Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 20 | 21 | (Page 22) | 23 | 24 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Mad Mad Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kampuni yake kuingia mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeneza filamu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba. 

  Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.  

  Na Ripota Wetu.

  KAMPUNI ya Mad Mad Entertainment iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program maalum ya kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la kukuza sanaa hiyo hapa nchini.

   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii  hao ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa nchini.

   “Kwa muda mrefu niliokaa London sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani nifanye ili  kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini.


  “Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.

  Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa,  alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu,  kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.

  Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.

  “Hapa kuna kuinua vipaji, soko la kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika hatua za awali za mchujo,” alisema
  Mwakifamba.

  Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalienamna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Msumbiji na Indonesia ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mhe.Zakaria Anshar wakiwasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Balozi mpya wa Msumbiji nchini Tanzania Dkt.Vicente Mebunia Veloso na Balozi Mpya wa Indonesia nchini.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Hadi leo Ankal anazimia na ngoma ya Otis Redding ya 'Direct Me'

  0 0

  Wachezaji wa timu ya Simba wapo nchini Oman kwa kambi maalum ya kujifua wakati wakijiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo jioni ya leo wanakipiga na timu ya taifa ya wanajeshi wa Oman ambayo nayo inajiandaa kucheza Kombe la Dunia la wanajeshi. 

  wakiwa nchini Oman walialikwa katika hafla fupi iliyoandaliwa na mdhamini wao wa safari ya Oman,Mama Rahma Al Kharoos iliyofanyika nyumbani kwake eneo la Al Kheri jijini Muscat, Oman jana usiku kwa ajili ya chakula cha usiku.

  Walikula pamoja na baadaye bendi maalum kutoka Tanzania iliwapigia muziki na wakaserebuka pamoja huku Rahma akimwaga noti kwa kuwatunza wachezaji wa Simba waliokuwa wakiyarudi magoma nyumbani hapo

  Katika hafla hiyo, Rahma alikabidhiwa jezi ya Simba na Musleh Rawah ambaye ni mmoja wa wadau wa Msimbazi na jezi ya timu ya taifa ya Oman na kocha wa makipa wa timu hiyo, Haroun Amur.
  Mmoja wa wadau wa Timu ya Simba,Musleh Rawah (mwenye kanzu) akimkabidhi Mama Rahma Al Kharoos Jezi ya timu ya Simba ikiwa ni Kama Shukran kwa Mwaliko wa Timu hiyo nchini Oman.
  Kocha wa Makipa wa Timu ya Taifa ya Wanajeshi wa Oman, Haroun Amur akikabidhi Jezi ya Timu yake kwa Mama Rahma Al Kharoos.
  Wachezaji wa Simba wakijisevia Msosi.
   Wachezaji wa Timu ya Simba wakiyarudi Magoma huku Mama Rahma Al Kharoos akiwatunza manoti.Picha zote na Saleh Ally.


  0 0

  Ankal, 
  Mdau katika harakati zake kutalii maeneo maarufu kwa watali toka pande zote za dunia akipeperusha jina TANZANIA kwa kutumia 'uzi' jezi inayovutia . Maeneo hayo ni pwani za SRI LANKA na Thailand ambapo watalii toka Marekani na Ulaya humiminika kwa wingi, Labda Bodi ya Utalii ifanye mpango wa kutengeneza jezi hizi nyingi na vipeperushi ili kutangaza jina na vivutio sehemu ambapo kuna 'potential' ya kuvutia watalii, tutizame jamaa akitutangaza kiaina;

  0 0
 • 01/18/13--00:13: Jamaa wametega.......
 • Wakati Mahabusu wakikosa haki ya kupelekwa mahakamani wilayani Ruangwa kwa kukosekana Mafuta ya gari la kuwachukua Magereza Nachingwea,Cha ajabu ni kwamba Mafuta ya kwenda umbali kama huo wa Nachingwea yapo kwa kwenda Kuvizia magari na pikipiki ili kujipatia ulaji yapo au mafuta yanapatikana hapo walipotega? Inatokea wakati mwingine Mfungwa akahukumiwa Ruangwa akakaa mahabusu ya Polisi Ruangwa kwa takriban siku tatu kabla ya kupelekwa Magereza.Wizara na Jeshi la Polisi Makao Makuu Tupieni macho Polisi Ruangwa na suala la Mafuta wakati mwingine ushindwa kuwahi tukio kwa sababu ya eti Magari yao hayana Mafuta.Ruangwa ina matukio mengi ya kujichukulia sheria Mikonini ikiwamo mauaji na ujambazi.Picha na Mdau Abdulaziz,Lindi

  0 0

  Kampuni ya Utalii ya Indoma Tours ya Mjini Zanzibar, inawaleate mchezo mkali wa Kirafiki wa Kimataifa wa Soka, kati ya timu ya Skonda Flota kutoka Barani Ulaya na Timu ya Sale Mdosi Hardware, ya mjini Zanzibar, mchezo utakaochezwa Februari 9, mwaka huu katika Uwanja wa Uzi Football Yard, kuanzia saa 10:00 jioni.

  0 0  0 0

   Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri wa Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu, akikata utepe kuzindua Safari za Ndege za Shirika la Precision Air za Mbeya kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Michael Shirima. 
    Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu, akishuka kutoka katika ndege ya shirika la Precision Air wakati wa uzinduzi wa Safari za Mbeya – Dar kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kabla ya kukata utepe kuzindua safari hizo. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Michael Shirima. 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air (PW), Michael Shirima, (Kushoto) akiteta jambo na abiria wa kwanza kununua tiketi ya safari ya Mbeya wakati wa uzinduzi wa Precision Air wa  njia ya Mbeya – Dar, Bw. Alfred Mwambeleko Jumatano hii.  

   Mzee akisaidiwa kupanda ndege, ambaye ni mkazi wa mkoani Mbeya wakati wa uzinduzi wa Safari za Ndege za Shirika la Precision Air za Mbeya – Dar uliofanyika Jumatano hii kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe uliofanyiwa marekebisho kutumika kwa safari za kimataifa.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (kulia) akizungumza na Walezi wa Kituo cha watoto yatima cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kituo hicho,mjini  Dodoma na kutoa Msaada wa Luninga kwa ajili ya Watoto hao yatima.kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Kituo hicho Fr Vicent Boseri na anaye fuatia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa (TAMISEMI),Mh. Hawa Ghasia
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Fr Vicent Boseri pamoja na msaidizi wa Vicent Sistar Rozaria ambao walimshukuru waziri mkuu kwakukumbuka watoto yatima hapa nchini.Picha na Chris Mfi

  0 0

  Tanroads tupieni jicho Barabara ya kutoka Lindi kwenda Ruangwa ukianzia Michenga hadi Kitandi Hali ni mbaya.Natoa wito kwa Madereva waedao Ruangwa kuwa makini kutokana na maeneo mengi ya barabara hiyo kukatika na Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.Picha na Abdulaziz,Lindi

  0 0

  On January 15, 2012 U.S. Embassy Public Affairs Officer Dana L. Banks (left) met with Ms. Scholastica Ponera, (right), Managing Director of Pongo Safaris and Tours Limited at the U.S. Embassy in Dar es Salaam. Ms. Banks presented Ms. Ponera with a 9.5 million Tanzanian shillings grant ($5,993 USD) to sponsor her attendance at the National Tour Association (NTA) convention in Orlando, Florida from January 20 through 24, 2013. By participating in the travel convention, Pongo Safaris will increase awareness of Tanzania as a tourist destination. Ms. Ponera, a conservationist and woman entrepreneur, seeks to strengthen women's roles in promoting development of Tanzania's tourism sector. Pongo Safaris supports Eco-Sustainable/Community Tourism and mainly operates in the Southern Circuit which offers unique safaris to many areas including Selous Game Reserve, Ruaha and Mikumi National Parks and historical sites of Kilwa. Ms. Banks lauded Ms. Ponera's leadership as an entrepreneur and conservationist and underscored the United States' support to promote women's entrepreneurship and tourism sector development in Tanzania.

  0 0

   Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius kambarage Nyerere.
  Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa shindano hilo,kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Pichani kushoto ni Shaffih Dauda,Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra,Mbwiga Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
   Nahodha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana tayari kwa kupambana na timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
   Waratibu kutoka Prime Time Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo mchana mara timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
   Shaffih Dauda akiwa ameambatana kocha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
   Wachezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa la timu ya Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa,Jijini dar.
   Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. kambarage Nyerere.Picha zote na JIACHIE BLOG.
  ======  ======= ======= =======
  WAKATI mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga kesho watacheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, kocha wa Black Leopards ametema cheche na kusema wataibuka na ushindi mkubwa kutokana na uzoefu wao wa mashindano ya Kimataifa.

  Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki wengi kufika.
  Mratibu wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha shs 5,000 na shs 7,000 na kuwa cha shs 3,500 ili kuwafanya mashabiki wengi kuona mechi hiyo.
  Viingilio vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni shs 15,000 , VIP B shs 20,000 na VIP A shs 30,000
  Dauda alisema kuwa Black Leopards wamewasili na kutamba kushinda mechi hiyo kutokana na uzoefu waliopata katika mashindano mbali mbali ikiwa pamoja na kombe la Shirikisho.
  Kocha wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja ya faraja kwao.
  “Ziara hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,” alisema Makhubela.
   Alisema kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao ambayo ipo katikati..

  0 0


  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akishirikiana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed (kulia) kukata utepe kuashiria ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri uliofanyika jana katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. Kushoto kabisa ni Mhe. Pascal Mabiti ambaye ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Tanzania Jumanne Maghembe naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

  Mbunge wa jimbo la Busega mkoani Simiyu  Titus Kamani naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

  Mama Maria akiondoka kwenye eneo la bomba kuu la kutekea maji mara baada ya kutwishwa ndoo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed huku wananchi wengine wakipiga makofi kuashiria kufurahia tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu.Picha kwa hisani ya Gsengo Blog.

  0 0

   Wanamichezo 50 kati ya 52 waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu hizo.

  Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar es Salaam.

  Orodha kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).

  Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

  Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).

  Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

  6 WAOMBA UONGOZI BODI YA LIGI KUU, WOTE WAREJESHA FOMU
  Waombaji wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha fomu.

  Kwa upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.

  Nafasi mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu Mwindadi.

  Kamati ya Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu zote zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa Bodi ya Ligi Kuu.

  Pia Kamati inapenda kuwakumbusha waombaji uongozi kuzingatia Kanuni za Uchaguzi, kwani baadhi yao wameanza kufanya kampeni kupitia vyombo vya habari. Kwa walioanza kufanya kampeni kabla ya wakati wanajiweka katika hatari ya kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo jana. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala wafungwa na mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) walipozitoa kupitia hotuba yao iliyotolewa wakati Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ziara katika gereza hilo jana.
   Afisa wa Magereza wa Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, Gibson Mwakibibi akiwaonyesha mfuniko wa Hotpot (Chombo cha kuhifadhia chakula) pamoja na Radio Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambapo vifaa hivyo vinatumika kuficha simu, visu, bangi na vifaa mbalimbali ambavyo ni hatari kwa usalama wa Mahabusu na wafungwa. Vifaa hivyo vilikuwa vinaingizwa na mahabusu hao pmaoja na baadhi ya ndugu zao wanapopeleka chakula gerezani hapo. Hata hivyo, maafisa magereza kwa kutumia chombo cha kugundulia vifaa mbalimbali (Metal Detector) kinachotumika gerezani hapo huvikamata vifaa hivyo.
   Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu pamoja na wajumbe wa kamati yake wakiwauliza maswali mbalimbali Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala Wafungwa na Mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.


  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, John Chiligati akizungumza na maofisa wa Jeshi la Magereza wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika Gereza la Mahabusu la Segerea, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi. Kushoto ni  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi, Mwamini Malemi akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu pamoja na kamati yake katika Gereza la Mahabusu la Segerea, jijini Dar es Salaam jana.
  PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0


  Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja akikabidhi jezi kwa timu mchezo wa raga (Rugby) ya Dar Leopards jijini Dar es Salaam. Anayepokea ni Mwenyekiti wa Dar Leopards Rugby Club,Bw. Phillippe Poinsot. Minja amesema kuwa wameamua kuunga mkono mchezo wa raga(Rugby) kwani ni miongoni mwa michezo iliyosahaulika nchini. Alliance Auto wameshirikiana na HSE Solutions kudhamini jezi Dar Leopards Club. Wanaoshuhudia tukio hilo ni baadhi wachezaji wa Dar Leopards Rugby Club.

  Kocha wa timu ya Dar Leopards Rugby Club Bw. Jonathan Taylor (kushoto) akipozi na baadhi ya wachezaji wa Club hiyo huku wakiwa wamevalia jezi hizo.
  Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Dar Leopards Rugby Club,Bw. Phillippe Poinsot.

  Kocha wa timu ya Dar Leopards Rugby Club Bw. Jonathan Taylor akipozi na baadhi ya wachezaji wa Club hiyo kwenye moja ya Brand ya magari ya Alliance Autos aina ya 'Volks Wagon AMAROK' huku wakiwa wamevalia Jezi walizokabidhiwa leo katika makao makuu ya kampuni hiyo.

  0 0
 • 01/18/13--12:03: Taarifa ya Msiba

 • Familia ya ndugu Demba Sow, inasikitika kutangaza Kifo cha mke wake mpenzi Monique Demba Sow Kasongo. Kilichotokea Burhani Hospital 14-1-13 saa 2 usiku. 

  Habari ziwafikie watoto wa Marehemu, Yan Sow na Didy Sow walipo America na Canada, ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. 

  Leo tunakesha nyumbani kwa Marehemu Mikocheni karibu na Clouds Fm. Mazishi ni kesho Jumamosi 19-1-13 ambapo Misa ya kumuombea Marehemu itafanyika nyumbani kwake Mikocheni kesho 19-1-13 saa 5 na kuagwa. 

  Mwili utazikwa Katika makaburi ya Kinondoni saa 9 mchana. 

  Kwa mawasiliano zaidi,Wasiliana na mwenye namba hii 0754280895

  Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi.

  -Amen.

  0 0

  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa kuhusu picha ya watoto wa wakulima wa zao la zabibu wanaosomeshwa na kiwanda hicho, alipotembelea kuona utendaji wa kiwanda hicho, Dar es Salaam hivi karibuni..
   Ofisa Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Athuman Mkungu akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kiwanda cha Konyagi.
   Mtaalamu wa Upishi wa Bia, Kelvin Nkya akimuonesha kompyuta inatumiwa kupikia bia katika kiwanda cha TBL Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Martine Calvin (katikati) jinsi bia inavyopikwa kitaalamu alipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam hivi karibuni.
   Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu wakati alipotembelea kiwandani hapo.


older | 1 | .... | 20 | 21 | (Page 22) | 23 | 24 | .... | 3285 | newer