Mwasisi wa Twist - Chubby Checker akionesha inavyochezwa
ngoma azipendazo ankal
↧
↧
Article 7
Registration is NOW open for CISA and CISM Review Class for the forthcoming CISA exam on 14th December, 2013. Our Reviews are due to begin on Monday 2nd September, 2013 to Thursday 17th October, 2013 (Monday to Friday) for weekday courses, and Saturday 2nd November 2013 – Sunday 8th December 2013 for weekend classes. Both the weekday and the weekend options will be for a total duration of 75 hours.
The review classes focus exclusively on the essential areas covered in the CISA or CISM exam. A series of sample exam questions that provide participants with a "feel" of the format and the types of questions encountered on the exam.
Our trainers are qualified Professionals with technical experience, skills and knowledge of specific domain(s). Participants will gain an overall understanding of the relevant CISA/ CISM Examination DOMAINS.
Study Materials
Our Courses utilize official ISACA presentations and study materials provided by ISACA. We will inform you about recommended materials upon your enrolment.
Fees- 1,000,000 Tshs. per Participant
For more details about the course and online registration visit our website www.isaca.or.tz or contact - info@isaca.or.tz
WARNING:
Any training institution offering review has to be approved by ISACA before it begins to offer review classes.
↧
USAILI WA KUTAFUTA MODELS WATAKAOSHIRIKI KWENYE ALLY REHMTULLAH 2014 COLLECTION FASHION SHOW WAFANYIKA JIJINI DAR.
Meza kuu ya Majaji walioshiriki katika Usaili ya kutafuta Models watakaoshiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion show kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja, Ally Hassan, Mrembo na mwigizaji maarufu nchini Wema Sepetu, Mwandaaji wa Onyesho hilo ambaye pia ni Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah, Mwanamitindo Jamillah Nyangasa, Sarah Raqey.
Mbunifu wa mitindo maarufu hapa nchini Ally Rehmtullah amefanya maandalizi ya awali ya fashion show yake itayofanyika Agosti 30, mwaka huu katika Hoteli ya Serena ambapo zaidi ya wanamitindo 30 wasichana na wavulana watashiriki katika maonyesho hayo kabambe.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwenye mahojiano maalum Rehmtullah amesema kwenye onyesho la mwaka huu wasichana watashiriki 20 na wavulana 10 ambao watavaa mavazi mbalimbali yaliotengezwa na kubuniwa na Rehmtullah mwenyewe kwa kuzingatia mila na desturi za Kiafrika.
Katika mchujo huo majaji watano watashiriki kuchagua warembo wenye mvuto, kujiamini na wenye kuwa na muonekano mzuri kwenye jukwaa ili kuwavutia wageni waalikwa ambao watakuwa ni wabunge, mawaziri na viongozi mbalimbali.
Rehmtullah alilisitiza mwaka huu kwamba onyesho la mitindo ya mavazi yatafana baada ya kudhamini wa makampuni kadhaa makubwa hapa nchini.
Pichani juu na chini ni Models wa kike wakipita mbele ya majaji wakati wa Audition ya kutafuta washiriki watakaonyesha mavazi kwenye Onyesho la Mavazi la Ally Rehmtullah 2014 Collection.
Pichani juu na chini ni Models wa kiume wakipita mbele ya majaji kwa ajili ya kuchaguliwa kushiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion Show.
↧
NMB emerge the best Bank in Tanzania
↧
TIMU YA POLISI YAFIKA SALAMA KATIKA JIJI LA WINDHOEK NCHINI NAMIBIA
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Hatimaye timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia imefika salama na imeanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza jumatatu tarehe 19 mwezi Agosti mwaka huu.
Timu hiyo ambayo ni tishio katika michezo hiyo kutokana na historia yake ya ushindi katika mashindano yaliyotangulia imekuwa kivutio kila inapopita huku kila mmoja akitaka kusalimiana nayo.
Timu hiyo inaundwa na wanamichezo 67 ambao wanacheza Mpira wa miguu wanaume, Mpira wa pete Wanawake, Riadha wanaumwe na wanawake na mchezo wa Vishale (Dats).
Michezo hiyo itashirikisha Nchi kumi na nne (14) katika michezo mbalimbali na lengo la michezo hiyo ni kujenga ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SARPCCO katika kukabiliana na uhalifu.
timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia,wakipiga jalamba wakati wa kujiandaa na mashindano hayo.
Timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo nchini Namibia ikiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya Wenyeji wao.
↧
↧
TANAPA YAFUNGA RASMI AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UJANGILI KWA UHARAKA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akikagua gwaride la Kikundi cha Kukabiliana na Uhalifu kwa Haraka (Rapid Response Team) kilichohitimu mafunzo yao katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mwishoni mwa wiki.
Wahitimu wa RRT wakiapa Kiapo cha Utii mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.
Wahifadhi wakifuatilia kwa makini zoezi la uhitimishwaji wa mafunzo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk. Christopher Timbuka, John Shemnkunde, Mtango Mtahiko na Godwell Meing’ataki.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Martin Loibooki akisoma maelezo kuhusu mafunzo hayo kwa mgeni rasmi.
↧
WARSHA YA WIKI MOJA KWA REDIO ZA JAMII NCHINI KATIKA KUTEKEKELEZA MRADI WA DEMOKRASIA NA AMANI WA UNESCO UNAOFADHILIWA NA UNDP YAMALIZIKA WILAYANI SENGEREMA
Meneja wa mradi wa Amani na Demokrasi (DEP ) kutoka UNESCO Courtney Ivins akizungumza na Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii kupata tathmini ya warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Washiriki wakijadiliana katika makundi mambo mbalimbali ya kuboresha kwenye redio jamii zao katika utekelezaji wa mradi wa DEP kuelekea uchaguzi 2015 wakati wa kuhitimisha warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma.
Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji mara baada ya kumalizika kwa warsha ya wiki moja kwa ajili ya kuwaanda redio za jamii kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasi kuelekea uchaguzi 2015 iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.
↧
POMBE HARAMU AINA YA GONGO YAKAMATWA NDANI YA BASI HUKO MASASI MKOANI MTWARA IKISAFIRISHWA
Na Elvan Limwagu wa Globu ya Jamii,Masasi
Basi dogo la kubeba abiria liitwalo BUTI LA ZUNGU lenye Namba za Usajili T510CFM aina ya Toyota Costa jana (18/8/2013) lilikamatwa na Polisi maeneo ya Njenga Ndanda na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Ndanda baada ya kupekuliwa na kukutwa na Madumu 5 ya Pombe haramu aina ya Gongo yakiwa yamefichwa chini ya siti.
Madumu hayo ambayo yalifungwa vizuri ndani ya mabox na juu yake kufunikwa kwa mifuko myeusi ya nylon pasipo kutoa harufu kabisa.
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Lindi – Masasi lilikamatwa majira ya saa 9 alasiri likisafiri kutoka Masasi kwenda Lindi. Baada ya upekuzi mmiliki wa mzigo huo hakujitokeza na Makondakta walishindwa kumtaja mwenye mzigo huo na hivyo Kondakta mmoja aitwaye ALLY alishikiliwa katika kituo hicho kwa kuisaidia Polisi. Basi hilo ambalo lilibeba abiria nikiwemo “mimi” liliruhusiwa kuendelea na safari saa 9:55 alasiri.
Askari Polisi wa Kituo cha Ndanda wakiendelea na ukaguzi kwenye basi hilo.
Mara madumu kadhaa yakaonekana na kuanza kushushwa.
Hili ndio basi lenyewe lililokuwa limebeba kilaji hicho haramu.
Hivi ndivyo kilivyokuwa kimehifadhiwa kilaji hicho,tena kwa ustaji mkubwa ili kisibainike.
Wadau wakidiskasi jambo.
↧
VODACOM YAOMBA RADHI WATEJA WAKE KUTOKANA NA HITILAFU ILIYOKEA HIVI KARIBUNI
↧
↧
NBC yazindua Huduma ya Mawasiliano ya papo kwa papo ya wateja (Hotline Service)
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya mawasiliano ya papo kwa papo (Hotline Service) kati ya mteja wa benki hiyo na maofisa wa benki nhuduma itakayopatikana ndani ya matawi ya NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha benki hiyo, Jane Dogani (kushoto), wakifurahia wakati mmoja wa wateja wao, Amin Juma (katikati) akijibiwa swali alilouliza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina akiongoza shughuli za uzinduzi wa huduma ya Hotline Service ya Benki ya NBC katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo pia kwa sasa inaweza kupatikana katikan matawi mengine.
↧
hepi besdei ya kuzaliwa mdau Fortunata
Keki ya Fortunata ambayo ilikuwa maalumu kwenye siku yake ya kuzaliwa ambayo alikula pamoja na wafanyakazi wenzake wa LAPF ,Dodoma.
Fortunata akimlisha keki rafiki yake Scola
Wakati wa kugonga glasi kama ishara ya kumpongeza Fortunata kwa kuongeza umri zaidi katika sherehe ndogo iliyofanyika kwennye Pub maarufu ya Ngonyani , Dodoma.
Fortunata akimimina champaigne kwa wafanyakazi wenzake wa LAPF waliojumuika nae siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyika hivi karibuni,Dodoma.
↧
MSIBA WA NEMELA PHILLIP MANGULA NYUMBANI KWAO OYSTERBAY, DAR ES SALAAM, LEO
↧
news alert: mtoto wa kike aokotwa upanga jijini dar es salaam leo, amehifadhiwa kituo kidogo cha polisi cha salender
Mtoto wa kike mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 3 ama 4 anayesema anaitwa Manka ameok otwa leo na wasamaria wema maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kupelekwaa katika kituo kidogo cha polisi cha Salender ambako hadi tunaenda mitamboni alikuwa amehifadhiwa hapo. Juhudi za kuwatafuta wazazi wake ama wanafamilia zinaendelea na wito umetolewa kwa yeyote anayemfahamu mtoto huyu ama wazazi wake aende kituoni hapo.
↧
↧
Mkurugenzi wa Mipango wa Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sera za Uhamiaji atembelea Balozi Dr. Kamala ofisini kwake Brussels
Mkurugenzi wa Mipango wa Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Sera za Uhamiaji Bi. Chantal Lacroix akimweleza Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa ushirikishaji wa sekta binafsi katika masuala ya Uhamiaji utakaofanyika Arusha tarehe 18 na 19, Septemba 2013. Mazungumzo yamefanyika katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya, Brussels leo.
↧
New England Umoja Organization (NEU) event cancelled
On behalf of the New England Umoja Organization (NEU) and its leadership, we regret to inform you that, our annual event which was planned for 8/24/13 has been cancelled due to circumstances which are beyond our control.
We sincerely regret the inconvenience this will cause. While the organization may not be able to compensate the leadership is asking for your understanding and patience as we works to improve the organization and its functions in the community.
We would like to thank all of you for continued support.
New England Umoja
Organization (NEU)
↧
Madaktari bingwa kutoka China wajitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,madaktari hawa wataungana na Madaaktari wazalendo katika kutoa huduma katika Hospitali za Serikali Unguja na Pemba.
Baadhi ya Madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza na madaktari hao leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Jimbo la Jiangsu Nchini China waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kusalimiana na Rais,madaktari hawa wataungana na Madaaktari wazalendo katika kutoa huduma katika Hospitali za Serikali Unguja na Pemba.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
↧
sheikh ponda apandishwa mahakamani mjini morogoro leo, asomewa mashitaka matatu
Sheikh Ponda Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi tarehe 28.08.2013
Ulinzi Ukiwa umeimarishwa mahakamani leo
Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu ambapo inadaiwa alisema kwamba ”Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ”katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro. Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilika na Dhamana Imefungwa na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro..
Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG
↧
↧
WANADMV MAZOEZI YANAENDELEA LEO JUMATATU AUG 19, 2013 MEADOWBROOK PARK
WanaDMV yanaendelea leo Jumatatu Aug 19, 2013 kuanzia saa 11 jioni mazoezi yatafanyika Meadowbrook Park kwa ajili ya kucheza kwenye Labor Day Tounament itakayofanyika Aug 31, 2013 kama maelezo yanavyojieleza hapo chini na Jumapili Aug 25, 2013 tutacheza mechi ya kirafiki na Vitambi FC katika viwanja vya Layhill
Tafadhali tuzingatie muda na upatapo taarifa hii mtaarifu na mwenzio asante
VITAMBI FCand the greater DMV Kenyan community invites you to the Annual Labor Day Soccer Tournament. This is a family event to be held on Saturday August 31statLayhill Park, 14901 Layhill Road, Silver Spring. MD 20906.The games begin at 11.00AM EST and promise to be action packed. This year’s event brings together local and non-local teams representing an array of African countries. Some of the featured teams are:
· VITAMBI FC
· WATEMBEZI FC (BALTIMORE)
· DC FLAMES (MALAWI)
· NEW JERSEY STARS
T TANZANIA STARS DMV
Teams are required to be at the tournament site by 10:00AM ESTThis event provides a fun opportunity for families to enjoy soccer, Bouncing castle, and field games for both children and adults. Food and refreshment will be available, especially the world famous Nyama Choma!
Local vendors are invited and encouraged to contact us for advertisement opportunities for their goods & services. This is a great opportunity to network while connecting with the community. Contact Erico at vitambifc@gmail.com with the subject “FAMILY COOKOUT” we will get back to you within 24 hours.
Thank you and we look forward to seeing you there!
↧
HAJA YA HOJA: OGOPA MAPENZI YA KICHAWI:
Naitwa Mama Jessica, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, mkaazi wa Tabata, Dar Es salaam.. Baada ya kuumizwa sana na wanaume katika mapenzi, niliamua kutafuta mganga wa kienyeji, shoga yangu alinipeleka kwa Mganga mmoja anayeitwa MUNGU WAKABILI, ambaye ni Mtaalamu aliyebobea sana katika masuala ya ULIMWENGU USIO ONEKANA.
Wakati naenda kumuona huyu mganga, tayari nilikuwa nimeanza uhusiano na mwanaume mmoja lakini na yeye akawa haeleweki heleweki. MUNGU WAKABILI, alinipa dawa ya mapenzi ambayo imenifanya nijutie kuitumia , kwani baada ya kumfanyia dawa mwanaume huyo, AMENIPENDA KUPITA KIASI! YANI AMEKUWA KAMA ZEZETA KABISA!
Alikuwa na mke wa ndoa na watoto watatu, ila amewatelekeza wote na kuja kuishi na mimi. Nyumba aliyo jenga na mke wake ameiuza na kuninunulia mimi nyumba nyingine ili tuishi pamoja, kama hiyo haitoshi alikuwa na magari mawili moja amempa mdogo wangu wa kiume, jingine ameliuza na kunifungulia duka la nguo Kinondoni. Ni mambo mengi sana, yote siwezi kuelezea, ila kibaya zaidi ni kwamba, sasa ameshindwa kuendelea na biashara zake,anataka kuwa na mimi wakati wote kwa sababu amekuwa na wivu sana, anahisi akiniacha hata kwa dakika mbili tu nitaibiwa na mwanaume mwingine. Kibaya kuliko vyote sasa ndugu wa mume, mke wake na ndugu wa mke wake, wameanza kunitishia maisha yangu .
Nilijaribu kwenda kumuomba huyu MUNGU WA KABILI anipe dawa ya kumrudisha huyu mwanaume katika hali yake ya kawaida lakini amegoma kufanya hivyo, anasema yeye hawezi kuharibu dawa aliyo kwisha itengeneza tayari na kwamba alinionya mapema.. Hapa nipo njia panda na sijui hatma ya jambo hili, natamani nikimbie mji lakini nashindwa.
Nimeamua kuandika waraka huu ili kwanza, kuwaonya wanawake wenzangu waachane na MAPENZI YA KICHAWI ili yasije kuwakuta kama yaliyo nikuta mimi, kwani naona wanawake wengi sana, wa Dar Es salaam, wanamkibilia mtu huyu kwa ajili ya kupata dawa za mapenzi..
Nakuonya usifanye hivyo mwanamke mwenzangu, kwani mtu huyu licha ya kuwa na umri mdogo tu tena wa miaka chini ya thelathini, lakini dawa zake ni za hatari sana na zina nguvu za ajabu sana! Usijaribu kabisa mwanamke mwenzangu, utaumbuka,kwani kila mtu atajua umetumia uchawi!
Lakini, pili, ninawaomba wanawake wenzangu mnisaidie kumshawishi MUNGU WA KABILI ili amrejeshe huyu mwanaume katika hali yake ya kawaida..
↧
MAMA SALMA KIKWETE APOKEA TUZO MAALUM TOKA TAASISI YA BEN TV DIPLOMATIC AWARDS 2012
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ofisini kwake tarehe 19.8.2013. Tuzo hiyo ilitolewa kwa Mama Salma baada ya kuibuka mshindi miongoni mwa mataifa ya bara la Afrika, Caribean, Asia na Pacific kutokana na kazi za kuendeleza rasilimai watu hapa Tanzania.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo kutoka kwa Taasisi ya Bright Entertainment Network ya Uingereza iliyokabidhiwa kwake na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara tarehe 19.8.2013.
Mwnyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya Waziri Mukangara kumkabidhi Tuzo hiyo.
Mke wa Rais na Mshindi wa Tuzo ya BEN TV DIPLOMATIC AWARDS-2012 Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na baadhi ya wajumbe wa bodi ya WAMA, Mheshimiwa Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti (kulia) na Mama Hulda Kibacha, Mjumbe wa bodi (kushoto).mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo ofisini kwake tarehe 19.8.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt.Fenella Mukangara wakati akitoa maelezo mafupi kuhusiana na tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012 aliyopewa dhamana na Taasisi ya Bright Entertainment Network (BEN) ya Uingereza ya kumkabidhi Mama Salma Kikwete Tuzo hiyo katika jitihada zake za kuendeleza rasilimali watu katika Taifa kwa mwaka 2012.PICHA NA JOHN LUKUWI
↧
More Pages to Explore .....