Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

INTRODUCING ALI KIBA'S NEW HIT "MVUMO WA RADI"


MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad Dodoma

Imeelezwa kuwa Ukuaji wa sekta ya utalii hapa nchini, umedhihirika mapato yatokanayo na utalii kuongezaka kutoka Dola bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola bilioni 2.2 mwaka 2017. 

Ongezeko la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017. Ambapo Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkta Hamis Kigwangala wakati akifungua kongamano la kupitia rasimu ya sera ya Taifa ya utalii ya mwaka1999 linalofanyika jijini hapa na kuwashirikisha wadau wa sekta ya utalii nchini kutoka sekta binafsi na za umma.

Kigwangala amesema kuwa maboresho hayo yaende sambamba na mwendelezo wa mchakato wa kazi nzima ya kupitia Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 ambayo ni muhimu kwa mstakabali wa sekta ya utalii hapa nchini ambayo Kama ilivyoelezwa hapo awali, mojawapo ya dhumuni la msingi la hatua hiyo linalenga kuwa na Sera inayoendana na mabadiliko ya kiuchumi, mazingira, tecknolojia, kijamii na kisiasa yanayotokea ndani na nje ya nchi yetu ambayo yanagusa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

Amesema kuwa warsha imejumuisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Umma na Binafsi ambao kwa namna moja au nyingine huguswa au hushiriki katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Aidha, kama mnavyofahamu, utalii ni sekta mtambuka na ili kufanikisha ukuaji wake unahitajika ushirikiano thabiti baina ya wadau wote. Ushirikiano huu utaweza kuleta matokeo chanya iwapo kuna Sera madhubuti ambayo mchakato wake wa maandalizi umeshirikisha wadau kikamilifu.

JUMIA YATOA SAMSUNG S9 NA S9+ KWA WATEJA WAKE

$
0
0
JUMIA imekabidhi simu mbili za Samsung Galaxy S9 na S9+ kwa wateja wake wawili ambao waliibuka washindi kupitia zoezi la kusaka simu kwenye mtandao wao (Treasure Hunt) kupitia kampeni ya ‘Mobile Week.’

Katika zoezi hilo wateja waliofanikiwa kuzipata simu hizo zilizofichwa, walipewa ofa ya kuzinunua kwa bei ya chini kupindukia tofauti na gharama yake halisi. Baada ya kufanikiwa kufanikiwa kuipata simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu, wakati mwenzake Lumby Elia yeye aliinunua Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!

Bei halisi ya simu ya Samsung Galaxy S9 ni shilingi 2,049,000 ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,500,000 wakati Samsung Galaxy S9+ ni shilingi 2,315,000 nayo ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,800,000! Hivyo unaweza kujionea ni kwa namna gani wateja hawa walivyokuwa na bahati!

Simu hizi zilizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu na kampuni ya Samsung duniani ambapo kwa hapa nchini Tanzania ilikuwa ikipatikana kwa malipo ya kabla kupitia kwenye mtandao wa Jumia pekee.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa simu yake ya Samsung Galaxy S9+, Lumby Elia amesema kuwa ana furaha sana hatimaye kuishika simu hiyo mkononi kwa mara ya kwanza kwani ni kama ndoto kuinunua kwa bei hiyo kwa sababu ni sawa na bure.

“Ni ndoto ya watu wengi kumiliki bidhaa ambayo ni toleo jipya hususani kama simu ambazo kila mwaka huwa zinakuja na matoleo na maboresho tofauti. Simu hii kwangu mimi ni kama ndoto kutokana na ubora na thamani yake pamoja na uwezo ilionao,” alisema na kumalizia Bi. Elia, “Naishukuru sana Jumia kwa zawadi hii lakini pia kwa fursa iliyoitoa kwa wateja wake kuweza kutumia bidhaa halisi na mpya kabisa iliyoingia kwa mara ya kwanza sokoni. Nawasihi wateja wengine wakiona fursa kama hizi wasizipuuzie, ni kweli kama hivi mnavyoona.”

Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliyoinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia aliyoinunua simu hiyo aina ya Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey, akizungumza kwenye mkutano huo.

COASTAL UNION YAMKABIDHI TUZO YA HESHIMA WAZIRI UMMY WA KUISAIDIA KURUDI LIGI KUU

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akipokea tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake kwa kuipandisha timu ya Coastal Union kucheza Ligi kuu msimu ujao kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu hiyo Salimu Bawaziri mapema leo kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati alipofungua mashindano ya Ligi ya Banda Cup . Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akionyesha waandishi wa habari tuzo aliyokabidhiwa na klabu ya Coastal Union kwa kutoa mchango wake kuipandisha kucheza Ligi kuu msimu ujao kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga (CCM) Azzah Hamadi Hilali Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)kushoto akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri ikiwa ni kutambua mchango wake wa kuisaidia timu hiyo kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao.

Tuzo hiyo walikabidhiwa pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano January Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli(CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM),Asas ya Iringa na Mo Dewji. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Wataalam Wawasilisha Usanifu Wa Awali Wa Kiwanja Cha Ndege Cha Kimataifa Cha Msalato Dodoma

$
0
0
Wahandisi Kamel Fazhani (kulia) na Marrarchi Walis (kushoto) wa Kampuni ya Studi ya Tunisia wakiwasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mbele ya wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga.
Meneja Mipango na Usanifu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mohamed Millanga (wa kwanza kushoto), akiangalia moja ya picha (hazionekani pichani) za usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo na Wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa Kampuni ya Studi ya Tunisia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo uliudhuriwa na wataalam mbalimbali wa usafiri wa anga.
Mhandisi Bernard Kavishe (aliyesimama) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), akichangia hoja katika mkutano uliofanyika leo wa uwasilishaji wa usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo umewasilishwa na wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
Bw. Said Mpwili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) (nyuma aliyenyanyua mkono), akiwasilisha mapendekezo ya ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege kwa wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia, ambao leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wamewasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma.
Mwonekano wa Jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo katika usanifu wa awali kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na wataalamu kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.

Picha na Bahati Mollel wa TAA

Watanzania Jiungeni Na NHIF Kabla Ya kuugua- Makinda

$
0
0
Na Grace Michael, Dodoma

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua ili kuepukana na usumbufu wa kutafuta au kutumia gharama kubwa za matibabu wakati wanapopatwa na magonjwa.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF), Anne Makinda wakati akizungumza na wadau kutoka Wizara zote Jijini Dodoma.

Amesema kuwa mwananchi anapokuwa na bima ya afya anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote bila kujali kama ana fedha ama hana ikilinganishwa na mwananchi ambaye hana bima ya afya ambapo akiugua ni lazima aanze kutafuta fedha za kujitibia.

“Ni lazima ifike mahali watanzania tujenge utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua, tunashuhudia namna wananchi wanavyopata shida wakati wakiwa wamefikwa na maradhi hali inayosababisha wengine hata kulazimisha kutumia njia za mkato au udanganyifu hivyo ili kuepukana na matatizo haya ni vyema tukawa na huu utamaduni wa kukata bima ya afya mapema,”alisema Mama Makinda.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya kwa kuhakikisha dawa, vifaa tiba na mahitaji yote katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ili mwananchi apate huduma kamilifu.

Kutokana na hayo, aliwataka wadau hao kushirikiana na Mfuko kwa karibu kwa kutoa maoni ama ushauri wao kwa uwazi ili kuleta mabadiliko chanya ya kihuduma kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hasa katika kipindi hiki cha kuelekea afya bora kwa wote.

Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa wananchi waliokuwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Anne Makinda akizungumza na Wadau wa Mfuko kutoka Wizara mbalimbali jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akieleza mikakati ya Mfuko katika kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

IGP SIRRO AWAPA SOMO WASTAAFU POLISI.

$
0
0
Na. Jeshi la Polisi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaasa Makamishna wastaafu wa Polisi kuendelea kukabiliana na uhalifu wawapo uraiani baada ya kustaafu utumishi wa Polisi kwa kuwa mapambano ya uhalifu hayana mipaka. 

IGP Sirro aliyasema hayo jana wakati wa hafla maalum ya kuwaaga waliokuwa Makamishna wa Polisi, Glodwing Mtweve na Elice Mapunda katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, hafla ambayo ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa Polisi, Askari na familia za wastaafu hao. 

“Mmefanya kazi kubwa sana wakati mlipokuwa nasi na uzoefu wenu tutaendelea kuuhitaji na kuutumia lakini sasa mnaporudi uraiani haina mana kuwa hamruhusiwi kuendeleza mapambano ya uhalifu la hasha hii ni fursa sasa ya kuwasaidia wananchi kupata mbinu ili kwa pamoja mshirikiane na Jeshi la Polisi kuukabili uhalifu kwa kuwa mtakuwa karibu na jamii zaidi” Alisema IGP Sirro. 

Kwa upande wake Kamishna Mstaafu Clodwin Mtweve amewataka Maofisa na Askari Polisi kuendelea kufanya kazi zao kwa kujituma na weledi ili kuhakikisha kuwa uhalifu unaendelea kupungua kwa kuwa uhalifu sasa unafanywa kisayansi. 

Mtweve amesema wanaoendelea kulitumikia Jeshi la Polisi hawana budi kuyafuata yale mazuri yote waliyofanya na yale mabaya kuyaacha ili nao waweze kumaliza salama utumishi wao salama na kuagwa kama ilivyokuwa kwao. 

Naye Kamishna mstaafu Elice Mapunda ambaye alikuwa Mwanamke wa kwanza kufikia cheo cha kamishna wa Polisi tangu kupata uhuru aliwataka askari wa kike nchini kujituma ili kupata mafanikio kama ilivyo kwa wanaume kwa kuwa kupata vyeo ndani ya jeshi hilo hakuangalii jinsia bali ni utendaji wa kazi. 

Amesema askari wa kike hana tofauti na wa kiume kwa kuwa mafunzo wanayopitia ni ya aina moja hivyo wakijituma zaidi na kufanya kazi zao kwa ufanisi wataonekana na kupewa madaraka kwa mujibu wa taratibu na kanuni za Jeshi hilo. 

Watanzania jiungeni na NHIF kabla ya kuugua - Makinda

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa wananchi waliokuwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Na Grace Michael, Dodoma

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua ili kuepukana na usumbufu wa kutafuta au kutumia gharama kubwa za matibabu wakati wanapopatwa na magonjwa.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF), Anne Makinda wakati akizungumza na wadau kutoka Wizara zote Jijini Dodoma.

Amesema kuwa mwananchi anapokuwa na bima ya afya anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote bila kujali kama ana fedha ama hana ikilinganishwa na mwananchi ambaye hana bima ya afya ambapo akiugua ni lazima aanze kutafuta fedha za kujitibia.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Anne Makinda akizungumza na Wadau wa Mfuko kutoka Wizara mbalimbali jijini Dodoma.

“Ni lazima ifike mahali watanzania tujenge utamaduni wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua, tunashuhudia namna wananchi wanavyopata shida wakati wakiwa wamefikwa na maradhi hali inayosababisha wengine hata kulazimisha kutumia njia za mkato au udanganyifu hivyo ili kuepukana na matatizo haya ni vyema tukawa na huu utamaduni wa kukata bima ya afya mapema,”alisema Mama Makinda.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya kwa kuhakikisha dawa, vifaa tiba na mahitaji yote katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ili mwananchi apate huduma kamilifu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akieleza mikakati ya Mfuko katika kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wengi zaidi.

Kutokana na hayo, aliwataka wadau hao kushirikiana na Mfuko kwa karibu kwa kutoa maoni ama ushauri wao kwa uwazi ili kuleta mabadiliko chanya ya kihuduma kwenye Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hasa katika kipindi hiki cha kuelekea afya bora kwa wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema, Mfuko umejipanga katika uboreshaji wa huduma zake ikiwemo taratibu zinazowawezesha wananchi kujiunga na huduma zake.

Alisema kuwa, kwa sasa mfuko unaangalia uwezekano wa kumwezesha mwananchi mmoja mmoja kujiunga na mfuko lakini pia utaratibu wa kulipa fedha kidogo kidogo, taratibu ambao zitawawezesha wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma za mfuko.

“Tumejipanga na tumedhamiria kufikia mwaka 2020 ni lazima tuhudumie wananchi wengi zaidi na kwa sasa tunajipanga kuzindua huduma mbalimbali ambazo zinalenga kumnufaisha mwananchi wa kawaida kabisa,”alisema.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda.

Akizungumzia suala la huduma bora, alisema mfuko umeweka mazingira rafiki kwa watoa huduma kupata mikopo rahisi kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao hususan vifaa tiba na uimarishaji wa miundombinu hatua ambayo imewezesha upatikanaji wa huduma nyingi na bora kupatikana nchini.

Alitumia mwanya huo pia kukemea tabia ya baadhi ya watoa huduma na wanachama wasio waaminifu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya udanganyifu ambapo alisema Mfuko hauko tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea na badala yake hatua kali zitachukuliwa kwa wanaofanya vitendo hivyo.

Kwa upande wa wadau ambao ni Maofisa Waandamizi kutoka wizara zote, waliupongeza mfuko kwa kazi kubwa ambayo umefanya ya utoaji wa huduma na uwekezaji katika sekta ya afya ambao umesaidia huduma nyingi za kitaalam ambazo awali hazikupatikana nchini kupatikana.

Dkt Kalemani azindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati na kutoa maagizo mbalimbali kwa Watendaji wa Wizara na Taasisi ili Sekta ya Nishati iendelee kuwa injini katika ukuaji wa uchumi.

Dkt. Kalemani amezindua Baraza hilo tarehe 11 Mei, 2018 mkoani Dodoma ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria uzinduzi huo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye alimwakilisha Katibu wa TUGHE Taifa na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.

Akizungumza na Wajumbe wa Baraza, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wajumbe wa TUGHE, Tawi la Wizara ya Nishati, Dkt. Kalemani alisema kuwa, jukumu kuu la Wizara na Taasisi zake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nishati ya umeme ya kutosha hivyo wana jukumu la kutafakari namna ya kutekeleza suala hilo.

Dkt. Kalemani, aliwaagiza watendaji wa Wizara na Taaisi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na miundombinu ya kutosha ya kusafirisha umeme ili umeme unaozalishwa uweze kuwafikia wananchi kwani kuna sehemu ambazo umeme umekuwa ni mwingi kuliko matumizi ya nishati hiyo. Aidha, Dkt Kalemani aliwataka watendaji hao kuhakikisha kuwa, wananchi waliolipia huduma ya umeme, wanaunganishwa na huduma hiyo ndani ya wakati ambao ni siku Saba.

Vilevile Dkt. Kalemani, alisema kuwa, kila mtendaji ana jukumu la kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kuhusu masuala yanayohusu Watumishi, Dkt Kalemani aliagiza kuwa watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu wathibitishwe katika nafasi hizo ili watumishi hao watekeleze majukumu yao kwa kujiamini na kuwa na ari.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kushoto), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (wa kwanza kulia),  Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (wa kwanza kushoto) na Katibu Mpya wa Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Nishati, Pascal Mduma (wa pili kulia) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (kulia) na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (kushoto) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.
 Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti (waliosimama) iliyoandaa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na kushoto kwake ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.

TAARIFA KWA UMMA

TFF YAWAONDOA WAAMUZI WAWILI ORODHA YA WAAMUZI WA LIGI YA MABINGWA WA MKOA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro.

Waamuzi walioondolewa katika orodha hiyo ni Seleman Nonga kutoka Arusha aliyekuwa katika kituo cha Geita na Dadu Fadhil Msemo wa Kilimanjaro aliyekuwa kituo cha Singida.

Nonga ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba A7 kati ya Kumuyange FC dhidi ya Ambassador.

Msemo ameondolewa baada ya kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba C6 kati ya Temeke Squad dhidi ya Mtwivila City.

Waamuzi hao wawili wanatakiwa kuondoka kwenye vituo vya Geita na Singida leo Jumamosi Mei 12,2018.

TFF haitawavumilia waamuzi watakaoendelea kuchezesha chini ya kiwango katika mashindano hayo ya RCL pamoja na mashindano mengine yote kwakuwa TFF imejielekeza katika uchezeshaji wa haki katika mashindano yake yote na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kuharibu mashindano ya RCL.

Cliford Mario Ndimbo

Afisa Habari na Mawasiliano TFF
Mei 12,2018

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KATIBU MKUU SEKRETARIETI YA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (wa pili kulia) na Msaidizi wake Ndg. Jenny Mbodi (kulia) na kushoto ni Mheshimiwa Aeshi Hilary.(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

WATUMISHI WA OFISI WAZIRI MKUU WAPEWA MAFUNZO YA KUZIMA MOTO

$
0
0
Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ruth Mwasakafyuka akizima moto katika mafunzo ya kuzima moto kwa kutumia kifaa rasmi cha kuzima moto yaliyoendeshwa na Maofisa wa Kikosi cha Zimamoto cha jijini Dodoma Mei 12, 2018. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. (Picha na Ofis ya Waziri Mkuu) 
Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Joseph Mboje akizima moto kwa kutumia kifaa rasmi cha kuzima moto katika mafunzo ya kuzima moto yaliyoendeshwa na Maofisa wa Kikosi cha Zimamoto cha jijini Dodoma Mei 12, 2018. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA EAGT DKT. MWAKIPESILE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt. Brown  Mwakipesile, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

LIVE: MATOKEO YA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA (TAPSEA) YAKITANGAZWA


BODI YA MIKOPO YAFAFANUA KUHUSU UMILIKI WA LESENI ZA BIASHARA KWA WAZAZI SIO SIFA YA MWANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUKOSA MKOPO

$
0
0
Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa waombaji wa mikopo ambao wazazi wao wanamiliki leseni za biashara hawatapata mikopo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2018/2019. Taarifa hizo sio sahihi na zinapotosha waombaji mikopo na umma kwa ujumla.

Ufafanuzi wa kina ni kama ifuatavyo:

a)   Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB inaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) pamoja na Mwongozo unaotaja sifa, vigezo na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo. Mwongozo huu unapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na hautaji kigezo cha umiliki wa leseni kama sifa ya kukosa mkopo;

b)   Pamoja na mwongozo huu, HESLB pia imeandaa kitabu kwa lugha nyepesi ya kiswahili chenye Maswali na Majibu 21 ili kuwawezesha waombaji mikopo kufahamu sifa na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa ukamilifu na usahihi. Kitabu hiki pia hakijataja umiliki wa leseni kwa mzazi au mlezi kama sifa ya mwanafunzi kukosa mkopo;

c)    HESLB inaamini umiliki wa leseni ya biashara kwa wazazi ni jambo jema na linapaswa kupongezwa kwa kuwa linaimarisha mifumo ya utambuzi kwa wafanyabiashara.

Bodi ya Mikopo inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wazazi, walezi na wanafunzi waombaji wa mikopo kusoma kitabu cha mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na kitabu chenye maswali 21 ambavyo vinapatikana katika tovuti (www.heslb.go.tz).

Vitabu hivi ndiyo nyaraka rasmi za HESLB zinazotoa mwongozo kuhusu maombi ya mikopo kwa mwaka 2018/2019. Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wanahabari, kusoma nyaraka hizo na kutumia kalamu na kamera kuwaelimisha waombaji mikopo kwa usahihi.



Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM

Makhtar Diop Takes Up Role as Vice President for Infrastructure

$
0
0
After six years as the World Bank's Vice President for Africa where he oversaw the delivery of a record-breaking $70 billion to Sub-Saharan Africa to help tackle key development challenges, Makhtar Diop (pictured) has been appointed as the World Bank’s Vice President for Infrastructure.  
The newly created Infrastructure Vice Presidency comprises Transport & Digital Development, Energy & Extractives, Infrastructure Finance and Public Private Partnerships (PPPs). 
In this global role, Makhtar Diop will oversee the Bank’s work on infrastructure and infrastructure finance and lead efforts to develop sustainable solutions and help close the infrastructure gap in developing and emerging economies. 
As Vice-President of the Africa Region, he was instrumental in mobilizing private finance to support Africa’s infrastructure and fostering the environment for more innovation and technology adoption. A passionate advocate for Africa’s right to clean and affordable sources of electricity, he also called for greater investment in renewable energy and pushed for greater regional interconnectivity in the power and transport sectors. 
Mr. Diop brings to the post a deep level of experience and understanding of complex infrastructure challenges. His prior experience includes serving as Director for Finance, Private Sector & Infrastructure in the Latin America and the Caribbean Region. From 2009 to 2012, Mr. Diop held the position of World Bank Country Director for Brazil where the World Bank helped finance major infrastructure work and was the Bank’s Country Director for Kenya, Eritrea, and Somalia.
A recognized opinion leader in the economic and social development field, Makhtar Diop has been named one of the 100 most influential Africans in the world.
His appointment will be effective as of July 1st, 2018. 

JAFO AAGIZA UJENZI KITUO CHA AFYA BWANGA UKAMILIKE NDANI YA MWEZI MMOJA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ametoa mwezi mmoja kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Chato mkoani Geita kusimamia ipasavyo na kukamilisha Ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Bwanga ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kutoka serikali kuu. 

Waziri Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa wilayani Chato mkoani Geita katika ziara ya kukagua wa miradi ya maendeleo. Jafo amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho na ametoa siku 30 kazi zote ziwe zimekamilika.Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari ya kidato cha tano na sita ya Magufuli.

Shule hiyo imeimarishwa miundombinu yake ya vyumba vya madarasa, vyoo, bwalo la chakula, pamoja na mabweni. Akizungumza shuleni hapo, Jafo amewapongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo ya Magufuli kwa kuwa miongoni mwa shule 25 bora nchini kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017.Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu kuweka jitihada zao kwenye masomo ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Magufuli wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya shule hiyo.
Majengo ya kituo cha afya Bwanga 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita kwenye ukaguzi wa ukarabati wa kituo cha Afya Bwanga.

WILAYA YA MADABA YAJA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUBORESHA KIWANGO CHA ELIMU.

$
0
0
Halimashauri ya wilaya ya MADABA mkoani Ruvuma imeadhimia kuandaa mikakati madhubuti ya kuboresha kiwango cha elimu katika shule za msingi na sekondari ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na makazi bora ya walimu katika shule husika. Hayo yamebainishwa katika baraza la madiwani la robo tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018.

Wataalam wawasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma

$
0
0
 Wahandisi Kamel Fazhani (kulia) na Marrarchi Walis (kushoto) wa Kampuni ya Studi ya Tunisia wakiwasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mbele ya wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga.
 Meneja Mipango na Usanifu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mohamed Millanga (wa kwanza kushoto), akiangalia moja ya picha (hazionekani pichani) za usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo na Wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa Kampuni ya Studi ya Tunisia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo uliudhuriwa na wataalam mbalimbali wa usafiri wa anga.
 Mhandisi Bernard Kavishe (aliyesimama) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), akichangia hoja katika mkutano uliofanyika leo wa uwasilishaji wa usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo umewasilishwa na wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
 Bw. Said Mpwili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) (nyuma aliyenyanyua mkono), akiwasilisha mapendekezo ya ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege kwa wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia, ambao leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wamewasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma.
Mwonekano wa Jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo katika usanifu wa awali kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na wataalamu kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
Picha na Bahati Mollel wa TAA.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images