Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 22 | 23 | (Page 24) | 25 | 26 | .... | 3283 | newer

  0 0

   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ni wasambazaji wakuu wa Ving'amuzi vya DStv,Salum Salum (kulia) akizungumza na Wapenzi wa soka walikuwa wamefurika kwa wingi kwenye kiota cha Samaki Samaki,Mlimani City jijini Dar es Salaam jioni ya leo kwa kushuhudia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (yanayofanyika huko nchini Afrika ya Kusini),ambapo DStv waliendesha zoezi hilo na pia kuchezesha bahati nasibu kwa wapenzi hao wa Soka walikuwepo hapo.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Salum Salum na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo,Barbara Kambogi wakichezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda King'amuzi cha DStv katika kipindi hiki cha Mashindano ya Kombe la Afrika.
   
  Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) akikabidhi King'amuzi hicho kwa Mshindi wa bahati nasibu hiyi,ambaye ni Mwanalibeneke wa Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog,Othman Michuzi (pili kulia) mara baada ya kuibuka kidedea.(Duuhh.....!! jamaa anazali huyu!).
  Baadhi ya Wadau wa DStv wakifuatilia Mtanange wa Ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika,kati ya timu ya Cape Verde na Afrika ya Kusini ambao ulimalizika kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.
  Wadau kibao toka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye Kiota cha Samaki Samaki jijini Dar kufuatilia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia DStv kutokea nchini Afrika ya Kusini yanakofanyika Mashindano hayo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),Liberatus Sabas (kulia) akiongea na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP),Camirius Wambura aliyeshika madawa ya kulevya aina ya mirungi nje ya jengo la Makao Makuu ya jeshi hilo Jijini Arusha mara baada ya kukamata shehena hiyo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),Liberatus Sabas (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na Waandishi wa habari nje ya jengo la makao makuu ya jeshi la Polisi Jijini Arusha.
  Gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo lilikuwa na shehena ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya uzito wa kilogramu 1800.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).

  0 0
 • 01/19/13--13:03: kumbukumbu
 • Marehemu John Franklin Chekani

  Baba, umepita mwaka mmoja sasa toka Mwenyezi MUNGU wetu alipopendezewa kukuchukua. Bado tuna majozi makubwa toka umetutoka na kuwa mbali nasi, lakini tunaamini upo peponi ukituombea na kutuongoza katika maisha yetu.

  Kwa maana hiyo,bado tunauhisi uwepo wako katika maisha yetu.

  Unakumbukwa sana na mke wako mpendwa- Susana Chekani, wanao – Franklin, Aneth pamoja na Jumbe Victor, mkwe wako Catherine na wajukuu wako Nicole, Susana na Sharlotte bila kuwasahau wanafamilia wote, wana ukoo na ndugu wote, rafiki zako na wale wote waliokupenda kwa moyo wote.

  Utaishi mioyoni mwetu siku zote, tunamuomba mwenyezi MUNGU akupe mapumziko ya amani. Nasi pia kwa mapenzi ya MUNGU, tupo njia moja.

  Amina.

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh. Philipo Mulugo (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Eng. Dr. Richard Masika wakiwa wameshikia mfano wa Hundi ya Sh. mil 10 kwa ajili ya Wanafunzi 10 bora . Fedha hizo ni Ahadi ya Mh. Mizengo Peter Pinda wakati wa mahafali ya mwaka 2012. Pembeni kushota ni baadhi ya wanafunzi bora.
  Mgeni Rasmi, Mh. Philipo Mulugo akihutubia wahitimu na wageni waalikwa.
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi, Eng. Dkt. Richard Masika akitoa Hotuba wakati wa mahafali ya Nne ya Chuo.
  Mkuu wa Bodi ya chuo cha Ufundi Arusha, Bw. Abraham Nyanda alitoa Hotuba wakati wa Mahafali.
  Kushoto ni Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh. Philipo Mulugo wakiwa na Mkuu wa Bodi ya Chuo cha ufundi(Katika), Bw. Abraham Nyanda pamoja na Mkuu wa Chuo cha Ufundi, Eng.Dkt. Richard Masika wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mahafali ya Chuo.
  Baadhi ya Wahitimu wakiwa na sura za furaha wakati wa mahafali ya Nne ya Chuo cha Ufundi Arusha.

  0 0

   Mtoto Hanifa Salum Hassan mwenye umri wa miaka mitano anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu (Leukemia) ambao umemfanya ashindwe kusimama na kutembea, anasumbuliwa na maumivu ya kichwa wakati wote, wakati mwingine hushindwa kupumua hivyo kulazimika kupumua kwa kutumia mashine pia hawezi kula analishwa kwa kutumia mirija na pia kila baada ya muda inabidi abadilishiwe damu.

  MATIBABU

  Matibabu ya mtoto Hanifa ni ya gharama kubwa sana. Ugonjwa wake haukujulikana alipopelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili lakini alipopelekwa nchini India gharama za uchunguzi pekee zilikuwa dola 7,600 ambapo mtoto Hanifa aligundulika kuwa na ugonjwa wa Acute lymphoblastic Leukemia.

  Matibabu yake yalipangwa yawe kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya matibabu iligharimu dola 10,000. Mwisho wa awamu ya kwanza zilihitajika dola 10,000 zingine ili aingie kwenye awamu ya pili ya matibabu lakini uwezo wa ndugu na jamaa ulikuwa ndio umeishia hapo hivyo matibabu ya mtoto Hanifa yalilazimika kukatishwa na Hanifa kurudishwa Tanzania.

  Ripoti za madaktari India zilipelekwa Muhimbili ambapo matibabu ya mtoto Hanifa yalipangwa kugharimu Tsh. milioni 2 kwa mwezi.


  Hakuna pesa za kumwezesha mtoto kuanza matibabu Muhimbili hivyo mtoto Hanifa amebaki nyumbani jijini Dar es Salaam akiwa kwenye hatari kubwa ya maambukizi mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake.


  Hadi sasa ndugu na jamaa wanahaha kutafuta pesa za kumwezesha mtoto Hanifa kumalizia awamu mbili za matibabu yake nchini India kama ikiwezekana au ikishindikana basi aweze kuanza matibabu Muhimbili.

  MICHANGO

  Kwa watakaopenda kujitolea kuokoa maisha ya Mtoto Hanifa wanaombwa watoe michango yao kupitia akaunti hizi

  Kwa walio Tanzania

  Jokha Khamis Issa
  Akaunti Namba: 041212000428
  People Bank of Zanzibar
  Kwa mawasiliano namba ya simu ni: +255 777 462587

  Kwa walio nje ya Tanzania wanaweza kutuma michango yao kwa akaunti hii

  Suleiman Maadini
  Account Number: 15092968
  Sort Code: 30-67-99
  Bank: Lloyds TSB
  Country: United Kingdom
  Kwa mawasiliano na Bwana Maadini: +44 78 18674305

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiendesha kikao cha Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,na katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.
  Baadhi ya waalikwa kutoka Taasisi walioshiriki katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
  Rais mstaafu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara,Viwanda na Wakulima,(Chamber of Comance) Zanzibar,akichangia mada wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Vuai Mwinyi,akichangia mada iliyozungumzia Utalii wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) ulichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
  Mbunge wa Jimbo la Mpendae,pia Mfanya Biashara Salum Turky,alipokuwa akichangia kuhusu suala la ujenzi wa viwanda vipya vitakavyo ondoa tatizo la Ajira kwa wananchi wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) ulichofanyika  katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Marium Hilali,(kushoto) wa kikundi cha Zaspo cha Kiembesamaki,wilaya ya Mahgaribi Unguja, wakati alipotembelea maonesho ya Bidhaa mbali mbali za Vikundi vya wajasiria mali yaliyofanyika leo katika mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Nassor Hamadi Omar, wa (ZOP) Zanzibar Orgave Prodiusears, cha Fuoni Unguja, wakati alipotembelea maonesho ya Bidhaa mbali mbali za Vikundi vya wajasiria mali yaliyofanyika katika mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Tatu Suleiman wa kikundi cha Zaidat Oil & Soap Spice,cha Chukwani Magharibi Unguja,(kushoto) alipokuwa akiangalia mafuta ya wakati alipotembelea maonesho ya Bidhaa mbali mbali za Vikundi vya wajasiria mali yaliyofanyika leo katika mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia kitabu wakati alipotembelea Kikundi cha Moto Hand Craft, cha Pete Wilaya ya Kusini Unguja,ambacho kinazalisha nguo aina ya Batiki,maonesho ya vikundi mbali mbali vya Wajasiria mali yaliyofanyika katika mkutano wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

  0 0

  Ngoma ya 'Last Night A DJ Saved My Life' ya kundi la Indeep ilikuwa mojawapo ya ngoma zilizokataza wadau kubaki vitini enzi hizo

  0 0

  Ngoma ya 20% 'YA NINI MALUMBANO' inatisha!

  0 0
 • 01/20/13--01:36: in loving memory
 • The Late Mzee Damas J.S. Kinabo 
  1933-2011

  Dad,
  It has been two long years since you went to be with the Lord. Today we pause to reflect upon your life and the impact in our lives. You have shaped our character, molded our spirits and touched our hearts. And every day we live is a reminder of the memories we have shared, a representation of the everlasting impact you have made upon our lives.

  You are forever in the hearts of your children: Dr. Grace; Alban; Oswald; Oliva; Morio; Juliet; and Dr.Baraka. You are missed by your grandchildren, in-laws, sisters, relatives and friends.

  Dad, your life was a blessing, your memory a treasure... You are loved beyond words and missed beyond measure...

  The heavens must have needed an accountant. May you continue to Rest in Peace.

  Those who we love don’t go away; they walk beside us every day. Unseen, unheard, but always near, so loved so missed, so very dear.

  0 0

  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya uendelezaji bonde la mto Rufiji (RUBADA), Prof. Raphael Mwalyosi (wa pili kushoto) akipokea ripoti na mapendekezo ya mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya nchini Brazil ya Odebrecht International, Bw. Fernando Soares jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA, Bw. Aloyce Masanja na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz (mwisho kushoto).
  Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya uendelezaji bonde la mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja, akipokea ripoti na mapendekezo ya mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya nchini Brazil ya Odebrecht International, Bw. Fernando Soares jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya RUBADA, Prof. Raphael Mwalyosi (mwisho kushoto) na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz (wa pili kushoto).

  0 0

  Na Mwandishi wetu,Lindi

  JESHI la Polisi mkoani Lindi,limezuia kufanyika kwa maandamano ya kuunga mkono majirani zao wa Mtwara,kupinga kusafirishwa kwa njia ya bomba la gesi asilia,kutoka mkoani humo kupelekwa Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufufua umeme utokanao kwa rasilimali hiyo.

  Kwa mujibu wa barua kutoka Ofisi ya Jeshi hilo,ambayo inaonyesha kukosewa kwa mwezi na mwaka,yenye kumbukumbu LND/271/VOL.1/17 ya Decemba 17/2012,na mwandishi wa habari hizi kupata nakala yake,na kusainiwa na Kamanda George Mwakajinga,imepelekwa kwa vyama vinne vya siasa.

  Vyama vilivyopelekewa barua za zuio la maandamano hayo ni pamoja na Chama cha mapinduzi (CCM), (CUF), CHADEMA na NCCR-MAGEUZI.

  Kwa mujibu wa barua hiyo,inawataka viongozi wa vyama hivyo vinne vya siasa kuchukua hatua mapema ya kuwasihi na kuwaelimisha wanachama wao kwanza, kwa ujumbe wa gesi kama ulivyotolewa na wananchi wa mkoa wa Mtwara.

  “Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaandikia kuwakumbusha tarehe kuwa 04/01/2013,siku ya Ijumaa mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila alipata fursa ya kuwaalika wadau wote,wazee wa mji wa Lindi,viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa,alizungumzia na kufafanua mwelekeo na msimamo wa Serikali katika suala la gesi na jinsi mkoa unavyochangia pato la Taifa kwa gesi ya Songosongo na jinsi anavyojiandaa kwa ugunduzi mpya kwenye kina kirefu cha bahari ya Hindi wilaya ya Kilwa”Imeeleza sehemu ya barua hiyo.

  Aidha,barua hiyo imeeleza kwamba Jeshi hilo la Polisi,lisingependa kukwaruzana na jamii katika maandamano hayo ya barabarani kwa hoja za kisera za kiuchumi ambazo ni za ki-Taifa, zinazoweza kuzungumzika katika mifumo mingine ya kiutawala kama vile katika vikao vya Bunge.

  “Tunaomba ushirikiano na ushirikishwaji wa Jamii katika utii wa sheria bila Shuruti katika kudumisha amani na utulivu ndani ya mkoa wa Lindi”Imeeleza barua hiyo.

  Baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama vilivyopelekewa barua hizo,wamemuomba kamanda huyo wa Polisi mkoani hapa,George Mwakajinga,kutoupotosha umma juu kauli yake,kwani maandamano yanayotarajiwa kufanywa ni kuunga mkono jirani zao wa Mtwara katika kutetea gesi iliyogunduliwa huko kutopelekwa nje ya mkoa huo kwa njia ya Bomba,na sio kupinga kauli ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

  “Sisi tunawaunga mkono jirani zetu wa Mtwara, juu ya kuondolewa gesi kupelekwa Dar es salaam,kwani huo ni uonevu na unyang’anyi mkubwa unaofanywa na hawa viongozi wetu waliopo madarakani”

  “Kwani sisi watu wa mikoa ya kusini tumeikosea nini hii Serikali,kama ni gesi tumewapa kutoka Songosongo Kilwa,licha ya wenzetu kuizuia kwa njia ya kiustaarabu,yaani kuifikisha mahakamani,lakini tuliwaachia na Kilwa kukosa kiwanda cha mbolea kama ilivyokuwa imepangwa,sasa leo wanataka kuihamisha ya Mtwara tuendelee kuwa masikini”Walisema viongozi na wanachama hao.

  Januari 04 mwaka huu,viongozi wa Chama cha wananchi (CUF) mkoani Lindi, wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja vya Sera,Manispaa ya Lindi,Walitoa wito kwa wananchi kushiriki katika maandamano yatakayofanyika Februari 23 mwaka huu,ili kuwaunga mkono jirani zao wa mkoa wa Mtwara,kupinga uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba na kuipeleka Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme.

  Mambo mengine yaliyotajwa na viongozi hao ni pamoja na kuwepo kwa mfumo wa ununuzi wa mazao kwa utaratibu wa mfumo wa Stakabadhi ghalani, kwa maelezo kwamba umekuwa hauwasaidii walengwa (wakulima) na badala yake umekuwa ukiwasaidia wachache

  0 0

  Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid. 
  Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula akiangali akikagua nyumba ya shirika hilo kabla ya kuikabidhi kwa mnunuzi wa nyumba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
  Baadhi ya nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KUONA ZAIDI NYUMBA HIZO

  0 0

  Hii ndio hali ilivyo katika barabara kuu iendayo Lindi na Mtwara kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo hayo.Abiria wa Mikoa hiyo wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na magari mengi kunasa kwenye tope lililotoea kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo,baada ya kukaa kwa muda mrefu,msaada wa kampuni ya Kharafy and sons -mkandarasi wa barabara hiyo ya km 60 alifika eneo la tukuo na kusaidia kuvutwa magari yaliyonasa.Picha na Mdau Abdulaziz Video,lindi.

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi wa vijiji vya Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza, alipokutana nao kwenye Uwanja wa Nyamagana, leo Januari 20, 2013, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja huo.
  Wajumbe wa nyumba kumi wakimsilikiza Mangula alipozungumza nao kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza muda huu kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara baadaye kwenye Uwanja huo.
   Wajumbe wa nyumba kumi wa vijiji vya Ilemelea na Nyamagana jijini Mwanza, wakiwa katika foleni kwa ajili ya kumuuliza maswali Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, alipozungumza nao kwenye Uwanja wa Nyamagana, leo Januari 20, 2013.

  0 0


  Ujenzi wa vifaa (turnstiles) vitakavyotumika kwa ajili ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja saba kati ya nane vitakavyotumia mfumo huo umekamilika kwa asilimia 80.

  Viwanja hivyo ni Chamazi (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Sokoine (Mbeya), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Mkwakwani (Tanga).

  Wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari una turnstiles, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza bado haujaruhusu ufungaji wa vifaa ukisubiri idhini kutoka kwa wamiliki wake (CCM Makao Makuu).

  Vifaa vitakavyotumika kusoma tiketi za elektroniki katika viwanja hivyo vinatarajiwa kuwa vimefungwa kufikia Februari 20 mwaka huu.

  Hakutakuwa na matumizi ya fedha taslimu mara baada ya mradi huo wa tiketi la elektroniki kuanza, kwani tiketi zitakuwa zikinunuliwa kwa kadi maalumu (smart card) katika vituo mbalimbali vitakavyotangazwa baadaye.

  Benki ya CRDB ndiyo iliyoingia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutengeneza tiketi za elektroniki baada ya kuibuka mshindi kwenye tenda.

  0 0


  Mashabiki wa soka wa jiji la Arusha, wamepata fursa ya aina yake ya kushuhudia uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka huu wa 2013, katika kiota maarufu cha Babylon Club kilichopo katika eneo la Metropole sambamba na wadau kutoka DStv ambao ndio waonyeshaji wa uhakika wa mashindano haya kupitia Channels zao za SuperSport. Hizi hapa ni picha na maelezo kutoka katika tukio hilo la uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yataendelea mpaka tarehe 10 Februari.
  Wadau wa Babylon Club,Arusha katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa ulioletwa na DStv kupitia channels zao za Super Sports. Experience The Spirit Of Africa...
  Ndani ya Babylon Club, kama unavyoona kuna screens kubwa na nyingi...Zote zimeunganishwa na DStv
  Meneja Masoko wa DStv,Furaha Samalu(kulia) akiwa na mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo, wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ndani ya Babylon Club. DStv wanaonyeshaji mashindano hayo Live na katika HD kupitia Channels zao za SuperSport.
  Sales Coordinator wa DStv Kanda ya Kaskazini, Christopher Mbanjo, akiteta jambo la Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo(www.millardayo.com) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ndani ya Babylon Club,Arusha.
  Macho yote kwenye screens mbalimbali zilizotapakaa ndani ya Babylon Club
  Baadhi ya mashabiki waliohudhuria kutizama mechi za ufunguzi za AFCON 2013 wakishuhudia mchezo wa kwanza wa mashindano hayo baina ya South Africa na Cape Verde. Timu hizo zilikwenda sare ya kutofungana.
  Panapo watu haliharibiki jambo.Lakini...endapo lingeharibika basi hawa jamaa walikuwa tayari kabisa kurekebisha au kutatua.Ndani ya Babylon Club,Arusha.
  Meneja Masoko wa DStv,Furaha Samalu, akiwa na mdau wa soka ambaye alikiri kwamba yeye huwaamini DStv pekee linapokuja suala la burudani kupitia mchezo wa soka.
  Soccer and Dance....Experience The Spirit Of Africa.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mke wa Rais wa Mali,Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na mke wa Rais wa Mali,Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini humo.
  Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Marcel Escure wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, tayari kuanza ziara ya yake ya kiserikali ya siku tatu.
  Mama Salma Kikwete akionega na mke wa Rais wa Mali,Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mvua kubwa iliyonyesha mapema leo mjini Mtwara imepelekea mafuriko katika maeneo mbali mbali ya mji huu na kufanya wakazi wa maeneo haya kupata kuanza kuhangaika kuhamisha vitu vyao na wengine wakiwa hawajui la kufanya maana maji yamejaa mpaka majumbani mwao.Ni balaa kubwa la mafuriko ya maji Mtwara leo hasa eneo la Chuno. Eneo hili ni karibu na nyumba ya Mzee Hokororo au Dr Mwakipa. Hali ni mbaya sana na maji yanaendelea kujaa hadi mchana huu.Hakuna taarifa yeyote mtu yeyote aliyepoteza maisha. Msaada wa haraka unahitajika kwa wananchi hawa.Picha na Mdau Abdulaziz Video wa Globu ya Jamii,Mtwara.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwahutubia watu wenye walemavu walioalikwa katika hafla ya cha mchana kilicho andaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi ikiwa ni katika kukaribisha mwaka mpya wa 2013 wa Walemavu hao.Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasimi katika hafla hiyo.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiasalimiana na Bi. Regina Mengi mtoto wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi wakati wa hafla ya watu wenye Ulemavu iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Redd's Miss Tanzania,Brigit Alfred ambaye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika kushiriki chakula hicho cha mchana na watu walemavu kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimsalimia mtoto Abrahamu Omari (miezi 3) aliyebebwa na mama yake ambaye ni mlemavu wa ngozi anaitwae Amina Fadhili wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi (nyuma ya Waziri Mkuu) ikiwa ni katika kuukaribisha mwaka mpya 2013.Picha na Chris Mfinanga.

  0 0


  BASI LA KAMPUNI YA NGANGA LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA DAR ES SALAAM LIMEPINDUKA LEO KATIKA ENEO LA IMEZU NJE KIDOGO YA MJI WA MBEYA. AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MBILI ASUBUHI NA ABIRIA MMOJA  ALIFARIKI PAPO HAPO NA WENGINE ZAIDI YA 40 WAMEJERUHIWA VIBAYA NA KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MJINI MBEYA. ABIRIA ALIYEFARIKI AMETAMBUWA KWA JINA LA ENOCK LWILA MKAZI WA ENEO LA MAMA JOHN MJINI MBEYA NA NIMFANYABIASHARA KWENYE SOKO LA MWANJELWA
  BAADHI YA WAKAZI WA IMEZU WAMESEMA AJALI HIYO IMESABABISHWA NA MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI HILO.

  MWILI WA MAREHEMU ENOCK LWILA  UKIWA UMELAZWA CHINI KUSUBIRI WANA USALAMA KUJA KUUCHUKUA.MAREHEMU ENOCK LWILA AMEKUTWA NA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KATIKA SOKSI NA KWENYE MIFUKO YAKE YA SURUALI INASEMEKEANA ALIKUWA ANAENDA DAR ES SALAAM KUNUNUA BIDHAA MBALIMBALI ZA DUKANI KWAKE.

  HAPA WANAUSALAMA WAKIHESABU PESA WALIZOZIKUTA KWENYE MWILI WA MAREHEMU ENOCK HUKU WANANCHI WAKISIMAMIA KWA MAKINI ZOEZI HILO LA KUHESABU HIZO PESA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15  ALIZOKUWANAZO MAREHEMU 

  PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG.

older | 1 | .... | 22 | 23 | (Page 24) | 25 | 26 | .... | 3283 | newer