Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 228 | 229 | (Page 230) | 231 | 232 | .... | 3278 | newer

  0 0

    

  Inter-university Business Competition (IBC) is a platform created to enhance university students who are enthusiastic in business and have ideal business ideas that can be implemented with sustainable capital. The event opens door for students to meet with successful entrepreneurs and business intellectuals offering experience and guidance on how to starts a business. This is an ideal tipping point to life changing of every participating individual.

  The first best five (5) ideas will be rewarded Laptops, Money and many more that our partner provides. The best 20 ideas will be given an opportunity to exhibit their ideas yet attend training ranging from business management, Business Proposal write up, communication and personality

  This is the second IBC to be hosted in Northern zone; it is organized by Kiliative Solutions EA ltd and facilitated by Mt. Meru University Arusha campus. This year’s event is on from August to October 2013. We encourage all University Students in Northern Region to submit their Business Ideas to email address ibc@kiliativesolutions.comfrom 1st August-30thSept 2013...Exhibition and idea presentation to take part from 23rd-26thOctober 2013 at Mt Meru University

  Contact Person

  Mrs Atwitye Makwetta

  Mt Meru University-Arusha Campus

  Dean of Students

  Mob. 0754 475924

  Email-atwitye@kittymail.com


  Allan Kalisa

  Business Development Manager

  Kiliative Solutions EA ltd.

  Mob.0783 857777


   E-mail marketing@kiliativesolutions.com


  0 0

   Ofisa Uendeshaji Mwandamizi wa Sekta Isiyo Rasmi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Khalfan akifafanua jambo kuhusu huduma wanazotoa wakati wa uzinduzi wa Ushirikiano wa Kikazi kati ya Umoja wa Wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi, NSSF, Equity Bank na Sanitas Hospital uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mlezi wa umoja huo, Ramadhani Madabida na Meneja wa Huduma za Wateja wadogo wa benki ya Equity, Janeth Zoya. (Picha na Habari Mseto Blog)
   Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakiwa katika uzinduzi huo.

  SHIRIKA La Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeupongeza Umoja wa Wafanyakazi wa Sekta Zisizo Rasmi (Informal Sector Workers Union -ISWU), huku likiwataka kutumia vema fursa itokanayo na unganiko la kikazi baina ya umoja huo, NSSF, Equity Bank na Sanitas Hospital.

  Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Sekta Zisizo Rasmi wa NSSF, Salim Khalfan, alipokuwa akizungumza na wanachama wa ISWU walioshiriki semina na uzinduzi wa ushirikiano huo chini ya programu ya ‘Community Cooparetive Micro Insuarance (CCMI).’ 

  Khalfani aliuambia umoja huo kuwa, NSSF inampongeza Mkurugenzi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Sekta Zisizo Rasmi, Dauda Wadauda kwa kuratibu umoja huo na kwamba shirika lake liko tayari kusaidiana katika kuwawezesha kufikia malengo yao kibiashara.

  Aliongeza kuwa, uwezo mkubwa wa kusaidia harakati za afya na matibabu kwa wajasiriamali iliyonao shirika lake  ulikuwa unakosa nguvu ya kuwafikia mmoja mmoja miongoni mwa wajasiriamali na kwamba kuungana kwao kunarahisisha NSSF kuwafikia na kuwawezesha.

  “Wanachama, mnapaswa kutumia fursa hii kwa kuwekeza kadri muwezavyo pesa zenu katika shirika letu, ili kunufaika na huduma za NSSF, ambayo kwa kushirikiana na Equity Bank na Sanitas Hospital, iko tayari kukabili changamoto zenu za ndani na nje ya ujasiriamali.

  Kwa upande wake, Mlezi wa ISWU, Ramadhani Madabida, aliishukuru NSSF kwa kukubali kuungana katika vita dhidi ya umaskini ambao aliutaja kama moja ya vyanzo vinavyochangia ukosefu wa amani katika nchi yoyote duniani na kwamba amani ni uwezo wa kukabiliana na changamoto.

  Mkurugenzi wa ISWU, Dauda Wadauda, aliwataka wajasiriamali hao kutumia vema elimu waliyopata katika semina hiyo na kuwataka wawe mabalozi wazuri kwa wajasiriamali walio nje ya umoja huo ili kuongeza idadi yao na kuwa na nguvu ya pamoja.

  0 0

  Mkuu wa Huduma za M-Pesa, Bw. Jackson Kiswaga (kulia) anamsikiliza Bw. Khalfani A. Khalfani (kushoto) mmiliki wa shule ya Answar, iliyoko Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwa wakuu wa shule kuhusu utumiaji wa huduma ya M-Pesa kulipa karo. Mkutano huo uliandaliwa na kampuni ya Vodacom pamoja na Elimu Solutions. Mkutano huo ulifanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Bw. Nixon Bonaventure kutoka kampuni ya Vodacom.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Taasisi na Ulinzi wa Ikolojia kutoka nchini China, wakati ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 17, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Tuzo ya Utunzaji wa Mazingira.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Taasisi na Ulinzi wa Ikolojia kutoka nchini China
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Tuzo ya Utunzaji wa Mazingira na Kiongozi wa Ujumbe huo, Dkt. Jiang Ningjun, wakati Ujumbe huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 17, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Tuzo hiyo. Kulia ni Xiaoyi Jin. Picha na OMR


  0 0  0 0


  DAKIKA YA 37 TAYARI STURRIDGE KESHAPACHIKA BAO LETU LA KWANZA LA MSIMU DHIDI YA STOKE CITY NDANI YA ANFIELD LEO

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Chen Qiiman Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Balozi Chen anakaribia kumaliza muda wa utumishi wake wa Ubalozi wa miaka miwili na nusu hapa Zanzibar.
  Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar akipokea zawadi wa mlango kutyoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kama ishara ya kufunguliwa mlango wa kuingia Zanzibar wakati wowote licha ya kwamba anamaliza muda wake wa utumishi hapa Nchini. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

   Kamera yetu leo imefanikiwa kuzinasa taswirazz mbali mbali ndani ya Jiji la Mwanza,ikiwemo hii ya Baiskeli kuovateki Pikipiki.
   Tatizo la Madereva wa Daladala kusimama hovyo ni la kila mahali hapa nchini,na wao hawana noma wala nini.
   Kipitata shoto cha Makutano ya Barabara ya Capripoint na Stesheni kikiwa bize kweli kweli.....
   Taswirazz ya Ziwa Victoria ashubuhi ya leo.
   Moja ya alama za Jiji la Mwanza ni Mawe haya yafahamikayo kama Bismark Rocks.


  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya wakuu wa nchi za SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 33 SADC uliofanyikaKatika ukumbi wa Bingu International Conference centre,mjini Lilongwe Malawi leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Waziri Mkuu wa Namibia Marko Hausiku,Makamu wa Rais wa Zambia Dr.Guy Scott,Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),Rais Dkt.Jakaya Kikwete,Mwenyeji Rais Dkt.Joyce Banda wa Malawi, Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji,Katibu Mtendaji wa SADC anayemaliza muda wake Dkt.Tomaz Salomao, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, na Rais Ian Khama wa Botswana. Chini Rais Kikwete akiongea na mwenyeji wa mkutano huo Rais Dkt. Joyce Banda wa Malawi.
  Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


  0 0

  Collective guilt over the genocide in 1994 has shaped the world’s relations with Rwanda ever since. Without question, the systematic killing of 800,000 people is one of the foremost historic blights of the last century. And the international community deserves blame for ignoring facts and avoiding action when intervention could have saved thousands.
  But it’s time to take off the kid gloves when dealing with this tiny, landlocked country with outsized influence in East Africa. If there’s any hope of Rwanda winning truly lasting stability, it must change course and stop fueling conflicts across its borders.
  The progress Rwanda has made since the genocide is nothing less than remarkable. Any visitor to Kigali today will immediately note the clean new streets. The capital is filled with new malls catering to the wealthy, restaurants offering panoramic views of the city and cafés brewing Rwanda’s own world-renowned coffee.
  Over the last decade, Rwanda’s economy has averaged above 8 percent growth per year, according to the I.M.F., and it is considered the best place in Africa to start a business, according to the World Bank’s latest rankings. Millions have been pulled out of poverty, people live more than 20 years longer than they did in the 1990s, maternal and child mortality rates have dropped dramatically, and health care coverage is nearly universal. When I was working with the U.S. Agency for International Development on health and economic projects in Rwanda, I couldn’t help but be impressed by how quickly the country was developing.
  All of this has made Rwanda a darling of aid donors, and Rwandan leaders are deft at handling them. Officials feel at home at international summit meetings and President Paul Kagame — one of the most popular African leaders on Twitter — exudes confidence on the global stage.
  This combination of international sympathy, impressive economic growth and political savvy has caused the United States, Britain and other powers to largely turn a blind eye to Kigali’s transgressions.


  0 0

  Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko,mapema leo asubuhi.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group ambao ndio waratibu wa tamasha kubwa la burudani hapa nchini la Fiesta 2013,imehudhuriwa na vijana mbalimbali kutoka kila pembe ya mkoa huo wakiwemo na wasanii mbalimbali maarufu kutoka jijini Dar,ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.Aidha katika Semina hiyo ya Fursa,baadhi ya vijana wengi walionekana kuvutiwa kwa kiasi kikubwa kwa yaliyokuwa yakizungumziwa,ikiwemo suala la ujasiliamali.
   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya mapema leo asubuhi,kwenye ukumbi wa Kibo Peak,uliopo Kigoma mjini,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa.Semina hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali,wakiwemo NSSF,Wasanii wa Bongofleva,wakazi  wajasiliamali mbalimbali ndani ya mji wa Kigoma.
   Pichani juu ni baadhi ya Wasanii wa Bongofleva na wadau wengine wakiwemo wakazi wa Kigoma wakisiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo kuhusiana na fursa mbalimbali. 
   Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY.
   Baadhi ya Wasanii wa bongofleva ambao wanatarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,wakitambulishwa kwa wakazi wa Kigoma,wakati wa kuanza kwa semina ya Fursa iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Kibo Peak mjini humo.
   Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa kigoma,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mji huo na wakazi wake.
  Baadhi akina mama walioshiriki semina hiyo wakijadiliana jambo huku wakinukuu baadhi vipengele vilivyowagusa kwa namna moja ama nyingine.
  PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0
 • 08/17/13--07:27: bwawa la maini oye!
 • Liverpool secured their first opening-day victory at Anfield since 2001 as goalkeeper Simon Mignolet marked his debut with a dramatic late penalty save to deny Stoke a point. For Source and more CLICK HERE

  0 0

  Kutoka Maktaba: Ma-DJ wakali kabisa wa enzi hizo wakiwa pamoja katika show Club Africana. Toka kulia ni DJ Meb, Neagre Jay, DJ Choggy Sly (RiP) , DJ John Peter Pantalakis, mratibu wao Nassoro Born City  (RiP), DJ Kalikali (RiP) na DJ Eddy Sally (RiP) pamoja na mdau.


  0 0
 • 08/17/13--07:44: yale yaleeee....
 • AFANDE MWEMA FUNGA KITUO HIKI NI KERO KWETU! Kwa kweli kituo hiki cha polisi pale Ferry jijini Dar ni kero kubwa kwetu wakazi wa Kigamboni tunaovuka na magari. Unaambiwa kila saa mapolisi wake wako bize kuvuta kidogodgo cha kuingiza kibabe kwenye foleni magari ambayo hayakuwa kwenye foleni na kusababisha magari kupigana pasi na kero ya foleni isiyotembea. Kama huamini tega mtego siku moja uone kama hujanasa panya - Mdau Kigambonino...


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa na viongozi wengine wa Serikali wakati wa kumswalia  Marehemu Mzee Ased Ramadhan.  Marehemu alikuwa Mtumishi wa Chama cha ASP na CCM,ambapo alishika nafasi mbali mbali zikiwemo Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya ASP na Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
   Wananchi walioshiriki mazishi ya Marehemu Mzee Ased Ramadhan wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu huyo Aliyefariki jana na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Ased Ramadhan.  Picha na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

  0 0


  0 0


    Msaani mwenye kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael "LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka Gerezani, iitwayo FOOLISH AGE 
  Filamu hii imetengezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited na itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 
  Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu. 
  Kupitia mtandao wa kijamii wa Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH AGE....Hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS"
  Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka yote ya Filamu nchini na Filamu hii imetengenezwa na itakuwa inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited
  Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013

  0 0

  Ankal akila pozi na Rais wa kwamnza wa Zambia Dkt Kenneth Kaunda  mwaka 2005 kabla ya kufanya naye mahojiano katika hoteli ya Sheraton (siku hizi inaitwa Serena Inn) jijini Dar es salaam.

  0 0  Taarifa kamili ya askari bandia wa Trafiki feki James Juma Hussein (45)  aliyekamatwa saa 1:30 asubuhi ya Agosti, 14, 2013 maeneo ya Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, jijini Dar es Salaam ni hii hapa.
    Je, ni kwa nini 'Afande' James alikamatwa? Asubuhi hiyo, afisa mmoja wa trafiki mwenye cheo cha ukaguzi (Inspekta) alikuwa akipita eneo hilo kwenda kazini. Alipomwona James alisimamisha gari. Akashuka kwenda kumsalimia. Lakini alipomkaribia alishangaa kuona vifungo vya shati lake ni vya kawaida (vya polisi vinatakiwa kuandikwa "police force", akamtilia shaka.  

  Baada ya machale kumcheza, afisa huyo alimkamata James Juma Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, Dar na kumfikisha kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari, wilayani Ilala, mkoa wa Dar es salaam, na kumfungulia jalada namba STK/RB/15305/2013 kwa tuhuma za KUJIFANYA ASKARI ili taratibu za kisheria zichukuliwe juu yake.
  Mahojiano ndani ya kituo cha polisi yalikuwa hivi: 
  Afande:Wewe mtu wa wapi?
  James: Mnyamwezi, wa Tabora.
  Afande: Una muda gani ukijifanya trafiki?
   James: Wiki moja sasa.
  Afande: Hii kofia ya polisi uliipata wapi?
  James: Nguo nyeupe juu ya kofia niliitengeneza kienyeji, krauni, tepe za usajenti na mkanda ni vya shemeji yangu. Alikuwa polisi mkoani Tabora, na sasa ni marehemu. Alikuwa akiitwa Shabani. James aliwaambia polisi kuwa suruali nyeupe ya kitrafiki aliishona mtaani lakini kamba ya filimbi na kizibao cha kung’ara vilikuwa vya polisi.
  Askari: Uliwahi kuwa polisi?
  James: Niliwahi kupata mafunzo ya upolisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) mwaka 1990-91 lakini nilifukuzwa kazi kwa sababu nilikwenda muziki. Nilirudi Tabora nikawa mkulima na mke wangu na mtoto mmoja ambao wote sasa ni marehemu.
  Ndani ya nguo za kitrafiki alizokuwa amevaa James, alikutwa na suruali ya bluu na fulana ya kijani. James alisema njaa ndiyo iliyomfanya ajifanye trafiki na ‘kuwapiga mikono’ madereva, hasa wa daladala ili anapowakuta na makosa kwenye magari yao ajipatie chochote.
   Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova amethibitisha kukamatwa kwa polisi huyo feki, ambaye atapandishwa kizimbani wakati wowote kuanzia sasa.

  0 0

  1187141_10151862610225879_247673981_n 
  Mdau Ben Mwanyika na wazazi wake baada ya kuchukua nondozzzz katika Chuo cha USIU Nairobi 

older | 1 | .... | 228 | 229 | (Page 230) | 231 | 232 | .... | 3278 | newer