Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

IGP Afanya Uteuzi wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai


Waziri Kairuki afanya ziara ya kutembelea GST

$
0
0
Mtalaam wa upimaji miamba kwa njia ya umeme, Octivian Minja wa Taasisi ya jiolojia na utafiti madini (GST) mwenye shati jekundu akimuelezea Waziri wa Madini, Angella Kairuki juu ya upimaji wa miamba kwa njia ya umeme kwa lengo la kujua aina ya usumaku uliopo katika miamba, waziri Kairuki tarehe 16 Mei 2018, alifanya ziara ya kutembelea GST ili kuangalia kazi mbalimbali zifanywazo na taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisis ya Jiolojia na Utafiti Madini (GST) Prof. Abdukarim Mruma alikimuelezea waziri wa Madini, Angella Kairuki juu madini ya Ulanga , alipotembea katika jumba la makumbusho ya miamba na madini iliyopo GST.
Waziri wa Madini, Angella Jasmine Kairuki pamoja na Manaibu waziri wa wizara hiyo, Dotto Biteko na Stanslaus Nyongo , na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ,wakielekea katika ofisi nyingine kwa ajili ya kutembelea baada ya kupata maelezo juu ya uchunguzi , upimaji wa miamba kutoka kwa watalaam wa Idara ya Jiofikia na Jiolojia jana tarehe 16 Mei 2018 , viongozi hao walifanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa Madini kwa lengo la kuona kazi mbalimbali zifanywazo na taasisi hiyo.

Dodoma Builders Expo 2018

$
0
0
On the 26th of April 2018 the residents of Dodoma had their breakfast in the Municipality of Dodoma and little did they know that they will enjoy their lunch in the City of Dodoma on the same day. Dodoma is now a city and there is no doubt about that. The President declared so. 

A few days later during a press conference the City Director Mr. Godwin Kunambi was speaking and hesaid something intriguing,he said “if you want to strike a fortune in Dodoma it is either you invest in the food industry or in the construction industry.” 

The latter is what this e-mail is about, we will talk about food the other day. If you have notalready heard, A.FM Radio (Dodoma) and Tanzania Standard Newspapers (Daily News and Habari Leo) under the stewardship of the office of regional commissioner of Dodoma are organizing the first ever builders’ expo for Dodoma to be held on the 23rd and 24th of June 2018 at Jamhuri Stadium. 

This is going to be a massive exhibition ever to be held in Dodoma and if you are in the construction industry this platform will make it easier for you because you will be able: 
I. Find new Buyers / Distributors in Dodoma & central zone at large for your products 
II. Establish / Promote Brand Name & Image 
III. Update Existing Customers / Agents 
IV. Launch New Products/Services 
V. Give Special offers & Promotions and so much more.

This is not an opportunity not to miss. Spaces are limited and many investors are already interested, Book your space now:

For early registration, please follow this link http://www.afmradiotz.com/dodomaexpo/

Maria na Consolata Waruhusiwa Leo, Waishukuru Muhimbili

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imewaruhusu Maria na Consolata waliokuwa wamelezwa katika hispotali hiyo kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na afya zao kuimarika.

Pacha hao walikuwa wakipatiwa matibabu na madaktari bingwa wa Muhimbili na leo wamepelekwa Iringa ambako watapokelewa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa.Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema pacha hao wamesindikizwa na madaktari wa Muhimbili haid Iringa na kwamba wakiwa huo wataendelea kupatiwa matibabu.

 “Consolata na Maria tumewaruhusu leo. Hii ni baada ya madaktari kujiridhisha kwamba afya  zao zimeimarika. Wataalamu wetu wamewafanyia vipimo mbalimbali na pia tumewasiliana na wenzetu wa nje na tukakubaliana tuwaruhusu sasa,” amesema Prof. Museru.Prof. Museru amesema kwamba pacha hao wamepatiwa machine ya CPAP & Oxygen ambayo itawasaidia kuwapatia tiba endapo watahitaji wakati wakiwa Iringa.

Wakizungungumza kwa nyakati tofauti, Consolata amesema kwamba Muhimbili imewapatia huduma nzuri na wanawashukuru wataalamu mbalimbali waliokuwa wakiwapatia matibabu tangu walipolazwa.

Naye Maria akizungumza kwa furaha amesema hivi sasa anajisikia vizuri tofauli na awali-kabla ya kupelekwa katika hispotali hiyo kwa ajili ya matibabu. Pia, amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili kwa kuwapatia huduma bora za matibabu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na Maria na Consolata leo kabla ya kuanza safari ya kwenda Iringa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai na wengine ni wataalamu waliokuwa wakiwapatia matibabu pacha hao.
 Kulia ni machine ya CPAP & Oxygen ambayo Maria na Consolata wamepewa endapo watahitaji matibabu yanayotolewa kwa kutumia mashine hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwaaga Maria na Consolata leo.
Maria na Consolata wakisaidiwa kuingizwa kwenye gari ikiwa ni safari ya kuelekea Iringa leo. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

WAHAMASISHWA KULIPA YA KODI YA ARDHI MTWARA

$
0
0

NA   JOSEPH MPANGALA- MTWARA.

Wamiliki wa Viwanja na mashamba waliopo kanda ya kusini,Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara wametakiwa kulipa Kodi ya Ardhi pamoja na malimbikizo ya Yamadeni kwa mwaka wa fedha 20017/2018ili kuepuka usumbufu wakupelekwa mahakamani,Kunadiwa malizao au kufutiwa miliki ya ardhi zao. 

Kodi hii inatakiwa kulipwa kila tarehe 1Julai hadi mwezi disemba kila mwaka na ifikapo januari mosi ya kila mwaka kodi hii hulipwa pamoja na adhabu ambayo ni asilimi1 kwa kila mwezi wa kodi husika. 

Akiongea na waandishi wa habari ofisin za kanda ya kusini mkoani Mtwara Kamishna Msaidizi wa ardhi Kanda ya Kusini Gasper Luanda amesema wananchii woote wanaomiliki Viwanja na Mashamba kwenda ofisi za Halmashauri za Wilaya,Miji,manispaa pamoja na Ofisi za kanda kwa ajili ya kupata Makadirio ya Ankara za malipo. 

“Tangazo hili linamuhusu mtu yeyote mwenye kiwanja na aliyemilikishwa lakini hata Yule aliyemilikishwa na amejenga kwa hiyo kama una jengo lako kwenye kiwanja ulichopewa inamana utalipa kodi mbili,Utalipa kodi ya ardhi kwenye wizara ya ardhi lakini kwa kupitia mawakala wetu ambao ni Halmashauri lakini sasa hivi tunamawakala kupitia banki za NMB na CRDB lakini ya kodi ya pango la ardhi unakwenda kulipiwa TRA kwa hiyo wananchii wasichanganye hizi kodi mbili kila moja inasimamiwa na Sheria zake. 

Aidha Luanda ameongeza kuwa muitikio wa ulipaji kodi ya majengo,Vianja na mashamba katika kanda ya kusini umekuwa mkubwa kutokana na Makadirio waliopewa ya ukusanyaji kuendelea kuongezeka kila mwezi. 

“Muitikio ni Mzuri kama mnavyojua makusanyo ya kodi yanakwenda na malengo sisi kama kanda Tulipewa jukumu la kukusanya Kodi ya Billion7.86 kanda kwa maana mikoa yote ya Mtwara Lindi na Ruvuma sasa watu wamelipa na Tunakaribia sasa Billion saba na Kitu lakini sasa kuna pengo la million mia sita/mia saba hivi halijakusanywa ndio maana tupo hapa kuwahimiza wale wachache ambao wamebaki basi nao watimize wajibu wao kwa sasabu kulipa kodi ni Lazima sio Hiari” 

Kwa sasa Miggogoro katika Mkoa ya kanda ya kusini imeonekana kupingua kutokana na Kuweka Dawati la Migogo ambalo linasikiliza Migogoro ambapo kwa sasa wanaokuja kulalamika wamepunua kwa kiasi kikubwa. 
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper .V.Luanda akongea na waandishi wa habari kuhusiana na Uahamisishaji wa Ulipaji wa kodi kwa wamiliki wa Viwanja na mashamba katika kanda ya Kusini Mikoa ya Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper .V.Luanda wakifurahi jambo na Afisa Mipango miji Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkono Werema wakati wa kipindi cha Maswali na majibu na waandishi wa habari juu ya kodi kwa wamiliki wa Viawanja na mashamba Mkoani Mtwara

TUNAJIVUNIA KUWA NA MHE. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI- WAZIRI MPINA

Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza atembelea JNIA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (mwenye suti ya bluu kulia), leo akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Bw. Matthew Rycroft mara baada ya kukamilika kwa zoezi la mbwa wa polisi kuonesha namna wanavyokamata dawa za kulevyia na nyara za serikali katika mizigo ya abiria kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kulia) akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela baada ya zoezi la mbwa kuonesha namna wanavyobaini mizigo yenye nyara za serikali na dawa za kulevyia leo kiwanjani hapo.
Koplo Chesco Mbise akimwongoza mbwa anayeitwa Max-Z kuondoka mara baada ya zoezi la kuonesha namna anavyokamata dawa za kulevyia katika mizigo ya abiria kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo leo Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (hayupo pichani) alipotembelea na kuona zoezi hilo. Mbwa huyu ni kati ya wawili waliotolewa kwa msaada na serikali ya Marekani.
Askari Hadson Muhuma akiwa amemshika mbwa anayeitwa Nopi wakati akifanya zoezi la kutambua mizigo ya abiria yenye nyara za serikali zikiwemo pembe za Ndovu, lililofanyika leo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya kutembelewa na Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (hayupo pichani).
Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Bw. Matthew Rycroft (wapili kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa pili kulia) wakimsikiliza Bw. Matt Jenkins (aliyekaa), ambaye ni Afisa wa UK Border Force wa Kitengo cha dawa za kulevyia katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). (Picha zote na Bahati Mollel wa TAA).

AMBASSADOR JUMA MWAPACHU'S BOOK LAUNCH TODAY AT NEW AFRICA HOTEL IN DAR ES SALAAM


BENKI YA TPB Pls YAWEKA REKODI KIUTENDAJI, SASA MTAJI WAKE WAFIKIA SHILINGI BILIONI 60

$
0
0
*Ofisa Mtendaji Moshingi aipongeza Serikali kwa uamuzi wa benki hiyo kuunganishwa na Twiga Bancorp

Na  Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
BENKI ya TPB Pls imesema imeweka rekodi nzuri ya utendaji katika kipindi cha miaka 6 iliyopita ambapo hadi sasa mtaji wake umeongezeka kutoka Sh. bilioni 8 mwaka 2010 hadi kufikia zaidi ya Sh.bilioni 60. 

Imefafanua aidha  kwa mwaka 2017, benki ya TPB ilitoa gawio la zaidi ya Sh. bilioni moja kwa Serikali ambaye ndiye mwenye hisa nyingi. 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi wakati anatoa shukrani zake kwa Serikali kutokana na uamuzi wake wa kuamua kuiunganisha benki hiyo na pamoja na Benki ya Twiga Bancorp.

Akifafanua kuhusu benki hiyo amesema katika kuendelea kutekeleza majukumu yao benki ya TPB kwa mwaka 2017 ilipata faida kabla ya kodi ya Sh.bilioni 18.4 ikilinganishwa na faida ya Sh.bilioni 15.7 iliyopatikana mwaka 2016. 

Amesema matokeo hayo ya awali kwa robo ya kwanza ya mwaka 2018 inaonyesha mwaka huu faida inaweza kuongezeka zaidi ya kiwango cha mwaka jana.

"Tunatoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kutuamini benki ya TPB kwa kazi tunayofanya kwa raia wa Tanzania, na tunahaidi tunaongea ufanisi zaidi, na kuwafikia walengwa wote katika jamii yetu,"amesema.

Kuhusu benki hiyo kuunganishwa na benki ya Twiga Moshingi amesema Mei 17 mwaka huu Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa niaba ya Serikali, imeamua kuziunganisha benki hizo na kuunda benki madhubuti itakayojulikana kama benki ya TPB na kusisitiza kuunganishwa kwa benki hizi mbili kunatokana na kutetereka kwa mtaji wa benki ya Twiga. 

Moshingi amesema anaishukuru Serikali kwa kuiamini benki ya TPB pamoja na menejimenti yake, na kuamua kuziunganisha benki hizo ili kupata benki moja yenye nguvu na kuongeza ufanisi. 

Amesema kuunganishwa kwa benki hizo kunazaa benki moja imara ya TPB Bank Plc, ambapo wafanyakazi, wateja, amana pamoja na rasilimali zote zilizokuwa za Twiga Bancorp zitahamishwa kwenda TPB Bank Pc.

"Nachukua fursa hii kuwatoa hofu wateja wote waliokuwa na amana zao kwenye benki ya Twiga kuwa wasiwe na hofu kwani amana zao ziko salama kabisa, na wataendelea kupata huduma zote za kifedha kupitia kwenye matawi yao ya Twiga kwa muda, wakati taratibu zinafanyika ili kupata huduma hizo kwenye matawi yetu benki ya TPB mara baada ya taratibu ya kuunganishwa kwa mifumo ya benki hizi mbili utakapo kamilika,"amefafanua.

Moshingi ameongeza kuwa hata hivyo mashine za kutolea fedha za benki hizo mbili ziko kwenye mtandao mmoja na hivyo wateja wake wote wataendelea kupata huduma kama kawaida.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Pls Sabasaba Moshingi (kushoto) akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa shukrani  kwa Serikali kutokana na uamuzi wa kuinganisha benki hiyo na Benki ya Twiga Bancorp.Kulia ni Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa Benki ya TPB Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa Benki ya TPB Pls Jema Msuya(kushoto) akibadilisha mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Ofisa Mtendaji Mkuu wao Sabasaba Moshingi kumaliza kikao kati yake na waandishi wa habari ambacho kilikuwa na lengo la kutoa shukrani zao kwa Serikali kwa uamuzi wa kuiunganisha benki hiyo na Twiga Bancorp.

KUTOKA BUNGENI DODOMA: WAZIRI MKUU AKEMEA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea uharibifu wa makusudi ​wa miundombinu ya barabara na majengo unaofanywa na baadhi ya wananchi na kuwataka waache tabia hiyo mara moja.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Mei 17, 2018) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Bw. Kiswaga Destery aliyetaka kujua Serikali inachukua hatua gani dhidi ya wananchi wanaoharibu miundombinu ili wakauze kama vyuma chakavu kwa vile Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu hiyo.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatumia fedha nyingi sana kuboresha miundombinu mbalimbali nchini na kwamba kila Mtanzania anao wajibu wa kulinda miundombinu hiyo.

“Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya barabara na majengo ili kutolea huduma, Watanzania wote tunao wajibu wa kuilinda na endapo itatokea mtu anaihujumu miundombinu hii, Serikali hatuwezi kukaa kimya, lazima tutachukua hatua,” ameonya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo, Bungeni jijini Dodoma, Mei 17, 2018.

Amesema jukumu la ulinzi ni la Watanzania wote, na kila Mtanzania anayo dhamana ya ulinzi na usalama wa ndani ya nchi ikiwemo kuilinda miundombinu. “Juzi niliona kwenye televisheni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mheshimiwa Jaffo akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Shinyanga, wamekamata Fuso lililojazwa vyuma vilivyong’olewa kwenye barabara, ni vile ambavyo vinawekwa kwenye daraja na kingo za barabara,” amesema.

“Huu ni uharibifu ambao hatuwezi kuvumilia, na katika hili Watanzania lazima tuungane pamoja tukemee tabia hii. Tunatumia fedha nyingi kujenga kingo za barabara, kuashiria maeneo yenye hatari lakini Watanzania wengine wanakuja kung’oa kwa matumizi yao. Mimi naamini Mkoa wa Shinyanga utakuwa umechukua hatua kali dhidi yao,” amesema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo akizungumza na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule, Bungeni jijini Dodoma, Mei 17, 2018.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile, akijibu swali, Bungeni mjini Dodoma, Mei 17, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Madini, Angela Kairuki, Bungeni jijini Dodoma, Mei 17, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA UWEKEZAJI CHA JWTZ NA VIWANDA VYA MAJI NA USHONAJI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo  na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu alipowasili kuzindua kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu wakifunua pazia kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembela kwainda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za kijeshi zinazoshinwa na kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akinywa maji  yaliyotengenezwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpa maji ya UHURU PEAK  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,wakati wa sherehe za kuzindua kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na kutengeneza maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakipata picha ya kumbukumbu na watendaji wa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
Picha na IKULU 

Jumuia ya Kihindu Tanzania shilingi milioni 68 matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto wenye matatizo

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami pamoja na viongozi wengine wa jumuia hiyo wa hapa nchini wakati kiongozi huyo alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.

Jumuia ya Kihindu Tanzania (BAPS) imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo ziatumika kwaajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto wenye matatizo hayo hapa nchini.

Fedha hizo ambazo zitatumika kwaajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto 30 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimetolewa hivi karibuni na kaimu kiongozi wa Dunia wa jumuia hiyo.

Akizungumza kuhusu msaada huo Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani Mtukutu Bhaktipriyadas Swami alisema wametoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia jamii yenye uhitaji hasa watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha zilizotolewa zitatumika kwa walengwa ambao ni watoto wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Prof. Janabi alisema kuwa Taasisi hiyo imekuwa na uhusiano mzuri na Jumuia ya BAPS ambao kila mwaka wamekuwa wakichangia fedha kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto ambao baada ya matibabu wamepona na wengine wamerudi shuleni kuendelea na masomo yao.

Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisalimiana na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Viongozi wa Jumuia ya Kihindu (BAPS) wakijadili jambo wakati Kaimu kiongozi wa Dunia wa Jumuia hiyo Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. BAPS imetoa kiasi cha shilingi milioni 68 fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami alipotembelea Tanzania hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji.
Kaimu kiongozi wa Jumuia ya Kihindu Duniani (BAPS) Mtukufu Bhaktipriyadas Swami akimpa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati kiongozi huyo alipotembelea nchini hivi karibuni. Tangu mwaka 2016 BAPS wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa jumla ya watoto 290 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. Picha na JKCI

WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AZINDUA COPA UMISSETA MJINI BUKOBA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta mjini Bukoba. 

 Akizindua mshindano hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema michezo ni burudani, inaleta undugu, umoja na upendo hivyo h aina budi kuienzi siku zote. "Nawaomba vijana mpende michezo maana ni burudani na ilateta afya kwa watu wa rika zote, mkizingatia hivyo hakutakuwa na watu wenye magonjwa ya ajabu ajabu," amesema. 

 Mashindano hayo yalipambwa na shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Kaitaba na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa michezo na wanzi wa shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyango, aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Said Kiganja.
 Waziri Mwakyembe akigawa vifaa vilivyotolewa na Coca-Cola kwa moja ya mwakilishi wa mmoja wa shule za sekondari.
 Waziri Mwakyembe akikagua moja ya timu wakati wa hafla ya uzinduzi.
 Wadau wa Umisseta katika picha ya pamoja na Waziri Mwakyembe.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

AZAM FC YATAMBA KUIFUNGA PRISON JUMAPILI

$
0
0
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, tayari imeianzia kambi Tanzania Prisons huku benchi la ufundi likijinasibu limejipanga kuendeleza ubabe dhidi ya maafande hao.

Timu hizo zinatarajia kuumana Jumapili hii katika Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1.00 usiku, ukiwa ni mchezo wa raundi ya 29 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa kikosi hicho kimeanza vema maandalizi yake huku akikiri ushindani mkubwa unaoonyeshwa na wachezaji mazoezini.

“Kila mtu anaonyesha ari ya kutaka kucheza kwa hiyo tutarajie tutakuwa na mechi ya ushindani na mechi ya burudani vilevile,” alisema.

Akizungumzia utofauti wa mchezo huo ukilinganisha na ule wa kwanza waliocheza Uwanja wa Sokoine na kuichapa Prisons mabao 2-0, Cheche alidai kuwa; “Mchezo wa kwanza ushapita na huo unaokuja ni mwingine tofauti na ule wa mwanzo.

“Kwa hiyo tunajipanga tofauti na vile tulivyojipanga mwanzo kwa sababu mwanzoni tulicheza uwanja tofauti na tulikuwa na baadhi ya wachezaji ambao sasa hivi hawapo, lakini sasa hivi tunajipanga kivingine kuhakikisha tunaendeleza ubabe wetu.”

Mabao ya Azam FC kwenye mchezo huo wa ugenini, yalifungwa na washambuliaji Yahya Zayd na Paul Peter.

Alisema kuwa kwa sasa haifikirii mechi ya mwisho dhidi Yanga, anachoangalia ni mchezo ujao dhidi ya Prisons kuhakikisha wanaendeleza ubabe kabla ya kujipanga tena kukipiga na Wanajangwani hao.

Matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex, wataingia kwenye mchezo huo wakitoka kuifunga Majimaji 2-0, matokeo yaliyoifanya kuzidi kujikita katika nafasi ya pili kwa pointi 52, ikiizidi Yanga kwa pointi nne ambayo ina mechi mbili mkononi huku tayari Simba ikiwa imeshatangaza ubingwa na pointi zake 68.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA UWEKEZAJI CHA JWTZ NA VIWANDA VYA MAJI NA USHONAJI VYA SUMA JKT MGULANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu wakifunua pazia kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembela kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za kijeshi zinazoshinwa na kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za kijeshi zinazoshinwa na kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kutembelea kiwanda cha ushonaji nguo  baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa kisasa wa Mikutano.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bidhaa za kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua utengenezaji wa maji ya kunywa  katika kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. 
 Maji ya kunywa ya UHURU PEAK yanayotengenezwa katika kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akinywa maji  yaliyotengenezwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akinywa maji  yaliyotengenezwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya UHURU PEAK baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. PICHA NA IKULU

WANANCHI WAFUNGUKA KUHUSU ELIMU BORA AU BORA ELIMU

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Twaweza limetoa matokeo katika utafiti wao wa Elimu Bora au Bora elimu ambapo wananchi wamefunguka na kudai viwango vya elimu viboreshwe hata kama itawalazimu kulipa ada.

Aidha imeelezwa katika kuchagua shule za Sekondari (kidato cha kwanza)  asilimia 72 ya wazazi huangalia viwango vya ufaulu katika shule, asilimia 6 umbali wa shule na asilimia 18 huangalia umbali wa shule. 

Pia kuhusu wazazi kisaidia uongozi wa shule asilimia 52 ya wazazi hushiriki kwa kuwaadhibu watoto wao, asilimia 22 hushiriki katika harambee za kuchangia shule, asilimia 14 kufuatilia mahudhurio na asilimia 4 kutoa maoni kwenye ukaguzi wa mahesabu ya shule.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema idadi ya wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza limeongezeka mara baada ya sera ya elimu bure kuanzishwa ambapo mwaka 2015.

Ambapo watoto walioandikishwa ni milioni 1.5 na mara baada ya sera kuanzishwa watoto milioni 2.2  na 21 waliandikishwa na hiyo inapelekea asilimia 90 ya elimu ya msingi na sekondari hutolewa na Serikali.

Imeelezwa kuwa mitazamo ya wananchi kuhusu elimu bure imebadilika kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka 12 ambapo mwaka 2005 asilimia 56 wamesema elimu itolewe bure kwa watoto wao hata kama ni ya kiwango cha chini na kwa mwaka 2017 wananchi 9 kati ya 10 ambao ni asilimia 87 wameeleza ni bora kuongeza viwango vya elimu.

Ameongeza na hata kama itawalazimu kulipia ada  na wangependa Serikali itumie fedha kwenye mpango wa kutoa mafunzo na kuwasaidia walimu kuliko kugawa sare za shule bure ikilenga kuwaondolea wazazi mzigo wa kununua sare hizo.

Imeelezwa kuwa utafiti huo ulifanyika ili kujua elimu waitakayo watanzania ambapo mwaka jana Septemba na Oktoba takwimu zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,786 Tanzania bara bila kuhusisha Zanzibar.

Aidha mdau kutoka Haki elimu  Boniventure Godfrey amepongeza tafiti huo na kueleza wananchi wameona tatizo baada ya kutoa maoni yao kuwa wanataka elimu bora kwa watoto wao hata kama ni ya kulipia na hiyo imedhihirika katika utafiti huo kwa kuonesha mchango wa wazazi katika kuchangia suala la elimu hasa katika suala la miundombinu.

Kwa upande wa  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Othiniel Mnkande ameeleza kwa kuangalia ongezeko la watoto shuleni lazima suala la ubora wa elimu hasa kwa walimu katika kuwawekea mazingira bora katika mafunzo na maslahi pia na kuangalia ubora wa walimu wanaopelekwa mashuleni na ili kwenda kwenye ubora lazima mambo muhimu yaangaliwe kama bajeti na mafunzo bora kwa kuangalia katika hali endelevu.

Wakati huo huo Mwanasiasa na Mwanaharakati Noerakindo Kessy amesema tatizo lililopo ni kutotambua mfumo wa elimu unahitaji nini kwa wakati huu kwani wazazi wengi wanaona ubora katika elimu kwakuwa wanaona changamoto  ambazo walipitia na zilizopo kama kukosa ajira na mmomonyoko wa maadili.

Kessy emeeleza suala la elimu ni la kushirikiana baina ya serikali na wananchi katika kuwalinda walezi wa taifa (walimu) bila kufuata mifumo ya nje.

DK. NDUGULILE AKABIDHI VITANDA,MAGODORO 14 HOSPITALI YA VIJIBWENI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Afya,Wazee,Jinsia na Watoto na Mbunge wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Dk.Faustine Ndugulile amekabidhi vitanda na magodoro 14 vinavyotarajiwa kuhudumia wagonjwa wa dharula kwenye  Hospitali  ya Vijibweni na kuwataka wataalamu kuvitumia vitanda hivyo kwa lengo lililokusudiwa.

Dk.Ndugulile ameyasema hayo leo wakati akikabidhi vitanda alivyopokea kutoka kwa Jamii ya Australia (Australia Tanzania society) na Kampuni ya JACANA ikiwa ni  matokeo ya mkakati ambayo Serikali inashirikisha sekta binafsi katika hali ya utoaji wa huduma za afya.
Pia amemtaka Mkurugenzi wa Manispa ya Kigamboni na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  kusimamia mapato na kuhakikisha mifumo ya kudhibiti mapato  inafungwa kwenye vituo vyotevya afya  ili fedha zitakazopatikana zitumike kuboresha huduma nyingine  za afya.
Aidha Dk.Ndugulile amesisitiza ofisi ya Mkurugenzi kuweka mfumo mzuri wa malalamiko ili kuwarahisishia wananchi wanaokuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma kujua waende kwa nani kuweza kuhudumiwa na kusikilizwa malalamiko yao.

"Mkurugenzi Mtendaji,Mganga Mkuu wa Wilaya na Mganga Mfawidhi wekeni tangazo la namba za simu kwenye bango i ili mwananchi akiwa na malalamiko ajue anampigia simu nani, tunataka uwazi na uwajibkaji kwenye serikali ya awamu ya tano,"amesema Dk.Ndugulile.
Pia Naibu Waziri  amesema ni vizuri  Wilaya na  hospitali  kujipanga na kuhakikisha dawa zote za msingi zinakuwepo kwa mujibu wa muongozo na kufafanua Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka  Sh.Biloni 30 hadi Sh.Bilioni 66.
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Vijibweni wakati wa kukabidhi vitanda vya wagonjwa.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Hoja Maabad akiwashukuru wafadhili kwa msaada wa vitanda
 Afisa uhusiano  Bw.Ahmed Merere kutoka JACANA akizungumzia lengo la kusaidia Hospitali ya Vijibweni .
 Baadhi ya Vitanda vya kuhudumia wagonjwa wa dharula vilivyokabidhiwa Hospitali ya Vijibweni leo na Naibu Waziri wa Afya.
 kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile ,Bw.James Chialo Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society,  Afisa Uhusiano wa JACANA Bw.Ahmed Merere,  Meya wa Manispa

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile wa kwanza kushoto akipeana mkono wa shukurani na Afisa Uhusiano wa JACANA wakati wa Makabidhiano ya vitanda.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SHEIKH WA MKOA DAR ASHAURI WALIOFUNGA NDOA KUELEKEA MWEZI WA RAMADHANI WASIBEZWE, BALI WAPEWE MOYO KWANI NI JAMBO JEMA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema vijana wa Kiislamu ambao wamefunga ndoa wakati wa kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wanatakiwa kupongezwa na kupewa moyo badala ya kuwabeza na kuwakejeli kwa uamuzi wao wa kufunga ndoa.

Sheikh Alhad ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao umeanza leo kwa waumini wa dini hiyo kuanza kutekeleza moja ya nguzo za Kiislamu.

Hivyo wakati anazungumza mfungo huo, waandishi wa habari walitaka kupata maoni yake ni kwanini ndoa nyingi zinafungwa wakati wa kuelekea mwezi wa Ramadhan ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua ndoa ni kitu kitukufu na hakuna sababu ya kuwabeza wanaofunga ndoa.

"Kwanza kabisa naoMba muheshimu kitu kinaitwa ndoa kwani ni kitu cha heshima sana na binadamu anapotaka kuongeza nasaba yake lazima itapatikana kupitia ndoa.Ifahamike kuna ndoa na tendo la ndoa na yule ambaye anafanya tendo la ndoa bila ndoa hana tofauti na mnyama.

"Hivyo wanaofunga ndoa ni aina ya toba, mtu ambaye ameamua kufunga ndoa maana yake ameacha zinaa na hilo ni jambo jema.Mtu ambaye ameamua kuacha zinaa anatakiwa kupongezwa na hao wanaofunga ndoa kwenye mwezi wa Shaaban huenda imetokana tu na taratibu za mipango kukaa vibaya na inapofika karibu na Ramadhan anaona bora tu afunge ndoa na hiyo ni kwa kuheshimu tu mwezi wa Ramadhan,"amesema Sheikh Alhad.

Amesisitiza hakuna sababu ya kuwabeza wanaooa kwenye pindi cha kuelekea Ramadhan na wala hapaswi kukatishwa tamaa bali wanatakiwa kupewa moyo na hata ile kauli ya kusema ni ndoa za uji si vizuri.

Sheikh Alhad amesema vijana hao wanatakiwa kupewa moyo kwa kutafuta hifadhi ya ndoa na kueleza hata wanaosema ndoa nyingi ambazo zimefungwa kipindi cha kuelekea mwezi wa Ramadhan huwa zinavunjika baada ya mwezi kwisha hazina ukweli wowote.

Wakati huohuo amezungumzia umuhimu wa waumini wa dini ya Kiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan kuhakikisha wanajiepusha na mambo yasiyompendeza Mungu huku akisisitiza funga si kujiuzuia kula na kunywa tu bali ni kujizuia na mambo yote yasiyofaa.

"Funga macho yako kwa maana ya kuyazuia kutooa mambo yasiyo faa, funga mikono yako kwa maana ya kutopokea rushwa na kushika vitu vyenye kumchukiza Mola, funga miguu yako kwa maana ya kutokwenda kwenye mambo yasiyo na tija kiimani na hakikisha unafunga mdomo wako kwa kujiuzuia kutoa lugha chafu.Kipindi cha mwezi wa Ramadhan ni muhimu kufanya toba na yote yaliyomema,"amesema Sheikh Alhad.

President Kenyatta signs the Computer misuse and Cybercrime bill into law

AZAM TV: MSEMAJI WA SIMBA SC HAJI MANARA ALIPOZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images