Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAJASIRIAMALI WA ILALA WAOMBA KUKOPESHWA VITENDEA KAZI NA DCB

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa(kulia) katika banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya siku mbili ya wajasiriamali wa Wilaya ya Ilala yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAJASIRIAMALI  wanawake na Vijana wa Wlaya ya Ilala wameutaka uongozi wa Benki ya DCB kuwapatia mikopo ya vitendea kazi na vifaa kazi ili waweze kujiwekeza vizuri zaidi katika kuendesha viwanda vyao .
Benki ya DCB wamekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa mikopo kwa vikundi mbalimbali vinavyojishugulisha na utengenezaji wa bidhaa za vyakula, nguo, viatu na hata dawa za kusafishia ndani na vyooni. Hayo wameyasema leo wakati wa maonyesho ya siku mbili ya  bidhaa za wajasiramali yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa amesema kuwa toka walivyoingia katika makubaliano ya kutoa mikopo na Manispaa ya Wilaya ya Ilala mwaka 2014 kwa wanawake na vijana  tayari wameshaweza kutoa mikopo ya takribani  bilioni 9.2 imetolewa kwa vikundi 2978.
 Ndalahwa amesema kuwa, changamoto iliyokuwepo kwa sasa ni uhitaji wa fedha kwani wanawake na vijana wanaohitaji mikopo hiyo ni wengi katika manispaa na kuiomba Halmashauri kuongeza feda za mfuko huo ili kuwezesha benki kuwahudumia wajasiriamali wengi zaidi.
“Tumelisikia ombi la wajasiriamali la kutaka kuboreshwa kwa mikopo ikiwemo kuongezwa kwa kiasi cha fedha pamoja na kukopesha vitendea kazi na vifaa kazi, sisi kama DCB benki mteja wetu atakapohitaji vifaa atakuja kwetu na tutakaa chini na kuingia makubaliano,”amesema Ndalahwa.
“kuelekea uchumi wa viwanda wanwake na vijana tuzingati ubunifu na kutumia fursa za kiuchumi kupata mitaji na kujiendeleza  na benki itandelea kutoa fursa za mitaji kwa wajasiriamali wa aina hii,”
Akizungumza  baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali hao na kujionea namna wanavyofanya kazi  zao na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli za watanzania kuwekeza zaidi katika shughuli za uzalishaji mali.
Mjema amesema kuwa wajasiriamali hao wameonesha kuwa mikpo waloyokuwa wanaipata imekuwa na msaada mkubwa sana kwao na wameweza kujiendeleza katika kukuza mitaji ya biashara zao na hata wengine waliweza kuanzisha biashara zinine na kujipatia faida.
“Wajasiriamali hawa wameonekana kufikia malengo yaliyowekwa na Rais JPM kwa kuanzisha viwanda, tumeona jinsi gani wameweza kutumia nafasi wakizozipata hususani katika mikopo waliyoipata na kujiendeleza zaidi,”amesema Mjema.
Maonesho hayo yanaendelea kwa  siku  mbili ndani ya viwanja vya mnazi mmoja na dc mjema amewaomba wakina mama na vijana kujitokeza kuja kuona namna wenzao wanavyojishugulisha na ujasiriamali.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akisalimiana na moja ya waanzilishi wa vikundi vya ujasiriamali Vicky Shayo wakati akitembelea mabanda wakati wa maonyesho ya wajasiriamali yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


Mjasiriamali Vicky Shayo akizungumza na waandishi wa habari namna walivyoweza kuanzisha kikundi chao na benki ya DCB kuweza kuwapatia mkopo ulioweza kuongeza tija katika miradi yao katika maonyesho ya wajasiriamali yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Maelfu ya Wateja wa Tigo waendelea kujishindia Simu Janja katika Promosheni ya Nyaka Nyaka

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Gladys Mtandila kutoka Makumbusho, Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promoshen hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00#.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Ramadhan Ali Ngolozi kutoka Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# .
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Sakina Kassanga, askari polisi kutoka Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00#
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo ilitoa simu janja 1,080 kwa wateja wake, pamoja na bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wote walionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# .

DONGOBESH FC YAICHAPA STAND FC YA HAYDOM GOLI 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KURUGENZI CUP 2018

$
0
0
 Mchezaji wa timu ya Dongobesh FC Antipas Vicent akiwa amebebwa juu juu na mchezaji mwenzake mara baada ya kumalizika kwa mchezo katika yake na timu ya Stand FC ya Mjini Haydom ambapo mchezaji huyo ndiye aliyeifungia timu yake goli 1-0 na timu ya Dongobeshi kufanikiwa kuingia nusu fainali katika michuano ya Kurugenzi Cup 2018 linaloandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.ikidhaminiwa na Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha Iringa.
 Wachezaji wa timu ya Dongobash FC wakisikiliza maelezo ya Mmoja wa Waratibu wa michuano hiyo Bw. Phars Nyanda wakati akiwapa utaratibu mara baada ya mchezo huo kumalizika.
 Benchi la Ufundi la Timu ya Dongobesh FC likinyanyuka juu na kushangilia mara baada ya kuifunga timu ya Stand FC ya mjini Haydom katika mchezo uliofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.
 Golikipa wa timu ya Stand FC ya mjini Haydom akisaidiwa na wenzake mara baada ya kuumia wakati wakiwania mpira uliokuwa unaingia golini mwake katika mchezo huo.
 Hekaheka golini mwa timu ya Stand FC ya mjini Haydom wakati wachezaji wa timu ya Dongobesh FC wakiliandama goli la wapinzani wao.

Introducing "TORNADO" by Papa Dennic Ft. Ray C

$
0
0
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya DENNIS MWANGI aka PAPA DENNIS aliyepo chini ya record label ya MALIZA UMASIKINI katoa wimbo wake mpya alioufanya na mwanadada REHEMA CHALAMILA maarufu kama Ray C unaokwenda kwa jina la TORNADO ukimaanisha kimbunga cha mahaba Wimbo huu unazungumzia mapenzi ambayo anaependwa kazidiwa na mahaba hadi anahisi mapenzi yake ya nguvu kama kimbunga Video ya wimbo huu imetengenezwa nchini Afrika ya kusini na muongazji wa video maarufu sana anae kwenda kwa jina God Father Mbali wimbo huu PAPA DENNIS Amesha fanya nyimbo na vinara wengi wa muziki wa Africa akiwemo Mr Flavour (Nigeria) ,Chiddimna (Nigeria) ,Korode bello (Nigeria) na sasa RAY – C (Tanzania) 
The song is now available in all platforms and the video is also on youtube
Youtube : https://www.youtube.com/channel/UCKPJmRtO6d0pc_Gf0DTDWsQ
Youtube : Maliza Umasikini
Instagram: @realpapadennis

HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA MKOANI MBEYA NI ASILIMIA 91.5

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa MSD Kanda ya Mbeya wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kuandaa mzigo wa dawa kwa ajili ya kwenda kuzisambaza kwenye vituo vya afya mkoani Mbeya.


Na Dotto Mwaibale, Mbeya

UPATIKANAJI wa dawa na vifaa tiba na vitendanishi vya maabara mkoani Mbeya umefikia asilimia 91.5 kwa mwezi huu wa Mei, kutokana na ongezeko la bajeti ya dawa kwa mwaka fedha 2017/2018. Imeelezwa katika mwaka huo wa fedha bajeti imeongezeka kwa asilimia 20.6 kwa hospitali za wilaya na asilimia 51 kwa zahanati na vituo vya afya.


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt.Yahya Msuya ameeleza hayo wakati maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) walipotembelea wateja wa vituo vya Afya vitatu, vya Wilaya ya Mbeya vijijini wakati wa kusambaza dawa za mgawo wa mwisho wa mwaka wa fedha wa 2017/2018. 


Dkt. Msuya alisema ongezeko la asilimia 91.5 la upatikanaji wa dawa umeimarisha huduma za afya na na kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu kukosekana kwa dawa.
Ofisa Mauzo wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mbeya, Rhoda Joseph (kushoto) na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ilembo, Sk.Bwire Biseko (kulia), wakihesabu dawa wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kituo hapa jana wilaya ya Mbeya Vijijini. Katikati ni mwanakamati ya Afya wa Kijiji cha Ilembo.

"Hospitali ya Rufaa ya Mbeya inahudumia wagonjwa wapatao 400 kwa siku; upatikaji wa dawa kwa sasa ni wa uhakika na uwepo wa maduka ya MSD ni chachu ya kuimarika kwa huduma," alisema.


Alisisitiza kuwa utekelezaji wa agizo la serikali, la kutoa dawa za malaria bure kwa wananchi pamoja na dawa za msaada katika vituo vya afya na hospitaliti linafanyika.

Mfamasia wa Wilaya ya Mbeya, Apolinary Mwakabana alisema pamoja na upatikanaji wa dawa kuridhisha kwa asilimia 91.5, jitihada zinahitaji ili kuwa na dawa zote, kwani asilimia 9 ya dawa zinazokosekana hulazimika kuzitafuta nje ya bohari.

Ofisa Mauzo wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mbeya, Rhoda Joseph, akimkabidhi dawa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kijiji cha Ilembo wakati wa zoezi la kukabidhiwa dawa hizo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ilembo, Sk.Bwire Biseko.

Alisifu ushirikiano wa kikanda uliopo kati ya halmashauri na MSD katika huduma hususani kukiwa na mahitaji ya dharula.


Naye Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Ilembo kilichopo Mbeya vijijini Sk.Bwire Biseko, alisema kwa siku kituo hicho kinahudumia wagonjwa 107 kutoka vijiji 10, vyenye wakazi zaidi ya wakazi 17,000.

Alisema uboreshaji wa huduma za afya katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarisha uchumi na huduma za afya kwa kuwa watu wengi hawamudu gharama za matibabu kutoka nje ya hospitali.

Ubia Enock ni kati ya wakazi ambao walijitokeza katika kamati ya afya ya Kijiji cha Ilembo kushuhudia makabidhiano ya dawa hizo ambapo alisisitiza haja ya serikali kuboresha huduma kwa watu wanaotumia bima za afya.

Baadhi ya wafanyakazi wa MSD Kanda ya Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuandaa mzigo wa dawa kwa ajili ya kwenda kuzisambaza kwenye vituo vya afya mkoani humo.

JAFO ATOA SIKU TANO KWA HALMASHAURI 10 KUJIELEZA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akifungua kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote
nchini.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhandisi Mussa Iyombe akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo kufungua kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala za Mikoa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akivishwa beji ya heshima kutokana na utendaji kazi wake.
 Wajumbe wa kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dk.Zainab Chaula akizungumza katika kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.

Zulfa Mfinanga na Magdalena Stanley

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jafo ametoa siku tano kwa wakurugenzi na waganga wakuu wa halmashauri 10 nchini kutoa maelezo ya kina kwa nini halmashari hizo hazijafika asilimia kumi ya matumizi ya fedha za miradi ya afya.

Jafo ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotekelezwa chini ya Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichowajumuisha Makatibu Tawala kutoka mikoa yote nchini.

Amesema halmashauri hizo zimeshindwa kutumia fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya afya kama inavyotakiwa ambapo matumizi yake yanaonekana kuwa chini ya kiwango, huku akizitaja halmashauri hizo kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mpimbwe, Mbulu Dc, Songwe, Simanjiro, Mkinga, Mkuranga, Namtumbo, Nzega Dc pamoja na Kilindi.

“Halmasharu hizi zina kila dalili ya kupata hati chafu, naagiza hadi kufika siku ya Jumatano niwe nimepata majibu ya kuridhisha ni kwanini hawajatumia fedha walizopewa kama maelezo yanavyotaka, tukiacha kufanya kazi kwa mazoea tutapata matokeo mazuri, lakini kwa hali hii tusitegemee matokeo mazuri kwa baadhi ya maeneo” Alisema Jafo

Kwa upande mwingine Waziri Jafo aliwaagiza Makatibu Tawala hao kuwaelekeza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwekeana malengo na watumishi wao kwa kuwafanya tathmini ya uwajibikaji kila mwaka ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kazini kwani bado wapo baadhi ya watumishi wanafanya kazi kwa mazoea.

Amesema kuwa iwapo mtumishi wataonekana amefanya kazi chini ya kiwango cha alama 50 kama ni mkuu wa idara atawajibishwa kwa kushushwa cheo, na yule ambaye ataonekana kufanya vizuri zaidi alishauri anastahili kupewa zawadi ya mfanyakazi bora wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani-Mei Mosi.

Aidha Waziri Jafo amesema kwa sasa kipaumbele cha utoaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo zitatolewa kwa kuzingatia kipimo cha matokeo mazuri kwa halmashauri husika, kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza uwajibikaji.

Wakati huo huo Waziri huyo aliagiza halmashauri zote nchini kuweka mfumo wa matumizi ya mfuko wa afya ya jamii wa CHF iliyoboreshwa sambamba ya kuhimiza matumizi ya ukusanyaji wa mapato wa njia ya kimtandao ili kuepuka upotevu wa fedha za serikali.

Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo Mratibu wa mfuko wa afya ya jamii TAMISEMI, Nkinda Shekalaghe amesema kuwa hadi sasa mfuko huo haujafikia lengo lililowekwa na serikali la kuunganisha wananchi kwa asilimia 30 hadi kufikia mwaka 2015, kwani kwa mwaka 2016/2017 wamefikia asilimia 24.

Alitaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na utayari wa wananchi kujiunga na mfuko, huduma duni za afya, kutokuwepo kwa mfumo rasmi wa utoaji wa taarifa pamoja na kiwango kidogo cha uchangiaji ambapo amesema tayai wameshachukua hatua mbalimba katika kukabiliana na changamoto hizo.

MICHUZI TV: MAMA JANETH MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUONDOKANA NA DHANA POTOFU

SARE YA YANGA SC DHIDI YA RAYON SPORTS, KOMBE LA SHIRIKISHO HATUA YA MAKUNDI.


CRDB BANK WALIVYOSHIRIKI NA KUTOA HUDUMA KWENYE MAONESHO YA WAJASIRIAMALI WA ILALA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo (kulia), akimpatia maelezo mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja na ya wajasiriamali kabla ya kuyafungua. 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), akimwuliza jambo Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo (kulia), akiwa kwenye banda la benki hiyo, wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja na ya wajasiriamali kabla ya kuyafungua maonesho hayo. 
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akiwa meza kuu pamoja na baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Ilala kabla ya kuyafungua maonesho hayo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Diwani wa Gongolamboto, Jakob Kisi, akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa CRDB Bank, Meneja Biashara, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. CRDB Bank, ni moja ya waliodhamini na kufanikisha maonesho hayo ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala.

VIONGOZI WASTAAFU WAJADILI AMANI NA USALAMA BARANI AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

KAMATI YA KUDUMU BUNGE YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI YATEMBELEA MRADI WA KURASIMISHA MAKAZI KIMARA KILUNGURE

$
0
0
 Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akizungumza na Wananchi wa kata ya Kilungule mara alipofanya ziara na Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili kujionea namna mradi wa urasimishaji makazi ulivyofanyika katika eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye akizungumza na Wakazi wa Kilungule wakati walipofanya ziara kukagua mradi wa urasimishaji Ardhi unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule A,Emanuel Komba akizungumza jinsi mradi huo ulivyokuwa rafiki kwa wakazi wa eneo hilo .
 Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye katika eneo Kilungule A mahali ambapo watu wa eneo hilo wamerasimishwa makazi yao.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye akiwa na baadhi ya Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu na Ardhi na Maliasili
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili , Nape Nnauye akiwa na Waziri wa Ardhi William Lukuvi  pamoja na Wajumbe wa kamati hiyo

DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga January Lugangika amewataka madiwani wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki katika kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuiepusha kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.

Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la Kwehangara.

Alisema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika. “Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya maendeleo hili ndio jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake gharama inayotumika inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.

Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi inayotekelezwa hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na wakandarasi”Alisema.Nay kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia kuwatatulia mambo mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
 MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Bumbuli ambacho kwa mara ya kwanza kilifanyika eneo la makao makuu ya Kwehangara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali akizungumza katika kikao cha robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo Jipya la Makao Makuu ya Halamshauri hiyo Kwehangala kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amiri Sheiza
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza akizungumza katika kikao hicho kwa kuwataka wananchi kuwa wamoja kuhakikisha halmashauri hiyo inbapata mafanikio kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali
 Mkurugenzi wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Halma shauri ya Bumbuli Amiri Sheiza wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho.

NIC YATOA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI KISARAWE KWA AJILI YA MIRADI YA AFYA NA ELIMU

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania(NIC) Sam Kamanga akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe,Hamis Dikupatile baada ya mbunge wa viti maalum mkoani Pwani ,Zainab Vullu kupokea msaada huo kutoka kwa Mkurugenzi huyo.

Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe

SHIRIKA la Bima la Taifa la Tanzania (NIC) ,limetoa msaada wa mifuko ya saruji 160 ,yenye thamani ya zaidi ya sh.mil.mbili ,wilayani Kisarawe Mkoani Pwani. Msaada huo umelenga kusaidia kumalizia miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya umma ikiwemo zahanati ,vituo vya afya na mashule katika kata zilizopo wilayani humo .

Akikabidhi msaada huo kwa mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani Zainab Vullu ,mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania, Sam Kamanga ,alisema shirika hilo linatoa misaada ya aina hiyo kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye changamoto za kijamii. Alieleza msaada huo ni moja ya kati ya shughuli za shirika za kurudisha kwa jamii.

"Katika mpango kazi wetu tumejiwekea kuwa na wananchi katika changamoto zao,Hii ni miongozo ya utawala bora kwa kuwa karibu na jamii ,tunatekeleza, tumeenza mkoani Iringa  ,Mwanza ,Sumbawanga katika sekta ya afya na elimu " alieleza Kamanga.
Mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani ,Zainab Vullu akiongea na baadhi ya madiwani na watendaji halmashauri ya Kisarawe.

Akipokea msaada huo ,mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab alishukuru shirika hilo na kusema aliongea nao juu ya ombi hilo na anashukuru amesaidia. Alisema mifuko hiyo ya saruji inaelekezwa katika kata zinazoendelea na ujenzi wa miradi ya elimu na afya.

Zainab alitaja kata hizo kuwa ni pamoja na Msimbu mifuko 20, Mafizi mifuko 30, Vihingo mifuko 30 ,Chole mifuko 10,Marumbo 10,Kazimzumbwi 10, Kiluvya 10 ,Vikumburu 10 ,Msanga 10 na kata ya Masaki mifuko kumi .

"Ndondo si chululu ,hiki tulichokipata kwangu ni kikubwa ,nawashukuru NIC kwani itakwenda kuboresha ujenzi wa mashule ,vituo vya afya na zahanati" alieleza Zainab. Mbunge huyo viti maalum Mkoani hapo ,alisema kuwa ,adhama ya serikali ni kuinua uchumi wa Viwanda na Viwanda bila waajiriwa wenye afya njema sio jambo jema .
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania,(NIC) Sam Kamanga, akizungumza jambo wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

Zainab alisema madarasa yakikamilika pia huku wanafunzi wakiwa na afya njema,kwa hakika inapendeza ,alisisitiza". Aliwataka madiwani kutumia saruji hiyo kwa matumizi lengwa badala ya kuiacha bila kutumia kwa wakati na matokeo yake ije kuharibika. Zainab aliliomba shirika hilo kuendelea kuwasaidia hasa kwenye upande wa vikundi vya wanawake na vijana ili viweze kujiinua kiuchumi .

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe ,Hamis Dikupatile alisema kwasasa wilaya ipo katika mkakati wa kuondoa 0 mashuleni hivyo aliwaomba wadau na shirika hilo kuangalia namna ya kuwezesha sekta ya elimu ili kuondokana na kushuka kitaaluma .

Dikupatile alimshukuru mbunge Vullu na NIC kwa jitihada zao na kuwaomba wasichoke kuitupia macho wilaya hiyo. Alisema wilaya ya Kisarawe inaendelea kupigania maendeleo na kuinuka kiuchumi kwa maslahi ya jamii na kuondokana na umaskini .

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ARDHI NA MALIASILI WATEMBELEA MRADI WA ILMIS NA MAJENGO YA NHC VICTORIA NA MOROCO

$
0
0
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akionyesha Faili lenye viambatanisho vya hati moja katika chumba cha  kubadilisha hati za kawaida kwenda Dijitali kinachosimamiwa na mradi wa ILMIS, ambapo kwa sasa mtu ataweza kupata hati yake kupita mtandao na akihitaji karatasi atapata moja amabyo itakuwa na viambatanisho vyote.
 Msajili wa  Hati kutoka Wizara ya Ardhi, Joanitha Kazinja akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye wakati walipotembelea chumba cha kubadilishia Nyaraka cha Mradi wa ILMIS.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili, Nape Nnauye  Akizungumza wakati wa kikao cha Majumuisho ya ziara ya kutmebelea Miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mradi wa ILMIS Unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi.
 Mtaalamu wa Maluala ya bacode Katika mradi  wa ILMIS Cristina Selaru akitoa maelezo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili jinsi mfumo huo utakavyokuw aunafanya kazi kumsaidia mtu kujua taharifa zake zote.

WATENDAJI WAKUU NA WAJUMBE WA BODI WAPIGWA MSASA NA OFISI YA MSAJILI HAZINA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shabani akizungumza na watendaji wakuu na wajumbe wa bodi katika mafunzo ya siku moja kuhusu uwajibikaji na utendaji katika taasisi na mashirika ya Umma yaliyoendeshwa na ofisi ya Msajili wa Hazina.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WATENDAJI wakuu na wajumbe wa bodi za taasisi na mashirika ya umma wamepatiwa mafunzo ya siku moja kuhusu uwajibikaji na utendaji katika taasisi na mashirika wanayofanyia kazi yaliyoendeshwa Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini.

Mgeni rasmi wa mafunzo hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban amesema kuwa Katika kutekeleza lengo hili, walivunja SCOPO mwaka 1992 na kuhamishia majukumu yake mengi Ofisi ya Msajili wa Hazina na wakatunga Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1992 na marekebisho yake ya mwaka 1993 na 2010 ili kuboresha usimamizi na kuleta tija katika Taasisi na mashirika yake.

Amina ammesema kuwa Mwezi Mei 2010, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilirekebisha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370 ya mwaka 2002 na kuifanya Ofisi inayojitegemea ili kuboresha uendeshaji na usimamizi wa Taasisi na Mashirika ya Umma katika dhana nzima ya kuruhusu ushindani katika soko la Uchumi huria.

"Tumelazimika leo kuwa na mafunzo haya ili kukumbushana Majukumu ya

Watendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma Pamoja na Bodi za Wakurugenzi kama mnavyofahamu, kufuatana na Sheria mbalimbali zinazounda Mashirika ya Umma, kila Shirika lina Mtendaji Mkuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ambayo ina wajibu wa kuiongoza Menejimenti katika utekelezaji wa majukumu ya Shirika husika,"amesema Amina.

"Kufanikiwa kwa Mashirika ya Umma kunategemea sana uimara wa Bodi za Wakurugenzi ambazo zinazingatia majukumu na mipaka yake ya kazi. Bodi ya wakurugenzi inawajibika kufuatilia, kusaidia na kuiwezesha Menejimenti ya Mashirika/Taasisi za Umma kuinua tija na kuongeza ufanisi,"

Amesema kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika baadhi ya Mashirika/Taasisi za Umma, ni Bodi kujiingiza katika mambo ya kiutendaji ya kila siku ya Shirika. Aidha, baadhi ya Wenyeviti wa Bodi wanafanya vitendo vinavyoashiria kwamba wao ni

Wenyeviti Watendaji badala ya kuwa Wenyeviti wa Bodi.

Tatizo hilo limejidhihirusha kuwa baadhi ya Wenyeviti wanadai nyenzo na marupurupu ambayo si stahili yao, kwa mfano Ofisi, nyumba, usafiri na posho mbalimbali, bodi kufanya maamuzi, kama vile kuidhinisha mikataba bila Msajili wa Hazina na Wizara Mama kutoa idhini, kuamuru uhamisho wa watumishi na kuitisha vikao vya watumishi huku Menejimenti kutokujulishwa na kurekebisha au kuidhinisha matumizi ya fedha za Shirika bila kufuata kanuni.

Mbali na hilo pia wanafanya miongozo ya usimamizi wa fedha za umma, pamoja na ununuzi.

Mashirika na Taasisi zote za Serikali zimetakiwa zihakikishe zinazingatia sheria, kanuni na taratibu zote zilizopo ikiwa ni pamoja na maagizo yanayotolewa na Serikali mara kwa mara sambamba na Sheria ya Msajili wa Hazina (Treasury Registrar ) (Powers and Functions) Sura 370 ya Mwaka 2002 na kama ilivyorekebishwa 2010,sheria ya Mashirika ya Umma (The Public Corporations Act) ya mwaka 1992 na marekebisho yake na Nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Serikali kwa ujumla.

Pili Kuhakikisha kuwa Shirika linafuata matakwa yote ya Sheria na kuendesha Shirika kwa ufanisi. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa Hesabu za Shirika zinakaguliwa kwa mujibu wa sheria,mapendekezo ya maoni ya wakaguzi wa hesabu kushughulikiwa na hoja za wakaguzi hao kujibiwa kikamilifu.

Kwa upande wa Uwajibikaji , Kila Bodi ina wajibu wa kutoa taarifa kwa mwenye mali kuhusu maamuzi makubwa yaliyochukuliwa au yanayotarajiwa kuchukuliwa na Bodi husika hususan, maamuzi yenye mwelekeo wa kisera au yenye maslahi ya kitaifa.

Kaimu Msajili wa Hazina Dkt Maftah Bunini amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeendelea kutekeleza jukumu lake la usimamizi wa Bodi kwa kuhakikisha zinakuwa hai na kuwa na Wajumbe wenye weledi wa kutosha. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2017, Taasisi na Mashirika ya Umma yapatayo 181 (77%) kati ya 234 yalikuwa na Bodi zilizo hai.

Aidha, Taasisi na Mashirika ya Umma yapatayo 53 hayakuwa na Bodi za Wakurugenzi. Ofisi ya Msajili wa Hazina imeandaa nyenzo ya Tathmini ya utendaji kazi wa Bodi (Board Evaluation Tool). Nyenzo hii inatumiwa na Wajumbe wa Bodi kutathmini utendaji wa kila mmoja wao na kufanya tathmini ya Bodi nzima kwa ujumla katika kipindi cha mwaka husika na kipindi chote wanachohudumu katika Bodi hiyo.

Mafunzo hayo yaliweza kuleta tija kwa wajumbe wa bodi na watendaji wakuu kutoka katika taasisi na mashirika ya Umma kuweza kufahamu majukumu yao na wajibu.
Kaimu Msajili wa Hazina Dkt Maftah Bunini akizungumza wakati wa mafunzo ya uwajibikaji kwa watendaji wakuu na wajumbe wabodi yaliyoendeshwa na ofisi ya Msajili wa Hazina.
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Leodegar Tenga akichangia jambo wakati wa mafunzo ya uwajibikaji kwa watendaji wakuu na wajumbe wa bodi.
Watendaji wakuu na wajumbe wa bodi wakifuatilia mafunzo hayo.

KILELE CHA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU KITAIFA WILAYANI MKALAMA, MKOA WA SINGIDA

$
0
0
Kampeni ya Juma ya Elimu Duniani huadhimishwa duniani kote kati ya mwezi wa nne na wa tano. Nchini Tanzania Maadhimisho haya huratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) Ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, serikali na taasisi binafsi.

Kwa  Mwaka 2018 maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yamefanyika Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kuanzia tarehe Mei 14 hadi Mei 18 2018 ambapo Mgeni rasmi katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa alikua Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Dk Rehema Nchimbi.

Akisoma majumuisho ya uhamasishaji wa juma la Elimu wilayani Mkalama Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania Dk. John Kallage alielezea mada ya Mwaka huu Kitaifa ni “Uwajibikaji wa pamoja kwa Elimu Bora kwa wote” na kwa wilaya ya Mkalama uhamasishaji ulifanyika katika Shule za Msingi sita na Shule za Sekondari tatu  ambapo ni katika vijiji sita ambavyo ni Mbigigi, Kikhonda, Ikolo, Mwangeza, Malaja na Nyahaa. 

Wadau wa elimu walifanikiwa kufanya mikutano ya kijamii ikijumuisha wazazi, wanajamii na viongozi wa serikali ya kijiji, dini na watu mashuhuri ili kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za Elimu kwa pamoja.

Wadau wa Elimu katika Ziara ya uhamasishaji wa Juma la Elimu katika wilaya ya Mkalama walibaini Changamoto mbalimbali ikiwemo Bajeti finyu ya Serikali isiyokidhi mahitaji ya Sekta ya Elimu, Upungufu Mkubwa wa  walimu  na hasa waalimu wa masomo ya Sayansi na walimu wa Kike, Upungufu wa madawati, Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada, Miundombinu isiyokidhi mahitaji mfano Vyumba vya madarasa, Vyoo, Maji na Nyumba za walimu pamoja na uhaba wa miundombinu rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dk Rehema Nchimbi  akizungumza na wadau wa elimu, walimu pamoja na wanafunzi wakati wa  kufunga maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa iliyofanyika katika wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Mwenyekiti Wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania Dk John Kallage akitoa risala ya majumuisho ya uhamasishaji ya Juma la Elimu Kitaifa yaliyofanyika katika wilayani Mkalama mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh Dk Rehema Nchimbi akigawa mipira ya Miguu kwa baadhi ya wakuu wa shule za Msingi na Sekondari katika wilaya ya Mkalama ambayo iliyotolewa na Mtandao wa Elimu Tanzania wakati wa kilele cha Maadhimisho ya juma la elimu Kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida. Dk Rehema Nchimbi akiendesha harambee ya kuchangia maboresho ya Elimu wilayani Mkalama wakati wa kilele cha juma la elimu yaliyofanyika wilayani humo.
Baadhi ya wanafunzi wakimuonyesha mabango yenye ujumbe wa Kuhamasisha Uwajibikaji wa Pamoja kwa Elimu Bora  wakati wa kilele cha juma la maadhimisho ya Elimu yaliyofanyika Wilayani Mkalama.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: CHINA YAIPIGAJEKI TANZANIA SHILINGI BILIONI 146

MKUTANO MKUU WA 23 WA BENKI YA CRDB WAFANYIKA LEO JIJINI ARUSHA, WANAHISA WAMTAKA DKT. KIMEI KUENDELEA KUIONGOZA BENKI YAO

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza wakati akitoa taarifa ya Benki kwa Wanahisa wa Benki hiyo, katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 19, 2018. Katika Mkutano huo, Sehemu kubwa ya wajumbe wamemuomba Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo,  Dkt. Charles Kimei kuendelea kuitumikia nafasi yake hiyo, ya kuingoza benki hiyo kwa miaka mingine mitano. 

Hatua hiyo ilifikia pindi, Dkt. Kimei alipowajulisha wanahisa hao wakati alipokuwa akitoa hotuba ya mwenendo wa benki, kuwa kwenye mkutano mkuu ujao, atawaaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kuitumia Benki hiyo.

Kwenye michango yao, baadhi ya wanahisa hao walisema hiki ni kipindi kigumu kiuchumi hivyo CRDB inahitaji mtu mwenye uzoefu wa kutosha kukabiliana na changamoto zilizopo. Mmoja wa wanahisa hao, Emburis Sirikwa wa Arusha alisema endapo mkurugenzi huyo ataondoka na kuiacha benki hiyo, ndani ya miaka miwili ya kutokuwanaye lazima ufanisi utapungua.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay akizunguza katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 19, 2018. 
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Abeid Mwasajone akizungumza jambo kwa wajumbe wa Mkutano huo, unaofanyika leo Mei 19, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, wakiwa kwenye Mkutano huo, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 19, 2018.
Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 19, 2018.
Sehemu ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakichangia mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 19, 2018.
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania na Mwanahisa wa Benki ya CRDB, Mzee Salim Mbonde akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 19, 2018.

SERIKALI YAKANUSHA KUONGEZEKA KWA DENI LA TAIFA

NEWS ALERT: CHINA YAIPIGA JEKI TANZANIA YA BILIONI 146.47 KWA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA USAFIRISHAJI NA UPEMBUZI YAKINIFU UJENZI WA RELI YA STANDARD GAUGE

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania imetiliana saini na Serikali ya China mkataba wa msaada wa kiasi cha Shilingi Bilioni 146.47. Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James na Balozi wa China nchini Wang Ke Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu alisema kuwa fedha hizo ni msaada na siyo mkopo na zitatumika katika miradi miwili ya miundombinu. Mradi wa kwanza ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) ambacho kitajengwa Mabibo Jijini Dar es Salaam kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 62 sawa na takriban Shilingi bilioni 138.3.

Mradi wa pili ni kwa ajili ya kusaidia upembuzi yakinifu na upembuzi sanifu wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (SGR), ambapo kiasi cha Sh. bilioni 3.2 kimetengwa kwa ajili hiyo.

Bw. Doto James alisema kwa sasa mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa umeanza kwa awamu mbili ambazo moja ni kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, na kuanzia Morogoro hadi Makutopora-Dodoma, upembuzi yakinifu utakaofanywa na Serikali ya China ni kwa maeneo mengine ya ujenzi wa Reli hiyo kuanzia Dodoma, Tabora hadi Mwanza na Kuanzia Kaliua hadi Kigoma.

"China imetusaidia miradi mingi ikiwemo mradi wa maji Chalinze, Ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Taifa, Mradi wa teknolojia za Kilimo mkoani Morogoro, Kituo cha upasuaji wa moyo na mafunzo, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Nyerere pamoja na misaada ya dawa na vifaa tiba" alieleza Bw. James

Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke, Alisema kuwa China inategemea kuona kuwa msaada huo utasaidia kuimarisha maendeleo na kuisaidia Tanzania kupata maendeleo haraka.

Aidha alisema China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo itawasaidia Watanzania na kuendeleza urafiki uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Balozi Wang Ke, amesema Pia Serikali ya China na Tanzania zinaendelea majadiliano kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, na kuongeza kuwa majadiliano hayo yatakapokamilika nchi yake itasaidia ujenzi wa bandari hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Taifa (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa ameishukuru Serikali ya China kwa msaada huo na kusema kuwa msaada huo utaisaidia chuo hicho kuweza kutoa wataalamu wa kutosha kuweza kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo sekta ya anga.

Amebainisha kuwa Chuo hicho Kikuu kitatoa mafunzo kwenye fani muhimu na zinazohitajika ikiwemo ufundi wa reli, masuala ya anga na sekta nyingine mtambuka kwa kutoa wataalamu waliobobea watakao changia kufanikisha azma ya Serikali ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania-TRC, Bw. Focus Msasani ameeleza kuwa msaada huo wa shilingi bilioni 3.22, utasaidia kuipunguzi serikali gharama ilizokuwa izitumie kwa kazi hiyo kenye mradi mkubwa wa kihistoria wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. Wang Ke wakitia saini mkataba wa msaada wa kifedha ambapo serikali ya China itaisaidia Tanzania jumla ya shilingi Bilioni 146.47  kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji pamoja na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard gauge. Hafla hii fupi imefanyika Ofisi za Hazina jijini Dar es salaam leo  Jumamosi Mei 19, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. wang Ke wakibadilishana mikataba baada ya kuitia saini makubaliano ambapo serikali ya China itaisaidia Tanzania jumla ya  shilingi Bilioni 146.47  kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji pamoja na  upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard gauge. Hafla hii fupi imefanyika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam leo  Jumamosi Mei 19, 2018 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. Wang Ke baada ya wawili hao kutia saini kwa niaba ya nchi zao wa mkataba wa msaada wa kifedha ambapo serikali ya China itaisaidia Tanzania jumla ya shilingi Bilioni 146.47 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji  pamoja na  upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard gauge. Hafla hii fupi imefanyika Ofisi za Hazina jijini Dar es salaam leo  Jumamosi Mei 19, 2018. Picha na IKULU.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images