Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

COST KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA NUNUZI KUPIMA THAMANI YA FEDHA KATIKA MIRADI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Taasisi ya Mkakati wa Uwajibikaji na Uwazi katika Sekta Ujenzi (COST) imesema kuwa itaendelea kushirikiana na taasisi nunuzi katika sekta ya ujenzi kuangalia uwajibikaji na uwazi katika ujenzi wa miradi mbalimbali.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Taasisi ya COST, Mhandisi Kazungu Magili wakati wa mkutano wa Sita wa Mwaka wa Taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kazi ya COST kuangalia miradi ya ujenzi kuwa na uwajibikaji na uwazi ili wananchi kuweza kupata ujenzi bora wa miundombimu mbalimbali inayojengwa nchini.

Amesema kuwa uwajibikaji na uwazi wa nguzo katika kupima thamani ya fedha inayoendana na miundombinu mbalimbali inayotekelezwa nchini.

Magili amesema wadau wana kazi ya kufatilia taarifa katika miradi katika kuweza kufatilia ujenzi wa miundombinu na ndipo umma utatambua uwajibikaji katika rasilimali zao.

Amesema kuwa COST itaendelea kungalia miradi ya miundombinu kuhakikisha taarifa zake zinapatikana kwa kila mdau kwa kila hatua za ujenzi wa mindombinu hiyo.

Sekta ambazo za ununuzi zinazoshirikiana na Tanroad , Tarura pamoja na taasisi ambazo zinasheria katika kufatilia manunuzi ili kuweza kufanya uwajibikaji na uwazi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mkakati wa Uwajibikaji na Uwazi katika Sekta Ujenzi (COST),Mhandisi Kazungu Magili akizungumza katika mkutano wa sita wa taasisi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
.Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya COST, Alhaj Arch Jehad Jehad akizungumza na wajumbe wa COST katika mkutano wa sita wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wajumbe na viongozi wa COST katika mkutano wa sita wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MKAZI DAR MBARONI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOISHA MUDA WAKE

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya kinamshikilia mkazi wa Tabata Segerea Chama jijini Dar es Salaam Joseph Jaumbe( 52) kwa tuhuma za  kukutwa na dawa za binadamu kinyume na sheria huku zingine zikiwa zimepita  muda wake wa matumizi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP), Alhaj Kabaleke Hassan amesema kupatikana kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na taarifa kutoka kwa wananchi kuwa anahifadhi dawa za kulevya ndipo wakafanya uchunguzi na nyumbani kwake hakuwa na dawa za kulevya kama walivyopata taarifa.

Amesema baada ya uchunguzi ndipo wakakuta ana dawa za binadamu zikiwa katika mifuko mbambali huku zingine zikiwa katika mfuko wa sandarusi.

Kamanda Hassan amesema kuwa baada ya kuwasiliana na Mamlaka Chakula na Dawa (TFDA) walipata dawa makopo 12 yenye vidonge 1000 ambazo hazijasajiliwa na mamlaka hiyo, dawa za Serikali makopo mawili ya vidonge 1000 , dawa za zilizoisha matumizi yake uzito wa kilo 25, dawa bandia zilizoisha muda wake makopo saba yenye vidoge 1000 , dawa za mashirika ya msaada makopo 12 yenye dawa 1000 kila kopo pamoja na vingashio za dawa mbalimbali.

Kwa Meneja wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Emmanuel Alphonce amesema Jeshi la Polisi liendelee kufanya uchunguzi kwa mtu huyo kujua dawa anakozipata ili kubaini mtandao huo.

Alphonce amesema dawa hizo ziingeingia mtaani zingeleta madhara kwa binadamu huku akishangaa kwa dawa hizo kufungwa mfuko wa kiroba pamoja na mifuko ya rambo. Amesema kuwa TFDA itaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kulinda watanzania katika matumizi ya dawa , vifaa tiba na vitendanishi.


Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP), Alhaj Kabaleke Hassan akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kukamatwa kwa Mkazi wa Tabata Segerea Chama Joseph Jaumbe( 52) kwa tuhuma kukutwa na dawa za binadamu kinyume na sheria huku zingine zikiwa zimepita muda wake wa matumizi , jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Emmanuel Alphonce akizungumza kuhusiana na dawa zilizokamatwa na jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya , jijini Dar es Salaam.
Dawa zilizokutwa kwa mtuhumiwa Joseph Jaumbe( 52) mkazi Mkazi wa Tabata Segerea Chama Joseph Jaumbe( 52)  

HOTUBA YA WAZIRI UMMY MWALIMU SIKU YA FAMILIA DUNIANI ILIYOSOMWA KWA NIABA YAKE NA MKUU WA WILAYA YA KONDOA.

Mtanzania Afundishaye ki-Swahili Marekani Akifurahia Kitabu Posted: 15 May 2018 03:58 PM PDT

$
0
0
Na Profesa Mbele 
Mimi kama mwandishi ninathamini maoni ya wasomaji juu ya maandishi yangu. Msomaji anapokuwa ametumia muda wake kusoma na kutafakari nilichoandika, halafu akatumia muda wake kuandika maoni, kwangu si jambo dogo. Ninashukuru. Katika blogu hii nina jadi ya kuwatambua wadau hao.
Hivi karibuni, nimeona andiko la Filipo Lubua (pichani chini) katika ukurasa wake wa facebook kuhusu kitabu changu Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Huyu anafundisha ki-Swahili katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh hapa Marekani. Anasema kwamba anakitumia kitabu hiki katika kozi juu ya Afrika Mashariki, na anasema ni kitabu kinachovutia sana. Ananishukuru kwa kukiandika kitabu hiki rahisi kusomeka juu ya mitazamo yetu, yaani sisi wa-Afrika na wenzetu wa-Marekani. Anasema kuwa wanafunzi wake wamo katika program ya masomo ambayo watasoma Tanzania. Watakuwa Dar es Salaam na Iringa kwa wiki yapata tano.

Katika mawasiliano ya ziada, mwalimu Lubua amesisitiza kuwa hiki kitabu muhimu sana hasa katika kufundishia utamaduni wa Kiswahili. Kauli yake hiyo imenikumbusha maelezo ya Leonce Rushubirwa, m-Tanzania mwingine mwalimu wa ki-Swahili Marekani, kuhusu matumizi ya kitabu hiki katika kufundishia ki-Swahili. Kuongea na wataalam wa aina hiyo ni fursa ya kujithibitishia ile dhana kwamba lugha imefungamana na utamaduni.

PANGABOI ZA BOMBADIER ZINAPOPIGWA PICHA KWA KAMERA YA SIMU NA KAMERA YA KAWAIDA

$
0
0
Na Ankal
Unapopiga picha ya ndege inayotumia pangaboi ni muhimu kuhakikisha kwamba kasi ya shata (shutter speed) ya kamera yako sio ya juu sana ama sivyo picha utayopata ni ya pangaboi kuonekana hazitembei wakati ndege ipo hewani, jambo ambalo litaua uhalisia wa picha.


Kwa kawaida kugandisha kitendo (action) ni jambo jema lakini kwa ndege picha itaonekana ya mgando na isiyo na afya. Yaani kama ndege ipo angani na pangaboi zimeganda itaonekana picha isiyotimia. Tatizo kwa wapiga picha wengi hasa wanaotumia simu, aghalabu wakati wa mchana kamera za simu huwa zinajitega kwenye “automatic’ hivyo shata inakuwa kwenye kasi kubwa. Kwa luigha ingine ni kwamba kasi ya shata ikiwa ndogo itaonesha mzunguko halisi wa pangaboi. 

 Hii imepigwa kwa kamera ya kawaida aina ya Canon EOS 5D Mark lll
Hii imepigwa kwa simu ya Iphone 7.

BALOZI WA INDONESIA AAHIDI KUWAALIKA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA NGUO, NGOZI NA MBOLEA KUWEKEZA SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof.Dkt. Ratlan Pardede amewaahidi viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa atawaalika wawekezaji wa Viwanda vya nguo, viwanda vya kuchakata ngozi  na viwanda vya kutengeneza  mbolea kutoka hini Indonesia kuja kuwekeza Mkoani Simiyu.

Mhe. Balozi Pardede ameyasema hayo Mei 15, alipokuwa katika ziara yake Mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea kiwanda cha Kuchambua pamba cha Kasoli Alliance kilichopo Wilayani Bariadi na Kiwanda cha kuchakata ngozi cha Senani wilayani Maswa.

Amesema atawaalika wafanyabiashara kutoka nchini Indonesia kuja Simiyu ili wakutane na viongozi wa mkoa huo pamoja na wafanyabiashara wenzao kujadili juu ya kuongeza uzalishaji wa pamba bora, bei ya pamba na kuona namna ya kuuza pamba ya Simiyu (Tanzania) nchini Indonesia moja kwa moja.

Pamoja na kuahidi kuwaalika wawekezaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za ngozi, Balozi Pardede akiwa katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Senani Maswa ameahidi kusaidia kuleta wataalam kutoka Indonesia watakaosaidia wafanyakazi wa kiwanda kutengeneza bidhaa bora za ngozi na kuwapeleka wafanyakazi hao Indonesia kujifunza na kupata maarifa na uzoefu.

Meneja mkuu wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Bw. Boaz Ogola amesema ujio wa Balozi wa Indonesia ni fursa kubwa kwa wanunuzi wa pamba kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji mkubwa wa pamba kwa ajili ya viwanda vya nguo na utafungua milango ya majadiliano na wafanyanyabiashara wa Indonesia na kufanya biashara ya moja kwa moja.
 Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (wa tatu kulia) akipewa maelezo juu ya hatua za utengenezaji wa kiatu cha ngozi wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi kilichopo Senani wilayani Maswa akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu.
 Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede  akiweka saini katika ubao kwa kutumia Maswa Chalks wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza Chaki  wilayani Maswa akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu.
 Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua Pamba cha Kasoli Alliance kilichopo wilayani Bariadi akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu.
 Meneja mkuu wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Bw. Boaz Ogola(kushoto) akitoa maelezo kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede( wa nne kushoto) wakati alipotembelea kiwanda hicho,  kilichopo wilayani Bariadi akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mhe. Dkt. Seif Shekalaghe ( wa pili kulia) akitoa maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede  (kulia) wakati alipotembelea kiwanda

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILIA IMARA NA TAIFA IMARA

$
0
0
Malezi bora katika familia imesemeka ni ndio msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wanapaswa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota  wakati akisoma Hotuba ya Wziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika  maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Vaileth Makota amesema kuwa wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na katika maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, wanaojithamini, na wenye maadili mema ili kulitumikia Taifa.

Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa walimu kwa matendo yao kwa watoto kwani watoto wanaiga yale ambayo wazazi wanafanya hivyo tabia na mienendo yao ni kati ya vitu ambavyo vitasababisha malezi mabaya au bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.
 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota akiwasisitiza wazazi kuchangia ujenzi wa famila na taifa kwa kuwapa  malezi bora watoto  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bibi Magreth Mussai akizungumzia umuhimu wa malezi bora katika familia na wajibu wa wazazi katika kutoa malezi hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota( wa pili kushoto) akipokea bango la wadau kutoka nchi za ulaya wanaounga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kupinga ndoa za utotoni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.  
Nesi akimchoma mtoto wa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Vanessa Makota Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi katika uzinduzi wa chanjo hiyo Wilayani Kondoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani humo.  
Wanafunzi na Wananchi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma wakifuatilia mambo mbalimbali katika Siku ya Familia Duniani yaliyokuwa yakifanyika katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


Watanzania wahimizwa kuchangamkia shindano la ujasiariamali la TBL

$
0
0
-Mshindi kujinyakulia kitita cha Dola 50,000/-

 Kampuni ya TBL Group, chini ya kampuni  yake mama ya, ABIn Bev, Imewataka watanzania kuchangamkia kushiriki shindano lililozinduliwa  karibuni la wazo la ubunifu kupitia ujasiriamali, ,(The Africa Sustainability Challenge) linalolenga kukabiliana na changamoto zinazolikabili bara la Afrika na changamoto endelevu za kidunia.Ushiriki wa shindano ni kupitia tovuti ya www.challengeaccepted.africa

Washiriki  wa shindano ambao wazo la ubunifu  la ABinBev, litaibuka na ushindi watajishindia fedha za  kuwawezesha kutekeleza wazo lao kwa vitendo kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya shilingi milioni za Tanzania.

 Akiongea juu ya shindano hili jijini Dar es Salaam,Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi,alisema “Tukiwa kampuni kubwa ambayo ina mtandao wa kidunia tuna mtazamo wa kufanya uzalishaji wa vinywaji vya bia sambamba na kupitia vinywaji  hivi kuwaunganisha watu pamoja kwa miaka zaidi ya 100 ijayo,na lengo hili hili lifanikiwe tunahitaji mawazo shirikishi kutoka wadau mbalimbali nchini na barani Afrika kwa ujumla”.

Mutiganzi,alisema mawazo hayo ya ubunifu yanatakiwa kujikita jinsi ya kutatua matatizo yanayolikabili bara la Afrika ambayo baadhi yake ni kuhusu kilimo bora,changamoto ya maji,hali ya  hewa na  kukuza ujasiriamali endelevu.

 Shindano hili la mawazo ya kukabili changamoto la AB InBev Africa linawataka washiriki kutoka nchi mbalimbali kubuni jinsi ya kukabili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao kama vile kukuza sekta ya kilimo,upatikanaji wa maji safi ,kuimarisha mifumo ya maji taka,kuwezesha familia zenye vipato vya chini,mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza wigo wa ajira kwa watu wengi  katika jamii.

 “Hii ni fursa pekee kwa wajasiriamali wenye mawazo ya ubunifu wa kukabiliana na changamoto zilizobainishwa kuweza kujishindia safari ya kwenda Silicone Savannah jijini  Nairobi nchini Kenya sambamba na kujishindi dola za Marekani

50,000 za mtaji wa kuendeleza wazo lililoshinda  pia washiriki watapata fursa ya kushiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo  na kushiriki katika mashindano ya ngazi ya dunia yatakayofanyika mjini Newyork nchini Marekani chini ya uratibu wa kampuni ya ABIn Bev”,alisisitiza.

Shindano hili liko wazi kwa washiriki kutoka nchi za Botswana, Ghana, Lesotho, Mozambique, Namibia, Nigeria, South Africa, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia na mwisho wa kutuma  ni mwisho wa mwezi huu .

RC NDIKILO AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA PWANI

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo(aliyeinama) wakati alipotembelea maduka ya bidhaa ya mafuta ya kupikia na sukari ,Loliondo ,Mailmoja ,Mjini Kibaha,(Wa pili kutoka kulia) ni kamanda wa polisi wa mkoa huo , (ACP) Jonathan Shanna na wa kwanza kushoto mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoani Pwani ,Abdallah Ndauka.(picha na Mwamvua Mwinyi).

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

SERIKALI mkoani Pwani, imewahakikishia wananchi kuwa inawasimamia wafanyabiashara wa mafuta ya kupikia, washushe bei ya bidhaa hiyo ambayo kwasasa inauzwa lita moja sh. 5,000 kutoka sh. 3,200 iliyokuwa ikiuzwa kipindi cha nyuma.

Aidha imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa sukari na mafuta hayo, ambao watajaribu kuficha bidhaa hizo kwa lengo la kujitajirisha haraka haraka baadae kwa kupandisha bei na kudai atakaefanya hivyo atakiona.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliyasema hayo wakati alipotembelea maduka ya bidhaa hizo, Loliondo, Mailmoja, Mjini Kibaha huku akiwa ameambatana na kamanda wa polisi wa mkoa huo, (ACP) Jonathan Shanna .
Alisema Mei 16 mwaka huu, waliamua kutembelea baadhi ya magodauni na maduka ya bidhaa hizo ambapo wamejiridhisha kwa kukuta sukari ikiuzwa bei nzuri na maeneo mengine wakishusha madumu ya mafuta kwa ajili ya kuuzia walaji. Ndikilo alieleza kwamba ,hategemei kuona wala kusikia kuna mfanyabiashara atakaefanya kitendo hicho ili bidhaa hizo ziwe adimu .

“Kama yupo mfanyabishara atakaejaribu kuficha mafuta na sukari kwa uroho wa fedha ,atakumbana na mkono wa sheria na hatutosita kumchukulia hatua za kisheria”

“Serikali inachunguza wote watakaoficha bidhaa hizo ,na jeshi la polisi mkoani hapa chini ya kamanda Shanna linaendelea na misako mbalimbali na kusimamia suala hili na wamejipanga”alisisitiza Ndikilo.

Akizungumzia sukari, Ndikilo ambae pia ni mkuu wa mkoa huo,alisema bidhaa hiyo ilikuwa ikiuzwa 2,600 kwa kilo lakini imeshuka hadi 2,400/2,300.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoani Pwani, Abdallah Ndauka aliwataka wafanyabiashara watoe huduma kama inavyostahili na kwa wakati. Aliwaomba wazalishaji wa bidhaa  viwanda kuzalisha na kusambaza kwa wingi bila kuwakwaza wananchi. Ndauka alisema kuwa,kama chama watawashughulikia wafanyabiashara watakaokwamisha jambo hilo na kuwaasa wawe sehemu ya kutoa huduma stahiki hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Nae kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ,Shanna alisema wameyabeba maagizo yaliyotolewa na kusema wanajua magodauni,store na maduka yote yanayouza bidhaa hizo hivyo asithubutu mfanyabiashara kulijaribu jeshi hilo. Shanna alielezea,ameshayapokea maelekezo kazi yake kubwa ni utekelezaji wa vitendo kwani wanaintelijensia ya kutosha.

Kwa upande wao wafanyabiashara akiwemo Kassim Haji ,alisema mafuta ya kupikia yalipotea lakini kwasasa kuanzia Mei 16 yameanza kuingia na kwa yeye anatarajia kupokea madumu 600. Alisema wanatarajia kushusha bei baada ya kuanza kupelekewa mafuta kwani awali kulikuwa na shida bandarini na anaahidi kushusha gharama ya bidhaa hiyo.

Nao baadhi ya wananchi waliokuwepo soko la Loliondo kwa ajili ya kujinunulia vyakula na bidhaa mbalimbali akiwemo Zulfa Rashid ,alisema bidhaa inayowaumiza ni mafuta ya kupikia. Aliomba mafuta hayo yashushwe bei kwani yanauzwa kwa sh,5,000 kwa lita moja fedha ambayo ni kubwa na maisha ni magumu hasa kuelekea kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Tunaomba gharama zishushwe ,serikali isimamie suala hilo,na tunashukuru mkuu wa mkoa kuja kuzungumza na sisi ,pamoja na kutuhakikishia bidhaa hizo zitashushwa bei.

Zulfa alisema, wengi wao wanatumia nazi na kuacha kununua mafuta kutokana na gharama kupanda tofauti na zamani.

Wateja 996 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure

$
0
0
Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Jeremiah Mwamlenga (kushoto) zawadi ya simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika prmosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Mwanaisha Bakari (kushoto) zawadi ya simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika prmosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Nuhu Munhambo (kushoto) zawadi ya simu janja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika prmosheni hiyo inayoendelea.
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, imewazawadia washindi 996 kutoka sehemu mbali mbali nchini simu za zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

Akikabidhi zawadi kwa washindi 11 jiijini Tanga leo, Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo alibainisha kuwa kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini. ‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini,’ alisema.

Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na hayo, wateja pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo

WAKUU WA MIKOA KANDA YA ZIWA VICTORIA WAKOSOA VIKALI TABIA YA WANASIASA KUIPAKA MATOPE DHAMIRA NJEMA YA SERIKALI KUPAMBANA NA UVUVU HARAMU

$
0
0
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akihutubia  hadhara ya kikosi kazi cha watu 260 alichokiunda kwa ajili ya operesheni Sangara 2018 na Wakuu wa Mikoa mitano inayozunguka Ziwa vicktoria  wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni  hiyo. Picha na John Mapepele

NA JOHN MAPEPELE, MWANZA

WAKUU wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wamekosoa vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa kuipaka matope dhamira njema ya Serikali ya kupambana na uvuvi haramu ulioshamiri katika ziwa hilo na kutaka viongozi wa aina hiyo kutangaza masilahi yao kwenye eneo la uvuvi kabla ya kuwashambulia viongozi wanaosimamia zoezi hilo kwa misingi ya kisheria.

Wakizungumza kwenye kikao cha tathmini ya operesheni sangara awamu ya pili iliyowahusisha Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Makamanda wa Polisi wa mikoa na Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wa mikoa yote inayozunguka Ziwa Victoria jijini Mwanza jana viongozi hao wametaka hatua zaidi zichukuliwe ili kunusuru rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alielezea kuchukizwa na tabia inayoanza kuota mizizi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuipaka matope dhamira nzuri ya Serikali ya kukabiliana na uvuvi haramu na kutaka viongozi wa aina hiyo watangaze masilahi yao kabla ya kuanza kuwashambulia viongozi wanaosimamia operesheni hiyo inayotekelezwa kwa mujibu wa sheria .
  Viongozi wakuu wa Wizara  ya  Mifugo na Uvuvi waliokaa  wakiwa katika picha ya pamoja na makamanda wakuu wa Operesheni Sangara 2018 (waliosimama) wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni  hiyo. 

“Viongozi wanaopinga operesheni ya kupambana na uvuvi haramu ni muhimu watangaze kwanza masilahi yao kuhusu eneo la uvuvi ili wasiendelee kuchafua taswira za viongozi wanaosimamia wizara hii”alisema Mtaka.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema kumekuwepo na dhana zinazojengeka kwamba viongozi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria hawaungi mkono mapambano ya kukabiliana na uvuvi haramu operesheni jambo ambalo alisema ni upotoshaji mkubwa na kwamba Serikali ya mkoa iko mstari wa mbele na kuwabana watendaji wa ngazi zote watakaobanika kufadhili uvuvi haramu.

Alisema ni muhimu operesheni hiyo iwe endelevu na kubainisha kuwa suala la uvuvi haramu haliwezi kumalizika kama hakuna dhamira ya dhati miongoni mwa wasimamizi wa sheria na kwamba uongozi wa mkoa huo hautakubali kuendelea kuwa na watumishi wazembe wataoshindwa kusimamia suala hilo.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alitangaza kuanza kwa awamu ya tatu ya Operesheni Sangara yenye lengo la kupambana na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria sambamba na kutangaza operesheni katika maziwa yote na kuagiza viongozi wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia hatua kali viongozi wa chini wanaobanika kujihusisha na kufadhili uvuvi haramu.
Viongozi wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na sekretarieti ya Operesheni Sangara 2018 (waliosimama) wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni hiyo. 

Pia alitangaza kuunda kanda mpya ya udhibiti na usimamizi rasilimali za uvuvi katika wilaya za Ukerewe na Sengerema huku akiunda ofisi mpya ya Kanda jijini Mwanza itakayokuwa inaratibu shughuli zote katika kanda hizo saba ili kuongeza usimamizi madhubuti wa rasilimali hizo.

Aidha Mpina aliongeza kuwa katika awamu ya tatu ya operesheni hiyo itahusisha pia Mahakama zinazotembea ili kuweza kutoa hukumu huko huko ziwani hali itayowezesha kuondokana kabisa na uvuvi haramu.

Aidha aliwataka watu wote wanaopinga operesheni ya uvuvi haramu wasome takwimu ili kujua ukubwa wa tatizo katika Ziwa Victoria ambapo jumla ya watuhumiwa 3,284 wamekamatwa kujihusisha na uvuvi haramu huku samaki wasioruhusiwa kilo 326,751 , mabondo kilo 5,142 zilikamatwa zikitoroshwa kwenda nje ya nchi na nyavu haramu 566,497 nazo zilikamatwa na kuteketezwa. Pia magari 257, mitumbwi 1278 , pikipiki 269 na injini za mitumbwi 564 vilikamatwa vikihusishwa na makosa ya uvuvi haramu.

Alisema katika baadhi ya maeneo ya Bushengere wilayani Ukerewe wazazi wamewaonya watoto wao kutotumika na mafisadi kwenye uvuvi haramu kwani wakikamatwa wao ndio wanaopata tabu na kutelekezwa ambapo wameweka azimio la kukataa kutumika tena kwenye jambo hilo.

Alisema kutokana na operesheni hizo zinazoendelea za kupambana na uvuvi haramu hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu watu wote wanaopinga na hata kuwaombea mabaya viongozi wa operesheni watapata aibu kubwa kwani idadi ya samaki itaongezeka huku akitoa wito kwa viongozi wa ngazi zote wenye mapenzi mema na nchi kuunga mkono vita hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba alisema wizara hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha sekta ya uvuvi inatoa mchango mkubwa katika pato la Taifa na kwamba operesheni hiyo itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kuhusu operesheni hiyo lakini kila walipofuatilia kupata ushahidi wa malalamiko hayo waliukosa jambo ambalo wamebaini kuwa ni njama za makusudi za kutaka kuhujumu nia njema ya Serikali ya kupambana na kutokomeza uvuvi haramu.

Kamanda Mkuu wa operesheni hiyo kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Hassan Shelukindo alisema katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 22 wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji na viongozi wa BMU wamefungwa jela huku wengine 17 mashauri yao yakiwa yanaendelea Mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na uvuvi haramu.

Shelukindo alisema pia watumishi 6 walikuwa kwenye operesheni hiyo waliondolewa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili ya kazi ambapo watumishi hao watachukuliwa hatua za kinidhamu na taasisi zao huku jumla ya sh. bilioni 7.5 zikikusanywa kutokana na faini pamoja mauzo ya mabondo,samaki na kayabo.

DC SHINYANGA AZINDUA RASMI ZOEZI LA KUGAWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI

$
0
0
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Mei 16,2018 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga. Mkuu huyo wa wilaya amekabidhi vitambulisho 12,918 kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa hiyo watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi. 

“Hapa nchini, hili ni zoezi la kwanza la ugawaji vitambulisho kwa wananchi kwa kutumia ugawaji wa mkupuo,tunaanzia katika manispaa ya Shinyanga,nakabidhi rasmi vitambulisho hivi kwa maafisa watendaji wa kata ambao watagawa vitambulisho kwa wananchi”,alieleza Matiro. 

Aidha aliwataka maafisa watendaji kuwa makini na kugawa vitambulisho hivyo haraka huku akisisitiza kuwa vitambulisho hivyo havitolewi kwa ubaguzi bali kila mwananchi ana haki ya kupata. 

“Zoezi kujiandikisha linaendelea katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga lakini kwa upande wa manispaa ya Shinyanga tumemaliza zoezi la uandikishaji kinachoendelea sasa ni kugawa vitambulisho,hili ni zoezi endelevu wale ambao hawajiandikisha wafike katika ofisi za NIDA kujiandikisha ili wapate vitambulisho”,aliongeza Matiro. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiwasisitiza maafisa watendaji wa kata kuwa makini katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wananchi ili kuepuka changamoto inayoweza kujitokeza ya kupotea kwa vitambulisho.
Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau akisoma taarifa ya zoezi la uandikishaji na utoaji vitambulisho vya taifa katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa.
Maafisa watendaji,madiwani na watumishi mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.

BoT YAAMUA KUZIUNGANISHA BENKI ZA TWIGA NA BENKI YA TPB

$
0
0
*Mali, madeni, wafanyakazi kuhamishiwa TPB, wateja waombwa kuwa watulivu

Na Said Mwishehe, Globu

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema Serikali ikiwa mmiliki mkubwa wa Twiga Bancorp imeamua kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa benki hiyo kwa kuiunganisha na benki TPB.

Akitangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam Naibu Gavana wa BoT Dk.Bernard Kibesse amesema kutokana na uamuzi huo wataja wa benki ya Twiga kuwa watulivu katika kipindi cha uunganishwaji wa benki hizo na kuendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaotolewa na menejimenti ya benki ya TBP.

Dk.Kibesse amesema muungano huo umeifanya BoT kusitisha usimamizi wa benki ya Twiga na masuala yote kuhusu benki ya Twiga Bancorp yatafanywa na benki ya TPB kuanzia kesho(Mei 17 ,2018)."Benki mpya ya TPB itakuwa na mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa kisheria chini ya kifungu cha 17 cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006,"amesema Dk.Kibesse.

Akifafanua kuhusu uamuzi wa kuunganisha benki hizo mbili, Dk.Kibesse amesema kwa mujibu wa Sheria ya mabenki na taasisi za fedha mwaka 2006, BoT imepewa mamlaka ya kusimamia shughuli zote za kibenki na taasisi za fedha nchini kwa lengo la kuhakiksha uimara na ustahimilivu wa sekta ya kibenki na fedha kwa ujumla.

"Ikumbwe BoT kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha sheria hiyo namba 56(1)(g)(i) namba 56(2)(a)-(d) Oktoba 28 mwaka 2016 iliiweka chini ya usimamizi wake benki ya Twiga Bancorp.

"Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na benki ya Twiga kuwa na upungufu mkubwa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Babenki na Taasisi za fedha mwaka 2006 na kanuni zake,"amesema.Amefafanua kwa wakati benki hiyo ilikuwa inahatarisha usalama wa sekta ya fedha  na pia kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kulihatarisha usalama wa amana za wateja wake.

Hivyo katika kuboresha utendaji na ufasini wa benki zinazomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Serikali ikiwa mmiliki mkubwa wa Twiga Bancorp imeamua kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa benki hiyo kwa kuiunganisha na benki ya TPB.

Dk.Kibesse amefafanua kutokana na uamuzi huo mali, madeni na wafanyakazi wa benki ya Twiga wote watahamishiwa TPB huku akifafanua BoT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki  kwa lengo la kuleta uthabiti katika sekta ya fedha.

Ameongeza dhamira ni kuimarisha sekta ya mabenki na taasisi za fedha na mikakati ya Serikali ni kuimarisha mabenki kwa kuangalia namna ya kuzifanya kuwa na benki chache zenye tija.

SANLAM, MAXCOM KUWAWEZESHA WATEJA WA BIMA KUFANYA MALIPO KWA NJIA YA SIMU ZA MKONONI

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu 

WATANZANIA watapata fursa ya kufanya malipo ya bima mbalimbali kwa njia rahisi zaidi kupitia simu zao za mikononi baada ya kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance na Maxcom kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara.

Akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman amesema sheria ya bima imebadilika, hivyo kuwataka wateja wa bima kufanya malipo yao  moja kwa moja kwenye kampuni za bima.

“Sheria ya bima huwa zinabadilika mara kwa mara kwa sasa sheria inamtaka mteja wa bima kufanya malipo bila kupitia kwa dalali au mawakala wa bima na tumegundua njia rahisi ya kuwawezesha wateja wetu ni hii ya kufanya malipo ni kupitia simu zao za mikononi,” ameongeza Suleiman.

Amesema utaratibu huo wa kulipa malipo ya bima kwa njia ya simu za mikononi unalenga kupanua wigo wa kulipa malipo na kuimarisha makusanyo ya michango na kumsaidia mteja wao kufanya malipo kwa njia rahisi zaidi ndani na nje ya nchini.

Amesisitiza kwa takwimu za hivi karibuni takribani asilimia 62 ya Watanzania wana miliki simu za mikononi ambapo ni sawa na watu milioni 20 lakini wanaofanya malipo ya bima  hawazidi laki moja.“Kwahiyo tumeamua kuungana na hawa ndugu zetu wa Maxcom ili kuwarahisishia wateja wetu kufanya malipo ya bima kwa njia ya simu za mkononi,"amesema Suleiman.

Hivyo amefafanua umuhimu wa kuingia kwenye malipo kwa njia ya simu kwa kuwa kwa mwaka watanzania wanaofanya malipo kwa njia ya simu za mkononi ni wengi na takribani Sh.bilioni 1.4 kwa mwaka miamala kwa njia ya simu hufanyika.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Jameson Kasati amefafanua mfumo wa kampuni yao wa kielectroniki ni imara na salama kwa wateja wa bima nchini kufanya malipo mbalimbali kama michango na kulipa ada kwa wakati wakiwa mahali popote.

“Tumejiunga na ulipaji wa njia ya kieletroniki na Serikali ambapo pia watu na kampuni binafsi wanaweza kupata fursa hiyo ya kufanya malipo yao kwa njia ya simu za mkononi katika juhudi za kuboresha ulipaji wa huduma mbalimbali nchini,” amesema  Kasati

Ameongeza uzinduzi wa huduma hiyo ni wakati muafaka wa watanzania kuweza kufanya malipo yao ya bima kwa njia ya simu za mkononi kwa mawakala mbalimbali ndani ya nchini. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wa pili kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa, Jameson Kasati, wakisaini  hati za makubaliano ya ushirikiano utakaowawezesha ulipaji rahisi wa bima mbalimbali kupitia simu za mkononi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni maofisa wa Sanlam na wa Maxcom. 
Baadhi ya maofisa wa Maxcom  wakiwa  katika picha ya pamoja na viongozi wa Sanlam Life Insurance katika hafla hiyo.

JENGO LA BEIT EL AJAB KUFANYIWA MATENGENEZO MAKUBWA KUTOKA SEREKALI YA OMAN

$
0
0
  JENGO la kihistoria la Beit el ajab liliopo Forodhani Mjini Zanzibar linalotarajiwa kufanyiwa matengenezo makubwa na Serekali ya Oman baada ya kubomoka baadhi ya sehemu zake miaka michache iliyopita.
  WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza katika hafla ya kumuaga  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk ( kushoto) iliyofanyika katika jengo la kihistoria la Beit el ajab Forodhani. Wa kwanza (kulia)  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Amina  Ameir  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Khadija Bakari Ali.
 KATIBU MKUU Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kuhusu matengenezo makubwa ya Jengo la Beit el ajab ambalo lilibomoka miaka michache iliyopita, (kulia)  Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo.
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi zawadi mbalimbali Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Maeneo mbalimbali ya historia ya Zanzibar.
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk baada ya kumaliza ziara yake Zanzibar.
(Picha na Abdalla Omar Maelzo Zanzibar).

DK.SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA CRCC NA CCECC KUTIKA CHINA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Railway Construction Corporation (CRCC) kutoka Nchini China  Bw.Zhuang Shangbiao (kulia)alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Rais wa Kampuni ya Civil Engineering Construction  Corporation (CCECC) Bw.Zhao Dianlong (wa pili kulia) pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara ya hapa Nchini,[Picha na Ikulu.] 16/05/2018.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Kampuni ya Railway Construction Corporation (CRCC) kutoka Nchini China  Bw.Zhuang Shangbiao (kushoto) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Ujumbe wake (katikati) Mkalimani Bw.Julius Liu,[Picha na Ikulu.] 16/05/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Kampuni ya Railway Construction Corporation (CRCC) kutoka Nchini China  Bw.Zhuang Shangbiao (wa tatu kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Rais wa Kampuni ya Civil Engineering Construction  Corporation (CCECC) Bw.Zhao Dianlong (katikati)pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara yao hapa Nchini.

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha


Benki ya CRDB inatarajia kufanya mkutano wake wa ishirini na tatu(23)wa wanahisa wa benki hiyo katika ukumbi wa Kimataifa wa AICC ulipo jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu moja.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei alisema kuwa mkutano huo wa wanahisa unatarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu


Dkt.Kimei alisema kuwa Mkutano huo wa wanahisa wa benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalumu kwa wanahisa wa benki hiyo utakaofanyika tarehe 18 mwenzi huu ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa watapata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali kibenki


Alisema kuwa agenda za mkutano huo ni kupokea na kupitisha taarifa za fedha na ripoti za wakurugenzi kwa mwaka uliopita tarehe 31 mwezi Disemba 2017,kuhidhinisha taarifa maalumu ya gawiyo wa mwaka ,kuchagua wajumbe wa bodi ,kuhidhinisha uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaokupalika kisheria


Dkt Kimei alitoa rai kwa wanahisa wa benki hiyo kuuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo mkuu huku akiongeza kuwa kwa mwanahisa ambaye hataweza kuudhuria anahaki ya kuchagua mwakilishi au wawakilishi kuudhuria na kupiga kura kwa niaba yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha leo ,kuhusu mkutano mkuu wa ishirini na tatu wa Wanahisa unaotarajia kuanza rasmi tatehe 18 na 19 utakaohudhuriwa na wanahisa zaidi ya Elfu moja  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC uliopo jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei kushoto,kulia ni Mkurugenzi wa mikopo James Mabula  kulia 
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa masoko wa CRDB Jadi Ngwale,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei
Waandishi wa habari wakiwa wanafanya mahojiano ya kina kuhusu mkutano huo

UPANDE WA UTETEZI KESI YA 'UCHOCHEZI' INAYOWAKABILI VIONGOZI CHADEMA WATOA MAOMBI YAO ,WAWASILISHA MAPINGAMIZI NANE

$
0
0
Na Karama Kenyynko,Blogu ya jamii

UPANDE wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, wameomba Mahakama kutupilia mbali mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa kuwa yanamapungufu, kisheria.

Maombi hayo yamewasilishwa leo mahakamani hapo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilabard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili Peter Kibatala.Hivyo amewasilisha mapingamizi nane ya kisheria yanayoshambulia uhalali wa hati ya mashtaka na mashtaka dhidi ya washtakiwa.

Katika mapingamizi hayo, Kibatala amedai, kibali cha DPP kina mapungufu ya kisheria kwa sababu haioneshi imetolewa kwa mashtaka yapi  na pia hati ya mashtaka imewataja majina washtakiwa wote bila ya kufafanua na pia imetaja tu kifungu cha sheria ambacho washtakiwa wameshtakiwa nacho 
Amedai, hakuna kibali kilichowasilishwa mahakamani hapo kwa maana hiyo mashtaka dhidi ya washtakiwa yamepelekwa mahakamani hapo bila ridhaa ya DPP.
Amedai Aidha Kibatala ametoa ombi mbadala na kuomba, iwapo Mahakama itashindwa kuifuta hati nzima ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao basi iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria. Ikiwamo shtaka la nne, latano, la sita na la saba.

Alidai, maelezo ya mashtaka hayo yanawachanganya washtakiwa na hawawezi kujitetea ipasavyo. Pia mashtaka hayo kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya (DPP) ambayo haipo kutokana na mapungufu hayo, inaonesha hakuna ridhaa yake.

Amebainisha kwa kuwa mashtaka hayo tajwa kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya DPP, lakini kuwa haipo tunaomba yafutiliwe mbali. Alidai Kibatala.Pia alidai hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu shtaka la pili na la Tatu hayana maelezo ya kutosheleza ya kuwapa washtakiwa msingi na uwezo wa kuweza kujitetea kikamilifu katika kesi hiyo ya jinai.

Alidai, katika shtaka la kufanya mkusanyiko bila kibali hati haijataja watu waliotishiwa na wametajwa kwa wingi hivyo haijulikani ni washtakiwa ama ni watu wengine.

Akiendelea kuwasilisha maoungamizi hayo, kibatala amedai, mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao yamejichanganya na hayaonyeshi walipelekeaje kifo cha Akwilina na hao majeruhi walijeruhiwa na nani na kwa kutumia nini.

MO AKUBALI KUNUNUA ASILIMIA 49 YA HISA ZA KLABU YA SIMBA

$
0
0
Na , Humphrey Shao, Globu ya Jamii 

MFANYABIASHARA maarufu nchini Mohammed Dewji 'Mo' amekubali kununua asilimia 49 za hisa za Klabu ya Simba SC kulingana na maelekezo ya Serikali katika mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo kuwa kampuni.

Hayo yamethibitishwa leo jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Klabu ya Simba ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka huu Haji Manara wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko ya klabu yao.

Pia Manara amesema wanachama wa Simba SC wajitokeze kwa wingi katika mkutano wa mabadiliko ya Katiba utakaofanyika Mei 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini.

"Mkutano huo ulioitishwa na Kaimu Mwenyekiti, Salim Abdallah ‘Try Again’ utaanza Saa 3:00 asubuhi na tayari wanachama wamekwishasomewa ajenda kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya klabu hiyo, kufungu cha nne,"amesema Manara.

Ameongeza mkutano huo unakuja baada ya kufanyika mkutano wa Desemba 3, mwaka jana, ambao uliazimia kumfanya mfanyabiashara Mo Dewji kuwa Mwanahisa mkuu wa klabu katika mfumo mpya wa uendeshwaji wa Simba SC.Mo pekee aliweka dau la Sh.bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada ya klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa Sh. Bilioni 20, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja.

Wanachama 1,320 walihudhuria mkutano uliofanyika Desemba na walitoka Dar es Salaam na mikoa jirani na kwa furaha ya ushindi huo, Mo Dewji alitoa ahadi 10 za kuleta mabadiliko makubwa, ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mazoezi wa nyasi za asili na nyasi bandia na hosteli ya kisasa ya wachezaji.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images