Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

BALOZI KIDATA AMUAGA MAKAMU WA RAIS LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Balozi Kidata ambaye aliapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tarehe 10, Mei 2018 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Balozi Kidata alifika leo kuona Makamu wa Rais na kumuaga rasmi tayari kwa kwenda kulitumikia Taifa kwenye kituo chake kipya cha kazi nchini Canada. 

Makamu wa Rais, Mhe. Samia amempongeza na kumtakia kazi njema ambapo alimtaka kwenda kufanya yale nchi imeelekeza haswa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa Viwanda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alphayo Kidata aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alphayo Kidata aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja  na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alphayo Kidata mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) ​\

KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA TANZANITE ONE YAKUBALI KUILIPA SERIKALI FIDIA MARA BAADA YA KUFIKIA MAKUBALIANO

$
0
0






 Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akitia saini pamoja na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya kufikia makubaliano na  Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini ambayo imekubali kulipa fidia kwa Serikali pamoja na mambo mengine ya Kimkataba.  
 Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akibadilishana hati za Makubaliano na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini kukubali kulipa fidia kwa Serikali.  
 Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi  akiwa na watendaji wa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Tanzanite One wakati akielekea kusaini hati za makubaliano baina ya kampuni hiyo na Serikali.

 Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na kusaini hati ya Makubaliano yatakayoiwezesha Serikali kulipwa fidia na Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzaniate.

 Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma akizungumza mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na kusaini hati ya Makubaliano yatakayoiwezesha Serikali kulipwa fidia na Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzaniate.

Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiagana na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini kukubali kulipa fidia kwa Serikali pamoja na mambo mengine ya Kimkataba kama walivyokubaliana. PICHA NA IKULU

UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA KUKAMILIKA MWEZI JUNI

$
0
0
Na. Theresia Mwami - TEMESA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), imeahidi kukamilika kwa ujenzi kivuko kipya cha Kigongo Busisi (MV. MWANZA) unaofanywa kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ifikapo mwezi Juni 2018. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kivuko hicho, uliofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA mapema leo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu alisema ujenzi huo unagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 na ulianza rasmi tarehe 28/08/2017 na kwamba tayari umekamilika kwa asilimia 95.

“Namuagiza Mkandarasi kuhakikisha kuwa ujenzi wa kivuko hiki unakamilika kwa aslimia 100 ifikapo mwezi Juni,2018 kama ilivyoainishwa kwenye mkataba ili kuweza kuboresha zaidi huduma ya uvushaji abiria na mizigo yao katika eneo Kigongo – Busisi”, aliongeza Dkt. Mgwatu.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kivuko cha MV. MWANZA kutafanya eneo la Kigongo Busisi kuboresha zaidi huduma za uvushaji kwani kwa sasa tayari kuna Kivuko cha MV. Misungwi ambacho pia kina tani 250, MV. Sengerema tani 170 na MV. Sabasaba tani 85.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri alisema kuwa, serikali inalengo la kuboresha hali ya maisha ya wananchi, kwa kuwawekea miundombinu salama ya vivuko, ili kuhakikisha wanapata huduma bora na salama wakati wote. 

Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutatoa nafasi ya ukarabati mkubwa wa vivuko vingine vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi kufanyika kwa awamu. Aidha alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza TEMESA kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa kivuko hicho, kwa kuhakikisha kuwa unakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye mkataba wa ujenzi wake.

Nae Mkurugenzi Kampuni ya Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd, Major Songoro, aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuahidi kuimaliza kazi hiyo kwa haraka na ustadi mkubwa.
Kivuko kipya cha MV. MWANZA chenye uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja, kinachojengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ambacho kinagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 fedha kutoka serikali ya Tanzania. Kitatoa huduma kati kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
Kivuko kipya cha MV. MWANZA chenye uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati mmoja, kinachojengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ambacho kinagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.9 fedha kutoka serikali ya Tanzania. Kitatoa huduma kati kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri, akipanda ngazi kukagua ujenzi wa kivuko kipya cha MV. MWANZA, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd (inayojenga kivuko hicho) Salehe Songoro, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme( TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme( TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari baada ya ukaguzi wa kivuko kipya cha MV. MWANZA kulia kwake mwenye miwani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri.Picha na Kitengo cha Habri na Mawasiliano TEMESA

TRA YAKAMATA BIDHAA MBALIMBALI KUPITIA NJIA ZA MAGENDO ZIKIWA NA THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 20

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Arusha

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekamata malori mawili yenye bidhaa mbalimbali eneo la Loliondo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kupitia njia ya magendo yakitokea nchini Kenya zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.

Akizungumza leo jijini Arusha, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere amesema kuwa, malori hayo yenye namba T 985 AJP na T 840 ABF yalikamatwa usiku wa Mei 10 2018 na kusisitiza kuwa wafanyabiashara wenye bidhaa hizo wamevunja sheria kwa kuwa hawakulipa kodi stahiki kama inavyotakiwa.

Kichere amefafanua kuwa, wafanyabiashara wenye bidhaa hizi zilizokamatwa, wamevunja kifungu cha sheria namba 82 na 200 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 na Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004. Hivyo kwa Sheria hizi, wafanyabiashara hawa wanatakiwa kulipa kodi pamoja na faini ya shilingi milioni 39 na magari yao kutaifishwa.

"Kwa ujumla bidhaa hizi zote zina thamani ya shilingi 20,037,330.15 ambayo kodi ya bidhaa hizi ni shillingi 28,524,758.11 na adhabu au faini ya bidhaa hizi ni shilingi 10,768,665.08. Hivyo jumla ya mapato yanayotakiwa kulipwa Serikalini ni shilingi 39,293,423.19," alieleza Kichere.

Amezitaja bidhaa zilizokamatwa kuwa ni pamoja na mifuko 362 ya sukari yenye uzito wa kilo 50 kila mmoja, maboksi 40 ya mafuta ya kula yanayoitwa Karibu, maboksi matatu ya mafuta ya kula yanayoitwa Daria, magaloni 100 ya mafuta ya kula yanayoitwa Nyata na maboksi matatu ya viungo vya mboga 

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Mkuu Kichere amewakumbusha wafanyabiashara wote kuzingatia taratibu za uingizaji bidhaa nchini ili kuepuka hasara kwenye biashara zao na kuongeza kuwa, TRA haitavumilia ukiukwaji wowote utakaofanywa na wafanyabiashara kwa kutozingatia sheria na taratibu hizo.

KAMPUNI ZA UKANDARASI ZAIDI YA 70 WAJITOLEA KUJENGA MITARO YA BARABARA JIJINI DAR BURE

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

KAMPUNI za ukandarasi zaidi ya 70 zimeamua kujitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam bure kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda.

Hatua hiyo inakuja baada ya Makonda kufanya ziara usiku na mchana kwa lengo la kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi hao ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo. 

Taarifa yake kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam Makonda pia amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi ya barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA) Wilaya kwa ajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo. 

Aidha Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya fedha za Serikali.

Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakandarasi wa kampuni mbalimbali zilizojitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam, bure kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa .

WIZARA YA VIWANDA , BIASHARA NA UWEKEZAJI, KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA WAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA UJERUMANI KUWEKEZA NCHINI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Ujerumani
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe ameongoza msafara wa Tanzania kwenda Ujerumani kushiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi za Afrika Mashariki na Ujerumani.

Ambapo Kongamano hilo limeanza jana  mjini Berlin na washiriki wa Tanzania ni kutoka taasisi za Serikali na wafanyabiashara wa kutoka sekta binafsi.

Imeelezwa kuwa lengo la kushiriki kongamano hilo ni kuvutia wawekezaji wa Ujerumani wenye mitaji, na teknolojia kuja kuwekeza nchini kwenye miradi mbalimbali na pia kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.

Ujumbe wa Tanzania ulifika Berlin Mei 13, 2018 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa TIC amoja na timu yake wamefanya kikao pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi. 

Katika mkutano huo Mwambe ameelezea kuwa ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo umejipanga  kwa kunadi fursa za uwekezaji katika sekta za viwanda, afya,  tekinolojia/mawasiliano, nishati na miundombinu.

 Hata hivyo Mwambe ameainisha maeneo mahsusi yanayotafutiwa uwekezaji katika nchi ya Ujerumani kuwa ni ujenzi wa viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu na vifaa tiba.

Pia uzalishaji wa umeme mbadala na usambazaji; utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu ya usafirishaji ikiwamo reli, viwanja vya ndege , bandari na barabara kwa ujumla na utekelezaji wa mradi wa usalama katika mitandao. 

Kwa upande wa wafanyabiashara imeelezwa kuwa wamejipanga kutafuta wabia katika sekta za ujenzi, utalii, madini, vifaa vya ujenzi na soko la bidhaa mbalimbali za kilimo kama vile , ( mtama, choroko, korosho na mbaazi).

Balozi  Dk.Possi alisisitiza kuwa ni vizuri  mamlaka za Serikali zinazohusika na utoaji wa vibali mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji zipunguze muda wa kuchakata upatikanaji wa vibali hivyo kwani kuchukua  muda mrefu unakatisha tamaa wawekezaji na kuwakimbiza kwenda kuangalia fursa nchi nyingine. 

 Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa TIC amehitimisha mkutano kwa kupongeza juhudi zinazofanywa na Dk. Possi katika kuhamashisha kampuni za Kijerumani pamoja na kuandaa misafara ya wafanyabiashara wa Kijerumani kuja Tanzania kuangalia fursa za uwekezaji. 

Amefafanuliwa Wajerumani mara zote  hawafanyi bishara ama uwekezaji mahali popote duniani ambapo hakuna uimara wa masuala ya siasa na ukuaji wa uchumi.

Hivyo ujio wa Wajerumani nchini pamoja na nia yao ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ni dhahiri kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji ya Tanzania yapo vizuri.

Na yanaendelea kuboreshwa siku hadi siku chini ya serikali ya awamu ya tano  inayoongozwa na Rais Dkt John  Magufuli. 

Mkurugenzi wa TIC  amemhakikishia Balozi Dk.Possi utayari wa TIC kuwapokea wawekezaji kutoka Ujerumani na kuwapatia usaidizi utakaohitajia ili kufanikisha uwekezaji wao nchini. 

Taasisi zinazozoshiriki mkutano huo kutoka Tanznaia ni  TIC, Bohari kuu ya Dawa Tanzania (MSD), Shirika la Umeme Tanzanaia (TANESCO) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Mwambe akiwa katika mkutano wa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe.  Dkt Abdallah Possi(katikati).

MSANII DIAMOND AZINDUA WIMBO WA COLOURS KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

$
0
0
MSANII wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake wakati akiimba wimbo maalum utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 wimbo uitwao Colours nyimbo aliyoshirikiana na Jason Derulo, katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola Tanzania ni moja ya mdhamini wa mashindano hayo makubwa ya soka duniani na inayofuraha kwa msanii kutoka Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano hayo na kwamba anaimani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano.
 
Msanii Diamond akipagawisha mashabiki wa Soka waliohudhuria katika Uzinduzi wa wimbo wa Colours maalum kwa ajili ya kombe la dunia 2018 linalofanyika nchini Urusi. 
Mkurugenzi wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios akiongea machache kuhusu hafla hiyo,(kushoto) ni Meneja wa Coca-Cola nchini, David Karamagi. 
Mkurugenzi wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios akikata keki wakati wa hafla hiyo.  Msanii Diamond akisalimiana na Mameneja Waandamizi wa Coca-Cola.  Msanii Peter Msechu na bendi yake wakipagawisha mashabiki wa soka waliohudhuria katika uzinduzi wa wimbo maalum alioshirikishwa msanii Diamond utakaosheresha Kombe la Dunia 2018. 

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO MEI 16, 2018


DC KASESELA ATOA SIKU 7 KWA WADAIWA SUGU WA MIKOPO YA SIDO WILAYANI IRINGA

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Iringa mkoani Iringa Richard Kasesela ametoa siku saba kujisalimisha kwa wadaiwa sugu vikuwemo vikundi viwili vya vya Mungu ametenda ambavyo kwa pamoja vinadaiwa mkopo wenye thamani ya Zaidi ya million 293,380,925 iliyotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidodo (SIDO) mkoa wa Iringa . 
Akizungumza na wanahabari jana ofisini kwake mkuu huyo wa wilaya ya Iringa ,Kasesela alisema kuwa vikundi namba moja na namba mbili vya Mungu ametenda pekee yake vinadaiwa kiasi cha shilingi milioni 32 wakati wadai sugu wengi wapo katika Manispaa ya Iringa ambao kwa pamoja wanadaiwa kiasi cha shilingi 269,331,225 wakati halmashauri ya Iringa vijijini wanadaiwa 4,858,700 ukiacha wadaiwa wa wengine kutoka wilaya za mkoa wa Iringa . 
 Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa shirika la SIDO ni la umma na lengo lake kuu toka kuanzishwa kwake ni kupanga na kuratibu na kukuza ukuaji ,upanuzi na maendeleo ya viwanda vidogo na vya kati Tanzania bara kwa ajili ya kuwezesha watanzania wengi kupata ajira. Hivyo alisema pamoja na shughuli hizo limekuwa likitoa ushauri wa fedha na mikopo ambayo inalenga kukuza biashara na viwanda vidogo vinavyoanzishwa au vilivyoanzishwa tayari lakini vinahitaji mikopo ili kukua Zaidi. Amesema kutokana na taarifa aliyofikishiwa na meneja wa SIDO mkoa ilionyesha kuna malimbikizo mengi ya mikopo kwa kuwa na wadaiwa sugu wengi Zaidi na pesa nyingi ipo nje . 
 Alisema katika mikopo hiyo ipo mikopo ya mtu moja moja na vikundi na kuwa kwenye taarifa ya SIDO kuna wadaiwa 891 wamelimbikiza jumla ya shilingi 293,380,925 huku wadaiwa binafsi wapo 167 ambao wanadaiwa jumla ya shilingi 181,396,500 na vikundi 15 vyenye wanachama 721 vinavyodaiwa jumla ya shilingi 111,984,425 ndani yake vipo vikundi hivyo viwili vya Mungu ametenda . 
 Hivyo alisema kwa kuanza msako huu utakaosimamiwa na ofisi yake amelazimika kutoa siku 6 hadi jumatatu ijayo mdhamini wa vikundi vya Mungu ametenda awe amejisalimisha pamoja na wanachama wake katika ofisi yake na wadaiwa wengine ndani ya siku saba kuanzia leo Mei 16 wawe wamejisalimisha ofisini kwake na kuanza kurejesha mikopo hiyo . 
 “ Nawaagiza wakopaji wote kupitia vyombo vya habari popote walipo ndani ya wilaya ya Iringa ama mkoa ama wawe nje ya mkoa huu waanze kujisalimisha kwa kulipa madeni kabla ya kutangaza majina yao na picha zao katika vyombo vya habari na wapo wengine ni viongozi wakubwa katika jamii ila katika hili watatusamehe lazima walipe madeni “ 
Meneja wa SIDO mkoa wa Iringa Francisca Simon alisema kuwa wameendelea kuwasaka wakopaji hao kwa kutumia madalali ila baadhi ya madalali wamekuwa si waaminifu badala ya kuwataka wakopaji kulipa mikopo yao kupitia akaunti ya SIDO wamekuwa wakipokea pesa mkononi na kula na kuwa wapo baadhi ya madalali wanawasaka kwa kukiuka taratibu walizokubaliana. 
Pia alisema kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya madalali kumechangia wakopaji wasumbufu kufanya marejesho kwa wakati na kuwa sasa wameweka dalali mwingine ambaye hatapokea hata senti moja toka kwa wadaiwa hao. 
Ofisa mikopo wa SIDO mkoa wa Iringa Neserian Laizer alisema kuwa mikopo hiyo ya serikali masharti yake huwa nafuu tofauti na mikopo ya taasisi nyingine ila hata hivyo wakopaji huwa wanakuwa na dhamana na kutolea mfano vikundi vya Mungu ametenda ambavyo kiongozi wake aliweka dhamana shamba lake la miti pamoja na nyumba na kuwa mwanzo walifanya vizuri ila mara ya pili wameshindwa kurejesha mikopo hiyo. 
 Alisema kuwa vikundi vya Mungu ametenda ni vikundi ambavyo awali vilikuwa vikifanya vizuri na kukopeshwa zaidi ya mara mbili na kurejesha kwa wakati ila awamu ya mwisho wameshindwa kurejesha kwa madai wanachama wamekimbia
Mkuu wa  wilaya ya Iringa  Richard  Kasesela  akizungumza na wanahabari  leo  ofisini  kwake  kuhusu  wadaiwa  sugu  wa  SIDO  kuanikwa
Mkuu  wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akifafanua  jambo  leo juu ya  wakopaji wa SIDO
Afisa  biashara wa  SIDO  Niko Mahinya  akifafanua  kuhusu  wakopaji  walioshindwa  kurejesha kwa  wakati  mikopo ya  SIDO ,kushoto  ni  meneja  wa  Sido  mkoa  wa Iringa  Francisca Simon
Afisa  mikopo  wa  Sido  mkoa  wa  Iringa Neserian  Laizer  akifafanua  kuhusu  mikopo  ambayo haijarejeshwa  kulia  ni meneja wa  Sido  mkoa  wa Iringa Francisca Simon 
Picha na habari na MatukioDaima TV

FC Barcelona yatua Afrika ya Kusini kucheza na Mamelodi Sundowns FC kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa mandela

YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga wameshindwa kuondoka na ushindi dhidi ya Rayon ya Rwanda baada ya kulazimishwa suluhu ya kutokufungana.

Yanga waliokuwa katika dimbani la nyumbani la Uwanja wa Taifa walikubali matokeo hayo baada ya kushindwa kupata goli la ushindi ma matokeo kuishia 1-1.

Mchezo huo ulioanza majira ya saa 1 usiku Yanga waliweza kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza wakionekana kutawala sehemu ya kiungo kilichokuwa kinaendeshwa na Thaban Kamosoku na Pius Buswita.
Kocha msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema kuwa hajaridhishwa na matokeo ya leo dhidi ya Rayon Sports kwani walihitaji ushindi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua inayofuata.

"Sijaridhishwa na matokeo ya leo, katika mchezo huu tulihitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua inayofuata ila wachezaji walikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizozitumia,"amesema Mwandila.

Mwandila amesema kwa sasa mashindano haya yanasimama kwa muda mpaka mwezi wa saba kwahiyo watatumia kipindi hiki kwa ajili ya kukiunda kikosi na kukifanyia marekebisho kwenye nafasi zinazohitajika na zaidi watahakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo inayofuata.
Baada ya mechi hii Yanga wanakuwa na alama 1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa huku Rayon wakiwa ma alama 2.

RAIS MAGUFULI ANATARAJIWA KUNOGESHA UBINGWA WA SIMBA SC UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI...

RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN ATOA RISALA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa risala ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi wa zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo. Amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi kuwa na mashirikiano ya pamoja na kumcha Mwenyeezi Mungu

RAMADHAN KAREEM: TUNAWATAKIA WAISLAM WOTE MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI

$
0
0
Mashindano ya Kombe la dunia la watoto wa mitaani chini ya shirika la Steet Child United na udhaamini wa makampuni na taasisi tofauti, zaidi kampuni ya mawasiliano ya simu ya nchini Urusi, Megafon yamefikia tamati leo kwa kuchezwa mechi za mshindi wa tatu na fainali kwa watoto wa kike na wakiume, ambapo timu ya Tanzania (wasichana) iliweza kuwa mshindi wa pili baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka Brazil, baada ya kutokea mawasiliano mabaya kati ya mlinzi wa Tanzania na mlinda mlango wake katika hatua za mwisho za mchezo huo.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa aina yake, huku Brazil wakimiliki mchezo sana na kufanikiwa kumficha kiungo mkuu wa Tanzania, Nahodha Asteria Robert na hapo Tanzania ikawa ishadhibitiwa. Kipindi cha pili Tanzania kidogo walicheza vizuri lakini hawakurudisha goli hilo.
Kipindi cha kwanza Tanzania walicheza kwa presha sana na hawakutulia na mpira na hali hio ikawapotezea kujiamini. Lakini mwisho wa siku asiekubali kushidwa sio mshindani. Tanzania ikashika nafasi ya pili katika mashindano hayo kwa wanawake. 


Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri, wakiwemo viongozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi pamoja na mchezaji wa zamani wa Arsenal na bingwa wa kombe la dunia kwa kikosi cha Brazil na kiungo maarufu na mwenye uwezo wa viwango vya dunia, Gilberto Da Silva. 
Timu zote baada ya mechi zilipata nafasi ya kumuuliza swali moja Gilberto Da Silva. Tanzania iliuliza swali kupitia Nahodha wake, Asteria Robert kwa Kiswahili na mkalimani Mohamed Masour Nassor akatafsiri moja kwa moja kwa lugha ya Kireno ya mchezaji huyo. Swali hilo lilikua hivi,"Je ni vipi Unawasaidia watoto wa mitaani kufikia ndoto zao na wale watoto ambao wanataka kuwa wachezaji wa viwango vya dunia kama wewe? Mwisho ikafuata sherehe ya ufungaji wa mashindano hayo. 

Muda wa zawadi ulipofika, Tanzania ilizawadiwa Kombe na medali za shaba kwa kila mchezaji na viongozi wa timu kutoka chama cha mpira cha Urusi na zawadi zengine kutoka kwa chuo cha Patrice Lumumba. Tanzania pia ilitoa kiungo bora wa mashindano ambae ni nahodha, Asteria Robert ambae kwa kweli alistahili sana. Kwa upande wa bingwa wa wanaume ni Timu  ya Uzbekistan baada ya kuilaza kwa mikwaju ya penati timu ya Pakistan.
 Kwa upande wa zawadi zengine, Mlinda Mlango bora alitoka Uingereza kwa wanawake, kwa wanaume alitoka Indonezia, Mfungaji bora kwa wanawake alitoka Brazil, mlinzi bora kwa wanawake alitoka Ufilipino, mlinzi bora kwa wanaume alitoka Uzbekistan, mchezaji bora kwa wanaume alitoka Pakistan, mchezaji bora kwa wanawake alitoka Brazil na wengine. 
Tanzania kwa ujumla imeweka rikodi nzuri pia kwa kuwa  mshindi wa pili mwaka huu kwa wanawake. Mwaka 2014 Tanzania ilikua bingwa wa mashindano haya kwa wanaume huko mjini Rio di Jeneiro, Brazil na mwaka 2010 Tanzania iliishia nusu fainali huko Afrika ya Kusini kwa upande wa wanaume. Nafikiri mwaka 2022 nchini Qatar, Tanzania kwa wanawake itafanya vizuri zaidi. Nchi zilizoshiriki ni 21 na timu zikiwa ni 24.  imeandikwa na Mohamed Mansour Nassor, SOYUZ Alumni Association of Tanzania

Watanzania Watakiwa Kutumia Matokeo ya Sensa Zinazofanyika Hapa Nchini Kujiletea Maendeleo

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisisitiza umuhimu wa kutumia takwimu na Tafiti mbalimbali katika kuchochea maendeleo na kufanya maamuzi mbalimbali kabla ya kuzindua matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi za Taifa za Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amewataka Watanzania kutumia takwimu za sensa mbalimbali zinazotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kuongeza tija na hatimaye kupunguza umasikini nchini.

Mhe. Mpina ametoa wito huo leo Jijini Dodoma, alipokuwa akizindua matokeo ya utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016/2017 ukiwa ni utafiti wa pili kufanyika nchini ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2014/2015.

"Tunapenda kufanya sensa lakini mwisho wa siku hakuna anayetumia sensa hiyo. Huwezi kufanya mapinduzi ya kiuchumi bila ya kutumia matokeo mbalimbali ya tafiti," alisema Mhe. Mpina.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya awali kuhusu matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Aliendelea kusema, matokeo ya tafiti hizo yametumika katika kupima mchango wa shughuli za kilimo katika Pato la Taifa, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2014 uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.10 wakati mwaka 2017 uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.1. Aidha mchango wa shughuli za kilimo kwa mwaka 2014 ulikuwa asilimia 28.8 wakati mwaka 2017 ulikuwa asilimia 30.1.

Vile vile amesema, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa zao la mahindi mwaka 2016/2017 uzalishaji wake ulikuwa tani 5,766,984 na kwa takwimu za utawala za mwaka 2017/2018uzalishaji ni tani 6,681,000. Katika mwaka 2017 ongezeko la thamani ya shughuli za kilimo cha mazao iliongezeka na kufikia shilingi trilioni 5.3 kutoka shilingi trilioni 5.1 mwaka 2016.

Mhe. Mpina amesema, kwa upande wa Tanzania Baramkoa wa Mbeya umeendelea kuongoza katika uzalishaji wa zao la mahindi kwa tani 578,280 (10%) wakati Mkoa wa Morogoro umeongoza.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akikata utepe kuzindua matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

Aidha kwa upande wa mifugo, Tanzania Bara inaidadi ya ng'ombe 30,496,687, mbuzi 18,947,657, kondoo 5,565,468 na kuku wa asili 38,595,106 ambapo mikoa inayoongoza kwa asilimia kubwa ya ng'ombe ni pamoja na Tabora (8.7%), Mwanza (7.9%) na Manyara (7.2%). Tanzania Zanzibar ina idadi ya ng'ombe wapatao 175,314, mbuzi 107,993, kondoo 517 na kuku wa asili 1,754,786 na mikoa inayoongoza kwa asilimia kubwa ya ng'ombe kwa Tanzania Zanzibar ni Kaskazini Pemba (30.3%) ikifuatiwa na Kusini Pemba (19.9%).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amewaomba watumiaji wa takwimu hizo kuzitumia kwa manufaa ya kufuatilia na

kutathimini mipango ya maendeleo ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na si vinginevyo.

Hata hivyo amesema, Tanzania bado ni nchi ya pili katika Bara la Afrika kwa kuwa na mifugo mingi hivyo ni dhahiri kuwa uwezo wa viwanda vya nyama hapa nchini na kuuza nyama na bidhaa zake zinazozalishwa kwa lengo la kujipatia fedha za kigeni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akimkabidhi Muwakilishi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi Elizabeth Ann Talbert ripoti ya matokeo ya utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo Jijini Dodoma.

HDIF KUANZA WIKI YA UBUNIFU MEI 21 KATIKA KUMBI ZA COSTECH

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu akizungumza juu ya wiki ya Ubunifu kwa vijana iliyoandaliwa na Tasisi ya HDIF kwa kushirikiana na UKaid
 Mwakilishi wa  Mfuko wa Msaada wa Serikali ya Uingereza UKaid, Berthy Arthy akizungumzia  ufadhili wa UKaid Katika wiki ya ubunifu itakayofanyika COSTECH. Kuanzia Mei 21.
 Kiongozi Mkuu wa HDIF Tanzania, David McGinty, akieleza namna Vijana ya ushiriki wa Vijana zaidi ya 2000 katika Wiki ya ubunifu  itakayofanyika Costech kuanzia Jumatatu.
 Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano Kutoka Taasisi ya HDIF, Hannah Mwandoloma akitoa maelezo ya ziada kwa Waandishi wa Habari katika Mkutano wa Waandishi wa Habari.

MICHUANO YA KURUGENZI CUP YAENDELEA KURINDIMA MJINI HAYDOM MKOANI MANYARA

$
0
0
Michuano ya Kurugenzi Cup 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga imeendelea kutimua vumbi kwa timu ya Airport SC kuifunga Makulusa FC mabao 3-0.

Katika mchezo huo uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom, hadi mapumziko timu ya Airport SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Abubakary Maina dakika ya nne kwa njia ya penati.

Kipindi cha pili timu ya Airport SC ilipata mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari Emmanuel Mallo kwenye dakika ya 50 na ya 55.

Kwenye mchezo mwingine timu ya Stand United timu ya Mlimani FC iliifunga bao 1-0 na kuiondoa kwenye michuano hiyo.

Fainali ya mashindano hayo iliyoshirikisha timu 10 inatarajiwa kufanyika jumapili ya wiki hii kwenye viwanja hivyo vya Haydom.

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Mbulu (MBFA) Joseph Nicodemus alisema michuano hiyo itakuwa chachu kwa vipaji vipya vya wilaya hiyo kupiga hatua kwenye mchezo huo.

Nicodemus alisema anatarajia timu zitakazoshiriki michuano ya ligi daraja la tatu ngazi ya wilaya zitapata wachezaji kwenye michuano hiyo ya Kurugenzi Cup 2018.
Waamuzi wa mashindano ya Kurugenzi CUP 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga wakishuhudia manahodha wa timu ya Makulusa FC Regi Gisimoy (kulia) na Samwel wa timu ya Airport FC wakitakiana heri ya mchezo ambapo walifungwa mabao 3-0.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Airport FC wakiwa benchi la ufundi huku wakiendelea furahi mchezo ambapo waliifungwa Makulusa Fc mabao 3-0.
 Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Baadhi ya wachezaji wakiushuhudia mpambano wa soka ukiwa unaendelea kwa kasi baina ya timu za Airtport FC dhidi ya Makulusa FC hazipo pichani.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Mmoja wa wachezaji akigangwa na madaktari baada ya kuumia mguu katika mchezo huo.

SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA

$
0
0
Serikali imekutana na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na Mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo  vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22); utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi. 

Akizungumza katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema Serikali imeamua kukutana na wadau ili kujadiliana na kupata maoni kuhusu utekelezaji wa Sera Mipango na mikakati ya Serikali katika masuala ya kijinsia ili kuweza kutekeleza kwa mafanikio masuala hayo.

Ameongeza kuwa Serikali inashirikiana na wadau wa Maendeleo kwa karibu ili kuwa na Mipango na  mikakati ya pamoja ya kutekeleza masuala mbalimbali ya kijinsia ikiwemo kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.

"Ni jambo la busara kuwashirikisha wadau wa Maendeleo katika masuala ya kimaendeleo ili kupeleke mbele kurudumu la maendeleo" alisisitiza Bi. Sihaba.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Slaam wakati wa majadiliano kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Vitendo vya  Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22); utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Kulia ni Mwakilishi wa UN Women nchini Bi. Susan Steffen.
 Mwakilishi wa UN Women nchini Bi Susan Steffen  akielezea Mipango ya Umoja wa Mataifa katika kuwezesha masuala ya Kijinsia na uwezeshaji wa wanawake  kiuchumi wakati wa kikao kati ya Serikali na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Slaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene akielezea kuhusu utekelezaji wa Mipango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22) (NPA) katika kikao kati ya Serikali na wadau kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi.Dorah Neema akielezea kuhusu masuala ya  Kamisheni ya hali ya Wanawake (CWS) katika kikao kati ya Serikali na wadau kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  (2017/18 – 2021/22) , utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson akiongoza  kikao cha thelathini na moja  cha mkutano wa kumi na moja cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni  akijibu maswali mbali mbali ya wabunge wakati wa  kikao cha thelathini na moja  cha mkutano wa kumi na moja cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akimskiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Sera, Bunge, Ajira, Vijana na wenye ulemavu  Mhe.Jenista Mhagama wakati wa  kikao cha thelathini na moja  cha mkutano wa kumi na moja cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na Mwanamitindo wa kimataifa Bi.Flaviana Matata  wakati  alipomtembelea leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Khamis Kigwangala na Mbunge wa Karagwe Mhe.Innocent Bashungwa wakiwa pamoja na Mwanamitindo wa Kimataifa Bi.Flaviana Matata katika viwanja vya Bunge leo Jijini Dar es Salaam. 
Picha zote na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images