Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA MAKOMBE YA UBINGWA WA SERENGETI BOYS NA TSC, AKABIDHI LA UBINGWA WA LIGI KUU KWA SIMBA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia  mchezo wa kutimiza ratiba kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba SC  na Kagera Sugar ambapo Simba walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia baada ya mchezo wa kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodaco kati ya Simba SC na Kagera sugar ambapo walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi kombe la Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka ya Vodacom kwa nahodha wa Simba SC John Bocco baada ya mchezo wa kutimiza ratiba klabu hiyo ya Msimbazi na Kagera sugar ambapo walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na viongozi wengine katika picha ya pamoja na timu ya Tanzania ambayo ni Washindi wa Pili wa michuano ya dunia ya vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo Tanzania ilifika fainali na kufungwa bao 1-0 na Brazil huku Urusi. Hii ilikuwa  baada ya mchezo wa kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodaco kati ya Simba SC na Kagera sugar ambapo walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na viongozi wengine katika picha ya pamoja na timu ya Serengeti Boys ambao ni mabingwa wa Kombe la vijana wa umri wa chini ya miaka 17 wa CECAFA wa  baada ya mchezo wa kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodaco kati ya Simba SC na Kagera sugar ambapo Simba walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na viongozi wengine katika picha ya pamoja waamuzi na wasimamizi baada ya mchezo wa kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodaco kati ya Simba SC na Kagera sugar ambapo Simba walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja wachezaji na iongozi wa Kagera Suger  baada ya mchezo wao wa  kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom  kati yao na Simba SC ambapo  Kagera sugar walishinda  bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018   
  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Klabu Bingwa ya Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC baada ya mchezo wa kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodaco kati yao Simba SC na Kagera sugar ambapo walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018   
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mashabiki wa soka mikono baada ya mchezo wa kutimiza ratiba wa Ligi Kuu ya Soka ya Vodaco kati yao Simba SC na Kagera sugar ambapo walifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumamosi Mei 19, 2018. Picha na IKULU    


REMA FC YAINYUKA AIRPORT FC MAGOLI 8-4,YATINGA FAINALI KURUGENZI CUP KUKUTANA NA DONGOBESH FC KESHO

$
0
0
Aziz Rashid wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom wilayani Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom, Timu ya Rema 1000 FC imeifunga timu ya Airport Magoli 8-4 na kutinga fainali ambapo sasa itakutana na timu ya Dongobesh FC ambayo nayo imeshinda mchezo wake wa leo wa Nusu Fainali baada ya kuifunga timu ya Young Boys FC magoli 2-0 .

Mashindano hayo yanaandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na yanafanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom kwa udhamini mkubwa wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mkoani Iringa na Benki ya CRDB.

Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kwenye uwanja wa huohuo kwa kuzikutanisha timu za Dongobesh FC na Rema 1000 FC ambapo pia kutakuwa na burudani mbalimbali za ngoma za asili wakiwemo pia wachekeshaji MC Pilipili na Katarina wa Karatu.
Aziz Rashid wa Rema 1000 FC ya Haydom Mbulu akimiliki mpira huku Elihuruma Daniel wa timu ya Airport FC akijaribu kunyanga'anya huku kiatu kikiwa kimechomoka mguuni wakati wa mchezo wao wa nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Kurugenzi Cup 2018 yanayoendelea mjini Haydom 
Kocha wa timu ya Rema 1000 FC Bw. Jared Ochieng akiwaelekeza wachezaji wa timu yake kwa kuchora chini kutokana na makosa waliyokuwa wakisababisha katika mchezo huo wakati wa mapumziko.
Bw.Samson Madawabora ambaye ni Daktari katika Hospitali ya Haydom na mmiliki wa timu hiyo akiwapongeza wachezaji wake mara baada ya kutinga fainali ya michuano hiyo leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga pamoja na baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo wakifuatilia mchezo huo.

CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KITUO CHA AFYA INYALA MKOANI MBEYA KUKAMILIKA MWEZI JULAI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Mbeya

KITUO cha Afya cha Inyala, kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha jengo litakalotumika kuhifadhia maiti ili kuondokana na changamoto ya kusafirisha maiti kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa.

Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Inyala, Alvin Mutiganzi wakati akipokea dawa za mgawo wa mwisho wa mwaka wa fedha wa 2017/2018 kutoka Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mbeya.

Mutiganzi alisema tayari majokofu ya kuhifadhia maiti hizo yaliyonunuliwa na MSD yalifika kituoni hapo mwezi Februari mwaka huu, na yana uwezo wa kuhifadhi maiti sita kwa wakati mmoja.

Alisema, ujenzi huo unatarajia kukamilika mwezi Julai mwaka huu na kuanza kutoa huduma mara moja.Kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo kutasaidia kutoa huduma ya kuhifadhi maiti kutoka vijiji 50, vinavyopata huduma katika kata ya Inyala na maeneo mengine ya jirani.

"Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti kwenye hiki kituo chetu cha afya kwetu ni jambo la faraja kwani hii ndio ilikuwa changamoto yetu kubwa ambapo kwa sasa tunalazimika kwenda kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa na Ifisi ambapo gharama zake ni zaidi ya shilingi 60,000 kwa kwenda na kurudi kwa maiti moja.

Mutiganzi aliongeza kuwa kwa mwezi, kituo hicho kinaweza kupokea maiti watatu hadi wanne ambao hulazimika kuwasafirisha kwenda hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya na kwamba wagonjwa wanaofika kutibiwa ni 40.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha cha Afya cha Inyala, Alvin Mutiganzi (kushoto), akitoa maelekezo ya ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti kwa maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) na waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho mkoani Mbeya jana. Kulia ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Victoria Minja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mbeya, Michaely Mwakuna.
Ofisa Huduma kwa Wateja wa MSD Kanda ya Mbeya, Michaely Mwakuna (kulia), akitoa maelezo ya jinsi ya ugawaji wa dawa na vifaa tiba za mgawo wa mwisho wa mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Inyala, Alvin Mutiganzi, akikagua moja ya boksi la dawa baada ya kupokea. Kulia ni Mariam Pamboma mkazi wa Inyala ambaye alishuhudia makabidhiano hayo na kushoto ni Muuguzi wa kituo hicho cha Afya na wa pili kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya afya wa Kijiji cha Inyala, Jairos Emanuel.
Dawa zikikaguliwa. Katikati ni Ofisa Mauzo wa MSD Kanda ya Mbeya, Rhoda Joseph.

WAKALA WA VIPIMO TANZANIA WAZIKAGUA TOCHI ZA ASKARI USALAMA BARABARANI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAKALA wa Vipimo Tanzania(WMA) wamefanya ukaguzi wa tochi za Askari wa Usalama Barabarani katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kupima ubora wa vifaa hivyo vya usalama.

Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Vipimo duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo Mei 20 ya kila mwaka ambapo Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa  amesema ukaguzi huo umelenga kupima ubora wa vifaa vya usalama barabarani ili kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani hapa nchini.

Pia amesema kumekuwepo malalamiko kwa watumiaji wa barabara kwa kuamini kuwa tochi zinazotumiwa na askari wa usalama barabarani zinawapunja speed, hivyo wameamua kuzipima ili kuangalia kama ni kweli ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa tochi hizo.

Kwa upande wa Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai amewahimiza madereva kutii sheria bila shuruti ili kupunguza ajali barabarani.

Pia amewatoa hofu watumiaji wa barabarani kuwa tochi zinazotumiwa na askari wa usalama barabarani zimekaguliwa na hazina tatizo, hivyo ni kutii sheria na ukomo wa speed ili kupunguza ajali za barabarani.
Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) pamoja na Askari wa Usalama barabarani mkoani Pwani wakifanya vipimo vya ubora wa tochi za barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) Siraji Moyo(kushoto) pamoja na Glory Mtana (kulia) wakihakiki vipimo vinavyotolewa na tochi za barabarani ili kujilizisha wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa(kushoto) akielekezwa  na mmoja wa Polisi wa usalama barabarani mkoani Pwani namna ya kupima spidi ya magari kwa kutumia tochi za Usalama barabarani  wakati wa maadhimisho ya wiki ya vipimo Duniani.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa tochi za Barabarani  zinazotumiwa Askari wa usalama Barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akionesha mmoja ya tochi wanazotumia askari wa usalama barabarani mara baada ya kufanyiwa ukaguzi na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Vipimo Duniani yanayoazimishwa Mei 20 kila mwaka.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi  na Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Pwani (ASP),Mossi Ndozero akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tochi zilivyosaidia kupunguza ajali za barabarani ambapo mwaka huu zimepungua sana mkoani humo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), Stella Kahwa, Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Kitengo Cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai, Maafisa Vipimo kutoka Wakala wa vipimo Tanzania (WMA) pamoja na askari wa Usalama Barabari wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya ukaguzi wa tochi wanazotumia Askari wa Usalama Barabarani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANAFUNZI 78 WATUNUKIWA TUZO YA BALOZI WA CHINA KWA KUHITIMU LUGHA YA KICHINA, WIZARA YATOA NENO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JUMLA ya Wanafunzi 78 kutoka baadhi ya shule za msingi, sekondari na Vyuo Vikuu nchini wametunukiwa Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke baada ya kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kichina huku Wizara ya Elimu ,Sayansi, Teknolojia na Ufundi ikihimiza Watanzania kuchangamkia fursa kwa kujifunza lugha hiyo.

Mafunzo hayo ya lugha ya Kichina na mchakato wa utoaji tuzo hiyo ya Balozi wa China nchini yameandaliwa na Chama cha Kukuza Uhusiano wa China na Tanzania(Tanzania China friendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dk.Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu ni Joseph Kahama.

Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati wa utoaji tuzo hizo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Ave Maria Semakafu amesema kuhitimu kwa vijana hao 78 kwa kuifahamu lugha ya Kichina kutatoa fursa nyingi kwao ikiwamo ya kupata ajira katika nchi ya China kwani kuifahamu lugha yao ni sawa na kufahamu utamaduni wao.

Amefafanua kwa vijana wa Kitanzania ambao watakuwa wanakifamu vema Kichina ni rahisi kufundisha nchini China na kufanya kazi za aina mbalimbali pale watakapohitaji na kwa Tanzania kuna Shule 24 zinafundisha Kichina na wanafunzi wanaosoma somo hilo wanafanya mtihani.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Dk.Ave Maria Semakafu(aliyevaa gauni)akimkabidhi tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke mwanafunzi  wa Shule ya Nsingi Msoga Arafa Shaibu ambaye amehitimu lugha ya Kichina

 Mgeni rasmi katika utoaji wa Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania Wang  ambao wamehitimu mafunzo ya lugha ya Kichina,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Dk.Ave Maria Semakafu (wa kwanza mstari wa mbele)akifuatilia hotuba wakati wa utoaji Tuzo hizo
Political Counceller wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Yang Tong akizungumza kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo nchini Wang Ke wakati wa utoaji Tuzo kwa wanafunzi 78 wa Tanzania ambao wamehitimu mafunzo ya lugha ya  Kichina.Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia utoaji Tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania kwa wanafunzi ambao wamehitimu mafunzo ya Lugha ya Kichina
 Political Conceller wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Yang Tong (kushoto)akiwa ameshika tuzo pamoja na mwanafunzi baada ya kumkabidhi
 Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bao Bao Mariam Said akiwa ameshika tuzo ya Balozi wa China nchini Tanzania baada ya kutunukiwa jijini Dar es Salaam kutokana na kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kichina ambayo yameandaliwa na Chama cha Kukuza Uhusiano Tanzania na China
 Baadhi ya raia wa China nchini Tanzania wakiwa wamebeba baadhi tuzo ambazo wametunukiwa wanafunzi waliohitimu kujifunza somo la Kichina.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA YA ARDHI YAKAGUA MAENDELEO YA UIMARISHAJI MPAKA WA KIMATAIFA KATI YA TANZANIA NA KENYA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Dkt. James Mtamakaya kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (wa nne kutoka kulia) akiangalia mojawapo  ya alama iliyoharibika katika Kijiji cha Nyakalima wilayani Tarime mkoani Mara wakati wa ukaguzi wa kazi  inayoendelea ya uimarishaji wa mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya. Kazi hii inayohusisha nchi zote mbili ilianza Machi mwaka huu na inatarajiwa kukamilika mwezi ujao.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Nyanza nchini Kenya Bw. Moffat Kangi.

MIGOMBA MABINGWA SIRRO CUP 2018 KIBITI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Migomba kutoka Rufiji kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Mjawa kutoka Kibiti katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mjawa kutoka Kibiti kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Migomba kutoka Rufiji katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Msanii Malima Ndolela akitumbuiza wakati wa sherehe za kufunga Michezo ya kuwania kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) katika uwanja wa Samora Kibiti. Timu ya Migomba kutoka Rufiji ililifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Chatanda akimkabidhi seti jezi nahodha wa timu ya Mjawa Bakari Tuga kutoka Kibiti baada ya kushika nafasi ya pili katika kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Migomba kutoka Rufiji katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya Migomba Maulid Mtupa baada ya kuibuka mabingwa wa kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) kwa kuichapa Mjawa kwa penati 12 kwa 11 katika uwanja wa Samora Kibiti. (Picha na Jeshi la Polisi).

Mwongozo wa Tathmini ya Mazingira Kuchochea Ukuaji wa Uchumi

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amezindua Muongozo wa Tathmini ya Mazingira  (SEA) ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kulinda mazingira ili yaweze kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta  maendeleo  endelevu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo  Jijini Dodoma Waziri Makamba amesema kuwa dhamira ya Serikli ni kuhakikisha kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali pamoja na wawekezaji inafanyiwa tathmini hiyo ili kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

"Nawapongeza WWF kwa kazi nzuri za tafiti wanazofanya na hata kupatikana kwa muongozo huu ni matokeo ya kazi nzuri waliyofanya kama wadau wetu ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira " Alisisitiza  Mhe. Makamba

Akifafanua amesema kuwa anazikumbusha Wizara ,  Taasisi na wadau wote wanaotaka kutekeleza  miradi ya maendeelo kuhakikisha kuwa wanazingatia muongozo huo ambao umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inajenga uchumi wa viwanda.

Aliongeza kuwa Ofisi yake ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa SEA  katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe. January   Makamba akihutubia  washiriki wa  hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
  Kaimu  Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Esther Makwaia akiwasilisha maelezo kuhusu muongozo wa  tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akiteta jambo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe. January   Makamba wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe. January   Makamba  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla ya  mwongozo wa  tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
( Picha zote na Frank Mvungi, MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MADIWANI WA UYUI WAAGIZWA KUSAIDIA KUDHIBITI UUZAJI OVYO WA CHAKULA MKOANI TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Uyui na maeneo mengine kuhakikisha wanasaidia kudhibiti uuzaji holela wa chakula unaofanywa na baadhi ya wananchi bila kujiwekea akiba kwa ajili ya siku za baadaye.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila familia iwe na akiba ya chakula ambacho kitaweza kuwafikisha  mavuno ya msimu ujao bila kuomba msaada Serikalini.

Mwanri ametoa kauli hiyo leo wilayani Uyui wakatika wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kinapitia mambo mbalimbali ikiwemo uhifadhi wa mazingira na chakula na kupitia taarifa za miradi mbalimbali.

Alisema utaratibu wa uuzaji wa chakula utakuwa kwa kila kaya kujaza fomu maalumu ambayo itaoonyesha chakula alichovuna msimu huu , matumizi yake kwa mwaka na ziada iliyobaki na ndipo ataweka sahihi ya kukiri taarifa kabla ya kuruhusiwa kuuza.

Mwanri alisema lengo la kufanya hivyo kutaka kuwabana wale wote wenye tabia ya kuuza ovyo ovyo chakula na kikiisha wanakimbilia kuomba msaada Serikalini wakati wenyewe ndio hawakuchukua tahadhari. Alisema pia mavuno ya mwaka huu kwa mahindi yanaweza yasiwe mazuri kutokana na mazao hayo kushambuliwa na wadudu , kwa hiyo ni vema watu wakachukua tahadhari mapema.

Mwanri alisema hamkatalii mtu kuuza mazao yake lakini akiwa Kiongozi wa Mkoa anabeba dhamana ya kuhakikisha usalama wa wananchi ukiwemo wa chakula ndio maana anataka atakayeuza awe kweli ana akiba ya kutosha ili isije ikafika wakati wa njaa anaandamana kwenda Mkoani kuomba msaada.

Kwa upande wa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Uyui, Said Ntahondi aliwataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ya utunzaji wa chakula na kwa kushirikiana na Watendaji katika maeneo yao ili waweze kutoa taarifa ambazo ndio zitawapa fursa ya kukubaliwa kuuza au kutouza. Alisema mtu atakayeruhusiwa kuuuza chakula ni yule kweli ambaye anacho chakula cha kutosha familia yake kwa mwaka mzima na awe na ziada iliyothibitika.

Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora , Uyui limekubalina kuwa kuanzia sasa kila familia lazima iwe na msitu wake na kila kijiji kiwe na msitu wake kama juhudi za kulinda mazingira. Ntahondi alisema hatua hiyo itasaidia katika kuhakikisha jamii inaanzakuwa na uwelewa mzuri kuhusu faida ya misitu na kukabiliana na wavamizi wa mistu.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwaagiza Madiwani na Watendaji mbalimbali kuhakikisha wanasimamia Sheria katika kulinda hifadhi za mistu na vyanzo vya maji kwa ajili ya ustawi mzuri wa Mkoa huo.

Aliongeza kuwa katika maeneo ya miji  na barabara ambayo viti hajapandwa ni vema ikapanda ili kuipendezesha miji na kulinda mazingira.

QNET Yatoa Faraja kwa jamii zisizojiweza katika nchi 13 za kiafrika

$
0
0
Mwakilishi wa kampuni ya QNET Tanzania Andrew Gerald akikabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya 9mil/- kwa Mlezi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif Dar Es Salaam, Bi. Zainab Bakary kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampuni ya QNET inatoa msaada kwa nchi mbali mbali 13 barani Afrika kwa ajili ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Wawakilishi wa kampuni ya QNET Tanzania wakikabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya 9mil/- kwa Mlezi wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif Dar Es Salaam, Bi. Zainab Bakary kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampuni ya QNET inatoa msaada kwa nchi mbali mbali 13 barani Afrika kwa ajili ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inayoongoza kwa kushirikiana na mwakilishi wake wa kijitegemea (IRs) kuleta shangwe na faraja kwa jamii mbalimbali zisizojiweza katika kuashiria mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika nchi 13 za Kiafrika.

Kampeni hii ya mwaka ina lengo la kuboresha maisha ya wengi na inaenda sambamba na falsafa ya kampuni hii ya (RYTHM) Jiinue kuwasaidia wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind) Mafunzo ya msingi ya (RYTHM) wakati wote yamekuwa yanalenga katika kuongeza juhudi zaidi ya wajibu katika kujali wale ambao hawana uwezo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi kwaajili yao, hasa watoto ambao ni alama ya kizazi chetu kijacho.

Kampeni ya mwaka huu ya Ramadhan katika Afrika itashuhudia ushirikiano mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa QNET, wakala na Wawakilishi Binafsi (IR) wakiunganisha jitihada zao katika kuandaa mfululizo wa mwezi mzima wa shughuli za kutoa misaada katika nchi kama Ivory Coast, Togo, Cameroon, Guinea, Burkina Faso, Tanzania, Niger, Uganda, Chad, Mali, Ghana and Senegal.

Nchini Tanzania, tukio la utoaji wa misaada ya Ramadhan litashuhudia utoaji wa mchele, tambi, sukari na bidhaa zingine za chakula na matumizi kwa kituo cha Kulelea watoto yatima cha Maunga Children Centre jijini Dar es salaam.

Kuna watoto 54 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Children Centre ambacho kilianzishwa katika mwaka 2008. Makazi haya ya watoto kwa sasa yanasimamiwa na Zainab Bakary na wanategemea misaada ya umma na wasamaria wema kuweza kukabiliana na gharama za mahitaji ya watoto ya vyakula na vinywaji.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo mwaka huu, Trevor Kuna, CEO wa QNET, amesema "Kampeni za kutoa misaada ya Ramadhan imekua moja kati ya kampeni zetu za msingi za kila mwaka. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. Kampeni kama hizi huhamasisha uwezeshaji wa jamii na pia huwa zinahamasisha sana kwa wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu binafsi (IR's) kwa kushiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya engine.

MAKONDA APOKEA VIFAA VYA THAMANI MILIONI 400/- KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa vifaa vya  ujenzi vyenye thamani ya Sh.milioni 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam.

Vifaa alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya Sh.million 360, nondo tani 22 zenye thamani ya Sh.million 40 ambapo kiwanda hicho kimemuahidi tena kumpatia vifaa vingine ikiwemo rangi, nondo na mabati. 

Akipokea vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam, Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya Mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu na kuwaomba wadau na wananchi kujitokeza kuchangia kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu. 

Aidha amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka Uingereza na kontena 10 za Maziwa kutoka China kwaajili ya watoto waliojitokeza wakati wa mchakato wa kutafuta haki ya watoto waliotelekeza kama sehemu ya msaada.

Kwa upande wake Patel amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu na kuunga mkono jitiada za RC Makonda katika uboreahaji wa elimu kupitia mazingira bora ya walimu kufanya kazi.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa vifaa mablimbali  kwa ajili  ujenzi wa ofisi za Walimu na kiwanda cha MIN Steel vyenye thamani ya shilingi milioni mia nne.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akiangalia mapati aliyo kabidhiwa na kiwanda cha MMI Siteel kwajili ya kuezekea ofisi za walimu.
 Mkuu wamkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda(katikati) akimshukuru  Mkurugenzi wa Kiwanda cha MMI Steel Ltd,Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu (kulia) Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam,Hamis Lissu.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

Dkt. Kalemani aiagiza TANESCO kuondoa mita za umeme za zamani kabla ya mwezi Julai

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo kuhakikisha kuwa, mwisho wa kutumia mita za zamani, ambazo wateja hufanya malipo baada ya kutumia umeme (Conventional Meters), ni mwezi Juni mwaka huu.

Dkt.Kalemani aliyasema hayo wilayani Ileje mkoani Songwe wakati akizungumza na Mkuu wa wilaya hiyo, Joseph Mkude, Mbunge wa Ileje, Janet Mbene,  Watendaji wa TANESCO Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Wizara ya Nishati, na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kabla ya kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu katika Wilaya husika.

Alisema kuwa, jumla ya wateja Laki Tatu (300,000), katika nchi nzima hutumia mita hizo za zamani huku wateja 48,000 wakiwa wanatumia conventional meters ambazo muda wake umeisha.

" Kuendelea kutumia mita hizi ni kupoteza mapato ya Shirika, kwa mfano hawa wateja 48,000 wanatumia umeme bila sisi kujua wametumia kiasi gani, hivyo nawaagiza kuwa, mwisho wa kutumia mita hizi ni mwezi Juni na wateja wote wafungiwe mita mpya za umeme ili Serikali ikusanye mapato yake ipasavyo," alisema Dkt Kalemani.

Aidha, Dkt. Kalemani aliwaagiza Mameneja wa TANESCO nchini kuhakikisha kuwa kazi ya kufanya marekebisho mbalimbali katika miundombinu ya umeme ikiwemo uondoaji wa nguzo zilizochakaa  iwe imekamilika kabla ya mwezi Juni mwaka huu kwani fedha za kufanya kazi husika zilishatolewa.

Akizungumzia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III), Dkt. Kalemani alisema kuwa, mradi huo unaolenga kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini, utakamilika mwezi Juni mwaka 2021 ambapo lengo ni kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wawe wameunganishwa na huduma ya umeme kufikia mwaka huo.

Waziri wa Nishati, pia aliwaagiza watendaji wa TANESCO, REA na Wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kuhakikisha kuwa vijiji vyote ambavyo vilipitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina umeme, visambaziwe nishati hiyo kupitia mradi wa REA III mzunguko wa kwanza unaokamilika mwezi Juni, 2019.

Vilevile, alitoa wito kwa Halmashauri zote pamoja na Serikali za Vijiji nchini, kutenga fedha zitakazosaidia Taasisi za Serikali katika maeneo yao kama vile Shule na  Vituo vya Afya kuunganishwa na huduma ya umeme ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.

kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude, alisema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme katika wilaya hiyo inaridhisha kwani wanapata umeme kutoka gridi ya Taifa  na kwamba vijiji 31 kati ya 71 tayari vimeungwanisha nishati hiyo.

Aliongeza kuwa, katika mradi wa REA III mzunguko wa kwanza, vijiji 28 katika wilaya hiyo vitasambaziwa umeme ambapo shilingi Bilioni 34.6 zitatumika kwa kazi husika.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa Tatu kushoto) akitia saini katika kitabu cha wageni mara alipowasili katika Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe  kwa lengo la kukagua mradi wa usambazaji umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo, Joseph Mkude, wa pili kushoto ni  Mbunge wa Ileje, Janet Mbene na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Mapogoro wilayani Ileje wakati alipofika kijijini hapo kukagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini pamoja na kuzindua huduma ya upatikanaji wa umeme katika Kijiji hicho.

BALOZI LUVANDA ATEMBELEA WANAFUNZI WATANZANIA WANAOSOMA JIMBO LA PUNJAB NCHINI INDIA

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchi India Mhe.  Baraka Luvanda ametembelea na kuhudhuria  hafla ya wanafunzi wa Kiafrika wanaosoma kozi mbalimbali katika vyuo jimboni Punjab. 
Hafla hii iliofanyika Mei18, 2018 ilijumuisha wanafunzi karibu wote wa Kitanzania wanaosoma Punjab. Ilijumuisha vyuo kama Gian Jyoti institute of management and technology( chuo kilichoandaa event) ambacho ni miongoni mwa vyuo bora vya masomo ya biashara nchini India,  CDac na vyuio vinginevyo.  
Hafla iliandaliwa na mwanafunzi Bakari Chuma wa mwaka wa pili anaesomea course ya MBA  akishirikiana  na uongozi wa chuo Gian Jyoti Institute of Management and Technology.
 Balozi wa Tanzania nchini  India Mhe. Baraka H. Luvanda wakiwa na mwambata wa elimu Bw. Yahaya A Mhata, Mwenyekiti wa Gian Jyoti groups of institutions  Bw. J. S. Bedi na  Dean wa wanafunzi wa kimataifa Gurdeepak Singh na  baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania Mariam Sunday na Vivian Omar na wengine kutoka mataifa mbalimbali. 
 Balozi Luvanda akiwa katika kilemba cha asili akikaribishwa na wenyeji
 Balozi Luvanda akiwa ndugu Yahaya A Mhata  pamoja na  Mr j. S. Bedi chairman na Mkurugenzi Dr Aneet (saree ya njano) wakifurahi na wanafunzi
 Balozi akiwa na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Punjab.

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI DOMINIKA YA SHEREHE YA PENTEKOSTE, KANISA LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya jumapili Dominika ya sherehe ya Pentekoste liyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam leo Mei 20, 2018.
  Paroko msaidizi wa parokia ya Osterrbay Padre Asis Mendokta akiongoza ibada ambayo pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amehudhuria Ibada hiyo ya Dominika ya sherehe ya Pentekoste liyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa Amani na wanafunzi waumini alijumuika na waumini wengine kusali Ibada ya jumapili Dominika ya sherehe ya Pentekoste liyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya jumapili Dominika ya sherehe ya Pentekoste liyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Paroko msaidizi Padre Asis Mendokta mara baada ya kushiriki Ibada ya jumapili Dominika ya sherehe ya Pentekoste liyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

DC WA SAME AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MEI 30 MWAKA HUU

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule amemtaka mkandarasi wa mradi wa maji Kijiji cha Hedaru kukamilisha mradi huo unaogharimu bilioni 1.18 ifikapo Mei 30 mwaka huu.

Akitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo juzi mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ni kuona mwanamke anatua ndoo kichwani kwa kupata huduma ya maji .

Alisema mradi huo umelenga kufikia vijiji 10 ambao ulitakiwa kukamilika toka mwaka 2015 ila hadi sasa umekuwa ukienda kwa kusuasua .Hivyo alimtaka mkandarasi kuhakikisha maji yanatoka sasa wakati wa kiangazi kwani wananchi wamekuwa wakihofu kama kweli mradi utatoa maji wakati wa kiangazi.
" Naitaka kamati iliyoundwa kusimamia maji kukagua maeneo yote na kutoa taarifa kwa mhandisi kabla mkandarasi hajakabidhi ili akabidhi mradi usio na kasoro"

Hata hivyo alisema katika ukaguzi alioufanya katika mradi huo amebaini mifumiko mingi imevunjika, koki nyingi zimeibiwa."Mji wa Hedaru ni mji unaaongoza kwa kukua kwa kasi Wilayani Same Mhandisi Mussa aeleza jinsi mradi huo utakavyoongezewa nguvu na tanki lingine linalojengwa mwaka huu, ili kukidhi ongezeko la watu"

Alisema kuwa mradi huu ni kati ya miradi iliyokuwa imeainishwa kwenye ilani ya CCM 2010- 2015 hivyo atakayecheza nao atawajibishwa vikali .
Mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule akikagua mradi wa maji katika wilaya ya Same 
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akitoa maagizo ya kutaka mradi wa maji Hedaru kukamilika haraka


SERIKALI YAWAASA VIONGOZI WA DINI KUEPUKE MIGOGORO

$
0
0
SERIKALI imewaasa viongozi wa dini waeuepuke migogoro ya mara kwa mara katika Makanisa yao na badala yake waendelee kuwajenga waumini wao wakue kiroho na kujenga dhana ya umoja na upendo katika Taifa.

Pia imesema inawashukuru viongozi wa dini na madhehebu yote ya dini kwa kuendelea kuiombea nchi amani, mshikamano na utulivu, jambo ambalo linaongeza chachu kubwa kufikia mafanikio ya maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Hayo yamesemwa leo (Jumapili, Mei 20, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ibada ya kutawazwa Askofu Dkt. Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga kuwa Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania. Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika Jijini Dodoma.

“Nawaombeni wote kwa ujumla wetu, tuendelee kutumia Makanisa yetu kuombea Taifa hili ili tuendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano”. Watu wa Mungu ni watu wa Upendo, watu wa Mungu ni watu wa amani, watu wa Mungu ni watu wa kiroho”.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “haitarajiwi kuona watu wa Mungu wakiwa katika mstari wa mbele kuchochea migogoro, kuvunja amani ya Kanisa na kuongoza makundi yanayopingana katika kazi ya Bwana”.Amesema jukumu la makanisa ni kuwajenga waumini kukua kiroho, na kazi ya kuwaongoza watu wamjue Mwenyezi Mungu, ambapo amewaomba imani yao iwe moja na matendo yao yafanane na yale ya Kristo Yesu wanayemuamini.

Waziri Mkuu amesema kuwa nchi haiwezi kupata mafanikio ya kiuchumi na kijamii bila kuilinda amani iliyopo, hivyo amewaomba warejee kumbusho la maandiko Matakatifu katika Waebrania 12:14 “Tatufeni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote”.

Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi hao na wananchi kwa ujumla waendelee kuwaombea viongozi wa Tanzania hususani Rais Dkt. John Magufuli, kuendelea kuwa na afya njema, busara, upendo, hekima katika kuiongoza nchi yetu.

Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli katika ibada hiyo amesema Serikali inatambua ushirikiano uliopo kati ya madhehebu mbalimbali ya dini nchini kwa ujumla wake na kwamba ushirikiano huo ni wa kihistoria.
 Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Maimbo Fabian Mndolwa  akila kiapo wakati alipotawazwa  kuw Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, jijini Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikan Tanzania, Jaco Chimeldya katika  sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mdolwa  jijini Dodoma, Mei 20,2018. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika sherehe hiyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza katika  Rais John Pombe Magufuli kwenye sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa saba, Maimbo Fabian Mndolwa, jijini Dodoma, Mei 20, 2018.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania,  Maimbo Fabian Mndolwa  baada ya Askofu huyo kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, jijini Dodoma, Mei 20, 2018, kulia ni mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. Waziri Mkuu alimwakilisha  Rais John Pombe Magufuli.
 Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania , Oscar Mnunga katika sherehe ya kumtawaza Askofu  Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mndolwa  jijini Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

kituo cha msaada wa kisheria chazinduliwa chuo kikuu cha Mzumbe wilayani Mvomero,mkoani Morogoro

$
0
0


Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha msaada wa kisheria Mohamed Utaly akikata utepe katika vitabu vinavyozungumzia mambo ya sheria kuashiria uzinduzi wa kuanzishwa kwa kituo cha msaada wa kisheria chuo kikuu Mzumbe Mkoani Morogoro,kulia ni Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha mzumbe Prof, Lughano Kusiluka .
Mkuu wa kitivo cha sheria chuo kikuu cha mzumbe Prof, syriacus Binamungu akimkaidhi Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Prof, Lughano Kusiluka vitabu vinavyohusu mambo ya sheria kwa ajili ya makamu Mkuu wa chuo kukabidhi  kwa mgenia rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly ili aweze kuzindua rasmi. Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Prof Lughano Kusiluka akiwasisitizia wanchuo kitivo cha sheria kuhakikisha wanajituma kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho chuoni hapo .
Mhadhiri msaidizi chuo kikuu mzumbe Hassani Ramadhani Gyunda (aliyevaa shati nyeupe) akimuelezea mgeni rasmi Mohamed Utaly (kushoto) jinsi watakavyoweza kufanya kazi katika kutatua changamoto za kisheria ambazo zinawakabili wananchi, aliyekaa chini upande wa mgeni rasmi ni mwananchi anayepatiwa msaada wa kisheria Rashidi Ramadhan mkazi wa sangasanga mkoani Morogoro .

SERIKALI YAKAMILISHA UJENZI BOMBA LA GESI KIWANDA CHA DANGOTE

$
0
0
JOSEPH MPANGALA,MTWARA
Serikali imesema imekamilisha ujenzi wa Bomba la gas utakoyoiwezesha kampuni ya kuzalisha saruji ya Dangote iliyopo mkoani Mtwara ambayo inataraji kuzalisha umeme wa megawatts 35 ambazo zitatumika kwa ajili ya matumizi ya Kiwanda Hicho.
Akiongea mara baada ya kutembelea plants ya Kuzalisha umeme ambayo inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani amesema kuwa tayari serikali ipo tayari kwa ajili ya kutoa nishati ya Gas ili kampuni ya Dangote  kuweza kuzalisha umeme.
“Na mm nawaambia tena TPDC wakichelewa baada ya mezi kuisha wakumbushe kwa barua ili lieleweke kama nani anayechelewa lakini sio wanachelewa kwa makusudi bali wanamaandalizi yao wenyewe lakini sisi kwa upande wetu kama serikali tupo tayari hata kama wangetaka leo jioni watachukua gas ili waendelee kwa hiyo nilitaka kuliweka hili Vizuri kwamba tumeendelea vizuri kati ya TPDC na Dangote”
Lakini naye Mhandisi wa kampuni ya BQ Cntractors Limited John Bura anasema Dangote ataendelea kununua nishati ya Gas zaidi ambapo kufikia mwisho wa mwezi June Mtambo itakuwa umekamilika tayari kwa kuanza kwa uzalishaji wa Saruji ambapo ni umbali wa kilomita 2.7 kufikia kiwandani
Aidha ameongeza kuwa kwa sasa uzalishaji wa saruji ni asilimia 50 lakini kukamika kwa ujenzi huo kutawezesha kampuni ya dangote kuzalisha saruji mifuko lakimoja na Nusu kwa siku.

Meneja Mkuu wa GASCO Mhandisi Baltazari T.Mrosso akimuonesha waziri wa Nishati Dk.Medard Kelamani Bomba la Gas linalopeleka Nishati hiyo katika Kiwanda cha Umeme cha Dangote.


Waziri wa Nishati Dr.Medard Kelamani akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata Gas na Bomba la Gas Linaloelekea Kiwanda cha saruji Cha dangote.
Waziri wa Nishati na madini Dr Medard Kelamani akiongea na Mkurugenzi wa kiwanda cha Dangote Alhaji Sada ladeubaki mara baada ya kutembelea ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha umeme utakaopelekwa katika kiwanda cha Dangote.

WAKULIMA MTWARA WA MLILIA JPM, WATAKA IUNDWE TUME YA UCHUNGUZI

$
0
0
Baadhi ya wanachama wa vyama vya Msingi vya ushirika wa Kilimo na Masoko katika wilaya Newala na Tandahimba Mkoani Mtwara wamemuomba Rais Dkt John Pombe Magufuli kuunda tume maalum ya kufanya uchunguzi juu ya Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU, ambacho hivi karibuni Naibu Waziri wa Kilimo Dakta Merry Mwanjelwa ametangaza kukigawa huku wanachama wake wakionekana kutoridhishwa na maamuzi hayo.

Katibu Mkuu wizara ya Habari Bi Suzan Mlawi azindua maandalizi ya Tamasha la Saba la 4CCP mjini Haydom mkoani Manyara

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi Bi Eliminata Awet Mratibu wa Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakiangalia nyumba ya wanyilamba wakati alipotembelea kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakitoka nje ya nyumba ya kabila ya Wanyiramba huku wakiongozwa na mzee Salum Shaban Mwakilishi wa wabantu na aliyekuwa akitoa maelezo kuhusu tamaduni za kabila hilo alipokuwa akiangalia nyumba ya kabila la Wanyiramba wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akiakiondoka mara baada ya kutembelea nyumba ya Wanyiramba na Wanyisanzu inazopatikana katika Kituo cha utamaduni cha 4CCP Haydom alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyeshwa picha mbalimbali zinazoonyesha matukio ya Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Bw. Edward Mashimba Mwenyekiti wa Kabila la Wahdzabe wakati akitoa maelezo kuhusu nyumba ya kabila hilo inayopatikana katika Kituo cha Utamaduni cha 4CCP Haydom wakati alipotembelea katika kituo hicho leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images