Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU ANATARAJIWA MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI KORAAN

0
0
Na Said Mwishehe,Blogu ya jamiii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya Afrika Mashariki ya kuhifadhi Koraan yanayotarajia kufanyika Uwanja wa  Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakati anazungumzia uwepo wa mashindano manne ya kuhifadhi Koraan ambayo yatafanyika kwa nyakati tofauti katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Sheikh Alhad amefafanua katika kipindi hiki cha Ramadhan katika Mkoa wa Dar es Salaam kutakuwa na mashindano manne ya kuhifadhi Koraan na kueleza Mei 20 mwaka huu yatafanyika mashindano ya kuhifadhi Koraan kwa Afrika Mashariki na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Majaliwa.

Mbali ya Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi pia anatarajiwa kuwepo Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu Mohammed Ghalib Bilal pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Al-Manahilul Islamic Centre.

Pia Mei 26 mwaka huu yatafanyika mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Koraan yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Suluhu Foundation yanayotarajia kufanyika Mnazi Mmoja jijini.Mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Hussein Mwinyi pamoja na viongozi wengine kadhaa.
Sheikh Alhad ameongeza Mei 27 mwaka huu yatafanyika mashindano yatakayohusisha Bara zima la Afrika na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Alhakim Foundation wakati Juni 3 mwaka huu yatafanyika mashindano mengine ya kimataifa yaliyoandaliwa na taasisi hiyo na mgeni rasmi bado haijafahamika atakuwa nani.

Amefafanua mashindano hayo yanafanyika mwezi wa Ramadhan ni kutokana na ubora wa mwezi huo kwani ndio Koraan Tukufu iliteremshwa na kufafanua kijana wa Kiislamu anayehifadhi Koraan husaidia kuishi kwenye misingi ya maadili mema kwani atakuwa anajua nzuri na baya.

Halotel yazindua duka jipya na la kisasa kwa wateja wao Mikocheni Shoppers Plaza,Kinondoni jijin Dar.

0
0


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Duka jipya na la kisasa la Halotel lililoko Kinondoni, Shoppers Plaza – Mikocheni, ambalo litawawezesha wateja wa Mtandao huo walioko maeneo ya Mikocheni, Msasani na maeneo jirani na hayo kupata huduma mbalimbali kama kusajili laini mpya, huduma za kifedha,kurejesha namba iliyopotea,vifaa vya mawasiliano na huduma nyingine nyingi kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

002: Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Duka jipya na la kisasa la Halotel lililoko Kionondoni, Shoppers Plaza – Mikocheni, ambalo litawawezesha wateja wa Mtandao huo walioko maeneo ya Mikocheni, Msasani na maeneo jirani na hayo kupata huduma mbalimbali kama kusajili laini mpya, huduma za kifedha,kurejesha namba iliyopotea,vifaa vya mawasiliano na huduma nyingine nyingi kwa urahisi na kwa gharama nafuu
Burudani ikitolewa mara baada ya uzinduzi wa duka hilo jipya na la kisasa la Halotel lililopo Kionondoni, Shoppers Plaza – Mikocheni,jijini Dar

MAOFISA KILIMO WOTE KIGOMA WATAKIWA KUHAMIA VIJIJINI KUWASAIDIA WAKULIMA

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

WAKULIMA wa zao la pamba wilayani Kakonko mkoani Kigoma wametakiwa kuwaepuka wanunuzi ambao hawatambuliki kisheria ili kuepukana na usumbufu wakati wa kuuza pamba zao huku Mkuu wa Mkoa huo akiwaagiza maofisa kilimo wote kuhamia vijijini kwa lengo la kutoa elimu kwa wakulima.

Kauli hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Kanyonza Wilaya ya Kakonko, na Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kigoma Joseph Lubuye wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa zao la pamba mkoani Kigoma.

Uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Kanyonza ambayo inaongoza kwa kilimo hicho katika Mkoa huo ambapo amewataka wakulima kuuza pamba yao katika kikundi cha ushirika na kampuni iliyopewa dhamana na Serikali ya kununua zao hilo.

Lubuye amesema kampuni itakayohusika na uuzaji na ununuzi wa pamba ni kampuni ya Kahama Cotton Campany Limited(KCCL) itakayoshirikiana na Chama cha Ushirika, lengo ikiwa ni kuhakikisha mkulima haibiwi na pamba inayouza na kununuliwa ni yenye ubora wa hali ya juu na kuepusha migogoro.

Amesema kwa mwaka huu pamba itauzwa kwa Sh.1,100 kwa kilo na kuwaomba wakulima kutumia nguo katika kubebea pamba na kusisitiza mkulima yeyote atakaeweka mchanga au maji kwenye pamba ili kuongeza uzito ataadhibiwa. Pia amewaomba wakulima kuwa wavumilivu kwani mwakani watapatiwa pembejeo za kilimo bure na viuwatilifu.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewataka maofisa kilimo wote kuhamia vijijini kwa msimu huu wa uuzwaji wa pamba na msimu wote wa kilimo maofisa kilimo wote wanatakiwa kuondoka mjini na kuhamia vijijini kuwafundisha wakulima kulima mazao yenye ubora.

" Niwaagiza maofisa kilimo msimu wote huu wa uuzwaji wa pamba mje huku kukaa na wananchi, mtoe maelekezo watakacho kula wananchi na nyie mtakula hicho hicho kwani wananchi hawa ndio waajiri wetu.Mkoa wa Kigoma hatuhitaji matabaka ya watu ya wenye nacho na wasio nacho,"amesema na kuongeza 

"Lazima tuhakikishe tunaunga mkono juhudi za wananchi kuweza kuinua uchumi wa wananchi na kipato kwa wakulima.
 Sehemu ye shamba la pamba
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bregedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga  akizungmza mbele ya Wananchi wakati wa wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa zao la pamba mkoani Kigoma.
 Baadhi ya Wananchi wa  Kijiji cha Kanyonza Wilaya ya Kakonko wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa Uzinduzi huo. 

Sethi apinga kuenguliwa IPTL,akanusha taarifa zinazosambazwa mtandaoni

0
0
Mkurugenzi na Mmilikiwa kampuni ya PAP/IPTL ,Harbinder Sing Sethi amekanusha taarifa zinazosambzwa mitandao kuwa amefutwa kuwa Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.

Hayo yameelezwa jana na Mwanasheria wa mmiliki wa Kampuni ya PAP/IPTL, Harbinder Sing Sethi, Hajra Mungula, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mteja wake na kusema Sethi bado Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.

Wakili Mungula amesema kuwa watanzania kupuuza kwa taarifa zilizotolewa awali na watu wanaojiita kuwa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo.atika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wakili Hajra Mungula imesema kuwa yeye kama mwanasheria wa Sethi, amewasiliana na mteja wake, ambaye yuko rumande na kushangazwa na taarifa hizo.

Ilisema hivi karibuni kumeripotiwa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kampuni inayomilikiwa na Harbinder Sing Sethi imebadilisha uongozi katika ngazi za Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Mkurugenzi mtendaji wake.

"Taarifa iliyosambazwa na anayejiita mwenyekiti wa bodi mpya, Ambroce Brixio imemtaja yeye kuwa na cheo hicho na Joseph Makandege kuwa Mkurugenzi wake ambaye kwa miezi kadhaa sasa hajawahi kuonana nae ikiwemo hata kutofika mahakamani siku ambazo kesi imekuwa ikitajwa" imesema sehemeu ya taarifa hiyo.Wakili Hajra, aliandika katika taarifa hiyo kuwa taarifa hizo zimemfikia kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti halali na mmiliki wa kampuni hii ya kuzalisha umeme ya IPTL ambayo kimsingi inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan Africa Power Solutions(PAP).

Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria huyo, pamoja na kuagiza wanasheria wake kuchukua hatua za haraka za kisheria mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote juu ya mabadiliko hayo."Mwenyekiti Seth anapenda kuutaarifu umma kupitia sisi kwamba wazipuuze taarifa hizo kwa kuwa hazitokani na mamlaka halali za kisheria za kampuni hiyo," ilisema mwanasheria huyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA KAMATI YA MAAFA YA MKOA

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
 

serikali mkoani Kilimanjaro imezindua kamati ya Maafa ya mkoa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria namba 7 ya mwaka 2015 kwa lengo la kumshauri Mkuu wa mkoa kuhusu masuala ya usimamizi wa maafa na kuratibu shughuli za dharura miongoni mwa taasisi za kisekta za serikali za mitaa.



Mbali na majukumu hayo kamati hiyo pia itakuwa na wajibu wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika mkoa,kufungamanisha mfumo wa tahadhari ya awali katika mkoa na kuwezesha uanzishaji wa mfumo wa takwimu na taarifa za maafa za mkoa kwa kushirikiana na wakala.



Akizindua kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini,wafanyabiashara ,Wataalamu mbalimbali pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalma ya mkoa ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira alisema kwa kipindi kirefu mkoa haujawa na kamati ya maafa iliyo hai ,inayojitambua na kuwajibika ipasavyo.



“Sheria hii inatafsriri maafa kwamba ni ya kimkoa kama zaidi ya wilaya moja ndani ya mkoa imeathirika au kama wilaya,mji au manispaa husika haina uwezo wa kushughulikia tatizo hilo au kama tatizo hilolimehusisha wilaya zinazopakana ndani ya mkoa “alisema Mghwira.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kamati ya Maafa ya mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika ukumbi Mdogo wa ofisi ya Mkoa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akiitoa katika uzinduzi rasmi wa kamati hiyo.
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour akizungumza wakati wa kikao hicho.
Wakuu wa wilaya za Siha,Onesmo Buswelu(kushoto)  ,Wilaya ya Same Rosemery Senyamule(katikati)  na Aron Mbogho wa wilaya ya Mwanga wakiwa katika kikao hicho ambao wao pia ni wajumbe  
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa kamati ya maafa ya mkoa huo.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AKUTANA NA KIKUNDI CHA KITAIFA CHA MASUALA YA JINSIA KATIKA SERA, MIPANGO, MIKAKATI, PROGRAMU NA BAJETI

0
0
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akizungumza katika kikao baina yake na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa katika Sekta mbalimbali. Kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Masuala ya Kisera UN Women nchini Bi. Usu Mallya.
  Mshauri Mwandamizi wa Masuala ya Kisera UN Women nchini Bi. Usu Mallya akielezea Mipango ya masuala mbalimbali ya kuwawezesha wanawake kiuchumi katika kikao baina ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa katika sekta mbalimbali. Kulia ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga.
 Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Maendeleo ya Jinsia  Bi. Mwajuma Magwiza (kulia) akielezea jinsi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa mwaka 2018 yalivyofanyika na kuwashuruku wadau kwa kuwezesha kufanikisha maadhimisho hayo katika kikao kilichowakutanisha Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga alipokutana na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam.
 Mwezeshaji wa Masuala ya Jinsia Dkt. Linda Mhando(kulia) akielezea masuala mbalimbali aliyoyapata katika utafiti alioufanya kuhusu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jinsia ya Mwaka (2000) na ushauri wake kuhusu maboresho ya Sera hiyo wakati wa kikao kati ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga na kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa jijini Dar es Salaam.

Baadhi wajumbe wa kikundi cha uingizaji wa masuala ya jinsia katika Sera, Mipango, Mikakati, Programu na Bajeti za kitaifa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasiliwa katika kikao kati yao na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga Jijini Dar es Salaam.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

LAAC YA UGANDA ZIARANI DODOMA, YAFURAHIA MJI WA SERIKALI

0
0

Na Ramadhani Juma
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ya Bunge la Uganda wameishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kwa kuipatia Serikali ya Nchi hiyo kiwanja chenye ukubwa wa eka tano katika Kata ya Mtumba eneo utakapojengwa Mji wa Serikali.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Reagan Okumu alitoa Shukrani hizo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma walipokuwa katika ziara ya siku moja ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama Dampo la kisasa la kuhifadhia taka kwa kuzifukia ardhini (Sanitary Land Fill) lililopo Kata ya Matumbulu ambalo ni moja ya miradi mikubwa katika eneo la usafi na utunzaji wa mazingira. 
Awali akizungumza mbele ya Kamati hiyo, Mhandisi wa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godwin Kunambi, aliwajulisha wajumbe hao kuwa, Halmashauri imetenga na kupima eneo litakalojengwa Mji wa Serikali hapa Dodoma na kwamba Serikali ya Uganda imepewa kiwanja chenye ukubwa wa eka tano kwa ajili ya matumizi ya kiofisi, ambapo pia walioneshwa ramani ya eneo hilo. 
Wajumbe wa Kamati hiyo waliezea kufurahishwa kwao na hatua hiyo huku wakiahidi kufikisha taarifa hizo njema kwa Wananchi wa Uganda mara watakaporejea Nchini humo. 
 Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Manispaa ya Dodoma Mhandisi Emanuel Manyanga akiwasilisha taarifa ya Miradi iliyotekelezwa na itakayotekelezwa kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati Tanzanzia (TSCP) mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa ya Nchini Uganda ilipokuwa katika ziara ya kujifunza katika Manispaa hiyo. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa ya Nchini Uganda Reagan Okumu (kushoto) akizungumza wakati alipowaongoza wajumbe wa Kamati hiyo katika ziara ya kujifunza katika Manispaa ya Dodoma.
 Mhandisi wa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Barnabas Faida akitoa neno la utangulizi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesbu za Srikali za Mitaa ya Uganda ilipotembelea Halmashauri hiyo.
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ya Bunge la Uganda wakifuatilia taarifa za miradi ya Ujenzi iliyokuwa akiwasilishwa na Mhandisi Emanuel Manyanga kutoka Idara ya Ujenzi ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma walipofanya ziara ya kujifunza juu ya utekelezaji wa miradi ya Kimkakati. 

Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China

0
0
Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Ujenzi ya Nchini China ya Civil Engineering Construction Corporation 'CCECC' Bw. Zhuang  Shangbiao alisema hatua iliyochukua  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  'SMZ' ya kuipa kazi ya ujenzi wa barabara Nchini imeleta heshima kubwa na ya kipekee kwa Kampuni hiyo.

Alisema kazi iliyo mbele kwa uongozi na wahandisi wa kampuni hiyo hivi sasa ni kujipanga vyema katika kuhakikisha heshima waliyopewa na SMZ wanailinda katika kuwajibika ipasavyo  wakati wa utekelezaji wa jukumu hilo zito katika misingi ya ari na bidii kubwa.

Bwana Zhuang  Shangbiao akiuongoza Ujumbe wa Viongozi saba wa Taasisi hiyo ya Civil Engineering Construction Corporation alisema hayo wakati akitoa shukrani katika mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema uzowefu wa ujenzi iliyokuwa nayo Kampuni hiyo ya CCECC kwa zaidi ya Miaka 50 iliyopita inahamishiwa Zanzibar  katika ujenzi wa barabara inayoanzia Bububu, Mahonda  kupitia  Kinyasini hadi Mkokotoni yenye urefu wa Kilomita 31.

Bwana Zhuang alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wahandisi wa Ujenzi wa Kampuni ya CCECC watakamilisha kazi hiyo kwa wakati ulliopangwa na katika kiwango kinachokubalika Kimataifa kwa vile wana utaalamu na uzoefu wa kutosha.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya Civil Engineering Construction Corporation 'CCECC' ya China Bw. Zuang Shangbiao Vuga Mjini Zanzibar.
 Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Bw. Zuang Shangbiao wa tatu kutoka Kulia akielezea shukrani zake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kuiamini Kampuni yake kujenga Bara bara ya Bububu hadi Mkokotoni kupitia Mahonda na Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.  Mohamed Aboud Mohamed.
  Balozi Seif kushoto akisifu umahiri wa Kampuni za Kichina zinazofanya kazi Nchini Tanzania wakati akibadilishana mawazo na Rais wa Kampuni ya CCECC Bw. Zhuang Shangbiao aliyekaa upande wa Kushoto.
 Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CCECC ya China Bw. Zuang Shangbiao Kushoto akimkabidhi zawadi ya picha ya Ukuta Mkuu wa China 'Great Wall' Balozi Seif mara baada ya mazungumzo yao.
 Bwana Zuang Shangbiao Kushoto akifurahia zawadi ya  viungo aliyokabidhiwa na Balozi Seif baada ya mazungumzo yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA

USHAHIDI KESI MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUSIKILIZWA JUNI 8

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

USHAHIDI dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando  utaendelea kusikikizwa Juni 8,mwaka huu.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa iendelee kusikilizwa kwa shahidi wa nne wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao, imeahirishwa sababu shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi Katika kesi hiyo anaudhuru.

Hayo yameelezwa na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai,  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu , Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 mwaka huu ambao mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu  wamekwishatoa ushahidi wao ambao ni Afisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887. 
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, 2008,   akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido aliyekuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20, 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11, 2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Katika shtaka la nne, anadaiwa kuwa  Novemba 16, 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Katika shtaka la mwisho,  anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 akiwa UAE, Tido aliisababishia TBCli hasara ya Sh.887,122,219.19.

MAMA JANETH MAGUFULI ATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WAFUNGWA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKO GEREZA LA SEGEREA

0
0
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea kabla ya kukabidhi vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. Wanaomsikilia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widson Mandarasi Mwanangwe. Msaada huo ni pamoja na tani 4.8 za mchele, tani 4.8 za Unga wa mahindi, tani 2.8 za sukari pamoja na tende
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. wanaoshuhudia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widson Mandarasi Mwanangwe. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsikiliza Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga akishukuru baada ya kumkabidhi vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. wanaoshuhudia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widsob Mandarasi Mwanangwe. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga na askari wengine waliofika kupokea vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana  na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga baada ya kukabidhi  vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018. 


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea na  Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza Gaston Kalam Sanga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje na Mkuu wa Gereza la segerea Kamishna Msaidizi wa Magereza Widsob Mandarasi Mwanangwe,  baada ya kumkabidhi vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018.  
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na asklari wanawake waliofika kupokea vyakula kwa ajili ya wafungwa wanawake na watoto waliko katika gereza la Segerea jijini Dar es salaam katika haflka fupi iliyofanyika ofisini kwake leo Mei 18, 2018.  
Picha na IKULU  

BENKI YA CRDB YAENDESHA SEMINA YA SIKU MOJA KWA WANAHISA WAKE, JIJINI ARUSHA LEO

0
0
Benki ya CRDB leo imeendesha semina ya siku moja kwa Wanahisa wake, ili kuwajengea uwezo katika maswala ya Usimamizi wa Uwekezaji katika Hisa, Usimamizi wa Miradhi pamoja na Mabadiliko ya Sekta ya Kifedha na Athari za Sarafu za Digitali. Semina hiyo, imefanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay akizunguza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa Wanahisa wa Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akifafanua jambo wa Wanahisa wa Benki hiyo, katika semina ya siku moja, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.
Mkufunzi na Mtaalam wa maswala ya Hisa kutoka REPOA, Dkt. Blandina Kilama akisisitiza jambo katika semina ya siku moja wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, wakati akiwasilisha mada yake iliyohusu Usimamizi wa Uwekezaji katika Hisa, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.

Grace Joachim kutoka Joachim and Jacobs, akiwasilisha mada ya Usimamizi wa Miradhi katika semina ya siku moja ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.
Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru akieleza jambo katika semina ya siku moja ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.
Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard Jensen akifatilia semina ya wanahisa wa Benki ya CRDB, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha leo Mei 18, 2018.

Hospitali ya Dodoma yapewa miezi 8 kujenga mtambo wa kuteketeza taka

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira nchini.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake Mhe. Lugola ametembelea Ofisi za Jiji na kupokea taarifa ya hali ya mazingira katika usimamizi wa Taka ngumu, taka za maji pamoja na madini ujenzi.
Akitoa taarifa ya Jiji Mkurugenzi Bw. Godwin Kunambi amesema kuwa Ofisi yake imepanga kujenga mabwawa makubwa ya maji taka katika eneo la Nzuguni na ujenzi wake uko mbioni kuanza.
Akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi  Dkt. Carolyne Damian amemueleza Naibu Waziri kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya mtambo wa kuteketezea taka.
Akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dodoma kuhakikisha changamoto hiyo ya mtambo wakuteketeza taka unapatiwa ufumbuzi mapema ili kuhifadhi mazingira.
Aidha, Mhe. Lugola ametoa muda miezi nane kwa uongozi wa Hospitali hiyo  kuhakikisha mfumo wa matumizi ya kuni kama nishati ya kupikia unasitishwa na kuwataka watumie gesi ili kuhifadhi mazingira. 
Ziara ya Naibu Waziri katika Jiji la Dodoma inaendelea kwa kutembelea machinjio ya Punda Kizota na Mamchimbo ya Mchanga na Kokoto - Chogongwe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akiwa na uongozi wa Hospitali ya Mkoa Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kikazi hospitalini hapo kukagua masuala ya taka ngumu na taka za maji na kuona uteketezaji wake. 
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akitoa maelezo kwa Bw. Carle Lyimo Afisa Afya Mkuu wa Jiji la Dodoma wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
Mtambo wa kuteketeza taka ulipo katika Hospitali ya Dodoma ambao miundominu yake kwa sasa haukidhi mahitaji. Waziri Lugola autaka uongozi wa hospitali hiyo kuweka kipaumbele ujenzi wa mtambo huo mapema.

AQRB YATAKIWA KUJITANGAZA - MAJALIWA

0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezungumzia juu ya umuhimu wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kutangaza huduma wanazotoa za ujenzi ili kuwawezesha wananchi kuelewa na kuzitumia huduma hizo na hivyo kuboresha Sekta ya Ujenzi hapa nchini.
Akifungua semina ya siku mbili ya maadhimisho ya ishirini na tisa ya elimu endelevu kwa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi jijini Dodoma, Waziri Mkuu amewataka wataalam hao kujiendeleza kitaaluma ili watoe huduma bora zaidi zinazouwiana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
‘Ongezeni wigo wa huduma zenu ndani na nje ya nchi ili huduma za ujenzi bora wa makazi katika miji na majini ziwe endelevu na zenye gharama stahiki”, amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu ameisisitiza bodi ya AQRB kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi na mafunzo ya ujenzi ili kuongeza idadi ya wanataaluma wanaoweza kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Aidha, amehimiza Wizara ya Ujenzi kushirikiana na Wizara ya Afya na Tamisemi katika ujenzi wa vituo vya afya vya kisasa katika mikoa na halmashauri mbalimbali nchini.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine 10 za kufyatulia matofali zilizotolewa na Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kabla ya kufungua semina ya 29 ya wataalam hao, Mkoani Dodoma. Wa tatu kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa mwaka  wa 4 wa kozi ya Usanifu Majengo, Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Mwita Mgaya, kuhusu ujenzi wa kisasa wa majengo wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea banda  la chuo hicho kabla ya kufungua semina ya 29 ya wataalam hao, Mkoani Dodoma, kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
 Wajumbe wa Semina ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani), wakati akifungua mkutano huo wa siku 2 uliowakutanisha wataalam kujadili Mustakabali wa Viwanda nchini na namna ya kutunza majengo ya kale mkoani Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akifungua semina ya 29 ya Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Mkoani Dodoma, wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi baada ya kufungua semina ya 29 ya wataalam hao, Mkoani Dodoma. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Ubalozi Kuwait wakabidhi kisima cha maji nambari 63 katika Chuo cha Ufundi cha Yombo kwa wanafunzi walemavu

0
0
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem hivi karibuni alizindua kisima cha maji safi na salama nambari 63 katika Chuo cha Ufundi cha Yombo kwa wanafunzi walemavu kilichopo Jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ambao ulishuhudiwa na mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Josephine Lyungi, Kaimu Mkuu wa Chuo, Bi. Maryam, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiwalani, Emannuel pamoja na walimu na wanafunzi. 

Huu ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait unaofahamika kwa jina la “KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE”. Katika hotuba fupi iliyotolewa na Balozi Najeem,  alisema kuwa uzinduzi wa kisima hicho ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mnamo tarehe Novemba 30, 2017 Chuoni hapo wakati wa uzinduzi wa "Mpango kamili wa kuwasaidia walemavu nchini Tanzania" wenye thamani ya dola laki tano kutoka Serikali ya Kuwait akiwa pamoja na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mhe.  Jenista Mhagama ambaye alimuomba Balozi ajenge kisima kituoni hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo, Bi. Maryam ameushukuru Ubalozi wa Kuwait kwa kuwajengea kisima ambacho kitawasaidia wanafunzi katika kufua, kuoga na kufanya usafi madarasani, mabwenini na maeneo mengine ya Chuo

Pembezoni mwa uzinduzi wa kisima cha maji, Al-Najem alitembea sehemu ya kujifunzia ushoni chuoni hapo kwa wanafunzi wenye ulemavu ambapo Ubalozi uliwahi kuchangia vyarahani katika ziara yake ya kwanza, na mara hii aliahidi kukipatia chuo hicho vitambaa na vifaa vyengine vinavyohitajika katika ushoni.
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akishuhudia wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Yombo, wakiteka maji katika kisima alichokizindua hivi karibuni.
 Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Yombo wakiendela na mafunzo yao wakati, Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem alipowatembela.

WASHINDI WA TIGO NYAKA NYAKA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

0
0
 Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Gladys Mtandila kutoka Makumbusho, Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promoshen hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00#  
 eneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Ramadhan Ali  Ngolozi kutoka Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# .
 Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi simu janja aina ya TECNO R6 4G kwa Sakina Kassanga, askari polisi kutoka Dar es Salaam aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 1,080 wa simu katika promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo pia ilitoa bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wateja wake wlaionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00#  
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni iliyoisha jana ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kupitia promosheni hiyo, Tigo ilitoa simu janja 1,080 kwa wateja wake, pamoja na bonasi nono za hadi GB 1 intaneti kwa wote walionunua bando za intaneti kupitia menu *147*00# .

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO MPAKA KATI YA MANYARA NA TANGA

0
0
Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Serikali yamaliza mgogoro wa mpaka kati ya mkoa wa Manyara na Tanga katika wilaya za Kiteto na Kilindi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi ambaye amesema moja ya sababu kubwa za kuwepo kwa mgogoro huo ni baadhi ya wapimaji mipaka waliokuwepo wakati huo kuhongwa na kupindisha mpaka.

Mgogoro huu uliwasilishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati alipofanya ziara yake mwezi januari mwaka 2017 ambapo wananchi walifikisha malalamiko ya mgogoro huo ambao umegharimu maisha ya watu wengi na mauaji ya mara kwa mara.

Waziri Mkuu alimtaka wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushirikiana na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuunda timu ya wataalamu ambao walianza kazi ya upimaji mwezi Machi 2017 ambao walipima mpaka huo kwa usahihi japo na wao walitaka kuhongwa pesa kutoka kwa baadhi ya watu hata hivyo walizikataa.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiongea na wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wakati akiwatangazia kuhusu Serikali kumaliza mgogoro wa mpaka wa wilaya hizo mbili.
   Eneo la mpaka wa Kiteto na Kilindi ambalo lilikuwa na mgogoro
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akisalimiana na wakazi wa wilaya za Kiteto na Kilindi wenyenyuso za furaha mara baada ya kumalizika kwa mgogoro huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo akisalimiana na wakazi wa wilaya za Kiteto na Kilindi wenyenyuso za furaha mara baada ya kumalizika kwa mgogoro huo.
  Baadhi ya wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wa utatuzi wa mgogoro kati ya wilaya hizo wakifuatilia kwa makini maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huo.
 wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi waliohudhuria katika mkutano wa utatuzi wa mgogoro kati ya wilaya hizo wakifuatilia kwa makini maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huo.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC MJEMA AFUNGUA MAONESHO YA WAJASILIAMALI YA WANAWAKE NA VIJANA JIJINI DAR

WAHITIMU WA ELIMU YA JUU NA VYUO VYA UFUNDI KUNUFAIKA NA MWONGOZO WA SERA YA MAFUNZO KWA VITENDO KAZINI

Serikali Yaandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Mafunzo kwa vitendo kwa Wahitimu wa Vyuo

0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali imeandaa mwongozo wa Kitaifa wa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa vyuo ili kuondoa pengo la ujuzi linalohitajika katika soko la ajira hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Zainab Athuman Katimba  juu ya Serikali haioni haja ya kutungwa sera ya mafunzo kwa vitendo kazini kwa wahitimu wa Elimu ya Juu na Vyuo vya Ufundi (Internship Policy for Higher Learning Institutions and Technical Colleges Graduates) ili vijana waweze kupata ujuzi utakaoendana na mahitaji ya soko la ajira.

"Katika kuhakikisha pengo la ujuzi (skills gap/skills mismatch) kati ya ujuzi walionao wahitimu na ule unaohitajika katika soko la ajira, ni kweli Serikali imeona kuna haja ya kuwa na miongozo ya kisera ambapo kupitia Ofisi yangu tumeandaa mwongozo wa Kitaifa wa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu (National Internship Guideline)," amesema Mhe. Mavunde.

Ameendelea kusema kuwa mwongozo huo ulizinduliwa rasmi Septemba, 2017 na kuanza kutumika rasmi ambapo katika mwaka wa fedha 2017/2018 zaidi ya nafasi 750 zimetolewa na waajiri mbalimbali kuwezesha wahitimu kufanya mafunzo.

Aidha amesema, Serikali inafanya marekebisho ya Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 ili kuendana na mahitaji ya sasa ambapo sera mpya pamoja na mkakati wa utekelezaji wake iko katika hatua za mwisho na inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni mwaka huu.

"Miongoni mwa matamko mahususi ya sera hii ni pamoja na kusisitiza kuwepo kwa mafunzo kwa vitendo kazini kwa wahitimu wa vyuo. Baada ya kupitishwa sera hii, suala la mafunzo ya vitendo kazini kwa wahitimu litawekwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004.

Hata hivyo, Mhe. Mavunde ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa programu ya mafunzo kazini kwa wahitimu kwa kutoa fursa kwa vijana wahitimu kujifunza katika maeneo yao ya kazi.

BALOZI JUMA MWAPACHU ASHAURI MABADILIKO SEKTA YA ELIMU NCHINI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MWANADIPLOMASIA wa siku nyingi nchini, Balozi Juma Mwapachu ameshauri mfumo wa elimu uliopo nchini ufanyiwe mabadiliko ikiwemo kuongeza vyuo vya ufundishaji walimu  kwa lengo la kukuza kiwango cha elimu kinachotolewa nchini.

Balozi Mwapachu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha pili kiitwacho ‘ Tanzania in the Age Of Change And Transformation’ na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wastaafu, waadhiri, majaji wastaafu, wanadiplomasia na wasomi kada mbalimbali.

Balozi Mwapachu amesema pamoja na juhudi  zinazoendelea kufanywa na Serikali kuboresha elimu nchini, bado kuna changamoto nyingi  katika elimu hiyo ambayo kwa kiasi fulani inakwamisha mipango mizuri ya baadae.

“Hakuna ubishi kuwa elimu ndiyo msingi  kwa Taifa lolote, hivyo ili kupiga hatua ipo haja ya kutafuta mapinduzi katika elimu yetu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo vikuu…hili zaidi ni kwa kuangalia mfumo wa ufundishaji wa vyuo vya kufundishia walimu,"amefafanua  Balozi Mwapachu.

Amesema uwepo wa idadi ndogo ya vyuo vinavyozalisha walimu hao ni sababu kubwa inayochangia kushuka kwa kiwango hicho cha elimu kinachotolewa nchini  katika ngazi zote kuanzia elimu ya awali hadi  chuo kikuu, jambo alilosema kuwa  ni vyema likafanyiwa mabadiliko mapema ili kuzalisha wanafunzi wenye tija.

Aidha katika hatua nyingine Balozi Mwapachu alizungumzia sekta binafsi kwa kusema kuwa pamoja na muendelezo mzuri unaofanywa na Serikali hususani katika uendelezaji wa kilimo,kuna haja ya kuongezwa kwa jitihada ili kuwaa na tija zaidi. 

“Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kulipa msukumo suala la uendelezaji kilimo na viwanda, na zaidi kwa namna ambavyo Serikali ilivyowekeza katika mapinduzi ya viwanda kuelekea uchumi wa kati wa viwanda ifikapo Mwaka 2020,” amesema Balozi Mwapachu.

Pia amesema bado hali siyo nzuri kwa mahusiano ya wafanyabiashara na Serikali kutokana na kutokuwepo kwa mahusiano mazuri siku za nyuma, tofauti na sasa ambapo mabadiliko yameanza kuonekana.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu hicho Profesa Mark Mwandosya, mbali na kumpongeza Mwapachu kwa kuzindua kitabu hicho, alisema  kuna umuhimu wa watanzania kuwa na utamaduni wa kuandika vitabu katika masuala mbalimbali kwa kuwa vinabeba kumbukumbu ya miaka mingi.

Amesema kila kitu kina misingi yake, na kwamba hakuna kinachoweza kusahaulika kirahisi kama vitabu, bila kujali kuwa maandiko hayo ni mazuri au mabaya kwa kuwa maandiko mabaya hupata fursa ya kuboreshwa.
 Balozi Juma Mwapachu akiwa na mkewe Rose Mwapachu wakiwa wameshika kitabu kinachofahamika Tanzania in the Age Of Change and Transformation jana jijini Dar es Salaam baada ya kukizindua.Wengine wanaoshuhudia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk.Reginald Mengi(kulia) na upande wa kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo Profesa Mark Mwandosya akiwa na mkewe.
Mgeni rasmi Profesa Mark Mwandosya akizindua kitabu cha Tanzania in the Age Of Change and Transformation jana Dar es Salaam ambacho mtunzi wake ni Balozi Juma Mwapachu. Aliyeshika kitabu hicho ni qmkewe Balozi Mwapachu, Rose Mwapachu wakati kutoka kushoto ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk.Reginald Mengi na Balozi Juma Mwapachu
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitabu hicho Prof.  Mark Mwandosya akichukua kitabu kabla kukizindua rasmi.Wanaoshuhudia ni Balozi Juma Mwapachu na mkewe Rose Mwapachu pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi .
 Mgeni rasmi Prof. Mark Mwandosya akichukua kitabu kabla kukizindua rasmi.Wanaoshuhudia ni Balozi Juma Mwapachu na mkewe Rose Mwapachu pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk.Reginald Mengi .
 Balozi Juma Mwapachu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha  Tanzania in the Age of Change and Transformation jijini Dar es Salaam
Mgeni Profesa Mark Mwandosya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho jana jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images