Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 21 | 22 | (Page 23) | 24 | 25 | .... | 3286 | newer

  0 0
 • 01/18/13--12:20: gado leo


 • 0 0


  Mstahiki Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda (kulia).
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini daftari la wageni la Shule ya Sekindari Azania katika sherehe za mahafali ya Kidato cha sita shuleni hapo.
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Azania.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akiwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam Ijumaa, jan 18, 2013. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.
  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally saleh akiongea katika mkutano na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliokutana na Tume kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Harry Kitillya (mwenye tai nyekundu) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba (wa sita kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodiu ya TRA Bw. Bernard Mchomvu (wa nne kutoka kushoto) mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowasa mara baada yakushuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam wakitokea mjini Dodoma.Mh. Pinda alikuwa Dodoma katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Serekali za mitaa.Nyuma yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa (TAMISEMI),Mh. Hawa Ghasia akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana ambaye alikuja kumpokea Waziri Mkuu uwanjani hapo.

  0 0

  Mabingwa wa soka Tanzania Bara,Simba wameshindwa kutamba mbele ya Wenyeji wao mara baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Jeshi la Oman. mechi hiyo ilichezwa Ijumaa jioni kwenye uwanja wa Qaboos Complex jijini Muscat. bao la simba lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'Boban' huku Mwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa simba, Rahma Al Kharoos na Musleh Rawahi pamoja na Kocha Talib Hilal wakiishuhudia Simba ikizama mbele ya wanajeshi hao ambao kikosi chao kina wachezaji tisa wanaocheza timu ya Taifa ya Oman.  PICHA NA SALEH ALLY.

  0 0


  Ngoma ya The Commodores ya 'Nightshift' ya mwaka 1985 ilikuwa balaa

  0 0

  Ngoma ya 'Dr Beat' ya Gloria Estefan ilikuwa sooo..!

  0 0
 • 01/18/13--22:33: Article 20

 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
  WAZEE WA KAZI
    MOT, VOSA, MOT!
  UKAGUZI WA MAGARI MOT/VOSA SASA KUFANYIKA KWENYE OFISI ZETU

  KIFURUSHI KWA NDEGE £1.80
  RATIBA YA MELI MPYA
  Vessel: Asian Vision v122
  CLOSING DATE 22/01/2013
  KUONDOKA: 24TH January 2013
  Eta: Mombasa: 18th Feb 2013-01-02
  Eta: Dar Es Salaam: 15th Feb 2013-01-02


  VEHICLE INSPECTION FOR KENYA & UGANDA NOW CAN BE DONE IN OUR OFFICES
  JUST DROP YOUR  CAR IN OUR OFFICE AND WE WILL INSPECT IT AND DELIVER IT TO THE PORT FOR YOU
  kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote tutumie email au tupigie kwenye namba zifuatazo;

  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
  SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
  HASSAN (RICHARD) +44 07405159255
  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh. Raymond Mushi (katikati),Meya wa Manispaa ya Ilala,Mstahiki Jerry Silaa na Mh. John Chiligati wakishirikiana kwa pamoja kufanya usafi katika Fukwe ya Ocean Road jijini Dar es Salaam,mapema leo asubuhi ikiwa ni Muendelezo wa kuhakikisha Halmashauri ya Ilala inaongoza kwa Usafi jijini Dar.Zoezi hilo limeendeshwa na Kampuni ya Kisasa ya Green WastePro Ltd ambayo ndio yenye Zabuni ya kufanya Usafi katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.na leo wameanza na Fukwe hii na kisha baadae wanaenda kwenye Fukwe ya Mchafu koge na sehemu nyingine nyingi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kisasa ya Usafi ya Green WastePro Ltd,Anthony Mark Shayo (kushoto) akishirikiana na Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni yake hiyo kuondoa tairi chakavu lililokuwa limejifukia kwenye mchanga wa ufukwe wa Ocean Road jijini Dar,wakati wa zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe huo lililoanza kufanyika mapema leo asubuhi na kuudhuliwa na watu mbali mbali.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya kisasa ya Usafi ya Green WastePro Ltd wakiendelea na zoezi la kufanya usafi katika eneo la fukwe ya Ocean Road jijini Dar mapema leo asubuhi.
  Baadhi ya wadau wa Kigeni waliojitokeza kufanyikisha zoezi hilo nao wakiendelea kuwajibika.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh. Raymond Mushi (wa pili kushoto) akimuonyesha kitu Meya wa Manispaa ya Ilala,Mstahiki Jerry Silaa (wa tatu kushoto) wakati wa zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe wa Ocean Road jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.Zoezi hilo limeendeshwa na Kampuni ya Kisasa ya Green WastePro Ltd ambayo ndio yenye Zabuni ya kufanya Usafi katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.Kushoto ni Mh. John Chiligati ambaye nae alishiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
  Baadhi ya vijana wa Ilala Jogging Club wakishiriki kwenye zoezi la kufanya usafi kwenye Zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe wa Ocean Road lililoendeshwa na Kampuni ya Kisasa ya Green WastePro Ltd ambayo ndio yenye Zabuni ya kufanya Usafi katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.


  0 0


  0 0


  BARAZA LA VIJANA MSIKITI WA RAHMANI NAMANGA MAKANGIRA MSASANI KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

  LINATOA PONGEZI KUBWA KWA TIMU NZIMA YA MICHUZI BLOG, KITUO CHA POLISI OYSTERBAY NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI VILIVYOCHANGIA KUPATIKANA KWA MZAZI WA MTOTO MICHAEL LAZARO JANA TAREHE 18/01/2013.

  MAKABIDHIANO YALIFANYIKA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY NA KITUO CHA TELEVISHENI CHA STAR TV – KILIKUWEPO ENEO LA TUKIO MUDA HUO NA KITARUSHA TUKIO HILO LEO USIKU SAA 2.

  AHSANTENI SANA.

  UONGOZI WA BARAZA LA VIJANA
  AMIRI/ MWENYEKITI: 0779 644934/0715 344 934
  NAIBU KATIBU:            0652 005 497
  MJUMBE:                        0715/0784 816 040

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,(katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Juliun Raphael,alipowasili katika Viwanja vya Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,kuufungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui.
  Wadau wa Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara ZBC wakiwa katika Mkutano Uliofanyika kwa kujadili masuala mbali mbali ya kukuza Uchumi wa Taifa ,Mkutano huo ulifanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.
  Wajumbe wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar,kutoka Taasisi na Makampuni mbali mbali ,wakifuatilia kwa makini taarifa na mada zilizotolewa katika mkutano huo,uliofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel,Mjini Unguja.
  Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisikiliza kwa makini mada mbali mbali zilizotolewa katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
  Baadhi ya watendaji wa Taasisi mbali mbali wakifuatilia kwa makini agenda za mkutano wa Saba ( 7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

  0 0


  UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA WAAHIRISHWA
  Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahirisha uchaguzi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliokuwa ufanyike leo (Januari 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

  Uchaguzi umeahirishwa kwa vile ulitaka kufanyika bila kuzingatia Katiba ya TAFCA Ibara ya 32(1) na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 10(6) na 26(2), hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeahirisha uchaguzi huo kwa vile nafasi zilizoombwa kugombewa na idadi ya waombaji uongozi haikidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA.

  Pia taratibu za kikanuni ikiwa ni pamoja na kuwaarifu waombaji uongozi ambao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA hazikukamilika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

  Licha ya upungufu huo, TAFCA haikuwasilisha taarifa za mchakato mzima kama ilivyoombwa na TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA kuandaa uchaguzi mpya utakaokidhi matakwa ya Kamati ya TAFCA baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF.

  TFF inaishauri TAFCA kutumia fursa ya Mkutano Mkuu wa leo (Januari 19 mwaka huu) kujadili mustakabali wa TAFCA kwa kuwa chama hicho kimeshindwa mara mbili kupata idadi ya wagombea wanaokidhi akidi ya Kamati ya Utendaji.

  Pia TAFCA haijawahi kufanya mikutano ya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu kwa karibu miaka minne.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0


  0 0  0 0

  Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa iringa katika pambano la kirafiki la raundi nane katika ukumbi wa D.I.D Hall uliopo mabibo mwasho.

  Mratibu wa pambano hilo Charles Christopher mzazi ameeleza kuwa maaandalizi ya pambano yapo kamili na mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani na wamepima wapo sawa kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo sawa kwa kupambana.

  Mabondia watakaocheza utangulizi ni kama ifuatavyo HAMIS MOHAMED na HARUNA MNYALUKOLO, PENDEZA SHOMARI atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO na KARIMU RESPECT, DOTO MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku ISSA OMAR akizipiga na JUMA J KASHNDE.

  Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe ama bigright amethibisha kuwa kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa na mabondia wapo katika hali nzuri ya kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi wa DID HALL mabibo mwisho kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL RAMADHANI SHAURI na SAID NJECHELE

  0 0

   Mkuu wa masoko na mawasiliano wa NMB Imani Kajula akimkabidhi kitita cha shilingi laki tano Frank Domayo,ambaye ameibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Yanga FC na Black Leopards ya Afrika Kusini,uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo jijini Dar.
   Golikipa wa timu ya Black Leopards,Ayanda Mtshali akijaribu kuokoa mpira uliotinga kimiani kwa njia ya penati na mchezaji wa yanga,Jerson Tegete,penati hiyo ilipatikana katika kipindi cha kwanza,katika kuoenesha Yanga wako fiti mnamo kipindi cha pili mchezaji Frank Domayo akaongeza goli la pili,haikutosha Tegete tena akapachika goli la 3.Mpaka dakika 90 Yanga imetoka kifua mbele kwa magoli 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,Mtanange huo uliandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar.
  Hatari golini kwa timu ya Black Leopards,Golikipa wa timu ya Black Leopards,Ayanda Mtshali akiokoa hatari golini kwake.
   Mchezaji wa timu ya Yanga,Kabange  Twite akimtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.Ama kwa hakika ihiiii ndiyo Yanga ya Uturuki iliotandaza kabumbu safi kabisa ndani ya Uwanja wa Taifa.
   Mchezaji wa timu ya Yanga,Haruna Niyonzima akitaka kumtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,kwenye mchezo wao wa kirafiki unaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa hivi sasa.
   Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mtanange wa Yanga na timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
   Mashabiki wa yanga kibao.
  Picha zaidi Bofya Michuzijr.Blogspot.com

  0 0

  KAMANDA WA POLISI MKOA MBEYA,DIWANI ATHUMAN (WA PILI KUSHOTO) AKIPONGEZANA NA MDAU WA HABARI JIJINI MBEYA,BW. MWAIGAGA KATIKA SHERHE YA KUAGA MWAKA 2012 NA KUUKARIBISHA 2013 ILIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MTENDA JIJINI MBEYA HIVI KARIBUNI.
  MDAU JOSEPH MWAISANGO WA LIBENEKE LA MBEYA YETU HAKUWA NYUMA KATIKA KUPONGEZANA KATIKA SHEREHE HIYO

  RUMBA LIMEANZA SASA.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  MRATIBU wa Mradi wa kuimarisha ushiriki wa Wanawake wenye ulemavu katika kutoa maoni ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Bi. Mwandawa Khamis Mohd,akifungua mafunzo ya siku tatu ya Katiba kwa wanawake wenye ulemavu Zanzibar,kwa ajili ya kua tayari kutoa maoni katika Tume ya Taifa ya kukusanya maoni ya katiba ya Tanzania.kushoto ni Mwantatu Mbaraka Khamis na mwasilishaji kutoka ofisi ya Mwanasheria kutoka Dar es Salaam Jasani Akhamad Bungala.
  MUWEZESHAJI Jasani Akhamad Bungala ambae ni Mwanasheria akionesha Katiba ya Tanzania wakati wa mafunzo kwa wanawake walemavu Zanzibar.
  VIJANA wanaotoa tafsri ya lugha za alama kwa Viziwi,wakiwatafsiria wanawake wenye ulemavu mbalimbali,wakati wa mafunzo ya siku tatu kujua katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzani,mafunzo hayo yalifanyika ukumbi wa Jumuia ya watu wenye ulemavu Zanzibar,kwa ajili ya kushiriki kikamilifu wakati wa kutoa maoni kwenye tume ya kupokea maoni ya katiba mpya Tanzani.
  BI Saada Hamad ambae NI MTAALAMU WA KUTOA TAFSIRI ZA ALAMA za Ishara kwa walemavu akimtafsiria kiziwi Salma Rajab katika mafunzo ya KATIBA kwa wajumbe wanawake wenye ulemavu.Picha na Abdallah Masangu.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu),Mh. Stephen Wassira (kulia) akimpongeza Rais mpya wa Jamhuri ya Ghana,Mh. John Dramani Mahama,muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo tarehe 7 Januari, 2013. Anayeangalia katikati ni Mke wa Rais huyo wa Ghana,Mama Lordina Mahama.Mh. Wassira alihudhulia hafla hiyo ya kuapishwa kwa Rais huyo mpya wa Ghana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

older | 1 | .... | 21 | 22 | (Page 23) | 24 | 25 | .... | 3286 | newer