia Msosa,na Mwenyekiti wa Umoja wa Africa (AU) Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma wakimpongeza  katibu Mtendaji mpya wa SADC Dkt.Stergomena Tax baada ya kula kiapo wakati wa kikao cha 33 cha wakuu wa nchi za SADC kilichofanyika jijini Lllongwe Malawi.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


Katibu Mtendaji mpya wa SADC Dr.Stergomena Tax ala kiapo leo

$
0
0
Katibu Mtendaji mpya wa SADC Dr.Stergomena Tax akila kiapo mbele ya jaji mkuu wa Malawi Mhe. Anastazia Msoza wakati wa mkutano wa 33 wa wakuu wa nchi za SADC uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi, leo.

MSHINDI WA NYUMBA YA AIRTEL YATOSHA AKABIDHIWA HATI NA UFUNGUO WA NYUMBA YAKE

$
0
0

 Mmbando  akitoa ufafanuzi juu ya mshindi  huyo alivyopatikana kabla ya  kumkabidhi hati yake  ya nyumba  leo
 Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando  akionyesha  hati ya  nyumba 
 Mshindi  wa  nyumba ya  Airtel yatosha  akisoma hati ya nyumba  yake aliyoshinda  baada ya  kukabidhiwa  leo

 Mshindi  wa  nyumba ya Airtel Yatosha  akionyesha  hati yake ya  nyumba aliyokabidhiwa  leo,huku akiwa na  wafanyakazi  wenzake  waliofika  kushuhudia 


Ofisa mahusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando akimkabidhi mke  wa mshindi  wa  nyumba ya Airtel yatosha Bw  Sylivanus Juma Wanga Bi Veronica Wanga huku kushoto mume wake ambae ni mshindi akishuhudia mshindi  huyo ni mhasibu  wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC inayojihusisha na mapambano dhidi ya ukatili  wa kijinsia mkoa wa Iringa ,wengine pichani ni wafanyakazi  wenzake waliofika kushuhudia  hafla  hiyo  iliyofanyika Hotel ya M.R mjini Iringa.

msaada tutani: BIBI SITI HAMAD KHAMIS ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU YA FIGO

$
0
0
BIBI Siti Hamad Khamis (pichani)  anasumbuliwa na ugonjwa wa figo ambazo zimeshindwa kufanyakazi. Kwa hiyo  anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema utakaomuwezesha kutibiwa.
 
Amelazimika kuomba msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha yake kutokana na gharama kubwa za matibabu zinazoendelea kuikabili familia yake kwa muda mrefu sasa. Kwa mfano kila wiki anatakiwa kwenda hospitali mara tatu ambapo kwa siku hulipa sh. 350,000. 
 
Matibabu anayopatiwa ni kusafishwa damu ili kupunguza sumu mwilini, kupimwa na chanjo.
 
Anaomba kwa wale watakaoguswa na tatizo linalomsumbua, wamsaidie matibabu ndani na nje ya nchi au wamchangie kupitia AC 2011601674 Benki ya NMB, tawi la Bank House.
 
Au wawasiliane na mumewe kwa simu namba 0774215217.
 
Ahsanteni. 

JK arejea Dar baada ya kuhudhuria mkutano wa 33 wa SADC nchini malawi

$
0
0
Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Katibu Mtendaji wa SADC Dkt.Stergomena Tax kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo wakati wa mkutano mkuu wa 33 wa viongozi wa nchi za SADC uliofanyika jijini Lilongwe Malawi mwishoni mwa wiki.Wapili kushoto ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik aliyefika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumlaki Rais na Ujumbe wake. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
Kwa mapicha zaidi ya mkutano huo BOFYA HAPA

MWANZA YALIPOKEA KWA SHANGWE TAMASHA LA KILI MUSIC TOUR 2013

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Fleva),Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwajibika jukwaani sambamba na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo kabambe.
Mkali wa Ryms afahamikae kama Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wa Mitulinga akiwapagawisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza
Mwanamuziki bora wa Hip Hop hapa nchini kwa mwaka 2013, Kala Jeremiah akiwarusha mashabiki wake waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Bob Junior na madansa wake.
Mkali wa RnB,Ben Pol akifanya vitu vyake jukwaani.
Ngoooshaaa....... Ngoooshaaaa....Ngooooshaaaaaa....... au ukipenda waweza muita Fareed Kubanda kwa jina alilopewa na Wazazi wake na pia waweza muita Fid Q akikamua vilivyo ndani ya Uwanja wa nyumbani huku shangwe zikitawala uwanjani hapo.
Shangwe tupu zilitawala uwanjani hao.

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article4620-live.html

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images