Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RC KIGOMA AHIMIZA WAKUU WA WILAYA, WATENDAJI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUJIKINGA NA EBOLA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga, amewataka Wakuu wa Wilaya, Watendaji na watushi wa idara ya afya kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama Ebola.

Pia pamoja na kuweka uangalizi katika mipaka kuzuia ugonjwa huo usiingie katika mkoa wa kigoma. 

Maagizo hayo aliyatoa jana katika kikao cha kujadili na kupanga mikakati kuhusu njia bora ya kuzuia uingiaji wa ugonjwa wa ebola kutokana na ugonjwa huo kuripotiwa kuwepo katika nchi jirani ya Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo na Mkoa huo kuwa na muingiliano wa wafanya biashara kutoka nchi hiyo na wengine kwenda kwaajili ya biashara kusababisha ugonjwa huo kuingia kwa urahisi nchini.Amesema hatamvumilia nkuu wa wilaya yeyote au ntumishi wa afya atakae kuwa sababu ya kuingia kwa ugonjwa huo.

Ameongeza kwani mkoa wa Kigoma umekuwa ukiongoza katika magonjwa mengi ya mlipuko kama kipindu pindu ambapo umekuwa ugonjwa mkubwa mkoani humo." Mkuu yeyote ambae wilayani mwake kutabainika kunaugonjwa wa mlipuko atachukuliwa hatua.

"Wakuu wa wilaya kazi yenu kubwa ni kutoa elimu kwa wananchi na kuwachukulia hatua watendaji wa afya wasiofanya kazi zao kikamilifu ambao wanasababisha magonjwa hayo kuingia nchini ni wakati wa kuanza kukagua vyoo katika vijiji vyenu," amesema.

Aidha Mkuu huyo amesema hayuko tayari kuona wananchi wanashindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa ya milipuko kwani kazi kubwa ya viongozi ni kuwahudumia wananchi.Pia na wananchi wasimamiwe kuweza kuzuia magonjwa ya milipuko na hakuna haja ya Mkoa wa Kigoma kuwa masikini lazima juhudi zifanyike kuhakikisha mkoa unakuwa salama.
 Baadhi ya Wadau walioshiriki kwenye mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu  Emanuel Maganga akimkabidhi choo cha Kisasa Mkurugenzi wa Kibondo Juma Mnwele kati ya vyoo 756  kwa niaba ya wakurugenzi wenzake kwa lengo la kuvipeleka mashuleni na katka vituo vya afya  kwa lengo la kuepusha na ugonjwa wa kipindu pindu.


TBC, KWESE FREE SPORTS (TV1) KURUSHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA (FIFA) BURE KWA KISWAHILI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

KITUO cha Televisheni ya Taifa (TBC), TBC Taifa na Kwese Free Sports (TV1)  wameingia makubaliano ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya michuano ya kombe la Dunia (FIFA World cup 2018) bure kabisa kwa lugha adhimu ya Kiswahili yatakayoanza 14 Juni hadi 15 Julai mwaka huu huko Moscow Urusi.

Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TBC Dk.Ayoub Rioba amesema huu ni wakati wa wananchi kufurahia michuano hiyo kupitia televisheni ya taifa bure kabisa na kwa lugha ya Kiswahili.

Ameeleza kuwa watanzania wategemee mambo mazuri kupitia Kwese Free Sports wakiwa sambamba na TBC1 na TBC Taifa.Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kwese Free Sports (TV1) Joseph Sayi amesema wameamua kuwaletea watanzania uhuru wa kufurahia bure kabisa kwa kuangalia michuano hiyo na kusikiliza kupitia TBC Taifa kwa lugha ya Kiswahili.

Meneja Masoko TBC Dafrosa Kimbory ameeleza kuwa licha ya watanzania kupata burudani hii pia ni fursa kwa wafanyabiashara kwa kutangaza bidhaa zao na wanaamini watawafikia watanzania wengi zaidi.

Aidha Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano TBC amewashukuru Kwese kwa ushirikiano na kueleza kuwa hii ni fursa kwao katika kubadilishana uzoefu wa kiteknolojia na maudhui na matangazo hayo yataanza hivi punde na kuendelea hadi mashindano yatakapoisha.

Aidha Walter Kimaro mbunifu kutoka TV1 ameeleza kuwa wamejipanga na hadi sasa studio kabambe imeandaliwa kwa shughuli hiyo hivyo watanzania watarajie mambo mazuri kutoka kwao.

Akizungumza kuhusu Kwese Free Sports Mkurugenzi mtendaji wa Kwese Free Sports Mgope Kiwanga ameeleza kuwa Kwese Free Sports ilianzishwa mwaka 2014 ikijulikana kama TV1 na baadaye kuwa Kwese Free Sports na Chaneli hii imelenga kuwaburudisha waafrika na ipo kwenye nchi zaidi ya 10 Afrika.
Mkurugenzi mtendaji TBC Ayoub Rioba (katikati) na Mkurugenzi wa Kwese Free sports wakionesha hati ya makubaliano baina ya vituo hivyo yalilenga kurusha michuano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Mkurugenzi mtendaji wa Kwese Free Sports (TV1) Joseph Swai akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo.

LULU APANGIWA KUFANYA USAFI WIZARA YA MAMBO YA NDANI

$
0
0
*Atakiwa kuripoti kila siku asubuhi, ikitokea akapata ujauzito atapewa likizo
*Ni marufuku kuzungumza na vyombo vya habari ,akitaka kuigiza filamu ruksa
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Msaidizi Idara ya Probesheni na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze amesema mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu amepangiwa kufanya shughuri za usafi wa mazingira katika maeneo ya Wizara hiyo na kwamba atakuwa akifanya usafi kwa saa nne kila siku na atapumzika siku za mapumziko tu.
Nsenza ameitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizunguza na Michuzi Blog ambayo ilitaka kufahamu Lulu baada ya kutolewa jela na kutakiwa kufanya shughuli za kijamii, ni kazi gani amepangiwa kuifanya na itakuwa sehemu gani.
Hivyo akijibu swali hilo amesema kuwa Lulu amepangiwa kufanya shughuli za usafi wa mazingira katika eneo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na alianza kufanya shughuli hizo kuanzia Mei 11 mwaka huu na ataendelea na adhabu hiyo hadi pale atakapomaliza kifungo chake cha nje kwa mujibu wa sheria.
"Lulu amepangiwa kufanya shughuli za usafi eneo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, hivyo ataingia asubuhi kufanya kazi hiyo ambapo kila siku atatumia saa nne kwa ajili hiyo na kisha ataendelea kufanya shughuli zake nyingine. Hivyo yupo hapa na ujio wake umefanya idadi ya wafungwa wanaotumikia vifungo vyao nje ya magereza kufikia 10 ambao wanafanya shughuli mbalimbali eneo hili la Wizara ya Mambo ya Ndani.

"Atakapokuwa hapa hakuna upendeleo , hivyo atafanya kazi kama wafungwa wengine kikubwa ni yeye kufanya kazi hiyo kwa ufasini mkubwa na kuendelea kuonesha tabia njema.Hatutauwa tunamsimamia wakati anafanya usafi na bahati nzuri Sheria ya Huduma za jamii imafafanua vizuri kwa wafungwa ambao wanatumikia vifungo vya nje ya gereza,"amesema Nsenza.

Ameongeza kuwa Lulu atafanya kazi hiyo bila malipo yeyote na kusisitiza ni mfungwa kama walivyo wafungwa wengine na isichukuliwe kuwa yeye tu ndio amepata kifungo cha nje kwani wafungwa wa aina hiyo wapo zaidi ya 12000 hapa nchini.

Alipoulizwa muda ambao Lulu atatakiwa kuripoti kwenye eneo lake la kufanya usafi, Nsenza amejibu kuwa atatakiwa kuingia kati ya saa 12 asubuhi, saa moja asubuhi au saa mbili asubuhi kila siku na atafaya usafi kwa saa nne.Amefafanua kwa Siku za Sikukuu atapumzika na pale anapopatwa na tatizo anaweza kuomba ruhusa na ataruhusiwa kwenda anakotaka.

Pia alipoulizwa kama Lulu atatakiwa kulindwa wakati anatumikia kifungo cha nje, Nsenza amejibu kuwa hatalindwa na mtu yeyote kwani kabla ya kupata kifungo hicho ulishafanyika uchunguzi wa kutosha kuhusu tabia yake na wamejiridhisha hana tatizo na hakuna sababu ya kulindwa."Si kwa Lulu tu bali hata kwa wafungwa wengine wa aina yake nao hawalindwi bali wanatimiza wajibu wao bila kushurutishwa."

Kwa mujibu wa Nsenza ni kwamba Lulu amepata adhabu hiyo kutoka na Sheria ya Huduma za Jamii yenye vifungu 16 na kanuni zake zote 67 atatumikia adhabu yake kwa mujibu wa sheria na kufafanuliwa kuwa sheria hiyo imefafanua kila kitu.

Lulu ambaye ametolewa gerezani Mei 12 mwaka huu(Jumamosi) imefahamika iwapo waandishi wa habari watataka kumhoji cha kwanza yeye mwenyewe atatakiwa kukubali na baada ya hapo ataomba ruhusa kwa mamlaka husika ili afanye mahojiano hayo na iwapo hatafanya hivyo kutakuwa na faini inayoanzia Sh. 500, 000.

"Sheria hairuhusu mfungwa kuingiliwa au kuhojiwa na vyombo vya habari lakini iwapo ataridhia mwenyewe atakubaliwa lakini baada ya sababu ambayo imetolewa kuturidhisha kuwa ipo haja ya kuhojiwa.Sheria hii maana yake ni moja haiko tayari kumzonga zonga mfungwa maana inaweza kuonekana ni unyanyapaa dhidi ya mfungwa.Hivyo kuna taratibu za kufuatwa tu,"amesema.

Ameongeza kuwa sheria hiyo imeeleza kuwa mfungwa atatakiwa kutumikia adhabu yake kwa saa nne kwa siku, hivyo kama kuna mambo anataka kufanya ni ruksa huku akisisitiza katika kifungo hicho wapo wafungwa wanaume na wanawake.Hivyo iwapo itatokea mfungwa mwanamke(akiwamo Lulu) amepata ujauzito atapa likizo na baada ya hapo ataendelea kutumikia adhabu yake.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Probesheni na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze akizungumza na Globu  ya jamii kuhusu mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu aliyepangiwa kufanya shughui za usafi wa mazingira katika maeneo ya Wizara hiyo leo jijini Dar as Salaam .(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)

SADC WATOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA SERIKALI

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeandaa Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa maafisa wa Serikali na taasisi za umma. Warsha hii inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 17 Mei, 2018.

Lengo la warsha hii ni kuwezesha wizara na taasisi mbalimbali za Serikali kufahamu utendaji kazi wa mfumo huu wa SADC ambao unalenga kukusanya taarifa za utekelezaji wa itifaki na programu mbalimbali za maendeleo za SADC ambazo zinatekelezwa ndani ya nchi na kikanda kwa ujumla. 

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa SADC uliridhiwa na Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilichofanyika katika Falme ya Eswatini (Swaziland) mwezi Machi, 2017. Pamoja na mambo mengine, mfumo huu utawezesha pia nchi wanachama kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Kanda uliofanyiwa maboresho wa mwaka 2015-2020 (Revised Regional Indicative Strategic Plan, 2005 – 2020). Mpango huu ndio mkakati mkuu (blueprint) unaosimamia programu zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazotekelezwa SADC. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent E. Shiyo akifungua Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa niaba ya Katibu Mkuu Prof. Aldof Mkenda, kulia kwake ni Meneja Mradi kutoka GIZ Bw. Robson Chakwama na wa mwisho ni mmoja wa Wakufunzi wa Warsha hiyo kutoka SADC Bi. Lerato Moleko 

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), yametolewa kwa Maafisa wa Serikali na Taasisi za Umma, tarehe 15 - 17 Mei,2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkutano ukiendelea
Picha ya pamoja baada ya mkutano.

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI MAOMBI UPANDE WA UETETEZI KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIONGOZI CHADEMA AKIWAMO MBOWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ya kutaka kesi yao ikasikilizwe Mahakama Kuu.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Hakimu Mashauri amesema kuwa amepitia hoja zote za utetezi na upande wa mashtaka, ambapo ameona hoja za upande wa mashtaka hazina mashiko."Natupilia mbali hoja za upande wa mashtaka kwamba kesi iende Mahakama Kuu," amesema ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi May 16,2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali, (PH).

Miongoni mwa hoja za utetezi kutaka kesi hiyo ipelekwe Mahakama Kuu ni kwa sababu kuna uvunjifu wa haki ya msingi ya Kikatiba. Pia shtaka la pili linalowakabili washtakiwa katika hati ya mashtaka linakiuka haki ya msingi ya washtakiwa ya kufanya shughuli za kisiasa za chama wanachotoka cha Chadema.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina Akwiline

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.Mbunge wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Kwa upande wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Ester Bulaya hawakuwepo mahakamani ambapo Wakili Peter Kibatala alieleza kuwa walikuwa safarini kutoka Bungeni Mjini Dodoma kuja Dar es Salaam kuhudhuria kesi lakini wakaharibikiwa na gari.

MFANYA BIASHARA MKOANI RUVUMA AKUTWA AMEHIFADHI BIDHAA CHOONI

$
0
0
Wafanyabiashara Watatu katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma,Wanashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kutunza bidhaa katika maghala yasiyotambulika na serikali, huku mwingine akihifadhi bidhaa katika mazingira hatarishi kwa afya ya mwanadamu.( Chooni).

WAMACHINGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA KUJISAJILI NA KUPATIWA VITAMBULISHO MAALUM

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Arusha.

Wito umetolewa kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi hususani wamachinga kujisajili na hatimaye kupatiwa vitambulisho maalum kwa lengo la kusaidia biashara zao kutambulika, kukopesheka na kurahisisha mawasiliano ya usimamizi wa biashara hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo uliofanyika leo mkoani Arusha, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Fabian Daqqaro amesema ni muhimu wafanyabiashara kutumia fursa hii ya kujisajili ili kurasimisha biashara zao.

“Ni matumaini yangu kuwa, wafanyabiashara wengi wadogo wadogo mkoani hapa, mtatumia fursa hii kujisajili kwa sababu ninafahamu wengi wenu malengo yenu siyo kuwa wafanyabiashara wadogo muda wote, bali mtakuza biashara zenu na kuwa wafanyabiashara wakubwa na hii itawezesha kuchangia mapato ya Serikali,” alisema Daqqaro.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Kodi za Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Abdul Zuberi ameeleza kuwa, zoezi hili la kuwasajili na kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogo limetokana na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

“Ni ukweli usiopingika kwamba, Rais wetu kwa nyakati tofauti amekuwa akiwapigania na kutaka wafanyabiashara wadogo wadogo kutambulika rasmi na kupatiwa vitambulisho ikiwa ni pamoja na kutafutiwa maeneo rafiki ya kufanyia biashara zao,” alisema Zuberi.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Daqqaro (katikati) akizindua usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Wa pili kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Bw. Faustine Mdessa.
Kiongozi wa Kikundi cha Levolosi Machinga Group Bw. Hassan Shayo maarufu kama G akikabidhiwa kitambulisho wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vitabulisho kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hafla hiyo imefanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara wadogo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Daqqaro (wa tatu kulia) akiwa ameketi meza kuu wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hafla hiyo imefanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara wadogo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hafla hiyo imefanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara wadogo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Daqqaro (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi viongozi mbalimbali na wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi baada ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wafanyabiashara wadogo.(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO.

Elimu ya Mlipa Kodi Kutolewa Mashuleni

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali imeona umuhimu wa kuingiza elimu ya mlipa kodi kwenye mitaala ya elimu nchini ili kwajengea Watanzania tabia, mwenendo na mazoea ya kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Lupembe Mhe. Joram Ismael Hongoli juu ya kwa nini Serikali isiingize kwenye mitaala ya elimu somo la umuhimu wa kulipa kodi ili lifundishwe kuanzia shule ya msingi ili wananchi wapate uelewa wa kodi na waweze kulipa kodi kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.

"Serikali inatambua umuhimu wa elimu ya mlipa kodi katika kumjengea mwananchi tabia ya kulipa kodi. Katika somo la Uraia na Maadili kuanzia darasa la III na kuendelea, mtaala umelenga kumjengea na kumuandaa mwanafunzi kuwa mwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya kila siku," alisema Mhe. Ole Nasha.

Vile vile mtaala umelenga kumjengea mwanafunzi kuiheshimu na kuithamini jamii yake kwa kuwa mwadilifu na mzalendo ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu ya kitaifa ikiwemo kulipa kodi.

Aidha amesema, kutokana na umuhimu wa kuwajengea vijana utamaduni wa kulipa kodi, elimu ya mlipa kodi ni jambo muhimu, Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikisha Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) itaendelea kuboresha elimu hiyo ili isisitizwe na kuwekewa mkazo katika mitaala ya elimu kuanzia elimu ya Msingi.


MAKAMU WA RAIS APOKEA VIFAA VYA UPASUAJI KUTOKA UBALOZI WA KUWAIT

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema uboreshaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kama MOI, zitaipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kupokea vifaa vya Chumba Cha Upasuaji wa Watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI) leo tarehe 15 Mei, 2018.“ Aidha kwa namna ya kipekee nakushukuru Mheshimiwa Balozi wewe binafsi na Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano ambao mnaendelea kuipatia Serikali yetu ya awamu ya Tano katika Sekta mbalimbali za maendeleo lakini hasa hasa katika sekta ya afya” alishukuru Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kuwa Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem amekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Afya hapa nchini ambapo leo wamesaidia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 258 ambavyo vitaiwezesha Taasisi kuimarisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Makamu wa Rais amesema msaada huo utaiwezesha Taasisi kuwa na chumba cha upasuaji ambacho kitakuwa maalum kwa watoto tu, hivyo idadi ya wagonjwa watakaopata huduma ya upasuaji itaongezeka kutoka 500-700 kwa mwezi, kufikia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa mwezi na watahudumiwa kwa haraka zaidi.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile  amesema Tanzania iatendelea kuimarisha uhusiano na nchi ya Kuwait kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada haswa msaada inayohusu sekta ya afya.Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem amesema kuwa Wananchi wa Kuwait wana mapenzi makubwa na Watanzania na kuahidi wataendelea kutoa msaada.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto Daniella Wilfred Pallangyo mwenye umri wa miaka 8 ambaye ana matatizo ya kichwa kikubwa wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya baadhi ya vifaa vya upasuaji kutoka kwa Dkt. Karima Khaled wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya chumba cha upasuaji wa watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence  Mattli (wa pili kushoto) alieambatana na Afisa kutoka Ubalozini, Ndg. Sandrine Denti (wa pili kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi  kutoka  kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence  Mattli (kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika  leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli (kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika  leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI KILICHOFANYIKA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo tarehe 15 Mei, 2018  Ofisini  kwake Jijini Dodoma. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA – OFISI YA BUNGE

MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI-MAKAMU WA RAIS

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Mifupa nchini MOI sasa itafanya upasuaji wa mifupa kwa wagonjwa wapatao 1000 kwa mwezi kutoka wagonjwa 500 mpaka 700 baada ya kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake kutoka kwa Serikali ya Kuwait .

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake vyenye thamani ya shilinigi milioni 186 leo katika Taasisi ya mifupa MOI leo jijini Dar es salaam.

“Hii ni faraja kubwa sana kwa Serikali kwani uboreshwaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kubwa kama MOI itaweza kuhudumia wagonjwa wengi Zaidi kutoka wagonjwa 700 kwa mwezi mpaka kufikia 1000 kwa mwezi” alisema Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Balozi wake Jasem Al Najem kwa msaada huo kwani utaisaidia kwa kiasi kikubwa MOI katika kuboresha utoaji huduma hasa katika fani ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi hapa nchini.

H.E. Benjamin Mkapa, former presidents to convene on peace and security in Africa

$
0
0
Former Presidents Benjamin Mkapa of Tanzania, Thabo Mbeki of South Africa and Hassan Sheikh Mohamud of Somalia are expected to meet in Dar es Salaam this week to discuss Africa’s position in the global peace and security architecture. The dialogue, convened by H.E. Mkapa and organised by UONGOZI Institute, is a follow-up to the African Leadership Forum 2017 which was held in South Africa in August last year.
The 2017 Forum had the theme of “Peace and Security for an Integrated, United, and Sustainable Africa”, and was attended by five other former African Heads of State, including H.E. Olusegun Mathew Obasanjo of Nigeria; H.E. Elson Bakili Muluzi of Malawi; H.E. Mohamed Moncef Marzouki of Tunisia; H.E. Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania; and H.E. Hassan Sheikh Mohamud of Somalia. The meeting was also attended by over 100 key African leaders, experts and thinkers working on issues of peace and security.
According to a statement released by UONGOZI Institute, the Forum examined the complex dynamics that fuel conflicts on the Continent, and how Africa can practically navigate these dynamics to secure lasting peace.  Specifically, the area on Africa’s Position in the Global Security Architecture was highlighted as a topic that needed further discussion, which prompted the organisation of this follow-up meeting.
The follow-up meeting will focus on specific conflict areas in the region, discussing the cases of the Democratic Republic of Congo and the Federal Republic of Somalia. H.E. Thabo Mbeki is expected to deliver the Keynote Address, and H.E. Hassan Sheikh Mohamud and Amb. Zachary Muburi-Muita, Executive Secretary of the International Conference on the Great Lakes Region are scheduled to speak at the event.
In addition to the former Heads of State, the meeting will gather 40 high-level practitioners and experts from across Africa. Resolutions from the follow-up meeting will be shared in a public statement at the conclusion of the event.  
About UONGOZI Institute:
UONGOZI Institute is an independent government agency that provides services to senior leaders who have a demonstrable impact upon their society’s development as well as individuals who have been recognised as emerging leaders with the potential to make a positive impact in their societies.

SWITZERLAND YAAHIDI KUIMARISHA UHUSIANO WA KIMAENDELEO NA TANZANIA

$
0
0
Switzeland imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kusaidia Sekta mbalimbali za Maendeleo hasa katika suala la Afya, kuongeza ajira na kukuza ujuzi .

Hayo yamebainishwa wakati wa Mkutano Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango na Balozi wa Switzerland hapa nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, ulioangazia uhusiano kati ya nchi hizo mbili na namna ya kuboresha ushirikiano.

Katika Mkutano huo Waziri Mpango amemuomba Balozi huyo kuangalia uwezekano wa kuwapa mafunzo madaktari Bingwa nchini ili kukidhi uhitaji uliopo hasa katika Jiji la Dodoma ambalo ndio makao Makuu ya Nchi na  idadi ya wakazi wake inaongezeka, na pia kufadhili mafunzo kwa Watumishi wa umma ili kuwajengea uwezo katika kada mbalimbali lengo likiwa ni  kuongeza ufanisi wa kazi.

Aidha waziri Mpango aliongeza kuwa miundombinu ya Jiji la Dodoma inahitaji kuboreshwa hivyo Switzerland iangalie uwezekano wa kufadhili miradi ya maendeleo katika Sekta ya Maji na mazingira.

 “Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na mifugo mingi Barani Afrika lakini ufugaji wa mifugo hiyo hauna ubora, kwa kuwa Switzerland imeendelea katika Sekta ya Mifugo fursa ipo ya uwekezaji katika eneo hilo hapa nchini” alieleza Dkt. Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango(Mb), akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Switzerland Nchini  Bi. Florence Tinguely Mattli (kushoto) kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu Jijini Dodoma.
 Balozi wa Switzerland Nchini Bi. Florence Tinguely Mattli, akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati yake na  Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea fursa za uwekezaji zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika Sekta ya Mifugo wakati wa Mkutano na Balozi wa Switzerland Nchini  Bi. Florence Tinguely Mattli (hayupo pichani),  Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiagana na Balozi wa Switzerland Nchini  Bi. Florence Tinguely Mattli (kulia) baada ya kumaliza mazungumzo yaliyolenga kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VYETI VYA WAHITIMU PROGRAMU ZA UUGUZI UKUNGA NA SAYANSI SHIRIKISHI ZA AFYA


TFF YAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWAKABIDHI KOMBE LA CECAFA VIJANA CHINI YA 17 ILI KUWAPA HAMASA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limemuomba Rais Dk.John Magufuli  kuwakabidhiwa Kombe la CECAFA vijana wa chini wa miaka 17 kwa lengo la kuwapa hamasa vijana hao.

Ombi hilo limesemwa leo jijini Dar es Salaam na Rais wa TFF Walaace Karia wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Makao makuu ya Shirikisho hilo. Karia amesema kuwa,wamezunguza na Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe na tayari ameshaandika barua kwenda kwa Rais Magufuli ili kumpa taarifa ya hafla hiyo itakayofanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa.

Mbali na hilo TFF wamemuomba Dk. Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 mwaka 2018.

Kwa mujibu wa Rais (TFF),Karia, amesema wamemwandikia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe yenye ombi la kumuhitaji Magufuli juu ya ugeni huo. Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.

Mbali na Simba kukabidhiwa taji hilo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Magufuli atawakabidhi pia vijana wa Serengeti Boys Kombe la CEFACA chini ya miaka 17 walilolitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwa mabao 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Ngozi, jijini Bujumbura.

Sherehe za Simba na Serengeti Boys zitaanza saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.

WAKALA WA MISITU TANZANIA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WANANCHI KUTUNZA MITI YA MIKOKO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFC) Profesa Dos Santos Silayo amesema ipo haja kwa Watanzania kuhakikisha wanatunza mikoko na kufafanua kuwa mikoko imekuwa ikichukua hewa ukaa mara 10 zaidi ya mimea mingine.

Ametoa kauli hiyo leo wakati wa upandaji miti ya mikoko katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam na kufafanua Wakala wa Misitu Tanzania wataangalia namna ya kufanya kwa kushirikiana na wadau wengine ili kwenye maeneo ya mikoko wananchi ambao wamekuwa wakiipanda na kuitunza mikoko kujipatia kipato kwa kufuga nyuki.

Pia Prof.Silayo amesema katika Taifa la Tanzania wanatoa msukumo wa kuifanya nchi kuwa kijani kwa kuendelea kuhifadhi maeneo ambayo yamehifadhiwa yaendelee kutunzwa, kupanda miti maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na miti na maeneo ambayo yalikuwa na miti na ikaharibiwa basi ni kupanda miti mingine huku akielezea pia kuitunza miti iliyopo.

"Kwa kufanya hivyo nchi itaendelea kuwa ya kijani kama ambavyo ilivyo kauli mbiu ya kuifanya dunia kuwa ya kijani ambapo kwa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu Tanzania tumekuwa tukichukua hatua mbalimbali ikiwamo ya kuhifadhi misitu iliyopo,"amesema.

Akizungumzia mikoko Prof.Silayo amefafanua ni furaha yake kwamba misitu ya mikoko ndio ya kwanza kuhifadhiwa ambapo ametoa historia kuwa ilianza kuhifadhiwa mwaka 1920 na kwa Tanzania ikaanza kuhifadhi miaka nane baadae.

Amesema nchi 121 duniani ndizo zenye mikoko na Tanzania ni ya tisa kwa kuwa na mikoko mingi ikitanguliwa na nchi ya Nigeria.

"Miti ya mikoko ina faida nyingi ikiwamo ya kusaidia kuzuia mmomonyoko kati ya bahari na nchi kavu. Robo ya watu duniani wanaishi karibu na bahari na hivyo mikoko husaidia kuepusha jamii hiyo kutoathirika na mawimbi ya mvua,"amesema Profesa Silayo.


 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania, Profesa Dos Santos Silayo akizungumza leo wakati wa upandaji miti uliofanyika katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka , Globu ya jamii)
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu, Profesa Dos Santos  Silayo (wakwanza kulia alievaa kofia)  pamoja na wadau mbalimbali  wa Mazingira wakipanda miti katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu, Profesa Dos Santosa Silayo akimsikiliza Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Mazingira Mbweni, Husna Hussein wakati akielezea upandaji wa miti ya mikoko ambayo wamekuwa wakipanda tangu mwaka 1998.
 Upandaji wa miti ya mikoko ukiendelea katika eneo la Mbweni Jijini Dar Es Salaam

Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva

$
0
0
OFISA Mkuu wa Idara ya Makumbusho Abdalla Magofu (aliyeshika mwamvuli), akitoa maelezo kwa ujumbe kutoka serikali ya Oman juu ya hali ya jengo la Ngome Kongwe lililoko Forodhani mjini Zanzibar. Kulia kwa ofisa huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Urithi na Utamaduni nchini Oman, Salum Mohammed Mahruki.

Na Salum Vuai, WHUMK

MAANDALIZI ya matengenezo ya jengo la Beit Al Ajaib lililoko Forodhani mjini Zanzibar yameanza kufuatia ziara ya ujumbe kutoka Wizara ya Urithi na Utamaduni ya serikali ya Oman.

Ujumbe huo unaoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Salum Mohammed Mahruki, uliwasili nchini jana Mei 11, na leo ulitembelea jengo hilo kujionea hali halisi ya uchakavu uliosababisha lisite kutumika kama kivutio cha utalii kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Msafara wa timu hiyo pia umemjumuisha mshauri mwelekezi ambaye ni mtaalamu wa uhifadhi majengo Dk.  Enrico d’Errico, ambaye amekuja mahsusi kushauri njia bora ya kulitengeneza jengo hilo na mengine ya kihistoria nchini.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha watendaji wakuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Urithi na Utamaduni ya Oman Salum Mohammed Mahruki, aliomba jengo hilo lisafishwe haraka, wakati wataalamu wakifanya tathmini ya kina ili kujua ukubwa wa kazi hiyo.
MSHAURI Elekezi na mtaalamu wa uhifadhi majengo kutoka Wizara ya Urithi na Utamaduni nchini Oman Dk. Enrico d’Errico (kushoto), akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Salum Mohammed Mahruki na wajumbe wengine, walipolitembelea jengo la Beit El Ajaib mjini Zanzibar, ambalo serikali ya Oman inakusudia kulifanyia matengenezo makubwa.

“Kwa namna tulivyoliona jengo hili, ni lazima kazi ya kulitengeneza ianze haraka iwezekanavyo, vyenginevyo tutazidi kuchelewa kwani tayari muda mwingi umepotea tangu lilipopata hitilafu,” alisisitiza.

Alifahamisha kuwa, sura ya Mji Mkongwe wa Zanzibar inaongezewa haiba na kuwepo kwa jengo hilo, ambalo kila mtalii anayefika anastaajabishwa na kuvutiwa na utaalamu pamoja na malighafi zilizotumika kulisimamisha tangu mwaka 1883. Aliongeza kuwa, serikali ya Oman chini ya uongozi wa Sultan Qaboos bin Said, na kwa mahaba aliyonayo kwa Zanzibar na watu wake, imedhamiria kwa dhati kusaidia kwa asilimia 100 ujenzi wa jengo hilo na kulifanya liwe la kisasa zaidi bila kuathiri taswira yake ya kale. Aliomba ushirikiano wanaoupata kutoka serikalini na wananchi wa Zanzibar uendelee ili kuifanya kazi hiyo iwe nyepesi ingawa inaonekana kuwa ngumu kutokana na sanaa ya ujenzi wake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe wa Zanzibar Issa Sariboko Makarani, mpango wa kulifanyia matengenezo jengo hilo umepata  baraka zote kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambako Mji Mkongwe wa Zanzibar umeorodheshwa miongoni mwa miji ya urithi wa kimataifa.

Alisema ukaguzi wa jengo hilo na mengine matatu waliyoyatembelea, ni sehemu ya makubaliano ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Oman yaliyofikiwa mjini Muscat takriban wiki mbili zilizopita juu ya mpango wa kuyatengeneza majengo hayo. Alieleza kuwa, matengenezo ya Beit El Ajaib yanahitaji utaalamu mkubwa, hivyo pande zote mbili zimekubaliana kuwa wakandarasi watakaopewa kazi hiyo ni wale wanaokidhi viwango vinavyohitajika, ambao huenda wakawa wengine kwa kila mmoja kupewa eneo lake.
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe Zanzibar Issa Sariboko Makarani, Katibu Mkuu wa Urithi na Utamaduni wa Oman, watendaji wakuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakiliangalia kwa nje jengo la Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Unguja, walipofanya ziara kukagua majengo ya kihistoria yanayohitaji kufanyiwa matengenezo.

“Tunatarajia matengenezo haya yatakapokamilika, jengo hili litakuwa na muonekano wa kisasa na mvuto wa ziada, ambao tunaamini litavutia watalii wengi zaidi kuliko wale waliokuwa wanakuja kabla,” alieleza Mkurugenzi huyo.

Ujumbe huo pia ulitembelea jengo la Makumbusho ya Kasri, Ngome Kongwe na iliyokuwa nyumba ya kulelea watoto yatima Forodhani ambayo yote yanakabiliwa na uchakavu mkubwa.  Hata hivyo, kwa sasa serikali inaifanyia matengenezo nyumba iliyokuwa ya kulelea watoto yatima, ili itumike kuhifadhi vitu na kumbukumbu zote zitakazohamishwa kutoka Beit El Ajaib kupisha matengenezo hayo.        

Kwa mara ya kwanza, baadhi ya kuta za Beit El Ajaib ziliporomoka mwezi Disemba 2012, na baadae Novemba 2015, na tangu hapo serikali imelifunga kwa matumizi yoyote, hali inayochangia kukosa mapato kutokana na ziara za kitalii zilizokuwa zimezoeleka kuonekana pahala hapo.

Mradi wa Bomba la Mafuta watoa ajira za awali kwa Vijana zaidi ya 200

$
0
0
Vijana zaidi ya 200 wamepata ajira ya kufanya  utafiti  wa athari za kijamii na kiuchumi katika njia ya Bomba la Mafuta Ghafi la  Afrika Mashariki kutoka Hoima Nchini  Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Vijana hao tayari wamepata mafunzo ya kazi  yaliyotolewa jijini Dar es Salaam na kampuni ya Digby Wells Consortium (DWC) kwa kushirikiana kampuni nyingine  za kitanzania na za  kimataifa kama  Digby Wells Environmental ( kampuni ya kimataifa yenye makao makao makuu nchini Afrika ya Kusini na Uingereza) na Paulsam Geo-Engineering Ltd (Kampuni ya Kitanzania inayotoa huduma za ushirikishwaji wadau, upimaji wa ardhi na  watakwimu wa mambo ya kijamii na uchumi ).
Kampuni nyingine zilizotoa mafunzo kwa vjana hao ni Whiteknights Real Estate Investment Analysts Ltd (kampuni ya Kitanzania inayotoa huduma za uthamini) na STCL (kampumi ya Kitanzania  inayotoa huduma za Afya na usalama na usafiri kwa makampuni ya  DWC).

Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa wahusika uelewa wa kufanya  tathmini  ya athari mbalimbambali za  kiuchumi na kimazingira katika maeneo yatakayopitiwa na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.

Mara baada ya kumalizika kwa mafunzo  husika, vijana  wataanza kazi  tarehe 16 Mei, 2018 chini ya kampuni ya kizalendo ya Paulsam ambayo ni mkandarasi  anayetekeleza kazi hiyo kwa kushirikiana na kampuni nyingine.
Zoezi hili litatekelezwa na Makundi 9 yatakayogawanyika katika Mikoa 8 bomba linapopita, Wilaya 25, kata 132 na Vijiji Zaidi ya 280. Aidha, zoezi litahusisha  kubaini athari za utwaaji ardhi  kwa ajili ya  Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), na kutengeneza mifumo ya kuzuia, kupunguza na kudhibiti athari mbaya kwa watakaoguswa na mradi, na kutengeneza mpango wa uhamishaji makazi kupisha Mradi wa Ujenzi wa Boma la Mafuta 
Kazi hii inajumuisha  ukusanyaji wa  taarifa za  ardhi na  rasilimali  kwa ajili ya uthamini na hatimaye  utwaaji wa ardhi ambayo itahitajika kwa ajili ya ujenzi wa njia ya bomba la mafuta  kabla  ya muda wa kuanza ujenzi. 
Zoezi hili litahusisha pia, uorodheshaji wa mali zote zisizohamishika na makaburi ndani ya eneo lililochaguliwa na mradi. 
Zoezi litatekelezwa kwa kutumia teknolojia ya vifaa vya kisasa (tablets)  kuchukua na kutunza takwimu. Mwisho fomu yenye rekodi itatolewa na kusainiwa na wahusika wote na nakala atapewa mhusika na kusaidia kubaini namna wahusika watakavyokuwa wameathirika. 
Katika zoezi hilo vijana watafanya kazi kwa kushirikiana na wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)

GCLA Watoa Mafunzo kwa Wasimamizi 60 wa Kemikali

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imetoa mafunzo kwa wasimamizi wanaohusika na shughuli za kemikali wapatao 60 wa Kanda ya Mashariki yatakayowasaidia kuzuia matatizo yanayosababishwa na uelewa mdogo wa masuala ya kemikali.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefunguliwa  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma ya Vinasaba, David Elias kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Fidelice Mafumiko.

Mkurugenzi Elias amesema kuwa kemikali zina umuhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu lakini pamoja na faida hizo, kemikali zikitumiwa vibaya zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu na mazingira.

“Ili kudhibiti madhara yanayosababishwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali mbalimbali Mamlaka imepewa jukumu la kutoa mafunzo kuhusu usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa wasimamizi wa shughuli hizi hivyo Mamlaka imeshatoa mafunzo kwa wasimamizi 86 kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu,”alisema Elias kwa niaba ya Dkt. Mafumiko.

Elias amefafanua kuwa kabla ya kuwekwa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani, kemikali zilikuwa zikiingizwa nchini kiholela na kutumika pasipo usimamizi lakini baada ya sheria kupitishwa na kuanza kutekelezwa Mamlaka hiyo imepunguza madhara mbalimbali yanayoweza kusababishwa na matumizi ya kemikali.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,  Bw. David Elias (kushoto) akizungumza na washiriki wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wasimamizi wa shughuli za kemikali viwandani na kwenye makampuni yanayojihusisha na shughuli za kemikali katika Ukumbi wa CEEMI, Dar es Salaam.  Mafunzo hayo yameandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga (aliyesimama) akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya usimamizi salama wa kemikali yaliyoandaliwa na Kanda ya Mashariki na kuanza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CEEMI, Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya usimamizi salama wa kemikali wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zinatotolewa na wawasilishaji kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki kwa  wasimamizi wa shughuli za kemikali kwenye Viwanda, Taasisi na Makampuni mbalimbali yanayojihusisha na shughuli za kutumia, kuhifadhi, kusafirisha, kuagiza na kuuza kemikali mbalimbali nchini.
Wakurugenzi na Meneja wa Kanda ya Mashariki kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (waliokaa) wakiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya usimamizi salama wa kemikali yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa CEEMI, Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamefunguliwa na kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba Bw. David Elias (aliyekaa katikati), kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali,    Dkt. Fidelice Mafumiko.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images