Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live

SPIKA WA BUNGE AFANYA MAZUNGUMZO NA WABUNGE WA IRELAND LEO JIJINI DODOMA

0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Paul Sherlock (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Paul Sherlock (katikati) na Mbunge wa Bunge la Ireland, Mhe. Catherine Conolly (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Ireland walioambatana na Maafisa waandamizi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Ireland walioongozwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Paul Sherlock (kushoto kwake) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Ireland ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Ireland, walioongozwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Paul Sherlock (kulia) baada ya mazungumzo nao yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Ireland wakutana na kuzungumza na Mtandao wa Wabunge wanawake wa Bunge la Tanzania (TWPG) leo katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Ireland katika tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kujenga urafiki na kubadilishana uzoefu katika utendaji wao wa kazi.

(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

WIZARA YA AFYA YATAMBUA UMUHIMU WA MAMALAKA MAABARA YA SERIKALI YA MKEMIA MKUU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MGANGA  Mkuu wa  Serikali  Profesa  Mohamed Kambi amesema Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inatambua umuhimu wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu katika kulinda ya afya ya wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ambapo amesema kikao cha baraza  ni kuhakikisha kuna kuwepo kwa uhusiano kati ya watendaji na Menejimenti.
Kambi amesema katika mkutano wa baraza wanatakiwa kujadili malengo ya taasisi na maslahi ya wafanyakazi ikiwemo mafunzo  ambayo yanatakiwa kutolewa kwa haki sawa.
Aidha Mganga Mkuu huyo ametaka wafanyakazi  wa (GCLA) kuachana na kuwa sehemu ya watu wanaolalamika badala yake wanatakiwa kutatua changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi (GCLA), Dk. Fidelice  Mafumiko  amesema katika kikao  hicho watajadili mada mbalimbali ikiwa ni kuijenga  taasisi hiyo.
Dk. Mafumiko amesema pia baraza hilo kupitia kikao hicho wataazimia mambo mbalimbali yakiwamo ya kujenga mamlaka  ikiwa pamoja na masuala ya maadili.
 Mganga Mkuu wa Serikali,  Profesa Mohamed Kambi  akizungumza katika mkutano wa baraza la  wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu (GCLA) uliofanyika katika ukumbi wa MSD  jijini Dar es Salaam .
 Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Maabara ya  Serikali Mkemia Mkuu (GCLA), Dk. Fidelice Mafumiko akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA  kuhusiana na mada ambazo watapitia uliofanyika katika ukumbi wa MSD jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tawi la la TUGHE wa GCLA, Juvitus Mukela akitoa neno kwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa GCLA uliofanyika katika ukumbi wa msd jijini Dar es Salaam .
 Baadhi ya wajumbe katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa GCLA wakifuatilia mada kwenye mkutano huo.
  Picha za pamoja 

SPORTPESA WAINDUA SUPER CUP AWAMU YA PILI,SIMBA,YANGA SINGIDA NA JKU KUWAKILISHA TANANIA

0
0
Awamu ya pili na mashindano yanayohusisha timu bora za Afrika Mashariki-SportPesa Super Cup yanatarajiwa kuanza Juni 3-10, 2018 nchini Kenya kwenye uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani.Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo kutoka Tanzania ni timu zinazodhaminiwa na SportPesa ambazo ni Simba, Yanga, Singida United pamoja na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi kutoka Zanzibar), wakati kutoka Nairobi timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards na Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Dar es Salaam ambapo pia walikuwepo wawakilishi na viongozi kutoka TFF pamoja na viongozi wa timu za Simba, Yanga na Singida United Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas alisema “michuano hii kuleta chachu na kumpata bingwa kwa upande wa Africa Mashariki”
Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika mapema na ukiangalia muda wa kupewa na taarifa mpaka kuanza ni zaidi ya mwaka mmoja, hivyo basi hakuna sababu kwa timu zetu za Tanania zisifanye vibaya zaidi ya mwaka jana kwani matayarisho yamefanyoka mapema na kwa hali hiyo timu zikifanya vibaya tutakuwa na sababu za kuwalaumu.Kutakuwa na jumla ya timu nane za Afrika Mashariki na mshindi wa michuano hiyo atacheza na moja kati ya timu iliyoshiriki ligi kuu uingereza, Everton.

Timu zitakazoingia robo fainali kwenye mashindano haya watapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola 7,500 na 10,000 kila mmoja.Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park.Napenda kuwatakia kila la kheri timu zetu tatu zinazokwenda kutuwakilisha jijini Nairobi, natumaini zitatutoa kimasomaso kwa kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, wataiwakilisha nchi yetu vilivyo kwa kucheza kwa uweledi na nidhamu” alimaliza Ndugu Tarimba

Kwa upande wa timu ya Simba Ndugu Said Tulliy alisema “Napenda kuchukua nafasii hii kuwataarifu wanasimba kuwa tunakwenda kushiriki mashindano kama timu shindani na si timu shiriki na tunajua mwaka jana tulipata nafasi kama hii lakini tuliipoteza na tusingependa kitu kama hicho kijirudie. 

Tumeona faida yake kutokana na jinsi wenzetu waliopita ni jinsi gani walivyofaidikakupitia mashindano hayo.Kama timu tumejiandaa na tuko tayari kuhakikisha tunalinda heshima ya Simba Sports Club na heshima ya Tanzania, tunakwenda na kikosi kamili ili kuhakikisha tunachukua ubingwa ili tuweze kushindana na timu iliyopangwa.
Tunathibitisha kuwa tutashiriki mashindano haya kwa sababu ni mashindano muhimu, tuko tayari kwa ajili ya mashindano na timu yetu nzima na tuko tayari ya kushinda” alimaliza Ndugu Said Tulliy.
“Changamoto ya mashindano iko pale pale lakini kwa mwaka huu nia yetu kuu ni kuchukua ubingwa ili kuleta heshima kimataifa” Charles Boniface Mkwasa Yanga.

“Kwanza napenda kuwashukuru SportPesa kwa sababu wamefanya timu yetu kujulikana kwenye kila kona ya nchi, moja kati ya wadhamini wetu wa nguvu ambao tunajivunia sana kutoka kampuni hii. Jambo kubwa tutakaloenda kulifanya kwenye michuano hii kimsingi kwa mwaka huu tumeweza kushirikishwa mapema ili tuweze kujipanga sisi kama timu lakini kikubwa zaidi ikumbukwe kuwa Singida United ni timu pekee iliyofanikiwa kufika nusu fainali kwa hapa Tanzania na mwaka huu tunaamini tutachukua kombe
Kwa watanzania na watu wa Africa mashariki tunaombawatuunge mkono timu yetu. Ningependa kuwaomba SportPesa kuhakikisha kanuni na sheria za mpira wa miguu zinafatwa ili michuano hii iweze kumalizika vizuri”–Shabani Mande Singida United.

Tunapenda kuwashukuru SportPesa kwa kututambua na kutupa nafasi ya kushiriki katika michuano hii na napenda kuwaahidi hatutawaangusha ingawa hii itakuw mara ya kwanza kushiriki.” Maalim Masoud, Katibu wa klabu, JKU.

ALIYEWAHI KUWA MBUNGE WA MONDULI KUZIKWA KESHO MJINI LONGIDO MKOANI ARUSHA

0
0
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Monduli na Mkuu wa wilaya Mstaafu, Luteni Mstaafu Lepilal Ole Molloimet aliyefariki Dunia Jumapili iliyopita,anatarajiwa kuzikwa kesho Ijumaa mjini Longido.Kwa mujibu wa msemaji wa familia Mh. Christopher Ole Sendeka, Luten Molloimet amefariki dunia kwa ugonjwa wa shinikizo la damu

REMA 1000 FC YAIBUKA KINARA,YAIFUMUA LAMBO FC MABAO 5-3

0
0
Kurugenzi CUP ’18 yazidi kutimua vumbi katika dimba la shule ya msingi
Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, kwa timu ya Rema 1000 FC kwa
kuigaragaza pasipo huruma timu ya Lambo FC kwa mabao 5-3.

Katika mchezo huo uliofanyika leo alasiri timu hizo zilitoana jasho,
upinzani mkali, katika kulisakata kabumbu na kuonyeshana ufundi,
kwenye mashindano hayo  yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga.

Bao la kwanza la timu ya Rema 1000 FC lilitiwa kimiani na winga
machachari wao Shafii Said wenye dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza
cha mchezo huo.

Mshambuliaji hatari wa timu ya Rema 1000 FC Masudi Juma aliipatia timu
yake bao la pili kwenye dakika ya 29 mara baada ya kuwachambua pasipo
na huruma walinzi watatu wa timu pinzani na kupachika kimiani bao la
kiufundi, hadi mapumziko timu ya Lambo haikuona nyavu ya timu pinzani.

Kipindi cha pili timu ya Lambo FC kupitia kocha wake ilifanya
mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wawili na kuingiza nguvu mpya
ambayo ilibadilisha sura ya mcheo na kuleta maajabu kwenye viwanja
hivyo kwa kurudisha mabao mawili na kuongeza la tatu.

Mchezaji Godfrey Ernest wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom Manyara akimtoka mchezaji wa timu ya Rambo FC pia ya Haydom katika mchezo wao uliofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom katika Mashindano ya  kombe la Kurugenzi Cup 2018 yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo timu ya Rema 1000 FC imeibuka na ushindi wa Magoli 5-3 dhindi ya Rambo FC.
 Wachezaji wa timu ya Rema 100 FC ya Haydom wakishingilia  mara baada ya mchezaji Raurenc Marco kuifungia timu yake ya Rema 1000 FC goli lao la tano katika mchezo huo uliokuwa mkali dakika zote za mchezo.
 Kikosi cha timu ya Rema 1000 FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Kikosi cha timu ya Rambo FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA AFYA

0
0
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wameipongeza Serikali  ya awamu ya Tano kwa kuhakikisha miundombinu ya afya inaboreshwa na kupunguza malalamiko ya kukosekana kwa huduma ya afya kwa jamii.


Wameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Mchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipotembelea  kituo cha afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.



Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema Serikali imeweza kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya  208 kwa  lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya  kwa wakati na karibu na   maeneo wanaoishi.



Wanasema kuwa awali miundombinu mingi ya afya ilikuwa duni, kukosekana kwa vifaa tiba na umbali wa vituo vya afya ilikuwa ni changamoto kubwa kwa jamii hali ambayo ilipelekea wananchi wengi hasa wamama wajawazito kujifungulia nyumbani.

 Majengo ya Kituo cha Afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara yaliyojengwa kwa shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Waziri wa Ardhi Mhe. Willium Lukuvi wakikagua kituo cha Afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akieleza kazi iliyofanyika katika Kituo cha afya cha Sunya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara kwa  Waziri wa Ardhi Mhe. Willium Lukuvi kwa kutumia shilingi milioni 500 zilizotolewa na Serikali.
Baadhi ya wananchi wa Sunya , Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati alipotembelea Kituo cha afya cha Sunya kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY

0
0


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.

Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani. 

Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma. 

Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo. 

“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.
 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya ufunguzi huo wa madarasa na makabidhiano kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza kwenye halfa hiyo kushoto  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizindua madarasa ya shule ya Msingi Bombo Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Selebosi.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 17.05.2018


Mashindano ya CDF Cup mzunguko wa Tano 2018 yafikia kileleni

0
0
Mzunguko wa Tano wa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi “CDF Cup 2018” yanatarajiwa kufungwa rasmi leo tarehe 18 Mei, 2018 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu za mpira wa miguu ya Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 
Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 08 Mei 18 huku yakishirikisha Kamandi zote za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi, Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji na Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 
Timu hizo zimechuana vikali katika michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Mpira wa Mikono, Ngumi za Ridhaa, Riadha na Ulengaji Shabaha. 
 Kamandi zote zimefanya vizuri lakini Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi na JKT zimeonesha ushindani mkubwa katika michezo mbalimbali hadi kufika hatua za fainali. 
Mpaka sasa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi imeonesha kushinda michezo mingi zaidi ikilinganishwa na Timu zingine.
Mchezaji wa timu ya Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi akirusha mpira dhidi ya Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa katika mchezo wao Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam. Picha na JWTZ

Dkt. Mwakyembe awataka Vijana kuiga mfano wa mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata

0
0
Na Loretha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza mwanamitindo wa kimataifa Bibi. Flaviana Matata kwa juhudi za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha  vifaa muhimu vya shule ikiwemo ada na madaftari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Dkt. Mwakyembe amewataka vijana wa kitanzania kuiga mfano wa mwanamitindo huyo ili kuchangia katika ujenzi wa taifa.
“Nawasihi vijana wengine wenye fursa kama za Flaviana Matata kuzitumia vizuri  kwa kuhakikisha jamii inanufaika na mafanikio waliyoyapata” ameongeza Dkt. Mwakyembe
Aidha, aliongeza kwa kueleza kuwa, Mwanamitindo huyo amekuwa ni balozi mzuri katika kupeperusha bendera ya Taifa katika nchi mbalimbali za Ulaya.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amempongeza Bibi. Flaviana kwa kuwa  mfano bora kwa watoto wa kike kwa jinsi ambavyo amekuwa akisaidia watoto wa kike nchini.
Naye Mwanamitindo wa Kimataifa Bibi. Flaviana Matata ameleza kuwa mbali na kujishughulisha na mitindo, ameweza kuanzisha kampuni ya Flaviana Matata Foundation ambayo inasaidia kutoa vifaa vya shule, ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa vifaa zaidi ya 5000 katika shule mbalimbali nchini.
Anazidi   kueleza kuwa, Taasisi hiyo imefanikiwa kurabati shule mbalimbali kwa kujenga madarasa na  kusomesha wasichana 15 ambao wanamaliza kidato cha sita mwaka huu na wengine watano bado wapo shule.
Mwanamitindo huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa jitihada za wazi wanazozifanya katika kusimamia haki za wasanii na hivyo kurudisha hadhi ya tasnia hiyo nchini.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katika)  akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano leo Jijini Dodoma, kulia ni Naibu Waziri  Mhe. Juliana Shonza na kushoto ni Mwanamitindo wa Kimataifa Bibi. Flaviana Matata.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)  akifafanua jambo kwa Mwanamitindo wa Kimataifa Bibi. Flaviana Matata(kulia) katika ofisi za Wizara leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) na kulia ni Mwanamitindo  wa Kimataifa Bibi. Flaviana Matata. Picha na Lorietha Laurence - WHUSM, Dodoma.

kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) ya Bunge la Ireland yatembelea Dodoma

0
0
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Ireland wakutana na kuzungumza na Mtandao wa Wabunge wanawake wa Bunge la Tanzania (TWPG) leo katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Ireland ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Ireland, walioongozwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Paul Sherlock (kulia) baada ya mazungumzo nao yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) kutoka Bunge la Ireland katika tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kujenga urafiki na kubadilishana uzoefu katika utendaji wao wa kazi 
PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE

VOA Swahili: Duniani Leo Mei 17, 2018

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO MEI 18, 2018

Mapacha walioungana Waruhusiwa Kutoka hospitali, Waishukuru Muhimbili

0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewaruhusu mapacha walioungana Maria na Consolata waliokuwa wamelezwa katika hispotali hiyo kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na afya zao kuimarika. 
Pacha hao walikuwa wakipatiwa matibabu na madaktari bingwa wa Muhimbili na  wamepelekwa Iringa ambako watapokelewa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema pacha hao wamesindikizwa na madaktari wa Muhimbili haid Iringa na kwamba wakiwa huo wataendelea kupatiwa matibabu.
 “Consolata na Maria tumewaruhusu leo. Hii ni baada ya madaktari kujiridhisha kwamba afya  zao zimeimarika. Wataalamu wetu wamewafanyia vipimo mbalimbali na pia tumewasiliana na wenzetu wa nje na tukakubaliana tuwaruhusu sasa,” amesema Prof. Museru.
Prof. Museru amesema kwamba pacha hao wamepatiwa machine ya CPAP & Oxygen ambayo itawasaidia kuwapatia tiba endapo watahitaji wakati wakiwa Iringa.
Wakizungungumza kwa nyakati tofauti, Consolata amesema kwamba Muhimbili imewapatia huduma nzuri na wanawashukuru wataalamu mbalimbali waliokuwa wakiwapatia matibabu tangu walipolazwa.
Naye Maria akizungumza kwa furaha amesema hivi sasa anajisikia vizuri tofauli na awali-kabla ya kupelekwa katika hispotali hiyo kwa ajili ya matibabu. Pia, amemshukuru mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili kwa kuwapatia huduma bora za matibabu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na Maria na Consolata leo kabla ya kuanza safari ya kwenda Iringa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai na wengine ni wataalamu waliokuwa wakiwapatia matibabu pacha hao.
 Kulia ni machine ya CPAP & Oxygen ambayo Maria na Consolata wamepewa endapo watahitaji matibabu yanayotolewa kwa kutumia mashine hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwaaga Maria na Consolata leo.
Maria na Consolata wakisaidiwa kuingizwa kwenye gari ikiwa ni safari ya kuelekea Iringa leo. Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili 

Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza atembelea JNIA

0
0

 Koplo Chesco Mbise akimwongoza mbwa anayeitwa Max-Z kuondoka mara baada ya zoezi la kuonesha namna anavyokamata dawa za kulevyia katika mizigo ya abiria kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakati  Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (hayupo pichani) alipotembelea na kuona zoezi hilo. Mbwa huyu ni kati ya wawili waliotolewa kwa msaada na serikali ya Marekani.
Askari Hadson Muhuma akiwa amemshika mbwa anayeitwa Nopi wakati akifanya zoezi la kutambua mizigo ya abiria yenye nyara za serikali zikiwemo pembe za Ndovu, lililofanyika kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya kutembelewa na Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (hayupo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (mwenye suti ya bluu kulia), leo akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Bw. Matthew Rycroft mara baada ya kukamilika kwa zoezi la mbwa wa polisi kuonesha namna wanavyokamata dawa za kulevyia na nyara za serikali katika mizigo ya abiria kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kulia) akiongea na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela baada ya zoezi la mbwa kuonesha namna wanavyobaini mizigo yenye nyara za serikali na dawa za kulevyia  kiwanjani hapo.
Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Bw. Matthew Rycroft (wapili kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa pili kulia) wakimsikiliza Bw. Matt Jenkins (aliyekaa), ambaye ni Afisa wa UK Border Force wa Kitengo cha dawa za kulevyia katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). 
Picha zote na Bahati Mollel wa TAA. 

Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini unaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza

0
0
Na Imani Hezron, Adventist
Mkutano wa Ufunuo wa Matumaini unaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ambapo mafundisho ya Afya, Kaya, Familia na neno la Mungu yanafundishwa. Muhubiri Mkuu kwenye mkutano huo ulioanza Mei 12, 2018 ni Mchungaji Dkt.Mark Finley kutoka Marekani.
Mkutano huo unaanza kila siku kuanzia saa 16:00 alasiri hadi saa 20:00 usiku huku pia yakikujia mubashara kupitia Hope Chanel Tanzania kwenye visimbuzi vya Continental pamoja na Ting bila kusahau kwenye Youtube. Pia yanapatikana 102.1 Morning Star Radio Mwanza na kwenye programu tumishi (Application) za Itune na TAMC.
Kupitia BMG, Karibu kusikiliza wimbo maalumu wa mkutano huo kutoka kwa vijana wa Melodies of Hope.

Waimbaji wa Melodies of Hope wakiimba wimbo maalumu kwenye mkutano wa Ufunuo wa Matumaini Jijini Mwanza.

Mkutano huu ulifunguliwa rasmi Mei 13, 2018 na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba.

Sikiliza wimbo maalum wa mkutano huu hapa chini. 

Balozi Dkt. Abdallah Saleh Possi awasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis jijini Vatican

0
0
Balozi wa Tanzania Dkt. Abdallah Saleh Possi, amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018. Pamoja na Ujerumani, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin pia unahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.
Kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatikani, wakiwemo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.
Mabalozi wengine waliowasilisha hati zao ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi Retšelisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark,  na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia. 
Baada ya uwasilishaji hati, pia Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na jumuia ya Watanzania wa Vatican. Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.

 Balozi Dkt. Possi akikabidhi hati za utambulisho kama Balozi wa Tanzania Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis.
 Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.
 Balozi Dkt. Possi katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Wengine ni Afisa wa Ubalozi Bw. Abdul Mhinte, na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana.
Balozi Dkt. Possi na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana, katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Picha kwa hisani ya Vatican

MKAZI WA NEWALA,SHAKILA AMRI ASHINDA MILIONI 140 SIKU YA MAMA DUNIANIA.

0
0
Mchezo wa namba unaongoza nchini Tanzania wa Tatu Mzuka mapema jana umemtangaza na kumtambulisha mbele ya vyombo vya habari mama aliyejinyakulia kitita cha milioni 140 na wakati huo ‘kumbusti’ mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake.

Shakila Amri Nyani, ambaye ni mkazi wa Newala, Mtwara na mama wa watoto 3 alisherehekea siku ya mama duniani kwa kumpa mama yake milioni 30 kama ishara ya kutambua mchango wake katika siku hiyo muhimu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Bwana Sebastian Maganga alikuwepo kuwakab
idhi hundi Bi Nyani pamoja na mama yake. “Mama zetu ni hazina na hakuna kiwango chochote cha pesa kinachoweza kutosha kulipa upendo, msaada na kazi kubwa walioifanya katika kutulea. Kwa ushindi huu Tatu Mzuka tunaamini Bi Nyani na mama yake watafurahia na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao” alisema Maganga

Bi Nyani, mwenye miaka 38 alikuwepo kuelezea furaha yake na namna ambavyo alicheza mpaka akapata ushindi huo mnono wa milioni 140.“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda mrefu sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama naweza kupata nafasi kama hii. Mimi ni mjasiriamali na ninapanga kutumia pesa nilizoshinda kuongeza mtaji wa biashara yangu” alisema Bi Nyani

Bi Fatuma Bakari ambaye ni mama mzazi wa Nyani aliishukuru Tatu Mzuka kwa kuja na kampeni ya ‘Wiki Maalumu ya mama’ ambayo imemfanya akabustiwa kwa pesa nyingi baada ya mtoto wake kushinda.“Mimi pia nitatumia pesa nilizobustiwa kuwabusti ndugu wengine na kufanya shughuli za maendeleo ili kuboresha hali ya maisha ya familia yangu.” Alisema Bi Fatuma

Maganga alimalizia shughuli kwa kutoa dondoo ya kampeni mpya ilioanza leo – Mzukapaswedi. “Na hapa kinachohitajika ni namba zako 3 tu!! Za Bahati, ambazo zitakufanya ufikie mafanikio yako,iwe ni kuongeza elimu,kununua gari,kujenga frame za maduka, kuwekeza kwenye kilimo, nk, fanikisha matunda ya mzuka-paswedi yako kwa ushindi wa laki 1 hadi millioni 6 kila saa.
Ushindi wa millioni 10 katika mzuka deile leo saa tatu na nusu usiku, na ushindi wa millioni 60, jumapili hii kuanzia saa 3 na nusu usiku, tuma 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na neno mzukapaswedi kutoka 3mzuka, ukishinda Tanzania inashinda.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema jana jijini Dar,wakati wa kumtambulisha mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.
  Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku akifafanua zaidi kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda kitita hicho cha TatuMzuka,aidha kufuatia ushindi huo Shakila pia  'alimbust' Mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.
 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30. 

AZANIA BANK KUWASAIDIA WANAWAKE KATIKA MAPINDUZI YA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
BENKI ya Azania imesema imedhamiria kuwasaidia wanawake katika kipindi hiki cha mapinduzi ya uchumi wa viwanda kwa kuwapatia mikopo mikubwa, ya kati na midogo kwa riba naafuu.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika kongamano la kuwainua wanawake kuelekea katika Mapinduzi ya nne ya viwanda barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' Mkurugenzi Mtendaji wa Azania ambao ndio wadhamini wakuu wa kongamano hilo Charles Itembe alisema wanawake ni kundi muhimu katika kufikia uchumi wa viwanda.

Alisema katika kuhakikisha hilo linafanikiwa pamoja na kukabiliana na hali ya soko ilivyo wameshusha riba za mikopo kwa wafanyabiashara hao.

"Benki nyingi sio sisi tu zimeshusha riba za mikopo hii ni kutokana na hali ya soko, na huenda zikaendelea kushuka hadi pale itakapoonekana imekuwa sawa kulingana na Benki yenyewe" alisema Itembe.

Aidha alisema Benki hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake wanaojihusiha na kilimo kwani kilimo ndio kinategemewa katika kuzalisha malighafi za viwandani na kuongeza kuwa kikitumiwa vizuri uchumi wa kati utafikiwa kwa wakati.

Meza Kuu wakiimba wimbo wa taifa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba yake wakati wa kongamano hilo.
 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Amina Salum Ali, akisoma hotuba yake.

Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka 'Princess of Africa' akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank, Charles Itembe, ambao ndio wadhamini wakuu wa Kongamano la Kuwainua Wanawake kuelekea Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Barani Afrika 'Africa Reconnected Forum' lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

Mwimbaji mkongwe wa Afrika Kusini, Yvonne Chaka Chaka, 'Princess of Africa' akiimba sambaba na msanii wa Bongo Fleva Ally Kiba 'King Kiba'.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATU 129 AMBAO SI RAIA WA TANZANIA WASHIKILIWA KIGOMA KWA KUINGILIA MCHAKATO UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

JUMLA ya watu 129 wanaodhaniwa Kuwa ni wahamiaji wasio rasmi  wamekamatwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wakiwa wamejitokeza katika mchakato wa uandikishwaji wa Vitambulisho vya taifa .

Akizungumza jana baada ya kutembelea Kituo cha Murusi wilayani humo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema watu hao ambao si raia wa Watanzania wamebainika wakiwa wamefika katika vituo vya kujiandikishia ili wapate vitambulisho hivyo jambo ambalo si halali kwa mtu ambaye si raia kuingia kwenye mchakato huo.

Brigedia Gaguti amesisitiza hawata mvumilia yeyote atakaeingilia mchakato huo wakati akitambua yeye si raia na amewataka   Wasimamizi kuhakikisha sheria na tararibu zinafuatwa na kuwabaini wote ambao si raia.

"Tumewashikilia watu hao kutokana na ushirikiano wa wananchi na maofisa wa uhamiaji.Endapo tutabaini raia wa Burundi au Congo kaingilia mchakato huu hatuta sita kumchukulia hatua, niwaombe wale wote ambao si raia mjitokeze kabla hatujaanza kuwabaini,"amesema 
Brigedia Gaguti.

Aidha Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali  mstaafu Emanuel Maganga amekuwa mstari wa mbele kufuatilia mchakato huo mkoani Kigoma na kuwasisitiza wananchi Mkoani kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo watabaini kuna mtu ambae si raia anaingilia mchakato huo kwani endapo watapata vitambulisho watavitumia vibaya kuichafua Nchi ya Tanzania.

Amesema atahakikisha anashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha zoezi hilo linaenda sawa sawa na kusimamia zoezi hilo ipasavyo na kwa weredi mkubwa kutokana na muingiliano uliopo katika mkoa huo.
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live




Latest Images